Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117140

Pikniki Adui wa Mazingira Ukanda wa Utalii - amber resort, zanzibar

$
0
0

Pikiniki zinazofanywa na watu mbalimbali  katika fukwe zilizoko kwenye ukanda wa utalii visiwani Zanzibar, zinachangia uharibifu mkubwa wa mazingira unaotishia kuwakimbiza watalii.

Shughuli ya kusafisha mazingira iliyofanywa juzi katika eneo dogo kwenye ufukwe wa Muyuni ulioko Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja, ilikusanya karibu tani moja ya takataka zikiwemo chupa za plastiki.
Operesheni hiyo iliyochukua saa moja, ilijumuisha wafanyakazi wa Amber Resort na Best of Zanzibar, na kusafisha eneo linaoandaliwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa kitalii utakaofanywa na kampuni ya Pennyroyal.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja Mradi wa Amber Resort Murtaza Hassanali, alisema vijana wanaotembeza watalii (mapapasi) pamoja na wageni wanaofika hapo, huondoka wakiacha vitu vingi visivyofaa ambavyo hugeuka kuwa taka na sumu kwa viumbe wa baharini.
Aidha alieleza kuwa, pikiniki zinazofanywa na watu kutoka mjini na maeneo mengine hasa vijana, ni chanzo kikuu cha uharibifu wa fukwe hizo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117140

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>