


SERIKALI imeahidi kuchukua hatua kali kwa mfanyabiashara yoyote atakaebainika kupandisha bei za bidhaa au huduma kwa utashi ama tamaa bila ya kuwepo sababu ya msingi kwani tayari imeshatoa bei elekezi za bidhaa muhimu za chakula.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema hayo leo katika risala yake aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka huu 2021 Miladia sawa na mwaka 1442 Hijria.
Katika risala yake hiyo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kwamba kwa pamoja ni vyema wananchi wenye kipato cha chini wakafikiriwa hasa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo mahitaji ya familia yanaongezeka.
Alisisitiza kwamba kwa msingi huo huo, wafanyabiashara wa bidhaa zote zikiwemo za nguo ni vyema wakazingatia uwezo wa wananchi kwani kuwakatia nguo watoto katika kipindi hichi kwa ajili ya Sikukuu ni sehemu ya utamaduni wa wananchi wote wa Zanzibar.
Aliongeza kuwa inafurahisha kuona kwamba licha ya kuwepo kwa changamoto za usafirishaji na upatikanaji wa biadhaa mbali mbali, shughuli za biashara na upatikanaji wa chakula hapa nchini zinaenda vizuri ambapo bidhaa zote muhimu zinapatikana wakati huu mwezi wa Ramadhani ukikaribishwa.
Alhaj Dk. Mwinyi alisema kuwa taarifa za Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo inatoa matumaini ya kuwepo kwa chakula cha kutosha yakiwemo mazao ya muhogo na ndizi ambayo hutumiwa na wananchi wengi kwa futari katika mwezi wa Ramadhani.
Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kuwa mnamo Machi 04 2021 alikutana na wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza chakula na kuwataka washirikiane na Serikali kufanya maandalizi mazuri katika kuhakikisha kwamba bidhaa zote hasa za chakula kwa wananchi wa Zanzibar ziweze kupatikana katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani na baada ya hapo.
Alhaj Dk. Mwinyi alieleza kwamba kwa hakika ibada ya Saumu ina mchango mkubwa katika kuimarisha uchamungu, jambo ambalo ni jema na linaleta manufaa hapa Duniani na kesho Akhera.
“Kwa hivyo, tuukaribishe Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa furaha na matumaini na tujiandae kunufaika kutokana na neema na fadhila mbali mbali zilizo katika kipindi chote cha Mwezi huu tunaoukaribisha”, alisema Alhaj Dk. Mwinyi.
Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Mwinyi aliwaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuhimizana kutekeleza ibada za Faradhi sambamba na kukithirisha ibada za Sunna ili kupata radhi za Mola ambapo miongoni mwa ibada iliyosisitizwa zaidi kufanywa kwa wingi katika mwezi wa Ramadhani ni kusoma Qur-an tukufu.
Alieleza kwamba katika kutafuta fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imehimizwa kujitahidi sana kutekeleza ibada ya sala zote za Faradhi na sala za Sunna, kuomba dua, kusoma nyiradi mbali mbali, kufanya itikafu, na kutekeleza Sunna nyengine zinazoambatana na Mwezi wa Ramadhani.
Aliongeza kwamba jambo jengine linalohimizwa kutekeleza zaidi ndani ya Mwezi wa Ramadhani ni kutoa sadaka hasa kwa watu wenye mahitaji, Mayatima, Wazee, Masikini na Mafakiri ibada ambayo inaongeza baraka na mahusiano mema katika jamii.
Alhaj Dk. Mwinyi pia, alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi pamoja na viongozi na Watumishi wa Manispaa zote nchini juu ya umuhimu wa kuzingatia usafi katika miji hasa katika masoko na maeneo yanayohusika na uuzaji wa vyakula ili kujiepusha na maradhi ya mripuko.
Kadhalika, aliwahimiza viongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi hasa katika maeneo ambayo huduma hiyo haipatikani kwa uhakika.
Aliwataka Masheha wa Shehia ambazo zina matatizo ya maji wawasiliane na (ZAWA) ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa zikiwemo kuwapelekea wananchi magari ya maji kwa lengo la kuondokana na usumbufu wa kupata huduma hiyo.
Sambamba na hayo, Alhaj Dk. Mwinyi aliwahimiza viongozi wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani pamoja na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanasimamia ipasavyo sheria za usalama barabarani wakati wote na kuongeza nguvu hasa katika kipindi hiki ambacho mahitaji ya usafiri huongezeka.
Aliwataka kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva watakaojaribu kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kwenda mwendo wa kasi pamoja na wale wenye tabia ya kuwasumbua wananchi kwa kuwashusha bila ya kuwafikisha mwisho wa vituo vilivyopangwa na Serikali.
Hata hivyo, Alhaj Dk. Mwinyi aliwakumbusha wananchi wenye dharura maalum na wale wasiokuwa Waislamu waendeleze utamaduni wa kujizuia kula hadharani, kutovaa nguo zisizoendana na maadili ya Kizanzibari sambamba na kuepuka matendo yatakayowakwaza Waislamu wenye kutekeleza ibada ya funga.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Afisa Tarafa Kata ya Ikungi mkoani Singida, Yahaya Njiku , akihutubia kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo wakati akizungumza na Vijana Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha
5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
AFISA Tarafa Kata ya Ikungi mkoani hapa Yahaya Njiku amewataka vijana wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) waliohitimu kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Ikungi kuwa wazalendo wa nchi yetu.
Njiku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo aliyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi hao katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha 5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.
"Mnapaswa kuwa wazalendo na uzalendo unatafusiri nyingi kwanza unapaswa kuipenda nchi yetu kuifahamu kuithamini na kuitunza." alisema Njiku.
Alisema wakiwa kama vijana wanaohitimu kidato cha sita na wale ambao wanaendelea na masomo ni lazima kwanza wawe wazalendo.
Alisema sisi tupo katika Taifa la Tanzania hatuna lingine zaidi ya Tanzania hivyo tunapaswa kulitunza na kulitetea popote pale duniani.
Njiku aliwaambia vijana hao kuwa uzalendo unatakiwa kuuanza wakiwa na umri mdogo na kuwa hawawezi kuwa wazalendo pasipo kulielewa taifa lao kuanzia historia yake, misingi na jinsi lilivyopatikana.
"Niwaombe ninyi wahitimu na nyie mnaoendelea na masomo ni lazima mfahamu historia ya taifa letu kwani leo hii mpo hapa mna furaha kwa kucheza muziki, michezo mbalimbali na kubadilishana mawazo kuna watu waliteseka kuliangaikia taifa letu akiwepo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere na wenzake.
Alisema ni muhimu kwa vijana hao kusoma masomo ya uraia ili waweze kulielewa taifa lao kwani wakilielewa wataweza kulitetea.
Katika hatua nyingine Njiku aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wa kuhamasisha amani hapa nchini na kuwaombea viongozi wetu hasa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliapishwa hivi karibuni kuongoza nchi baada ya aliyekuwa Rais wetu Dkt.John Magufuli kufariki.
Aliwataka wahitimu hao kuendelea kumuomba Mungu ili waweze kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu kwani kumaliza kidato cha 5-6 sio mwisho wa kusoma.
"Nyinyi wanafunzi mnakila sababu ya kuendelea na masomo kwani Serikali kupitia Rais wetu Mama Samia Suluhu imeweka mazingira bora ya kusoma kwa kutoa elimu bure." alisema Njiku.
Aidha Njiku aliwaambia wahitimu hao kuwa nidhamu na uwajibikaji ni jambo jema litakaloweza kuwafanya waishi vizuri wakiwa shuleni, nyumbani na jamii na bila kuacha kumuomba Mungu ambaye siku zote hawezi kumuacha mtu amuombaye.
Njiku aliwataka vijana hao kuto jiingiza katika vitendo visivyo na maadili badala yake watumie muda wao kwa kujisomea na kuendeleza vipaji vyao vya michezo walivyonavyo na kuwapa heshima wazazi wao wanao wasomesha kwa kufanya vizuri mitihani yao.
Wahitimu hao 19 katika risala yao kwa mgeni rasmi walitaja baadhi ya mafanikio waliyopata wakiwa shuleni ni kushiriki katika kuchangia ujenzi wa parokia ya mtakatifu Rita wa Kashia wilayani humo.
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWANASIASA Maarufu nchini Mexico Carlos Mayorga ameingia katika mijadala mbalimbali baada ya kuzindua kampeni zake za Ubunge akiwa ndani ya jeneza France24 imeripoti.
Carlos Mayorga alitumia njia hiyo kuonesha hali halisi ya taifa hilo ambalo mamia ya watu wanakufa kutokana na virusi vya Corona pamoja na vurugu zinazohusiana na biashara.
Akiwa mgombea kutoka chama cha Encuentro Salidario kusini mwa jimbo la Chihuahua Mayorga alisema, alifikia uamuzi huo kwa malengo ya kufikisha ujumbe kwa wanasiasa ambao wanasababisha watu kupoteza maisha kutokana na kutojali kwao.
Mwanasiasa huyo aliwasili katika kampeni zake katika daraja linalotengenesha mji wa wa Ciudad Juarezy na El Paso Texas akiwa ndani ya jeneza la rangi ya fedha.
Carlos Mayorga aliambatana na wasaidizi waliovaa mavazi na vifaa vya kujilinda wakiwa na mashada ya maua kama ishara ya kupaza sauti juu ya janga hilo ambapo hadi sasa watu 200,000 wamefariki nchini humo kutokana na Covid-19.
Vyombo vya habari vilimnukuu mwanasiasa huyo akisema;
"Wanasiasa wameendelea kukaa kimya wakati matukio ya uhalifu yakiendelea, na wameendelea kukaa kimya kuhusu hali mbaya ya Covid-19." Alinukuliwa.
Zaidi ya watu 300,000 wameuawa nchini Mexico tangu Serikali itoe nguvu kwa jeshi katika kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya 2006 kwa mujibu kwa taarifa rasmi.
***************************
Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam.
Klabu ya Taliss –IST imenyakuwa ubingwa wa Taifa wa mashindano ya kuogelea baada ya kukusanya pointi nyingi zaidi ya klabu nyingine tano zilizoshiriki katika mashindano hayo.
Klabu hiyo imepata jumla ya pointi 1, 826 ambapo pointi 586 zilikusanywa kwa upande wa wanawake na pointi 1, 160 zilikusanywa kwa upande wa wanaume.
Huu ni ubingwa wa tatu mfululizo kwa klabu hiyo tokea mwaka 2018. Mwaka 2019 pia ilitwaa ubingwa huo na mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona.
Meneja wa klabu hiyo Hadija Shebe alisema kuwa moyo wa kujituma, mafunzo mazuri na ushirikiano baina ya shule, klabu na wazazi ndiyo nguzo pekee ya kupata mafanikio katika mashindano hayo yaliyoshirikisha waogeleaji zaidi ya 90.
“Waogeleaji wetu wamefanya vizuri sana na wanahitaji pongezi, tunajivunia kwa mafanikio haya, ni makubwa kwa upande wa klabu hasa baada ya kuunganika na shule,” alisema Hadija.
Klabu ya Bluefins ya jijini ilishika nafasi ya pili kwa kupata pointi 1,748 baada ya kupata pointi 818 kwa upande wa wavulana na pointi 862 kwa wasichana.
Muasisi na kocha wa klabu hiyo, Rahim Alidina, aliwapongeza waogeleaji wote, makocha na wazazi kwa ushirikiano na kuifanya klabu yao kumaliza katika nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Klabu ya Dar es Salaam (DSC) ambayo ilipata pointi 1,486 ambapo kwa upande wa wanaume walipata pointi 888 na pointi 538 zilikuwa kwa wanawake huku nafasi ya nne ikienda kwa Mwanza kwa kupata pointi 904 na kufuatiwa na FK Blue Marlins katika nafasi ya tano kwa kupata pointi 578 na Mis Piranhas wakishika nafasi ya sita kwa kupata pointi 410.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro alisema mashindano hayo yamefanikiwa na waogeleaji kuleta ushindani mkubwa.
Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania leo Jumatatu tarehe 12 Aprili, 2021 limepitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26.
Mpango huo utakaogharimu zaidi ya shilingi trilioni 114.8 umepangwa kutekeleza maeneo makuu matano ya kipaumbele, ikiwemo kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma.
Vipaumbele vingine ni kukuza uwekezaji na biashara, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.
" Tutahakikisha kwamba miradi yote ya kimkakati iliyoainishwa kwenye Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano itatekelezwa kama ilivyopangwa", alisema Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akihitimisha mjadala kuhusu Mpango huo Bungeni jijini Dodoma.
Shabaha ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26 ni pamoja na kupandisha kiwango cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 6.0 ya mwaka 2021 hadi kufikia wastani wa asilimia 8.0 itakapofika mwaka 2026.
Aidha mfumuko wa bei umebashiriwa kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja kwa wastani wa asilimia kati ya 3.0 hadi 5.0 katika kipindi cha muda wa kati na akiba za kigeni kukidhi mahitaji ya uagizaji wa huduma na bidhaa kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.
Malengo mengine ni kuhakikisha kuwa mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka kutoka asilimia 15.9 ya pato la Taifa mwaka 2021/22 hadi asilimia 16.8 itakapofika mwaka 2026 na sekta binafsi inatarajiwa kuzalisha ajira mpya zipatazo milioni nane kati ya Julai 2021 na Juni 2026.
Miongoni mwa viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, waliohudhuria uhitimishaji wa mjadala huo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ni Naibu wake Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) pamoja na Manaibu Katibu Mkuu Bi. Amina Khamis Shaaban na Bw. Adolf Ndunguru na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akihitimisha hoja za Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akihitimisha hoja za Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akifafanua hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kuchangia kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) wakifuatilia michango mbalimbali iliyotolewa na wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) muda mfupi baada ya kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Wabunge wakishangilia wakati wa kuhitimisha hoja kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, uliowasilishwa juma lililopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), bungeni jijini Dodoma.
Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Bw. Adolf Ndunguru (kulia) wakiwa na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo wakifuatilia michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(kushoto) na Naibu wake, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb)(kilia) wakitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) wakiteta jambo na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo baada ya Bunge kupitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, wakiwa nje ya viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM)
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Tanzania, Raymond Komanga (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Zakaria Muyengi (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Zakaria Muyengi akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Tanzania, Raymond Komanga ( kushoto ) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
……………………………………………………………………………
Jukwaa la kidijitali linalowezesha upatikanaji wa huduma za bima kwa urahisi zaidi na za bei nafuu kwa kushirikiana na kampuni ya Britam Tanzania.
Tarehe 12 Aprili 2021. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza ya Teknolojia na Mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania leo imetangaza kuzindua ‘VodaBima’ – huduma ya kidijitali itakayowapa wateja huduma ya bima kupitia M-Pesa na hivyo kuchochea matumizi ya huduma za bima kwa Watanzania kwa kutumia huduma hiyo kwa njia ya kidijitali.
Kulingana na ripoti ya Finscope 2013, matumizi ya Bima nchini ilikuwa asilimia 13.0 ikiwa imeongezeka kutoka kutoka asilimia 6.8 2009. Pamoja na ukuaji huu, bima bado ni moja ya huduma za kifedha ambazo hazitumiki sana nchini. Sababu tofauti zinatajwa ikiwa ni pamoja na mwamko mdogo, kutokuaminika kwa huduma na vikwazo vya kupata huduma. Kama kampuni ya teknolojia iliyo na maono ya kuibadilisha Tanzania na kubadilisha maisha kupitia teknolojia, Vodacom inapenda kuziba pengo hili kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litarahisisha upatikanaji wa bidhaa za Bima.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni alisema kuwa VodaBima ni nyongeza mpya kwa jalada la M-Pesa la bidhaa na huduma zote zinalenga kufanya ujumuishaji wa kidijitali nchini Tanzania uwe wa kweli.
“Kwa miaka 13 sasa, Vodacom M-Pesa imekuwa kichocheo muhimu katika ukuaji wa ujumuishaji wa kifedha nchini na kila wakati tunatafuta njia mpya za kushinikiza uchumi jumuishi wa kidijitali. Vodacom inakusudia kuziba pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za Bima.
VodaBima huwapa wateja fursa ya kujiwekea akiba ya Bima bila malipo katika mkoba wao wa VodaBima kwa mwaka mzima. Jukwaa la VodaBima litatuma taarifa za kumbukumbu kupitia SMS wakati Bima ya gari yako inakaribia kuisha.
Bwana Mbeteni ameongeza kuwa bidhaa hiyo mpya italeta huduma za bima karibu na wateja na kuongeza urahisi na upatikanaji wa huduma hiyo. Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuza sekta ya bima nchini kwa ujumla. VODABIMA inatumia miundombinu bora ya teknolojia ya M-Pesa na mtandao mpana wa Vodacom ambayo inapatikana katika maduka Vodacom nchini kote kuhakikisha usalama, urahisi wa upatikanaji wa huduma za bima.
“VodaBima ni huduma ya kwanza ya aina yake sokoni, huduma hii inarahisisha upatikanaji wa huduma za bima pamoja na mfumo wa kufanya madai. Kwa sasa tunatoa bima ya gari lakini tunapanga kuleta bidhaa zingine ili kukidhi mahitaji ya wateja na kwenda sambamba na mabadiliko ya soko,” alisema Mbeteni.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania – TIRA, Zacharia Muyengi alisema kuwa kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za bima kupitia simu za mkononi kutawanufaisha wateja zaidi kwani sasa watafahamu kwa kina huduma mbalimbali za bima zinazotolewa sokoni.
“Tunafanya kazi kukuza na kudumisha soko la bima linalojumuisha, lenye ufanisi, la haki na salama kwa faida na ulinzi wa wamiliki wa sera. Tunakaribisha matumizi ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na ubunifu wa bidhaa ili kuleta huduma hizi karibu na watu. Uzinduzi wa VodaBima ni hatua inayoelekea kuboresha huduma ya bima nchini,” alifafanua Muyengi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Britam Tanzania Raymond Komanga ambao wanashirikiana na Vodacom kusambaza huduma ya bima kupitia teknolojia ya kidijitali alisema kuwa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya simu katika kupata bima ni hatua itakayofanya huduma hiyo ipatikane kwa watu wengi zaidi. Aliongeza kwamba huduma hiyo itasaidia kuhamasisha watu wengi zaidi kutumia huduma ya bima na kukuza sekta hiyo kwa ujumla.
“Huduma ya VodaBima ni ya kimapinduzi kwa sababu italeta urahisi kwa wateja kupata huduma za bima kutoka kwa watoa huduma. Wateja hawatalazimika kutembelea kampuni za bima kwani wanaweza kupata huduma hiyo kupitia simu zao za mkononi,” alisema Komanga huku akiongeza kwamba jamii itaelimika zaidi juu ya bidhaa na manufaa ya utumiaji wa huduma za bima.
Uzinduzi wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji kupitia teknolojia ya kidijitali ya kampuni ya Vodacom na hatua nyingine zaidi katika kuleta huduma karibu na wateja kupitia ubunifu na teknolojia ya mawasiliano kupitia simu za mkononi.
“Tunataka wateja wetu wapate huduma ya bima iliyoimarishwa pande zote. VodaBima ni bidhaa ya ziada ambayo inaweza kupatikana kupitia zana (App) mpya ya M-Pesa ambapo wateja wanaweza kupata bidhaa zingine kama huduma za mikopo na akiba kama Songesha na M-Pawa,” alihitimisha Mbeteni.
Uzinduzi wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji kupitia teknolojia ya kidijitali ya kampuni ya Vodacom katika kuleta huduma karibu na wateja kupitia ubunifu na teknolojia ya mawasiliano kupitia simu za mkononi.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Maulid Mwatawala (wa kwanza kulia) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika Chuoni hapo mwezi huu mwishoni kulia kwake ni Prof. Samweli Kaboto Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho hayo Prof. Samweli Kabote ( Wa kwanza kushoto) akizungumzia maandalizi hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na waandishi wa habari. Katikati ni Prof. Maulid Mwatawala Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Mariam Mwayela.Wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano na Masoko wa SUA.
Na Calvin Gwabara, Morogoro.
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeahidi kunedelea kuenzi mchango wa AliyekuwaWaziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine kutokana na ushupavu wake kama kiongozi katika kusimamia uchapakazi, Kilimo vijijini, Uzalendo na kuchukia rushwa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala wakati akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo juu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe Sokoine kwa mwaka 2021.
“Chuo kiliamua kutekeleza maamuzi ya kuadhimisha siku hii kuanzia mwaka 1992 kwa kuwa kiongozi huyu alikuwa mchapa kazi na alipigania ,masuala ya kilimo hasa katika mapinduzi vijijini na utoshelevu wa chakula kwa watanzania” Alisisitiza Prof. Mwatawala.
Prof.Mwatawala aliongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake Hayati Sokoine alipiga vita suala la rushwa na kuimarisha uadilifu katika utumishi wa umma ambapo serikali iliyopomadarakani inayazingatia na kuyaenzi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.
Kaimu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo alibainisha kuwa maadhimisho hayo kwa mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 24-27 Mei, 2021 chuoni hapo baada ya kuhairishwa hapo awali kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John PombeMagufuli.
Aidha alisema mambo yatakayofanyika katika wiki hiyo ya maonesho yateknolojia na ubunifu katika Kilimo, Ufugaji naUvuvi, kufanya mkutano wakisayansi kwa wanataaluma, watafiti, wanafunzi na wadau mbalimbalii, mdahalo wa kitaifa wa kumbukizi yaSokoineutakaofanyika siku ya tarehe 27 Mei 2021, kutoa huduma za afya kwa binadamu hususani magonjwa yasiyo ambukiza, kutoa huduma za tiba ya mifugo
kupitia hospitali ya rufaa ya wanyama bure kwa jamii, kuchangia damu salama na kufanya michezo mbalimbali ambayo itaambatana na zawadi kwawashindi..
Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 46 katikaMkoa wa Morogoro akitokea Dodoma katika kikao cha Bunge na katika kipindi chake cha uongozi alihudumu kwa vipindi viwili.
“Kwa mwaka huu 2021 itakuwa ni maadhimisho ya 17 kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine toka kumbukizi ya kwanza mnamo mwaka 1992 ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka Chuoni ” alisema prof. Mwatawala.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kumbukizi ya hayati Edward Sokoine Moringe Prof. Samweli Kabote kutoka SUA alisema kuwa huwezi kuongea historiaya Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA bila kumtaja Hayati Sokoine kwasababu Chuo kimebeba jina lake.
Wiki ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo, Teknolojia za kilimo, kuzalisha kwa tija na ushindani katika Soko, Kuelekea Nchi ya Uchumi wa juu wa Kati.
Na Amiri Kilagalila, Njombe
Na Woinde Shizza , Michuzi TV-ARUSHA
Malezi bora katika familia ndiyo msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wametakiwa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto wao ndani ya familia na jamii kwa jumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jelly Murro wakati akizindua account ya mtoto ijulikanayo kama [Junior Jumbo account] kutoka CRDB ambapo alisema wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na wawe na utaratibu wa kuwawekea akiba ya pesa kwa ajili ya maisha yao ya badae ili iweze kuwasaidia katika masomo yao na itawajengea maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, kujithamini.
Muro alisema wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu, uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.
“unapo muwekea mtoto akiba yake katika benki kwanza inakusaidia wewe mzazi kuwa na uhakikia wa kulipa ada kwa muda wowote pia ,mnajua kabisa wazazi mtoto unaporudishwa rudishwa ada unamuathiri kisaikolojia kwani atapata mawazo mengi ambayo yatampelekea hata kushidwa kufanya vizuri darasani”alisema Muro
Kwa upande wake Neema Njau ambae ni mzazi alisema kuwawekea watoto na vijana akiba ni utaratibu mzuri wa kuweza kuwasadia katika kujiendeleza kielimu na kujenga taifa lenye maadili na upendo.
Kwa upande wake meneja biashara wa kanda David Peter alisema kuwa wanatambua wateja wao wana malengo ambayo wamejiwekea katika maisha yao, na wao kama Benki ya kizalendo wana jukumu la kuhakikisha wateja wanafikia malengo yao kupitia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki ikiwemo huduma ya kuweka akiba kupitia akaunti mbalimbali kama vile akaunti hii ya Junior Jumbo account.
Alisema wanaendelea kuboresha huduma na miundombinu yake ya kutoa huduma hususani ile ya kidijitali, ambapo aliwataka wateja kuwafungulia watoto wao akaunti hii kwani ni mkombozi mkubwa sana kwa mtoto na nimsaada mkubwa pia kwa mzazi.
Afisa Tarafa Kata ya Ikungi mkoani Singida, Yahaya Njiku , akihutubia kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo wakati akizungumza na Vijana Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha
5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
AFISA Tarafa Kata ya Ikungi mkoani hapa Yahaya Njiku amewataka vijana wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) waliohitimu kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Ikungi kuwa wazalendo wa nchi yetu.
Njiku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo aliyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi hao katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha 5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.
"Mnapaswa kuwa wazalendo na uzalendo unatafusiri nyingi kwanza unapaswa kuipenda nchi yetu kuifahamu kuithamini na kuitunza." alisema Njiku.
Alisema wakiwa kama vijana wanaohitimu kidato cha sita na wale ambao wanaendelea na masomo ni lazima kwanza wawe wazalendo.
Alisema sisi tupo katika Taifa la Tanzania hatuna lingine zaidi ya Tanzania hivyo tunapaswa kulitunza na kulitetea popote pale duniani.
Njiku aliwaambia vijana hao kuwa uzalendo unatakiwa kuuanza wakiwa na umri mdogo na kuwa hawawezi kuwa wazalendo pasipo kulielewa taifa lao kuanzia historia yake, misingi na jinsi lilivyopatikana.
"Niwaombe ninyi wahitimu na nyie mnaoendelea na masomo ni lazima mfahamu historia ya taifa letu kwani leo hii mpo hapa mna furaha kwa kucheza muziki, michezo mbalimbali na kubadilishana mawazo kuna watu waliteseka kuliangaikia taifa letu akiwepo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere na wenzake.
Alisema ni muhimu kwa vijana hao kusoma masomo ya uraia ili waweze kulielewa taifa lao kwani wakilielewa wataweza kulitetea.
Katika hatua nyingine Njiku aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wa kuhamasisha amani hapa nchini na kuwaombea viongozi wetu hasa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliapishwa hivi karibuni kuongoza nchi baada ya aliyekuwa Rais wetu Dkt.John Magufuli kufariki.
Aliwataka wahitimu hao kuendelea kumuomba Mungu ili waweze kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu kwani kumaliza kidato cha 5-6 sio mwisho wa kusoma.
"Nyinyi wanafunzi mnakila sababu ya kuendelea na masomo kwani Serikali kupitia Rais wetu Mama Samia Suluhu imeweka mazingira bora ya kusoma kwa kutoa elimu bure." alisema Njiku.
Aidha Njiku aliwaambia wahitimu hao kuwa nidhamu na uwajibikaji ni jambo jema litakaloweza kuwafanya waishi vizuri wakiwa shuleni, nyumbani na jamii na bila kuacha kumuomba Mungu ambaye siku zote hawezi kumuacha mtu amuombaye.
Njiku aliwataka vijana hao kuto jiingiza katika vitendo visivyo na maadili badala yake watumie muda wao kwa kujisomea na kuendeleza vipaji vyao vya michezo walivyonavyo na kuwapa heshima wazazi wao wanao wasomesha kwa kufanya vizuri mitihani yao.
Wahitimu hao 19 katika risala yao kwa mgeni rasmi walitaja baadhi ya mafanikio waliyopata wakiwa shuleni ni kushiriki katika kuchangia ujenzi wa parokia ya mtakatifu Rita wa Kashia wilayani humo.
*Bashiri na Meridianbet na Uwe Miongoni Mwa Mabingwa!
HII ni wiki ambayo tutazijua mbivu na mbichi za baadhi ya timu kunako Mashindano ya UEFA na Ligi ya Europa. Dakika 90 zitaamua.
Jumanne hii, Chelsea watawakaribisha FC Porto pale Stamford Bridge. Chelsea anafaida ya magoli 2 aliyopata kwenye mchezo wa kwanza, vipi ataendelea kuwa mbabe au Porto atapindua meza? Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.50 kwa Chelsea.
PSG kuwaalika Bayern Munich katika jiji la Paris. Matokeo ya 3-2 yanawapa matumaini PSG lakini lolote linaweza kutokea kwa mabingwa watetezi – Bayern Munich. Meridianbet tumekusogezea Odds ya 2.30 kwa Bayern Munich.
Jumatano tutatua pale Signal Iduna Park, Borussia Dortmund kuwaalika Manchester City, hapatoshi. Matokeo ya 2-1 pale Etihad ni faida kwa City lakini Dortmund wananafasi ya kupindua matokeo wakiwa kwenye ubora wao. Hii itakuwaje? Unaweza kuifuata Odds ya 1.75 kwa City kupitia Meridianbet.
Liverpool kuwaalika Real Madrid pale Anfield. Licha ya kuwaumiza Aston Villa wikiendi iliyopita, wanakwenda kukutana na Madrid iliyotoka kumfunga Barcelona kwenye El Classico. Faida ya magoli 3, ni motisha kwa Madrid. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 2.00 kwa Liverpool.
Alhamisi hii tunasafiri mpaka nchini Italia, AS Roma watawaalika Ajax. Faida ya magoli 2 kwenye mchezo wa kwanza, inawapa nguvu Roma. Ajax watapindua matokeo? Meridianbet tumekupatia Odds ya 2.45 kwa Ajax.
Tutamaliza kwa mchezo wa Slavia Prague vs Arsenal. Timu zote zilitoka sare ya 1-1 pale Emirate Stadium, lakini hali itakuaje Alhamisi hii? Odds ya 1.95 kwa Arsenal inaweza kukutoa kimasomaso baada ya dakika 90 za mchezo huu.
Meridianbet, Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!