Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120247 articles
Browse latest View live

MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI KWA MABASI KUANZA KUTUMIKA JULAI MOSI MWAKA HUU.

$
0
0


Serikali imesema kuwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu Wamiliki wote wa mabasi watatakiwa kukatisha tiketi kwa njia ya kielekriniki kwa mabasi yaendayo mkoani ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya kuboresha utoaji huduma hizo kwa wananchi.

Akizungumza jijini Dodoma Katibu Mkuu- Uchukuzi Gabriel Migire amesema nia ya kuanza utaratibu huo ni pamoja na kuthibiti Mapato yanayopatikana kwa njia ya tiketi na kuwarahisishia wamiliki kwa kujua idadi ya tiketi zilizouzwa kwa siku.

“changamoto zote Zilizowasilishwa awali na wadau zimerekebishwa kupitia Mamlaka Udhibiit Usafiri Ardhini LATRA hivyo kukamilika kwa marekebisho haya Kutafanya zoezi hilo kuanza mwezi Julai” Alisema migire. 


Katibu Mkuu Migire amesema kwa sasa LATRA itaanza na majaribio kwa miezi mitatu ili kujiweka sawa na endapo itabainika kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo zitakamilishwa ili Julai uanze rasmi.

Karibu Mkuu Migire Ameelezea Faida za mfumo kwa abiria ikiwemo Kutolazimika kwenda stendi ili kukata tiketi hivyo kumpunguzia adha ya kutafuta wakala kwani tiketi yake ataipata kupitia simu yake ya kiganjani.

Aidha, Ameongeza kuwa kwa abiria wa sio kuwa na simu janja watapata tiketi hizo kupitia mawakala wa mabenki ili kuwapunguzia kadhaa ya kutafuta mawakala walio katika stendi za mabasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Latra Giliard Ngewe amesema mamlaka itaanza kutoa elimu kuanzia April mosi ili kuwapa abiria uelewa wa namna ya kukata tiketi hizo kwa kuzingatia Makundi yote ya jamii.

Ngewe ameongeza kuwa elimu hiyo imeshirikisha taasisi zote muhimu ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) ili kufikia watumiaji kwa haraka.


WAZIRI MCHENGERWA ATEUA KAMATI YA HAMASA KWA MICHEZO JUMUIYA YA MADOLA NA KOMBE LA DUNIA KWA WATU WENYE ULEMAVU.

PAC: TUMEONA THAMANI YA FEDHA KWENYE MIRADI YA MAJI DAWASA

$
0
0

Na Fredy Mshiu

Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya majisafi katika Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati katika mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo uliogharimu kiasi Cha sh. Bilioni 65 na kuonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa wake.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za Serikali Mh. Japhet Hasunga (Mb) ameeleza lengo la ziara hiyo ililenga kukagua thamani ya fedha zilizotolewa na kutekeleza katika miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA.

"Sisi kama kamati ya Bunge tumefanya ziara hii Ili kuona na kutathmini thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali katika mradi mbalimbali, na kwa niaba ya Kamati nikiri kuwa tumeridhishwa sana na kazi zilizotekelezwa na DAWASA na kila mmoja wetu amejionea na kuridhika na kiasi cha fedha kilichotumika kwenye miradi hii."ameeleza Mh.Hasunga
Aidha Mh.Hasunga ameongeza kuwa pia lengo la ziara ilikuwa kuona namna bodi ya wakurugenzi DAWASA inavyowajibika katika kusimamia miradi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange ameieleza kamati kuwa mojawapo ya siri yakufanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maji ni kutokana na uongozi mzuri uliopo na weledi mkubwa baina ya Menejimenti na watumishi.

"Tumepata mafanikio hasa katika kusimamia miradi mbalimbali ikiwemo huu wa kuanzia Makongo hadi Bagamoyo kutokana na kufuata sheria na taratibu zilizopo zinazoongoza Mamlaka na mashirika ya Umma".ameleeza Jenerali mstaafu Mwamunyange

"Tunafurahi kuona Kamati imeridhika na kazi kubwa tunaiyofanya ya usimamizi wa fedha na utekelezaji wa miradi kwa thamani halisi ya hela, hii inatutia moyo sana na tunawaahidi uwajibikaji zaidi ili kufikia malengo yaliyowekwa" ameongeza Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.

Mradi wa maji *Makongo hadi Bagamoyo* unatekelezwa kupitia fedha za wadau wa maendeleo na kusimamiwa na DAWASA kwa gharama ya kiasi cha Tsh Bilioni 64. Mradi utakapokamilika utahudumiwa wakazi zaidi ya 450,000 wa maeneo ya Changanyikeni,Vikawe, Goba, Bunju, Madale, 
Wazo, Ocean Bay, Salasala na sehemu ya mji wa Bagamoyo

Mitel roots for remote working solutions

$
0
0

 


Dar-es-Salaam, Wednesday March 28, 2022--Mitel, a global leader in business communication technology, has rooted for investment in remote working solutions as organisations adopt to new work environment models post Covid-19. Following disruptions caused by the Covid-19 pandemic, the company is investing in demand generation using various tools such as tele- calling, social media and webinars to align more with the latest market trends.

Whereas the pandemic has affected virtually all sectors of the economy, notable changes have taken place in the area of IT spending. According to leading marketing research agencies, in the pre-Covid days, spending was more on areas such as government, finance, manufacturing, utilities and transport. But with Covid-19 having ushered in a new normal, spending has shifted from these traditional verticals to two major ones: healthcare and education. With the global pandemic, IT firms and providers are experiencing heightened demand for a scalable Unified Communication as a Service (UCaaS) portfolio to serve their remote workforce, even as the pandemic eases.

“Covid-19 brought about the need for flexible home working solutions, a situation that has continued even after the pandemic eased, as it is the new normal. The market is ripe for collaborative communication and remote working solutions, smart digital workspaces as well as endpoint security and management solutions”, said Mr Asif Khan, Channel Director, Middle East and Africa (MEA).

These collaborative solutions include mobile apps that can be tied directly into organisations’ workspaces, as today’s technology is geared towards remote working, collaborative efforts and enhancing online presence.

“Healthcare, education, hospitality, contact centre, SME and mid-market, as well as cloud business, will be the key focus areas for Mitel this year. We create our marketing strategy built around those segments to effectively communicate with our end customers and partners”, said Mr Khan.

Mr Khan was speaking during an industry symposium held for channel partners at a Dar-es-Salaam hotel. According to him, Tanzania is a SME dominated market and the strength of the market lies in government, banking and hospitality sectors. It is also a price sensitive market but by looking at the dynamics, feeling the gap is in SME & mobility sector and organizations in Tanzania are looking for flexible & subscription based solutions.

“The Mitel Symposium was very helpful to us. Tanzania is not new to us, but we weren’t active much with regards to holding a physical event due to COVID since last 2 years. This event helped us in building immense confidence in the channel community, with great turnout from all industries, we had channel partners who are specialised in hospitality, focused on contact centers, and government sectors. Overall it was a good feedback in the open platform and had our local distributor with us for the event Networks Distribution. Overall it’s a good start”, said Mr Khan.

He said Mitel would continue enabling more channel partners with more events, trainings, workshops, webinars and marketing support.

Currently, Unified Communication (UC) service providers are experiencing demand for a scalable UCaaS portfolio, which comes at a low cost with a strong presence in instant messaging, mobility and conferencing services. Original Equipment Manufacturers (OEMs) in the region will also focus on the mid-market and small-to-medium business segment to expand and reduce the dependency on large enterprises.

The main driving force behind UCaaS is mobility. Employees today are no longer restricted to traditional office spaces and prefer to work from home and on the go. As such, UCaaS assumes a new importance in the organization to stay connected with employees, as the landscape of the traditional office environment changes dramatically.

When people started working remotely, Mitel had to create remote solutions to suit the growing demand for working from home. The growth in demand for UCaas will be driven increasingly by the implementation of hosted solutions as enterprises look to reduce costs and improve productivity.

“Cloud UC makes more sense for large organizations, because their markets are spread over different geographies and diverse user communities, and their communications are unlikely to change for the foreseeable future. With growing concerns on recession and a volatile world economy, the focus of big firms today has been on cost cutting and reducing expenses as much as possible”, added Mr Khan.

Mitel offers a range of integrated communications solutions that businesses of all kinds and levels of maturity can utilise to boost efficiencies, deliver exceptional customer experience and engage employees. Mitel retains the Number 1 position in Global Cloud Users, with over 5.2 million cloud users worldwide, Number 1 in 5 core markets, with over 1.5 million UCaaS users globally and Number 3 in contact centre systems shipped globally.

Mitel operates in over 100 countries, with a sales and service organization of over 70 offices, in conjunction with over 3000 value-added resellers and partners around the world. Mitel is now a clear market leader, with combined annual revenue of over US$1.3 billion, 70 million customers worldwide, and top market share in Western Europe.


About Mitel


With 45 years of industry leadership, Mitel helps businesses connect, collaborate and provide better experiences for their customers. Mitel is trusted by 70 million business users in more than 100 countries. Throughout our long history of industry experience, innovation has been core to Mitel’s DNA – allowing us to become experts in evolving to meet your needs and help you do the same for your customers. It’s why we’re the only company that wakes up every day exclusively focused on helping you take your communications from where they are today to where you – and your customers – need and expect them to be.

Mitel is now a clear market leader, with combined annual revenue of over US$1.3 billion, 70 million customers worldwide, and top market share in Western Europe. The combined business provides Mitel with a $100 million annual Research and Development budget used to pursue innovation and the development of a broad range of regional and global solutions.



The following achievements attest to our market leadership:

• 5 times Gartner Magic Quadrant Leader for UC

• More than 1 million UCaaS subscribers

• #1 in private cloud worldwide

• #1 in UC market share for Europe

• #2 in UCaaS market share worldwide

• Over $1.3B in revenue

• Frost & Sullivan 2017 Growth Excellence Leader in UC in North America

• Over 1,800 patents & applications



Benki ya Exim, ZATI Watiliana saini Makubaliano ya Kukuza Utalii Zanzibar

$
0
0

 
BENKI ya Exim Tanzania na Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) wametiliana saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya ushirikiano wa kiutendaji hatua inayolenga kuinua kuboresha utoaji wa kwa sekta ya utalii katika Visiwa hivyo vya kihistoria.

Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo Zanzibar zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha.

Akizungumza wakati hafla fupi ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bw Simai Mohamed pamoja na kuwapongeza wadau hao wawili kwa hatua hiyo alitayataja makubaliano hayo kuwa ni ya aina ya kipekee yakiwa yameainisha viashiria mahususi vya utendaji kwa pande zote mbili ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu bora ya utalii na shughuli kote Visiwani.

Alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na azma ya serikali ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa taasisi za sekta binafsi pamoja mahusiano baina ya serikali na sekta binafsi.

“Ni imani yangu kuwa mahusiano mazuri baina ya wadau wa serikali na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya Exim yatasaidia zaidi wadau mbalimbali wa utalii Zanzibar ambao wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na athari za kiuchumi za COVID-19 ili waweze kujikwamua na hatimaye kurejesha uwezo wao wa kiuchumi. Natoa wito kwa taasisi nyingine za fedha kuiga mfano huu kwa kuwa karibu na wadau wa utalii hasa katika zama hizi ambapo serikali inajikita zaidi katika uchumi wa bluu ‘’ alisema.

Utalii unachangia takribani 25 asilimia ya pato la Taifa Zanzibar (GDP) na hadi asilimia 80 ya mapato ya fedha za kigeni visiwani humo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu alisisitiza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuendelea kukuza sekta ya Utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

"Sekta hii muhimu ya utalii ni moja ya sehemu ambayo tunaitazama zaidi hususani katika visiwa hivi vya Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini hivyo na niahidi kwamba tutaendelea kujidhatiti zaidi hilo. Utalii ni nguzo muhimu ya uchumi wa Zanzibar na sisi tutaendelea kuzingatia hilo kwa kuwekeza zaidi muda wetu, juhudi , rasilimali watu na mtaji zaidi katika kuhudumia sekta hii na msimamo wetu huo hautabadilika’’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya miaka mitatu, benki hiyo itahusika katika kuhakikisha wadau wa utalii wanapata mikopo ya biashara kubwa na ndogo inayoandaliwa kulingana na mtiririko wa fedha za mwanachama husika.

“Pia tutaendelea kutoa huduma bora zaidi za kubadilishia fedha kwa kuzingatia viwango vyenye ushindani zaidi kwa sarafu zote ikiwemo Shilingi ya Kitanzania pamoja na Dola ya Kimarekani.

Ni kutokana na mkakati wetu huu ndio maana hata kwenye matawi yetu tunahakikisha kwamba wadau wa utalii hususani wanachana wa ZATI wanakuwa na upendeleo maalum katika kupata huduma, ikiwemo kupatiwa Meneja Mahusiano maalum kwa ajili yao tu.

Pia tunahakikisha wanapata huduma nyingine nyingi ikiwemo huduma za Bima, uwepo wa makubaliano maalum katika viwango vya ushuru (tarrifs) pamoja na kuwapatia Mashine za malipo (POS) ili kuwarahisishia watalii kufanya malipo na kutokuwa na wasiwasi wa kubeba au kutembea na pesa.’’ Alisema Matundu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ZATI, Rahim Bhaloo, aliipongeza Benki ya Exim kwa ushirikiano huo, na kusema hatua hiyo itaiwezesha sekta ya kimkakati ya utalii Zanzibar kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake, kuinua ubora wa huduma na kuongeza zaidi mvuto wa Visiwa hivyo kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

“Ni muhimu kueleza kuwa hatua hii ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na wenye tija kati ya ZATI na wadau wake wakiwemo wanachama wake, taasisi za fedha kama Benki ya Exim na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ushirikiano huu huu utatuwezesha kusaidia ipasavyo biashara yetu ya utalii, kutengeneza ajira, na kuboresha ustawi wa wawekezaji wadogo na wakubwa katika sekta ya utalii.’’ Alisema.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) Bw. Rahim Bhaloo (kulia) wakitia saini hati za Makubaliano ya kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha. Wanaotazama ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed (katikati), Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban (wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk (wa tatu kulia) na wawakilishi wengine kutoka sehemu zote mbili.




Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo Zanzibar zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha.




Akizungumza wakati hafla hiyo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bw Simai Mohamed (Pichani) pamoja na kuwapongeza wadau hao wawili kwa hatua hiyo alitayataja makubaliano hayo kuwa ni ya aina ya kipekee yakiwa yameainisha viashiria mahususi vya utendaji kwa pande zote mbili ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu bora ya utalii na shughuli kote Visiwani.


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban akizungumza kwenye hafla hiyo.




Akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (Pichani) alisisitiza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuendelea kukuza sekta ya Utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.



Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa ZATI, Rahim Bhaloo (Pichani) aliipongeza Benki ya Exim kwa ushirikiano huo, na kusema hatua hiyo itaiwezesha sekta ya kimkakati ya utalii Zanzibar kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake, kuinua ubora wa huduma na kuongeza zaidi mvuto wa Visiwa hivyo kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.



Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed (Katikati walioketi), Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban ( wa tano kulia walioketi) na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk (wa pili kulia walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na maofisa wa Benki ya Exim pamoja na Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya Makubaliano ya kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.

WAZIRI JAFO AWAPONGEZA WADAU KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo akizindua jiko banifu ambalo litakalobaidhiwa kwa Shule ya Sekondari Kimani wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambalo litasaidia kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni ambapo amewapongeza wadau wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha mazingira yanalindwa.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo akifurahia mandhari ya Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati wa Kongamano la Wasaa wa Mazingira lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kwa ushirikiano na Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo akiwa ameshika mche wa mti kwa ajili ya kuupanda katika Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati wa Kongamano la Wasaa wa Mazingira lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kwa ushirikiano na Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania.

…………………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo amewapongeza wadau wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha mazingira yanalindwa.

Ametoa pongezi hizo wakati aliposhiriki katika Kongamano la ‘Wasaa wa Mazingira’ lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kwa ushirikiano na Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania na kufanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Akizindua jiko banifu Dkt. Jafo alisema Serikali inatambua mchango wa taasisi zisizo za kiserikali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinashiriki kikamilifu katika suala zima la utunzaji wa mazingira.

Akizungumzia jiko hilo Mratibu wa Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia (TATEDO) Bw. Shima Sago alisema litasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha ukataji wa miti kwa ajili ya kuni.

Alisema waligungua kuwa katika Shule ya Sekondari Kimani wilayani humo ambayo ilitarajiwa kukabidhiwa jiko banifu hilo, walitumia takribani kuni 3,200 kwa wiki hivyo kwa sasa watapunguza na kutumia kuni 400 kwa wiki mbili.

Pia Sago alisema jiko hilo linatunza afya ya mtumiaji kwa kuepuka moshi unaoweza kutoka wakati wa kupika na badala yake utapita kwenye bomba maalumu nje ya mahali pa kupikia.

Hata hivyo akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira mara baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la msitu, Waziri Jafo aliitaka jamii kuutunza msitu huo sambamba na kupanda miti kwani unasaidia kunyonya hewa ya ukaa.

Kwa upande wake Balozi wa Mazingira, Bi. Yvonne Cherry ‘Monalisa’ alisema Kampeni ya ‘Soma na Mti’ hiyo haiwahusu tu wanafunzi na wanachuo bali kila mtu anatakiwa ashiriki.

Monalisa ambaye pia anasimamia kampeni hiyo alitoa rai kwa wazazi na walimu kwenye shule na vyuo mbalimbali nchini kuwasimamia wanafunzi katika kushiriki upandaji miti.

Aliongeza kuwa upandaji miti uende sambamba na utunzaji ili kuhakikisha inakua nma hivyo kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa ya kijani hatua itakayosaidia kuhifadhi mazingira.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR HAITAMVUMILIA YOYOTE ATAKAEJIHUSISHA NA MATENDO YA UDHALILISHAJI - RAIS MWINYI

$
0
0


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitamvumilia yoyote atakaejihusisha na matendo ya udhalilishaji kwa lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa kauli hiyo katika Hotuba iliyosomwa kwa Niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akizindua Kongamano la Nane la kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Amesema Serikali imejipanga na inaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wanaojihusisha na matendo hayo ambayo yanaiathiri jamii hasa kwa vizazi vijavyo.

Alhajj Dkt Mwinyi amesema imefika hatua kwa wananchi kuacha muhali na kutowaonea huruma wafanyaji wa vitendo hivyo ili kuisaidia Serikali katika kusimamia kesi za matukio hayo ya udhalilishaji.

Aidha Rais Dkt Mwinyi ameiasa jamii iendelee kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuwafichua wahusika wa matendo hayo kwa pamoja na kutoa ushahidi unapohitajika ili sheria iweze kufata mkondo wake.

Pamoja na hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewataka waumini hao kuiga kigezo chema na Mtume Muhammad (S.A.W) ambae alikuwa akikemea kwa maneno na vitendo juu ya udhalilishaji wa wanawake na watoto.

"Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akikerwa na matendo yote ya kuwadhalilisha wanawake na watoto na kufikia kuwakaripia wale wote wenye tabia na mienendo hiyo" Alisema Dkt Mwinyi

Sambamba na hayo Rais Dkt Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwaasa waumini kujiandaa kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kuzidisha Ibada na kuacha yote yaliyokatazwa na Sheria yetu.

" Naomba tukumbushane kwamba Mwezi Mtukufu wa Ramadhan upo mlangoni na ni wajibu wetu kujiandaa kuupokea namna bora kabisa ya kuupokea ugeni huu ni kuzidisha Ucha Mungu kwa kufanya Amali njema na kuacha yale yote tuliyokatazwa" Dkt Mwinyi.

Pia Rais Dkt Mwinyi amewaasa wafanyabiashara kujitahidi kuwaonea huruma waumini katika Mwezi wa Ramadhan kwa kuweka tahfifu bei ya bidhaa na kukemea tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara kupandisha bei kiholela ili kuepuka chumo la haramu.

Kwa upande wake Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kujikita katika Ibada kufikia Daraja la Uchamungu ambali ndio lengo la kuweko kwa funga ya Ramadhani.

Amesema Uislamu umeeleza kuwa ni hasara kubwa kwa Muumini ambae amediriki Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutosamehewa madhambi yake.

Nae katibu Mkuu wa Taasisi ya Zanzibar Relief and Development Foundation (ZARDEFO) Ali Muhammad Haji ameeleza kuwa lengo la kuandaa Kongamano hilo ni kuwaweka tayari waumini kuweza kuukabili Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwakumbusha waumini kuweza kujikita katika Ibada katika Mfungo mzima wa Mwezi wa Ramadhan.

Akiwasilisha Mada katika Kongamano hilo Alhabyb Muhammad Bin Hussein Alhabshy kutoka Seuni Hadhramut Nchini Yemen ameeleza kuwa ili kumaliza tatizo la Udhalilishaji ni vyema waislamu kurudi katika Sheria ya Allah Mtukufu.

Mada kuu katika kongamano hilo ni athari za udhalilishaji katika uislamu.

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini wa kiislamu katika uzinduzi wa kongamano la nane la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan lililoandaliwa na  Taasisi ya Zanzibar Relief and Development Foundation (ZARDEFO) katika ukumbi wa idris abdulwakil kikwajuni.

katibu Mkuu wa Taasisi ya Zanzibar Relief and Development Foundation (ZARDEFO) Ali Muhammad Haji akizungumza katika uzinduzi wa kongamano la nane la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan lililoandaliwa na  Taasisi ya hio.

waumini wa DINI ya kiislamu wakifatilia mada katika kongamano la nane la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan lililoandaliwa na  Taasisi ya Zanzibar Relief and Development Foundation (ZARDEFO) katika ukumbi wa idris abdulwakil kikwajuni

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO MACHI 28,2022


NI WAJIBU WA WATANZANIA KUWEKA MKAZO KATIKA KUHAMASISHA UWEPO WA BENKI ZA MBEGU ZA JAMII NDANI YA NCHI

$
0
0



Na Said Mwishehe, Michuzi TV

NCHINI  Tanzania chini sekta ya kilimo ni  muhimili wa maendeleo ya uchumi na ukweli ni kwamba sekta hiyo inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa huku robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya asilimia 75  ya Watanzania.

Kwa kukumbusha tu sekta hiyo ya Kilimo ina uhusiano mkubwa na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa.

Kubwa zaidi  Tanzania inazalisha takribani asilimia 97 ya  mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.

Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya Serikali/fedha za umma kwa kipindi kirefu. Hata hivyo marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo.

Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji , uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo. Serikali imebaki na kazi ya usimamizi na usaidizi wa umma na dhima ya uwezeshaji.

Umuhimu wa sekta ya Kilimo katika nchi yetu pamoja na mambo mengine ndio sekta iliyopewa nafasi kubwa na Watanzania ,asilimia kubwa ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo.Wapo wanaolima Kilimo kwa ajili ya mazao ya biashara na wapo wanaolima kwa ajili ya chakula.

Tunafahamu Kilimo hakimtupi mkulima,hivyo kila Kona ya nchi yetu kilimo kimepewa nafasi kubwa.Wakulima wanakifurahia Kilimo bila kujali changamoto wanazokumbana nazo, changamoto kwao wakati mwingine wanaigeuza kuwa fursa .Ni jambo la kawaida kumuona mkulima anatumia jembe la mkono na bado akafurahia kilimo.

Ni jambo la kawaida kwa mkulima kulima kilimo cha kisasa na mambo yakaenda vizuri.Kubwa kuliko yote  Tanzania imejaaliwaa kuwa na aridhi yenye rotuba,kuna maji ya kutosha yanayoweza kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Kwa kutambua kuwa kilimo kimeajiri maelfu ya Watanzania, Serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha Kilimo kinaendelea kukuwa na kuwa na tija kwa wakulima na Watanzania kwa ujumla.Bajeti ya Serikali kwenye sekta ya Kilimo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Kama ambavyo tunafahamu kuhusu Kilimo na umuhimu wake Ilani ya CCM ya mwaka 2020 inaeleza kwa kina mipango na mikakati ya kuendeleza kilimo na kupitia Ilani hiyo inafafanua kuwa hata katika kukabiliana na umasikini kilimo ndio njia sahihi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini hasa umasikini wa kipato .Hivyo tunapozungumza Kilimo lazima tuelewe Kilimo kimebeba hatma ya Watanzania walio wengi.

Nikiri sekta ya Kilimo imegawanyika katika maeneo mengi tu,katika Makala haya nataka kuzungumzia umuhimu wa kuhifadhi Mbegu bora za asili, mbegu ambazo zinahimili hali ya hewa ya nchi yetu ya Tanzania, Mbegu za asili ambazo zinahimili mazingira yaliyoko.Kwa kifupi nataka kuzungumzia umuhimu wa kuwa na benki za  Mbegu za jamii.

Tunafahamu kwa sasa kukua kwa teknolojia, tumeshuhudia Mataifa mbalimbali duniani yakijikita katika kuzalisha mbegu na kuzisambaza katika Mataifa mengine.Lakini kwa upande wangu naamini Tanzania bado tunao uwezo wa kuhifadhi mbegu zetu za asili kwenye benki za mbegu za jamii.Ninaposema benki sina maana ya zile benki za kutunza fedha bali nazungumza maeneo maalum yanayotumika kuhifadhi na kutunza mbegu.

Hivyo tunakuwa na benki za mbegu ambazo zitasaidia kupunguza ile changamoto ya wakulima kuhaha kutafuta Mbegu  inapofika msimu wa kilimo.Benki hizi zinaweza kuanzishwa na mtu mmoja,kikundi au taasisi.Ukweli uliopo benki za mbegu zinapatikana katika maeneo mengi duniani na zimekuwepo kwa miaka mingi zikiwa na lengo la kuhifadhi,kurejesha ,kuimarisha na kuboresha mifumo ya mbegu ya ndani.

Nieleze kitu kidogo kuhusu benki ya mbegu, kwa hapa nchini kwetu Tanzania mwamko wa wanajamii katika kuanzisha na kusimamia benki za mbegu ni mdogo.Benki hizo zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache ya Dodoma na Mbeya.Benki hizo zinafahamika kwa majina mengi,wapo wanaoziita benki za Jeni za Jamii, nyumba za mbegu za mbegu za wakulima,vibanda vya Mbegu,hifadhi ya Mbegu za Jamii,maktaba ya Mbegu na wengine huziita benki za mbegu za jamii.

Kwa wakulima ambao wanazo benki za mbegu za jamii huhifadhi Mbegu za mazao ya aina mbalimbali zikiwemo zile zinazolimwa kwa wingi,mfano mahindi,mpunga aina nyingine za mbegu.Pia wanahifadhi mbegu za mazao yanayolimwa kwa uchache kama vile Mtama na mazao ambayo walaji wameyatelekeza  kama viazi vikuu.Mbegu hizo zinaweza kuhifadhiwa kwa kiasi kidogo au kikubwa kulingana na hitajio na upatikanaji wake.

Kwa kufafanua zaidi zipo hatua na mchakato wa kuanzisha na kusaidia benki za mbegu za jamii.Aidha kuanzisha na kuunga mkono benki ya mbegu ya jamii inahusisha htua kadhaa, hivyo ni muhimu kupitia mchakato huo bila kukimbilia na kuruhusu muda wa kutosha wa kuingiliana na wakulima.Kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kusimamia benki ya mbegu.

Miundombinu kwa ajili ya kuhifadhi Mbegu ije badae baada ya jamiii kuwa na uelewa wa kutosha na kuwa tayari kuanzisha na kusimamia benki husika.Pia kuwa na jengo nzuri peke yake kwa ajili ya benki ya mbegu haifai ikiwa wakulima hawana motisha na ujuzi wa kulitumia.

Ni vema tukafahamu kuwa kuna hatua kuu tisa katika kuanzisha na kuunga mkono benki ya mbegu.Baadhi ya hatua hizo ,ya kwanza ni uchambuzi wa hali halisi ya Mbegu, hatua hiyo inahusisha shughuli tatu; uchambuzi wa aina mbalimbali za mazao yanayolimwa na mwenendo wake, uchambuzi wa mifumo ya mbegu na uteuzi wa jamii na sehemu la kuanzisha benki za mbegu.

Aidha uchambuzi wa aina mbalimbali za mazao yanayolimwa n muelekeo wake , iko hivi  uchambuzi huo ni muhimu kwa kuwa unasaidia jamii kuelewa aina za mazao yaliyoko mashambani na pia kujua kama mazao hayo yako eneo moja tu au yamenea kwenye jamii nzima .

Pia hujulisha mazao yale yanayolimwa kwa wingi na yale ambayo yanakaribia kutoweka au ambayo yameshatoweka .Zoezi hili linaweza kukamilishwa kwa kuwa na maonesho ya mbegu ili kusaidia kujua mahali zilipo Mbegu ambazo ni adimu na kukamilisha orodha ya mbegu zilizopo na taarifa zake ambazo huingizwa kwenye daftari la mbegu.Shughuli hiyo husaidia kutambua walinzi wa rasimali adimu na za kipee na kujenga uelewa kuwa watu wengi kuhusu umuhimu wa mbegu za mbegu.

Katika uchambuzi wa mifumo ya mbegu,hiyo ni mahususi katika kutambua mifumo ya mbegu iliyopo na michango yake katika kutosheleza hitajio la mbegu kwa wakulima.Kuhusu  uchambuzi wa jamii na sehemu ya kuzalisha benki ya mbegu hapa ni vema ikafahamika sababu mbalimbali zinapaswa kuzingatiwa wakati wa kuchagua jamii au eneo la kuanzisha benki za mbegu za jamii.

Hapo utaangalia upatikanaji wa aina tofauti za mbegu kwenye jamii, uzalishaji wa mbegu wa kutosha kwa mahitaji ya jamii , upatikanaji wa mbegu nzuri na bora ,mfano uwepo wa maduka ya pembejeo yanayouza mbegu za asili,uwepo wa wakulima wanaobadilishana ,wanaotunza na kuchagua mbegu na uwepo wa soko lenye wigo mpana wa mbegu.

Pia uwepo ujuzi shirikishi wa jadi wa mbegu, maarifa ya kutosha ya kuchagua mbegu bora ,nia ya vijana katika Kilimo, Mazingira mazuri ya sera yanayounga mkono mbegu za asili ,eneo liwe linafikika kiurahisi kwa wana jamii walio wengi .Eneo la kuhifadhi mbegu linaweza kuwa ni jengo la mwana kikundi.

Hatua ya pili ni kuhamasisha na kuiandaa jamii, ,hii ni kulingana na uelewa wa hali halisi ya bioanuai ya kilimo ndani ,wakulima wanaweza kuanza kuhamasishwa kushiriki katika shughuli za benki ya mbegu.Vikundi vidogo vy wakulima vinaweza kuanzishwa ambavyo vitaainisha mazao muhimu na kukusanya mbegu kwa niaba ya jamii kisha kufuatilia uzalishaji wa mbegu zilizopotea ,zilizopo hatarini kupotea .

Kuzalisha mbegu ni shughuli ya vitendo na kiashiria kuwa walulima wamehamasika .Hiyo inaweza kupanuliwa baadae kwa wanachama wa benki y mbegu ambayo pia wanakusanya mbegu kwenye mitandao yao.

Akielezea zaidi hatua hizo Mratibua Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kilimo hai( TABIO) Abdallah Mkindi anasema hatua ya tatu ni kuchagua aina za mbegu kwa ajili ya kuhifadhi ambapo anaeleza benki za mbegu za jamii huwa na lengo la kutunza Mbegu za mazao muhimu."Baadhi wanasisitiza kutunza mbegu za mazao ya jadi yanayohusiana na utamaduni wa ndani.

"Wengine wanaweka kipaumbele cha kutambua ,kuzalisha na kusambaza mbegu ambazo zinauwezo wa kuhimili changamoto za magonjwa na mabadiliko ya tabianchi kama vile joto,ukame na mafuriko.Mbegu za asili na zile zilozoboreshwa zinaweza kuchaguliwa kwa ajili ya kutunza, ni muhimu kwa Wana jamii kushauriana kuhusu aina za mbegu ambazo wanapendekezwa zikiwekwe kwenye benki zao"anasema Mkindi.

Wakati hatua ya nne , Mkindi anasema ni kuchagua mbegu bora na safi .Kigezo muhinu katika Uchaguzi wa mbegu ni kupata sampuli na kuchagua ambazo hazina magonjwa, hiyo inawezekana kwa kuchagua kutoka kwenye maeneo mbalimbali ya shamba na kutoka kwenye mimea na mashuke bora mbalimbali.

"Epuka kuchagua mbegu kunta kutoka kwenye mimea iliyo pembezoni mwa shamba ili kuondoa uwezekano wa maingiliano ya chavua . Tahadhari ichukuliwe ili kuchagua mimea ambayo haina magonjwa.Ni vema mbegu zisafishwe kuanzia shambani ili kuondoa zile zenye magonjwa,magugu na wadudu.Magonjwa ya mbegu husababishwa na kuvu,bakteria na virusi.

"Magonjwa mengi y kuvu yanatokana na udongo na hutokea kwenye uso ( mabano sehemu ya juu) ya mbegu ambazo hudsbabisha kushindwa kuota au kuwa na miche yenye magonjwa.Umakini unapaswa kuzingatiwa wakati wa kukusanya/ kuchukua mbegu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mikononi, vifaa vya kuvunia kama vile kisu au panga, na mifuko au vyombo vingine ni safi,amesema.

Aidha Mkindi anasema ni muhimu kuondoa sampuli yoyote ya mbegu ambayo ina dalili ya kuliwa na wadudu au ina magonjwa na kurudia zoezi hilo wakati wa kusafisha, kwa kuwa wadudu na magonjwa yanaweza kuongezeka wakati mbegu zimehifadhiwa.

Anasema ubora wa mbegu unatakiwa kufuatiliwa mara kwa mara kwa kufanya yafuatayo; kuchunguza kwa macho chombo kilichohifadhia mbegu, kuondoa kwa mkono mbegu zote au sehemu yake na kukagua kiwango cha unyevu,uwepo wa wadudu na magonjwa .Pia kufuatilia kiwango cha joto na unyevu kwenye vyombo vilivyohifadhia mbegu kwa kutumia kupima joto na unyevu .

Kwa mujibu wa Mkindi hatua ya tano ni kuweka miundombinu inayofaa ili kuweka mbegu katika hali ya usafi,afya na kuwa hai, miundombinu stahiki ni muhimu iwepo."Miundombinu hii inaweza kuwa ya kawaida mwanzoni lakini ikaaendelea kuboreshwa kulingana na wakati na hitajio.

"Miundombinu hiyo ni pamoja na rafu( shelfu au biliji kama inavyotambulika kwa wenyeji wa Mtwara) ,makabati ya mbao na chuma,mzani wa kupimia mbegu, kaushio la jua , vifaa vya kuhifadhia mbegu vyenye ujazo tofauti, kifaa cha kupangia madaraja ya mbegu ( CD grader), nyaraka za kutunzia kumbukumbu, ubao wa matangazo pamoja  na kipima joto na unyevu,anafafanua.

Hatua ya Sita ni kuingia taarifa za mbegu kwenye daftari la kumbukumbu , ambapo anaeleza benki za mbegu za jamii sio tu kuwa ni sehemu ya kuhifadhia mbegu na vipando lakini pia ni sehemu ambayo ujuzi wa asili na taarifa husika kuhusu mbegu za asili zinaweza kupatikana."Hivyo ni muhimu wakulima wakafundishwa kuweka taarifa za mbegu kwenye benki.

"Taaarifa hizo ni jina la mbegu( la asili au la kisayansi) ,matumizi yake maalumu, hali ya Sasa ya upatikanaji wa mbegu hiyo , sifa za jumla za mbegu hizo ,mbinu za kulima mbegu hizo ,kiwango cha usambazaji wa kilimo chake, uwezo wake wa kuvumilia magonjwa, ukame,thamani ya lishe yake, matumizi mbalimbali ya mbegu hiyo,"anafafanua Mkindi.

Aidha rejesta za kuweka kumbumbu za mbegu ambazo zinahifadhiwa kwenye daftari zijulikanazo kama rejesta ambazo ni rejesta ya mbegu zilizokusanywa na hilo ni daftari la mbegu zote zilizokusanywa kutoka kwa wakulima na kuhifadhiwa katika benki za mbegu za jamii.

Wakati hatua ya saba ni Kuzihuisha mbegu kwa kuzipanda  mara kwa mara ,ambapo kwa ujumla benki za mbegu za jamii zinakuwa na kiaisi kikubwa cha mbegu za asili na pia zinahifadhi kiasi kidogo cha mbegu zilizoboreshwa.Kulingana na upatikanaji wa rasilimali benki za mbegu hufanya zoezi la kuzipanda mbegu mara kwa mara ili kubakia kuwa hai na kubaki na ubora wake wa uotaji.

"Kwa aina za mbegu ambazo zinamahitaji , wanachama wa benki za mbegu za jamii wanaweza kutoa kipande cha ardhi kwa ajili ya kuzizalisha.Kwa aina ambazo zina soko kubwa ni rahisi kuamua kiasi kinachozalishwa kila mwaka kulingana na mahitaji ya wakulima."anasema Mkindi.

Anataja hatua ya Nane ni Kushirikiana habari ambapo anasema kushirikiana habari na uzoefu Kati ya mwanachama,wasio wanachama na wadau wengine ni jukumu jingine muhimu la benki za mbegu za jamii.Kushirikishana huku kunaweza kufanyika kwa njia ya kufanya maonesho ya mbegu.Pia inaweza kufanyika kwa kuandaa matukio ya misimu ambapo wakulima hubadilishana mbegu na maarifa yanayohusiana na mbegu.

Pia vikundi vya wakulima vinaweza kutenga baadhi ya siku za kutembelea mashamba ili kujionea aina mbalimbali za mbegu zinazopandwa, kutumia fursa za mikutano ya Kijiji na mingineyo katika kupashana habari zinazohusiana na benki za mbegu  .

Hatua ya tisa; Kufanya Ufuatiliaji na kupima matokeo ambapo benki za mbegu za jamii zinatumia mbalimbali ili kuhakiku kuwa mbegu zinazohifadhiwa ni zile zenye ubora ambao hauna magonjwa, wadudu,magugu na uchafu.

Pia Ufuatiliaji wa shughuli za benki pamoja na kupima matokeo yake hufanywa na timu ya usimamizi iliyoundwa .Dhumuni ni kuangalia nyuma na kupima malengo yanafikiwa au laa, Ufuatiliaji wa kila mwaka unaweza kujulisha jinsi benki ya mbegu ya jamii yaliyoweza kusimamiwa vizuri, ambaye alichangia katika shughuli zake na ambaye hakuwa na mbegu.


 

TANZIA; PROFESA NGOWI AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0

Rasi wa ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akiwa na Dereva wake Innocent Gerson Muringo wakati walipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam Machi 11, 2022. Ambao wote wamefariki duni leo 
Gari alilokuwa akisafiria Profesa Honest Ngowi.
Profesa Honest Ngowi enzi za uhai wake.

MAKAMU Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo Machi 28, 202kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Lughano Kusiluka, ambaye ametangaza kifo cha Prof. Ngowi na Dereva wake, waliofariki kwa ajali ya gari wakiwa njiani kwenda Kampasi Kuu Morogoro.

"Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine.

"Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imetoka eneo la Mlandizi mkoani humo ikihusisha magari matatu.

"Ni kweli ajali imetokea leo saa 12 asubuhi ikihusisha magari matatu aina ya Noah, Land Cruiser alilokuwa anasafiria yeye na lori ambalo ndio chanzo cha ajali lilihama njia na kuiangukia Noah ubavuni kisha kuilalia gari ya Ngowi," amesema Lutumo.

Lutumo amesema hadi wanamtoa eneo la tukio alikuwa bado mzima akiwaishwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Mkoa wa Pwani.


https://issamichuzi.blogspot.com/2022/03/wanawake-chuo-kikuu-mzumbe-wawafariji.html

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI KWENDA NA WAKATI

$
0
0



Na Mwandishi Maalum,Dodoma


Kasi ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa inayoikabili Tanzania na Dunia kwa ujumla inawataka Mawakili wa Serikali na hususani vijana, kuwa tayari kwa kujiendeleza , kujijengea uwezo na umahili katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na kasi hiyo.

Hayo yameelezwa leo ( Jumatatu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mawakili wa Serikali Vijana takribani 27 kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Kanda ya Dodoma.

AG Feleshi amewaambia Mawakili hao wa Serikali kwamba, ni kwa kujiendeleza na kujiongezea maarifa ndipo watakapoweza kuishauri vema na kwa weledi Serikali na kuedesha mashauri na mashtaka kwa ubora na viwango vya hali ya juu kama Mawakili wa Serikali.

“kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani sana kukutana nanyi Mawakili wa Serikali Vijana, na leo imewezekana. Na kubwa ambalo nimependa tubadilishane mawazo ni hili la kujengeana uwezo na maarifa katika sehemu zetu za kazi ili kupitia maarifa hayo muweze kutekeleza majukumu yenu na katika viwango vinavyokubalika” akasema AG Feleshi

Amebainisha kwamba yeye binafsi ni muumini mzuri sana wa dhana ya kujiendeleza na kujiengea maarifa na umahili mahali pa kazi. “Nimelisimamia hili katika maeneo mbalimbali niliyofanya kazi baada ya kuona changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu nikiwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na pia nikiwa Jaji kiongozi kwa sababu, niliona haja na umuhimu wa suala hilo na nimeona matokeo chanya ya dhana hiyo”.

Katika mazungumzo hayo na ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mtumba, Dodoma . AG Feleshi amesema uwezeshwaji wa Mawakili wa Serikali waliopo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mataifa ya Mashtaka kunaweza kufanyika kwa kuweka utaratibu mzuri wa Mawakili Waandamizi wenye uzoefu na waliobobea kuwafundisha na kuwaelekeza Mawakili wa Serikali vijana ili nao waweze kuboresha utendaji wao wa kazi.

“Tutambue wazi kwamba, dunia inabadilika kwa kasi sana, nasi lazima tuenende na kasi hiyo, nitawapa mfano mdogo, vita vinayoendelea hivi sasa kati ya Urusi na Ukraini italeta changamoto nyingi na kubwa, mnasoma huko Ulaya wanavyojadiliana kuangalia namna na hatua za kukabiliana na changamoto zitakazotokana na vita hiyo zikiwamo za masuala ya gesi na mafuta. Kwa hiyo tunaweza kujikuta tunapokea wawekezaji wengi katika maeneo hayo je kama mawakili wa Serikali tunajipangaje” akaeleza AG Feleshi.

Akawataka Mawakili hao wa Serikali kutambua kwamba leo wao ni vijana lakini kesho watakuwa viongozi na huwezi kuwa kiongozi pasipo kuwa na nia, hamu, utashi na uthubutu wa kujiendeleza na kujijengea maarifa. Nyinyi mmesoma katika mazingira mazuri na bora kuliko sisi wa huko zamani, rai yangu kwenu zitumieni fursa hizi vizuri”.

Amebainisha kuwa ni lazima na muhimu kwa wakili wa serikali kuwa na ujuzi na maarifa mtambuka na kuweza kutekeleza majukumu mbalimbali kwa wakati mmoja.

“Usiridhike kwamba wewe ni mwendesha mashtaka basi ukaishia hapo, au wewe ni Muandishi wa Sheria ukaridhika hivyo au wewe ni Mpekuzi wa Mikataba ukaridhika na hali hiyo. Kama ni mwendesha mashtaka basi uwena uelewa pia wa kuedesha kesi za madai, ujue pia kuandika sheria, ujue pia kupekua mikataba, na hivyo hivyo kwa muandishi wa sheria, ama mpekuzi wa mikataba, uwe tayari kufanya kazi sehemu au katika taasisi yoyote”

Akitilia mkazo juu ya umuhimu wa Mawakili wa Serikali kujiendelea na kujengea uwezao na umahili sehemu za kazi. Mwanasheria Mkuu Feleshi hata muelewa wakili yoyote wa serikali wakiwamo viongozi watakaofanyia mzaha jambo hilo na kwamba watakuwa kama kama wahujumu wa maendeleo yao binafsi ya na Taifa.

Vile vile amewahimiza Mawakili wote wa Serikali, kujiamini, kujithamini na kujipambanua kwa sababu nafasi yao kama Mawakili wa Serikali ni kubwa na ya heshima sana.

Kwa upande wao Mawakili hao wa serikali pamoja na kumshukuru Mhe. Mwanasheria Mkuu kwa kukutana nao na kubadilishana mawazo wameahidi kuzingatia ushauri wake na pia wameomba kuandaliwa utaratibu wa namna ya kubadilishana uzoefu ikimo namna ya kwenda mahakamani kuendesha.

“Mhe. Tunakushuru kwa kukutana nasi, tutayazingatia haya na tunaomba utaratibu uaandaliwe ili tuweze kubadilishana uzoefu na kujifunza na pia kwenda mahakamani”. Akasema Dkt. Dalfina Ndumbalo Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi  katika picha ya pamoja na  Mawakili wa Serikali  vijana kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Kanda  ya Dodoma. AG  Feleshi alikutana na Mawakili hao  Ofisini kwake Jijini Dodoma na  kubadilishana  mawazo na kubwa la kuwahimiza kujiendeleza mahali pakazi kila wapatano  fursa ili  kujijengea uwezo, maarifa na ujuzi wa kukabiliana na  kasi ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.  kulia ( mwenye  suti ya blu) kwa AG ni  Bw. Seth Henry Mkemwa Wakili wa Serikali Mkuu na Kaimu  Mkurugenzi Sehemu ya  Makosa ya Udanganyifu na  utakasaji Fedha.
Mawakili wa Serikali  kutoka Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Kanda ya  Dodoma,  wakimkiliza Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji  Dkt. Eliezer  Feleshi hayupo  pichani wakati walipokutana nae leo  Jijini Dodoma


ICS YAJA NA MKAKATI WA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO KWA NJIA YA KIDIJITALI

$
0
0

 

Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine (kulia chini) akizungumza kutoka Shinyanga Tanzania na Wazeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa (Sibongile Tsoanyane (kushoto) na Sussie Mjwara (kulia juu) wakishiriki mafunzo hayo wakiwa Afrika Kusini. Kushoto ni Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakiwa katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga wakishiriki mafunzo hayo kwa njia ya Mtandao (Tele Conference).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and Strengtherning their Societies (ICS ) linalohusika na masuala mbalimbali ikiwemo malezi na makuzi bora ya watoto,ulinzi na usalama kwa watoto na wanawake limetoa mafunzo kwa wafanyakazi wake 22 kuwajengea uwezo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Programu Tumishi (Aplikesheni) ya Parent App.

 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza leo Jumatatu Machi 28,2022 katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga, Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine  amesema timu ya ICS inajifunza na kujinoa kila siku kuendana na kasi ya kukua kwa teknolojia duniani.

 

Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference) na shirika la Crown Without Borders South Africa na wafanyakazi wa ICS Tanzania wapatao 22 wanajengewa uwezo kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi mpya wa Parenting for Life Long Health (PLH).


“Mafunzo kwa wafanyakazi 22 wa Shirika la ICS kwa ajili ya kujifunza mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App  ni sehemu ya kujijengea uwezo kabla ya kuanza utekelezaji yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference) na shirika la Crown Without Borders South Africa.  Baada ya mafunzo haya kazi ya utekelezaji itaanza katika mkoa wa Mwanza na Shinyanga ”,amesema Kudely.

 

“Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kidunia wa kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto ili kuondoa ukatili  dhidi ya watoto na wanawake (The Global Parenting Initiative) . Sisi ICS tumeanza mafunzo haya ili kutekeleza mkakati huu kupitia mradi wa Parenting For Life Long Health (PLH) ambapo tunashirikiana na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini”,ameeleza Kudely.


Amefafanua kuwa Shirika la ICS litakuwa linafanya utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini na kufanya utafiti wa kina ili kutambua ni kwa kiasi gani kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto kwa njia ya kidigitali na inaleta tija ili kupunguza ukatili dhidi ya watoto na wanawake.


“Tunaanza utekelezaji wa  mradi huu mkoani Shinyanga na Mwanza na awamu ya kwanza tumepanga kufikia wazazi/walezi 1100 na awamu ya pili tunatarajia kutanua utekekezaji na kufikia mikoa Zaidi ya 6 Tanzania na kufikia wazazi /walezi wasiopungua 6000”,amesema Kudely.


Ameongeza kuwa Utekelezaji wa mpango huu umekuja kama sehemu ya ubunifu (Innovation) wa namna ya kufikisha elimu katika jamii kwa njia ya teknolojia na kuwafikia wanufaika wengi zaidi ili kuleta mabadiliko na kuchangia kuondoa ukatili dhidi ya watoto na wanawake. 

“Na sisi kama ICS kila wakati tunapotekeleza afua zetu tunajifunza na kuja na ubunifu ambao unaweza kuleta tija Zaidi katika jamii lakini pia kufanya tafiti zitakozopima na kuthibitisha afua tunazotekeleza zinaleta matokeo chanya (Evidence Based Intervention)”,amesema

 

“Sisi kama ICS na washirika wetu (Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini) tunajitahidi kila siku kuwa wabunifu na kuja na mikakati ambayo inaweza kutumia rasilimali kidogo na kuleta matokeo makubwa katika afua zetu zote tunazozitekeleza”,ameeleza. 

Amefafanua kuwa Utekelezaji wa mradi huu (Pareting for Life Long Health-PLH) wa kutoa elimu ya malezi na makuzi ya bora ya mtoto kwa njia ya kijitali utachangia mpango wa dunia (The Global Parenting Initiative-GPI) wa kufikisha elimu ya malezi wa wazazi/malezi na pia mpango wa Taifa (NPA-VAWC) wa kupunguza Ukatili dhidi ya watoto wa wanawake na watoto.

“Wazazi/Walezi wengi wana simu kwa hiyo tumebuni namna ya kuwafikishia elimu kwa njia rahisi kabisa na inayotumia muda mfupi maana ParentAppmzazi/mlezi anaweza kuitumia hata wakati hayupo kwenyeInternet akajifunza na kupata ujumbe murua kabisa kuhusu malezi na makuzi bora ya watoto”,amesema Kudely.

Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine akizungumza leo Jumatatu Machi 28,2022 wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi 22  wa Shirika la ICS kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Programu Tumishi (Aplikesheni) ya Parent App. Mafunzo hayo yamefanyika kwa njia ya Mtandao (Tele Conference). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa Sussie Mjwara (kulia) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS (kushoto) wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa Sussie Mjwara (chini) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS  (kushoto juu) wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Sibongile Tsoanyane (chini) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine akifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.Wa kwanza kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Alex Nyembele.
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akielekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting).
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akiwaelekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting).
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akiwaelekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting). Wa kwanza kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Alex Nyembele.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


SPIKA DKT. TULIA ATAKA MABUNGE YA AFRIKA KUJIENDESHA KWA MFUMO WA KIDIGITALI

$
0
0

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza wakati wa kuendesha katika mfumo wa kimtandao katika kuendesha shughuli zake ili kuendana na teknolojia ya sasa.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ameshauri Mabunge ya Afrika kujiunga na kujiendesha katika mfumo wa kimtandao katika kuendesha shughuli zake ili kuendana na teknolojia ya sasa.

Spika Tulia ameyasema hayo leo Machi 28, 2022 wakati akifungua semina ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Ramada, Jijini Dar es salaam.

Pamoja na mambo mengine, amesisitiza kuwa kwa kutumia mfumo wa Bunge mtandao itawawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali za Bunge kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kujua yale yote yanayoazimiwa na Bunge lao lakini na wao pia kuwasilisha maoni na ushauri wao.

“Semina hii tunahitaji kuwajengea uwezo Wabunge kutoka Mabunge yote Afrika ili waweze kwenda kushauri kwenye nchi zao, zipo faida nyingi za kuwa na Bunge mtandao kwamaana zipo nyakati Wananchi, watafiti wanahitaji taarifa fulani za Bunge lakini zinamlazimu hadi aende Dodoma wakati angeweza kwa kutumia progam hii akayapata yote kwa wakati” amesema Spika Dkt. Tulia

Vilevile Spika Dkt. Tulia amesisitiza mfumo huo utawezesha pia kutoa uwanja mpana wa Wabunge kujadili mambo mbalimbali ya kiuchumi likiwemo suala la mapinduzi ya kilimo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MAJALIWA AREJEA NCHINI KUTOKA JORDAN

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi, 28, 2022 amerejea nchini akitoka Aqaba nchini Jordan alikomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan nchini Msumbiji na maeneo ya jirani (Aqaba Process). Pichani, Mheshimiwa Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakisalimiana na viongozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wa tano kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi, 28, 2022 amerejea nchini akitoka Aqaba nchini Jordan alikomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan nchini Msumbiji na maeneo ya jirani (Aqaba Process). Pichani, Mheshimiwa Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa (kulia) wakizungumza na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


KATIBU WA UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI UVCCM TAIFA CDE. VICTORIA MWANZIVA AKUTANA NA WAHAMASISHAJI UVCCM NGAZI YA TAWI

$
0
0

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva ashiriki Darasa la itikadi Tawi la UVCCM Msakuzi Mashariki- Kata ya Mbezi- Wilaya ya Ubungo- Mkoa wa Dar-Es-Salaam.

Cde. Victoria Mwanziva amewafunda vijana wa Hamasa katika darasa la Itikadi lilioandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Msakuzi; akiwasihi kujidhatiti ya kwamba hamasa ya kukipigania Chama huanzia ngazi ya Tawi; kwani huko ndiko kwenye wanachama wengi.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva amewasihi Vijana wote wa UVCCM; Kuendelea kutembea kifua mbele kusemea mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa taifa letu la Tanzania.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva aliambatana na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Dar-Es-Salaam Cde. Eng Ally Ummiy- na Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mbezi Mary Biita
katika tukio lililoandaliwa na Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Msakuzi Mashariki Cde Noel Kapinga ambaye alikuwepo na viongozi wa Tawi na Kata wa Chama na Jumuiya.




Wagonjwa saba wenye tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo watibiwa katika kambi maalum ya matibabu ya moyo

$
0
0




Wataalamu mabingwa wa moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri wakimwekea mgonjwa kifaa kinachousaidia moyo kufanya kazi kinachojulikana kwa jina la Cardiacresychronical Therapy–CRTD kinachotumia umeme mkubwa (High Power Device) wakati wa kambi maalum ya siku mbili ya matibabu hayo iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa saba wenye tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo walitibiwa katika kambi.

Na Mwandishi Maluum – Dar es Salaam
WAGONJWA saba wenye tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo wamepatiwa matibabu katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na wataalamu mabingwa wa mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri.

Akizungumzia kuhusu kambi hiyo iliyomalizika hivi karibuni daktari bingwa wa mfumo wa umeme wa moyo kutoka JKCI Yona Gandye alisema kambi hiyo ya siku mbili ilikuwa maalum kwaajili ya kutoa tiba kwa wagonjwa pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari na wataalamu wengine wa Taasisi hiyo.

Dkt. Gandye alisema matibabu ya wagonjwa hayo waliyagawa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni la wagonjwa ambao moyo ulishindwa kufanya kazi ukiambatana na tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo unaokwenda taratibu (Heart failure & slow electrical conduction). Wagonjwa hao walipandikizwa kifaa kinachojulikana kwa jina la Cardiac Resynchronical Therapy – CRTD) kinachotumia umeme mkubwa (High Power Device).

“Kifaa hiki cha CRTD ambacho waliwekewa wagonjwa watatu kinasawazisha mgawanyiko wa umeme wa moyo kufanya kazi kwa pamoja (Synchronization). Uwekaji wa kifaa hiki unatumia zaidi ya saa moja kutegemeana na tatizo alilokuwa nalo mgonjwa”, alisema Dkt. Gandye.

Kundi la pili la wagonjwa waliotibiwa katika kambi hiyo ni wale waliokuwa na tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo unaosababisha mapigo ya moyo kwenda haraka kuliko kawaida ambapo matibabu yao yalichukuwa zaidi ya masaa mawili.

Dkt. Gandye alisema, “Wagonjwa hawa ambao walikuwa watatu walipata huduma ya matibabu ambayo kwa kitaalamu yanajulikana kwa jina la EP Study & ablation ambapo wataalamu kwa kutumia vifaa maalum vilivyopo katika mtambo wa Carto 3 System 3D & Conventional System wanauwezo wa kutambua sehemu ambayo hitilafu ya umeme inapotokea na kisha kuithibiti ili hali hiyo isitokee tena”,.

“Kundi la tatu lilikuwa ni la mgonjwa mmoja kutoka Zanzibar aliyekuwa na tatizo la umeme wa moyo kwenda taratibu (Atrial Fibrillation with slow Ventricular response) na kuwekewa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi ambacho kwa jina la kitaalamu kinajulikana kwa jina la Pacemaker”,.

Dkt. Gandye alisema hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na kuna wagonjwa ambao wamesharuhusiwa na kurudi nyumbani na wengine wataruhusiwa siku chache zijazo.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo Prof. Mervat Aboulmaaty kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufunga vifaa tiba vya kisasa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kusomesha wataalamu ambao wanatoa huduma za matibabu ya kibigwa kwa wananchi.

Prof. Mervat alisema kambi hiyo pamoja na kutoa matibabu kwa wagonjwa pia ilienda sambamba na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya ndani na nje ya nchi.

“Wakati tunafanya matibabu ya upandikizaji wa kifaa cha CRTD yalirushwa moja kwa moja kwa njia ya satellite kupitia mtandao wa Zoom kutokea katika mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory) ambayo ni maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo inayotumia mionzi maalum uliopo hapa JKCI Tanzania ambapo wataalamu 42 waliweza kuona moja kwa moja tulichokuwa tunakifanya”,.

“Pia tulitoa mafunzo kwa njia ya mtandao wa Zoom kuhusu matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo na upandikizaji wa kifaa cha CRTD ambapo wataalamu zaidi ya 291 walihudhuria na kuweza kuuliza maswali mbalimbali kwa njia ya ujumbe fupi wa maandishi. Kutoa mafunzo kwa njia hii kunasaidia kwa kiasi kikubwa elimu hii kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi”, alisema Prof. Mervat.

Kwa upande wake Sabina Machange ambaye ni mwalimu mstaafu alishukuru kwa huduma alizozipata na kusema kwa muda wa miaka mitatu amekuwa na tatizo la kutokupumua vizuri, kuvimba tumbo na miguu baada ya kufanyiwa uchunguzi wataalamu walimwambia moyo wake haufanyi kazi vizuri na hivyo kutakiwa kuwekewa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri CRTD.

“Jumatano ya tarehe 23 mwezi huu nilifanyiwa upasuaji mdogo na kuwekewa kifaa hiki, sasa hivi ninajisikia vizuri nilikuwa siwezi kuinama kabisa lakini sasa hivi ninainama bila shida, nilikuwa siwezi kupumua vizuri sasa hivi ninapumua bila wasiwasi. Leo hii nimeruhusiwa, daktari ameniambia nirudi kliniki jumanne ijayo”,.

Mama Sabina alisema changamoto kubwa aliyokutana nayo ni gharama kubwa ya matibabu na kuambiwa kuwa bima ya taifa ya afya (NHIF) ambayo anaitumia hailipii matibabu hayo na kuiomba Serikali iangalie ni namna gani itawasaidia wagonjwa wenye matatizo kama yake ili waweze kupata matibabu.

“Niliambiwa gharama ya kuwekewa kifaa hiki ni shilingi milioni 29 na laki mbili nikaenda makao makuu ya mfuko wa taifa wa bima ya afya Dodoma na kuwaandikia barua ili wanilipie nusu gharama wakanijibu kwa barua kuwa utaratibu huo haupo”,.

“Lakini ndugu na jamaa zangu walinichangia fedha, nikaweza kulipia nikawekewa kifaa hiki. Ninaiomba Serikali kupitia mfuko wa Taifa wa bima ya afya ishiriki kulipia hata kwenye matibabu yenye gharama kubwa kwa kuchangia japo nusu gharama”, alisema Mama Sabina.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alimshukuru Prof. Mervat na timu yake ya madaktari wawili kutoka nchini Misri kwa huduma waliyotoa kwa wagonjwa na kuweza kuokoa maisha yao.

“Ninawashukuru madaktari, wauguzi pamoja na mafundi sanifu wa moyo (Technician) wa Cathlab kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa wageni wetu pamoja na kupokea mafunzo yaliyotolewa na wataalamu hao pia kwa huduma nzuri waliyoitoa kwa wagonjwa ambao walipatiwa matibabu katika kambi hii”, alishukuru Prof. Janabi.

Mradi wa Wanawake na Uongozi Zanzibar wachukua sura mpya utatuzi vikwazo kwa wanawake

$
0
0


WADAU wa haki za wanawake Pemba wamesema wapo tayari kushirikana na ofisi za serikali kujadili mbinu bora za utatuzi wa mapungufu na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao na kupelekea kukwaza ufikiaji wa hazi za wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya uongozi.

Wametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kujadili mpango kazi wa namna ya kuzitaftia ufumbuzi changamoto zilizoibuliwa na wahamasishaji jamii kupitia mikutano iliyofanyika kwenye shehia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ushiriki wa wanawake katia uongozi unaotekelezwa na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania, (TAMWA Zanzibar), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Pamoja na PEGAO kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini.

Walisema baada ya kuzibaini changamoto hizo zilizopo katika jamii, watasaidia kuongeza nguvu kuzifikia taasisi zote zinazohusika na utatuaji wa kero hizo ili kushauriana njia bora za kutatua matatizo hayo.

Aidha walizitaka taasisi hizo ambazo zimeonekana kuwepo kwa changamoto katika utoaji wa haki kwa wananchi kuwa tayari kushirikiana na wadau hao ili kuzitaftia suluhu ya Pamoja changamoto hizo.

Safia Saleh Sultan, mhamasishaji jamii Wilaya ya Chake, alisema moja ya changamoto iliyoibuliwa ni uwepo wa sheria zinazokwaza ufikiaji wa usawa wa kijinsia kwa wanawake kushiriki katika ngazi za uongozi kutokana na sheria hizo kuweka masharti magumu kwa wanawake wanapohitaji kugombea.

Alitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni; Sheria ya watumishi wa Umma No.3/2003, Sheria ya Mahakama ya Kadhi No.7/2001, Sheria ya Vyama vya Siasa (1992) na Sheria ya Uchaguzi no 4/2018, ambapo sheria hizo zimeweka masharti magumu kwa wanawake wanapohitaji kugomea nafasi za uongozi.

Alisema kutokana na masharti ya sheria hizo kuwa ngumu kwa wanawake watumishi wa umma inapelekea kukosekana kwa wanawake wenye uwezo mzuri wa kiutendaji katika ngazi za maamuzi.

Nae mhamasishaji jamii Wilaya ya Wete, Rukia Ibrahim, alisema kuwepo kwa wanawake wengi wasiojua kusoma na kuandika ni miongoni mwa changamoto pia zilizobaika kwenye shehia kuwakosesha wanawake kushiriki kikamilifu katika michakato ya kiuongozi.

Alieleza, “kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya wanawake wengi tulibaini ni changamoto inayokwaza wanawake wengi kukosa haki zao za kushiriki katika masuala ya demokrasia na uongozi.”

Mapema mkurugenzi wa jumuiya ya PEGAO, Hafidh Abdi, alisema mkutano huo ulilenga kuwaleta Pamoja wadau wa haki za wanawake kuzipitia changamoto zilizoibuliwa na wahamasishaji jamii kwenye shehia na kuandaa mpango kazi wa Pamoja kuhusu namna ya kutafta ufumbuzi wa changamoto hizo.

“Mkutano huu tumejikita kuzipitia changamoto zote zilizoibuliwa kwenye jamii ambazo kwa namna moja au nyingine zinakwaza upatikanaji wa haki za wanawake na kuzijadili hapa kwa pamoja ili tuone ni njia gani bora tunaweza kuzitumia ili kusaidia changamoto hizo kutaftiwa ufumbuzi,” alisema Mkurugenzi huyo.

Changamoto nyingine ambazo ziliibuliwa na wahamasishaji jamii ni pamoja na, ukosefu wa vitambulisho vya mzanzibar na kuzaliwa kwa wanawake wengi, pamoja na huduma nyingine muhimu za kijamii ikiwemo maji safi na salama kwa baadhi ya shehia.

Mkutano huo uliwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali Pemba wakiwemo, viongozi wa vyama vya siasa, Dini, taasisi na idara za serikali, wasaidizi wa sheria, pamoja na asasi za kiraia zinazotetea haki za wanawake ambapo Pamoja na mambo mengine wliahidi kufanyia kazi changamoto zilizoelekezwa kwenye taasisi zao katika kipindi cha wiki mbili.


 

VIJIJI VYA VIJANA VYA KILIMO MBIONI KUANZISHWA ILI KUCHOCHEA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA KILIMO

$
0
0


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amebainisha kuwa Serikali imeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha inaanzisha vijiji vya kilimo vya vijana katika maeneo ya kilimo nchini kupitia mfumo wa mashamba makubwa ya pamoja “block farms” ili kuchochea ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana tarehe 27 Machi, 2022 Jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi kwenye Maonesho ya Wajasiriamali Wanawake na Vijana yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara Wanawake na Vijana Tanzania (TABWA) na katika uzinduzi wa mpango wa kushirikisha Vijana na wakina mama kwenye mnyororo wa kuongeza thamani wa mazao ya kilimo

"Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Toboa na Kilimo, tumedhamiria kuanzisha mfumo wa mashamba ya pamoja ya vijana (block farming), ili vijana walime, wajenge makazi yao na waishi hapo hapo, hii itakuwa ni ya hatua kubwa ya mfumo mzuri wa kuwawezesha vijana kwenye utatuzi wa chamgamoto ya Ajira na itavutia vijana wengi kuingia kwenye kilimo.

Kupitia program hii Vijana wataandaliwa ardhi ambayo itakuwa imepimwa Afya ya udongo,itakayowekwa mifumo ya umwagiliaji,upatikanaji wa pembejeo na baadaye kutafutiwa masoko ya mazao watakayozalisha.

Tunamshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake kupitia benki kuu ya Tanzania juu ya riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,ambapo hivi sasa riba ya mikopo ya kilimo imeshuka mpaka chini ya 10% kwa Taasisi nyingi za fedha na hivyo kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wadau wa kilimo” Alisema Mavunde

Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alipokea taarifa ya Vijana waliokwenda kwa ufadhili wa serikali katika maonesho ya Biashara ya Dubai Expo na maonesho ya Kilimo Mjini Konya,Uturuki na kuwataka kutumia ujuzi na fursa walizopata kwa ajili ya kuendeleza kilimo nchini Tanzania na kuwa mabalozi wazuri wa ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo.

Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa TABWA, Bi. Noreen Mawala amesema kuwa Taasisi yake itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanawake na vijana wengi zaidi wanachangamkia fursa nyingi zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo na kuishukuru serikali kupitia wizara ya kilimo kwa hamasa kubwa wanayoitoa katika kuhakikisha ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo ili kutatua changamoto ya Ajira miongoni kwa Vijana na kupunguza umaskini wa wananchi.








Mpiga debe wa mabasi ya BM adaiwa kuwawa Kwa kuchomwa kisu Morogoro, jeshi la polisi latoa wito

KAMATI YA PAC YATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA MAJI MKURANGA

$
0
0





Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akibonyeza kitufe cha kuwashia pampu ya maji wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiangalia tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)



PICHA NA OFISI YA BUNGE
Viewing all 120247 articles
Browse latest View live