Habari ya kazi ndugu zangu.
Ninayo furaha kuwajulisha ya kwamba sasa kazi zangu zote za muziki zitakuwa zinapatikana kwenye mitandao yote ya kununua nyimbo za wasanii duniani. Tayari nishasambaza Album yangu ya kwanza " Pwaa The Album" na singles zingine kama "Hmmm", na "Mambo" kwenye mitandao ifuatayo:
iTunes, Amazon MP3, Spotify, Google Play, Xbox Music, Deezer, Rhapsody, Simfy, MySpace Music, Nokia, Wimp, Sony Music Unlimited,Napster, Verve Life, Media net, Shazam,eMusic, iHeartRadio, Muve Music, and Rdio.
kwa wale mliokosa nafasi ya kujipatia nakala za album yangu ya kwanza, hii ni fursa kwenu kujipatia Album hiyo kupitia mitandao hii kwa bei nafuu sana. Tupeane support ili tukuze muziki wetu.
kwa sasa namalizia kurekodi album yangu ya pili ambayo ipo kwenye mahadhi ya kimataifa zaidi na punde ikikamilika ntaanza kuachia single moja moja kupitia mitandao hii, mitandao ya simu kwa njia ya RBT na pamoja na wa "The Kleek" chini ya mkataba wangu mpya na Universal Music Group.
Asanteni sana na hii hapa ni link ya
kupata nyimbo zangu zote kupitia iTunes.