Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 118890 articles
Browse latest View live

MEDEA TANZANIA KUPITIA MRADI WA JENGA SAUTI, KUUREJESHA MUZIKI WA MCHIRIKU

$
0
0
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Taasisi ya MEDEA Tanzania wamekutana kufanya kikao chenye lengo la kuurejesha mziki wa mtindo wa mchiriku ambao ulitamba na kujizolea umaarufu miaka ya 1990 hadi 2000 na kupotea miaka ya hivi karibuni.

TAASISI ya MEDEA Tanzania wamekutana na kufanya kikao na wadau wa Sanaa ya Muziki wa Mchiriku kujadili namna ya kuurejesha kwenye fomu baada ya kutamba na kujizoelea umaarufu miaka ya 1990-2000 na kupotea miaka yaa hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Nov 23,2023, Meneja Ufatiliaji na Tathimini wa MEDEA Tanzania ,Bw.Hassan Kiungi amesema wameanzisha mradi wa JENGA SAUTI wenye lengo la kuurejesha upya mziki huo ambao kupitia ujumbe wake ulileta ushawishi mkubwa katika jamii katika mambo mbalimbali.

"Miaka ya nyuma muziki wa mchiriku ulikua ukipigwa katika vyombo vya habari na uliweza kuleta ushawishi katika jamii hususani katika ujumbe wake, \ miaka ya hivi karibuni ujio wa miziki fulani tena inayofanana na mchiriku umeweza kuathiri muziki wa mchiriku". Amesema

Amesema changamoto inayo ukabili muziki wa mchiriku ni pamoja na jamii kuuchukulia kama muziki wa kihuni,ambapo mara nyingi hupigwa katika maeneo ya uswahilini na mara chache sana kutokea kupigwa katika majukwaa makubwa.

Aidha Bw. Kiungi amesema katika mradi wao pia wanashughulika kuwapatia mafunzo na kuwajengea uwezo wasanii ili kuzalisha maudhui mazuri ambapo wameanza na bendi mbili Atomic na Jaguar na baadae kuweza kuwafikia makundi ya wasanii wengine.

Pamoja na hayo amesema kuwa wamepanga kuandaa Matamasha kwa ajili ya kuwaweka karibu na hadhira ambao ndio watakuwa wadau wakubwa wa muziki huo ili kuachana na dhana ya zamani kuwa muziki huo ni kwa ajili ya matukio tu kwenye sherehe au harusi.

Kwa upande wake Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Gabriel Awe amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Sanaa zilizo lala au kuanza kupotea zitaweza kuinuliwa tena na kuweza kufanya vizuri.

Naye Mwanamuziki wa Mchiriku kutoka bendi ya Atomic Bw. Hassan Mtengela ameipongeza Taasisi ya MEDEA kuanzisha Mradi wa JENGA SAUTI kwani unawapatia uwezo na elimu ya mambo mbalimbali ambayo awali hawakuyajua na kubainisha kuwa baadhi ya changamoto zinarekebishika hasa katika upande wa sanaa ya muziki huo.

Aidha Mdau muziki huo na Mtangazaji wa TVE na EFM radio Bw.Fido amesema changamoto mojawapo iliyochangia kukwamisha muziki wa mchiriku ni pamoja na ubabe ambao nyakati zilizopita watu waliogopa kupigwa wale walio kuws wanahudhuria katika maonesho hayo.

"Muziki ili uweze kukua unahitaji kupata mashabiki, labda tu niseme kuwa sahivi muziki mrefu hauna mashabiki kama bolingo,taarabu hata vyombo vya habari huwezi kupiga wimbo wa dakika nane, bado Mtangazaji hajaongea hata sapoti inaweza kugharimu, kwahiyo hili nijambo linalotakiwa kufanyiwa marekebisho" Amesema Bw.Fido.











MADINI KUWEKA MIKAKATI SHIRIKISHI UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

$
0
0
# Kushirikiana na Makampuni bingwa ya Ushauri nchini kuitangaza sekta ya madini

# Wizara ya Madini kufungua Dawati maalum la Uwekezaji TIC

Kufungua kiwanda cha uchenjuaji kitakacho hudumia Ukanda wa Sub Sahara Afrika

Wizara ya Madini imepanga kuweka mikakati shirikishi ya uwekezaji katika Sekta ya madini itakayowavutia na kuwanufaisha wachimbaji wadogo,wa kati na wakubwa.

Hayo yamebainishwa Novemba 21, 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali wakati akizungumza na uongozi wa kampuni ya BHP na Lifezone katika mkutano wa biashara baina ya Tanzania na Uingereza unaoendelea jijini London.

Sambamba na hapo, amesema wizara ya madini itaandaa mpango wa mafunzo maalum yaani Apprenticeship Program katika maeneo kazi kwa maafisa ili kuongeza ujuzi na maarifa kwenye mnyororo mzima wa uwekezaji ndani na nje ya nchi.

Mahimbali ameongeza kuwa , wizara ya madini kwa kushirikiana na kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) itafungua Dawati maalum la uwekezaji kwa ajili ya kuratibu shuguli za uwekezaji ndani ya sekta ya madini.

Akielezea kuhusu ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji madini mkakati, Mahimbali ameeleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya BHP Group Limited na Lifezone Metals kupitia kampuni tanzu ya Tembo Nickeli imepanga kujenga kiwanda kikubwa nchini Tanzania cha uchenjuaji madini mkakati yatakayochimbwa katika nchi zilizo Ukanda wa Sub Sahara Afrika.

Akiwa ameambatana na wataalam kutoka wizara ya madini, Mahimbali amesema kuwa Wizara ya Madini imeridhishwa na mwamko ulioneshwa na wawekezaji wa nchini Uingereza na kuahidi kutoa kushirikiana mzuri kwa faida ya nchi zetu.

Akizungumzia maendeleo na ukuaji wa sekta ya madini nchini , Mahimbali amebainisha kuwa kwa mwaka 2022 Sekta ya Madini imekuwa kwa asilimia 10.9 na imechangia asilimia 9.1 kwenye Pato la Taifa na kuingiza asilimia 56 ya fedha zote za kigeni nchini.

Aidha, akielezea kuhusu mafanikio ya ziara hiyo, Mahimbali amesema kuwa timu ya wataalam imejifunza mambo mbalimbali ya kibiashara ikiwemo umuhimu wa wachimbaji madini kuwa na taarifa nzuri za biashara zinazoweza kushawishi uwekezaji , kuongeza uratibu wa takwimu za kitaifa zinazohusu sekta ya madini na kuwajengea ujuzi na maarifa maafisa ili waweze kuhudumia wawekezaji kwa kiwango kinachotarajiwa kimataifa.

Vilevile, Mahimbali amewashukuru watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) kwa ushirikiano wao waliouonesha katika kufanikisha ziara hii na kuaahidi kuwa wizara itateua Afisa Dawati Maalum la Madini ambaye atakuwa ndani ya Kituo cha Uwekezaji kwajili ya kushughulikia uwekezaji sekta ya madini.

VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI




Airtel, itel washirikiana kuzindua simu janja mpya na ya kisasa aina ya A70

$
0
0

 
• Wateja wa Airtel kuunganishwa na GB 75 kwa miezi kumi na 12 wakinunua simu ya Airtel katika maduka ya Airtel na itel popote nchini
• Ni toleo maalum kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel leo kwa pamoja wameshirikiana wamezindua simu mpya ya itel A70 iliyoambatanishwa na ofa ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 75 ambacho kinadumu kwa muda wa miezi kumi na mbili.

Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A70.

Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuu, hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.

Simu ya A70 itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 75GB kwa muda wa miezi kumi na mbili.

Kwa upande wake, Meneja wa Chapa wa itel kutoka itel Mobile Bw, Thomas Wang, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A70 ambayo ni Smartphone ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima.

Simu ya A70 ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu,
Aliongeza kuwa simu ya itel A70 ina uwezo wa 128GG ROM + 8GB RAM, 6,6” na ukubwa wa kioo wa 13MP super HDR CAM. Hivi vyote kwa pamoja vinampa mtumiaji kufarahi matumizi ya simu hii pamoja na kumpa Uhuru wa mawasiliano.

‘Sababu kubwa ya ushirikiano baina ya Airtel na itel ni kuwapa Watanzania kuwa na uwezo wa kutumia smartphone za kisasa zenye ubunifu wa hali ya juu kwa gharama nafuu pamoja na kufurahi kifurushi cha intaneti cha 75GB kutoka Airtel kwa mwaka mzima.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania,  Bwana Jackson Mmbando, akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu mpya aina ya Itel A70 AWESOME ya kampuni Itel kwa ushirikiano na Airtel katika  hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania,  Bwana Jackson Mmbando (kushoto) Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Itel, Bwana Thomas Wang (wa pili kulia)., pamoja na wengine kutoka kampuni hizo, wakipozi wa picha ya 'selfie' katika hafla ya uzinduzi wa simu mpya aina ya Itel A70 AWESOME ya kampuni Itel kwa ushirikiano na Airtel katika  hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.

TUWE WAZALENDO NA MIRADI YETU- MHE.MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amezitaka Taasisi na Mashirika ya Umma kote nchini yanayotekeleza miradi mbalimbali kuwa na uzalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo ikiwa ni matokeo ya kutekelezwa kwa weledi,ufanisi, kiwango na uzalendo mkubwa kwa Mradi wa Maji wa Itumba-Isongole wilayani Ileje,mkoa wa Songwe,ambapo Leo tarehe 23 Novemba, 2023 ameweka jiwe la msingi la mradi huo.

Mhe. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ((Mb na Naibu wake , Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) pamoja na wataalamu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa usimamizi mzuri wa fedha za mradi wa maji wa Itumba -Isongole na kutekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 2.6 kati ya bilioni 4.9 ambazo zilitengwa ili kutekeleza mradi huo,hivyo kubaki kwa fedha ya serikali ambayo itatekeleza miradi mingine ya maji, na kwamba ni vema watekelezaji wa miradi ya serikali wakajenga utamaduni wa uzalendo na uadilifu katika matumizi ya fedha za umma.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Mary Prisca Mahundi (Mb) amemuwakilisha Waziri wa Maji, katika ziara hiyo ya siku nne ya Mhe. Waziri Mkuu,mkoani Songwe kuanzia tarehe 22 -25 Novemba, 2023.

Mhe. Godfrey Kasekenya, Mbunge wa Jimbo la Ileje ameipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa mradi wa maji wa Itumba-Isongole ambao utaondoa kabisa tatizo la hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 100 wilayani Ileje na kuwa na ziada ya maji.

Mradi wa Maji wa Itumba-Isongole katika Wilaya ya Ileje,mkoani Songwe unatekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji ( NWF) na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023 na utahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini wa miji ya Itumba na Isongole wilayani Ileje.



MAKONGAMANO YASAIDIA MABORESHO 57 YA KODI MWAKA 2023/24

$
0
0
Na. Peter Haule, WF, Mwanza



Makongamano ya Kodi yanayofanywa na Wizara ya Fedha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida yamewezesha kufanyiwa maboresho kwa zaidi ya maeneo 57 ya kikodi katika mwaka wa Fedha 2023/2024 huku hatua hiyo ikilenga kusisimua ufanyaji biashara, kulinda viwanda vya ndani na kuchochea uwekezaji nchini.



Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, wakati timu ya watalaam wa masuala ya fedha na uchumi wa Wizara ya Fedha ilipokusanya maoni ya kuboresha kodi kwa ajili ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.



Alisema kuwa kuanzishwa kwa Kongamano hilo kumeleta tija katika maboresho ya mfumo wa kodi ambapo katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2023/24 ushirikishwaji wa wadau uliongezeka.



“Maoni yaliyotolewa yalisaidia kufanya maboresho kwenye maeneo 57 ambapo malengo yake ni pamoja na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, kulinda viwanda vya ndani, kuvutia uwekezaji nchini na kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani”, alieleza Bw. Mhoja.



Bw. Mhoja aliyataja baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi kuwa ni pamoja na kuongeza kima cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka shilingi milioni 100 hadi milioni 200.



Maeneo mengini ni kuanzisha utaratibu wa kufanya marekebisho kwenye viwango vya ushuru wa bidhaa kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya utulivu wa kisera, kusamehe VAT ya uuzaji, uingizaji na ukodishwaji wa ndege ikiwa ni pamoja na matengenezo ya ndege.



Pia alisema kuwa Serikali imeondoa VAT kwenye malighafi zinazotumika kutengeneza vifungashio vya madawa na kuondoa ada ya ukaguzi kwenye madini yanayouzwa kwenye vituo vya kusafishia madini nchini.



Bw. Mhoja alisema kuwa lengo la makongamano hayo yatakayofanyika maeneo mbalimbali nchini ni kuboresha uratibu wa ukusanyaji maoni na kuongeza ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ili kuborsha Sera za utozaji Kodi hatua itakayochochea ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na ya kimkakati halikadhalika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.




Aidha amewashukuru wananchi wa mkoa wa Mwanza kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao kuhusu kodi katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji, alisema timu ya wataalamu wenye weledi wa kutosha imeyachukua maoni hayo ili kuweza kuyafanyia kazi.



Kwa upande wake Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo mkoa wa Mwanza (TCCIA) Gabriel Kenene, ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuamua kuwafuata wananchi ili kuweza kupata maoni yao ikiwa pia ni shauku ya wabunge walio wengi.



Ameiomba Wizara ya Fedha kuendelea kufanya makongamano kama hayo ili kuwasikiliza wananchi na kujionea hali halisi ya mazingira yao ya biashara ili Sera zinazotungwa ziwe rafiki kwa wananchi.



Makongamano ya kodi Kitaifa yanayofanyika kikanda yanaendelea na lengo ni kukusanya maoni ya kodi kwa ajili ya kuboresha Sera za Utozaji kodi kwa mwaka 2024/25.



Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akieleza kuhusu umuhimu wa maoni ya wananchi katika kuboresha Kodi, wakati wa Kongamano la Kodi Kikanda lililofanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa makongamano hayo ya uboreshaji wa Kodi. Kulia ni Afisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, Bw. Giliard Nguve na kushoto ni Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo mkoa wa Mwanza (TCCIA) Bw. Gabriel Kenene.



Katibu Mtendaji wa Viwanda vya Samaki Mkoa wa Mwanza, Bw. Onesmo Sulle, akitoa maoni ya Kodi kuhusu sekta ya Viwanda vya Samaki wakati wa Kongamano la Kodi Kikanda lililofanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa makongamano hayo ya uboreshaji wa Kodi.



Mkurugenzi wa wazalishaji wa Mvinyo Mkoani Mwanza, Bw. Leopord Lema, akiipongeza Serikali kwa maboresho ya kodi kwenye vinywaji vikali na kupendekeza kuendelea kwa maboresho hayo wakati wa Kongamano la Kodi Kikanda lililofanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa makongamano hayo ya uboreshaji wa Kodi.



Meneja wa kiwanda cha kutengeneza nyavu za kuvulia dagaa (Ziwa Met Ltd), Bi. Gift Christopher, akieleza namna ya kuboresha kodi ili kurahisisha uvuvi endelevu wa dagaa, wakati wa Kongamano la Kodi Kikanda lililofanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa makongamano hayo ya uboreshaji wa Kodi.


Mzee Abubakar Hassan Self Mkazi wa Mwanza, akitoa maoni yake kwa Timu ya Wataalamu wa Sera za Kodi waliofika Mkoani Mwanza kukusanya maoni kwa lengo la kuboresha kodi ikiwa ni mwendelezo wa Makongamano ya Kodi Kikanda.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mwanza)



WAZIRI MSTAAFU MHE. PINDA ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia), akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu namna ya utekelezaji wa miradi kwa njia ya ubia, kutoka kwa Kamishna Msaidizi, Idara ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP), Bw. Bashiru Taratibu, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha, wakati wa Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Maadhimisho hayo yanawakutanisha Taasisi ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Arusha.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (wa pili kulia), akizungumza na Maafisa wa Idara ya Sera kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Abdul Ndachi (wa pili kushoto) na Bi. Mwanaidi Kanyawanah (kushoto), katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi” , yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza. Maadhimisho hayo yanawakutanisha Taasisi ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Arusha.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (kushoto), akisikiliza maelezo kuhusu malipo ya pensheni na mafao ya uzeeni kwa wastaafu kutoka kwa Afisa Hesabu Mwandamizi kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Fadhili Izumbe (katikati) alipotembelea Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Maadhimisho hayo yanawakutanisha Taasisi ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Arusha Kushoto ni Mhasibu Mkuu, Bi. Joyce Chaki.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Maadhimisho hayo yanawakutanisha Taasisi ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Arusha. Akishudiwa na Bi. Aziza Baraka Omar, Afisa Masoko wa Banki hiyo na Bw. Hassan Khamis Hamad, Afisa Mauzo wa Benki hiyo.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa Serikali kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Bi. Antelma Mtemahanji, kuhusu taratibu za usajili wa vikundi alipotembelea Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Maadhimisho hayo yanawakutanisha Taasisi ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

WAHITIMU 100,000 WA AWAMU YA TATU WATUMIKA MFANO WA USALAMA

$
0
0

SHINCHEONJI Makabila 12 Kituo cha umisheni cha Kikristo cha sayuni Sherehe ya 114 ya Kuhitimu iliyofanyika katika Uwanja wa Daegu Novemba 12, 2023

Wahitimu 108,084 mwaka huu, wakifuatia 103,764 mwaka 2019 na 106,186 mwaka 2022.

Wachungaji 6,724 wa zamani na wa sasa walihitimu, mara 10 zaidi ikilinganishwa na sherehe ya kuhitimu ya mwaka jana ya 100,000

Sherehe ya '100,000 ya Kuhitimu' iliyofanyika tarehe 12 na zaidi ya waumini 100,000 ambao walijiunga na Kanisa la Shincheonji la Yesu, Hekalu la hema ya Ushuhuda (Mwenyekiti Lee Man-hee, inajulikana kama Shincheonji kanisa la Yesu) walikusanyika katika sehemu moja tarehe 12 na ilikamilishwa kwa utaratibu bila tukio baya hata moja.

Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni (Mkurugenzi Mkuu Tan Young-jin), taasisi ya elimu ya Biblia ya Shincheonji Kanisa la Yesu, ilifanya 'Shincheonji Makabila 12 Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni Sherehe ya mahafali ya 114th ' katika Uwanja wa Daegu siku hii. Jumla ya wanafunzi 108,084 walihitimu katika mahafali haya 100,000. Hii ni mara ya tatu kwa wanafunzi zaidi ya 100,000 kuhitimu, baada ya 103,764 mwaka 2019 na 106,186 mwaka 2022. Hii ilikamilishwa kwa njia ya utaratibu.

Sherehe ya kuhitimu, ambayo ilianza na tamko la ufunguzi na Mwenyekiti Lee Man-hee wa Kanisa la Shincheonji la Yesu, iliendelea na kurusha video za pongezi kutoka kwa watu kutoka duniani kote, ikiwa ni pamoja na jaji wa zamani wa Mahakama ya Katiba ya Kiromania Petre Rugeroayu, na hotuba ya kumbukumbu ya Mwenyekiti Lee. Katika hotuba yake , Mwenyekiti Lee alisema, "Mungu atakuwa akiangalia mkutano wetu. Tuifanye dunia kuwa mahali pazuri zaidi kulingana na mapenzi ya Mungu," alihimiza kwa wahitimu na wageni wa pongezi

Kuhusu neno lililofunuliwa ambalo wahitimu walichukua, Mwenyekiti Lee alisema, "Kitabu cha Ufunuo sio kirefu sana, lakini kina habari kubwa juu ya kuja kwa ufalme wa Mungu." Aliongeza kuwa,

"Kuamini katika hili na kufanya yote haya yajulikane kwa watu wengi ni lengo la Mungu.""Hii ina maana," alisisitiza.

Wakati huo huo, alisema, "Mungu na mbingu huja duniani na kuwa kitu kimoja, ambayo inamaanisha kuwa itakuwa ulimwengu mtakatifu unaotawaliwa na Mungu," na akahimiza, "Na tufanye ulimwengu mzuri kulingana na mapenzi ya Mungu."

Katika hotuba yake ya pongezi, Mkurugenzi Mkuu Tan Young-jin wa Kituo cha umisheni ya Kikristo cha Sayuni alisema, "Wahitimu walisikia moja kwa moja neno kubwa zaidi lililofunuliwa la miaka 6,000 na kuthibitisha kile Mungu ameahidi leo. Kwa hiyo, naamini kwamba umetambua wazi wewe ni nani kama ilivyosemwa katika Biblia. "Sasa hebu tuwe mstari wa mbele katika kufufua mataifa yote na kufikia amani ya ulimwengu," alihimiza.

Katika sherehe ya kuhitimu, maonyesho ya kadi ya dakika 15 ulifanyika chini ya mada ya 'Kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya kilichoshuhudiwa na Shincheonji: Matukio ya Usaliti, Uharibifu, na Wokovu,' na washiriki zaidi ya 10,000, wakipokea shangwe na makofi ya shauku. Sehemu hii ya kadi, ambayo inafupisha maana ya 'Sura za Kitabu cha Ufunuo,' inatathminiwa kama maudhui ya kina ya kitamaduni na kisanii ulimwenguni ambayo yanaonyesha unabii wa kitabu cha ufunuo na uhalisia wake kwa kupitia kadi.

Hotuba ya mwanafunzi aliyehitimu Jeong Hyun-mo kuhusu kuhitimu, ambayo ilitangazwa kufuatia uwasilishaji wa cheti, kuhamisha tassels, na kutoa cheti, pia ilipokewa kwa umakini mwingi.

Mwanafunzi wa sasa wa I.U.C. Jeong, Makamu wa Rais wa Korea Graduate School of Education, alisema, "Mwaka jana, nilialikwa kama mgeni aliyealikwa kwenye Sherehe ya Kuhitimu ya 100,000 kwa darasa la 113. Nilikuwa na hamu sana juu ya siri nyuma ya mkusanyiko wa watu 100,000 kila mwaka licha ya mateso makali, na nilikuwa na hamu ya kujua jinsi vijana waliojaza uwanja walikuwa wanaonekana vjema na wenye kupendeza. "Niliamua kuchukua kozi katika Kituo cha umisheni cha sayuni baada ya kusikia kwamba siri ilikuwa ni neno,” alisema

Alisema, "Kufuatia imani kwamba sitatembea isipokuwa ikiwa njia sahihi, wakati huo huo nilichukua kozi katika Kituo cha umisheni ya Kikristo cha Sayuni na (madhehebu ya kitamaduni) master’s na kozi za doctoral kwenye chuo cha theolojia," na kuongeza, "Kiwango cha Neno kilikuwa kwakweli kama pengo la kati ya mbingu na dunia. Shincheonji alishuhudia bila kuongeza au kupunguza sio tu maana ya kweli ya Kitabu cha Ufunuo lakini pia ukweli wa kile kilichotimizwa kama ilivyotabiriwa. " Kama mtoto wa nuru ambaye hueneza neno la Mungu, nitalipa neema hii na upendo," alisisitiza.

Katika mahafali haya 100,000, jumla ya wachungaji 6,274 wa sasa na wa zamani na wa seminari kutoka ndani na nje ya nchi walihitimu, wakivutia watu. Hili ni ongezeko la zaidi ya mara 10 ikilinganishwa na sherehe za kuhitimu mwaka jana, ambapo wachungaji 522 walihitimu.

Wakati huo huo, sherehe hii ya kuhitimu ilihitimishwa kwa mafanikio na juhudi kubwa zilizowekwa katika utaratibu na usalama. Wakati idadi kubwa ya watu wakikusanyika katika sehemu moja, Kanisa la Shincheonji la Yesu lilianzisha mpango wa usafiri ili kuruhusu washiriki kuingia na kutoka kwa njia iliyotawanyika kwa zaidi ya masaa 10. Karibu mabasi 2,200 ya watalii yalihamia kuhudhuria hafla hiyo siku hii, na Kanisa la Shincheonji la Yesu lilipunguza msongamano wa magari kwa kusambaza karakana zake katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Dalseong-gun, Changnyeong-gun, and Ulsan-si.

Kwa kuongezea, kiongozi wa timu aliwekwa katika kila gari na waongozaji wa kujitolea waliwekwa kila sehemu. Wafanyakazi 14,000 wa usalama na wafanyakazi walipangiwa kuzingatia usimamizi wa usalama. Aidha, vibanda vya matibabu, huduma za dharura za matibabu, na timu za kusimama kwa gari la wagonjwa ziliendeshwa.

Aliendelea, "Kati ya madhehebu yote ulimwenguni, Kanisa la Shincheonji la Yesu ndilo pekee ambalo zaidi ya watakatifu 100,000 hukusanyika kila mwaka. Hii ni kwa sababu neno la ukweli liko Shincheonji na Mungu na Yesu wako pamoja. "Natumaini utachunguza Neno na kuwa mmoja ndani ya Biblia," alisema.
1. Lee Man-hee, Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji la Yesu, anatoa hotuba ya kumbukumbu katika 'Shincheonji Makabila 12 Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni Sherehe ya mahafali ya 114th' iliyofanyika katika Uwanja wa Daegu tarehe 12.

2. Wahitimu waliohudhuria 'Shincheonji Makabila 12 Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni Sherehe ya mahafali ya 114th' iliyofanyika katika Uwanja wa Daegu tarehe 12.

3. Wahitimu waliohudhuria 'Shincheonji Makabila 12 Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni Sherehe ya mahafali ya 114th' iliyofanyika katika Uwanja wa Daegu tarehe 12.

4. Wahitimu waliohudhuria 'Shincheonji Makabila 12 Kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni Sherehe ya mahafali ya 114th' iliyofanyika katika uwanja wa Daegu tarehe 12 wanaangalia sehemu ya maonyesho ya kadi iliyochezwa na watu wapatao 10,000.




SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0

Na WAF – Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja asasi za kiraia imepanga kuendelea kumiarisha rasilimali watu katika sekta ya afya kwa kuajiri watumishi na kutumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kufikisha huduma za afya kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo 23 Novemba 2023 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakati akifungua Mkutano wa 23 wa mwaka wa kitaalam wa mapitio ya mafanikio na changamoto katika sekta ya afya unaoendelea jijini Dodoma.

Dkt. Jingu amesema rasilimali watu ndiyo watendaji wakuu wa sekta ya afya hivyo mkutano huo umelenga kujadili upatikanaji wao sehemu ambapo kuna mapungufu lakini pia kuangalia namna ya kuwawezesha kufanya kazi kwa uadilifu wanapokua kwenye maeneo yao ya kazi.

“Uwepo wa rasilimali watu wa kutosha unaenda sambamba na utayari wa kukabiliana na changamoto pale zinapojitokeza hivyo tunataka tujenge utayari wetu wa kutosha ili majanga yanapoingia nchini yakute tukiwa tumejikamilisha”. Amesema Dkt. Jingu.

Aidha, Dkt. Jingu ameongeza kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza vya kutosha kwenye sekta ya afya ambapo miundombinu ya afya imejengwa maeneo mengi nchini, hivyo Serikali ina wajibu wa kuhakikisha huduma za afya zinapatikana katika maeneo hayo kwa kupeleka vifaa tiba pamoja na watumishi wenye ujuzi na weledi wa kutosha.

Katibu mkuu huyo ameongeza kuwa katika Mkutano huo utajadili mafanikio na changamoto zilizopatikana katika kipindi cha mwaka 2021-2022 ili kuendeleza pale palipofanikiwa na kuweka mikakati mathubuti kwenye changamoto zilizojitokeza.

Kwa upande mwingine Dkt. Jingu amesema katika nchi kujiweka tayari na changamoto za afya zinazoweza kujitokeza, Serikali imeamua kuwatumia watumishi wa afya ngazi ya jamii (CHW) kuona nini kinachoendelea katika jamii yao kuweza kuwa chachu katika kuhamasisha jamii kushughulikia changamoto zilizopo katika maeneo yao.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Wilson Mahela amesema Mkutano huo ni muhimu wa kujifanyia tathmini ya utoaji huduma katika Vituo vya kutolea huduma kuanzia ngazi ya msingi mpaka Taifa kuonyesha mafanikio na changamoto zilizoibuka.








 


WAZIRI UMMY AITAKA WIZARA YA AFYA KUWA NA MPANGO WA HUDUMA ZA METHADONE KATIKA KILA HALMASHAURI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza wakati halfa ya kukabidhi vifaa tiba,vitendanishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo ambapo zoezi hilo lilikwenda sambamba na kugawa vifaa ujasiriamali kwa ajili ya vijana waliokuwa wakipata huduma ya methadone na kuhitimu kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu na kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Doroth Lema


KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Doroth Lema ambaye pia ni Mratibu wa Huduma za Mama na Mtoto Mkoa wa Tanga


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika akikate utepe wakati wa halfa hiyo kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Doroth Lema


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Naima Yusuf aliyevaa hijabu akifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika halfa hiyo kulia ni Katibu wa Hospitali hiyo Abas Mlawa

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja










Na Oscar Assenga, TANGA.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ameielekeza Wizara ya Afya kuweka mpango wa kuhakikisha huduma za Methadone zinakuwepo katika kila Halmashauri zote 184 nchini ili kuwapunguzia wahitaji umbali wa kuzipata.

Ummy aliyasema haya leo wakati akikabidhi vifaa tiba,vitendanishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo ambapo zoezi hilo lilikwenda sambamba na kugawa vifaa kwa ajili ya vijana waliokuwa wakipata huduma ya methadone na kuhitimu.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa sambamba vile vya ujasiriamali kwa ajili ya waraibu waliomaliza matibabu yao na walipo hatua za mwishoni kupata matibabu ili waweze kupata vifaa vya ujasiriamali zitakavyowasaidia katika maisha yao watakaporudi kwenye maeneo yao

Alisema kwa sababu watu hao nauli wanapata wapi na kila siku wizara ya afya wataka kuona mpango wenu mwakani wanaongeza vituo vingapi na mwaka kesho ili mwaka 2025 wawe wamezifikia Halmashauri zote nchini.

“Kwani kuna watu wanatoka Pangani,Handeni ,Muheza Korogwe hao watu nauli kila siku wanapata wapi kuja kupata dawa na kurudi jambo ambalo linakuwa ni changamoto kwao”Alisema

Akizumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo alisema vitawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi lengo likiwa ni kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato halali na hivyo kuachana na kufikiria kurudi kwenye matumizi ya dawa hizo.

Vifaa walivyokabidhiwa vifaa kwa ajili ya kutenegeneza maridhisha ya milango seti mbili thamani ya Milioni 38 na vyerahani 10 vyenye thamani ya Milioni 48 pia watakwenda kutatafuta shule ambazo watakuwa wakiwashonea wanafunzi kila mwaka.

Aidha pia watakabidhi mashine mbili za matofali kwa siku zenye thamani ya Milioni 70 ambapo alimtaka Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga tenda ya kwanza oda ipewe watu wa MAT ili kuweza kulisaidia kundi la vijana waliokuwa wakitumia dawa zaa kulevya

Alisema msaada huo ni sehemu ya kuwainua kiuchumi ili washiriki kwenye shughuli za kimaendeleo na hatimaye wasirudi kule walipotoka katika matumizi ya dawa za kulevya.

Aidha Waziri Ummy alisema kwamba kutokana na uwepo wa maombi ya baadhi yenu kuona eneo la kuoshea magari watapeleka mpango huo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru na ile ya Mkoa wa Dodoma Utenga mashine za kuoshea magari zenye thamani ya milioni 90 .

Alisema pia katika mwezi Desemba mwaka huu watanunua vifaa vya saluni za kiume na kike lengo likiwa ni kuinua kipato cha vijana waliopo kwenye hali nzuri baada hya kupata huduma ya methadone wanaamini wataweza kujisaidia na wanawaomba wasirudi kule walipotoka.

“Ndugu zangu vijana wa Tanga ambao bado hamjaingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya msiingie huko lakini nafurahi kuna taasisi zinaelimisha vijana wa Tanga naomba waongeze nguvu katika hili ili kuwaepushga vijana na utumiaji”Alisema

Waziri Ummy pia alizitaka Taasisi ambazo zimekuwa zikitoa elimu kwa vijana viwafikie vijana kwenye shule za Msingi na Sekondari kuwahamasisha wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

“Tunaomba nyie muwe mabalolozi tuwe na mpango wa kupita kwenye shule za Msingi na Sekondari na tunaandaa mambo mbalimbali kuhakikisha tunatoa elimu kwa wanafunzi”Alisema

Kuhusu ukatishaji wa matibabu kwa waraibu.

Waziri Ummy alitumia halfa hiyo kuwataka waraibu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya dawa za kulevya kuhakikisha hawakatishi matibabu mpaka watakapoambiwa wapo sawa.

“Kwa maana kuna ambao mnapata matibab na kuamua kuacha wenyewe hapana msikatishe matibabu mpaka mtakapoambiwa mpo sawa lakini pia niwatake vijana waliopo majumbani tuache kujiingiza kwenye matumizi ya dawa hizi”Alisema

Alisema kwamba kukabidhiwa kwa vifaa hivyo inaonyesha namna Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu inavyowajali na kuwathamani watu wa aina zote ikiwemo wanyonge.

Alisema kitendo hicho ni Imani na huduma ya Rais Dkt Samia Suluhu anawajali watu wake na kuwapenda na vifaa hivyo ni kwa ajili ya kutengeneza madirisha ya milango seti mbili zenye thamani ya sh Milioni 38 .

“Hivyo niombe Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow kwamba wakati tunajenga,ofisi za kata ,oda ya kwanza watoe kwa vijana hao ambao leo wanapewa vifaa hivyo ili waweze kujikwamua kiuchumi”Alisema

Vifaa walivyokabidhiwa ni vyerahani 10 vyenye thamani ya Milioni ambapo watatafuta shule ambazo watakuwa wakiwashonea wanafunzi kila mwaka watakabidhi mashine mbili za matofali 500 kwa siku zenye thamani ya Milioni 156.

Alisema kupitia Madiwani kuhakikisha tenda za ujenzi katika maeneo mbalimbali Jijini huo kuwaangalia namna ya kjuwkwenye mashine amemuomba meya na madiwani wanafanya ujenzi mara nyiny wanaomba tenda ya kwanza wapewa watu wa MAT.

Awali akizungumza katika Halfa hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuangalia makundi yote kwa namna ya kipekee na Waziri Ummy kwa kumsaidia vizuri Rais.

Kanali Maulid ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga alisema watapokea vifaa hivyo vitavyosaidia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga- Bombo ambapo alisema vikitumia vizuri vitaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya Afya kwa wananchi wa Tanga.

Sambamba na kukabidhi dawa za tiba asili ambapo alisema ni ukweli tangu dunia imeanza wamekuwa wakipata tiba asili na zile za kisasa lakini kwa muda mrefu zilikuwa hazipewe kipaumbele .

Hivyo niwapongeze wizara kwa kutekeleza hilo wakiwatambua na kuwathamani wanaimani kwa miaka ijayo watanzania watatengeneza dawa zinazofanana na wenzao waliotutangulia.

Dkt. Kisenge: Leteni Wagonjwa wa moyo kutibiwa JKCI; Msiwapeleke nje ya nchi

$
0
0

Na Mwandishi Maalumu - Dar es Salaam.


23/11/2023 Madaktari nchini wameombwa kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu na siyo nje ya nchi kwani Serikali imewekeza vya kutosha katika vifaa tiba na rasilimali watu.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kambi maalumu ya upasuaji wa moyo inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Open Heart International la nchini Australia.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa moyo alisema kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Serikali umeufanya katika Taasisi hiyo hivi sasa wagonjwa wengi ambao ni watanzania na wasio watanzania wanatibiwa JKCI.

“Ni muhimu wagonjwa wenye matatizo ya moyo wakatibiwa hapa nchini hakuna haja ya kuwapeleka nje ya nchi kwani huduma zinazotolewa huko ndizo zinazopatikana katika Taasisi yetu”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge alisema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia Julai hadi Oktoba taasisi hiyo imepokea wagonjwa 60 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Demokrasia ya Kongo,Malawi,Visiwa vya Comoro, Burundi na Zimbabwe.

"Tulishangazwa kupokea wagonjwa kutoka Ujerumani na Ufaransa ambao wamekuja kutalii hapa nchini lakini baada ya kupata matatizo walikuja kutibiwa katika hospitali yetu, miaka ya nyuma walikuwa wanakwenda Kenya na mataifa mengine lakini sasa wanakuja kwetu hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika,"alisema Dkt.Kisenge.

Dkt. Kisenge alisema katika kambi hiyo ambayo itamalizika kesho wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji huku wataalamu wa Taasisi hao wakipewa mafunzo ya kubadilishana ujuzi katika upasuaji wa moyo.

Akizungumzia kuhusu magonjwa ya moyo Dkt. Kisenge alisema sababu kubwa ya ugonjwa huo ni shinikizo la juu la damu ambalo chanzo chake ni ulaji wa chumvi isiyopikwa, kutofanya mazoezi,matumizi ya sigara, pombe, unene kupitiliza na msongo wa mawazo na namna ya kukabili ugonjwa huo ni kuepuka vihatarishi vyake.


Aidha Dkt. Kisenge aliwasisitiza wananchi kujiunga na bima ya afya kwani gharama ya matibabu ya moyo ni kubwa lakini kama mtu akijunga na bima hiyo itamsaidia kulipia gharama za matibabu pindi atakapoumwa.


“Gharama ya upasuaji wa moyo zinafika hadi milioni 15 au zaidi lakini kama mgonjwa atakuwa na bima ya afya itamsaidia kulipia gharama za matibabu hayo”, alisisitiza Dkt. Kisenge.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Shirika la Open Heart International la nchini Australia Dkt. Darren Wolfers alisema wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya JKCI tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015.

Dkt. Wolfers alisema jambo kubwa linalowavutia kufika mara kwa mara JKCI kutoa mafunzo na kufanya kambi za upasuaji wa moyo ni upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na wataalamu wenye ujuzi mkubwa vinavyowawezesha kufanyika kwa upasuaji.






RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA EAC UNAOJADILI MASUALA YA TABIANCHI NA USALAMA WA CHAKULA MKOANI ARUSHA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye pamoja na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023


Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023

Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023
Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud pamoja na viongozi wengine wakishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto mara baada ya kuwasili Ngurdoto Mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, Rais wa Kenya Mhe. William Ruto pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Peter Mathuki wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili kuhusu masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 23 Novemba, 2023

WAZIRI JAFO ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI EAC UNAOJADILI MASUALA YA MABADILIKO YA TABIANCHI NA USALAMA WA CHAKULA JIJINI ARUSHA

$
0
0


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Usalama wa Chakula Ngurdoto mkoani Arusha leo Novemba 23, 2023. Wengine kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kariuki na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis.

Awali mkutano huo ulitanguliwa na mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira ngazi ya Mawaziri.

WATUHUMIWA WALIOJIFANYA MAAFISA TRA WATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI.

$
0
0
Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutapeli wananchi katika maeneo tofauti tofauti Mkoani humo.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Malaki (34) mkazi wa Karakata, Francis Mwita (42) mkazi wa Ukonga, Fidelis Joseph (27) mkazi wa Msumi Mbezi, Selina Fortunatus (43) makazi wa Temeke wote kutoka Jijini Dar es salaam na Fereji Hamadi (40) mkazi wa Tabora.

Aidha ACP Masejo amebainisha kuwa bado Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na pindi upelelezi utakapo kamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtka kwa hatua zaidi za kisheria.

Sambamba na hilo ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kujiridhisha na watu wanaofika maeneo yao ya biashara na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa TRA ambapo amewaomba wananchi kutoa taarifa za baadhi ya watu hao wachache wanaofanya matukio ya uhalifu hususani ya utapeli katika Mkoa huo ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake Afisa wa kodi mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Bw. Hamenyimana Ayoub amesema mamlaka ya mapato imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na uwepo wa baadhi ya watu wanaojiita maafisa wa mamlaka hiyo na kuchukua fedha.

Afisa huyo mwandamizi amendelea kufafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo kwa kushirikiana na Jeshi hilo pamoja na Wananchi walifanikiwa kuwakamata Watuhumiwa hao huko maeneo ya Manyara Kibaoni Wilayani Karatu wakati wakijaribu kutoroka.

Nae Bw Karatu John ambaye ni muhanga amebainisha kuwa watuhumiwa hao walifika dukani kwake na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa mamalaka ya mapato (TRA) nakuanza kuwahoji huku wakitaka kulipwa kiasia cha fedha ya kitanzania Milioni nne na nusu.

MHE.KIKWETE: eGA INAJUKUMU NYETI LA KUIHUDUMIA SERIKALI ILI KUTOA HUDUMA KIDIJITALI

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ina jukumu nyeti la kusanifu na kutengeneza mifumo ya TEHAMA ili iweze kutoa huduma kwa umma kwa haraka na ufanisi.

Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea Ofisi za eGA-Kituo cha Iringa ili kukagua utendaji kazi wa Mamlaka katika kituo hicho ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Dunia inakwenda kasi na teknolojia ni kila kitu kwa sasa, hivyo ni muhimu kwa eGA kufanya utafiti, kubuni na kutengeneza mifumo ya TEHAMA Serikalini kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma” amesema Mhe. Kikwete.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa eGA imeweka juhudi kubwa katika kusimamia TEHAMA Serikalini na imetengeneza na inaendelea kutengeneza mifumo ya TEHAMA ambayo imewarahisishia wananchi kupata huduma kwa haraka, mahali popote na kwa gharama nafuu na kuchagiza utawala bora.

Aidha, Mhe. Kikwete ameridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao katika ofisi zake zilizopo Iringa na amewataka watumishi wa Mamlaka kwa jumla kuendelea kubuni Mifumo ya TEHAMA inayotatua changamoto zilizopo nchini pamoja na kuwa wazalendo kwa maslahi ya Taifa.

Vile vile, amewasisitiza eGA kuhakikisha mifumo inayotengenezwa na iliyopo inakuwa na uwezo wa kuwasiliana ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Eng. Benedict Ndomba amemshukuru Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kutenga muda wake kutembelea kituo hicho cha Iringa na kuahidi kutekeleza maagizo yote aliyotoa.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora   Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa   Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wa Kituo cha Iringa ikiwa ni zaira yake ya kikazi mkoani humo 


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora   Mhe. Ridhiwani Kikwete akiangalia eneo ambalo    Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) inatarajia kujenga   Kituo chake Mkoani  Iringa.


Sehemu ya Watumshi Watumishi wa   Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wa Kituo cha Iringa ikiwa ni zaira yake ya kikazi mkoani humo wakimsiliza  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora   Mhe. Ridhiwani Kikwete

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora   Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa   Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wa Kituo cha Iringa ikiwa ni zaira yake ya kikazi mkoani humo 

KUELEKEA MIAKA 60 YA MAPINDUZI KAMPENI YA MKONO KWA MKONO YAZINDULIA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ramadhan Bukini amezindua kampeni ya mkono kwa mkono ili kutangaza Fursa zinazopatikana Nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko Afisini kwake Karume House amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 25 Mwaka huu na kurushwa moja kwa moja kupitia shirika hilo.

Alifahamisha kuwa kampeni hiyo itawashirikisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya zote za Zanzibar pamoja na Taasisi zinazohusika na uwezeshaji Wananchi ili kutoa fursa kwa taasisi hizo kuzitangaza fursa kwa jamii.

“ Kampeni hiyo inayolenga kuzitambulisha fursa zinazopatikana katika mikoa ya Zanzibar na mbinu za kuzifikia ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo.”alisema Mkurugenzi Bukini

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar Juma Burhan Mohamed amesema kampeni hiyo itasaidia kutoa taarifa zinazohusu uwekezaji,fursa za kujiajiri pamoja na upatikanaji wa masoko jambo ambalo litasaidia kuwanyanyua wajasiriamali Nchini.

Kampeni ya mkono kwa mkono imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Wakala wa uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Taasisi ya Afisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini (PDB) na Kampuni ya Mwananchi Communication ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi .
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Ramadhan Bukini akitoa ufafanuzi kuhusiana na kampeni ya mkono kwa mkono iliyoandaliwa kwa mashirikiano kati ya Shirika hilo,Maelezo Zanzibar ,Kampuni ya Mwananchi ,Taasisi ya Afisi ya Rais ufuatialiaji na usimamizi wa utendaji Serikalini (PDB), Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Wakala wa Uwezeshaji Wananachi kiuchumi (ZEEA) kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi, hafla iliyofanyika Karume House.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi,hafla iliyofanyika Karume House.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uwezeshaji Wananachi kiuchumi (ZEEA) Juma Burhan Mohammed akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi , hafla iliyofanyika Karume House.
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Mwananchi Communications Bakari Machumu akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi , hafla iliyofanyika Karume House.

Mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Muhammed Khamis akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi.

PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR


UJUMBE WA STEVE NYERERE KWA WASANII BAADA YA KUTINGA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MSANII maarufu nchini katika Tasnia ya Filamu za kibongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengele 'Steve Nyerere' amewaomba wasanii wote nchini kuungana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kukomesha matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Aidha amesisitiza watatoa kila aina ya ushirikiano kwa Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kukomesha dawa za kulevya nchini huku akiweka mkakati madhubuti wa kuwalinda wasanii dhidi ya dawa hizo na hatimaye kuwa na wasanii wenye kujikita kulinda vipaji vyao.

Akizungumza Novemba 22, 2023 baada ya kufika ofisi za Mamlaka hiyo na kupokelewa na Kamishina Jenerali Lyimo Stebe Nyerere amewaomba wasanii wenzake wamuunge mkono Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuhakikisha msanii wa Tanzania havuti unga wala havuti bangi.

Amesisitiza ni vema kuona wasanii wakiendelea kufanya sanaa zao kwenye weledi mkubwa ili kusaidia familia zao lakini vile vile kupeperusha bendera ya Tanzania."Kamishina ana nia nzuri sana ya kukuokoa kizazi chetu , Tanzania imebarikiwa na vipaji vikubwa vya kutangaza utamaduni ndani ya nchi na nje ya nchi

"Vipaji hivi kazima tuhakikishe vinaenda na utamaduni lakini vikiwa na hali na afya njema ambayo inapatikana kwa kuwa msaani mwenyewe anajitambua, tunajua wasanii wengi na ni jambo ambalo halifichiki inawezekana bila kupata stimu hawezi kupanda kwenye stegi, bila stimu mtu hawezi kucheza mpira...

" Bila kupata stimu haonekani kama anamuonekano , anataka stimu na stimu zimegawanyika katika hatua mbalimbali , kuna stimu nyingine ya unga, kuna stimu nyingine ya dawa za kulevya na kuna stimu ya Msuba.Lakini kuna stimu hata ya pombe kali lakini hivi vyote vinanyong'onyesha vipaji , hivi vyote vinamharibu msanii wetu kutokuwa na kipaji cha kupeperusha bendera yetu ya dhati, "amesema Steve Nyerere.

Aidha amesema katika mazungumzo yake na Kamishina Jenerali Lyimo amebaini dhamira ya dhati aliyonayo ya kuwapenda wasanii wa Watanzania lakini ameonesha dhahiri yake ya kuhakikisha msanii anafanya sanaa yake katika mazingira yenye afya bora.

" Lakini kikubwa zaidi tunasema yajayo yanafurahisha , ni msanii mwenyewe kujitambua na Kamishina ameelezea hapa jambo jema kwani yeye ni mpenda sanaa na alikuwa anaipenda na enzi zake alikuwa balaa lakini alijilinda mpaka akafika kwenye ndoto yake.

"Kwa hiyo na wasanii lazima tujilinde na tutimize ndoto yetu kwenye sanaa , sanaa ni ajira kama ilivyokuwa ajira nyingine, kwa hiyo ajira yote inalindwa kwa njia yoyote ili ufike malengo

Kwa upande wake Kamishina Jenerali Lyimo amemshukuru Stive Nyerere kwa kufika ofisini kwao lakini pia kwa ujumbe mzuri ambao umewapatia kutoka kwa wasanii , na wao kama Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wanatambua msanii ni hazina.

Ameongeza msanii ndiye anayefanya Tanzania ifahamike, ijulikane na kwamba msanii ni hazina, msanii ni kioo cha jamii, hivyo ni lazima sasa hiyo hazina pengine kwa gharama zozote zile ilindwe.

Amefafanha inasikitisha unapoona msanii amekuwa kwa kipaji chake na uwezo wake anatoa nyimbo nzuri zinazotambulika mpaka kidunia lakini mwisho wa siku anaingia kwenye dawa za kulevya, anapotea, hivyo wanakuwa wamepoteza kipaji, wamepoteza hazina.

"Kwa hiyo jukumu la Mamlaka ni kulinda hivyo vipaji ambavyo ni hazina ili usanii uwe ni usaniii ambao unaleta hadhi kwa taifa , unaleta hadhi kwa serikali lakini hata viongozi wa serikali na serikali kwa ujumla inawatumia wasanii katika shughuli zake mbalimbali lakini wakiwa wanaheshimika na jamii pamoja na serikali

" Ndio maana tunataka kuanzia sasa hivi tunataka tuwatoe huko , kwa hiyo tunalinda hii hazina , sote twende kwa pamoja na wasaniii iwe ni kuelimisha jamii kweli , kuifanya jamii iondokane na maovu na kurudi kwenye hali halisi ,hali nzuri , hali yenye heshima , hali yenye maadili na ndicho wanachokijenga kama Mamlaka."






WANANCHI PATENI HUDUMA KWA WATOA HUDUMA WALIOSAJILIWA NA TCRA

$
0
0


Afisa uhusiano Aika Swai kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)akitoa elimu kwa wateja waliotembelea katika banda hilo juu ya namna ya uapatikanaji wa leseni Kijiditi katika viwanja vya Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwenye maonyesho ya huduma za kifedha kitaifa

Afisa Mwandamizi mkuu,TCRA Semu Mwakyanjala TCRA akitoa elimu kwa wateja waliotembelea katika banda hilo juu ya namna ya uapatikanaji wa leseni Kijiditi katika viwanja vya Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwenye maonyesho ya huduma za kifedha kitaifa


Mmoja wa wateja waaliotembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani akisoma kipeperushi chenye miongozo mbalimbali ya Mamlaka hiyo katika wiki ya huduma za kifedha kitaifa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha
Semu Mwakyanjala Afisa Mwandamizi,TCRA,akionyesha kwa waandishi wa habari kitabu chenye mwongozo wa namna ya kujiunga kwenye klabu za kidijiti, ambapo ni kitabu cha kuanzisha na kuratibu klabu za kidijiti ambapo kitabu kilichopo mkono wa kushoto ni kwaajili ya watu wenye mahitaji maalum






Na.Vero Ignatus,Arusha


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania inaendelea kuhamasisha upatikanaji wa Leseni Kijitali kupitia mfumo wa lango kuu la utoaji wa huduma za mawasiliano (Tanzanite Portal) leseni zinazotoa huduma ni 2,518,Watoa huduma za mawasiliano wapo 1,531,Vyeti vya wanaothibitisha ubora wa vifaa vya mawasiliano wapo 2,157(type Aproval)

Semu Mwakyanjala ni Afisa Mwandamizi,TCRA Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha katika wiki ya huduma za Fedha Kitaifa alisema kuwa mfumo huo utamrahisishia mtoa huduma kuhuhisha leseni zao kirahisi kupitia mfumo huo ambapo amewasisitiza wananchi kupata huduma kwa mtu aliyesajiliwa na TCRA.

Mwakyanjala amesema katika hali ya kuendeleza huduma za kidijiti nchini TCRA inatoa rasilimali hadimu za masafa, namba na kikoa bure kwa wabunifu kwaajili ya majaribio ya tafiti zenye tija,
pia TCRA imeanzisha klabu za kijiditi Tanzania kuanzia shule za awali,msingi ,sekondari vyuo vikuu ili kukuza ustadi wa kijiditi na teknolojia miongoni mwa wanafunzi.

"Kama wewe ni fundi na unajishughulisha na nanukarabati wa vifaa vya mawasilianao kama vile simu unapaswa kuwa na leseni ya TCRA ni rahisi kujisaili kupitia www tanzanite. tcra. go. tz ili ili kupata leseni yako" alisisitiza Mwakyanjala.

Ameaniasha shughuli katika klabu hizo ni pamoja na kujumuisha mafunzo ya program mbalimbali zinazohusu teknolojia za kijiditi , ubunifu uvumbuzi kwa njia ya kompyuta , kujifunza jinsi ya kutumia programu za zana za kijiditi na miradi ya kiteknolojia inayohisiana na masuala ya kijamii na kiuchumi.

"Kwenye klabu hizi vijana wanafunzi wanaweza kunufaika kwa fursa za semina zinazotolewa na wadau mbalimbali wa sekta, pia vigezo vinaweza kubadilika kulingana na klabu,shule au chuo, na mara nyingi tunashauri wanafunzi wajiunge kwenye klabu hizi kwa hiari na inaweza kuwasiliana na mwalimu wa jukumu la. Klabuau kiongozi wa klabu"

Aidha ameainisha njia ambavyo TCRA inachukuabili kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika klabu za kijiditi ni pamoja na kuandaa kitabu cha kuanzisha na kuratibu klabu , kushirikiana na wadau wakiwemo wadau wa elimu kuhakikisha uanzishaji wa klabu pamoja na kutoa elimu.

"Wananchi mtumiaji wa husuma za. Mawasiliano za simu, intaneti , utangazaji naposta kumbuka mara zote kutumia huduma ya watoa hiduma ya liosajiliwa na TCRA , huduma iliyosajiliwa inakupa hakikisho lamusalama na ulinzi wanhaki zako za huduma" alisema

Sambamba na hayo amewata wananchi kutambua kuwa udhalilishaji mtandaoni ni kosa la jinai,hivyo amewataka kutoa taarifa kupitia mfumo wa mrejesho kwenye ukurasa wa mtandao husika,pia amewataka kutokuchapisha ma

GGML, CCBRT WAKABIDHI VITIMWENDO 55 KWA WENYE ULEMAVU GEITA

$
0
0



Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na shirika la CCBRT imetoa msaada wa viti mwendo na vifaa saidizi 55 kwa watu wenye ulemavu kutoka mkoani Geita kwa lengo la kuwarahisishia kutembea na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Msaada huo umekabidhiwa jana tarehe 22 Novemba 2023 Mjini Geita kupitia mpango maalumu wa usambazaji viti mwendo lengo la kudhihirisha dhamira ya GGML kujitolea kwa jamii na kuleta matokeo chanya mbali na shughuli za uchimbaji madini.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amesema kampuni imejitolea kuendelea kuzingatia utu kwa watu wote ikiwamo wadau wetu na jamii tunayofanyia kazi.

“Huu ni miongoni mwa mipango kadhaa ya huduma za afya ambayo tumeifanya kwa ushirikiano na CCBRT, ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii katika kutoa huduma za matibabu na urekebishaji wa viungo mbalimbali vya mwili kwa gharama nafuu na kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu na familia zao kurejesha tabasamu.

“Tunaamini kwamba kila mtu anastahili utu, heshima, na fursa sawa za kustawi maishani. Pia tunatambua kwamba watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi na vikwazo katika kupata huduma za msingi, elimu, ajira na ushirikishwaji wa kijamii. Ndiyo maana tunajivunia kuunga mkono mpango huu ambao utawapa huduma zinazofaa na zilizoboreshwa ambazo zitaboresha uhuru na ubora wa maisha,” amesema Mkurugenzi huyo.

Naye Mwakilishi kutoka CCBRT, Dk. Neophita Lukiringi amewashukuru GGML kwa kuwafikiria watu wenye ulemavu na kuwapatia viti mwendo ambavyo ni sahihi.

Amesema mtu mwenye ulemavu akipatiwa kiti mwendo ambacho si sahihi kwake kinaweza kumletea madhara zaidi.

“Lakini GGML waliona pamoja na kuwasaidia watu wenye ulemavu hawakutaka kugawa hovyo hovyo wakafikiria tupate vifaa ambavyo vitawasaidia kweli. Kwa hiyo napenda kuwashuruku sana GGML kwa kuonesha mfano mzuri kwani mtu mwenye ulemavu ukimpatia kiti mwendo sahihi utakuwa umemsaidia sana,” amesema.

Daktari huyo kutoka CCBRT amesema mtu mwenye ulevu akipatiwa kiti mwendo kisicho sahihi kinaweza kumsababisha apinde mgongo, kifupishe misuli yake na kumuongezea ulemavu zaidi.

“Kama amechukua kiti mwendo ambacho si sahihi utamfanya apate vidonda mgandamizo ambavyo vinachukua muda mrefu sana kupona na wakati mwingine vinasambaza wadudu kwenye mfumo wa damu mwisho wanakufa kabla ya wakati.

“Nasisitiza GGML wamefanya jambo zuri kutoa msaada sahihi ambao hautawaongezea ulemavu watu wenye ulemavu lakini pia utawasaidia watoto kwena shule na kushiriki kucheza na wenzao huku watu wazima nao wakishiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

“Natoa mwito kwa Watanzania ambao wanapenda kusaidia watu wenye ulemavu wasitoe viti mwendo bila kutafuta watalaam wa kushirikiana nao kwa sababu hata Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza viti mwendo vitolewe na watu waliofunzwa ili kukabili madhara hayo,” amesema.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Geita, Kanali Boniphace Maghembe ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya makabidhiano hayo, aliwapongeza GGML kwa kuendelea kuijali jamii ya watu wanaouzunguka mgodi huo.

Pia aliipongeza CCBRT kwa kuungana na GGML kutoa elimu ya kitaalamu kuhusu matumizi sahihi na kutoa ushauri sahihi wa vifaa hivyo vya watu wenye ulamvu.

Amesema, “GGML wamekuwa washirika wakubwa wa shughuli za maendeleo, wamefanya mambo mengi na mazuri kwa manufaa ya wananchi na wanaoishi katika mkoa huu, tunawashukuru sana.”

Aidha, aliahidi Serikali kuendelea kuunga mkono wawekezaji ikiwamo GGML ambayo ni kampuni inayoungana na jamii kutoa vitu na misaada ya utu kwa watu wenye mahitaji mbalimbali.

Aidha, mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Matendo Sitta aliishukuru GGML na CCBRT kwa moyo wa upendo waliouonesha na kuwapatia viti mwendo ambavyo sasa vitawasaidia kuchangamana na jamii.

“Tunaomba msiishie kwetu kwa sababu kuna wenzetu wengi wenye changamoto hivyo tunaomba waendelee kuwa na moyo wa utoaji kwa sababu sasa hivi tunaweza kwenda hata kwa jirani kupiga story na tunaahidi kutunza vyombo hivi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Kanali Boniphace Maghembe (kulia) wakiwasukuma baadhi ya walemavu walionufaika na viti mwendo vilivyotolewa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited kwa ushirikiano na Shirika la CCBRT.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong akizungumza katika hafla ya kukabidhi viti mwendo 55 kwa watu wenye ulemavu mkoani Geita.
Baadhi ya watu wenye ulemavu waliopatiwa msaada wa viti mwendo 55 na vifaa saidizi kutoka GGML na CCBRT wakiwa katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa Serikali waliojitokeza katika halfa ya makabidhiano iliyofanyika mjini Geita

VIJIJI 11,313 VIMEWASHWA UMEME VINGINE 1,005 VILIVYOSALIA KUKAMILIKA JUNI 2024

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Tanzania Bara kuna vijiji 12,318 ambapo hadi kufikia jana tarehe 23 Novemba 2023 vijiji 11,313 vimeunganishwa na umeme huku vijiji 1,005 vilivyosalia wakandarasi wapo kazini kukamilisha na kuwasha umeme.

Inatarajiwa kufikia Juni, 2024 vijiji vyote vitakuwa vimewashwa umeme kabla ya lengo kwa sababu ya serikali na wadau wa maendeleo kuwekeza nguvu zaidi katika uwezeshaji.

Aidha, mpaka sasa jumla ya vitongoji 28,659 vimefikiwa na umeme kati ya vitongoji 64,760 vilivyopo nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Jones Olotu wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kueleza utekelezaji wa majukumu ya REA katika ukumbi wa NSSSF-Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Olotu amesema kuwa serikali kupitia REA ipo mbioni kuhakikisha kuwa vitongoji 36,101 vinafikiwa na umeme na kwamba serikali imekwisha andaa mipango madhubuti na kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote vitakuwa vimefikiwa na umeme.

Kuhusu changamoto ambazo REA inakabiliana nazo amesema kuwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ikiwemo uharibifu wa nguzo kutokana na shughuli mbalimbali za wananchi katika maeneo ambayo wanachoma moto ovyo.

Hata hivyo Mhandisi Olotu ametoa mwito kwa jamii kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele kuilinda miundombinu ya nishati ili iweze kuwanufaisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati mbadala na Jadidifu Mhandisi Advera Mwijage amesema kuwa kwa sasa serikali kupitia REA inatekeleza mradi wa kupeleka umeme katika visiwa na maeneo yaliyo mbali na gridi ya Taifa.

Amesema kuwa Mradi huo unajumuisha ujenzi wa mifumo midogo ya kusambaza umeme katika maeneo yenye vyanzo vya nishati jadidifu kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ambapo mikataba miwili ya mradi wa Ikondo-Matembwe Hydro Power ulisainiwa mwezi Februari 2023 na mkataba wa mradi wa Mwenga Hydro Power ulisainiwa mwezi Machi 2023.

Amesema kuwa miradi hiyo itaunganisha jumla ya wateja wa awali 2,168 katika vijiji 42 kwa gharama ya Shilingi 3.06 bilioni.

Aidha, amesema kuwa Serikali kupitia REA imewapata waendelezaji watatu (3) ambao ni Jumeme, Volt Africa na Green Leaf Technology wa miradi ya kusambaza umeme kwa kutumia nguvu ya jua, itakayotekelezwa katika visiwa 28 vilivyopo katika mikoa ya Kagera (8), Mwanza (13), Mara (3) na Lindi (4) na hivyo kuunganisha wateja 9,515 kwa gharama ya Shilingi 11.18 bilioni.

“Wakala unakamilisha taratibu za kusaini mkataba na Kampuni ya Jumeme wakati Kampuni za Volti Africa na Green Leaf Technology zikikamilisha taratibu za kimazingira kabla ya kuendelea na hatua ya kusaini mikataba” Amesisitiza

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Ndg Deodatus Balile ameipongeza REA kwa kazi kubwa inayoifanya ya kusambaza umeme vijijini kwani hatua iliyofikia mpaka sasa ni kubwa ya kuungwa mkono.

“Pongezi hizi siyo tu za kwenye jukwaa, kwa wale waliopata fursa ya kufika vijijini wakaona kinachoendelea hakuna sehemu utapita bila kuona nguzo imelala chini, hongereni sana kwa kazi mnayofanya REA, ” amekaririwa Balile.

Kadhalika, ameitaka REA kuhakikisha kuwa inaongeza fursa ya kukutana na wahariri mara kwa mara ili kutoa elimu kuhusu miradi inayotekelezwa na serikali kupitia REA jambo litakalorahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi na jamii kwa ujumla wake.







MKOA WA PWANI UMEKABIDHI VISHKWAMBI 345 KWA MAOFISA KILIMO

$
0
0
Nov 23

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKOA wa Pwani umekabidhi vishkwambi 345 kwa Maofisa Kilimo wa Wilaya ili kuleta tija na kuongeza mnyororo wa thamani.


Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa huo ,Abubakar Kunenge wakati akikabidhi vifaa hivyo ambavyo vimetolewa na Serikali.


Kunenge amesema, vitasaidia kusajili wakulima ambao bado hawajaingizwa kwenye mfumo na kuboresha taarifa za wale waliosajiliwa ili wahudumiwe kwa idadi na kujua mahitaji yao ya pembejeo.


"Ili kilimo kiwe na tija lazima wataalamu wawe na vifaa vya kisasa na hata iwe rahisi kutoa taarifa juu ya maendeleo ya kilimo au kama kuna changamoto," amesema Kunenge.


Amesema kuwa, kupitia vifaa hivyo wataweza kutoa taarifa sahihi za pembejeo kwa wakulima kuanzia afya ya udongo, mbegu bora, mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi sahihi ya mbolea.


"Tunaipongeza Serikali kwa kutoa pikipiki 129, vifaa vya kupimia udongo sita na sasa Vishkwambi, hii inaonyesha jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kutaka kubadili kilimo kiwe na tija kwa wakulima na nchi," amesema Kunenge.


Aidha amesema , mkoa umepata mafanikio makubwa kwa sasa ambapo ubora wa zao la korosho ya daraja la kwanza umeongezeka kutoka asilimia 12 hadi 96.6.


"Zao la ufuta ubora na uzalishaji umeongezeka na tunaongeza nguvu kwenye mazao yakiwemo katani, mahindi, miwa, mihogo, chikichi, mpunga ,mbaazi pamoja na ndizi ambapo tayari kuna wawekezaji wakubwa wameshajitokeza,"


Amewataka maofisa hao kuongeza mnyororo wa thamani kupitia mazao ya kibiashara ambayo yanaongeza pato kwa wakulima.


Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Shangwe Twamala ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kutoa taarifa mbalimbali kwa Wizara na kutoa elimu kwa wakulima juu ya masuala ya kilimo.


Naye Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Joseph Njau amesema kuwa vishkwambi hivyo vitawawezesha kutekeleza majukumu yao na kuongeza uzalishaji na kuleta tija kwa wakulima kwenye maeneo yao.





Viewing all 118890 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>