Na A bdulaziz Video Lindi
Wakazi wa Manispaa ya Lindi, kwa takribani juma moja sasa, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa upatikanaji maji safi na salama na kulazimika kutumia maji ya visima vya kienyeji vilivyochimbwa kwenye baadhi ya makazi ya watu.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mtandao huu kuhusiana na tatizo hilo, wameonesha hofu yao ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa ya matumbo ikiwemo kipindupindu kwa vile maji ya visima wanayotumia kwa sasa siyo safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Lindi mjini(LUWASA), Idrisa Sengulo, pamoja na kukiri kuwepo kwa tatizo hilo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mamlaka, amewaomba radhi wananchi kwa tatizo hilo ambalo amesema kama mambo yakienda vizuri linaweza kutatuliwa ktk kipindi cha siku mbili zijazo.
Amesema mahitaji ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Lindi ni lita milioni 5 kwa siku, ikilinganishwa na lita lita milioni 1,340,000 tu kwa siku zinazopatikana kwa sasa.