Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge watatu wa Ukawa na Makada wao baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu. Wabunge hao na wenzao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kiridhika kwamba ushahidi ulioletwa mahakamani hapo haukuwa unatosha kuwakuta washtakiwa na kesi ya kujibu.
Amesema kuwa katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha kwani, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani alimjeruhi. Ameongeza kuwa, ushahidi wake ulielezea tu Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.
Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema kitendo hicho kingeweza kupelekea mlalamikaji kufungua kesi nyingine lakini siyo kujeruhi.
Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliita mashahidi watatu kutoa ushahidi ambapo hakuna ushahidi ulioweza kuwatia hatiani watuhumiwa hao na kukutwa na kesi ya kujibu.
Wabunge wa Chadema, na makada wao pamoja na Wakili Wao Peter Kibatala wakifurahi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kiachiwa huru kwa kuonekana hawana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma iliyokuwa inawakabili ya kumjeruhi Katibu Tarafa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando. Habari kamili BOFYA HAPA