Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo ameshiriki Mashindano ya Sita ya Kuhifadhi Quran takatifu ambapo ametoa wito kwa Mashirika yaliyopewa usajili kwa lengo la kusaidia jamii hususani yatima na wasiojiweza kuhakikisha wanatenda haki kwa walengwa.
RC Kunenge amesema haipendezi kuona Shirika linapokea msaada wa vitu kwaajili ya kuasaidia Yatima, Makundi maalumu na waishio Katika Mazingira Magumu na kutumia msaada huo kujinufaisha wenyewe pasipo kuwafikia walengwa ambapo amesema kitendo hicho ni "ubabaishaji".
Aidha RC Kunenge amesema ndani ya Jamii tumebarikiwa kuwa na Wadau wengi wanaopenda kusaidia watu wasiojiweza lakini uwepo wa Taasisi zisizofuata misingi ya usajili imekuwa ikiwavunja moyo Wadau.
Akizungumza kuhusu Mashindano hayo RC Kunenge amesema yanasaidia Jamii kuelewa kwa undani Vitabu vya dini Jambo linalojenga Jamii yenye maadili na hofu ya Mungu.
Hata hivyo RC Kunenge ameipongeza Taasisi ya Faraja Islamic Foundation kwa chini ya Mkurugenzi wake Hashim Madenge kwa kuona umuhimu wa kuandaa Mashindano ya Kuhifadhi Quran takatifu ambapo amesema Serikali itampatia ushirikiano sababu anachokifanya kina manufaa kwa wananchi.
RC KUNENGE AZIASA TAASISI NA MASHIRIKA YALIYOSAJILIWA KUTOA HUDUMA KWA JAMII KUFUATA MISINGI YA USAJILI.
WAKULIMA WA TUMBAKU KUPATA NEEMA KUPITIA USHIRIKA
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe Aprili 11, 2021 wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 3 wa T.C.J.E Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri ameeleza kuwa ili mkulima wa Tumbaku aweze kupata pembejeo ikiwemo Mbolea kwa gharama nafuu ni vyema Mradi huo ukafanya taratibu za kukusanya mahitaji ya pembejeo za wakulima wa Tumbaku kutoka kwenye Vyama vya Ushirika wanachama wa Mradi huo. Akiongeza kuwa kufanya hivyo kutapunguza riba za gharama za mikopo ya mabenki, mianya ya ubadhilifu na kuondokana na madeni hewa ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.
“T.C.J.E katika msimu mpya wa Tumbaku mwaka huu 2021 hakikisheni mahitaji ya wakulima ya Mbolea yanakusanywa mapema na mnunuzi anasambaza mbolea hiyo moja kwa moja kwa wakulima kupitia Vyama vya Ushirika,” alisema Naibu Waziri
Aidha, Mhe. Bashe alieleza kuwa Kilimo ni Sekta muhimu inayochangia kutoa ajira kwa watanzania kwa wastani wa asilimia 60 hadi 75 na kuchangia pato la Taifa kwa wastani wa asilimia 25. Hata hivyo, Naibu Waziri amebainisha kuwa mapato kutokana na zao la Tumbaku kwa sasa yameshuka kutoka Dola Millioni 300 hadi 146.5 jambo ambalo linachangiwa na kushuka kwa uzalishaji pamoja na kupungua kwa matumizi ya zao hilo.
Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amesema bado Serikali ina dhamira ya kuendelea kulinda na kusimamia zao la Tumbaku. Akiongeza kuwa Ilani ya Chama Tawala imetoa maelekezo mahususi ya kuimarisha na kujenga Ushirika.
Ili kuhakikisha kuwa Ushirika unaendelea kuendeshwa kwa kufuata Sheria Naibu Waziri Bashe amemuagiza Mrajis wa Vyama vya Ushirika kukamilisha ripoti ya baadhi ya Vyama vya Ushirika ambavyo vina shutuma za ubadhilifu na ripoti hizo ziwasilishwe katika Mamlaka husika kwaajili ya hatua zaidi.
Akiongea wakati wa Mkutano huo Naibu Waziri amempongeza Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege kwa utekelezaji wa kuanza utaratibu wa kutumia wahitimu wa Vyuo vikuu katika shughuli za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika kwa lengo la kutoa fursa kwa wahitimu hao kujitolea kutumia weledi wao katika nyanja mbalimbali na wao kupata uzoefu wa kazi. Alisema kuwa hatua hiyo ni jambo la kupongezwa kwani wahitimu wengi wanamaliza vyuo na hawana sehemu za kukuza taaluma zao na wakati huohuo Ushirika unapata fursa ya watendaji wasomi watakaoongeza tija kwenye vyama hivyo.
Mkutano huo ulifuatiwa na Uchaguzi wa Viongozi wa T.C.J.E uliowezesha kupata Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi uliofanyika kwa mujibu wa Sheria Na.6 ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2013. Hatua ambayo itafuatiwa na Mafunzo elekezi, makabidhiano, fomu za kiapo na maadili yatakayowezesha kuzingatiwa kwa Sheria, Kanuni na Taratibu za Ushirika.
Naibu Waziri Mhe.Hussein Bashe akisistiza janbo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Wakulima wa zao la Tumbaku Tobbacco Cooperative Joint Enterprise Limited (T.C.J.E) wakati wa Mkutano Mkuu wa tatu uliofanyika Mkoani Morogoro April 11, 2021.
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Morogoro Bw. Keneth Shemdoe akieleza masuala ya Ushirika wa Mkoa wa Morogoro wakati wa Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Wakulima wa zao la Tumbaku Tobbacco Cooperative Joint Enterprise Limited (T.C.J.E) wakati wa Mkutano Mkuu wa tatu uliofanyika Mkoani Morogoro April 11, 2021
IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO APRIL 12,2021
HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA KIKE CHUO CHA CBE MKOANI MBEYA.
Ungana na Mhe. Naibu Spika Dr. Tulia Ackson (MB) na Mlezi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya MBEYA kwa Kuchangia fedha kwaajili ya Ujenzi hosteli za wanafunzi wa kike katika kampasi ya Mbeya. Hosteli hizi zimekadiriwa kuwa na thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 1.15.
Unaweza kushiriki kwa kupitia namba za Changizo hapo juu.
#ChangiaZaidiYaHarusi
NDAHANI AVISHAURI VYAMA VYA MICHEZO KUTIMIZA AGIZO LA RAIS SAMIA LA KUENDELEZA MICHEZO YA WANAWAKE.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAIMU Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amevitaka vyama vya mechezo katika Mkoa wa Singida kuhakisha wanawasaidia vijana wa kike kutimiza ndoto za vipaji vyao kupitia agizo la Rais Samia Suluhu Hasssn alipolitoa kwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wakati akiapisha Baraza jipya la Mawaziri.
Rais Samia aligiza kuona michezo kwa upande wa wanawake inathaminiwa kama ilivyo kwa wanaume ,hivyo vyama vya michezo vinawajibu kuweka mikakatika ya kukuza vipaji vya vijana wanawake kuanzia ngazi ya chini,
Ndahani aliyasema hayo wakati akitoa zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika mjini Singida iliyokuwa na lengo la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Michezo hiyo ilidhaminiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Men engage,Youth of United Nation Association Tanzania (YUNA),Youth Movement for Change (YMC), Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa na Chama cha Mpira wa Miguu Manispaa ya Singida.
Akimkaribisha mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Shirika ya YUNA, Ally Mwamzola amewataka wanaume kuhakikisha kuwa ukatili kwa wanawake na watoto unatoweka nchini kwani wanaume bado wanashiriki katika ukatili wa kijinsia.
Naye Afisa michezo wa Manispaa hiyo Samweli Mwaikenda ameyashukuru mashirika hayo Kwa kuamua kutumia michezo katika kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia,ameyataka mashirika mengine kuiga mfano kwani kuna faida kubwa kutumia michezo katika kutoa elimu.
Mkurugenzi wa Shirika la YMC Fudelis Lyunde amemshukuru Kaimu Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Ndahani kwa kukubali kuja kushiriki na vijana katika michezo na kuomba aendelee na moyo huo wa kuwa karibu na vijana ili wafikie ndoto zao katika nyanja za michezo na uchumi.
SimBanking yatajwa kuwa mkombozi huduma za kibenki

WALIMU MWANGA WAPONGEZWA KWA KUFANYA KAZI KWA NIDHAMU NA WELEDI
Na Adili Mhina
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imewapongeza walimu wa Wilaya ya Mwanga kwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi na nidhamu licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Idara ya Ajira, Maadili na Maendeleo ya walimu kutoka TSC, Christina Hape alipofanya ziara wilayani hapo kwa lengo la kukutana na kuzungumza na walimu juu ya masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Hape alieleza kuwa TSC inatambua changamoto mbalimbali za wilaya hiyo ikiwemo upungufu wa walimu pamoja na shule nyingi kuwa maeneo ya mbali ambapo miundombinu na huduma mbalimbali bado hazijafika.
Aliongeza kuwa, licha ya changamoto hizo, walimu wa wilaya hiyo wamekuwa mfano wa kuigwa kutokana moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu, kitu kinachofanya Mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri kitaaluma.
“Kwa kweli Mwanga mnajitahidi kufanya vizuri, tunatambua kuwa yapo maeneo ya milimani ambayo hata kufikika kwake ni changamoto. Nimeelezwa kuwa hata kufika hapa kwenye mkutano huu wapo baadhi yenu mliolala kwenye magari ili muweze kuwahi”, alisema Hape.
Aliongeza kuwa, “pamoja na changamoto hizo mmeendelea kufanya kazi kwa kujituma na kwakweli hata kule makao makuu hatujapokea rufaa nyingi zinazohusu utovu wa nidhamu kwa walimu wa mwanga, naomba niwapongeze sana kwa hilo.”
Mkurugenzi Hape alifafanua kuwa, suala la upungufu wa walimu sio la wilaya hiyo peke yake bali maeneo mengi ya nchi kuna upungufu wa walimu na tayari serikali imeamua kuchukua hatua za haraka ili kukabiliana na tatizo hilo.
“Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan alizungumzia suala la upungufu wa walimu na kuagiza suala hilo tulishughulikie kwa haraka. Vilevile, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu naye amesisitiza kuwa hataki kuona shule yenye walimu wawili au watatu,” alisema Hape.
Aliongeza kuwa maagizo ya viongozi hao kuhusu kutatua changamoto ya upungufu wa walimu inaifanya TSC pamoja na mamlaka nyingine zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha walimu wanaajiriwa ili kujaza maeneo yenye upungufu.
Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo alipongeza ushirikiano uliopo kati ya ofisi ya TSC wilaya pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga na kusema kuwa ushirikiano huo ndiyo unaofanya walimu wafanye kazi kwa moyo, nidhamu na weledi.
“Nishukuru ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na ofisi ya TSC wilaya kwa kuwa mnafanya kazi kama timu moja, hakuna mivutano. Kaimu Katibu wa TSC, Maafisa Elimu pamoja na Maafisa Utumishi mnazungumza lugha moja katika kutatua kero za walimu. Hii imefanya hata katika masuala ya kupandisha madaraja sijasikia malalamiko kuwa kuna mwalimu amesahaukika,” alisema Hape.
Akitoa taarifa fupi ya utendaji wa TSC wilayani hapo, Kaimu Katibu Msaidizi wa TSC wilaya ya Mwanga, Catherine Kimaro alisema kuwa, wilaya hiyo ina jumla ya walimu 1120 wanaofundisha shule za Serikali. Katika idadi hiyo, walimu 558 ni wa shule za msingi na 562 ni wa shule za sekondari.
Kimaro alieleza kuwa, wilaya hiyo kwa sasa haina shauri lolote la nidhamu kutokana juhudi za ofisi yake za kutoa elimu kwa walimu mara kwa mara kuhusu miiko na maadili ya utendaji wa kazi.
TAWA , CHUO KIKUU CHA UDSM WAZINDUA MAGOFU MARATHON KILWA LENGO NI KUTANGAZA UTALII WA WILAYA YA KILWA NA MKOA WA LINDI
Kwa upande wa mbio za kilometa 10 mshindi wa kwanza alikuwa ni Azilu Kiumjile (73:10), wapili ni Joseph Chiza (73: 45), na watatu ni Jacob Machesa (74: 30) .
Katika mbio za kilombeta 21 mshindi wa kwanza alikuwa ni Zishi Imran (93: 10), mshindi wa pili ni Sudi Said (95: 50) na mshindi wa tatu ni Semedo Athuman (99:10).
Wengine walioshiriki na kuunga mkono kuanzishwa kwa Magofu Marathon kwa kukimbia umbali wa kilometa tano ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Tawa , Meja Jenerali Mstaafu Semfuko ,Naibu Kamishna wa Huduma za Utalii na Biashara wa Tawa , Imani Nkuwi ,Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Udsm , Profesa William Anangasye.
RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI JIJINI DAR ES SALAAM

KUMBUKIZI YA MIAKA 37 YA KIFO CHA EDWARD MORINGE SOKOINE ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI 1984 AKIWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA
"April 12, 1984 ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Taifa la Tanzania. Ni siku ambayo hatutaisahau kwani siku hiyo tulimpoteza Kiongozi wetu tuliyempenda sana aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Sokoine. Mh. Sokoine alifariki kutokana na ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Wami- Dakawa".
ATILIO TAGALILE, April 11, 2011 (The Citizen, Tafsiri yangu.)
1. Usuli
Jumatatu ya leo, April 12, 2021, Taifa letu linatimiza miaka 37 toka marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE, mmoja wa viongozi bora kabisa kuwahi kutokea nchini, afariki kwa ajali ya gari Aprili 12, 1984 eneo la Dakawa, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Miaka 37, kwa umri wa mwanadamu, ni mingi sana. Hivyo, kuna baadhi ya "Bongolanderz" , hasa wa "Dot.com generation", ambao hawamjui kabisa na wengine wanamjua kijuujuu tu marehemu SOKOINE ndio maana mwandishi Bi HELLEN MATABA, alilibaini ombwe hili na kulielezea hapo Aprili 11, 2011-:
Today, 27 years after his tragic death, majority of Tanzanians aged below 27 years might not know who this man called Edward Sokoine was to Tanzania".
Hivyo basi, " MZEE WA ATIKALI" amewiwa kuziba ombwe hili kwa kumuelezea Mzalendo huyu wa kipekee kabisa toka siku anazaliwa hadi anafariki.
2. SOKOINE Azaliwa
Jumatatu ya Agosti 1, 1938, katika kitongoji cha Kilasho, kijiji cha Emairete, Monduli Juu, Arusha, huku mvua kubwa ikirindima, alizaliwa mtoto wa kiume. Mtoto huyo alikuja kuitwa EDWARD MORINGE SOKOINE ambapo baba yake aliitwa SOKOINE OLE SEVERE na mama yake aliitwa NAPELEL SINYATI NOOMAYAKI.
3. Elimu
3.1 Elimu ya Msingi
SOKOINE alisoma Shule ya Msingi Monduli kuanzia mwaka 1949 hadi 1953 na kisha akajiunga na "Monduli Middle School" toka mwaka 1953 hadi 1956.
3.2 Elimu ya Sekondari
SOKOINE alifaulu mitihani yake hivyo mwaka 1956 alijiunga na shule ya sekondari ya Umbwe.
4. SOKOINE Ajiunga na TANU
Januari 1 1961,SOKOINE alijiunga na chama cha "Tanganyika African National Union" (TANU), ikiwa ni miezi michache kabla ya Tanganyika haijapata uhuru.
5. SOKOINE Aenda Masomoni
Mwaka 1962, SOKOINE alienda Ujerumani Magharibi kusomea mambo ya utawala na kurejea mwaka 1963.
6. SOKOINE Awa DEO
Baada ya kurejea toka Ulaya, SOKOINE alipangiwa kazi kama "District Executive Officer" (DEO) wa Maasai.
7. SOKOINE Agombea Ubunge
Septemba 30, 1965, SOKOINE, akiwa kijana mdogo tu wa miaka 27 lakini mwenye akili na ubunifu mkubwa, aligombea na kushinda ubunge jimbo la Masai. Mpinzani wake alikuwa Bw. EDWARD CARLO BONIFACE OLE MBARNOTE aliyekuwa Chifu wa Wamasai.
SOKOINE aliibuka mshindi baada ya kuhomola kura 6,977 wakati mpinzani wake, Chifu MBARNOTE aliduchua kwa kura 871.
8. Mh. SOKOINE Atema Cheche
Baada tu ya kuapishwa bungeni, Mh. SOKOINE alianza kutema cheche ambapo maswali yake ya kwanza yalikuwa-:
8.1 "Kwanini Wamasai wa Ngorongoro wanazuiwa kulima, wakati hawana mifugo ya kuwapatia chakula?"
8.2 "Kwakuwa tangu kuanza kwa Taifa hili, kuna makabila yamepata maendeleo sana na mengine yapo nyuma sana, je serikali ina mpango gani wa kuwaelimisha walioko nyuma kimaendeleo ili wawe sawa na wenzao?"
9. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Mdogo
Mwaka 1967, Mh.SOKOINE aliteuliwa na Rais NYERERE kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi.
10. Mh. SOKOINE Awa Waziri wa Nchi
Mwaka 1970, Rais NYERERE Alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri wa Nchi.
11. Mh. SOKOINE Akonga Nyoyo
Mh. SOKOINE alijulikana kwa uchapakazi wake toka akiwa Naibu Waziri. Hivyobasi, haikushangaza katika kikao nyeti cha NEC ya TANU, 1971, Mh. SOKOINE alipokonga nyoyo za wajumbe kwa hotuba kuntu kuhusu nchi kujilinda.
12. KINGUNGE "Amfagilia" Mh. SOKOINE
Baada ya hotuba hiyo mujarab, Rais NYERERE alimwita chemba, Mh. KINGUNGE NGOMBARE MWIRU na kumtaka maoni yake amwonavyo Mh. SOKOINE. Mh. KINGUNGE akamsifia sana, kama Prof ISSA SHIVJI aelezevyo katika kitabu cha "A Biography of Julius Nyerere" Mh. KINGUNGE alivyojibu-:
"Sokoine's speech was brilliant".
13. Rais NYERERE Amteua Mh SOKOINE Kuwa Waziri
Mwaka 1972, Rais NYERERE akamteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
14. Mh. SOKOINE Awa Mjumbe wa CC
Baada ya CCM kuzaliwa kutokana na TANU na ASP kuungana Februari 5, 1977, Mh. SOKOINE akawa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
15. Mh. SOKOINE Ateuliwa kuwa "PM"
Februari 13, 1977, kutokana na utendaji kazi wake makini, Rais NYERERE alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu.
16. Mh. SOKOINE na Vita ya Kagera
Mh. SOKOINE alikuwa kiungo muhimu kwenye vita ya Kagera 1979. Kabla ya vita kuanza, SOKOINE aliwaagiza RCs wote wakusanye nyenzo zote tayari kwa kumtandika Nduli. Januari 23, 1979, alitembelea Mutukura. Hatimaye, TZ ikashinda vita hiyo. Mh. SOKOINE alikuwa halali usingizi wakati wa vita, hali iliyopelekea afya yake kutetereka; kama "Wikipedia" inavyoeleza-:
"Sokoine had gone many days without sleep during the conflict and was left in ill health by its end."
17. Mh. SOKOINE Aomba Kujiuzulu
Novemba, 1980, Mh. SOKOINE aliomba na kukubaliwa kujiuzulu u-Waziri Mkuu na akaenda Yugoslavia kwenye matibabu na nafasi yake ikashikwa na Mh. CLEOPA DAVID MSUYA. Prof ISSA SHIVJI anatanabaisha-:
"Sokoine requested Nyerere to be relieved of his post because of his illlness; he suffered from severe diabetes. Sokoine went to Yugoslavia for treatment"
Mh. PIUS MSEKWA alieleza kuwa Mh. CD MSUYA alikuwa "anamshikia tu" Mh. SOKOINE cheo hicho-:
"Sokoine returned from Yugoslavia in 1983 having fully recovered from the disease that was troubling him. That was the time when President Nyerere reappointed him Prime Minister to replace Msuya who, apparently, had been "housewarming" that position in Sokoine's absence".
Prof ISSA SHIVJI nae alieleza vivyo hivyo-:
"In hindsight, it appears as if Msuya's premiership was a holding operation:
Baada ya kurejea, Rais NYERERE alimteua tena Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu Februari 24, 1983. Aidha, mwaka huo wa 1983, Mh. SOKOINE alianza kusomea shahada ya "Political Science".
18. Mh. SOKOINE: Muasisi wa Daladala
Mh. SOKOINE alikuwa ni mtu wa kutafuta majawabu ya matatizo ya wananchi. Alipoona UDA "inambwelambwela" akaasisi utaratibu wa daladala.
Prof. ISSA SHIVJI anafafanua-:
"Sokoine allowed private mini-bus operators to provide transport in Dar es Salaam under licence from the state bus company, UDA. Mini-buses came to be called "Daladala" because the newly minted five-shilling coin was the fare, and it happened to be the exchange rate of a US dollar. "Daladala" is one of Sokoine's lasting legacies".
19. SOKOINE & Uhujumu Uchumi
Aprili 5, 1983, Rais NYERERE alizindua kampeni kabambe ya kupambana na wahujumu uchumi baada ya kupitishwa kwa Sheria ya "The Economic Sabotage Act No. 9 of 1983" . Kampeni hii iliendeshwa na kusimamiwa na SOKOINE.
Sheria hii ilimtaka mtu aeleze mali aliyokutwa nayo aliipata wapi. Zilianzishwa Mahakamani Maalum na Mawakili hawakuruhusiwa kuingia, watu walitakiwa wajitetee wenyewe (Rais NYERERE aliona wahalifu wangeweza kutumia ujuzi wa mawakili kuachiwa). Katika zoezi hili, watu walimuogopa sana SOKOINE kwani sehemu nyingi nchini hasa Dsm mf Oysterbay & Upanga walitupa barabarani na mitaroni vitu vya thamani vilivyokuwa vimeingizwa nchini kinyemela mf TVs, na pia walitupa mabunda ya fedha na wapita njia waliogopa kuviokota vitu na fedha hizo kwa kumuogopa SOKOINE hivyo polisi walikuwa wakiziokota fedha hizo na kuzipeleka BOT!. Vita hii ilimjenga sana SOKOINE kisiasa na akapendwa nchini kote.
Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kutokana na jinsi zoezi hilo lilivyoendeshwa yaliyopelekea Mh. SALIMN AMOUR, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, aombe radhi-:
"Mistakes were made during the campaign but it was not the intention of the government to victimise anybody. Those who were unfortunately involved should forgive the nation as the move was aimed at improving the situation".
Baada ya kifo cha SOKOINE, Sheria hii ilifutwa na ikatungwa "The Economic & Organized Crimes Control Act, 1984" ambapo mambo mbalimbali, mf uwepo wa mawakili, yalirekebishwa.
20. Mh. SOKOINE Ahudhuria Bunge
Mh. SOKOINE alihudhuria kikao cha bunge jijini Idodomia mwezi April 1984.
Jumatatu ya tarehe April 9, 1984, Mh. SOKOINE alikwenda kusali kanisa la Mtakatifu PAUL, Idodomia. Usiku wa Jumanne, tarehe April 10, 1984, Mh. SOKIONE aliandaa karamu ya chakula cha jioni kwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo alionekana kuongea na kila Waziri na kila Mkuu wa Mkoa. Jumatano, tarehe April 11, 1984, aliandaa chakula cha jioni kwa Wabunge wote wa mkoani kwake Arusha ambapo aliwasihi wafanye jitihada kuwaondoa wananchi wao kwenye lindi kubwa la ufukara.
21. Mh. SOKOINE Aliasa Bunge
Mh. SOKOINE, siku ya Jumatano ya tarehe April 11, 1984, akilivunja Bunge, aliasa kwa uchungu:
"Ndugu Spika, ningependa kumalizia kwa kukubaliana na wabunge wote waliosema na ambao hawakusema lakini wana mawazo haya kwamba jambo hili la kutumia fedha bila idhini ya bunge lazima tutafute kila njia ya kulikomesha".
22. SOKOINE Apangiwa Ndege, Agoma
Mh. SOKOINE alipangiwa kusafiri kwa ndege lakini akaamua kusafiri kwa njia ya barabara na sababu ya kufanya hivyo aliiainisha bungeni-:
".... Mungu akipenda tutakutana tena kwenye kikao kijacho cha bunge. Mimi nasafiri kwa njia ya barabara ili nijionee hali ya mazao ya wakulima...".
23. Mh. SOKOINE Aanza Safari
Mapema Alhamis, tarehe April 12, 1984, Mh. SOKOINE aliondoka na msafara wake Idodomia saa 4.30 asubuhi akiwa ndani ya Mercedes Benz ambapo msafara huo uliongozwa na msafara wa polisi. Magari yote yaliyokuwa yakikutana na msafara huo yalikuwa yakipaki pembeni kuupisha msafara huo.
24. Gari la Mh. SOKOINE Lilikuwa Kwenye Mwendo wa Kasi!
Msafara wa SOKOINE ulikuwa na mwendo wa kasi; kama "Minutes" za CC ya CCM ya April 17, 1984 zinavyoeleza-:
"... Msafara wa Sokoine uliondoka Dodoma majira ya saa nne na nusu asubuhi na ulikuwa ukienda kwa spidi ya kilomita 154 kwa saa".
Baada ya gari hilo kufika eneo la Dakawa, ghafla kilisikika kishindo kikubwa. Gari la Mh. SOKOINE lilikuwa limegongana na gari aina ya Toyota Land cruiser lililokuwa likiendeshwa na Bw. DUMISAN DUBE (23), mpigania uhuru wa chama cha ANC, aliyekuwa akiishi Mazimbu, Morogoro.
Bw. DUBE, licha ya kusimamishwa na polisi, hakusimama kwani nae alikuwa kwenye mwendo wa kasi. Bw. DUBE, katika msafara huo, alikuwa na abiria wawili ambao ni Bw. BOYCE MOYE & Bw. PERCE GEORGE.
Mh. SOKOINE, ambaye alikuwa ni mtu wa miraba minne, alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku akiwa hajafunga mkanda. Katika ajali hiyo, Mh. SOKOINE alirushwa toka nyuma hadi akagonga kioo cha mbele na hivyo kupelekea aumie sana. Mh. SOKOINE alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Morogoro ambako madaktari walithibitisha kifo chake.
25. SOKOINE Alipata Majeraha Makubwa
Marehemu SOKOINE alipata majeraha makubwa na kwa mujibu wa "Postmortem Report" yake iliyowasilishwa mbele ya CC ya CCM, mbavu na mifupa ya mikononi na miguuni vilivunjika. Mbavu zilizovunjika zilipelekea kuchoma mapafu yake!.
26. Mabodigadi wa Mh. SOKOINE Hawakuumia Sana
Ajali hiyo ilichukua maisha ya Mh. SOKOINE tu kwani wengine wote walisalimika na kupata majeraha ya wastani.
Bw. YUSTO CHUMA, aliyekuwa bodigadi wake ambaye alikaa kiti cha mbele kulia, na Bw. ALLY ABDALLAH aliyekuwa dereva wake, walijeruhiwa kiasi. Prof. ISSA SHIVJI anatanabaisha-:
"Neither Sokoine's bodyguards in the car nor anyone else in the other vehicles, including Dube, were seriously injured".
27. Rais NYERERE Atangaza Kifo
Alasiri ya siku hiyo, RTD ilisitisha ghafla matangazo yake na ukapiga wimbo wa Taifa.
Rais NYERERE, baada tu ya wimbo huo na kwa uchungu mkubwa, akalitangazia Taifa msiba huo wa kihistoria kama ifuatavyo-:
"Ndugu wananchi, leo hii ndugu yetu, kijana wetu, Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Tanzania, alipokuwa akirejea Dar es Salaam toka Dodoma, gari lake lilipata ajali na amefariki. Ndugu Watanzania naomba muamini Edward amefariki kwa ajali na si kitu kingine".
28. Rais NYERERE Aangua Kilio
Baada tu ya Rais NYERERE kutoa taarifa hiyo alibubujikwa na machozi kutokana na uchungu mkubwa. Mwandishi nguli, Bw. ATILIO TAGALILE, aliyekuwa "Daily News" kipindi hicho, alieleza April 15, 2015 kuwa Mwalimu NYERERE, baada tu ya kutangaza, akatokwa machozi!.
29. Vilio Vyatamalaki Nchini
Baada tu ya taarifa hiyo, vilio na simanzi kubwa vilitamalaki nchi nzima. Kwenye maofisi, vyuoni, mashuleni, kwenye mabaa, mabarabarani, kote huko wananchi walionekana dhahiri wamevurugwa!.
Kikao cha UWT kilichokuwa kikifanyika Lumumba, kilisambaratika ghafla bila hata Mwenyekiti wake, mama SOPHIA KAWAWA, kukiahirisha kwani mara tu baada ya taarifa hiyo iliyoleta huzuni, jakamoyo na jitimai kubwa, wakinamama waliangua vilio kwa sauti za juu sana!.
30. Serikali Yatangaza Wiki Mbili za Maombolezo
Serikali ilitangaza wiki mbili za maombolezo na kuamuru bendera nchi nzima kupeperushwa nusu mlingoti.
31. Rais NYERERE Aangua Kilio Baada ya Kuuona Mwili wa Mh. SOKOINE
Mwili wa marehemu SOKOINE uliwasili Ikulu, Dsm toka Morogoro saa 11 jioni siku hiyohiyo ukiwa umefunikwa kwa bendera ya Taifa.
Rais NYERERE, akiongozana na Mama MARIA, waliujongelea mwili huo na kisha Rais NYERERE akaifunua bendera na kuweka mikono yake miwili kwenye paji la uso wa SOKOINE.
Rais NYERERE na Mama MARIA, aliyekuwa na kitambaa cheupe, walilia kwa uchungu sana hadi kuondolewa na walinzi wao. Bw. ATILIO TAGALILE, mwandishi wa "Daily News" wakati huo aliyekuwepo Ikulu, aliandika-:
"Mwalimu Nyerere burst into tears and was whisked away by his bodyguards".
32. JOSEPH NYERERE Azua Kimuhemuhe Ikulu!
JOSEPH NYERERE, mdogo wa Rais NYERERE, ambaye alijulikana kwa kutomung'unya maneno, alikwenda kwa kasi ulipokuwepo mwili huku akiwa na huzuni kubwa na akasema-:
"Mwalimu huna ulinzi. Waziri Mkuu anafia barabarani?!!!" .
Prof. ISSA SHIVJI anafafanua jinsi JOSEPH NYERERE alivyoondolewa-:
"Security guards quickly whisked Joseph Nyerere away from the casket and he was driven away from the State house".
Mwili wa marehemu SOKOINE ukapelekwa hospital ya Lugalo kwaajili ya kuhifadhiwa.
33. Jeneza la SOKOINE Latengenezwa Usiku wa Manani
Shughuli ya kutengeneza jeneza la SOKOINE alipewa Bw. GEORGE CHRISTOS, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari TZ. Huyu alikuwa ni chotara kwani baba yake alikuwa ni Mgiriki na mama yake Msukuma akiitwa MARIA, aliyekuwa mmoja wa mabinti wa Chifu KIDAHA.
Saa 12 jioni ya siku hiyo, Bw. CHRISTOS na mkewe, Bi. ELIZABETH WALKER & Bw. PAUL MKANGA, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, walienda hospitali kuchukua vipimo vya mwili wa SOKOINE. Kisha wakaelekea Chang'ombe kilipo kiwanda cha HEM-SINGH ambako bahati nzuri mwenye kiwanda alikuwa hajafunga.
Kazi ya kutengeneza jeneza ikaanza mara moja na kumalizika usiku wa manane. Kisha, Bi WALKER akalipamba jeneza hilo na likapelekwa hospitalini.
34. SOKOINE Aagwa na Wakazi wa Dsm
Siku ya Ijumaa, Aprili 13, 1984, maelfu ya wakazi wa jiji la Dsm na mikoa ya jirani walifurika "Karimjee Hall" kumuaga mpendwa wao, marehemu SOKOINE. Kwa hakika, umati uliokuwepo uliweka rekodi iliyokuja kuvunjwa na umati uliojitokeza Octoba 21,1999 kufuatia kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERE.
35. Daladala Zapeleka Abiria Bure "Airport"
Jumamosi ya Aprili 14, 1984, mwili wa marehemu SOKOINE ulipelekwa "airport" kwaajili ya kusafiridhwa kwenda Arusha kwenye mazishi. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Daladala zote jijini zilipeleka abiria bure uwanja wa ndege kumuaga mpendwa wao. Mwandishi Bi. HELLEN MATABA anajuza zaidi-:
"Sokoine was the brainchild of city commuter buses commonly known as "Daladala" and no wonder hundreds of thousands of Dar es Salaam residents were ferried on Daladala free of charge and then Sokoine's body was flown to Monduli for burial".
36. SOKOINE Azikwa kwa Heshima Zote
Kaburi la aina yake lilijengwa huko Monduli na MJ JOHN BUTLER WARDEN "Black mamba", Mtanzania chotara, na aliifanya kazi hiyo kwa kushirikiana na askari wa TPDF.
" Black Mamba" alifanya kazi nzuri kiasi cha kupewa "mchongo" wa kujenga kaburi la aliyekuwa Rais wa Nchumbiji, marehemu SAMORA MACHEL aliyefariki baada ya ndege yake aina ya "Tupulov Tu 135" kuanguka Octoba 19, 1986.
Mazishi ya marehemu SOKOINE yalipewa heshima zote na yaliyohudhuriwa na umati wa watu wakiongozwa na Baba wa Taifa .
Bw. OLIVER TAMBO, aliyekuwa Rais wa ANC na ALFRED NZO, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ANC, walihudhuria na kuelezea kusikitishwa sana na kifo hicho kilichosababishwa na raia mwenzao wa Afrika Kusini.
37. SOKOINE Aacha Wake 2, Watoto 11
SOKOINE alikuwa na wake wawili ambao ni NAPONO na NAKITETO na watoto 11.
38. DUMISAN DUBE Afikishwa kwa Pilato
Mei 17, 1984, Bw. DUMISAN DUBE alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro ambako kesi yake iliahirishwa.
Juni 12, 1984, upande wa mashaka ukiongozwa na Bw. JOHNSON MWANYIKA (SSA) ulitinga mahakamani na mashahidi 21. Hata hivyo, Bw. DUBE aliposomewa mashtaka 7 alikiri hivyo Mh. SIMON KAJI (PRM) akampa kifungo cha miaka mitatu.
39. Kwanini SOKOINE Alipendwa Sana?
Nukuu zake kuntu zinajibu swali hilo-:
39.1 SOKOINE alichukia sana wazembe:
"Ole wake kiongozi asiye na nidhamu na mzembe ntakaemkuta. Viongozi wazembe na wabadhilifu wahesabu siku zao"
39.2 SOKOINE alitaka Wazazi Wawajibike kwa Watoto Wao:
"Vijana wengi siku hizi wana mali kuliko wazazi wao waliofanya kazi kwa miaka zaidi ya 40 lakini wazee hao wanataka Serikali ndio iwaulize watoto hao wamepata wapi mali hizo. Mzazi unashindwa nini kumuuliza mwanao?"
39.4 SOKOINE Alihimiza Majeshi Yawe kwa Faida ya Wote:
"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi kuwa chombo cha kulinda haki na maslahi ya wengi. Kamwe hayaruhusiwi kuwa chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao".
39.4 SOKOINE Alikuwa Mzalendo wa Kiwango cha Juu:
"Viongozi wanaoteuliwa lazma wawe wazalendo wa hali ya juu. Naskia huko mikoani kuna viongozi wanagombania magari na nyumba. Mambo hayo si muhimu. Viongozi wanatakiwa kugombania juu ya Maendeleo ya wanavijiji. Huu ni ugomvi mtakatifu".
39. 5 SOKOINE Alichukia Upuuzi
Mwezi Machi 1983, PM SOKOINE alifanya ziara Singida. Mmoja wa viongozi mkoani humo akamfuata Bw. ACCADOGA CHILEDI aliyekuwa "Press Secretary " wa PM SOKOINE na kumwambia-
"Mzee tumeishamtayarishia blanketi chapa ya mtu" (akimaanisha kimada). Bw. CHILEDI akamuuliza kiongozi huyo- "Brother, Mh. Sokoine unamjua au unamsikia? Hilo blanketi lako ondoka nalo haraka na utoweke kabisa maana nikimjulisha ujue unapoteza kazi yako sasa hivi"
39. 6 SOKOINE Alikuwa Mchapakazi Hodari:
SOKOINE alikuwa mchapakazi hodari na alipenda sana kuwatumikia wananchi. Prof ISSA SHIVJI anadadavua-:
"Sokoine's personal integrity was beyond reproach. He worked hard and demanded an equal level of hard work and accountability from his subordinates"
SOKOINE daima alifanya kazi hadi usiku na mara nyingine hadi usiku wa manani. Mh. MARTENS LUMBANGA (Baba wa Bi HARRIETH ), aliyefanya kazi kwa karibu na SOKOINE, alitiririka April 7, 2021-:
"Mimi nilikuwa Kamishina wa Planning. Nilikuwa nafanya kazi na makamisha wengine na Sokoine mara nyingine hadi usiku wa manani kisha anatusindikiza ye anarudi kuendelea na kazi. Asubuhi tunakuta ameishatoa mafaili. Marehemu Sokoine alikuwa Mfanyakazi hodari, Mwaminifu na Muungwana sana".
39.7 SOKOINE Hakupenda Utajiri
Maisha ya SOKOINE yalielezewa kwa ufasaha na Mwalimu NYERERE kwenye msiba wake-
"Edward hakuwa na mali yoyote ukiachilia ng'ombe wa urithi. Alikuwa na suti tatu na viatu pea mbili tu".
39.7 SOKOINE Alikuwa Mbunifu Sana
SOKOINE alianzisha "PRESIDENTIAL TRUST FUND" Ikulu ambapo alikuwa akiweka sehemu ya mshahara wake ili kuwasaidia akina mama kuweza kukopa. Mshahara wa PM wakati huo ulikuwa ni TZS 3, 000/= kama alivyobainisha Mh. CD MSUYA (PM 1980-1983) "Kwenye sherehe ya siku yangu ya kutimiza miaka 80 niliwaambia marafiki zangu kuwa nilipokuwa PM nilikuwa napokea mshahara wa TZS 3,000/= tu, hawakuamini."
39.8 SOKOINE Alikuwa Mcha Mungu Sana
SOKOINE alikuwa Mkristo Mkatoliki na aliipenda sana dini yake na alikuwa mwanachama wa utawa wa tatu wa Mt. Fransisca. SOKOINE alikuwa akisali kanisa la Mt. Joseph, Dsm ambako Jumatatu, Aprili 12, 2021 kutakuwa na misa maalum kumkumbuka iliyoandaliwa na familia yake.
39.9 SOKOINE Alipambana Vikali na Wahujumu Uchumi
SOKOINE aliendesha mapambano makali na wahujumu uchumi yaliyopelekea hadi Mh. EDWARD BARONGO, RC Kilimanjaro "aliwe kichwa" na kuwekwa "detention" kwa miezi minne hadi alipoachiliwa na Rais NYERERE".
40. Rais Marehemu Dr. JPM Alimkubali Sana SOKOINE
Marehemu Dr. JPM alimkubali sana SOKOINE, kama alivyoeleza Aprili 12, 2018-:
"Aprili 12, 1984 Sokoine alipofariki ilikuwa ni huzuni kubwa sana. Mimi nilikuwa kwenye mafunzo ya lazima JKT Mpwapwa "Operesheni Nguvukazi". Sokoine kamwe hatasahaulika kwani alipiga vita rushwa, wizi na unyonyaji. Alikuwa Mzalendo wa kweli hivyo ni wito wangu kwa Watanzania tumuige na tumuishi."
41. Jeshi Lilimpenda Sana SOKOINE
SOKOINE alipendwa sana na Jeshi toka alipoongoza Wizara ya Ulinzi; kama Prof. ISSA SHIVJI anavyofafanua katika kitabu cha "A Biography of Julius Nyerere"
"Sokoine was the political leader whom the Army respected most after Nyerere because he earned their trust when he was the Minister of Defence for five years between 1972 and 1977"
42. Mwalimu NYERERE Ampa Mjukuu Wake Jina la MORINGE
Baba wa Taifa alikuwa na watoto 7 na wajukuu kedekede na alifanya kazi na Mawaziri Wakuu wengi. Hata hivyo, ni jina la MORINGE tu ndilo alilompa mmoja wa wajukuu zake. Prof. SAIDA YAHYA-OTHMAN anatujuza zaidi katika kitabu chake cha "A Biography of Julius Nyerere"-:
"Nyerere named one of Magige's sons Moringe, after Edward Sokoine, who was much beloved by Nyerere, and whose death in 1984 was absolutely devastating to him".
43. SOKOINE Alimchagua mwanae JOSEPH Kuwa Mkuu wa Familia
Kati ya watoto wake wote 11, SOKOINE alimpenda sana JOSEPH na alikuwa akimuamsha mara kwa mara usiku kuandika "notes" za masuala ya kitaifa. Jumamosi moja alimuamsha usiku wa manani na kumwambia amemteua yeye kuwa mkuu wa familia. JOSEPH akamwambia mbona kuna kaka zake wakubwa na pia kesho yake wanaenda kanisani asubuhi, si watachoka sana? SOKOINE akamjibu-:
"Nimezoea kufanya kazi hadi usiku mwingi ili kuwatumikia wananchi. Aidha, nina sababu zangu za kukuteua wewe kuwa Mkuu wa familia lakini usifikiri nakupa ufalme. La hasha. Nakupa utumwa na utumishi wa familia yangu".
Bw. JOSEPH alikuja kuwa Balozi na Naibu Katibu Mkuu.
44. "LANDCRUISERS" Zapewa jina la DUBE!
"Bongolanderz" ni viumbe wasioishiwa maneno. Kutokana na kuwa Bw. DUBE ndiye aliyeendesha gari lililomuua SOKOINE lilikuwa aina ya "Toyota Landcruiser", basi toka wakati huo, aina hiyo ya magari ikawa inaitwa "DUBE"!.
45. TAMATI
Huyu ndiye marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE, mmoja wa viongozi bora kabisa kuwahi kutokea nchini, ambaye alikuwa mzalendo wa kweli aliyewapenda wananchi wenzake kwa dhati kabisa ya moyo wake na aliyejitolea kwa hali na mali kuwasaidia na alichukia na kupambana vilivyo na wezi wa mali za umma, wala rushwa na walanguzi.
SOKOINE alikuwa mchamungu na alichukia maovu kwa dhati ya moyo wake na hakushiriki hata kidogo kwenye vitendo viovu.
46. Tafakuri Jadidi
46.1 Je, ni viongozi wangapi leo wanaweza kujitolea sehemu ya mshahara wao kusaidia wengine kama alivyokuwa akifanya SOKOINE?
46.2 Je, wewe kama Kiongozi ( iwe Kiranja darasani, kiongozi wa Kata Serikalini na kwingine) unamuenzi na kumuishi marehemu SOKOINE kama alivyoasa hayati Dr. JPM?
46.3 Kwakuwa maneno ya mwisho ya SOKOINE bungeni Idodomia alionya vikali na kusema "Jambo hili la kutumia fedha bila ya idhini ya Bunge lazima tulikomeshe", je Taifa linamuenzi kivitendo marehemu SOKOINE kwa kutofanya jambo hilo?
Na Mzee wa Atikali ✍️✍️✍️
atikaligbm@yahoo.com
0754744557
Atikali Hii Inalindwa na Hatimiliki
April 12, 2021.
Kwa nini hakuna kidonge cha kudhibiti uzazi kwa wanaume?



MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 12, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 12, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Makete, Festo Sanga Bungeni jijini Dodoma, Aprili 12, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 12, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillaly kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 12, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAFUNZO YA KUDHIBITI UADILIFU KWA KAMATI ZA MAADILI TAASISI ZA UMMA YAZINDULIWA LEO JIJINI ARUSHA
Mafunzo ya kudhbiti uadilifu kwa kamati za maadili kwa Tasisi za umma zilizopo jijini Arusha yameazinduliwa leo Makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki yaliyopo jijini Arusha. Ambapo washiriki wa mafunzo hayo wametakiwa kuhakikisha wanasimamia na kukuza maadili ya watumushi wa umma katika taasisi zao.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Dk.Remigius Kawala wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo amesema kuwa hatua ya kuwepo kwa kamati hizi za maadili katika taasisi za umma ni lengo la serikali katika kujali na kusimamia maadili mema kwa wafanyakazi wake.
“Hizi kamati zinalengo la kusimamia madili mahala pa kazi na kuondoa ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya watumishi wa umma unaosababisha uwepo wa masuala mbali mbali yakiwemo vitendo vya rushwa, ulevi, uonevu, n.k. Hivyo naamini haya mtayajadili kwa kina katika kuleta ufumbuzi wake huko kwenye kamati zenu” alisema Dk. Kawala.
Baadhi ya masuala yatakayojadiliwa kwenye mafunzo hayo ni pamoja na kanuni za maadili ya utumishi wa umma na namna ya kushughulikia malalamiko mbali mbali ya kimaadili,mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa, dhana ya rushwa mahala pa kazi na dhana ya mgongano wa maslahi.
Taasisi zinazoshiriki mafunzo hayo ni pamoja na CARMATEC, ATC, TEMDO na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).
KAMPENI KAMBAMBE YA MAZINGIRA KUZINDULIWA - JAFO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Ofisi yake inaandaa Kampeni kubwa ya Mazingira itakayoenda sambamba na mashindano katika ngazi mbalimbali ikihusisha upandaji miti, utunzaji na usafi wa mazingira kwa ujumla wake.
Akizungumza wakati wa kikao kazi na Menejimenti ya Ofisi yake pamoja na waandishi wa habari kilichofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, Mhe. Jafo amesema kampeni hiyo kubwa na ya aina yake itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani tarehe 5 Juni 2021 kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa kielelezo katika utunzaji wa mazingira.
“Kampeni hii kubwa itahusisha Mikoa yote 26 na itahusu usafi na Utunzaji wa Mazingira kwa ujumla wake ambapo tuzo na zawadi zitatolewa kwa washindi katika ngazi mbalimbali mara baada ya tathmini kufanyika na zawadi zitatolewa wakati wa Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka 2021” Mhe. Jafo alisisitiza.
Kampeni hii pia itashindanisha Majiji, Manispaa, Halmashauri za Miji na Majiji, Kata na Vijiji. Katika nyanja za elimu na Afya, Vyuo, Shule za Sekondari, Shule za Msingi Hospitali, Zahanati na Vituo vya afya pia zitashindanishwa.
“Tunafahamu changamoto kubwa za usafiri katika mashule yetu na taasisi za elimu ya juu, zawadi kama Magari, Pikipiki, Vifaa vya kufundishia na kompyuta zitatolewa, pia vifaa tiba katika sekta ya afya ikiwemo vitanda katika hospitali zitakazoibuka vinara zitatolewa” Jafo alisisitiza.
Makundi mengine yatakayoshindanishwa ni pamoja na Viwanda, Migodi, Hifadhi za Taifa, Madampo, Viwanja vya Ndege, Stendi za Mabasi, Masoko, Hoteli za nyota (1-5) na Waandishi wa Habari za Mazingira.
“Nataka kutoa rai kwa waandishi wa Habari wa magazeti, televisheni, bloggers na mitandaoni kushiriki katika kampeni hii na mashindano haya tuzo na zawadi zitatolewa kwenu” alisisitiza Mhe. Waziri
Aidha, ameiasa jamii na watanzania kwa ujumla kupanda miti rafiki kwa mazingira hususan ile ya matunda kulingana na jiografia ya maeneo yao kwa lengo la kuboresha na kuimarisha afya zao.
Katika kampeni hii kubwa na ya kipekee jumla ya washindi 152 kutoka makundi mbalimbali watapatikana na kupatiwa zawadi ikiwa ni pamoja na kupata fursa za kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za Wanyama hapa nchini.
BARABARA YA HAYDOM-MBULU KUJENGWA KWA LAMI
Na Mwandishi wetu, Mbulu
Naibu Waziri Kasekenya amesema barabara hiyo ya lami itaanza kujengwa kilomita 50 kwenye mwaka huu wa fedha unaoishia mwezi Juni mwaka huu.
Amesema wataanza kujenga barabara hiyo ili kutimiza ahadi ya Rais na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM ambayo imetamka ujenzi wa barabara hiyo.
"Ahadi zilizotolewa na hayati John Magufuli zitaendelea kutekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan hivyo barabara hii nayo itajengwa kama ilivyoahidiwa kwenu," amesema Kasekenya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dokta Chelestino Simbalimile Mofuga amemshukuru Naibu Waziri Kasekenya kulia kwa kuwapa ahadi hiyo kwani wananchi wataondokana na kero ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Maasay amesema barabara hiyo inatumika kusafirisha mazao, abiria na wengine kupelekwa hospitali ya rufaa ya Haydom kupata matibabu.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu mjini, Paul Isaay ameishukuru Serikali kwa kujenga daraja la mto Magara linalounganisha wilaya za Mbulu na Babati, hivyo ujenzi wa barabara ya lami ya Mbulu-Haydom itachochea maendeleo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa Kata ya Magara alipotembelea na kukagua daraja la Magara linalounganisha Wilaya za Babati na Mbulu Mkoani Manyara.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa Kata ya Haydom Mkoani Manyara juu ya ujenzi wa barabara ya lami, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dokta Chelestino Simbalimile Mofuga na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Maasay.
SEKTA YA HARUSI YAPEWA SHAVU
Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MCHAKATO Wa Tuzo za Wauzaji na Watoaji Huduma za Harusi maarufu Kama "Harusi Awards" lazinduliwa rasmi.
Akizungumza na Waandishi Wahabari Muwakilishi Kutoka Kampuni iliyoandaa Tuzo hizo 361 Degree Benedict Msofe amesema ni Wazi Kuwa Sherehe ni moja ya eneo ambalo Linatoa Fursa Mbalimbali .
"Sherehe ni moja ya eneo pana ambalo Watu wengi hujipatia kipato kwa sababu ya Mahitaji ya eneo husika,Sherehe itahitaji Chakula,Mapambo,Muziki,Mavazi na Kadhalika."
Msofe ameeleza Sababu ya Kuanzishwa Kwa jukwaaa la Tuzo za Harusi ni kutunuku ufanisi na ubora kwenye Sekta ya Harusi.
Aidha,Msofe ameweka wazi Maandalizi ya Tuzo hizo na Mpaka sasa Takribani ya Washiriki 65 katika Vipengele 20 Watawania Tuzo za Jukwaa la Harusi Kwa Mwaka huu ambapo zinatarajia Kufika kilele Mei 16 Katika Ukumbi Wa Serena hoteli huku kilele cha upigaji wa kula mwisho Mei 13.
Miongoni Mwa vipengele hivyo ni pamoja na Saluni bora,mpakaji makeup bora,Mapambo bora,Mshonaji bora,Mpishi bora wa Keki,Mpishi na Muandaaji wa Chakula kizuri na Vipengele vingine Vingi.
Kwa upande wake Mdhamini Wa Tuzo hizo Upendo Fatukubonye Kutoka Kampuni ya Uhakiki Usalama data pamoja na Mifumo ya Makampuni amesema Kazi yao kuu itakua ni Kuendesha Mchakato wa kupata Kura Kwa haki bila upendeleo kupitia tovuti husika.
ZEMBWELA NA BABA LEVO KUWATAFUTA WASHINDI WA CHEKA TU
*Wachekeshaji watakiwa kuipa kipaumbele Sanaa ya uchekeshaji
Na Khadija Seif Michuzi Tv
WASANII wa Vichekesho watakiwa kuijengea heshima tasnia hiyo.
Akizungumza na Michuzi Tv Conrad Kennedy maarufu Kama "Coy Mzungu" amesema kuwa tasnia hiyo ya uchekeshaji imekua ikidharaurika kutokana na wasanii wenyewe kutoipa kipaumbele na kuijengea heshima Kama tasnia zingine.
"Tunajiweka Sana nyuma matokeo yake unakuta tunadharaurika mno wakati Miongoni Mwa tasnia ngumu katika Sanaa ni uchekeshaji ni unatumia akili na maarifa Kumtoa mtu mawazo na kumfanya acheke na kusahau kwa wakati huo."
Mzungu amesema kuwa kupitia Kampuni yake ya "Cheka tu" imeamua Kuandaa Mashindano ya Kusaka vipaji vya Ucheshi yanayotarajia kuanza kufanyika mapema April mwaka huu.
"Mashindano hayo yanalenga Kuzalisha vipaji vya fani ya ucheshi si Kwa ajili ya Kusaka washindi pekee balu Kuinua vijana wenye uwezo."
Pia amesema Mashindano hayo yatafanyika katika Mikoa mitano ikiwemo Mwanza,Arusha,Mbeya,Dodoma na Dar es salaam ikijumuisha pande 3 wakiwemo washiriki,majaji na watazamaji na Majaji Kutoka wasafi Media Zembwela pamoja na Baba levo.
Mshindi wa Kwanza atazawadiwa Milioni 10 ,Mshindi wa pili Milioni 5 pamoja na Milioni 2 pamoja na kuwezeshwa kukuza vipaji vyao kwa kusainiwa kufanya kazi na "Cheka tu" huku dalali mwanamke akiwazawadia washindi watatu viwanja.


Sahara Tanzania expands petroleum product storage capacity to 72m litres
Sahara Tanzania Limited, a Sahara Group company, has expanded its storage capacity for petroleum products to 72 million litres in line with its commitment to promoting availability and reliability of top-quality products in Tanzania and other neighbouring African countries.
Since our Tanzania operations commenced in 2015, Sahara has expanded its infrastructure from 10 loading arms and 4 storage tanks with a combined storage capacity of 36million litres to 20 loading arms with 8 storage tanks, with a combined capacity of 72million litres, spurring economic development in Tanzania through availability of petroleum products,” said Olumuyiwa Aladejana, Country Manager, Sahara Tanzania Limited. The company has an ongoing expansion project aimed at increasing its storage capacity further to store more Automotive Gas Oil (AGO), Premium Motor Spirit (PMS) and JET A1. The project is expected to make Sahara Tanzania one of the largest storage terminals, providing an avenue for increasing employment opportunities and economic growth in Tanzania.
“It is also important to note that our terminal is automated, and we have since committed to the construction of 2 Liquefied Petroleum Gas (LPG) tanks which gives a total capacity of 6,000cbm as part of Sahara’s drive for technological innovation and enhancing access to clean energy in Tanzania, Rwanda, Zambia, Malawi and Congo,” he added.
Aladejana who was addressing media analysts on Sahara Tanzania’s performance, said the company was delighted at the opportunity to support the nation’s Vision 2025 as a leading player in the oil and gas sector, which contributes significantly to economic growth and development in Tanzania.
Vision 2025 represents Tanzania’s broad vision of its development goals as a middle-income country in 2025, characterized by high-quality livelihoods; peace, stability, and unity; good governance; a well-educated and learning society; and a competitive economy capable of sustainable growth and shared benefits. “Sahara Tanzania is committed to contributing to the achievement of this noble target through our operations in the energy sector and interventions by way of sustainable development projects in Tanzania. We commend the government’s robust policies and firmly believe Tanzania is on course to achieving the target and Sahara will continue to collaborate with all stakeholders in this regard,” he added.
Aladejana said it was heartening to see energy conglomerate, Sahara Group and other leading Africa energy companies ramp up their competitiveness in the global energy market. She however, noted that African countries need to harmonize their product specifications to boost intra-Africa transactions. “We see the world leaning towards cleaner fuel with lower carbon and Sulphur content. Standardized specifications will facilitate easy flow of products across African regions, ultimately making Africa more competitive, “ he said.
Also speaking, Mwajabu Mrutu, Business Development Executive at Sahara Tanzania Limited said Sahara Tanzania’s commitment to bringing benevolence to the nation is enshrined in its corporate citizenship programmes. Mrutu said Sahara Tanzania’s interventions include upgrading the Library at Pugu Secondary School that serves over 1000 students and the provision of toilets and washrooms at Salma Kikwete Secondary School to promote the Sustainable Development Goal that speaks to good hygiene and sanitation. The company has also implemented several youth empowerment interventions, including career guidance and personal finance advisory sessions and the widely commended #MyFutureStartsWithMe conference that urged young Tanzanians not to give up on their dreams.
MAKAMU WA RAIS PHILIP MPANGO AKABIDHI VYAKULA KWA WATOTO YATIMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Vifaa mbalimbali ikiwemo Mchele, Sukari, Mafuta Unga wa Ngano, Sabuni, pamoja na Vinywaji Baridi kwa ajili ya maandalizi ya Ufungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Unaotarajiwa kuanza hivi karibuni, katika Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Rahman Orphanege Centre Chang'ombe Jijini Dodoma leo April 12,2021, pamoja na Milango na Madirisha kwa ajili ya kumalizia Ujenzi wa Jengo la Madrasa ya Kituo hicho.
TAKUKURU MANYARA YAREJESHA SHAMBA LA URITHI
Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, imerejesha shamba la mjane wa Profesa Joshua Doriye aliyetaka kudhulumiwa na viongozi wa Kijiji cha Getanuwas Wilayani Hanang’.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati amesema mjane huyo wa Profesa Doriye aliyekuwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa wakati huo, alitaka kudhulumiwa shamba hilo na Mwenyekiti wa kijiji hicho Adam Maulid Mwanga.
Makungu amesema Profesa Doriye katika uhai wake kama ilivyo kwa watanzania wengine alikuwa na haki ya kumiliki mali ikiwa ni haki ya kikatiba iliyoainishwa chini ya ibara ya 24 (1) (2) katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomeka pamoja na madhumuni ya kutungwa kwa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Amesema kati ya mali alizofanikiwa kumiliki wakati wa uhai wake ni pamoja na shamba lilillopo kijiji cha Getanuwas wilayani Hanang’ mkoani Manyara.
“Mwaka 2019 mjane wa marehemu huyo Profesa Doriye wakati akishuhulikia shughuli ya mirathi Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Getanuwas Adam Maulid Mwangu kwa kushirikiana na watu wengine waliokuwa na nia ovu ya kutwaa shamba hilo alikataa kutambua umiliki wa ardhi wa marehemu Profesa Doriye katika kjiji hicho hivyo kukwamisha ufungaji wa shauri la mirathi namba 47/2019 uliokuwa ukiendelea mahakama ya mwanzo Kawe.
“Baada ya Mwenyekiti huyo kutotambua umiliki huo mjane aliwasilisha malalamiko yake TAKUKURU na tukaanzisha uchunguzi wa kina wa mjane huyo wa Profesa Doriye,” amesema Makungu.
Amesema uchunguzi wao umebaini kwamba marehemu Profesa Doriye alipewa shamba hilo na serikali ya kijiji cha Getanuwas tangu mwaka 1978 na umiliki wake haukuwahi kuangaliwa na mtu yeyote katika kipindi chochote na nyaraka zote kuhusu umiliki zipo na viongozi wa wakati huo wamethibitisha pasipo shaka umiliki wa shamba hilo kwa Profesa Doriye.
“Tulipomuhoji Mwenyekiti huyo wa kijiji wa sasa Adam Maulid Mwangu kupitia ushahidi wa nyaraka mbalimbali alionyesha kujutia kitendo alichomfanyia mjane, aliomba msamaha akieleza kwamba yeye hakuwahi kuziona nyaraka za umiliki wa shamba hilo na hivyo kukiri kumtambua mmiliki na kukiri kutomsumbua tena mjane na wanufaika wa shamba hilo,” amesema Makungu.
Amesema shamba hilo pamoja na nyaraka walikabidhi rasmi kwa mjane wa marehemu ili aweze kuendelea na utaratibu wa kufunga mirathi hiyo katika mahakama ya mwanzo Kawe.
“Tunawaonya baadhi ya wenyeviti wa vijiji wachache wa aina ya Adam Maulid Mwangu kuwa hawakuchaguliwa kwenda kutegua maamuzi halali yaliyoamuliwa na vikao halali vya serikali za vijiji zilizotangulia hasa katika eneo hili la ardhi, kufanya hivyo kama alivyofanya Mwangu kwa nia ya kujipatia ardhi ni matumizi mabaya ya madaraka na kinyume cha kifungu cha 31 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2017 na watakaobainika sharia itachukua mkondo wake,” amesema Makungu.
Alitumia nafasi hiyo kuwafahamisha wana Manyara na watanzania kwa ujumla kwamba ukisoma madhumuni ya kutungwa kwa sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa namba 11/2007 yameainishwa kwamba sheria hiyo imetungwa ili kuhakikisha kuwa wanaondokana na rushwa na dhuluma za aina zote na sheria hiyo imetungwa ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa na haki ya kumiliki mali aliyoipata kwa njia halali na umiliki huo utalindwa kwa msingi wa sheria kama ilivyofanyika kwa mali ya marehemu Profesa Doriye.
“Hivyo tunaendelea kuchukua hatua kwa wale wachache ambao kwa tamaa zao wanagombea nafasi za kisiasa zikiwemo uenyekiti wa mtaa na vijiji kwa nia ovu ya kwenda kupora mali za wananchi zilizopatikana kwa njia halali,’’ amesema Makungu. Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Babati.