Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120322 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MBEYA

$
0
0

 


AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUGONGA MAGARI 02 BAJAJI NA PIKIPIKI NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.

Mnamo tarehe 27.03.2022 majira ya saa 21:18 usiku huko katika Barabara ya Mbeya – Tunduma, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya. Gari yenye namba za usajili T. 909 DQC na tela namba T.205 DSFaina ya Scania likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ABDULRAZACK HASSAN alishindwa kulimudu gari hilo akiwa anashuka mlima Iwambi baada ya kufeli break na kwenda  kugonga  Bajaji  yenye namba ya usajili MC.999 CUD aina ya TVS King iliyokuwa uelekeo mmoja ikiendeshwa na SHUKRANI PAUL na kusababishia majeruhi na kugonga Gari yenye namba ya usajili T.128 ALE aina ya Nissan Double Cabin ikiendeshwa na EMMANUEL MAKONGANYAna kusababisha kifo kwa JEREMIAH MWASENGA ambae alikuwa abiria kwenye gari hiyo, kisha kugonga Gari yenye namba ya usajili T.387 DBD aina ya Toyota Noah  iliyokuwa ikiendeshwa na dereva  ANYENGULILE MWAMULUKI na mwisho kugonga Pikipiki yenye namba ya usajili MC.205 ARK  aina ya T-Better iliyokuwa ikiendeshwa  SUSA MBWIGA na kumsababishia kifo. 

Katika ajali hiyo watu wawili wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu Hospitali Teule ya Ifisi – Mbalizi. Aidha vyombo vyote vilivyohusika katika ajali hiyo vimeharibika. Chanzo cha ajali ni kufeli breki ya Gari Lori yenye namba ya usajili T.909 DQC/T.205 DSF Scania na kusababisha dereva kushindwa kulimudu Gari hilo. Jeshi la Polisi mkoani hapa nilimshikilia Dereva wa Gari T.909 DQC/T.205 DSF Scania kwa hatua zaidi za kisheria.

 

KUKAMATA SILAHA NA RISASI KUMI.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 28.03.2022 majira ya saa 06:30 asubuhi huko maeneo ya uhindini, Kata na Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya lilifanikiwa kukamata silaha aina ya Pistol – Liger M80, CAL.9x9 yenye Maker namba B.94554 rangi nyeusi ikiwa na risasi kumi ndani ya magazine na mkasi mmoja mkubwa.

 

Silaha hiyo ilikamatwa wakati askari wakirudi nyumbani kutokea kazini ndipo walipofika maeneo ya uhindini jirani na duka la wakala mkuu wa M-PESA aitwaye IRENE KAHEMELE waliwaona watu wawili huku mmoja akiwa amebeba begi dogo jeusi mgongoni na kuwatilia mashaka na walipojaribu kuwasogelea walianza kukimbia hali iliyopelekea askari kuanza kuwakimbiza huku akipuliza filimbi kuomba msaada ndipo watu hao walitupa begi hilo na kutokomea.

Katika upekuzi ndani ya begi hilo ndipo ilikutwa silaha moja na risasi 10 ndani ya magazine na mkasi mkubwa mmoja. Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea.

KUPATIKANA NA NOTI ZIDHANIWAZO KUWA NI BANDIA. 

Mnamo tarehe 26.03.2022 majira ya saa 13:30 mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msakohuko kijiji cha Nsongwi Mantanji, Kata ya Ijombe, Tarafa ya Tembela, Wilaya na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata FIDELIS KOMBA [42] Mganga wa tiba asilia, Mkazi wa Nsongwi – Mantanji akiwa na noti 219 za Tshs 10,000/= zote zikiwa na namba KL 4105891na noti 230 za Tshs.5,000/= zote zikiwa na namba HF 4424893zinazodhaniwa kuwa ni noti za bandia.

Mtuhumiwa kabla ya kukamatwa alitajwa na mtuhumiwa mwenzake aitwaye  FERUZ SELEMAN [35] Fundi ujenzi na Mkazi wa majengo mapya Nsalaga ambaye alikamatwa tarehe 25.03.2022 majira ya saa 20:45 usiku huko maeneo ya Isyesye -Madukani, Kata ya Isyesye, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya akiwa na noti bandia 69 za Tshs 5,000 zote zikiwa na namba HF 4424893hivyo kufanya jumla ya noti 299 za Tshs.5,000/= akiwa katika harakati za kutaka kuziingiza kwa wakala wa mitandao ya fedha kwa nia ya kuzihalalisha fedha hizo  na baada ya kuhojiwa kwa kina ndipo alimtaja FIDELIS KOMBA kuwa ndio aliyempa noti hizo. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa noti bandia.

 

Imetolewa na:

[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


CHUO KIKUU MZUMBE CHATOA TAARIFA YA VIFO VYA WATUMISHI WAKE

TANZANIA YAISHUKURU OPEC FUND KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0



Na Benny Mwaipaja, Dodoma

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameushukuru Mfuko wa nchi zinazozozalisha Mafuta kwa wingi Duniani (OPEC FUND), kwa kuwekeza hapa nchini zaidi ya dola za Marekani milioni 218, sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 504, kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Dkt. Nchemba, alitoa shukrani hizo Jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika hilo ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Mfuko huo.

 

Alisema kuwa fedha hizo zimeelekezwa kwenye miradi mbalimbali, ukiwemo mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe, mradi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu, barabara ya Uvinza-Ilunde – Malagarasi pamoja na kufadhili mradi wa kupambana na Umasikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF

 

“OPEC FUND, mmekuwa msaada mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu katika kukuza uchumi wa nchi, kupunguza umasikini wa wananchi nana kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii watu wetu” alisema Dkt. Nchemba

 

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua umuhimu wa Sekta Binafsi katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi na imejitahidi kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyajibiashara katika sekta hiyo.

 

Alisema kuwa Serikali imeongeza kiwango cha mikopo kwa Sekta Binafsi kutoka asilimia 5.1 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 5.9 mwaka 2021 na kuahidi kuwa kiwango hicho kitaendelea kuongezeka kadri hali ya uchumi itakavyoimarika, pamoja na kuendelea kuimarisha sera za kiuchumi na kifedha zitakazoendelea kujenga imani kwa wawekezaji na sekta binafsi.

 

Aidha, Dkt. Nchemba alitumia fursa ya mkutano huo kuliomba Shirika hilo kutoa fedha kwa njia ya mikopo nafuu na misaada kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya iliyopangwa kutekelezwa na Serikali, ikiwemo ujenzi wa nyumba 10,000 za watumishi wa umma, kukuza mauzo ndani na nje ya nchi kupitia taasisi za fedha na sekta binafsi, pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tunguu – Makunduchi visiwani Zanzibar, yenye urefu wa km 48.

 

Aliitaja miradi mingine inayoombewa fedha kutoka Shirika hilo kuwa ni Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Songea mkoani Ruvuna, Mradi wa Maji Safi na salama wa Mafinga, mkoani Iringa na Ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Dawa na Vifaa Tiba, Chamazi, Jijini Dar es Salaam.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa OPEC FUND, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, aliahidi kuwa Mfuko wake utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ili kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.

 

Alisema kuwa Mfuko huo umepanga pia kushirikiana na Tanzania kuisaidia sekta binafsi ili iweze kukua zaidi na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwa sekta binafsi ndiyo injini ya ukuaji huo wa uchumi na maisha ya wananchi.


Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Nadhifa Kemikimba na viongozi kutoka idara mbalimbali za Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ujumbe kutoka Mfuko wa OPEC.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi zawadi yenye picha ya baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo, ofisini kwake, Jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi zawadi yenye picha ya baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo, ofisini kwake, Jijini Dodoma.




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, baada ya kukamilika kwa mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh (wa tatu kulia), Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Nadhifa Kemikimba, na Mkurugenzi Mkuu Msadizi anayesimamia Idara ya Sekta Binafsi (OFID), Bw. Fuad Albassam (wa pili kushoto), jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na Ujumbe wa OPEC FUND, Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhe. Nadhifa Kemikimba.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, zawadi yenye picha ya kazi zinazofanywa na Serikali katika kuwaondolea wananchi umasikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF, ofisini kwake, Jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akipokea zawadi ya kisahani chenye alama ya shughuli zinazofanywa na Mfuko wa OPEC, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, alipomtembelea Waziri wa Fedha, Ofisini kwake, Jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa OPEC, Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh (wa nne kushoto), pamoja na ujumbe wa Tanzania na OPEC FUND, Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

KAMATI YA PAC IMMETEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UKARABATI NA UJENZI KATIKA CHUO CHA UALIMU VIKINDU

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet Hasunga wakiangalia kisima cha maji katika Chuo cha Ualimu Vikindu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho.



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa mabweni katika Chuo cha Ualimu Vikindu, Kamati ya PAC imetembelea Chuo hicho na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho.



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Japhet Hasunga akivalishwa skafu na kijana wa skauti wakati kamati hiyo ilipowasili katika Chuo cha Ualimu Vikindu na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo hicho



Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na watendaji wa Chuo cha Ualimu Vikindu wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo hicho na kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali, katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Japhet Hasunga na Mkuu wa Chuo Amina Tou

PICHA NA OFISI YA BUNGE

AJALI YAUA WAWILI NA KUJERUHI WENGINE WAWILI HUKO MIWALENI KIBAHA VIJIJINI- RPC LUTUMO

$
0
0

 Mwamvua Mwinyi,Pwani


WATU wawili wamefariki dunia pamoja na kujeruhi wengine wawili ,katika ajali iliyohusisha magari matatu kugongana huko maeneo ya Miwaleni, Halmashauri ya wilaya Kibaha Vijijini mkoani Pwani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,Pius Lutumo alieleza, ajali hiyo imetokea march 28 asubuhi.

Alieleza kuwa, gari namba T608 AGV  likiwa na tela lenye namba T.317 AQM aina ya scania likiendeshwa na Raymond Kimaro (36) ,mkazi wa Ubungo likitokea nchini Kongo kwenda Dar es salaam ambapo lilihamia upande wake wa barabara na kugonga gari namba T.256 CMF aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Alieleza,hali hiyo ilisababisha kontena kuchomoka na kuangukia gari SU 38223 aina ya Toyota land cruiser iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kwenda Morogoro ikiendeshwa na Innocent Gerson Mringo na kusababisha vifo na majeruhi hao.

Lutumo alitaja waliofariki dunia kuwa ni profesa Prosper Ngowi (55) mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Na Innocent Gerson (33) mkazi wa Dar es Salaam na dereva.

Majeruhi ni Raymond Kimaro (39) dereva wa lori T.608 AGV na Abdallah Mohammed (33)dereva wa Noah mkazi wa Dar es Salaam na kusababisha uharibifu wa magari.

Kamanda huyo alifafanua, chanzo Cha ajali bado kinachunguzwa hata hivyo uchunguzi wa awali unaonyesha Kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya scania kuhama upande wake wa barabara na kugonga gari aina ya Noah na kupelekea kontena kuchomoka na kuliangukia gari Toyota cruiser.

Lutumo alisema, mwili wa marehemu profesa Prosper Ngowi umehifadhiwa hospital ya rufaa Tumbi na mwili wa marehemu Innocent Gerson umehifadhiwa katika kituo cha afya Mlandizi.

Majeruhi wametibiwa na hali zao ni nzuri huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa hatua zaidi.

Lutumo aliwaasa madereva kuacha kuendesha pasipo kufuata Sheria za Usalama Barabarani,na wawe makini ili kujiepusha na ajali.

 

TANZANIA, LIECHTENSTEIN KUWEKEZA KATIKA KILIMO HAI Inbox

$
0
0

Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania na Liechtenstein zimekubaliana kuweka mpango mkakati wa kuwekeza katika kilimo hai na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo katika mikoa ya Morogogo na Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler ambaye yuko nchi kwa ziara ya kikazi.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubalia kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Utalii, Viwanda, na Elimu, hususan kumuendeleza mtoto wa kike katika masomo ya sayansi na teknolojia.

“Tumekubaliana mara baada ya ziara yake tuweze kuangazia namna gani tunaweza kudumisha na kuendeleza maeneo mapya ya ushirikiano baina yetu kwa maslahi ya Tanzania na Liechtenstein,” Amesema balozi Mulamula.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler amesema Liechtenstein ina uhusiano imara na wa siku nyingi, na tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo hapa nchini Tanzania hivyo kuja kwetu hap ani kuja kuiona miradi hiyo na kutuwezesha kujadiliana kwa pamoja ni namna gani tunaweza kuendele kushirikiana katika miradi hiyo.

"Katika kikao changu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tumejadili mambo mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zetu, lakini kubwa kabisa tumekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano," Amesema Waziri Hasler.

Waziri Hasler akiwa nchini atatembelea miradi mbalimbali ya kilimo hai inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Liechtenstein kupitia Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) katika mkoa wa Morogoro na Dodoma.



Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Mjumbe aliyeambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler akifafanua jambo wakati wa kikao


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler na Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (kulia mwa Balozi Mulamula). Wengine ni Viongozi walioambatana na ujumbe wa Waziri Hasler pamoja na Afisa Mwandamizi kutoka wizarani.

WAZIRI DKT. GWAJIMA AFUNGUKA MAFANIKIO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0


Na MJJWM - Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima ameyataja mafanikio ya Wizara hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani na kusema Wizara yake imepata mafanikio yakupigiwa mfano.

Waziri Dkt. Gwajima, ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma Machi, 28, 2022 kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Waziri Dkt. Gwajima alisema ndani ya mwaka mmoja Serikali ya Rais Samia, imewatambua rasmi Wamachinga kuwa Kundi Maalum ambapo tarehe 22-23 Februari 2022, Wizara iliandaa semina elekezi iliyofanyika Jijini Dodoma ikijumuisha viongozi 10 wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) ngazi ya Taifa pamoja na viongozi 78 kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

“Kwenye kutekeleza ajenda ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia na malengo ya jukwaa la kimataifa la kizazi chenye Usawa, tayari Mheshimiwa Rais Samia ameshaunda Kamati ya kitaifa ya ushauri yenye Wajumbe 25 kutoka Pande mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar) na kufanya uzinduzi jijini Dodoma Desemba16, 2021” alisema Dkt. Gwajima

Dkt. Gwajima alisema Serikali ndani ya mwaka mmoja tayari wamejenga Makao ya Taifa ya watoto yaliopo Kikombo Dodoma yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.7 ambapo jumla ya watoto 250 wanahudumiwa katika makao hayo.

Waziri Dkt. Gwajima ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kukabiliana na vitendo vya ukatili ambapo hadi kufikia Februari 2022, jumla ya Madawati saba (7) yameanzishwa katika Taasisi za Elimu saba (7) ambazo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya cha Bugando.

Dkt. Gwajima amezidi kufafanua kuwa katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2022, Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto 1,843 zimeanzishwa na kufanya idadi ya kamati za hizo kufikia 18,186 kati ya Kamati 20,750 zilizokusudiwa kuanzishwa kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa hadi Taifa ifikapo Juni 2022

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amesema katika kukabiliana na upungufu wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Tasisi ya Manedeleo ya Jamii Kijitonyama, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vimeendelea kutoa elimu kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambapo Mwaka 2021/22, jumla ya wanafunzi 5,014 wa fani ya maendeleo ya jamii na wanafunzi 3,234 wa fani ya ustawi wa jamii walidahiliwa kwa mujibu wa vigezo vya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

“Jumla ya wanafunzi 4,500 walihitimu katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Vyuo sita (6) vya Maendeleo ya Jamii vya Buhare, Rungemba, Ruaha, Uyole, Mlale na Monduli pamoja na Vyuo viwili (2) vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai. Aidha, jumla ya wanafunzi 2,493 walihitimu katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama” alisema Dkt. Gwajima.

Mafanikio mengine yaliyopatikana ni kuhamashisha jamii katika ujenzi wa nyumba bora ambapo zimeongezeka kutoka nyumba 751 mwaka 2020 hadi kufikia nyumba 3,257 Februari 2022 ambapo nyumba hizo zilizojengwa Mikoa ya Arusha, Morogoro, Songwe, Shinyanga, Pwani, Katavi, Mtwara, Singida na Mwanza.

Akizidi kufafanua mafanikio hayo Dkt. Gwajima alisema, Wizara imeendelea kusimamia uanzishaji na uendeshaji wa huduma za vituo vya kulelea watoto wachanga na watoto wadogo mchana, ambapo katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2022, Wizara imefanikiwa kusajili vituo 303 vilivyodahili watoto 6,772 (Me 3,194 na Ke 3,578), vituo hivyo vimewezesha watoto kupatiwa huduma zinazochochea uchangamshi wa awali wa makuzi kimwili, kiakili, kihisia, kijamii na ukuaji wa lugha pamoja.

Dkt. Gwajima, alisema kutokana na maelekezo Ilani ya Uchaguzi Mkuu CCM Kifungu 93 (A na D na F); Serikali imekamilisha uundaji wa Mabaraza ya Wazee katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na kisha kuunda Baraza la Taifa la Wazee na hivyo kufikia lengo la kuwa na Mabaraza 20,749. Aidha uwepo wa mabaraza hayo imesaidia kupunguza mauaji ya wazee kutoka 190 mwaka 2015 hadi 54 kufikia Februari, 2022.

”Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Juni 2021, wazee 758,498 (475,252 Me na 283,246 Ke) wametambuliwa ambapo wazee 508,595 sawa na asilimia 67 wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure na Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF) ’’. alisema Dkt. Gwajima

Akiwa anahitimisha taarifa yake kwa vyombo vya Habari Dkt. Dorothy Gwajima, alItoa muelekeo wa bajeti ambapo amefafanua kuwa ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya wizara, Serikali imewezesha kuongezeka kwa bajeti ya Wizara kutoka Shilingi 33,195,738,400 Bilioni, mwaka 2020/21 hadi Shilingi 43,625,929,000 Bilioni, mwaka 2021/22 ikiwa ni ongezeko la Shilingi 10,430,190,600 sawa na asilimia 31.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ni Wizara mpya iliyogawanywa kutoka iliyokuwa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Watoto.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima kaizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaid Ali Khamis kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amon Mpanju.
Baadhi ya wakurugenzi kutoka WIzara ya na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Picha zote na Kitengo cha Mawasilianio Serikalini WMJJWM

 



 

TANZANIA YASHIRIKI MAKABIDHIANO YA MAJUKUMU BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Innocent Shiyo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika hafla ya kupokea majukumu ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yaliyokabidhiwa kwa Nchi 15 wanachama wapya, Tanzania ikiwemo na wajumbe wa Baraza hilo wanaomaliza muda wao.

Hafla hiyo ambayo imefanyika hivi karibuni jijini Maseru, Lesotho na kuratibiwa na Sekretarieti ya Umoja wa Afrika, ilitanguliwa na warsha iliyolenga kuwawezesha Wajumbe wa Baraza kubadilishana uzoefu na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu majukumu ya Baraza hilo.

Wakati wa warsha hiyo ambayo ilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Ufalme wa Lesotho, Mhe. Mats’epo Ramakoae, Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi Wanachama 15 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika walibadilishana uzoefu kuhusu mamlaka na taratibu za Baraza hilo, vihatarishi kwa amani na usalama barani Afrika na namna ya kuimarisha ufanisi wa Operesheni za Kulinda Amani za Umoja wa Afrika. Aidha, maeneo ambayo yanakusudiwa kupewa kipaumbele na Baraza jipya pia yalijadiliwa.

Akizungumza baada ya warsha hiyo, Mhe. Balozi Shiyo alieleza kuwa, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika na watu wa Afrika kwa ujumla wana matarajio makubwa kwa chombo hicho katika kuchangia na kuimarisha hali ya amani na usalama barani Afrika, Bara ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi. “Tanzania chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa mchango wake kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutumia Baraza la Amani na Usalama kutatua changamoto za kiusalama na kuimarisha amani na utulivu barani Afrika” alisema Balozi Shiyo.

Itakumbukwa kuwa,Tanzania ilichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2022. Tanzania itahudumu kwenye Baraza la Amani na Usalama kwa kipindi cha miaka 2 kuanzia tarehe 01 Aprili 2022. Nchi 15 Wanachama wapya wa Baraza jipya la Amani na Usalama ni Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Djibouti, Gambia, Ghana, Morocco, Namibia, Nigeria, Senegal, Afrika Kusini, Tanzania, Tunisia, Uganda na Zimbabwe.

Kwa mujibu wa Mkataba ulioanzisha Umoja wa Afrika, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ni chombo cha kudumu na cha maamuzi kuhusu masuala yote yanayohusu kuzuia, kukabiliana na kusuluhisha migogoro barani Afrika.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Innocent Shiyo akikabidhiwa Bendera ya Taifa kutoka kwa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania, Ethiopia, Bi. Elizabeth Rwitunga kama ishara ya kupokea rasmi majukumu ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 15 zinazounda Baraza hilo. Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Maseru, Lesotho. Tanzania ilichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2022. Tanzania itahudumu kwenye Baraza hilo kwa kipindi cha miaka 2 kuanzia tarehe 01 Aprili 2022.


Mhe. Balozi Shiyo (wa nne kushoto) akiwa na wajumbe wengine wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mara baada ya wajumbe hao wapya 15 kukabidhiwa majumu ambayo yataanza kutekelezwa rasmi tarehe 01 Aprili 2022.


Picha ya pamoja


Wajumbe wengine wakiwa na Bendera za Nchi zao mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya Baraza la Amani na Uslama la Umoja wa Afrika.




Waziri Makamba akutana na ujumbe wa Benki ya Dunia, wajadili maendeleo Sekta ya Nishati

$
0
0

Na Zuena Msuya DSM,

Waziri wa Nishati January Makamba amekuta na ujumbe wa benki ya dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa benki hiyo kwa upande wa Tanzania, Mara Warwick, na kuzungumzia mambo mbalimbali kubwa likiwa ni uendelezaji wa Sekta Nishati ikiwemo masuala ya umeme na gesi.

Katika mazungumzo hayo, Makamba ameishukuru benki hiyo kwa ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania pia kuwezesha utekelezaji wa miradi ya Maendeleo nchini ukiwemo ule wa kuinganisha Tanzania na Zambia (TAZA).

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022, pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yamelenga zaidi kuimarisha ushirikiano kati ya benki hiyo na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Serikali ya Tanzania inaishukuru Benki ya Dunia kwa kuwezesha miradi ya nishati hapa nchini, tunawaahidi tutaendelea kushirikiana na katika nyanja mbalimbali kwa kuwa tumeona matokeo chanja katika miradi ambapo benki hiyo imeiunga mkono hasa katika Sekta ya Nishati,” alisema Makamba.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Seif Said na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Anitha Ishengoma pamoja na Viongozi wengine waandamizi kutoka Wizarani, REA na TANESCO.

Katika kikao hicho wamejadili mradi wa Usambazaji wa umeme vijiji, njia kuu za kusafirisha umeme pamoja masuala ya gesi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Warwick amemueleza Waziri wa Nishati kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kuinguka mkono sekta ya Nishati, ili kutanua wigo wa ukuaji wa maendeleo ya sekta hiyo.

Pia watawajengea uwezo wataalam wa kada hiyo ili kuweza kuongeza tija na ufanisi katika sekta hiyo.

Waziri wa Nishati January Makamba, (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa upande wa Tanzania, Mara Warwick, (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya miradi ya sekta ya Nishati, kilichofanyika mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022.

Waziri wa Nishati January Makamba, (katikati), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa upande wa Tanzania, Mara Warwick ,(wa pili kushoto) wakati wakizungumza wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya miradi ya sekta ya Nishati, kilichofanyika mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Seif Said,( kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Wakala wa Nishati Vijijini( REA), Mhandisi Jones Olotu, wakiwa katika kikao cha kujadili maendeleo ya miradi ya sekta ya Nishati, kilichofanyika mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022.

Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali (wa pili kushoto) na Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Umeme Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangira (kushoto) wakiwa katika kikao cha kujadili maendeleo ya miradi ya sekta ya Nishati, kilichofanyika mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022.
Waziri wa Nishati January Makamba, (katikati) akizungumza na ujumbe kutoka Benki ya Dunia, Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya miradi ya sekta ya Nishati nchini, kilichofanyika mkoani Dar Es Salaam, Machi 28, 2022.

 

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UINGEREZA TONY BLAIR IKULU CHAMWINO JIJINI DODOMA

$
0
0


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


TUNAIWAZA ROBO FAINALI KULIKO KITU CHOCHOTE - AHMED ALLY

$
0
0


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Wawakilishi pekee kwenye Michuano ya Kimataifa, ngazi ya Klabu, Simba SC wikiendi hii, Aprili 3, 2022 watakutana na timu ya USGN ya Niger katika mchezo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho barani Afrika, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Ahmed Ally amesema wamejipanga kufanya vizuri katika mchezo huo kuhakikisha wanafuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo, amesema wanataka zaidi kufuzu hatua hiyo kuliko kitu chochote.

“Tunaingia kwenye mchezo wetu dhidi ya USGN, tukiwa tumejiandaa kufanya vizuri ili tufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho. Tunashukuru hadi sasa tuna majeruhi mmoja tu, ambaye ni Hassan Dilunga, lakini Sadio Kanoute amerejea tayari Kikosini licha na yeye kutoka kwenye majeruhi”, ameeleza Ahmed.

Pia ameeleza kuwa Simba SC imejifunza kuwa makini katika michezo muhimu zaidi, tangu ilipotolewa na UD Songo ya Msumbiji na Jwaneng Galaxy FC ya Botswana ambao waliwatoa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua muhimu ikiwa hatua ya kufuzu makundi.

“Wachezaji wetu wanajua nini kipo nyuma yao, wanajua nini Wanasimba wanahitaji, wanajua mchezo huo ni muhimu kuhakikisha tunafuzu Robo Fainali ya Michuano hiyo”, amesema Ahmed.

Union Sportive Gendarmerie Nationale wanatarajiwa kutua siku ya Alhamisi, Machi 31, 2022 kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Simba SC. Mwamuzi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Helder Martins kutoka nchini Angola.


 

Makamu wa Rais mgeni rasmi uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa 2022 Njombe

$
0
0


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 zitakazo fanyika mkoani Njombe tarehe mbili mwezi April.

Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Prof. Jamal Katundu ametoa taarifa hiyo mkoani Njombe mara baada ya kukagua uwanja wa Sabasaba uliopo mjini Njombe kutakapofanyika sherehe hizo.

“Ukiangalia uwanja zaidi ya 90% umekamilika kwa hiyo nitumie nafasi hii kuwapongeza Njombe na kuwaomba wananchi mjitokeze kwa wingi tarehe mbili katika uzinduzi wa mbio za mwenge.tunategemea mgeni rasmi atakuwa makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Philip Mpango”alisema Katundu

Prof. Katundu amesema ameridhishwa na hali ya maandalizi inayoendelea ambapo amepongeza kamati za maandalizi za mkoa wa Njombe kwa kuandaa maonesho ya wajasiriamali ambayo yameanza ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya siku ya uzinduzi wenyewe.

“Kwa mara ya kwanza wanaNjombe wamejiongeza,kabla ya kufikia kilele watakuwa na shughuli mbali mbali za kibiashara tuwaombe pia watu wajitokeze kwenye hayo maonesho”aliongeza Katundu

Wakazi wa mkoa huu wameendelea na shughuli mbalimbali za maandalizi huku wakihamasishana kujitokeza kwa wingi. Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Njombe kwa mwaka huu 2022 ukiwa na kauli Mbiu “Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa.”


 

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI ATAKA UADILIFU MIRADI YA TASAF MWANZA

$
0
0




NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka Waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Mkoa wa Mwanza kusimamia kwa uadilifu miradi 104 yenye thamani ya Sh Bilioni 7.8 itakayotekelezwa ndani ya Mkoa huo.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati alipokua akizungumza na watendaji wa TASAF Mkoa huo ambapo aliwataka kusimamia miradi hiyo kwa uzalendo huku pia akiwataka Waratibu hao kuwashirikisha viongozi wa Wilaya na Mkoa kwenye kila mradi unaotekelezwa na TASAF.

"Ndugu zangu Rais Samia ametoa Sh Bilioni 7.8 kwenye Mkoa huu pekee kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 104 ambayo imepitishwa na Wizara. Miradi 31 ya Afya, Miradi 49 ya Elimu na Miradi 24 ni ya kutoa ajira za muda.

Miradi Hii itatekelezwa kwenye Halmashauri zote nane za Mwanza, hakikisheni inakamilika kwa wakati na thamani ya fedha ionekane, kama kuna mtu anafikiria hizo fedha ajue zitamtokea puani, hatutoruhusu ubadhirifu wowote utokee na TAKUKURU niwatake muwe macho kwenye ujenzi wa miradi Hii yote," Amesema Ndejembi.

Naibu Waziri Ndejembi pia amewataka Waratibu hao kuwashirikisha viongozi wengine juu ya utekelezaji wa miradi hiyo ili waweze kuifahamu na kuifanyia ufuatiliaji pindi inapokua inatekelezwa.

" Msifanye miradi bila kuwashirikisha viongozi, Wakuu wa Wilaya na Wabunge, wao pia ndio wenye kujua mahitaji haswa ya wananchi wa eneo husika, nyie mnaweza kusema hapa paletwe kituo cha Afya kumbe Mbunge alishaomba Serikalini na akaahidiwa atapatiwa sasa mkishauriana inakua ni vizuri maana yake mtapang kwa pamoja jambo la kufanya ambalo litawanufaisha wananchi," Amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Mwanza, Monica Mahundi amesema TASAF awamu ya tatu imekua na mafanikio makubwa ambapo Kaya zilizotambuliwa na kuandikishwa kwa kuzingatia vigezo zinaendelea kupokea malipo ya ruzuku, Kaya nufaika zina uhakika wa kula milo miwili au mitatu tofauti na awali kwa asilimia 92 na Walengwa 38,804 wameanzisha shughuli za kujiongezea kipato ambazo ni Kilimo, Ufugaji na Biashara ndogo ndogo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Mwanza na Waratibu wa TASAF Mkoa huo kwenye kikao kazi chake na Waratibu hao.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike, Wakuu wa Wilaya za Ilemela na Magu na baadhi ya wawakilishi wa TASAF Makao Makuu mara baada ya kumaliza kikao kazi na Waratibu wa TASAF Mkoa wa Mwanza.
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TASAF, Sarah Mshiu akizungumza na Waratibu wa TASAF Mkoa wa Mwanza wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi na watumishi hao leo Jijini Mwanza.
 
Waratibu wa TASAF Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi alipofika kuzungumza nao Jijini Mwanza leo.

Kamisaa wa sensa Zanzibar ataka wananchi kuelewa umuhimu sensa ya watu na makazi

$
0
0


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wakati zoezi la ukusanyaji wa taarifa za mfumo wa anwani za makazi na postikodi likiendelea kote nchini,Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Mohamed Haji Hamza ametoa agizo kwa wakusanya taarifa za makazi na makarani kote nchini kuifanya kazi hiyo kwa umakini kwa kuwa zoezi hilo linabeba mipango ya muda mrefu ya serikali.

Balozi Mohamed Haji Hamza amesema hayo wakati alipokutana na katibu tawala wa Mkoa wa Njombe, Judica Omari ofisini kwake kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa na kusema mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu zimelenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa.

“Hapa tupo na vitu viwili kwa maana mkoa umebeba hili la mwenge kwasababu sehemu kubwa ya ujumbe wa mwenge itakuwa na sense ya watu na makazi”alisema Balozi Mohamed Haji Hamza

Akizungumza namna serikali ilivyojipanga kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kiwango cha juu Balozi Mohamed Haji Hamza amesema.

“Tunahitaji kuwa na nguvu za pamoja kuweza kuhamasisha na kueleimisha wananchi ili waweze kukubali kuhesabiwa siku ya sensa”

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Judica Omari amesema wakati mkoa umejiandaa kikamilifu kushiriki uzinduzi wa mbio za Mwenge suala la kufanyika kwa sensa ya watu na makazi nalo lina umuhimu mkubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tunajua swala hili litasaidia kwa kuwa maendeleo yetu sasa tunayoyapanga,yanaenda kupangwa kwa usahihi zaidi kutokana na takwimu tutakazo kuwa nazo zitakuwa za uhakika zaidi”

Wakati serikali ikihimiza utekelezaji wa zoezi hilo, Mkuu wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amezindua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa kukusanya taarifa za mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa makarani katika halmashauri ya mji wa Njombe. 

Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Mohamed Haji Hamza akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa Njombe alipofika mkoani Njombe.

Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Mohamed Haji Hamza akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Njombe.


MTANZANIA ANAYEISHI NCHINI CANADA AONESHA NIA YA KUWEKEZA NCHINI KATIKA SEKTA YA MIUNDOMBINU YA BARABARA

$
0
0

Mtanzania anayeishi nchini Canada Bw. Joseph Katallah ameonesha nia ya kuja kuwekeza nchini katika sekta ya miundombinu kwa kushirikiana na kampuni ya Geopolymer Solutions LLC ya nchini Marekani hususan kwenye ujenzi wa barabara za lami kwa kutumia teknolojia mpya iliyogunduliwa na kampuni hiyo.

Wawekezaji hao wanaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wapo nchini kwa ziara ya wiki moja ambapo wanatumia fursa hiyo kukutana na wataalamu wa sekta ya barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania - TARURA, Wakala wa Barabara Tanzania - TANROADS, na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Lengo la ziara ya wawekezaji hao pamoja na mambo mengine ni kuitangaza teknolojia mpya ya utengenezaji wa barabara za lami zisizotumia saruji ya kiwandani na badala yake zitatumia udongo mwekundu ambao pia unapatikana nchini.

Wawekezaji hao wameeleza kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kupewa kipaumbele katika uwekezaji wa teknolojia hiyo kufuatia uwepo wa rasilimali za kutosha hapa nchini zitakazowezesha matumizi ya teknolojia hiyo yenye gharama nafuu na rafiki kwa mazingira ili iweze kutumika kuchochea maendeleo chanya kwa Taifa.

Wakati huo huo, wataalamu kutoka sekta ya barabara wameeleza kuwa ni vema uwekezaji wa aina hiyo ukafuata taratibu zilizowekwa katika mfumo wa Serikali na kuruhusu kufanyika kwa tafiti inayopimika ili kujiridhisha na ufanisi wake katika ardhi na hali ya hewa ya Tanzania.

Vilevile, wakaeleza umuhimu wa teknolojia hiyo kufanyiwa majaribio katika maeneo korofi kufuatia wawekezaji hao kueleza ufanisi wa teknolojia hiyo katika maeneo mengi korofi ambayo kampuni zenye teknolojia nyingine zimeshindwa kukidhi na kudhibiti changamoto hiyo.

Hivyo, kikao hicho kiliazimia wawekezaji hao wakutane na wataalamu wanaoshughulikia viwango vya ubora wa barabara nchini ili kujihakikishia ubora na ufanisi wa teknolijia hiyo mpya kabla ya kufikia hatua ya kukubaliana na uwekezaji huo. Pia uhakiki huo utasaidia kufahamu unafuu wa gharama, uokoaji wa muda, sambamba na upekee na uwezo wa teknolojia hiyo mpya ukilinganishwa na teknolojia inayotumika sasa.

Kampuni ya Geopolymer Solutions LLC inauzoefu wa kufanya kazi katika nchi za Canada, Marekani na Uingereza. Kwa upande wa nchi za Bara la Afrika, pamoja na kutoa kipaumbele kwa Tanzania pia nchi ya Ghana imeonesha kuhitaji kujifunza teknolojia hiyo mpya.



Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago (Kushoto) akifafanua jambo kwenye kikao kati ya Wawekezaji wa Kitanzania wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) na Taasisi zake ambao ni; (Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini - TARURA, Wakala wa Barabara Tanzania-TANROADS) na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kilichoratibiwa na Idara hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi John Ngowi.


Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi, Alois Matei (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya taratibu za ugunduzi wa teknolojia mpya na uwekezaji zinavyofanyika nchini ili kuweza kurasimisha ugunduzi huo unaofanywa na Watanzania pamoja na Wawekezaji kutoka Nje. Kulia kwake ni Rais wa Kampuni ya Geopolymer Solutions, LLC, Bw. Rodney Zabrod, Bw.Amon Mahuza, Mtanzania mwenyeji aliyeambatana na wawekezaji hao na Bw. Joseph Katallal mtanzania anayeishi nchini Canada.


Wajumbe wengine kutoka sekta za Ujenzi wakifuatilia kikao hicho.


Kikao kikiendelea.



Bi. Mwakawago akizungumza na Mhandisi John ngowi na Dkt. Philemon Msomba kutoka Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TATURA) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.




WIZARA YA MADINI YAWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA KAMATI YA BUNGE

$
0
0

 

Dodoma
.
Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini yake zimewasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 katika vikao vya kamati  za bunge vinavyoendelea  jijini Dodoma.

Akiainisha maeneo ya kipaumble  kwa  Mwaka wa Fedha 2022/2023, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini  Bw. Adolf  Ndunguru amesema kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa; kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi wa madini; na kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na  kuhamasisha biashara na uwekezaji katika Sekta ya Madini;  kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya Wizara ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi; kusimamia mfumo wa ukaguzi wa shughuli za migodi; na  kuendeleza rasilimali watu na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

Pia,  Katibu Mkuu Ndunguru ameieleza kamati hiyo  kuhusu misingi ya Makadirio ya makusanyo katika Mwaka wa Fedha 2022/23  kwa  kusema kuwa ni pamoja na kuongeza mapato yatokanayo na madini ya ujenzi na viwandani kwa kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli katika madini hayo;  kuimarisha ufuatiliaji, usimamizi na ukaguzi wa shughuli za Sekta ya Madini;  kudhibiti kikamilifu biashara haramu ya madini inayohusisha utoroshaji wa madini;  kuimarisha na kusimamia biashara ya madini ikihusisha masoko na vituo vya madini  yaliyoanzishwa na yatakayoanzishwa ili kuongeza ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi kununua na kuuza madini katika masoko hayo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan Kitandula ameishauri wizara kuweka mfumo wenye mwelekeo mpya wa madini ya kimkakati unaoendana na mahitaji ya sasa ya dunia ili hatimaye ziweze kulinufaisha taifa ipasavyo.

 “Tusipojipanga tutajikuta tumebaki na rasilimali zisizokuwa na manufaa kwetu. Mathalan kwa hivi sasa dunia imeanza kuhama katika matumizi ya makaa ya mawe, kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki sisi tumejipangaje kuhakikisha tunaitumia rasilimali hii haraka? Vipi kwa madini yanayohitajika hivi sasa ikiwemo ya viwandani?,” amehoji Kitandula.

 Aidha, Kitandula ameishauri wizara kuangalia ikiwa Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inayotumika hivi sasa inaakisi mwelekeo wa sasa wa mahitaji ya rasilimali madini zinazohitajika zaidi duniani kwa wakati huu na hivyo kuitaka wizara kuiwezesha kikamilifu taasisi yake ya Jilolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili iendelee kufanya tafiti za kina ikiwemo kutafiti maeneo mapya ili kuibua zaidi madini ya kimkakati  yanayohitajika kwa sasa duniani.

Awali, wakichangia  taarifa ya wizara na taasisi, wajumbe wa kamati  hiyo wameitaka wizara kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuharakisha utekelezaji wa mradi wa makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia kutokana na umuhimu wake katika kukabiliana na athari za ukataji  miti  ikiwemo urahisi wa makaa hayo katika matumizi ya majumbani.

Kwa mujibu wa taarifa ya  STAMICO, shirika hilo hivi sasa linasubiri matokeo ya sampuli zilizowasilishwa kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya uthibitisho wa viwango kabla ya kusambazwa kwa walaji.

Vilevile, wajumbe  wa kamati wameendelea kuipongeza wizara  na taasisi zake kutokana na namna inavyosimamia sekta hiyo ikiwemo kasi ya ukuaji wa sekta, maendeleo yake pamoja na namna inavyochangia katika ukuaji wa uchumi, Hata hivyo, wajumbe wameshauri kuhusu kuhakikisha kwamba mchango wa sekta hiyo unawagusa  moja kwa moja wananchi hususan wanaozungukwa na shughuli za miradi ya madini ikiwemo kuhakikisha wizara inaendeleza usimamizi na utekelezaji wa madini mengine ambayo yana tija kwa taifa ikiwemo madini ya ujenzi na chumvi.

Wizara ya Madini inatarajia kukutana tena na kamati hiyo tarehe 29 Machi, 2022.


 


FAMILIA YA MWL NYERERE YAIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

$
0
0






Wizara ya Maliasili na Utalii nchini imepongezwa kwa maamuzi ya kuandaa maadhimisho makubwa ya miaka miamoja tangu kuzaliwa kwa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jambo ambalo litazidi kuamsha Ari na hamasa kwa jamii ya kuendeleza urithi wa Baba wa Taifa.

Hayo yamesemwa na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere katika kikao maalum cha maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Aprili 13, 2022 wilayani Butiama Mkoani Mara.

Madaraka Nyerere aliongeza kuwa, kwao ni faraja kubwa kuona namna Wizara hiyo imeweka mpango wa miaka 10 ya kuhakikisha inamuenzi Mwl. Nyerere kwani katika kipindi hicho jamii itajengewa uelewa mpana kuhusu maisha ya Baba wa Taifa na kizazi kilichopo kuendeleza utamaduni huo.

Akiendesha kikao cha kujadili utekelezaji wa majukumu ya kamati ndogo ya maandalizi ya adhimisho la Miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasi na Utalii, Juma Mkomi licha ya kuzipongeza kamati hizo kwa kazi nzuri pia amezitaka ziongeze kasi ya kufanikisha maadhimisho hayo.

”Japokuwa mnaendelea kufanya vizuri kwenye maandalizi ni watake muongeze kasi ya maandalizi kwa ubora mkubwa maana Hayati Baba wa Taifa ni Tunu ya Taifa letu pia kimataifa, hivyo ni lazima tumuenzi kwa kishindo kikuu na ninawataka wanakamati wote kushiriki matukio ya maadhimisho yanayoendelea sasa”. Amesisitiza.

Mratibu Mkuu wa Maadhimisho hayo Dkt. Kristowaja Ntandu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kamati zote, amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri akitaja baadhi ya shughuli zinazoendelea kufanyika kuelekea maadhimisho hayo ambazo Makongamano, mijadala ya mada mbalimbali na matamasha.

Naye Mkazi wa Mkoa wa Dodoma Mzee Antony Mavunde ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere mkoani humo licha ya kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua adhimu ya kumuenzi Mwl. Nyerere, ametaja hatua hiyo ni zaidi ya sadaka maana maadhimisho hayo yatapanda mbegu kwa jamii hasa vijana juu ya uwelewa kuhusu urithi wa Hayati Baba wa Taifa.

Adhimisho hilo ni sehemu ya Mpango wa miaka 10 wa Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Utamaduni unaotokana na Maisha ya Mwalimu Julius Nyarere ambao kwa nyakati mbalimbali litakuwa likiadhimishwa kila mwaka Aprili 13 na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mwl Nyerere yanayotarajiwa kufanyika Aprili 13,2022 Butiama mkoani Mara.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,  Juma Mkomi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

AGIZO LA MAKAMU WA RAIS DKT.MPAGO LAANZA KUTEKELEZWA KIGOMA

$
0
0


 

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akiongea na wajumbe wa timu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamija na Wizara ya Maliasili na Utalii ambao wamefika mkoani humo kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyato Januari 29, 2022 kuboresha Kituo cha Makumbusho ya Dkt. Livingstone kilichopo Ujiji mkoani humo.



Baadhi ya wajumbe wa timu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamija na Wizara ya Maliasili na Utalii ambao wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye walipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kujitambilisha ikiwa ni hatua ya kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyato Januari 29, 2022 kuboresha Kituo cha Makumbusho ya Dkt. Livingstone kilichopo Ujiji mkoani humo.

……………………………………………….

Na Eleuteri Mangi, WUSM-Kigoma

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii wapo mkoani Kigoma kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyato Januari 29, 2022 kuboresha Kituo cha Makumbusho ya Dkt. Livingstone kilichopo Ujiji na kubainisha maeneo mengine ya utalii mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa timu hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni nchini Dkt. Resani Mnata amesema lengo la ziara yao ni utekelezaji wa maagizo ya Mkamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyoyatoa wakati wa ziara yake katika kituo cha Dkt. Livingstone mapema mwaka huu.

Dkt. Mnata amesema kuwa matarajio ya Serikali ni kuhakikisha kituo hicho kinakuwa chachu ya kutunza mila na desturi za wakazi wa mkoa wa Kigoma ikiwemo kujenga nyumba halisi za wakazi wa mkoa huo, kuwa kituo cha kutoa elimu kwa vijana, kuwa kituo cha kufanya tafiti pamoja na kuwa na kituo cha watoto kuwa na michezo mbalimbali.

Akiongea na wajumbe wa Kamati hiyo ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema mkoa huo unavivutio lukuki vya utalii wa kiutamaduni, wanyama katika hifadhi ya Taifa ya Gombe, Mahale, fukwe katika mwambao wa ziwa Tanganyika na vivutio vingi katika maendeo mbalimbali katika mkoa huo.

“Ujio wenu hatuwezi kuutafsiri kwenye utamaduni tu, tunautafsiri kwenye uchumi, tunataka vitu vifanyike vyenye thamani kwenye maisha. Mtu anakuwa na utamaduni wake, tuutunze ili tuendelee kuwa na heshima” amesema Mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma.

Mkuu mkoa Andengenye amesema kuwa ujio wa kamati hiyo imekuja muda mwafaka wa kutunza kumbukumbu na simulizi za historia walizonazo watu ambao ni maktaba hai ziweze kutunzwe kwa njia ya kisasa kutoka maeneo ya kihistoria ama kimila za wakazi wa mkoa huo ili ziweze kutumika kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Aidha, amesisitiza kuwa mkoa huo una hifadhi ya Taifa ya Gombe ambayo inafungua mkoa huo ndani na nje ya nchi ambapo amesema kuwa wanampango wa kufuingua iweze kufikika kwa njia ya barabara kutoka Mwandiga kupitia Chakere hadi kijiji cha Mwamgongo ili hifadhi hiyo iwe chanzo cha uhakika cha uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Hatua hiyo itawawezesha watu wengi wataweza kufika kwenye hifadhi hiyo kwa njia ya barabara ambao hawawezi kufika katika hifadhi hiyo kwa njia ya maji ama kwa njia ya anga.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI – WAZIRI UMMY MWALIMU

$
0
0


Na Englibert Kayombo WAF- Dodoma

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha zinapatikana hapa nchini na zinakuwa za uhakika na karibu zaidi na maeneo ya wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Afya na Taasisi zake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

“Lengo letu sio tuu kupunguza gharama za Serikali kulipia Watanzania kwenda nje ya nchi kupata huduma za matibabu, bali pia tunataka huduma hizo zipatikane hapa hapa nchini karibu zaidi na maeneo wanayoishi lakini pia wawe karibu na familia zao waweze kuhudumiwa vizuri” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa Huduma Bora za Afya kwa wananchi kwa kusogeza Huduma za Ubingwa na Ubingwa bobezi karibu na wananchi wanapoishi kwa kujenga, kupanua na kukarabati Hospitali za Rufaa kuanzia ngazi ya Mikoa hadi Taifa.

Kuhusu hali ya utoaji wa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi, Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022, Wizara kupitia hospitali za kitaifa, kanda na hospitali maalum imehudumia jumla ya wagonjwa 3,341,393 kati ya hao wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 3,035,427 na wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 293,680.

Waziri Ummy amesema kuwa Wizara ya Afya inaratibu jumla ya miradi 39 ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Hospitali 8, ukarabati na upanuzi wa Hospitali 31, ambapo utekelezaji wa miradi hiyo umeendelea katika Hospitali za Rufaa za Kanda 4, hospitali maalum moja (1) na Hospitali za rufaa za Mikoa 26.

Waziri Ummy amesema kuwa Wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za tiba nchini ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari, 2022 jumla ya Wagonjwa 21,230,469 walipatiwa huduma, ambapo Wagonjwa 20,428,932 ni wa nje na Wagonjwa 801,537 walilazwa na hivyo kupungua kwa idadi ya Wagonjwa ikilinganishwa na jumla ya Wagonjwa 21,586,217 walipatiwa huduma katika kipindi kama hicho cha Julai 2020 hadi Februari 2021.

Kuhusu upatikanaji wa dawa, Waziri Ummy amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22, kiasi cha shilingi bilioni 200 kilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi. Hadi kufikia mwezi Februari 2022, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 119.8 sawa na asilimia 59.9 ya fedha yote iliyotengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo ili Watanzania waweze kupata huduma bora za matibabu hapa hapa nchini.

“Watanzania wanahitaji kutibiwa, na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka fedha nyingi kwenye upande wa elimu na afya na tumeona hapa tunajenga vituo vya kutolea huduma za afyat tunataka huduma zipelekwe kwa wananchi na pamoja na upatikanaji wa dawa kwa uhakika” amesema Mhe. Nyongo.

Aidha Mheshimiwa Nyongo ameishauri Serikali kulitazama kwa mapana zaidi suala la Bima ya Afya kwa wote na kusema kuwa ndio suluhisho la uhakika wa matibabu kwa Watanzania pamoja na ustahimilivu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

“Leo tunajenga majengo na huduma zinatolewa na dawa kupelekwa lakini Watanzania wengi bado hawana uwezo wa kulipia gharama za Bima, ipo haja ya sisi Kamati kukaa na Serikali kuishauri vyema zaidi juu ya mustakabari wa Bima ya Afya kwa wote” ameseme Mhe. Nyongo


BAADA YA KUWA NAMBA MOJA KATIKA UUZAJI MAFUTA PUMA ENERGY TANZANIA SASA KUANZA KUUZA GESI ZA MAJUMBANI

$
0
0

KAMPUNI namba moja katika uuzaji wa mafuta nchini Tanzania ya Puma Energy imetoa tuzo kwa Mawakala wake wa kuuza mafuta huku ikitumia nafasi hiyo kutoa muelekeo wake katika kujiimarisha zaidi kibiashara.

Akizungumza wakati wa utoaji huo wa tuzo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dk.Seleman Majige amesema baada ya kufanikiwa katika uuzaji mafuta sasa wanataka kuanzia Mei mwaka huu kuuza gesi za majumbani.Gesi hiyo itauzwa kwenye vituo vya mafuta vya Kampuni hiyo kote nchini.

Dkt.Majige amesema kuwa kwakuwa kampuni ya Mafuta ya Puma Energy ndio namba moja na yenye huduma bora hapa nchini hivyo hata kwenye uuzaji na usambazaji wa nishati hiyo ya gesi watakuwa namba moja kama ilivyo kawaida yao.

"Nitumie nafasi hii kuwapongeza Mawakala wote waliopata tuzo hizi na kwakweli tunajivunia kwa huduma bora ambazo mnazifanya na niwaombe mkaendelee kuitangaza, na kuilinda Puma Energy limited ili iendelee kuwa kampuni namba moja kwa ubora.

"Na hivi karibuni tunakwenda kuaza kufanya huduma ya biashara ya usambazaji gesi ya majumbani ,tayari bodi imeshakaa na kupitisha hilo,hivyo matarajio yangu nikuona tunaendelea kuwa namba moja kwa ubora wa huduma zetu hivyo nawapongeza nyote kwa kazi nzuri mnayofanya. "amesisitiza Dk.Majige.

Kuhusu Kampuni hiyo amesema kuwa wameendelea kuwa namba moja kwani kila kituo cha Puma ambacho utakwenda utakuta huduma hiyo ya mafuta na hivi sasa wameongeza vituo kutoka 52 vya awali na kufikia vituo 80 lakini lengo ni kuona hadi kufikia mwaka 2025 wanakuwa na vituo 150 na sio 100.Hivyo ametoa rai kwa Menejimenti ya Kampuni hii ya Puma hadi kufikia mwaka 2025 wawe wameongeza vituo hadi kufikia 150 na sio 100 kama walivyokuwa wamepanga.

Dk.Majige amewakumbusha wadau hao kuwa Puma ni kampuni kubwa hivyo waendelee kuilinda na kuhakikisha mafuta yanakuwa salama huku akiiitaka menejimenti kuweka mkakati wa kuaziasha vituo vijijini ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi.

Amesisitiza umuhimu wa lugha na matendo mazuri ya mawakala wakati wanawahudumia wateja wa Kampuni hiyo kwani hiyo ndio silaha ya Puma Energy Tanzania kuendelea kuwa namba moja.

Kwa upande wake Miurugenzi Mtendaji wa Puma Tanzania Dominic Dhanah amesema Kampuni hiyo ndio inayoongoza nchini na inashika namba moja kwa ubora.

Amesema kuwa namba moja ni kazi kubwa sana lakini wataendelea kuwekeza nakwamba hadi kufikia sasa Puma inavituo 80 kutoka vituo 52 vilivyokuwepo hapo mwanzo na lengo nikufikisha vituo 100 kufikia mwaka 2025.

"Ndugu Mgeni rasmi kampuni imeendelea kuwa wabunifu na tumeongeza huduma nyingine ya vilainishi vya kwenye magari na mapema mwaka huu tunatarajia kuzindua nishati ya gesi ya majumbani ambayo itakuwa inapatikana kwenye vituo vyetu vyote na hakuna shaka kwamba itapokelewa vizuri. "Amesema Dhanah

Aidha amewapongeza watoa huduma wote wa Puma kwani wao ndio wamekuwa chachu ya mafanikio ya kampuni hiyo huku akiwataka waendelee kufanya vizuri zaidi na katika tuzo hizo kituo cha mafuta kutoka Arusha Cetral Station kimefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa uuzaji wa mafuta kwa mwaka wa pili mfululizo.


Ilikuwa ni shangwe furaha nderemo na vifijo kwa waliojishindia zawadi mbalimbali siku hiyo




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akimkabidhi zawadi mshindi wa mawakala wa jumla wa vituo vya mafuta waliofanya vizuri katika vituo vya kampuni hiyo iliyofanyika hibi karibuni lJijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Bw. Dominic Dhanah akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Bw. Dominic Dhanah kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika hivi Karibuni Jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akimkabidhi zawadi mawakala mbalimbali waliofanya vizuri kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya Puma Energy Tanzania katika hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya kampuni hiyo nchini iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.







Viewing all 120322 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>