*Aisisitiza Wizara ya Fedha iimarishe mifumo ya kuwalinda watumiaji wa huduma hizo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha iimarishe mifumo ya kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha ili baadhi ya watoa huduma wasio waadilifu wasitumie changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya fedha kwa baadhi ya wananchi na kuwadhulumu.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema Wizara ya Fedha iendelee kushirikiana na na watoa huduma za fedha kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo muhimu yakiwemo ya usimamizi wa fedha binafsi, kuweka akiba, mikopo, uwekezaji kupitia hatifungani na hisa, bima, mpango wa kujiandaa na maisha ya uzeeni pamoja na kodi.
“Wizara ya Fedha iandae mpango maalumu wa kutoa hamasa kwa Watanzania ili wajenge utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha, pia elimu iendelee kutolewa kuhusu wajibu wa kila mmoja kudai na kutoa risiti kwa malipo yanayofanyika. “
Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 22, 2023) alipofungua Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa, jijini Arusha, ambapo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watoa huduma za kifedha wapunguze gharama za upatikanaji wa huduma za fedha zikiwemo riba na ada ili wananchi wengi watumie huduma za fedha zilizo rasmi.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameisisitiza Wizara ya Fedha iendelee kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya kutoa elimu ya fedha kwa umma na kuhakikisha kuwa elimu hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi mijini na vijijini.
Waziri Mkuu amesema Wizara ya Fedha inatakiwa iandae mpango maalumu wa kutoa hamasa kwa Watanzania ili wajenge utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha pamoja na kuratibu gharama za huduma za fedha. “Pia, elimu iendelee kutolewa kuhusu wajibu wa kila mmoja kudai na kutoa risiti kwa malipo yanayofanyika.“
Waziri Mkuu amesema watoa huduma za kifedha hawana budi kujenga uelewa wa kutosha kwa wananchi kabla ya kufunga nao mikataba, pamoja na kuwafafanulia taratibu na masharti yao kabla hawajatoa kwao huduma hizo za fedha. Pia amewataka watoa huduma hao waweke mkakati mahususi wa kuongeza matumizi huduma kwa njia ya kidijitali pamoja na kuzisogeza hadi maeneo ya pembezoni na vijijini ili wananchi walio wengi wanufaike.
“Watoa huduma za fedha ongezeni ubunifu katika utoaji wa huduma. Toeni huduma zinazoendana na wakati, mahitaji ya soko na kuzingatia uhitaji wa makundi mbalimbali katika jamii. Suala hili liende sambamba na kuwaunganisha wajasiriamali na fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao. “
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wasimamizi wa Sekta ya Fedha na wadau wengine wazingatien sheria na kanuni za kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha ikiwemo kutatua malalamiko na migogoro na kulipa fidia na mafao kwa wakati.
Amesema lengo la maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa na Maonesho ya Huduma za Fedha yamejikita katika kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa, kusimamia vizuri rasilimali fedha ikiwa ni pamoja na kuimarisha utamaduni wa kujiwekea akiba, kukopa kutoka vyanzo salama na njia sahihi za kulipa madeni ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini.
Naye, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaendelea kukuza uelewa kwa Watanzania kuhusu masuala ya kifedha huku akitoa wito kwa Watanzania kuweka utaratibu wa kusoma vigezo na masharti ya huduma za kifedha wanazopata kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza baadae.
"Ni vyema tukaweka utaratibu wa kusoma na kuelewa vigezo na masharti tunapokuwa tunapatiwa huduma za kifedha hasa mikopo ili tujiepushe kuingia kwenye mikopo yenye masharti magumu ambayo wakati mwingine tunaweza kushindwa kuyatekeleza."
Kwa Upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Natu El-maamry amesema maadhimisho hayo ya tatu ni muendelezo wa jitihada za Serikali katika kuongeza uelewa wa masuala fedha kwa Watanzania ili waweze kuwa na uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha.
Amesema taasisi mbalimbali za kifedha na wadau wa kisekta wanatumia kipindi hiki kutoa elimu na huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
WAZIRI MKUU AFUNGUA WIKI YA HUDUMA YA FEDHA KITAIFA
WAANDISHI WA HABARI 72 WATANGAZWA KUJIUNGA RUJAT

Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT) katika kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro, Novemba 22, 2023, kwa mamlaka kiliyopewa na Mkutano Mkuu wa RUJAT, pamoja na mambo mengine kimejadili maombi 77 ya uanachama na kupitisha waombaji 72 kuwa wanachama wapya.
Hatua hii imeongeza idadi ya wanachama kufikia 109.
RUJAT inawakaribisha tuungane katika kujenga tasnia ya habari inayojali maslahi ya jamii vijijini.
Majina ya wanachama wapya ni haya yafuatayo:



BOFYA <<HAPA>> KUJIUNGA RUJAT

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Neville Meena akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya RUJAT

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Neville Meena akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya RUJAT

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Neville Meena akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya RUJAT

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Prosper Kwigize akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya RUJAT

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Prosper Kwigize akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya RUJAT

BOFYA <<HAPA>> KUJIUNGA RUJAT
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YAPATIWA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA KUTUMIA VIPIMO SAHIHI.
Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Deodatus Mwanyika amesema kuwa taasisi ya Wakala wa Vipimo ni muhimu sana kwenye uchumi kwakuwa inahakikisha wananchi wanapata bidhaa zenye vipimo sahihi na kamati imeelekeza Wizara kuwa na mkakati endelevu wa usimamizi wa vipimo vinavyotumika katika maeneo mbalimbali nchini hususani kuanza mara moja usimamizi wa vipimo katika maeneo ya muda wa maongezi na taxi za mitandao, kwa kuwa maeneo hayo yanalalamikiwa sana na wananchi.
"Sisi kama kamati ya Bunge tunaosimamia na kuishauri Serikali tunnailekeza Wizara kuwa na zoezi endelevu la ukaguzi wa vipimo sahihi sambamba utoaji elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipimo hasa kwa wananchi wa chini ambao ndio walaji wa mwisho ili kuhakikisha kiasi cha fedha wanacholipa kiendane na kiasi cha bidhaa wanazonunua " Amesema Mwanyika.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akichangia katika Semina hiyo ameelekeza Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuzingatia mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati ya Bunge katika Semina hiyo na kutaka utekelezaji wake uanze mara moja ili kuendelea kuwalinda walaji na kuhakikisha wanapata huduma na bidhaa zenye vipimo sahihi wakati wote na kudhibiti matumizi ya vipimo batili.
"Kama Wizara Kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara tumepokea maelekezo ya Kamati na michango yote iliyotolewa kwenye Semina hii, naelekeza wataalamu wetu kupitia WMA kuendelea kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo na kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kuhusu utumiaji wa Vipimo sahihi ili Wananchi wasipunjwe kupitia vipimo” ameeleza Mhe. Exaud Kigahe.
Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa ameishukuru kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kwa michango na maelekezo yao waliyotoa kuhusu usimamizi wa vipimo kwenye sekta mbalimbali ili kuhakikisha Wananchi wanapata bidhaa zilizo sahihi wakati wote na vipimo vinavyotumika vinakuwa sahihi wakati wote na pia ameeleza kuwa semina hiyo ni ya siku mbili na Kamati ya kudumu ya Bunge itapata nafasi ya Kutembelea Ofisi ya Wakala wa Vipimo iliyopo kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda Mutukula.
Bi. Stella ameeleza kuwa Wakala wa Vipimo ina ofisi katika mipaka mbalimbali Mutukula ukiwa ni mmoja wa mipaka hiyo ikiwa na lengo la kuhakiki usahihi wa bidhaa zote zinazoingia nchini kupitia mipakani ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zinakuwa sahihi wakati wote kwa lengo la kuwalinda walaji na amesisitiza kuwa Wakala itaendelea kufungua ofisi kwenye mipaka mipya itakayoendelewa kufunguliwa kwa ajili ya kuwalinda walaji kwa kukagua mizigo itakayopita kwenye mipaka hiyo ili iwe kwenye vipimo sahihi.















WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI SIMAMIENI HUDUMA ZA MATIBABU YA MENO KABLA YA KUFIKIA KUNG’OA
Na. WAF - Tanga
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wametakiwa kuhakikisha wanasimamia matibabu bora ya Kinywa na Meno na kupunguza kung’oa meno bali waongeze watu wanaotibiwa meno.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Novemba 22, 2023 wakati akifungua Kongamano la 38 la kisayansi la Kitaifa na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno linalifanyika Jijini Tanga.
“Mbali na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri lakini pia Hospitali zote za umma zinazotoa matibabu ya Kinywa na Meno zihakikishe zinaboresha miundombinu ya kliniki za Kinywa na Meno pamoja na kununua vifaa vya kisasa.” Amesema Waziri Ummy
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Takwimu za kuziba meno zimeongezeka kutoka asilimia 2 mwaka 2020 mpaka asilimia 36.1 mwaka huu wa 2023 ambapo hali hii imesaidia kutokana na juhudi za Serikali ya awamu Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Kuna Mikoa na Wilaya ambazo zimevuka 60%, nataka nione takwimu za kuziba meno zikiendelea kuongezeka na takwimu za kung’oa meno zikipungua, hali hii iende sambamba na utoaji wa elimu ya kinywa na meno kwa ajili ya kuzuia magonjwa yatokanayo na kukosa elimu sahihi ya kujikinga na magonjwa hayo.” Amesema Waziri Ummy
Pia, Waziri Ummy amesema katika jitihada za Serikali za kuendelea kufanya mapinduzi Katika Sekta ya Afya imeweza kuajiri wataalam wa Kinywa na Meno 186 na kununua vifaa tiba vya kinywa na meno ikiwemo viti vya kutibia 55 vilivyokwenda kwenye Halmashauri 40 katika Mikoa yote nchini.
Amesema, Mwaka 2023/24 katika robo ya Kwanza na ya Pili ya mwaka jumla ya viti 207 vimeenda kwenye Halmashauri 160 vifaa tiba vya uchunguzi 82 zimeenda kwenye Halmashauri 70, na OPG mashine 1, CBCT mashine 1, gharama za Vitu vyote hivi ni zaidi ya TZS. Bilioni Saba.
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema Sambamba na uwekezaji huo, Serikali imeongeza ufadhili wa wataalam wa Sekta ya Afya hasa nafasi za kibingwa na ubingwa bobezi ndani na nje ya nchi kwa kutenga shilingi bilioni 8 ambapo kati ya hizo Tsh. Bil 3 zimetengwa kwa ajili ya kusomesha wataalam kwa seti ili kuleta ufanisi wakati wa utoaji huduma za kibingwa bobezi za Afya.
“Upande wa uzalishaji wa wataalam wa Kinywa na Meno vyuo vinavyozalisha Madaktari ngazi ya shahada vimeongezeka kufikia vitatu ambapo tunategemea hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa inazalisha zaidi ya Madaktari 100 wa Kinywa na Meno kwa mwaka kulinganisha na sasa ya wastani wa madaktari wanaozalishwa ni 40-60.” Amesema Waziri Ummy.
HUDEFO KUPITIA EPR YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MADHARA YA TAKA ZA PLASTIKI
Na Mwandishi Wetu Bagamoyo
TAASISI ya Human Dignity and Environmental Care Foundation (HUDEFO) imeamua kuandaa semina maalum ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini kuelewa kuhusu madhara ya plastiki na jinsi gani wanaweza kushiriki katika kuiwezesha jamii kuepukana na madhara yatokanayo na plastiki.
Semina hiyo ya kuwajengea uwezo waandishi hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali inafanyika kupitia Mradi wa Extendend Produver Responsibility(EPR).Mradi huo unatekelezwa na HUDEFO ambaye ameshirikiana na Chuo Kikuu Dar es Salaam, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC), serikali za mitaa, watafiti mbalimbali na sekta binafsi.
Akizungumza wakati wa semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa HUDEFO Sarah Pima, Mshauri Mwelekezi Aman Mhinda amesisitiza lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa kuhusu madhara yanayotokana na uwepo wa matumizi ya taka plastiki.
"Pia kupitia semina hii tunaihamasisha Serikali kuendelea kuwa na mikakati ya kisheria na miongozo ya kiutendaji kwa wazalishaji ikiwa pamoja na ukusanyaji na uondoaji wa taka za plastiki baada ya kutumika, "amesema Mhinda.
Akielezea zaidi kuhusu taka za plastiki, amesema pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa plastiki duniani pamoja na matumizi yake lakini ni asilimia 14 tu ya plastiki ndizo zinarejeshwa kwa ajili ya recycling huku akifafanua takwimu zinaonesha kwa mwaka metric tani milioni 350,000,000 za plastiki huingia katika mfumo wa matumizi.
Aidha amesema kuwa uwepo wa plastiki hizo umesababisha maeneo mengi kuwa na taka za plastiki na miongoni mwa maeneo hayo ni kwenye vyanzo vya maji kama baharini, ziwani na mito kutokana na kusafirishwa kwa njia mbalimbali na plastiki hizo zinaathari nyingi zikiwemo za kiafya na kimazingira.
Amesema kuwa taka za plastiki ziko nyingi kuliko zinazoonekana na utafiti unaonesha kwamba ifikapo mwaka 2050 plastiki kwenye vyanzo vya maji zitakuwa nyingi kuliko samaki.
Hata hivyo wakati wa semina hiyo watoa mada mbalimbali wamepata nafasi ya kuelezea uwepo wa taka za plastiki na madhara yake kwa jamii ya Watanzania huku pia wakielezea hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuepusha madhara yanayotokana na uwepo wa plastiki hizo.
Kw upande wake Mhadhiri Msaidizi Shule Kuu ya Sayansi Akua na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Dk.Bahati Mayoma amesema katika utafiti ambao alishiriki kuufanya mwaka 2014 moja ya matokeo ya utafiti yameonesha kuhusu athari za matumizi ya plastiki.
Amefafanua katika utafiti huo umeonesha asilimia 20 ya samaki wamekutwa na vipande vya plastiki ndani yao matumbo yao jambo ambalo ni hatari kwa afya.
Wakati huo huo Mkaguzi wa Mazingira wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam, Enock Tumbo amewaambia washiriki wa semina hiyo kuwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 haimbani moja kwa moja mzalishaji taka za plastiki.
Ameongeza kwa kuwa sheria haibani mzalishaji, imesababisha mzigo wa kuondoa taka hizo za plastiki kuachwa kwa halmashauri wakati wazalishaji wapo.



.jpeg)

Profesa Ndalichako aanika umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa Watanzania
Na MWANDISHI WETU, ARUSHA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amewataka Watanzania kuona umuhimu wa kujiunga na kuchangia katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Profesa Ndalichako alisema hayo tarehe 22 Novemba, 2023, wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofunguliwa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkoani Arusha.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi’.
Profesa Ndalichako alisema Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine inasimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo kupitia maadhimisho hayo Mifuko hiyo ni sehemu ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kwamba wanapopata fedha wanawajibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yao kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
“Ukitembelea mabanda yetu utakutana na Mifuko yote ya Hifadhi yaJjamii ukiwemo wa NSSF ambao unaendelea kuwahamasisha wananchi kuwa na matumizi sahihi ya fedha kwa kujiunga, kuchangia na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye,” alisema Mhe. Profesa Ndalichako.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

CMSA Yatoa Tahadhari Upatu Haramu
Na Mwandishi wetu, Arusha.
MAMLAKA ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) imeitaka jamii kujihadhari na upatu haramu kwani ni hatari kwa maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Meneja uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, ameyasema hayo jijini Arusha kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa.
Shirima amesema jamii ijihadhari na matapeli wanaoahidi watu kuvuna pesa nyingi kirahisi hivyo waepuke kupoteza pesa ya jasho lao kupitia upatu haramu.
"Kutokana na hali hiyo Watanzania wanapaswa kujiunga kwenye masoko ya mitaji kwani ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo ya muda mrefu yaani mwaka mmoja," amesema
Amesema fedha za maendeleo hupatikana kwa kuuza hisa za kampuni, hatifungani na vipande katika uwekezaji wa pamoja.
Mchambuzi fedha mwandamizi wa CMCA, Witness Gowelle, amesema kupitia maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo zaidi.
"Elimu mbalimbali tuliyotoa kwa wajasiriamali watanufaika nao kupitia masoko ya mitaji ili kujiepusha na upatu haramu," amesema Gowelle.
Mjasiriamali kutoka wilayani Ngorongoro, Sas Kotete, amesema wengi wameathirika kupitia upatu haramu hivyo elimu waliyoipata kutoka CMSA itawasaidia kuepuka hayo.
Mjasiriamali mwingine wa mkoani Arusha, Naini Losusu ameipongeza CMSA kwa kuwapa elimu hiyo kwani inawajengea uwezo zaidi juu ya upatu haramu
Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa kupitia kauli mbiu ya elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya uchumi, yanafanyika jijini Arusha, kwa siku sita kuanzia Novemba 20 hadi 26 mwaka huu.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kufungua rasmi maadhimisho hayo Novemba 22, jijini Arusha
.jpeg)



BoT yapongezwa usimamizi thabiti wa sekta ya fedha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa usimamizi thabiti wa sekta ya fedha nchini pamoja na jitihada inazofanya katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma za fedha.
Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo alipotembea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo alipokelewa na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo.
Bi. Msemo alisema kuwa katika maadhimisho hayo BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu haki zao kutoka kwa taasisi za fedha pamoja na wajibu wa wananchi katika kutumia huduma za fedha.
Katika banda la Benki Kuu wananchi wanapata fursa yakujifunza kuhusu sera za uchumi na fedha; uwekezaji katika dhamana za serikali; usimamizi wa fedha binafsi, akiba, mkopo; namna BoT inawalinda watumiaji wa huduma za fedha; utunzaji sahihi wa noti na utambuzi wa alama za usalama; mifumo ya malipo ya taifa na namna Bodi ya Bima ya Amana inavyokinga amana za wateja wa benki na taasisi za fedha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akipewa maelezo na Naibu Gavana, Bi. Sauda Kassim Msemo, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akipewa maelezo na Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akielezea jambo kwa Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
WAZIRI MBARAWA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA TASAC
Waziri Mkuu Majaliwa Avutiwa na Jitihada za Benki ya Exim Kusogeza Huduma kwa Wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo jana alipotembelea banda la maonesho la Benki ya Exim Tanzania muda mfupi kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha yanayoendelea kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Benki ya Exim ni moja ya wadau muhimu wa Maonesho hayo yanayotarajiwa kuhitimishwa Novemba 26, mwaka huu.
Akiwa kwenye banda la benki ya Exim, Waziri Mkuu alipata wasaa wa kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi Kauthar D’Souza ambae pamoja na kuelezea baadhi ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki ya Exim Tanzania pia alielezea kuhusu mkakati wa benki hiyo katika kujitanua katika maeneo mbalimbali nchini.
“Niwapongeze sana kwa jitihada mnazoendelea kuzifanya katika kupanua zaidi huduma zenu, hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili hizi huduma nzuri mnazoendelea kuzitoa ziwafikie wananchi wengi zaidi hususani waliopo pembezoni huko ambao bado hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha.’’ Alishauri Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watoa huduma za kifedha nchini kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya fedha kwa umma sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa huduma hizo zikiwemo riba na ada ili wananchi wengi watumie huduma za fedha zilizo rasmi.
Awali akielezea kuhusu huduma za benki ya Exim Tanzania mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa, Bi Kauthar alisema licha ya jitihada za benki hiyo katika kujitanua zaidi nchini ambapo hadi sasa ina mtandao wa matawi 33 na mawakala 1500 nchi nzima, bado mkakati wake ni kuwekeza zaidi katika utoaji wa huduma kupitia ubunifu wa kidijitali ili kutoa masuluhisho ya kibenki yanayofaa na salama kwa wateja wake.
“Pia tunatambua wajibu tulionao katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini na ndio sababu moja ya kipaumbele chetu ni kuwawezesha watu binafsi na wafanyabiashara wakiwemo wanawake na wajasiriamali kupitia huduma zetu mahususi kwa ajili yao ikiwemo akauti ya Wajasiriamali pamoja na akaunti ya ‘Supa woman’ iliyobuniwa kwa ajili ya wanawake wanaopambana kukuza mitaji ya biashara zao," aliongeza.
Zaidi, Bi Kauthar alibainisha kuwa benki ya Exim Tanzania imeendelea kujitolea kuinua jamii huku akiutaja mpango wa Exim Cares wa benki hiyo kama nguzo muhimu katika utekelezaji wa juhudi mbalimbali za benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) hususani katika sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, michezo na utunzaji wa mazingira (Exim Go Green Initiative). Katika kuthibitisha dhamira hiyo benki ya Exim kupitia maonesho hayo imeambatana na baadhi ya wajasiriamali wanawake ambao ni wanufaika na Programu ya Uwezeshaji Wanawake (WEP) ya benki hiyo waliopata fursa ya kuonesha bidhaa zao wakiwa kwenye banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maadhimisho hayo.
“Kwa kufanya hivyo, sio tu kwamba tunatimiza wajibu wetu kama benki lakini tumekuwa mawakala wa mabadiliko chanya ndani ya jamii zetu,” alisisitiza.





BALOZI FATMA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MAWAKALA WA AJIRA NA UONGOZI WA DIASPORA WA TANZANIA NCHINI OMAN
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab mapema wiki hii amekutana kwa mazungumzo na Mawakala wa Ajira jijini Muscat, Oman.
Balozi Fatma alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa mawakala hao ikiwa ni mkutano wake wa kwanza na Mawakala hao tangu ateuliwe kuwakilisha kituo hicho.
Pamoja na mambo mengine mazungumzo yao yalijikita katika kujadili changamoto, kupokea ushauri na kuangalia namna ya kuweka mazingira bora na yenye ufanisi katika kukamilisha mchakato wa mikataba ya ajira za kuleta Wafanyakazi kutoka Tanzania hususan wafanyakazi wa ndani.
Wakati huo huo, Mhe. Balozi Fatma alikutana na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Oman (Diaspora) kwenye mkutano uliofanyika katika makazi ya Balozi jijini Muscat, Oman.
Lengo la mazungumzo lilikuwa ni kujitambulisha rasmi kwao na kusikiliza maoni na changamoto zinowakabili Diaspora na kujadili njia bora ya kuzitatua.
Kadhalika, Balozi Fatma alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa ushirikiano wao ambao umewezesha kuwakutanisha pamoja Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman na pia alisisitiza umuhimu wa kuzingatia na kufuata sheria za nchi hiyo na kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuitangaza vyema.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab (kulia) akizungumza na Mawakala wa Ajira wa nchini Oman (hawapo pichani) alipokutana nao jijini Muscat kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na mikataba ya ajira kwa watanzania nchini humo.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab (mwenye nguo ya bluu) akizungumza na Mawakala wa Ajira wa nchini Oman alipokutana nao jijini Muscat kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na mikataba ya ajira kwa watanzania nchini humo.

Moja wa Mawakala hao akiwasilisha mchango wake katika kikao hicho.

Mkutano ukiendelea.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Balozi Fatma Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Diaspora wa Tanzania wa nchini Oman.

Picha ya pamoja.
HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2023
MOROCCO YAPATA FUNZO HILI KWA TANZANIA, CHEZA KASINO USHINDE MAPENE!!

WATUMISHI WA TCAA WAPONGEZWA KWA UTENDAJI KAZI KWA WELEDI
MESSI KUWEKA REKODI NYINGINE BACK TO BACK. CHEZA KASINO USHINDE KIRAHISI
SIMBA SC YAFUNGIWA KUSAJILI KISA SAKHO
Lameck Ditto adai Bil 6 MultChoice Tanzania Kutumia wimbo wake bila ridhaa yake
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Bw.Lameck Ditto ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iamuru Kampuni ya MultiChoice Tanzania Limited imlipe fidia ya Sh 6 Bilioni mara baada ya Kampuni hiyo kutumia wimbo wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake.
Lameck Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Benard Bwakeya ameiomba Mahakama iamuru alipwe Milioni 200 kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo.
Ditto alitoa ushahidi wake kwa saa 6, mbele ya jaji Hamidu Mwanga wa Mahakamani hiyo katika kesi ya madai, akiilalamikia MultiChoice Tanzania Limited kutumia wimbo huo kwenye matangazo yao ya biashara kipindi cha Kampeni ya Afcon 2019.
Akiwasilisha ushahidi wake, alidai, MultiChoice imempora fursa ya kunufaika na kazi yake kupitia wimbo huo.
Miongoni mwa vielelezo alivyoviwasilisha Mahakamani hapo ni mawasiliano ya barua pepe (email) ambayo alidai alifowadiwa na Emmilian Mallya aliyekuwa mratibu wa Tamasha la Urithi ambayo ilionyesha ushiriki wa wimbo wake huo kwenye Tamasha hilo.
"Mheshimiwa jaji, huu ni wimbo wangu na mimi ndiye mmiliki, niliutunga wa kwanza nikaimba mwenyewe, nikaombwa nitunge wa pili kwa ajili la Urithi ambao umeimbwa na wengi," alidai Ditto wakati akitoa ushahidi wake.
Awali, Wakili anayeiwakilisha MultiChoice alidai walitumia Wimbo wa Nchi Yangu, lakini sio huo unaolalamikiwa na mdai.
Hata hivyo, Jaji Hamidu alisema, kinacholalamikiwa Mahakamani hapo ni Wimbo wa Nchi Yangu uliotumiwa na kampuni hiyo, sio wimbo wa Nchi yangu mwingine.
Katika ushahidi wake, Ditto pia aliwasilisha flash Disc yenye audio na video za matangazo anayolalamikia na nyimbo hiyo ambayo alidai yeye ndiye mmiliki halali.
Kabla ya Mahakama hiyo kupokea kielelezo hicho, wakili anayeiwakilisha Multi Choice Tanzania Limited, Mlano Mlekano alihoji uhalali wa video hizo kama si za kutengenezwa.
Kwenye ushahidi wake, Ditto alidai ni halali na endapo links za matangazo hayo hazijafutwa, Mahakama iridhie waangalie kwenye google, na Jaji Mwanga aliliridhia ombi hilo, na video hiyo ilipochezwa, ikafunguka na kumuonyesha mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Akida Mapunda akihamasisha Afcon huku kukiwa na matangazo ya DSTV na katika (background) ulisikika wimbo wa Nchi Yangu.
Ditto pia aliwasilisha vielelezo vingine ambavyo Mahakama ilivipokea kama ushahidi wake.
Nje ya Mahakama, wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta alisema kesi hiyo imeanza kusikilizwa na upande wa mdai una mashahidi watano.



TANZANIA MWENYEJI WA TAMASHA LA DUNIA LA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU
Tanzania ni mwenyeji wa tamasha la dunia la watu wenye usikivu hafifu (viziwi) likihusisha shindano la kumsaka mrembo, mtanashati pamoja na wanamitindo litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Dar es salaam.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi amesema maadalizi yanaendelea vizuri na Tanzania imejipanga kufanikisha tamasha hilo ambalo Tanzania imepewa heshgima ya kuwa mwenyeji kwa miaka miwili mfululizo.
Maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vyema kwa washiriki kujinoa ili kutoa taji la urembo, utanashati pamoja na wanamitindo dunia kwa viziwi ambapo mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo hapa nchini baada ya kufanyika kwa mara ya kwanza Afrika na Tanzania kwa 2022.
Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.



HAFLA YA KUMBUKIZI KUFANYIKA JUMAMOSI KESHOKUTWA LEADERS CLUB - HIZI HAPA NI TASWIRA ZA MWAKA JANA 2022 YA SIKU YA KUKUMBUKA WAPENDWA WETU
Unakaribishwa kuhudhuria shughuli yetu ya kuwarehemu Ndugu, Jamaa na Marafiki zetu wa Club za Tazara, Singasinga, Sigara , Checkpoint, Mango Garden, Masai ambao wametangulia mbele za haki.
Shughuli hii, ambayo iliasisiwa na Marehemu Balozi Cisco Mtiro, itafanyika katika viwanja vya Leader's Club jijini Dar siku ya Jumamosi 25/11/2023 kuanzia saa 5 asubuhi.
Kutakuwa na Sala/Dua kutoka kwa Sheikh na Padre na baada ya hapo kutakuwa na chakula kwa wote.
Wote mnakaribishwa
MFUMO UNGANISHI KUONDOA CHANGAMOTO SEKTA YA ARDHI- PINDA
Serikali imesema Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi unaoboreshwa na timu ya wataalamu jijini Arusha utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto mbalimbali za sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huo unaotarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga utarahisisha na kuharakisha upatikanaji wa huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda mkoani Arusha tarehe 22 Novemba 2023 alipokutana na kuzungumza na Menejiment ya Wizara pamoja na Timu ya wataalamu inayooboresha Mfumo huo.
Amesema, sekta ya ardhi imekuwa na changamoto nyingi lakini hatua ya wizara ya Ardhi kufanya maboresho ya kimfumo kutasaidia kuondoa kero na kelele za wananchi kwenye masuala ya ardhi.
‘’Kikubwa ambacho nimeanza kufarijika ni kwamba ‘mmeadvance’ mpaka hapa mlipofika katika kuboresha mfumo, hongereni sana baada ya muda tutakwenda kumaliza kelele za wananchi wa nchi hii’’ alisema Mhe. Pinda.
Kupitia maboresho ya mfumo huo unganishi wa kutunza taarifa za ardhi changamoto zote za sekta ya ardhi ikiwemo upatikanaji namba ya malipo, malipo ya ada mbalimbali, upatikanaji hati, uthamini pamoja na migogoro ya ardhi zinaenda kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya kimtandao.
Kwa mujibu wa Pinda, itachukua muda kufikia malengo yaliyokusudia katika kuboresha mfumo huo kwa sababu kinachofanyika sasa ni kuwahamisha wananchi kutoka kwenye mfumo waliouzoea na kwenda katika teknolojia mpya.
Hata hivyo, amewatahadharisha wataalamu wanaoboresha mfumo huo pamoja na maofisa wa wizara ya ardhi kuwa makini kutokana na upinzani wanaoweza kuupata kutoka kwa baadhi ya watu aliowaeleza kuwa ni wanufaika wa mifumo ya sasa ambayo wizara ya ardhi inaenda kuachana nayo.
‘’lazima mkawe standby wakurugenzi na maofisa, wale waliokuwa wanakula kupitia mfumo wa kawaida mjue ndiyo ‘threat’ namba moja wao ndiyo watakaoanza kusema mfumo wa ardhi bure kabisa lazima tutengeneze timu ya kuwaattack’’ alisema Pinda.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera alimueleza Mhe. Pinda kuwa, Menejiment ya wizara imepitia kila hatua ya jinsi mfumo unavyofanya kazi lengo likiwa kufanya maboresho yatakayowezesha idara za wizara hiyo kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
‘’Kupitia mawasilisho ya wataalamu tungetamani mfumo ukamilike mapema lakini kwa kuwa kazi hiyo inahitaji utaalamu, tunaamini kazi hiyo itakamilika ndani ya muda mfupi’’ alisema Lucy
Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Bw. Flateny Michael Hassan alisema, kufutia wizara ya ardhi kuwa na changamoto kadhaa kwenye mifumo yake imeonekana upo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.
Amebainisha kuwa, kazi inayofanyika ya kuboresha mfumo kwa sasa imefikia asilimia 75 na ni matarajio yake mapema Januari 2023 mfumo utaanza kutumika katika mkoa wa Arusha kabla ya kuendelea na mikoa mingine.
Ameyataja maboresho yanayoendelea kufanyika kuwa ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtandao na huduma ya Mobile App ambapo mwananchi anaweza kupata huduma kupitia simu ya kiganjani.
‘’Katika maboresho yanayoendelea, kuna mifumo mitatu wa kwanza ni Back Office unaoruhusu watumishi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi, wa pili ni Public Portal unaoruhusu wananchi kuomba huduma online na wa tatu ni Mobile App ambapo wananchi wanaomba huduma kupitia simu janja’’ alisema Flateny.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikana kwa urahisi na haraka na uboreshaji mfumo huo pamoja na uwepo wa Klinik za Ardhi ni sehemu jitihada hizo ambazo zinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wananchi.