Na.Khadija Seif,Michuziblog
TAASISI na Makampuni yameaswa kusaidia wanamichezo ili waweze kufanya vizuri mashindano ya kimataifa na kuliwakilisha vyema taifa la Tanzania kidunia.
Hayo yamesemwa Leo Novemba 21,2023 na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu Taasisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Loy Mhando wakati akikabidhi vifa ya kimichezo timu ya Taifa ya mpira wa netiboll ( TAIFA QUEENS) ,amesema brela ni mdau mkubwa wa michezo na inatambua mchango mkubwa kupitia kwenye tasnia ya michezo kwani ni sehemu ya biashara na ajira kwa vijana wengi.
Aidha mhando ameeleza kuwa Taasisi hiyo imekua ikishirikiana kwa karibu na michezo mbalimbali ikiwemo michezo inayoandaliwa na Shirikisho la michezo ya wizara na idara za Serikali na mikoa (SHIMIWI).
Mhando amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo trucksuits jozi 25 pamoja na mipira mitano ya netiboli yenye thamani ya shilingi milioni tatu za kitanzania kama sehemu ya kuwapa moyo wa kufanya vizuri wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli ( TAIFA QUEENS).
"Ufadhili huu unatokana na maombi ya Chama cha mpira wa netiboli (CHANETA) kuomba sehemu ya ufadhili wa vifaa vya kimichezo kwa timu ya taifa queens ili waweze kujiandaa na mashindano mbalimbali ya kitaifa hivi karibu."
Pia amewaomba makampuni na taasisi zingine kutoa mchango wao katika michezo kwani bado timu nyingi zina uhitaji wa hali na mali kuhakikisha timu zao zinakuwa imara na zinailetea sifa taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA) Rose Mkisi ametoa pongezi kwa taasisi ya brela kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu kuhamasisha na kutoa misaada mbalimbali kwa timu za michezo hapa nchini.
"Vifaa hivi vilivotolewa vitaenda kuamsha ari,hamasa zaidi na morali kwa wachezaji wetu kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wa mpira wa netiboli kimataifa."
Mkisi amefafanua zaidi kuwa vifaa hivyo vinaenda kuongeza chachu ya kufanya vizuri kuelekea michuano mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Loy Mhando Leo Novemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam akikabidhi trucksuits pamoja na mpira kwa Katibu Mkuu wa Chama cha mpira wa netiboli (CHANETA) Rose Mkisi kama sehemu ya kuwasilisha ugawaji wa vifaa vya kimichezo kwa timu ya taifa ya mchezo wa netiboli (TAIFA QUEENS)A
fisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Loy Mhando katikati,kushoto kwake Katibu Mtendaji mkuu Chama cha mpira wa Netiboli (CHANETA) Rose Mkisi huku kulia kwake Katibu kamati ya michezo Taasisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Robert Mashika mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo Jozi 25 pamoja na mipira miatano kwa Chama cha mpira wa netiboli (CHANETA) Jijini Dar es Salaam