IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO MACHI 29,2022
KOKA APANIA KULETA MAGEUZI KWA WANACHAMA CCM AKABIDHI SIMU JANJA KWA KATA ZOTE 14
Na Victor Masangu Kibaha
Katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha mapinduzi (CCM) Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kushirikiana bega kwa began a Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wameamua kutoa simu janja 14 kwa ajili ya kuweza kusaidia kusajili wananchama kwa mfumo wa njia ya kielekroniki.
Koka akizungumza katika halfa hiyo ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama kutoka ngazi za Kata pamoja na matawi alisema kwamba alisema ameamua kujitolea simu hizo ili ziweze kurahisisha zaisi zoezi la kuwasajili wanachama wa zamani pamoja na wapya kwa njia ya kisasa zaidi.
“Nimeamua kukabidhi simu hizi kwa sababu jambo hili lilikuwa linatutatiza kwa mipindi cha muda mrefu kwa hiyo kata zote 14 nimezipatia simu janja hizo ambazo sasa zitatumika kuwasajili wanachama wetu wa CCM kwa njia ya kidigitali zaidi na hili jambo ni kwa ajili ya manufaa ya chama cetu cha mapinduzi,”alisema Koka.
Mbuge huyo aliongeza kuwa wakati chama kinaelekea katika kuchagua viongozi wake mbali mbali ni lazima itambue wanachama wake wamefanyiwa usajili kwa mfumo wa kidigitali ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.
Katika hatua nyingine aliwataka wanachama wote wa CCM Katika jimbo lake kuhakikisha wanazingatia kanua na sheria zilizopo ikiwa sambamba na kuwajushusha kuendelea kulipa ada na kuwataka viongozi ambao wamekabidhiwa simu hizo kuhakikisha wanazitunza vizuri na kuzitumia kwa matumizi ambayo yamepangwa na sio kuziweka kabatini.
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma alisema anatambua mchango mkubwa ambao unafanywa na chama chake hivyo akaamua kusapoti kwa kutoa simu nne kwa wanachama hao lengo ikiwa ni kupata fursa ya kujisajili kwa urahisi kwa njia ya kieletroniki.
Pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa hatua hiyo ya kutoa simu sambamba na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote wa Tanzania.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Pwani Said Goa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo alisema kwamba simu hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kufanya usajili kwa wanachama katika kata zote 14 ambazo zipo katika Jimbo la Kibaha mjini.
Goa alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ya mwisho kwenye usajili wa wanachama kwa njia hiyo kati ya Wilaya tisa za mkoa huo.
Alisema kuwa moja ya changamoto walizokuwa nazo ni ukosefu wa simu za kusajilia wanachama.
Naye Diwani wa Viti Maalum Selina Wilson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha alisema kuwa msaada huo utasaidia kwani walikuwa na wakati mgumu kujichangisha hadi kununua simu hizo.
Wilson alisema kuwa watashirikiana na viongozi wa kata ili kusajili wanachama kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM kata ya Kongowe Simon Mbelwa alisema aliwapongeza kwa dhati wabunge hao kwa kuweza kutoa simu janj ahizo ambzo zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwasajili wanachama hao.
Aliongeza kwamba malengo yao makubwa ni kuhakikisha kwamba wanawasajili wanachama wote wa CCM kwa kutumia mfumo huo wa kieletroniki na kwamba watajitahidi kupitia katika maeneo yote kuanzia kazi za mitaa.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa ameshika simu janja ambazo amezikabidhi kwa viongozi wa kata kwa ajili ya kuweza kutumika katika kusajili wanachama wa CCM kwa njia ya kieletroniki.
Mbunge mstaafu wa jimbo la Kibaha vijijini wa kushoto akiwa anamkabidhi simu janja Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani wakati wa halfa fupi ambayo ilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM halmashauri na mji Kibaha.
LITA YATAKIWA KUWA CHANZO CHA ELIMU BORA YA MIFUGO
Na. Edward Kondela
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda ameitaka Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) kuwa chanzo cha elimu bora ya mifugo ndani na nje ya nchi.
Bw. Nzunda amesema hayo jijini Dodoma (28.03.2022) wakati akifungua rasmi kikao cha tisa cha Baraza Kuu la Wafanyakazi la LITA na kubainisha kuwa ni wakati sasa wakala hiyo kuwa chanzo cha kuwashauri wafugaji na kutoa maarifa kwa wadau wa sekta ya mifugo ili sekta hiyo iweze kuimarika na kuwa ya kisasa zaidi.
Ameongeza kuwa wakufunzi wa LITA wanatakiwa pia kuwa chanzo cha kuandaa majarida mbalimbali vikiwemo vitabu vya ufugaji na kuwa chanzo cha kubuni na kupatikana kwa maarifa mapya yanayotokana na tafiti zinazofanywa na wakufunzi hao.
Aidha, katibu mkuu huyo amefafanua kuwa wajibu wa LITA ni kuwa karibu na umma kwa kutoa huduma bora ikiwemo ya wanafunzi wanaohitimu kuwa bora na wanaoheshimika, kutambulika, wenye maarifa, wanajiamini na kuandaliwa vizuri kwenda kusaidia sekta binafsi.
Awali Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la LITA Dkt. Pius Mwambene, akizungumza kabla ya ufunguzi rasmi wa kikao hicho amesema wakala hiyo imeendelea kuimarisha mahusiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inaboresha miundombinu ya kufundishia.
Dkt. Mwambene ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa LITA amefafanua kuwa kwa sasa wakala hiyo inakaribia kukamilisha makubaliano ya ujenzi wa kampasi ya LITA Mkoani Songwe ikiwa ni jitahada za kuongeza wigo wa elimu ya mifugo katika maeneo mbalimbali nchini.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wafugaji wanapata mwongozo wa ufugaji bora LITA imeanisha utaratibu wa kuwashikiza wanafunzi wa hatua ya nne kwa wafugaji katika maeneo yao wakati wa likizo ili kuanza kujenga uzoefu ujasiri wa kuwahudumia wafugaji mapema.
Pia, amebainisha kuhusu vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi LITA, kuwa vinalenga kuishauri wakala kutekeleza majukumu yake kama ilivyoelekezwa kwenye sheria, kupokea na kujadili makadirio ya mapato kwenye matumizi ya wakala na kujadili mipango ya utekelezaji wake kwa ajili ya ustawi wa wakala na wafanyakazi wake.
Kufuatia malengo hayo amewataka wajumbe wa baraza kushiriki kikamilifu na kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya wakala.
Akitoa neno la shukran baada ya kufunguliwa rasmi kwa kikao cha tisa cha Baraza Kuu la Wafanyakazi LITA, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa amesema wataendelea kusimamia maadili na weledi kwa wafanyakazi wa LITA na kuongeza ushirikishwaji ili kuwa na matokeo makubwa yenye maslahi mapana yatakayoleta tija.
Dkt. Mwilawa amefafanua kuwa nguvu zaidi zitaelekezwa kwenye maeneo ambayo yatagusa jamii na kwamba maelekezo yote yatafanyiwa kazi kwa kuweka vigezo na kupima vizuri ili kufikia malengo.
Amesema kuwa kila mfanyakazi aliyepo LITA atahakikisha anapata stahiki zake ili aweze kutekeleza majukumu yake kama anavyotegemewa katika kutoa mafunzo ya elimu bora ya mifugo kwa wanafunzi.
Nao baadhi ya wajumbe wa baraza katika kikao hicho, wametoa maependekezo kadhaa ya kuboresha utendaji kazi pamoja na mazingira ya wafanyakazi ili waweze kufanya kazi kwa morali na kufikia malengo ya LITA.
Wamesema kikao hicho ni muhimu katika kukumbushana utekelezaji wa mambo mbalimbali yakiwemo ya kiutawala kwa kuwashirikisha wafanyakazi na kutatua kero na kuwapatia taarifa sahihi kwa wakati ili kuondoa manung’uniko kazini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha tisa cha baraza hilo na kuitaka LITA kuwa chanzo cha elimu bora ya mifugo ndani na nje ya nchi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Dkt. Pius Mwambene, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha tisa cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma, na kubainisha kuwa wakala hiyo imeendelea kuimarisha mahusiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inaboresha miundombinu ya kufundishia ukiwemo ujenzi wa Kampasi ya LITA Mkoani Songwe ambao uko katika hatua mbalimbali ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha tisa cha Baraza Kuu la Wafanyakazi la Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) jijini Dodoma, ambapo amesema wataendelea kusimamia maadili na weledi kwa wafanyakazi wa LITA na kuongeza ushirikishwaji ili kuwa na matokeo makubwa yenye maslahi mapana yatakayoleta tija. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA), na viongozi wengine kutoka wizarani, mara baada ya kufungua kikao cha tisa cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo
MHE. JENISTA AWATAKA TAKUKURU KUISHI MAONO YA RAIS SAMIA KUHAKIKISHA MIPANGO NA HUDUMA ZA MAENDELEO ZINAWAFIKIA WANANCHI KWA UKAMILIFU
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameielekeza Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha wanayaishi maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mipango na huduma za maendeleo zinawafikia wananchi kwa ukamilifu.
Mhe. Jenista amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya TAKUKURU alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Mhe. Jenista amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali anayoiongoza ya Awamu ya Sita imejipanga kikamilifu kuleta mageuzi makubwa kwenye taifa katika sekta zote ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati, hivyo, TAKUKURU wanao wajibu wa kuhakikisha maono ya Mhe. Rais pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita yanafikiwa kwa ukamilifu.
“TAKUKURU tuna deni kubwa sana kwa Watanzania katika kuhakikisha mipango na huduma zinazotakiwa kuwafikia Watanzania zinawafikia kwa ukamilifu,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Ameongeza kuwa, yale ambayo Watanzania wanafikiria Serikali yao iwafanyie, hayawezi kufanikiwa kwa ufasaha kama miongoni kwa taasisi wezeshi ikiwemo TAKUKURU isipofanya kazi yake sawasawa.
“Ili taifa liweze kupiga hatua kimaendeleo, basi TAKUKURU katika kutekeleza majukumu yetu ni lazima tuzingatie Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo uliopo, maono ya Mhe. Rais aliyepo madarakani pamoja juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kufanya mabadiliko makubwa ya mwenendo mzima wa uchumi, upelekaji wa huduma kwa wananchi, nidhamu, maadili ya taifa hili,” Mhe. Jenista amefafanua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni amemshukuru Mhe. Waziri kwa kufanya nao kikao kazi na kuahidi yeye pamoja na watendaji wengine kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili kuendana na matarajio ya Serikali ya kufikisha huduma bora kwa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi wa Intelijensia –TAKUKURU, Bw. Malimi Mifuko akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo kilichofanyika leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Saudia Yaonesha nia kuwekeza kwenye Mwendokasi
Na.Mwandishi Wetu.
Nchi ya Saudiarabia imeonyesha nia ya kufanya uwekezaji mkubwa katika mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) katika uendeshaji wa Mabasi, Teknolojia pamoja na mifumo ya uendeshaji kutokana na uzoefu wa miaka mingi walio nao katika sekta hiyo, lakini pia kutokana na Tanzania kuwa na mazingira mazuri na tulivu kwaajili ya uwekezaji.
Akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka pamoja na wawakilishi wa makampuni ya uwekezaji kutoka Saudiarabia, Balozi wa Tanzania nchini Saudiarabia Mh. Ally Mwadini amesema ujumbe huo umeonyesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya usafirishaji hasa katika mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka kutokana na mazingira wezeshi yaliyopo Tanzania ambayo yanawahakikishia wawekezaji uhuru wa kuwekeza.
“Leo tumekuja kwa ajili ya kuona ni namna gani Saudiarabia inaweza kushiriki katika mradi huu wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama mwendokasi, hii inatokana nan chi ya Saudiarabia kuwa na uzoefu katika uendeshaji wa Miradi kama hii, lakini pia kwakua Tanzania ni nchi ya Amani na utulivu na yenye watu wakarimu pamoja na mazingiza wezeshi yaliyopo katika uwekezaji” Alisema Balozi Mwadini.
Amesema Tanzania ina umuhimu mkubwa sana kibiashara na uwekezaji katika ukanda huu wa Afrika kwani imepakana na nchi nyingi ambazo hutegemea huduma na bidhaa zake kupitia hapa nchini suala ambalo linawafanya wawekezaji kuona fursa hiyo na kuvutiwa kuja kuwekeza.
“Nimeambatana na wawakilishi wa kampuni ya Saudiarabia Public Transport Company (SABTCO) pamoja na Taasisi ya Uwekezaji ambayo inahusika na kuwekeza nchini Saudiarabia pamoja na nje ya nchi lengo kubwa ni kuja kuona na kutathmini namna watakavyoweza kuja kujiunga na Tanzania katika kuendeleza sekta ya Usafirishaji pamoja na sekta nyingine ambazo watavutiwa nazo” Alisema Balozi Mwadini.
Balozi Mwadini alisema Saudiarabia ni nchi iliyoendelea na yenye mahusiano mazuri na Tanzania hivyo wameamua kuja kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mh.Samia Suluhu Hassan za kuwaletea Watanzania maendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni ya SABTCO Bw.Hassan Abduljawad alisema wameona mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ni eneo sahihi kwa wakati huu kutembelea na kuona namna wanavyoweza kuwekeza kwakua kuna awamu sita za mradi huo katika Jiji la Dar es Salaam jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa watu wengi na wa fedha nyingi.
“Sisi tuna uzoefu wa kuendesha miradi kama hii kwa miaka mingi tumeona kwa awamu zote za mradi hapa Tanzania tunawez na sisi kuja kuwekeza katika moja ya awamu ili tuweze kutoa mchango wetu na uzoefu wetu kwa ajili ya watanzania” Alisema Bw. Abduljawad.
Ujio wa wawekezaji kutoka Saudiarabia ni moja ya Juhuzi zilizotokana na ziara ya Mh.Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi za Ulaya na Falme za kiarabu za kutafuta wawekezaji kwaajili ya kuja kuwekeza katika sekta mbali mbali hapa nchini.
Aidha kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kimekua mstari wa mbele katika kutafsiri maono ya Rais Samia ya kutaka kuona Tanzania inayokua kiuchumi kupitia uwekezaji wenye tija kwa kuendelea kuratibu na kuleta wawekezaji katika sekta mbalimbali ili kutumia fursa nyingi zinazopatikana nchini.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mh.Ally Mwadini akizungumza na wanahabari (Hawapo Pichani) Katika ukumbi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Ubungo Maji Jijini Dar es Salaam baada ya kikao baina ya Wakala na wawekezaji kutoka Saudi Arabia, Machi 28, 2022.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mh.Ally Mwadini (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Katika ukumbi wa Wakala Ubungo Maji Jijini Dar es Salaam baada ya kikao baina ya Wakala na wawekezaji kutoka Saudi Arabia, Machi 28, 2022.
ZAIDI YA WANANCHI 22,000 WA NYANGAO - MTAMA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA
Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao - Mtama
Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446
Mradi huo utatekelezwa jimboni humo kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13 vya Nyangao A, Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni
Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti comred Athumani Seif Hongonyoko.
Waziri Nape amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia na baadhi ya Wananchi wa jimboni kwake mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi mradi wa maji safi na salama baina ya RUWASA na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Ltd kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye kata tatu za jimbo hilo
WATUMISHI CHUO CHA TAIFA CHA UTALII WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA BIDII,NIDHAMU
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KATIBU Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael amefanya mazungumzo na watumishi na viongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) huku akitumia nafasi kupongeza chuo hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vema na kuwambusha kwamba jambo nzuri kwa watumishi wa umma ni kuchapa kazi kwa nidhamu ya hali ya juu
Dk.Michael amesema hayo baada ya kufanya ziara katika Chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kuzitekeleza taasisi,idara na mashirika yaliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.Akiwa katika Chuo hicho amejionea shughuli za chuo hicho.
"Jambo kubwa katika utumishi wa Umma ni kuchapa kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa weledi na kwa juhudi kubwa , kufuata miongozo na taratibu zilizopo, kutii viongozi sambamba na kutumia muda mwingi kwenye kazi.Lakini naomba niseme Chuo hiki kina bahati ya kuwa na watumishi wengi vijana wanaofanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu,"amesema.
Ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Chuo hicho kuwatafutia nafasi za masomo watumishi hao ili kujiendeleza na kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza morali ya kazi kwa watumishi hao na kufanyakazi kwa bidii na weledi.
"Hapa naona kuna damu changa, kuna wakufunguzi wengi wadogo nikuombe Mkurugeni kuwatafutia nafasi za masomo wajiendeleze kimasomo, wapelekeni kwenye masomo kwani kusomesha watumishi ni kazi ya Taasisi, kuna faida kubwa ikiwemo kumfanya mtumishi aipende Taasisi
"Hivyo nikuombe sana Mkurugenzi tafuta fedha na mimi nitakusaidia kutafuta ili hawa watumishi waende shule wakirudi utakuwa umeongeza motisha ya kazi na kuendelea kuipenda kazi yao na kuifanya Taasisi kuwa na wataalamu wa kutosha na hivyo kufikia malengo yake"ameongeza Dkt. Michael.
Awali akitoa hotuba ya utangulizi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka ameelezea kazi mbalimbali za utoaji mafunzo zinazofanywa na Chuo hicho katika Kampasi zake nne ikiemo Bustani iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Temeke, Arusha na Mwanza, na kwamba kwa sasa Chuo hicho kinaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kinapata watumishi wa kutosha kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukiwezesha Chuo kuendelea na mipango yake mbalimbali.
Aidha amesema katika mwaka huu wa fedha Chuo hicho kimekuwa na vipaumbele saba ambavyo mpaka sasa ndio majukumu yao wanayoendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kuimarisha mafunzo na shughuli za chuo hicho.
Amesema katika mwaka huu wa fedha wamekuwa na vipaumbele ambavyo ni pamoja na kuimarisha kampasi yetu mpya iliyopo kule mwanza, kuandaa sheria mpya ya uendeshaji wa chuo, kuongeza wigo wa kukusanya mapato ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu.
Pia walikuwa na kipaumbele cha kuongeza uwezo wa kufanya utafiti katika Sekta ya Utalii na Ukarimu."Pia tuna lengo la kupanua Kampasi yetu ya Arusha ambapo kimkakati Arusha ndio Mkoa unao ongoza katika shuguli za Utalii, lengo letu lingine ni kuhamisha Kampasi yetu ya temeke iliyopo kwenye Wilaya ya Temeke."
Pia Dkt. Sedoyeka amemueleza Katibu Mkuu huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi katika maeneo mbalimbali, changamoto ya Chuo kutokuwa na Muundo wake, miundombinu chakavu, madeni ya ndani na nje ya muda mrefu,ufinyu wa bajeti .
Ambapo ameeleza kuwa changamoto hii imefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa na katika mwaka huu wa fedha Chuo kimepata fedha kwa wakati hivyo kuishukuru Serikali na kwamba ana imani kubwa kwa mwaka ujao wa fedha wataongezewa fedha katika bajeti yao.
Watumishi wa Chuo cha Taifa Utalii wakifuatilia ootuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael
Mkurugunzi wa Fedha na Utawala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) CPA Munguabela Kakulima akizungumza wakati alipokuwa akifanya utambulisho katika mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kulia) wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chuo cha taifa cha Utalii (NCT) CPA. Munguabela Kakulima mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Jijini Dar es Salaam
SHILINGI BILIONI 10 ZA RAIS SAMIA ZATEKELEZA MIRADI TARAFA YA NDAGO IRAMBA
Na Dotto Mwaibale, Iramba
SHILINGI BILIONI 10 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka mmoja wa uongozi wake zimewezesha kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Tarafa ya Ndago iliyopo Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda wakati akiwahutubia Wananchi wa Tarafa ya Ndago kwenye mkutano wa hadhara baada ya kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo zilipomaliza kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Tarafa hiyo jana.
Mwenda alisema kamati hizo zilifanya ukaguzi wa miradi hiyo ili kuona nini kimefanyika katika mwaka mmoja wa uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi katika Tarafa hiyo.
Aliwataja alioongozana nao kufanya ukaguzi huo kuwa ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo na kamati ya siasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo na timu yake wakiwemo wataalam, Mwenyekiti wa Halmashauri na kamati ya ulinzi na usalama.
Alisema mambo yaliyofanyika katika wilaya hiyo ni mengi na kuwa wamepanga kila Tarafa kati ya nne zilizopo waielezee miradi iliyofanyika ambapo wameanza na Tarafa ya Ndago yenye kata sita ambayo ni kubwa kuliko tarafa zingine zote katika wilaya hiyo ambapo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imetekelezwa miradi yenye thamani ya Sh. 10. Bilioni.
Alisema yeye kama kiongozi mkuu wa Serikali na CCM wameona baada ya kufanya ukaguzi huo waitishe mkutano wa hadhara ili waweze kuwaeleza walichokiona katika miradi hiyo, changamoto zilizopo,inaendeleaje, usimamizi wake upoje, lini itakamilika na watarajie nini.
Alisema miradi ya elimu iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika shule za msingi wamekamilisha ujenzi wa darasa moja Shule ya Msingi Senenkwa ambalo limegharimu Sh.11.3 Milioni, ujenzi wa darasa moja Shule ya Msingi Azimio ambapo pia wamepeleka kiasi hicho cha fedha.
Mwenda alisema wamekamilisha ujenzi wa bweni moja katika Shule ya Watoto wenye mahitaji maalumu ya Songambele ambapo wamepeleka Sh.80. Milioni, kumalizia chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Mtekente walipeleka Sh.20 Milioni, ujenzi wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Ulugu walitoa Sh.20 Milioni.
Aliongeza kuwa wamejenga vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ushora ambapo pia walitoa Sh.40 Milioni, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Ndulungu tayari tumetoa fedha awamu ya kwanza Sh.470 Milioni na awamu ya pili tunategemea kupokea Sh.130 Milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari kutaifanya Tarafa nzima ya Ndago kila kata kuwa na shule ya sekondari hivyo ni jambo la kujivunia na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyowafanyia Wana Ndago.
Akizungumzia sekta ya Afya alisema wanajenga Kituo cha Afya Mwanduigembe ambapo Serikali itawapelekea Sh.500 Milioni, ujenzi wa Kituo cha Afya Ulugu kwa gharama ya Sh.500 Milioni tayari wamepokea Sh. 250 Milioni.
Mwenda alisema tangu nchi hii ipate Uhuru Tarafa ya Ndago ilikuwa na kituo kimoja tu cha afya na hicho kilichopo ambacho wanakitumia kilijengwa mwaka 1976 kikiwa ni Zahanati ndogo na ilikuwa kabla hata ya CCM hakijazaliwa lakini ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan anajenga vituo viwili vya afya katika kila kata ili ni jambo la kushangilia kwani ni zaidi ya miaka 50 kulikuwa na kituo hicho kimoja tu.
"Ni mwaka mmoja tu wa uongozi wake amefanya hivyo je akimalizia na hiyo miaka yake tisa kuwa madarakani si atajenga vituo vya afya katika kata zote za Wilaya ya Iramba" alisema Mwenda.
Akizungumzia Maji alisema katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan wamepelekewa Sh. 465 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Zinziligi na Sh.730 Mradi wa Maji Kaselya yote ikiwa Tarafa ya Ndago.
Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Malango alisema wamepeleka Sh.201 Milioni na sasa inafanya kazi, alisema wanafungua barabara kutoka Ulugu, Mang'ole hadi Mpugizi ya kilometa 9.5 kwa gharama ya Sh.765 Milioni.
Alisema wanajenga barabara ya ya kutoka Mtekente, Msansao hadi Ujungu ambapo wametoa Sh.999 Milioni karibu Bilioni moja na mkandarasi anaendelea na kazi, ujenzi wa barabara ya Kibaya, Luzurukulu hadi Kipuma ambayo inajengwa kwa Sh.624 Milioni.
"Hivi ndugu zangu kuna Rais kama Mama Samia ambaye ameweza kutoa hela nyingi kiasi hiki tena katika Tarafa ya Ndago tu na si Wilaya nzima ebu pigeni hesabu ninyi wenyewe" aliuliza Mwenda kwenye mkutano huo huku yakipigwa makofi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwenda alisema mambo hayo ya maendeleleo hayajafanyika katika kata hiyo pekee bali ni kata zote za wilaya hiyo ya Iramba na kuwa hayo ni baadhi tu kwani hajazungumzia ujenzi wa madarasa ya UVIKO na umeme.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba Ashery Samwel alisema wameridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo na aliwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza badala ya kuisubiri Serikali.
Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi katika wilaya hiyo ambapo aliwaomba wakandarasi kujenga miradi hiyo kwa viwango kulingana na fedha walizolipwa.
Aidha Msengi alitoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kujenga tabia ya kulipa ushuru wa mazao ili kusaidia wilaya hiyo kukusanya mapato yatakayosaidia kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Diwani wa Kata ya Ndago Ernest Kadege alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wao Dk. Mwigulu Nchemba kwa kufanikisha miradi hiyo katika Tarafa hiyo na jimbo zima la Iramba Magharibi.
Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza viongozi wote wa wilaya hiyo, wakuu wa idara kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kufanikisha miradi hiyo kutekelezwa miradi hiyo kwa uaminifu kwa ufanisi mkubwa.wakuu wa shule na viongozi waliosimamia fedha za kutekeleza miradi hiyo kwa uaminifu na kuifanikisha.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alifanikiwa kumaliza mgogoro wa barabara ya kutoka Mtekente kwenda Msansao na Ujungu uliotokana na baadhi ya wananchi kugomea isipite katika mashamba yao lakini baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara uliongozwa na Mwenda wakiwepo viongozi mbalimbali wananchi hao waliridhia barabara hiyo ipite katika eneo hilo baada ya kuomba wiki moja ya kuondoa mazao yao katika maeneo itakapo pita barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo yao.
WIZARA NA WADAU WA MICHEZO WAMPA TANO RAIS SAMIA
Na. John Mapepele
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirkiana na wadau wa mbalimbali wa michezo nchini leo Machi 29, 2022 wanaadhimisha kilele cha wiki ya Rais Samia ikiwa ni kampeni maalum ya kuelimisha umma, kujadili na kutafakari mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mwaka mmoja wa utendaji wake tangu aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19, mwaka jana.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ndiye Mgeni Rasmi atakayeongoza kongamano hilo la michezo katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Michezo.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa nane mchana na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo. Yusuph Singo Omary, wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi watatoa mada kwenye kongamano hilo.
Amewataja wadau wengine watakaowasilisha mada kuwa ni pamoja na Peter Sarungi ambaye ni Rais wa TAFF, Jackson Ndaweka ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha nchini, Salum Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na Amina Mfaume ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Kuogelea (TSA).
Aidha, amesema lengo la Kongamano hilo ni kuelezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwenye Sekta ya Michezo.
‘Kongamano hili tumeliratibu vizuri ili kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu Kipenzi, mama Samia Suluhu Hassan” ameongeza Mkurugenzi Omary.
Mkurugenzi Singo amesema baada ya kongamano hilo kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Sudan na Taifa Stars ambao utachezewa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka na wapenda michezo kujitokeza kushiriki kwenye kongamano hilo la aina yake na baadaye kwenye mechi dhidi ya Sudan na Taifa Stars ili kuja kujionea burudani na kuishangilia timu ya Taifa.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa
Ripoti ya kukabiliana na majanga ya asili yazinduliwa Arusha
Na Jane Edward, Arusha
Utafiti mdogo uliofanywa kwa jamii ya wafugaji wa asili wanaoishi katika vijiji vitano vya wilaya ya Simanjiro Mkoa Manyara kuhusu uwezo wa jamii hiyo kukabiliana na majanga yakiwemo yanayotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi umebaini kuwepo kwa njia nyingi za asili zenye kuleta matokea chanya kwa jamii hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika uzinduzi wa ripoti ya kukabiliana na majanga ya asili Wilayani Simanjiro, Afisa mifugo na uvuvi Dkt Swakeh Masaza amesema kwa sasa jamii ya kifugaji inakabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha ripoti ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa na shirika la Pingo's Forum kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la masuala ya maendeleo (OSIEA)ambapo imezinduliwa jijini Arusha huku njia moja wapo ya asili ikiwa ni ya wafugaji wa asili kuhama kwa ajili ya kuisalimisha mifugo
Ameongezea kuwa kwa sasa wafugaji wameanza kujikita kwenye kilimo na kuhama hama ili kutafuta sehemu yenye maji ya uhakika na malisho ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Gideon Sanago ni afisa mabadiliko ya tabia nchi Pingo's ambapo anasema jamii ya wafugaji hutumia utabiri wa asili ili kung'amua baadhi ya mambo lakini kwa sasa elimu hiyo ya maarifa ya asili inapotea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
"Uwepo wa wafugaji kuwa na tabia ya kuhama hama unasaidia kuacha nafasi ya hiyo sehemu hiyo kustawi na kutunza mazingira na inasaidia mfumo wa mazingira na ustawi kuendelea kustawi vizuri zaidi" Alisema
Amesema kuwa maeneo mengi yenye wafugaji wa asili yanatunzwa tofauti na wengine na kwamba ripoti hiyo ni kwaajili ya watunga Sera ili kuwezesha wao kuelewa na ikiwa tayari itaandikwa kwa lugha rahisi.
Kwa upande wake afisa jinsia kutoka Pingo's Forum Nailejileji tipap anasema ripoti hiyo itasaidia kupata taarifa ya kuitumia kila siku na kutoka nje zaidi ya Sayansi ambayo itatusaidia kupata maarifa mengine na kuyatumia kila siku.
Hata hivyo ripoti hiyo imefanyika toka mwaka jana na eneo la simanjiro katika vijiji vitano limechaguliwa kwa lengo la kuangalia namna wafugaji wa asili wanavyokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo mabadiliko hayo yamesababishwa na shughuli za kibinadamu zinazomsaidia meanadamu kujipatia kipato.
Aidha ili kuhakikisha kuwa njia hizo za asili zinaboreka na kuwa endelevu wataalamu wa sheria na mabadiliko ya tabia nchi wanashauri kuwepo kwa sera rafiki zinazomtambua mfugaji wa asili.
Wadau wa mabadiliko ya tabia nchi Wakishika ripoti ya kukabiliana na majanga ya asili kuashiria uzinduzi wa ripoti hiyo .
BENKI YA STANDARD CHARTERED NA VSO KUZINDUA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA AJIRA NA STADI ZA UJASIRIAMALI, MWANZA
BENKI ya Standard Chartered Tanzania imezindua mradi unaojulikana kama Kuimarisha Ujasiriamali na Ajira kwa Vijana (EYEE) ili kusaidia vijana mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Voluntary Service Overseas (VSO). Mradi huu unatolewa chini ya Futuremakers na Standard Chartered, mpango wa kimataifa wa Benki wa kukabiliana na ukosefu wa usawa.
Mradi wa EYEE unalenga kuwawezesha vijana, hususani wanawake na watu wenye ulemavu wa macho, ujuzi na maarifa ili kuanzisha biashara zao na kutambua fursa za kuajiriwa. Mradi pia utajikita katika kuimarisha mazingira wezeshi katika jamii kwa kutoa mafunzo ya uwezo, kuongeza uelewa, kulinda, na kuzingatia haki zao za kiuchumi.
Mradi huo wa miezi 11 utawanufaisha vijana 400 wa wilaya za Ilemela na Sengerema mkoani Mwanza. Vijana 400 watajumuisha wafanyabiashara vijana 80 wa Biashara Ndogo Ndogo na za Kati na vijana 320 kuajiriwa na wamiliki wa biashara. Asilimia 5 ya Vijana 400 watakuwa watu wenye ulemavu wa kuona na 60% ya Vijana watakuwa wanawake.
Mradi huo pia utatolewa kwa ushirikiano na washirika wa utekelezaji wa ndani kama vile Randstad, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC).
Hafla ya uzinduzi iliongozwa na Mhe. Neema Kipeja, Afisa Tawala wa Wilaya ya Ilemela aliyemwakilisha Mhe. Eng. Robert Gabriel Luhumbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo wanufaika wa mradi huo (vijana) pamoja na wawakilishi wa sekta binafsi na umma.
Bi. Desideria Mwegelo, Mkuu wa Masuala ya Biashara, Chapa na Masoko katika Benki ya Standard Chartered alitoa maoni, “Kukosekana kwa usawa wa kijamii na kiuchumi, na kuongezeka kwa pengo la mapato ndani na kati ya nchi, ni changamoto inayokabili kote ulimwenguni. Takriban watu milioni 97 zaidi wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku kwa sababu ya janga hili. Kufikia 2030, inakadiriwa kuwa asilimia moja ya watu duniani watamiliki theluthi mbili ya utajiri wake. Tunaamini kila mtu anapaswa kuchangia, na kufaidika na ukuaji endelevu wa uchumi katika jamii yake. Tunakuza ushirikishwaji mkubwa wa kiuchumi kupitia Futuremakers na Standard Chartered, mpango wetu wa kimataifa wa kukabiliana na ukosefu wa usawa. Futuremakers inasaidia vijana kutoka kaya za kipato cha chini, hasa wasichana na watu wenye ulemavu wa macho, kupitia programu za jumuiya zinazozingatia elimu, kuajiriwa, na ujasiriamali. Tunaamini mradi huu wa EYEE utawanufaisha vijana wa Mwanza”
Akizungumzia uzinduzi wa mradi wa EYEE, Bw. Frank Girabi, Kiongozi wa Utekelezaji wa Mpango wa Nchi katika Huduma ya Hiari Nje ya Nchi alibainisha kuwa mradi huo utawanufaisha vijana kupitia kuajiriwa na ujasiriamali. Kupitia uwezo wa kuajiriwa, mradi unalenga kuandaa utayari wa nguvu kazi kwa vijana wakiwemo watu wenye ulemavu wa macho kupitia mafunzo ya ufundi stadi, ukuzaji ujuzi pamoja na kuwaunganisha vijana kupata mafunzo ya kazi, uanagenzi, na kupata kazi zenye staha. Kupitia ujasiriamali, mradi unalenga kusaidia vijana kujihusisha na ujasiriamali, kukuza biashara zao, kuongeza mapato na kupata fursa za soko. Mradi huo pia utajikita katika kuwawezesha vijana kutenda kama viongozi na mifano ya kuigwa katika familia zao na jamii kwa kusaidia maendeleo ya mitandao ya vijana inayotambulika.
Mhe. Neema Kipeja, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilemela alisema, “Kulingana na utafiti ulioongozwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuhusu Utafiti Jumuishi wa Nguvu Kazi 2020/21 (ILFS) ulionyesha kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 – 35 imeongezeka kutoka 12.1% mwaka 2014 hadi 12.6% mwaka 2020/2021. Takwimu kama hizi ni ukumbusho kwetu wote kwamba tunahitaji kucjukumujukumu hili katika kukuza ujumuishaji wa kijamii na kiuchumi kwa vijana. Tayari Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kutoa ujuzi wa maarifa ili kurahisisha uwezo wa kuajiriwa pamoja na kutafuta njia za kutoa mikopo kwa vijana ili wajihusishe na ujasiriamali. Natambua msaada mkubwa wa Benki ya Standard Chartered katika kutekeleza mradi wa EYEE kwa ushirikiano na VSO, Randstad, SIDO, TCCIA na TWCC. Natoa wito kwa wadau wengine wa sekta binafsi kuungana na Serikali katika kusaidia vijana wetu kwa fursa za ujasiriamali na kuajirika.
Mradi wa EYEE ni mojawapo ya Mradi wa Futuremakers ambao unafanywa na Standard Chartered Foundation, msingi wa hisani ambao unakabiliana unazingatia usawa. Futuremakers ndio msingi wa maono yetu ya kuwa benki endelevu na inayowajibika zaidi ulimwenguni. Iko chini ya nguzo ya jumuiya ya mkakati wetu wa uendelevu na inalingana na Kusudi letu la kuendesha biashara na ustawi kupitia utofauti wetu wa kipekee na kuimarisha ahadi yetu ya kuwa Hapa kwa manufaa.
USHINDI MKUBWA KWENYE KASINO YA MERIDIANBET!!

*Mzungungo Mmoja, Umezalisha €152,835. Ushindi Bab-Kubwa.
Kwa muda mrefu sasa, unapoizungumzia Kasino ya Meridianbet, unazungumzia Jakipoti za Kasino na ushindi mkubwa! Kwa mwaka 2022 pekee, mpaka sasa kuna washindi wawili wametusua ushindi mkubwa!!
Mchezaji mwingine wa Kasino kupitia Meridianbet alijaribu bahati yake kupitia mchezo wa Crazy Time unaotengenezwa na kampuni ya Evolution. Gurudumu lenye maajabu ya kusaka pesa lilifanya kazi yake na mshindi kuibuka na kiasi kikubwa cha takribani €152,835!
Mwezi Machi unaendelea kuwa ni mwezi wa ushindi mnono kwenye Kasino ya Meridianbet, hakika, sifa yetu ya mabingwa wa dunia na watengenezaji wa jakipoti kubwa, inatendewa haki!
Mwezi Februari, Kasino ya Meridianbet ilitoa ushindi mkubwa wa jakipoti ya thamani ya €15,616 kupitia Sloti ya Secrets of Alchemy
Mwishoni mwa mwaka 2021, Kasino ya Meridianbet ilitoa jakipoti yenye thamani ya €1,129,692.15 kwenye mchezo wa sloti yaWild Crusade: Empire Treasures. Huu ni ushindi mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye soko la Ulaya.
Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
WAZIRI WA NCHI BALOZI. DKT. PINDI AONGOZA KIKAO CHA BAJETI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao cha kujadili Bajeti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika (DCEA) kaika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akifafanua jambo wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya (wa kwanza kulia) akieleza jambo katika kikao hicho na (katikati) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana na anayefuata ni Naibu Waziri wake Mhe. Mhe. Ummy Nderiananga kikao kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Gerald Kusaya akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria kikao cha kujadili Bajeti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wakifuatilia kikao hicho katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
(SERA, BUNGE NA URATIBU)
Benki ya CRDB yasaini mkataba wenye thamani ya Sh. Bilioni 182 na Proparco kuwezesha wajasiriamali nchini

WAFANYABIASAHARA SITA WAFARIKI NA WENGINE SABA WAJERUHIWA KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA WILAYANI HANDENI
Na Mwandishi Wetu, Lushoto
WAFANYABIASHARA 6 waliokua wakiwahi gulio wilayani Handeni, wamefariki dunia papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Fuso walilokuwa wakisafiria kuacha njia alfajiri ya jana na kupinduka katika korongo katika barabara ya Soni-Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Ajali hiyo ilihusisha Fuso hiyo yenye namba za usajili T 239 AFD lililokuwa limebeba watu pamoja na bidhaa zao kama nyanya, vitunguu, makabichi, Matunda aina ya Peasi na nyombo vya nyumbani, kupinduka baada ya kufeli breki.
Mashuhuda wa ajali hiyo iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, ACP Safia Jongo wanasema Fuso lilishindwa kupunguza mwendo kwenye mteremko mkali wa eneo la Kijiji Cha Nyasa baada ya breki zake kufeli na hivyo kutumbukia kwenye korongo lenye mteremko mkali kwa chini kiasi cha mita 150 za mraba.
Akizungumza kwa simu kutokea kwenye eneo la ajali Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo alisema taarifa za awali ziliomesha watu 4 ndio waliopoteza maisha papo hapo kwenye ajali na baadaye watu wengine wawili walifariki wakikimbizwa kituo Cha Afya kilichopo Mombo wilayani Korogwe.
"Waliotutoka mwanzoni tukipata taarifa, walikuwa wanne, wakaongezeka majeruhi wawili na jumla kufikia 6 ambapo kati yao waliofariki wanaume ni 4 na wanawake ni wawili, "alisema Kamanda Jongo.
Kamanda aliwataja watu waliofariki, kuwa Juma Mustafa Mohamed mkazi wa Handeni, Mwajuma Hatibu mkazi wa Handeni, Jumanne Adam mkazi wa Soni, Mohamed Said Makakala mkazi wa Handeni mjini, Zaina Ramadhani mkazi wa Handeni Kwa mkono, huku mtu wa 6 akiwa bado hajajulikana jina lake.
Aliwataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Rumisha Zuberi Msagati mkazi wa Bumbuli wena, Rasuli Said Makalala mkazi wa Handeni Komwale, Mussa Enock Kajia mkazi wa Lukozi mjini, Amina Zuberi Mhina mkazi wa Handeni, Mwajabu Mrisho Mpulizi mkazi wa Handeni Chogo na Mama Latifa mkazi wa Handeni.
AU Member states urged to enhance sustainable fishing
By Mbaraka Kambona,
The Deputy Minister For Livestock And Fisheries, Tanzania, Hon. Abdallah Ulega has asked the AU Member states to continue enhancing sustainable fishing because the sector plays an important socio-economic role in building national economies through income generation, employment and food security thus supporting multitude of livelihoods.
Hon. Ulega made the remarks on 28 March, 2022, when officiating the Consultative Meeting “To Support AU Members States Involvement, Compliance With Global Instruments And Promote Their Use By AU Member States” held in Dar Es Salaam, Tanzania.
“We are all aware that there is an ever-increasing demand for fish and fisheries products over the past decade. Trade in fish and fishery products now constitute the most highly traded food commodities internationally, leading to increase in demand which have some negative impacts on the fishing ecosystems and environment as well as declining fish stocks. We are therefore facing common challenges in fisheries management such as overfished stocks, illegal, unreported and unregulated (IUU) fishing, inadequate benefits from trade in fish and fish products, therefore, we need to be careful on how we meet this demand to enable us have sustainable fisheries industry in Africa”, insisted Hon. Ulega.
But, according to him, the implementation of the Policy Framework and Reform Strategy for Fisheries and Aquaculture in Africa and the African Fisheries Reform Mechanism will go a long way in helping AU member states to address some of those challenges and bring the sector to the reform path.
“Tanzania is committed to the conservation of our fisheries resources and sustainable development of aquaculture. My Ministry is working closely with the key players in the fisheries sector, including fishers, aqua farmers, fish processors and exporters, regional fisheries management bodies, relevant regional multilateral environment agreements, the private sector and the development partners to bring about reforms and improved governance of the fisheries sector with a view to increasing socio-economic benefits and stock sustainability”, he added
Moreover, he congratulated the African Union for spearheading the development of the Policy Framework and Reform Strategy for Fisheries and Aquaculture in Africa (PFRS) as well as the African Fisheries Reform Mechanism (AFRM) and their proactive leadership in the implementation of the Fisheries Governance Projects (FISHGOV) in Africa saying that the PFRS and the AFRM through the FISHGOV projects have provided the much needed guidance to the African Union Member States in the actualization of the Malabo Declaration on Accelerated Agricultural Growth and Transformation for Shared Prosperity and Improved Livelihoods.
The Director of AU-IBAR, Dr Nick Nwankpa said that the overall purpose of the meeting was in line with the activities as provided for by the FishGov 2 project and he therefore encouraged the participants to analyse the possibility for the programme to focus at key issues affecting all African countries and particularly prioritise a strategy to increase the rate of adoption, domestication and implementation of those Global Instruments as a gateway to tackle key challenges and constraints affecting the growth of the fisheries and aquaculture sector.
“Our attention should be on enhancing partnerships, participation in high seas fisheries, market access and integration, equitable investments, sustainable fisheries and resources exploitation and illegal fishing which result in depletion of the fisheries resources and loss of income amounting to billions of dollars for the continent”, Dr Nwankpa elaborated
Deputy Minister for Livestock and Fisheries, Tanzania, Hon. Abdallah Ulega (Centre) pose in group photo with participants of The Consultative Meeting To Support AU Members States Involvement, Compliance With Global Instruments And Promote Their Use By AU Member States held in Dar Es Salaam, Tanzania From March 28 – 30, 2022. Third from left is Dr. Mohamed Seisay, Senior Fisheries Officer, Inerafrican Bureau for Animal Resources (IBAR).
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI WORLD GOVERNMENT SUMMIT DUBAI MACHI 29

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa North Hall kushiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 akishiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
…………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo ambapo
Pamoja na mambo mengine lina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana mbinu za kuimarisha utendaji wa serikali.
Katika Ufunguzi wa Jukwaa hilo viongozi wakuu wa serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na sekta binafsi kutoka nchi mbalimbali wamekutana na kujadili namna bora ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za serikali kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali kupitia utafiti kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani.
Hapo kesho tarehe 30 Machi 2022 Makamu wa Rais Dkt. Mpango anatarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo akichangia mada ya “kwanini Afrika imekua ni muhimu sana kwa wakati huu katika uchumi wa dunia”
NAMTUMBO KUMWAGIWA MABILIONI FEDHA ZA MRADI WA HEWA UKAA
NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Akitoa taarifa ya mradi wa hewa ukaa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa waheshimiwa madiwani ,wadau wa maendeleo na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo afisa wanyama pori na misitu wa halmashauri ya wilaya hiyo Prisca Msuha alisema mradi wa hewa ukaa utaifanya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kumwagiwa mabilioni ya fedha wakati mradi utakapoanza kazi.
Priska katika taarifa yake alidai mradi wa hewa ukaa utatekelezwa katika vijiji vinavyopatikana katika jumuiya za uhifadhi za wanyamapori za kimbanda,kisungule na Mbarang”andu zilizopo katika kata za Kitanda,Mgombasi,Ligera,
Priska alisisitiza idara yake kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi TAWA,TANAPA,na TFS walishatoa mafunzo kwa viongozi wa vijiji, watendaji wa vijiji ,kata na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ngazi ya kata na vijiji kuhusu mpango wa hewa ukaa .
Aidha Priska alifafanua lengo la mpango wa hewa ukaa ni kuzinufaisha jamii inayotunza misitu ambayo hewa yake kutoka katika misitu hiyo ndiyo inayosaidia kunyonya hewa chafu inayozalishwa katika viwanda vikubwa duniani ili waendelee kulinda na kupanda miti katika mazingira yao .
Diwani wa kata ya Likuyuseka Kassim Gunda alisisitiza kuwepo kwa uwazi katika kutekeleza mpango huo na kuagiza idara inayohusika kushirikisha jamii moja kwa moja ili kuepuka sintofahamu ambayo inaweza kutokea kama jamii ambayo ndiyo yenye maeneo ya uhifadhi kutofahamu vizuri juu ya mpango huo.
Diwani huyo alidai ushirikishwaji wa jamii katika kutekeleza mpango huo upewe kipaumbele kwani jamii ndio inayotakiwa kupatiwa elimu zaidi kutokana na maeneo ya uhifadhi hayo yapo katika vijiji ambapo jamii hiyo ndiyo ipo ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kujitokeza hapo baadae alisema diwani huyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Jumma Pandu aliwasisitizia waheshimiwa madiwani kwenda kuelimisha jamii katika maeneo yanayoenda kutekeleza mradi huo kuelimisha jamii umuhimu wa mradi huo kwa jamii,halmashauri na serikali kwa ujumla.
Pandu aliwataka madiwani kwenda kuwaelekeza wananchi matumizi ya maeneo na kuzingatia kutochanganya matumizi ya maeneo na kwenda kuwasisitizia wananchi kutumia maeneo kama yalivyopangwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi yao.
Nchini Tanzania mradi wa hewa ukaa unatekelezwa katika wilaya za Kiteto,Tanganyika ,karatu na Makame ambapo kwa wilaya ya Tanganyika yenye lenye eneo la msitu wa kilomita 2500 hunufaika na shilingi 3,000,000,000 kwa mwaka.
RAIS SAMIA AMTEUA ACI.HASSAN ALI HASSAN KUWA KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR
BENKI KUU YA ETHIOPIA NA SAFARICOM ETHIOPIA WAJIFUNZA NAMNA HUDUMA ZA KIFEDHA ZA M-PESA ZA VODACOM ZINAVYOFANYA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.

Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni akiwaelimisha maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.

Meneja Uendeshaji kituo cha huduma kwa wateja Vodacom Tanzania, Deogratius Massawe akiwaelezea maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna kituo hicho kinavyofanya kazi za kuweka usalama na kutunza taarifa za wateja wao

Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima akiwa kwenye kituo cha mafuta kwa ajili ya kuwaonesha maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna ambavyo wateja wanaweza kulipia kwa kutumia huduma ya “Lipa kwa simu” ikiwa ni sehemu ya kuwaonesha namna huduma ya kulipa kidijitali kupitia M-Pesa inavyofanya kazi.