Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119823 articles
Browse latest View live

WAITARA AAGIZA WANANCHI KUTUMIA FURSA YA SGR

$
0
0

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, kuhusu hatua ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR, Sehemu ya Makutupora-Morogoro, wakati alipokagua mwishoni mwa wiki, Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akimsikiliza Meneja Mradi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) anayesimamia Sehemu ya Makutupora-Morogoro, Mhandisi Mateshi Tito, akimweleza namna mashine ya kuunganisha mataruma inavyofanya kazi katika ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR, wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro., mwishoni mwa wiki.

Meneja Mradi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) anayesimamia Sehemu ya Makutupora-Morogoro, Mhandisi Mateshi Tito, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, nati za kufungia mataruma, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR, Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akiangalia sehemu ya mataruma iliyoungwa katika reli ya kisasa ya SGR, sehemu ya Makutupora hadi Morogoro, wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake, mwishoni mwa wiki.

Mmoja wa mafundi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), akifunga nati katika mataruma, katika kiwanda cha Mataruma kilichopo Igandu, Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma, mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akimsikiliza Mtaalam wa Maabara katika kiwanda cha Mataruma Kelvin Kimaro, akimweleza kuhusu ubora wa mataruma, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Igandu, Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Kisasa ya SGR Sehemu ya Morogoro- Makutupora, wilayani Kilosa, Mkoani, wakati Naibu alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Igandu, Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

……………………………………………………………………………………….

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amewataka wananchi wa Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro kuhakikisha wanatumia fursa ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (SGR) kujiimarisha kiuchumi kwa kuongeza uaminifu katika utendaji kazi wakati wa ujenzi.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa reli hiyo Sehemu ya Makutupora hadi Morogoro (KM 422), Naibu Waziri Waitara amesema kuwa uaminifu wao katika mradi huo utapelekea kuwea kupata fursa kwa wao kuajiriwa kama wafanyakazi baada ya mradi kukamilika.

“Mradi huu ni wa kihistoria na ninyi mmepata ajira hapa, tumieni fursa hii vizuri kwani mkifanya kazi hii kwa uaminifu, mradi unaweza kukamilika na mkapata ajira ya moja kwa moja kwenye shirika la reli” amesisitiza Naibu Waziri Waitara.

Aidha, Naibu Waziri Waitara amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anazingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba ili mradi huo uweze kuwa na matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.

Ameongeza kuwa kwa changamoto yoyote inayojitokeza lazima watendaji na wafanyakazi waziripoti kwa wakati na kwenye vyombo sahihi ili zisikwamishe mradi kukamilika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema mpaka sasa sehemu ya Makutupora hadi Dodoma imefikia asilimia zaidi ya 55 na kumuhakikishia Naibu Waziri kusimamia mradi huo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwenye mkataba.

Kadogosa amesema kuwa mpaka sasa suala la wafanyakazi limezingatia mkataba kwa kuwa na wafanyakazi wazawa asilimia 88 na wafanyakazi kutoka nje asilimia 12 na kusema kuwa shirika linaendelea kupata ujuzi utakaopunguza gharama kubwa za kuwarudisha wataalam kutoka nje mara baada ya mradi kukamilika.

Naye Meneja Mradi wa TRC Sehemu ya Makutupora hadi Morogoro, Mhandisi Mateshi Tito amesema kuwa licha ya uwepo wa changamoto za mara kwa mara ikiwemo mvua zinazoendelea kunyesha bado kazi ya ujenzi inaendelea vizuri na TRC imejipanga kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza.

Mradi wa reli ya Kisasa ya SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza wenye jumla ya Kilomita 1912, unatekelezwa kwa awamu tano ambazo ni pamoja na Dar es Salaam hadi Morogoro KM 300, Morogoro hadi Makutupora KM 422, Makutupora hadi Tabora KM 371, Tabora hadi Isaka KM 162 na Isaka hadi Mwanza KM 349 ambapo mpaka sasa Sehemu ya Dar-Moro, Moro-Makutupora na Isaka-Mwanza wakandarasi wanaendelea na mradi.

(Imetolewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.)


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.NDUMBARO AELEZEA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII INAVYOPAMBANA NA JANGA LA KORONA KATIKA SEKTA YA UTALII

$
0
0



Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Damas Ndumbaro amesema mashine za kupimia Virusi vya Korona kwa Watalii kwa sasa zimepelekwa na zinatoa huduma kwa watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na Arusha ikiwa ni Juhudi za makusudi zilizochukuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kukuza sekta ya utalii kwa kuondoa adha kwa Watalii wanaotembelea Vivutio vya Utalii nchini.


Aidha, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Wadau wa Utalii nchini kuendelea kushikamana ili kukiza sekta ya Utalii katika kipindi kigumu kinachoikabili sekta hiyo kutokana na janga la Virusi vya Korona huku Serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuendelea kupambana na ugonjwa huo.



Akizungumza na Vyombo vya habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara yaAfya...itaendelea kusogeza huduma hizo ikiwa ni jitihada mahsusi za kukabiliana na ugonjwa huo kwa lengo la kukuza sekta ya utalii nchini.

Amezitaja Jitihada hizo kuwa kwa sasa Watalii wataweza kupata huduma za vipimo vya Korona katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo awali huduma hiyo ilikuwa ikipatikana jijini Dar es Salaam pekee.

Amefafanua kuwa Watalii wanaotembelea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti watakuwa wakipatiwa vipimo vya ugonjwa huo baada ya hapo wanaendelea kutalii huku wakisubiria majibu ya vipimo vyao wakati hapo awali watalii hao walilazimika kukaa Dar es Salaam hadi pale majibu vya vipimo vitoke ndipo waweze kuanza kutalii

Pia, Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa upande wa Arusha imepeleka mashine ya kupimia Virusi vya Korona kwa lengo la kuwawezesha Watalii wote kupata huduma ya kupima virusi vya Korona ambapo hapo awali huduma hiyo ilikuwa ikitolewa Jijini Dar es Salaam pekee

Amesema mashine hizo mbili za kupimia Virusi vya Korona zilizopelekwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Jijini Arusha ni jitihada za Wizara hiyo baada ya kufanya mazungumzo na Wizara ya Afya... kwa lengo la kuwaondolea usumbufu Watalii kwa kukaa muda mrefu Jijini Dar es Salaam wakiwa wanasubiria kupatiwa majibu yao.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amempongeza Rais wa Tanzania, Mhe.Samiah Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kutaka kuunda timu ya kuchunguza kwa namna gani Serikali inaweza kukabiliana zaidi na na ugonjwa huu hasa kipindi hiki cha msimu wa Utalii unaokaribia.

Dkt.Ndumbaro ametoa wito kwa Wadau kuendelea kuufuata mwongozo wa Kujikinga na Virusi vya Korona uliotolewa mwaka jana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Afya  kwa lengola kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika hatua nyingine, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuchukua juhudi za makusudi katika kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini ambapo hivi karibuni jumla ya Watalii 15 waliwasili nchini wakitokea nchini Israeli.

Ameongeza kuwa Mwezi Mei mwaka huu Wizara inatarajia kupokea kundi lingine kubwa la Watalii wakitokea nchini Israel.

" Tunapambana usiku na mchana katika kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopon nchini katika katika nchi nyingi Duniani ili tuweze kupata Watalii wengi zaidi" alisisitiza Dkt.Ndumbaro

Akizungumzia athari za ugonjwa wa Korona katika Sekta ya Utalii nchini, Dkt.Ndumbaro amesema Tanzania imepata ahueni kubwa ambapo licha ya tishio la ugonjwa huo lakini imeendelea kupokea idadi ya kuridhisha ya Watalii kutokana na kulegeza masharti ugonjwa huo.

" Ukiona sisi Utalii umeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 kwa Wenzetu huko hali ni mbaya sana kwa sababu Watalii wengi ni Wasafiri wa kutoka nchi za nje, Nchi nyingi zimefunga mipaka yao, nchi nyingi zimefanya karantini" amesema Dkt. Ndumbaro

Katika hatua nyingine, Waziri Dkt.Ndumbaro amewaonya baadhi ya Watanzania kuacha mara moja tabia ya kuhusisha kila kifo kinachotokea kuwa kimetokana na ugonjwa wa Korona kuposti kwenye mitandao ya Kijamii, amesema hali hiyo imekuwa ikiharibu taswira ya nchi kwa kuonesha kuwa vifo vingi vinesababishws na Korona wakati sio kweli.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na vyombo vya habari jana Jijini Dar es salaam kuwa  mashine za kupimia Virusi vya Korona kwa  Watalii kwa sasa zimepelekwa  katika  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na Arusha ikiwa ni Juhudi za makusudi zilizochukuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kukuza sekta ya utalii kwa kuondoa adha kwa Watalii wanaotembelea Vivutio vya Utalii nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Allan Kijazi mara baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuzungumza na Vyombo vya habari jinsi inavyochukua hatua katika kupambana na Ugonjwa virusi vya Corona ambao umeathiri sekta ya utalii nchini kwa zaidi y asilimia 50 ambao Wizara katika kukabiliana nao imepeleka mashine mbili kwa ajili ya kuwapimia Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na Arusha

WIZARA KUJENGA VITUO 40 VYA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI, UHOLANZI YAVUTIWA

$
0
0

Na. Edward Kondela

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu amesema nchi yake iko tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya mafunzo ya ufugaji samaki nchini ili kuunga mkono mkakati wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inafikisha huduma za mafunzo hayo kila wilaya.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza jana (10.04.2021), mara baada ya kufanya mazungumzo na balozi huyo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam, amesema Mhe. Balozi Verheu ameridhishwa na mkakati wa wizara ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo arobaini vya mafunzo ya ufugaji samaki.

“Sisi kama wizara tumeanza na mkakati huo na tumetenga fedha kwa ajili ya vituo arobaini katika bajeti ijayo na kwamba wamesema wako tayari kusaidia kwa kuweka vituo vingine zaidi, tunataka kuweka vituo vya mafunzo kila wilaya kwa ajili ya wafugaji wa samaki wapate mahali pa kujifunza badala ya kwenda kwenye vituo ambavyo viko mbali.” Amesema Mhe. Ndaki

Kuhusu uchumi wa bluu Waziri Ndaki amesema balozi huyo amemhakikishia wanaweza kuisaidia Tanzania kupitia mpango wao maalum ujulikanao “Global Development Program” ambao unalenga kusaidia nchi zinazoendelea kwenye masuala ya uchumi wa bluu na kuiomba wizara iangalie maeneo ambayo inaweza kunufaika kupitia mpango huo.

Aidha, Mhe. Balozi Verheu ameisifia Zanzibar kwa hatua ilizofikia kuhusu uchumi wa bluu, huku Waziri Ndaki akimhakikishia pia Tanzania Bara imeweka malengo ya kutengeneza uchumi unaotokana na Bahari ya Hindi, maziwa na mabwawa.

Pia, katika Sekta ya Mifugo Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu ameonesha nia yake kubwa namna nchi yake iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili.

Waziri Ndaki amefafanua kuwa Uholanzi iko tayari kusaidia maeneo ya malisho ya mifugo pamoja na ushirikiano wa kitaalamu kwa kutoa utaalamu kwa watanzania nao kupata utaalamu kutoka kwa watanzania juu ya sekta ya mifugo.

“Nchi ya Uholanzi wameendelea sana katika tasnia ya maziwa na wamesema wako tayari kushirikiana na Tanzania katika kukuza soko la maziwa na wazalishaji wa maziwa ambapo hawako rasmi takriban asilimia 98, tunaweza kuwafanya hao wazalishaji wakawa rasmi na maziwa yao yakasaidia nchi kimaendeleo.” Amefafanua Mhe. Ndaki

Katika mazungumzo hayo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu wamekubaliana kuongeza wigo zaidi wa ushirikiano katika sekta za mifugo na uvuvi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu, mara baada ya balozi huyo kufika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es salaam, kwa ajili ya mazungumzo na Waziri Ndaki ambapo wamekubaliana kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta za mifugo na uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es salaam, ambapo balozi huyo amemhakikishia Waziri Ndaki nchi yake inaunga mkono mkakati wa wizara kujenga vituo vya mafunzo ya ufugaji samaki kila wilaya. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimsindikiza Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu mara baada ya kuwa na mazungumzo naye katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es salaam, ambapo katika sekta ya mifugo wamekubaliana kuhakikisha asilimia 98 ya wazalishaji maziwa nchini wasio rasmi wanakuwa rasmi katika kukuza maendeleo ya nchi

SERIKALI KUOWANDOA KWENYE MPANGO WANUFAIKA WA TASAF WATAKAOSHINDWA KUTUMIA RUZUKU KUBORESHA MAISHA YAO

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja Uhawilishaji Fedha wa TASAF Bw. Selemani Masala, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Nkala Wilayani Momba.

Baadhi ya wananchi Kijiji cha Msangano Wilayani Momba wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa TASAF katika kijiji hicho.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimpatia fedha mnufaika wa TASAF Kijiji cha Nkala Wilayani Momba, Bi. Sarafina Simfukwe mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake na kuona maendeleo aliyoyapata kutokana na ruzuku anayoipokea kutoka TASAF. 

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF Kijiji cha Nkala wilayani Momba wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.

Baadhi ya wananchi Kijiji cha Nkala Wilayani Momba wakinyoosha mikono hewani kuashiria ni wanufaika wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa TASAF katika kijiji hicho.

Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condesta Sichalwe akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na wananchi, kijiji cha Msangano wilayani Momba wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji wa Mpango wa TASAF katika kijiji hicho

…………………………………………………………

Na. Veronica Mwafisi-Momba

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, Serikali haitosita kuwaondoa wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini watakaoshindwa kutumia vema ruzuku wanayopewa na TASAF ili kuboresha maisha yao kama ambavyo Serikali imekusudia.

Mhe. Ndejembi amesema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vya Msangano, Nkala na Chiwanda Wilayani Momba na kuongeza kuwa, baada ya mwaka mmoja atarejea kujiridhisha kama fedha za ruzuku zilizotolewa kwa kaya maskini zimetumika vizuri kuboresha maisha hivyo kaya zitakazobainika kutumia tofauti na malengo zitaondolewa kwenye mpango.

Amesisitiza kuwa, ni wajibu wa kila mnufaika kutumia ruzuku anayoipata katika shughuli zitakazomuongezea kipato kama kilimo na ufugaji ili kuboresha maisha yake, na kuongeza kuwa Maafisa Ugani wana jukumu la kuhakikisha wanawasaidia wanufaika kufuga na kulima kisasa.

Amewaasa wanufaika juu ya ruzuku wanayoipata kuwa si kwa ajili ya anasa kwani Serikali inatoa kwa kaya maskini ili kuziwezesha kujikwamua kwenye lindi la umaskini.

“Serikali inatoa fedha kwa kaya maskini ili ziweze kujishughulisha na ufugaji, kilimo na ujasiriamali na baada ya muda ziweze kuondokana na umaskini” Mhe. Ndejembi amefafanua.

Kuhusiana na Kijiji cha Msangano ambacho hakijanufaika na Mpango wa TASAF toka uanze, Mhe. Ndejembi amewaahidi wananchi wa kijiji hicho kuwa, ifikapo mwezi Julai kaya maskini kijijini hapo zitaanza kunufaika na TASAF.

Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amewataka Watendaji wa Serikali kutokata fedha za ruzuku za wanufaika kwa ajili ya kuchangia huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na michango mingineyo kwani fedha hiyo ni yake kwa ajili ya kuboresha maisha yake. 

Mhe. Ndejembi amesisitiza kuwa, kama kuna mchango wowote ni wa hiari hivyo si lazima akatwe ruzuku yake, na kuongeza kuwa mnufaika apewe fursa ya kuitumia fedha kujiendeleza kiuchumi katika ufugaji au kilimo ili akifuga na kuvuna achangie kwa hiari yake mwenyewe.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewahakikishia wananchi wa vijiji vya Msangano, Nkala, Chiwanda na maeneo mengine kuwa, Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuzijali kaya maskini kwa kuzipatia ruzuku, hivyo amezitaka kutumia vizuri ruzuku hizo ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya kaya maskini nchini. 

Mhe. Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Momba kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa hivi karibuni kwa Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condesta Sichalwe wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa. 

MAUAJI YA VIKONGWE SHINYANGA SASA NI HISTORIA-RC SHINYANGA

$
0
0

 

Baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama Shinyanga wakishiriki kikao cha Championi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni Mkoani Shinyanga.

 Baadhi ya washiriki wa kikao cha Championi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni Mkoani Shinyanga kilichofanyika jana mkoani umo.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha Championi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni Mkoani Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja jana mara baada ya kushiriki kikao hicho.

……………………………………………………………………………………….

Na Anthony Ishengoma-Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amesema Mkoa wa Shinyanga hauna tena mauaji ya vikongwe kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na vyombo vya vya ulinzi na usalama zilizofanikisha kuyakamata makundi ya mapanga yaliyokuwa yanatekeleza mauaji hayo Mkoani Shinyanga.

Bi. Telack alisema hayo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha siku moja na Shirika la Msichana Initiative na Championi wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga kilichowakutanisha baadhi ya wabunge ambao wanaunda kikundi hicho pamoja na wadau wengine waliokutana leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Bi. Telack aliongeza kuwa kipindi cha nyuma vyombo vya habari kila kukicha vilikuwa vinaandika sana kuhusu mauaji ya mama wazee waliokuwa wanauawa kutokana na ramli chonganishi lakini sasa hali ni shwari na vyombo vya habari havitoi tena habari za mauaji hayo kwani hayapo tena.

Kuhusu mimba na ndoa za utotoni Bi. Telack alisema kuwa juhudi zilizofanyika ni pamoja na kukamata watoto wakiwa wanafungisha ndoa na juhudi hizo zilifanyika baada ya Mkoa huo kuwa na takwimu za juu kwani awali Mkoa wa Shinyanga uliongoza 59% ya ndoa za utotoni Nchini.

Bi Telack alisema msukumo wa mikakati ya kupambana na mimba na ndoa za utotoni ulitokana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kutoa takwimu hizo kwa Mkoa wa wake wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyoadhimisha Kitaifa Mkoani Shinyanga mwaka 2016. 

Bi. Telack aliongeza kuwa wanaume ambao wamekamatwa kwa kuwapa mimba watoto wa shule wamekuwa wakipata kifungo cha miaka 30 jela pomoja na changamoto ya baadhi ya Wazazi kushawisi watoto wao wasitoe ushahidi mahakamani lakini pia na wasimamizi wa sheria kwa kushirikishwa katika masuala haya kwa sasa hakuna ucheleweshaji kesi hizi.   

Bi. Telack amewataka wanaume kutambua kuwa mtoto wa mwenzeke mwenye umri sawa na mtoto wake sio mke kama ilivyo kwa mtoto wake hivyo wawachukulie watoto wa wenzao kama watoto wao na hivyo kukomesha vityendo vya mimba na ndoa za utotoni ili kutoa fursa kuwalinda watoto wakike.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative Bi. Rebeca Gyumi amewaambia wabunge machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni kuwa lengo la kikao hiki ilikuwa ni kuwapa fursa kwao kufahamu juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Shinyanga katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili iwe fursa kwao kutumia uzoefu huo kwa bunge lakini pia katika maeneo yote ya Tanzania.

Aidha Bi. Ng’washi Damasi Kamani Mbunge viti  maalum Vijana Mkoa wa Shinyanga amesema kuwa anafahamu sana mira na desturi za wasukuma na madhara yake kwa wanawake na hivyo kutumia fursa hiyo kupongeza juhudi za mkoa na kuwataka wazazi mkoa wa Shinyanga kuwasomesha watoto wakike ili waweze kufikia ndoto zao.

Bi. Ng’washi amewataka wazazi kote nchini kujifunza kutokana na uwepo wa mwanamke mwenye nafasi ya juu ya uongozi Nchini akimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamke na hivyo kuwataka kusomesha watoto wakike wakiamini kuwa ipo siku mtoto wao anaweza kubahatika kushika kiti kikubwa cha uongozi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Wanawake Waislam na Mbunge wa Zamani wa Bungela la Jamhuri wa Tanzania Bi. Shamim Khani amewataka wabunge ambao ni Chamipioni wa Ukatili wa Ndoa za Utotoni kukaribisha Uongozi wa Mkoa Bungeni kwa lengo la kutoa Elimu hii kwa wabunge ikiwemo pia kutambulisha Mkakati wa Mkoa wa Kukambana na Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

Bi. Shamimu amewataka viongozi wa dini hapa Nchini kutumia nafasi waliyonayo katika jamii kutoa elimu kwa wafuasi wao kuhusu utokomezaji wa mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa wanayo nafasi kubwa zaidi ya kushawishi jamii kutokomeza vitendo hivyo.

Naye Championi wa Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto Mbunge Bi. Aid a Kenani amesema kuwa ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake hatuwezi kumuacha mdau muhimu mwanaume kwani wanawake peke yake hawataweza bila kuanza na chanzo cha ukatili.

Bi. Kenani Aliongeza kuwa wabunge wako hapa kujifunza mbinu zilizotumiwa na mkoa wa Shinyanga kukomesha ukatili inabidi kuigwa ili ziweze kutumika maeneo mengine kwa kuwa tatizo hili haliko Shinyanga peke yake bali ni Tanzania nzima uku akiwaimiza viongozi wa dini kuimiza waumini hao kuacha dhambi ya uzinzi.

Mkoa wa Shinyanga tayari umekamilisha na kuzindua Mkakati wa Kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkakati unaotokana na Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ujalikanao kama NPA-VAWC 2017/18-2021/22.

MSICHANA INITIATIVE NA MACHAMPIONI WAO WAKUTANA NA WADAU WA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI SHINYANGA

$
0
0
Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakiongozana na Machampioni wao wa kutokomeza ndoa za utotoni wakiwemo wabunge na viongozi mbalimbali wamefanya ziara mkoani Shinyanga na kufanya kikao cha pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, Sekretarieti ya mkoa, Kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto, kamati ya amani ya mkoa na wadau wa ndoa za utotoni mkoa wa Shinyanga ili kujadili namna ya kushirikiana pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumamosi Aprili 10,2021 kikiwa na lengo kujadili mafanikio na mikakati ya kupambana na matukio ya ndoa za utotoni kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amesema wamekuja kujifunza mikakati inayofanyika mkoani Shinyanga katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto zikiwemo ndoa za utotoni ili kuangalia namna ya kutumia mikakati hiyo katika maeneo mengine nchini.

“Tumekutana na wadau wa ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara ya Shirika la Msichana Initiative tukiongozana na Machampioni wetu wa kutokomeza ndoa za utotoni ambao ni wabunge na baadhi ya viongozi mbalimbali”,amesema Rebeca.

“Kupitia ziara hii tukaona ni muhimu Machampioni wakae kwenye kikao pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga,kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto,kamati ya amani ya mkoa na wadau wa ndoa za utotoni mkoa wa Shinyanga ili kujua jitihada zinazofanywa mkoani Shinyanga katika mapambano dhidi ya ndoa za utotoni na nini tufanye kwa pamoja kama njia ya kuhakikisha hili suala linatokomezwa”,ameeleza Rebeca.

Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenani ambaye ni miongoni mwa Machampioni hao amesema suala la ukatili dhidi ya wanawake na watoto siyo jambo la Shinyanga tu bali ni la nchi nzima hivyo wamekuja kuchukua mbinu zilizotumika mkoani Shinyanga katika kulinda mtoto wa kike akieleza kuwa wamepata uzoefu mpya wa jinsi ya kukabiliana na changamoto ya ukatili kwa mtoto wa kike.

“Kazi mliyoifanya Shinyanga ni kubwa sana. Niwapongeze sana kwa kuandaa kuunda Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025, naona mmeandika kwa lugha ya Kiingereza naomba muandike pia kwa lugha ya Kiswahili ili hata wananchi wa kawaida waweze kuelewa na kuachana na vitendo vya ukatili”,amesema Khenani.

“Ili kutokomeza ukatili Sheria peke yake haiwezi kumaliza tatizo hili ambalo lipo nchi nzima. Lakini pia ni lazima tumshirikishe mwanaume kwa sababu ndiyo chanzo. Ni lazima pia wadau wote tushirikiane, tuachane na mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike”,ameongeza.

Akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia, Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kumaliza mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kufuatia mikakati kabambe iliyowekwa na mkoa huo.

Telack amesema miongoni mwa mikakati iliyofanyika ni kufanya utafiti na kuwabaini na kuwakamata watu waliokuwa wanawakata mapanga watu wenye ualbino na vikongwe.

“Baada ya Mhe.Rais kutupa dhamana ya kumsaidia kazi katika mkoa wa Shinyanga mwaka 2016,tulianza kwa kubaini changamoto kubwa zilizokuwepo katika mkoa wetu wa Shinyanga ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni mauaji ya watu wenye ualbino,vikongwe na ukatili wa kijinsia unaojumuisha kuwapa mimba mabinti wadogo,ubakaji,mila na desturi kandamizi kwa wanawake”,amesema Telack.

Amesema kufuatia takwimu za utafiti wa Maendeleo ya watu na afya Tanzania (TDHS,2010) zilizoonesha kwamba mkoa wa Shinyanga ulikuwa unaongoza kwa kuwa na ndoa za utotoni kwa asilimia 59, kitendo hicho hakikumfurahisha akaamua kuwaita viongozi wenzake na wadau mbalimbali na kuweka mikakati thabiti ya kukomesha changamoto hizo zote.

“Tulijipa muda wa kufanya utafiti wa kuwabaini wale wote waliokuwa wanawakata mapanga watu wenye ualbino na vikongwe. Tulifanya utafiti huu kwa siri kubwa, tuliwatumia wananchi wenyewe katika ngazi za vijiji wakati wa kupata taarifa,tuligundua kwamba wakata mapanga wakifanya uhalifu huo walikuwa wanakimbilia mikoa ya jirani kwa hiyo tukashirikiana na viongozi wenzetu wa mikoa jirani”,ameeleza Telack.

“Baada ya utafiti wetu wa siri kukamilika,tulianza kuwakamata mmoja baada ya mwingine mpaka tukawamaliza wote.Baada ya kujiridhisha kwamba wote wamekamatwa,tukawafikisha kwenye vyombo vya sheria na tukaendelea kuzisimamia kesi hizo mpaka haki ikatendeka. Tangu mwaka 2016 hadi mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe katika mkoa wetu imebaki historia na sasa ukisikia kuna mauaji basi ni yale yanatokana na ugomvi wa mashamba watoto wakitaka kurithi ardhi ambayo nayo tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha nayo yanakoma”,ameongeza Telack.

Amesema pia waliunda na kutoa mafunzo ya kamati za ulinzi na usalama wa wanawake na watoto kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji na mpaka sasa kuna kamati moja ya mkoa, kila halmashauri na kata 130 kila kata ina kamati moja na kamati zote zimepewa mafunzo ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.

Amefafanua kuwa mkoa huo umeendelea kufanya vikao mbalimbali na taasisi mtambuka za serikali zinazohusiana na kesi za watoto na akina mama wanaofanyiwa ukatili ili kuwa na nguvu ya pamoja na kuharakisha upelelezi wa makosa yote ya jinai yanayohusiana na ukatili wa kijinsia pamoja na mimba na ndoa za utotoni.

“Pia tumetoa mafunzo kwa wasaidizi 223 wa huduma za msaada wa kisheria juu ya haki ya ustawi wa watoto pamoja na kukutana na waganga wa kienyeji,viongozi wa kimila na viongozi wa dini ili kuondoa mila na desturi kandamizi kwa wanawake na watoto”,ameeleza.

“Tuligundua kuwa wananchi wengi wanaojihusisha na vitendo viovu kwa wanawake na watoto hawana hofu ya Mungu hivyo tukaamua kuunda Kamati ya Amani ya Mkoa yenye wajumbe 10 kutoka madhehebu mbambali ya dini,tukaipa jukumu la kuwafikia wananchi wote ndani ya mkoa na kuzungumza nao kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na sasa wananchi wameanza kubadilika kwa kuingiwa na hofu ya Mungu”,amesema Telack.

Ameongeza kuwa ili kuondoa kabisa changamoto ya ukatili wa kijinsia pamoja na na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,mkoa wa Shinyanga uliamua kuunda Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025).

Mkuu huyo wa mkoa amesema kufuatia mikakati hiyo kabambe,hivi sasa kesi zote zinazohusisha ukatili wa aina yoyote ile kwa mtoto wa kike zinafanyiwa kazi haraka kwa kukamilisha uchunguzi pamoja na mahakimu kutoka hukumu kwa wakati.

Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiatives, Rebeca Gyumi kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusimamia haki za mtoto wa kike.

Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuzungumza na watoto wao kuhusu masuala ya ukatili na kuhakikisha wazazi wote (baba na mama) wanashiriki katika malezi ya watoto badala ya watoto kulelewa na mama pekee ama dada wa nyumbani.

Pia ameeleza kuwa mkoa wa Shinyanga una mpango wa kuleta mabasi kwa ajili ya kuwapeleka wanafunzi shuleni ambapo wazazi watakuwa wanawapa nauli watoto wao.

Akiwasilisha maazimio ya kikao hicho, Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia amesema wamekubaliana kuzuia uzururaji wa mtoto,kuanzisha mabasi ya kubeba watoto na kuzuia watoto kwenda kuchunga mifugo pamoja na kuhakukisha marekebisho ya sheria ya ndoa 1971 yanafanyika bungeni na kualika mkoa wa Shinyanga na wadau waende bungeni kutoa uzoefu kuhusu Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto na mwanamke Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao. Mbele kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba akifuatiwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga ACP Elizabeth Mbezi (katikati) na  Mwakilishi wa Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga (Mwanasheria wa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga) Elizabeth Godfrey Kaka wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (kulia) ambapo ni Ma Champion wa kutokomeza ndoa za utotoni wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wanaharakati wa haki za wanawake (Champion wa kutokomeza ndoa za utotoni) John Myola na Nancy Sumari wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mwenyekiti  Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Hajat Shamim Khan  ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Amani taifa akionesha Mpango Mkakati wa Mkoa wa Shinyanga Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025) ambapo ameupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa mpango huo na kushauri waandaaji wa mpango huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack waitwe bungeni kuelezea ili mikoa mingine iige ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya wanawake na watoto.
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti  Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Hajat Shamim Khan  ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Amani taifa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Ng'wasi Damas Kamani akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ambapo alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni lazima wanaume pia washirikishwe katika mapambano hayo.
Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ambapo alisema kamati hiyo inaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali na wadau katika kulinda haki za wanawake na watoto.
Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa shirika  la Investing in Children and their  Societies(ICS), Kudely Sokoine akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani akiomba Mpango Mkakati wa Mkoa wa Shinyanga Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025) uandikwe pia kwa lugha ya Kiswahili
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto na mwanamke Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao. Mbele kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga ACP Elizabeth Mbezi (kulia) wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga

Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Ma Champion wa Kutokomeza ndoa za utotoni
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake mkoa wa Shinyanga na Sekretarieti ya mkoa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wadau wa haki za wanawake na watoto kutoka mashirika mbalimbali.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI UGANDA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe Sam Kutesa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe alipowasili nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumapili Aprili 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe Sam Kutesa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe alipowasili nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumapili Aprili 11, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wa Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe alipowasili nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumapili Aprili 11, 2021

 

RAIS SAMIA AKARIBISHWA NA MWENYEJI WAKE RAIS MUSEVENI WA UGANDA IKULU YA ENTEBBE ALIPOWASILI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021. PICHA NA IKULU. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akikaribishwa na  mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kwa mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitambulisha ujumbe wa Tanzania alioongozana nao kwa mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitambulisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Dkt Mataragio kwa mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili katika Ikulu ya Entebbe leo Jumapili Aprili 11, 2021

BILIONI 12.6 ZATUMIKA UJENZI WA DARAJA LA MAGARA

$
0
0

 

Sehemu ya Daraja la Magara lenye urefu wa meta 84, lililokamilika kujengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG), kwa gharama ya shilingi bilioni 12.6 kwa kipindi cha miezi 24. Daraja hilo liko kwenye mto Magara eneo la Mwada katika barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akimuelekeza jambo Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Manyara Mhandisi Bashiri Rwesingisa (wa kwanza kushoto) wakati akikagua Daraja la Magara katika Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akiongea na baadhi ya wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini eneo la Haydom, alipopita kukagua barabara ya Mbulu hadi Haydom Kilometa 81 inayoombewa fedha na mbunge wa jimbo hilo ili iweze kujegwa kwa kiwango cha lami.

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini eneo la Haydom, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), alipopita kukagua barabara ya Mbulu hadi Haydom Kilometa 81, inayoombewa fedha na mbunge wa jimbo hilo ili iweze kujegwa kwa kiwango cha lami.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Ghaibu Lingo, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akikagua barabara ya Mugitu hadi Haydom Kilometa 68.35 katika eneo la ziwa Basoutu, barabara inayoombewa fedha na Mbunge wa jimbo la Hanang ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. 

………………………………………………………………………..

Ujenzi wa Daraja la Magara lililo umbali wa kilometa 21 kutoka barabara kuu iendayo Arusha eneo la Magara katika barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu (Kilometa 50.5), mkoani Manyara umekamilika. 

Akikagua daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewaambia waandishi wa habari kuwa ameridhishwa na ujenzi wa Daraja la Magara ambalo ujenzi wake umekamilika ndani ya muda kama ilivyo kwenye mkataba wake. Ameeleza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

“Serikali ya awamu ya sita itaendelea kusimamia uboreshaji wa miradi miundombinu ya barabara kama ilivyo kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa miradi yote na ahadi zote zitaendelea kutekelezwa na serikali yake ili kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi zitakazopelekea maendeleo kwa taifa letu.” Amesema Mhandisi Kasekenya.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange, ameishukuru serikali kwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Magara kwa wakati, ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutawezesha ukuaji wa shughuli za kilimo na ufugaji kwa wananchi wa mkoa wa Manyara na kwamba serikali ya wilaya itahakikisha miundombinu ya daraja la Magara haihujumiwi ili kuilinda thamani ya mradi wa ujenzi wake.

Akisoma taarifa ya mradi huo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara Mhandisi Bashiri Rwesingisa amesema kuwa, mradi wa Ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa meta 84, umefanywa na kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG) kwa gharama ya shilingi bilioni 12.6 kwa kipindi cha miezi 24 kwa mujibu wa mkataba wake, kuanzia Februari 2018 hadi Februari 2020 na kwamba kipindi cha matazamio cha mwaka mmoja tayari kimeisha bila tatizo lolote.

Naibu Waziri Kasekenya alikuwa mkoani Manyara kwa ziara ya siku mbili kukagua barabara za Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu Kilometa 50.5, Mbulu hadi Haydom Kilometa 81, Mugitu hadi Haydom Kilometa 68.35 na Singe kwenda Kimotorok hadi Sukuro Kilometa 155, zinazoombewa fedha na wabunge wa Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini na Babati Vijijini ili ziweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Makamo mwekiti Act wazalendo wateta Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar

$
0
0

 

 Makamu wa Mwenyeikiti wa chama cha  ACT wazalendo Juma Duni Hajji kizungumza na Makamu wa Kwanza Wa Rais zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa Othman Masoud Othman Shariff alipofika Afisi Kuu ya Chama hicho Vuga Mjini Zanzibar kwa Ajili ya kuhudhuria  Kikao cha Kamati Maalum ambapo kwa Upand wa makamu huyo ni kikao cha kwanza chama kuhudhuria.

COCA-COLA TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YA SISIMUA MAISHA NA FANTA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 


Mtangazaji wa East Africa TV, Kelvin Lyimo maarufu kama ‘Kevoo’ (kulia) akifurahia picha ya pamoja na wanafunzi wa Sekondari wa jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana. 

Kutoka kushoto ni Mtangazaji wa vipindi vya Televesheni Salama Jabir, Winnie Nzunda na Rukia Yazid wakishiriki kwenye baadhi ya michezo iliyofanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kulia) na Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Fredrick Mtui wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ ndani ya treni la abiria linalofanya safari kati ya Ubungo na Stesheni lenye chapa ya rangi mbalimbali za Fanta. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania hivi karibuni jijini Dar es Salaam ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.


Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-fm, Hamis Mmandi al-maarufu B-dozen akifurahia jambo na marafiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.

Mshereheshaji kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Fanta ya ‘Sisimua maisha na Fanta’ Japhet Mwaipopo akiuliza maswali kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.

Wapenzi wa soda ya Fanta jijini Dar es Salaam wakifurahia uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ ndani ya treni la abiria linalofanya safari kati ya Ubungo na Stesheni lenye chapa ya rangi mbalimbali za Fanta. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania hivi karibuni jijini Dar es Salaam ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.

Mtangazaji wa kipindi cha Genge cha E-fm al-maarufu ‘Fido’ (kushoto) na Mtangazaji wa East Africa Radio, ‘DullahPlanet’ wakifurahia picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ ndani ya treni la abiria linalofanya safari kati ya Ubungo na Stesheni lenye chapa ya rangi mbalimbali za Fanta. Kampeni hiyo imeziduliwa na Coca-Cola Tanzania hivi karibuni jijini Dar es Salaam ikilenga kuhamasisha burudani, rangi na michezo mbalimbali inayopendwa na vijana.

GSM GROUP KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUHUSU UWEKEZAJI, WAZINDUA MADUKA MPYA KATIKA JENGOLA SALAMANDER TOWER JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

UONGOZI wa Kampuni ya GSM Group umeweka wazi utaendelea kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imesisitiza itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maduka mapya ya mitindo yaliyoundwa maalum kuhudumia mahitaji ya watu kwa jinsi zote, umri wote na haiba zote, Ofisa Mtendaji Mkuu wa GSM Group Fatma Abdallah amesema wanajisikia fahari kuendelea kuwa kitovu cha kibiashara ambacho kimetoa na kitaendelea kutoa ajira ,kutengeneza fursa za kibiashara,kuchochea ndoto za wote wanaokuja na kuchangia uboreshaji wa biashara ndani ya Tanzania.

Fatma Abdallah amefafanua GSM Group wamefurahishwa na kauli ya Rais Samia ambaye ameendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji na kwamba siku zote wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za viongozi wakuu wa nchi kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua.

" Tutaendelea kuunga juhudi za Serikali yetu katika kuhakikisha GSM Group tunashiriki kikamilifu katika eneo hili la uwekezaji na kufanya biashara kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,"amesisitiza.

Akizungumzia uzinduzi wa maduka mapya yaliyopo kwenye jengo la Salamander Tower ambayo ni ya Babyshop,Splash,Max na Shoexpress yote yakiwa ndani ya jengo moja ,jengo jipya na la kisasa katika Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam amesisitiza inaonesha jinsi ambavyo GSM Group imeamua kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi.

Awali akizungumzia uzinduzi wa maduka katika jengo hilo la Salamander, Ofisa Biashara wa GSM Group Allan Chanjo amesema wanamshukuru Mungu kwa kuwapatia nafasi nyingine na ya kipekee kabisa kushuhudia uzinduzi mkubwa kabisa ambapo GSM Group kupitia GSM Retail wanafungua maduka mapya ya mitindo yaliyoundwa maalum kuhudumia mahitaji ya watu wote.

"Dhumuni na tumaini letu tulipoamua kufungua maduka haya ndani ya Salamander Tower sio tu kuwafanya watu waingie na kununua,bali nia yetu inaenda mbali kwa kuwa sehemu ya kitovu cha biashara ambacho kimeendelea kutoa ajira, kwani tumetoa ajira zaidi ya 3000 hadi sasa na kwa jinsi tunavyoendelea kuwekeza tutatoa ajira zaidi,"amesema Chonjo.

Aidha amesema kama biashara,faida na matokeo chanya ambayo wameyapata sio ya kwao peke yao bali ni ya sote, jamii na nchi kwa ujumla hasa wanapoanza safari mpya pamoja na Watanzania."Tunaamini tutaendelea kukua nanyi, tukishirikiana katika kila hatua."

Amesisitiza " Na kitu ambacho leo ningependa tutafakari pamoja ,kwenye uzinduzi huu ni Ujumbe wa maandishi (almaarufu text) .Ninaamini wote leo tumepokea  na tumetuma text ,kwa kifupi kutumiana text imekua ni mtindo wa maisha na imebadili kabisa jinsi tunavyowasiliana, unaweza kusema kuna ujumbe unaotumwa na text kwa kila mmoja wetu katika maisha.

"Kina text kea mabosi zetu,wafanyakazi wenzetu na wafanyabiashara wenzetu, kuna text kwa wapenzi wetu zinazoambatana na viomoji vya makopakopa ,kuna text kwa marafiki zetu zenye majina ya utani na lugha mnayoielewa ninyi tu, kuna text kwa wanafamilia zinazotukumbusha sisi na familia na tunapendana hata bila kusema na kuna text ya kwanza haha msiofahamiana ambayo akiisoma tu anajua wewe ni nani,"amesema Chonjo.

Amesisitiza kwamba angependa wote wayafikirie mavazi wanayovaa au mitindo wanayotaka kuichagua kuwa ni text inayotuma ujumbe kwa mabosi wao,wafanyakazi wao,wafanyabiashara wenzao,wapenzi wao,marafiki zao na kwa namna ya kushangaza hata watu wasiowajua au wanaowajua kila siki kwa namna fulani.

Aidha amefafanua Babyshop ni ujumbe unaongea moja kwa moja na watoto ( miaka 0-14), Splash ni ujumbe unaongea moja kwa moja na mabasi,wafanyakazi,wafanyabiashara wenzako kwamba wewe ni mtanashati, Max ni ujumbe rahisi kwa familia kwamba wanaweza kupata kila wakitakacho kwa kila mmoja ndani ya duka moja wakati Shoexpress ni ujumbe rahisi kuyaambia mavazi yako kwamba "hujakamilika bila mimi".

Chonjo amesema wanawaambia wanawataarifu wateja wao ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kwenye maduka yao yaliyoko Mlimani City,GSM Mall Msasani ,Pugu Mall na Aura Mall kuwa wamefungua maduka hayo kwa ajili yao."Sasa tunaweza kufanya kazi na kufanya manunuzi yetu hapahapa katialkati ya Jiji la Dar es Salaam (ndani ya Posta).

"Na kwa kuanza tuna of maalum kwa ajili ya wateja wetu wote wapya na tuliokuwa tayari tunawahudumia kupitia maduka yetu mengine kuanzia Aprili 9 mpaka Aprili 11,2021 ambapo kila ukimaliza manunuzi yako ,ukiwa kaunta,utapasua puto na kujihakikishia punguzo la hadi asilimia 50,"amesema.

Msemaji wa Chapa ya GSM Antonio Nugazi(wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kabla ya kukata keki baada ya kuzinduliwa rasmi kwa maduka mapya ya Kampuni za GSM Group katika jengo la Salamander eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam, wengine katika picha hiyo ni baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo pamoja na wageni waalikwa .Wa kwanza kushoto ni Msanii Omar Nyembo maarufu kwa jina la Ommy Dimpoz ambaye ni balozi wa GSM.
Utepe ukikatwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jengo la Salamander Tower pamoja na maduka mapya ya GSM Group katika eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam.
Ofisa Biashara wa Kampuni ya GSM Group Allan Chonjo akiangalia nguo katika moja ya maduka ya GSM  baada ya kuzinduliwa.Maduka hayo yapo katika jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wa timu ya soka ya Yanga Carlos Carlinhos akichagua fulana baada ya kuingia kwenye maduka ya GSM  yaliyopo jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shetta (wa kwanza kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa akipiga makofi wakati wa ufunguzi  wa maduka ya GSM Group yaliyopo jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wachezaji wa timu ya soka ya Yanga wakiwa makini kusikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa uzinduzi wa maduka ya GSM Group.



Rais Samia na Museveni washuhudia utiaji saini mkataba wa bomba la mafuta

$
0
0

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha tamko la pamoja la yeye na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe baada ya  hafla ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga
Maafisa wandamizi wa kampuni ya TOTAL ya Ufaransa  wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt James Mataragio akiweka saini kwa niaba ya Tanzania mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo
hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha ratiba ya hafla  ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga baada ya yeye na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuombwa na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya Total duniani Bw. Patrick Poyanne kufanya hivyo ili iwe kumbukumbu yake ya
siku hiyo ya kihistoria katika Ikulu ya Entebbe leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe
mchache kabla viongozi hao kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na  mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe baada ya  hafla ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakipata picha ya kumbukumbu na  mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya
TOTAl duniani Bw. Patrick Pouyanner na viongozi waandamizi wa kampuni hizo mbili na kampuni hiyo  katika Ikulu ya Entebbe baada ya  hafla yauwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika
Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga


Angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa siku tatu kwa zaidi ya mikoa 15 nchini latolewa

$
0
0

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Aprili 11,2021, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho Aprili 12 hadi Aprili 14  mwaka huu katika mikoa 15.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA imeonyesha mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kesho Aprili 12, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani,  Tanga, Lindi na Mtwara.

Pia mvua hiyo inatarajiwa kunyesh kesho kutwa, Aprili 13, katika mikoa hiyo n mikoa mingine kiwemo pia Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro.


Aidha mvua hiyo inatarajiwa kunyesha Aprili 14  kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro

"Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo,.

Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Aprili 12 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Aprili 15, 2021

ABOOD ATANGAZA NEEMA KWA WATOTO YATIMA KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

$
0
0

 NA FARIDA SAID MOROGORO.


Kuelekea Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdal aziz Abood amekutana na watoto yatima, wazee wasiojiweza pamoja na watu wenye ulemavu walio chini ya taasisi ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania yenye makao makuu yake Mkoani Morogoro na kuahidi kusaidia futari katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhan.
 
Mhe, ABOOD amekutana na makundi hayo katika Kongamano la kukaribisha mwezi  mtukufu wa Ramadhan lililo andaliwa na Taasisi ya kiraia ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania, inayowasaidia watu wenye mahitaji mbalimbli, wakiwemo watoto yatima,Watu wenyeulemavu pamoja na wazee wasio jiweza.
 
Akizungumza katika kongamano hilo Mhe Abood amesema pamoja na kuchangia futari katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini pia atatoa mavazi kwa vijana 80 wanalelewa na taasisi hiyo katika siku kuu ya EDD ELFITRI ili wawezi kufurahia sikuku hiyo kama vijana wengine.
 
“Mimi kama Mbunge wenu nawapatia mavazi ya kusherekea siku kuu ya Edd watoto wote yatima ambao nimeambia idadi yao ni 80 waliopo hapa kwenye jumuiya ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania  na nitaendelea kushirikiana nanyi kwa kila jambo.”Alisema Mhe Abood.
 
Wakati huo huo Mhe Abood amekabidhi kitimwendo kwa taasisi ya Ukumbusho wa Zaka kitakacho wasaidia watoto wenye ulemavu wanao lelewa na taasisi hiyo, ambao awali walikuwa na uhitaji wa kiti hicho kinacho wasaidia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
 
“Kutoa msaada kwa watu wasio jiweza ni moja ya njia ya kupata thawabu, lakini pia kunasaidia kudumisha upendo kwa ndugu na jamaa zetu, na ndio maana hata kwenye Quaran tukufu na vitabu vingine vya dini vimeandika na mwenyezi mungu ametuamrisha kuwasaidia watoto yatima na watu wasio na uwezo.”Alisema Mhe Abood.
 
Awali akiwasilisha changamoto zinazo wakabili katika jumuiya hiyo kwa Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mhe Abdalaziz Abood ,Mwenyekiti wa Jumuiya Sheikh Omari Mahmudu Katura amemuomba Mhe ABOOD awasaidie kuwatafutia wahisani watakao weza kuwasaidia makundi hayo ya watu wenye uhitaji .
 
Pia wamewataka watanzaia kutoa misaada katika vituo maalumu vya kulelea watoto yatima na watu wasiojiweza, kwani kufanya hivyo  kutasidia kufikia kundi kubwa zaidi kuliko kutoa kwa mtu mmoj mmoja.

 

Njombe:Vijana waliojiajiri kwenye kilimo cha Nyanya wavuna mamiloni ya fedha

$
0
0

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Vijana na wakazi wa kijiji cha Matembwe wilayani Njombe wanaojishughulisha na kilimo pamoja na biashara ya nyanya wilayani humo,wametoa wito kwa vijana nchini kujishughulisha na kilimo ili kuepukana na changamoto kubwa ya ajira  inayoikabili taifa.

Vijana hao akiwemo Joseph Kabelege na Jastine Malekela wametoa wito huo walipotembelewa na mwandishi wetu katika shamba lao la nyanya lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja na kutegemewa na wakazi wa kata na kijiji hicho pamoja na wilaya kwa ujumla huku wakifanikiwa kiuchumi kutokana na kupata fedha mara baada ya mavuno ya Nyanya katika shamba lao.

“Ifike wakati sasa vijana tufunguke tuache kukaa na kuipigia kelele serikali haitoi ajira,hakuna serikali inayoweza kumaliza kutoa ajira kwa watu wote ni lazima tuthubutu hata kwenye kilimo”alisema Kabelege

“Kwenye hii ekari moja na robo nimepanda miche 6500 na kwa shina moja nilishafanya mahesabu kutoka linapoanza mpaka linapomalizia linaota matundu sio chini ya 100 au 120 na sio chini ya debe moja kwa mche mmoja na toaka nilipoanza kuvuna mpaka hapa leo wastani kwa debe moja nimekuwa nikuza kwa shilingi elfu kumi 10,000/=”aliongeza Kabelege

Ezekiel Mwansopo ni mshauri wa maswala ya kilimo anyefanya kazi na kampuni ya Namaingo ni miongoni mwa vijana waliotembelea katika shamba la nyanya linalolimwa na vijana hao wa kijiji cha Matembwe.amesema licha ya kilimo kuwa na changamoto lakini anashukuru kuona vijana wameanza kufuata fursa katika kilimo.

“Tumeona hapa kijana analima na anaweza akapata debe moja katika mche mmoja na debe linauzwa shilingi elfu kumi kwa sasa na ana miche karibu 6500 ni kiasi gani cha fedha anachokizalisha lakini wengine unaona wapo huko mitaani wanasema wanahangaika na ajira wakati hapa wamejiajiri na wanapata pesa, niwasahuri vijana waweze kujituma kwenye kazi kama hii na ukiangalia Kabelege anaamua nizashile milioni ngapi kwa muda gani”alisema Ezekiel Mwansopo

Kwa upande wake Lusiana Nchine afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Matembwe amewataka vijana kuiga mfano wa wachache wanaojishugulisha na kilimo ikiwemo kilimo caha Nyanya katika kijiji hicho kwa kuwa ni kilimo cha muda mfupi lakini zao lake limekuwa na soko katika jamii.

“Fursa za kilimo zipo nyingi ni kiasi tu cha mtu kukaa na kutazama kipi kinaweza kunilipa kwa hiyo hata vijana wengine wanaweza wakaangalia huyu anaendesha maisha yake kwa kilimo cha nyanya je mimi naweza nikafanya kipi kwasababu hata kufuga nako ni kilimo nah ii tutaondokana na changamoto ya ajira”alisema Lusiana Nchine.

Nyanya zilizokwisha kuchumwa na kupelekwa gengeni kwa ajili ya kuwafikia walaji wa kijiji cha Matembwe wilayani Njombe.

 

Mgomo wa wakulima uliodumu kwa mwezi mmoja wasitishwa,warejea shambani kwa masharti

$
0
0

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Muungano wa wakulima wa zao la chai kupitia vyama vya ushirika MVYULU tarafa ya Lupembe mkoani Njombe wamekubaliana kusitisha mgomo wa uchumaji wa majani ya chai uliodumu kwa mwezi mmoja na kukubaliana kurejea shambani hapo kesho April 12 mara baada ya makubaliano ya ulipwaji wa madeni yao zaidi ya Bil 1 kutoka kwa wawekezaji wa viwanda vya Ikanga na Igombola.

Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale amesema uamuzi huo umefikia mara baada ya majadiliano kadhaa ikiwamo vikao vya mara kwa mara yaliokuwa yakifanywa baina ya serikali,wakulima,uongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wawekezaji wa viwanda hivyo vya Ikanga na kiwanda cha Chai Lupembe (Igombola)

“Tumefanya uamuzi huo mkubwa tukiwa tumekubaliana kwamba kuanzia sasa hatutasubiri wakulima kukaa zaidi ya miezi miwili bila kulipwa tena,kwa hiyo kwenye ahadi na wawekezaji wa Ikanga fedha ambazo wameahida kuwalipa wakulima wa chai mpaka mwishoni mwa mwezi 4, basi tarehe 15 mwezi wa 5 tunakutana kuthibitisha”alisema Edwin Swale

Amesema mgomo wa kuchuma chai ulianza March mbili kutokana na malalamiko ya wakulima hao kuto kulipwa stahiki zao ili waweze kujikimu katika maisha

“Tulifanya uamuzi huo tarehe mbili mwezi wa tatu kwamba wananchi wa tarafa ya Lupembe,tusitishe kuchuma chai na tuzungumze kwanza kuhusu malipo,wakati tunafanya uamuzi ule tulikuwa na madai ya miezi mitano ya kulipwa,na mpaka hivi ninavyozungumza mwekezaji wa Ikanga amelipa fedha ya miezi 5 na anadaiwa mwezi wa pili tu” aliongeza Edwin Swale Mbunge wa Lupembe

Ameahidi kuzungumza na waewekezaji ili kuweka utaratibu mzuri wa ulipwaji wa fedha za wakulima“Tunataka tuweke utaratibu mzuri ni lazima wakulima wa chai walipwe kila mwishoni mwa mwezi fedha yao wanayostahili kulipwa na niwahakikishie wananchi hii ndio kazi mliyonituma,niwahakikishie madai ya mwezi wa pili yatalipwa na madai ya mwaka 2018 yatalipwa” Edwin Swale Mbunge wa Lupembe akiwa kwenye mkutano na wananchi wa Lupembe

Vile vile amesema wawekezaji wa kiwanda cha Igombola mpaka sasa ndio waliobakiwa na madai ya muda mrefu ukilinganisha na madai yaliyopo kwa wawekezaji wengine kutokana na kupunguza madeni yao.

“Wawekezaji wa Igombola hali yao ni mbaya zaidi,kwasababu kuanzia mwezi wa 12,1,2 na 3 hawajawalipa fedha wakulima wa chai na ahadi waliyoitoa kwenye kikao mpaka tarehe 26 mwezi huu watakuwa wamewalipa wakulima malipo yote” Edwin Swale

Hata hivyo amewataka wakulima wa chai kuto kukata tama na kilimo hicho na kuhamia katika kilimo kingine badala yake waweze kujihusisha na kilimo kingine pia ili kuwa na uwanja mpana wa kukuza vipato vyao

“Mlio kata tamaa ya kuchuma chai na kuamua kwenda kupanda parachichi na miti,nawaombeni mfanye mambo yote,kwasabbu unavyopanda parachichi na zenyewe zikawa nyingi,kuna siku soko litaanguka kwa hiyo msitupe chai.Wajibu wangu na viongozi wengine tutahakikisha wakulima mnalipwa kwa wakati” alisema Swale

Kutokana na hali hiyo wamiliki wa viwanda hivyo wamesema kutokana na kufikia makubaliano hayo pia ikiwemo kuchuma majani safi na yenye viwango stahiki wapo tayari kukamilisha malipo kabla ya mwezi Mei huku wakulima wakikubaliana kukutana Mei 15 ili kujadili utekelezaji wa makubaliano hayo.

Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale akiwaeleza wananchi wa Lupembe katika mkutano uliofanyika eneo la Barazani namna walivyofanya vikao vya mara kwa mara na kufikia makubaliano mazuri na wawekezaji kuwalipa wakulima kwa wakati stahiki zao.
Baadhi ya wakulima na wananchi wa jimbo la Lupembe wilayani Njombe wakati wakimsikiliza mbunge wao mikakati sahihi ya upataji wa stahiki zao mara baada ya kufikisha majani ya chai viwandani.
Mfano wa Shamba la chai na wakulima wakionekana katika shughuli yao ya kusafisha shamba ili kuboresha mashamba hayo,picha ni kutoka mtandaoni.



 

TPSF inaungana na serikali awamu ya sita kujenga uchumi.

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema kuwa inaungana na Rais Samia Hassan Suluhu katika muongozo na maelezo aliyoyatoa katika hotuba ya April 6 mwaka huu yanayolenga kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza ushiriki mpana wa shughuli za kujenga uchumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini Angelina Ngalula amesema kuwa Sekta Binafsi inafarijika kumpata Rais anayeendelea kuamini Sekta Binafsi katika kukuza na kuinua uchumi wa maendeleo ya watanzania wote huku Rais akishauri na kuelekeza namna bora ya ukusanyaji wa mapato hivyo Sekta Binafsi itashirikiana na Serikali kuhakikisha wanasimamia misingi ya uzalendo na uadilifu katika suala zima la ulipaji kodi ili kazi iendelee kwa kasi zaidi.

Ngalula amesema TPSF inashauri mifumo ya kodi ifanyiwe marejeo na maboresho ili kuondoa migongano kati ya Taasisi zinazotoza Kodi na walipa kodi na tunaomba ushauri wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango ambaye ni Makamu wa Rais katika kikao cha Baraza la Biashara (TNBC) April 7 2019 aliongelea kuhusu uhitaji wa kufanya tathimini ya mifumo ya Kodi na kumnukuu"Mhe Rais nafikiri kwamba mifumo wetu wa kodi na umekuwa kukuu kama nakumbuka vizuri,mara ya mwisho kama taifa tumefanya a Comprehensive review ,ya mifumo wa kodi ,tozo, mapato yote ya Serikali na matumizi ilikuwa mwaka 2009 .Ninavyoona mimi Sasa , uchumi umebadilika na tunaendelea kutumia mfumo ambao ni out of date.Ndio maana malalamiko ni mengi Sana".mwisho wa kunukuu.

Aidha amesema katika eneo la ukusanyaji wa kodi wanashauri vitengo vya utafiti vya wizara Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania viimarishwe kwa kuwa na wataalam waliogombea katika masuala mbalimbali ya kitaalam kama kilimo ,Mafuta na Gesi,madini usafirishaji ,viwanda,Tehama,Ujenzi na Utalii na kipaumbele kitolewee kwenye matumizi ya Teknolojia ya Habari hasa matumizi ya Data katika kufanya uchambuzi wa data ili isaidie katika maamuzi mbalimbali.

Ngalula amesema katika kutanua uwigo wa walipakodi ni kurasimisha wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali kwani zaidi ya asilimia 70 ya Sekta Binafsi siyo rasmi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Angelina Ngalula akizungumza na waandishi Habari namna walivyoipokea Hotuba ya Rais Samia Hassan Suluhu  katika kujenga mazingira ya biashara nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Francis Nanai  akitoa maelezo kuhusiana na mkutano huo kwa serikali ya awamu ya sita .
Mkurugenzi wa Bodi ya TPSF Sylvester Koka akizungumza namna walivyojipanga.
 

ZAIDI YA VIJANA 48,000 WANUFAIKA NA KAMPENI YA KIJANA NI USAFI.

$
0
0

 NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.


Vijana wametakiwa kuzingatia tabia chanya za usafi katika maeneo hayo ikiwemo kunawa mikono,kutumia maji safi pamoja na kudhibiti kusambaa kwa taka ngumu katika maeneo yao hali itakayosaidia kutunza na kulinda mazingira.
 
Wito huo umetolewa  wakati wa kampeni ya KIJANA NI USAFI ambayo inalenga kuhamasisha tabia ya usafi kwa vijana wakitanzania inayosimamiwa na Shirika la Raleigh Tanzania chini ya ufadhili wa   shirika  la msaada wa Uingereza( UKAID).
 
Kampeni hiyo itakayodumu ndani ya miezi 6 inawalenga vijana wa wakike na kiume wenye umri wa miaka kati ya 15-35,ambapo inatarajia kufikia zaidi ya vijana 48,000 katika mikoa ya minne ambayo ni Iringa,Morogoro,Dodoma na Dar es salaam. 
 
Akizungumza katika kampeni hiyo Mratibu wa Mradi,Bwana Augustino  Dickson amesema kampeni hiyo katika Manispaa ya Morogoro itajikita katika itahimiza matumizi ya maji safi na salama,na kuitaka jamii kuacha kuishi kwa mazoea.
 
Hata hivyo ameongeza kuwa Mkoa wa Morogoro unaathiwa na Magonjwa ya mlipuko ya mara kwa mara ya kiwemo mlipuko wa ugonjwa wa  Kipindupindu hali ambayo inatokana na  jamii kutotumia maji safi na salama.
 
Aidha ameongeza kuwa kampeni ya KIJANA NI USAFI itaendelea kulenga kundi la vijana kwa sababu vijana ndio kundi lenye idadi kubwa ya watu Nchini, huku akiongeza kuwa vijana wanaweza kuwa wakala wa mabadiliko chanya katika jamii endepo watajengewa uwezo kuhusu elimu ya mazingiara. 
 
Katika kampeni mafunzo mbalimbalia ya namna ya kuhifadhi maji safi na salama yametolewa kwa wananchi,huku wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakilishukuru Shirika la Raleigh Tanzania kwa kuwapatia elimu ya mazingira.

 

PROF MKUMBO AAGIZA UIMARISHWAJI WA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA ILI ICHANGIE KIWANGO KIKUBWA CHA UKUAJI WA UCHUMI

$
0
0

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb)  ametoa maelekezo kwa ajili ya kuimarisha sekta ya viwanda na biashara ili  sekta hizo zichangie kwa kiwango kikubwa  katika ukuaji wa uchumi na kutekeleza malengo ya  Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26,  Ilani ya CCM ya uchaguzi 2020 na Maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita  na Ushauri na maoni maelekezo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi wa Viwanda nchini.  

Profesa Mkumbo ametoa maelekezo hayo alipokutana na menejimenti ya wizara na wakuu wa taasisi zilizochini ya wizara hiyo kwa lengo la kutoa  mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kikao kilichofanyika  tarehe 10/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Akiongea katika kikao hicho, Waziri alisema Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 inalenga kuona Tanzania inahitimu na kuondokana kuwa nchi masikini  inayotegemea kilimo na uchumi wa uzalishaji duni na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025  ambapo wananchi wengi wajihusihe na kilimo cha kisasa kinachofunganishwa na viwanda na huduma. Hivyo alisisitiza kuwa ili kufikia dira hii wizara hiyo ina nafasi na mchango mkubwa  katika kufanikisha azma hiyo.

“ Uchambuzi wa maudhui ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na  Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26 unaonesha wazi kabisa nafasi ya Sekta ya Viwanda na Biashara…sisi kama Wizara tunatarajiwa kutoa mchango karibu kwa kila eneo la matokeo tarajiwa.”

Alisema pia katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26, malengo sita kati ya malengo mahsusi 12 yanahusu sekta ya viwanda na biashara, kati ya vipaumbele vitano vya mpango huo vitatu vinahusu wizara hiyo, katika Sekta 30 za mpango  huo Sekta 6 zinahusu  Wizara na katika hatua 156  hatua 54  zinahusu  Wizara ya Viwanda na Biashara.


“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zinamchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26, malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020, Maelekezo ya Serikali awamu ya sita. Hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo”

Hata hivyo, Profesa Mkumbo alisema hakusudii kutumia muda mwingi katika kutunga Sera, Sheria na mikakati na kuwa yeye analenga katika utekelezaji na kuona matokeo ya utekelezaji huo kwa kuchochea ukuaji wa haraka wa Sekta ya Viwanda na Biashara.

Pia aliwataka wataalamu wa Idara ya Sera na Mipango ya Wizara kusimamia uhuishaji wa nyaraka mbalimbali za kisera na sheria  ili ziende na wakati na kuakisi maudhui ya Mpango wa tatu wa Maendeleo na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akitoa maelekezo mahususi kwa upande wa sekta ya viwanda, Profesa Mkumbo alitaka kuwa bayana na dhana na aina ya viwanda tunavyotaka kuviendeleza hapa nchini, kuwa na kanzi data ya kisasa ya viwanda. Pia alielekeza katika kupima maendeleo ya viwanda kwa kuzingatia kiwango cha uzalishaji na ajira, kuweka mazingira namasharti rahisi katika kukuza na kuchochea viwanda vidogo vidogo vinavyotumia teknolojia rahisi na ya kisasa na vilivyojikita vijijini na mijini,

Profesa Mkumbo pia alisisitiza mkazo katika kuwatambua, kuwawezesha na kuwahudumia wawekezaji katika viwanda vikubwa na vyenye tija katika uchumi na kuhuisha Mkakati wa Viwanda nchini, ikiwemo dhana ya EPZ na SEZ. Alisema pia kusimamia kwa karibu miradi ya kielelezo iliyopo katika Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Taifa ambayo ni mradi wa Chuma wa Mchuchuma na Liganga, Magadi Soda wa Engaruka, ujenzi wa Kiwanda cha Sukari-Mkulazi na kanda Maalum za Uchumi na Maeneo Maalum ya Uwekezaji

Profesa Mkumbo alisema pia kuimarisha utafiti na matumizi yake katika maendeleo ya viwanda, ikiwemo kuwa na ushirikiano wa karibu na taasisi za utafiti na elimu ya juu na kupanua na kuboresha mahusiano na ushirikiano na taasisi za sekta binafsi.

“ Pia kuimarisha ushirikiano na OR-TAMISEMI katika maendeleo ya viwanda vidogo vidogo, tunataka kuona uwezekano wa kuwaongeza majukumu maafisa biashara wa Halmashauri ili pia wasimamie viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao kwa kushirikiana na SIDO.”

Kwa upande wa sekta ya biashara, Profesa Mkumbo aliweka msisitiza katika suala la kujenga imani kwa wafanyabiashara kupitia, uwazi na mawasiliano chanya ya mara kwa mara. “Tunataka tunapokutana na wafanyabiashara tufanye mazungumzo yenye tija ya kubadilisha mikakati ya kukuza biashara na masoko, badala mikutano hiyo kutumika tu kama jukwaa la kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara.”

Alisema pia kuendelea kuzipitia kanuni za mamlaka za udhibiti zinazoonekana kukwamisha biashara, kuchochea na kuhamasisha tabia ya kujali wateja miongoni mwa watendaji wa Serikali wanaohudumia sekta mbalimbali za biashara.

Profesa Mkumbo alisema pia kuipitia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa “Blue Print” kwa lengo la kuona maeneo ambayo bado hayajatekelezwa na kusimamia utekelezaji wake kikamilifu na kwa haraka, kushirikiana na OR-TAMISEMI, kuchambua na kuchakata kwa umakini maoni ya wabunge na wadau wengine kuhusu haja ya kuwa na Mfuko mmoja wa Mtaji kwa ajili ya wajasiriamali na wafanya biashara wadogo.

Alisema pia kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa sera ya maendeleo ya sekta binafsi, ikiwemo biashara ndogo zinahitaji upendeleo maalumu ili kukua na kuweka msisitizo wa pekee katika kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania ndani ya nchi na nje ya nchi na kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa maeneo maalum ya kibiashara hususani kwa maeneo ya mipakani. Pia, kuona namna ya kuimarisha eneo maalumu la kibiashara la Kariakoo ambalo kihistoria limekuwa likifanya vizuri na kuwalinda walaji.

Aidha, Profesa Mkumbo amesisitiza haja ya watendaji wa wizara na wataasisi kubadilisha mtizamo katika utendaji kazi na kuwa na “corporate thinking” na tabia ya kujali wateja kwa kuzingatia kuwa wadau tunaowahudumia ni wafanyabiashara.

Pia amewalekeleza wataalamu wa wizara hiyo kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalamu wenye ushahidi wa kisayansi na ameahidi atatoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyabiashara

Aidha, Profesa Mkubwa alisikiliza maoni na changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo kutoka kwa Wakuu wa Taasisi kutoka TBS, WMA, BRELA, TANTRADE, SIDO, NDC, EPZA, FCC, FCT, WRRB, TIRDO, CAMARTEC, TEMDO na CBE na kuahidi kuzitatua.

Viewing all 119823 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>