Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119842 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI KIPANGA ATAKA UBUNIFU KATIKA KUKUZA ELIMU NCHINI

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imewataka watumishi wake wote nchini kuzingatia nidhamu, ubunifu, maadili na weledi katika kazi zao ili kukuza kiwango cha elimu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati akifunga mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Akizungumza na watumishi hao, Naibu Waziri Kipanga amewataka watumishi hao kuzingatia yale yote waliyoelekezwa na Waziri wa wizara hiyo, Prof Joyce Ndalichako jana wakati akifungua baraza hilo ambapo alisisitiza nidhamu kazini na kuacha kutumia lugha za ubabe kwa wateja ambao ni wananchi.

Ametoa rai kwa vyama vya wafanyakazi kama Tughe na Chama cha Walimu Tanzania CWT kushirikiana na Menejimenti ya Wizara kuhakikisha wanasimamia ipasavyo nidhamu na kukuza ubunifu kwa wafanyakazi lengo likiwa ni kuifanya wizara izidi kufanya vizuri kama ambavyo ilisifiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

" Nasisitiza mshikamano baina yetu watumishi, ili tuzidi kupongezwa kwa kufanya kazi vema ni lazima tushikamane tukiwa wamoja na wenye upendo, niombe kwa pamoja tuwe mabalozi wazuri wa kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwenye vituo vyetu vya kazi.

Wizara yetu ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, bila kukuza kiwango cha elimu na kuzalisha watalaamu wengi nchini ni vigumu kama Taifa kupata maendeleo, ni vema tukatoka na mkakati wa kuhakikisha tunazalisha vijana wasomi wenye tija kwa Taifa letu katika kuajiriwa na kujiajiri wenyewe," Amesema Kipanga.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Dk Leonard Akwilapo ameahidi kuwa watayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa kwao na Waziri Prof Ndalichako na kwamba watatekeleza yale yote yaliyokusudiwa na baraza hilo katika kukuza kiwango bora cha elimu nchini.

Nae Mwenyekiti wa Tughe, Archie Mntambo amesema wataendelea kufanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa ili kulinda sifa ya wizara hiyo ambayo imekuepo kiasi cha kupokea sifa kutoka kwa Rais Samia.

" Nikuhakikishie Naibu Waziri yale yote mliyotuelekeza tutayafanyia kazi kuhakikisha tunakua wabunifu, wenye weledi na nidhamu katika kazi lengo likiwa ni kuzalisha kundi kubwa la vijana wasomi wenye tija kwa Taifa letu," Amesema Mntambo.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo katika mkutano wa 28 wa baraza hilo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo akizungumza katika mkutano wa Baraza hilo jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Archie Mntambo akitoa shukrani zake kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati wa kufunga mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo ya Elimu.
Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakiwa kwenye mkutano wao wa pamoja uliofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili jana na leo.
 


Nsekela atoa Sadaka ya Futari kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum kuelekea Ramadhan

$
0
0
Kuelekea mfungo wa Ramadhan, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela leo ameambatana na familia yake pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kotoa sadaka ya futari ya thamani ya shilingi milioni 10 kwa vituo 5 vya watoto yatima katika mkoa wa Dar es Salaam. 
 
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee na kutanguliwa na ibada ya Ijumaa iliyoongozwa na Imam, Haroub Khamis katika Masjid ya Karimjee. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Nsekela amesema sadaka hiyo ni sehemu ya shukrani ya familia yake na muendelezo wa utamaduni wa Benki ya CRDB kutoa sadaka kwa makundi yasiyojiweza na kuandaa futari maalum kwa ajili ya wateja na wadau wake katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
“Tukikaribia kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo mioyo na fikra vipo katika kumnyenyekea Muumba tumeona ni jambo la faraja kujumuika kwa pamoja na watoto yatima katika ibada hii ya funga kwa kuwapatia msaada wa futari,” alisema Nsekela huku msaada huo pia utatolewa katika vituo vya watoto yatima katika kanda zote nchini.  
 
Akisisitiza juu ya umuhimu wakuwasaidia watu wasiojiweza, Nsekela alisema katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vyema jamii ikafahamu wapo watu ambao iliwaweze kutimiza funga yao kikamilifu wanahitaji msaada kutoka kwa wale ambao wenye uwezo.
“Kutoa msaada kwa watu wasiojiweza ni kujitafutia thawabu, lakini pia kunasaidia kudumisha upendo kwa ndugu, jamaa, marafiki na jamii kwa ujumla wake. Hata katika Quran takatifu Surah Al-Baqarah aya ya 2:83, Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuwasaidia yatima na wasiojiweza,” aliongozea Nsekela.  
 
Akipokea msaada huo kwa niaba ya vituo vya watoto yatima, Sheikh Issa Othman Issa amemshukuru Nsekela na familia yake pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwa msaada huo huku akitanabaisha kuwa kusaidia wasiojiweza wakati wa mfungo wa Ramadhan ni ibada na kunafungua milango ya baraka.

 
“Mafundisho ya Mtume SAW yanatuambia atakayemfuturisha aliye na swaum atapata thawabu kama zake bila ya mwenye swaum kupungukiwa na kitu. Kwa niaba ya vituo hivi na watoto hawa niwashukuru sana na Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki Benki yetu ya CRDB,” alimalizia Sheikh Issa.  
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Amani Foundation for Orphans, Hajjaty-Zubeida Abdallah kilichopo Wilaya ya Kigamboni, aliishukuru kwa msaada huo akisema umekuwa faraja kwa watoto hao na utawasaidia kukamilisha funga yao ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kikamilifu.

“Mkurugenzi Mtendaji kwa niaba ya vituo hivi nikushukuru sana kwa msaada huu, nichukue pia fursa hii kuwakaribisha katika vituo vyetu ilituweze kujadiliana kwa pamoja namna bora ya kuwasaidia watoto wetu hawa,” alisema Hajjaty-Zubeida.
 
 Vituo vilivyopatiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Tarbia kilichopo Wilaya ya KinondonI, Kituo cha Irshad Islamic kilichopo Wilaya ya Ubungo, Kituo cha Amani Foundation for Orphans kilichopo Wilaya ya Kigamboni, Kituo cha Hiyari Orphans kilichopo Temeke, Kituo cha Busara Orphans kilichopo Wilaya ya Ilala.  
 
Kila kituo kimepatiwa Unga wa Ngano kilo 50, Sukari kilo 50, Maharage kilo 50, Tambi pakiti 30, Tende pakiti 20, Mafuta lita 20, Njugu kilo 20, Sabuni za Unga za Kufulia Ndoo 5 pamoja na maziwa ya unga makopo makubwa 5 sambamba na majani ya chai pakiti 10.

TANZIA : MAMA MZAZI WA IGP SIRRO AFARIKI DUNIA JIJINI DSM

PROF MKUMBO ATAKA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU KWA WATUMISHI WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

$
0
0

 WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo  amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu  zinazotumika kusimamia taasisi hizo na sikuwa kikwazo katika kutoa huduma  bora kwa wananchi.

Waziri  Mkumbo  aliyasema hayo alipokuwa akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kikao na Wakuu wa Taasisi hizo  kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zinamchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo”  Amesema Waziri Mkumbo.

Aidha, Wakuu wa Taasisi waliohudhuria kikao hicho kutoka TBS, WMA, BRELA, TANTRADE, SIDO, NDC, EPZA, FCC, FCT, WRRB, TIRDO, CAMARTEC, TEMDO na CBE walipata fursa ya kutoa maoni na changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Waziri Mkumbo ameahidi kuendelea kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka katika taasisi hizo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo upatikanaji Bodi zinazofanya kazi katika kila taasisi ili kurahisisha utoaji wa maamuzi sahihi na kwa wakati.

Naye Naibu Waziri akiongea na Wakuu wa Taasisi hizo, alisema kuwa mchango wa taasisi hizo  ni muhimu na zinategemewa katika kuifanikisha Wizara  kufikia malengo ya taifa katika ukuaji wa viwanda na biashara shindani na hivyo kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara  alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika kikao kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Dkt John Mduma akitoa maoni kuhusu ukamilishaji wa mapitio mbalimbali ya Sera na Sheria zinazosimamia taasisi zilizopo chini ya Wizara ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji akitoa maoni kuhusu uboreshaji wa huduma zinazotolewa na SIDO kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Katibu Mkuu wa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akifafanua jambo katika Kikao cha Wizara na Wakuu wa Taasisi zake Kikao hicho kilicholenga kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara kilifanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara  alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika kikao kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa, Katikati ni Mrajis wa Baraza la Ushindani Bw Renatus Rutatinisiwa akifuatiwa na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu waa  NDC Bi Rhobi Sattima wasilikiliza maelekezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo  katika kikao na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt  Hashil  Abdallah (kushoto) wakiwa katika Kikao  cha Wizara na Wakuu wa Taasisi zake. Kikao hicho kilicholenga kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara kilifanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma

.

UKARABATI BARABARA YA KATOKORO KUANZA MWEZI HUU.

$
0
0


Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Serikali tayari imetenga Milioni 579 za Ujenzi wa Daraja na ukarabati wa Barabara Eneo Korofi la Katokoro Kata Katoro Halmashauri ya Wilaya Bukoba, kazi inayotegemewa kuanza Mwezi Aprili Mwaka huu.

Akiongea na Wananchi wa Kata Katoro wakati akijibu Risala iliyosomwa kwake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Samson Rweikiza, katika Mkutano wa Hadhara alipofika Kata hiyo kufahamu changamoto zilizopo na kuwashukuru kwa kumpatia Kura katika Uchaguzi uliopita.

Katika shukrani hizo Dkt Rweikiza (MB) hakusita kuwakumbusha Wananchi hao Juu ya Miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha Miaka mitano iliyopita licha ya Kata hiyo kuongozwa na upinzani, ikiwemo Miradi ya Afya, Elimu, Umeme, Barabara ambayo imetekelezwa na CCM bila hiyana.

"... Tukiwa kwenye Kampeini mengi tuliyasema na kuyaahidi, ingawa wengine walidhani Ni Uongo lakini Mimi sipendi kusema Uongo, na leo Nimekuja kutekeleza ahadi yangu.." Alisema Dkt Rweikiza (Mb).

Ameongeza kuwaomba Wanachi wa Kata hiyo kuendelea kujitolea Nguvu zao kuchangia maendeleo huku akichangia Milioni Tano Kati ya Milioni Sita alizoahidi kuchangia.

Aidha kuhusu Mradi wa Maji amewaomba Wananchi kuendelea kuwa  wavumilivu wakati ambapo Serikali inaendelea na Tatatibu za usanifu na uhakiki wa Mradi Mkubwa wa Maji kwa Kata Sita za Bukoba Vijijini zikiwemo kata za Izimbya, Mugajwale, Ruhunga, Katoro, Kaibanja na Kyaitoke.

Eneo korofi la Katokoro ambapo yatajengwa Madaraja madogo 12 pamoja na Daraja Moja kubwa ili kuondoa Kero ya Usafiri eneo hilo.

Baadhi ya Mitumbwi ikiwa imeegeshwa kusubiri kuvusha Wananchi eneo la Katokoro Kata Katoro Bukoba Vijijini, Usafiri huo ukiwa Ni msaada Mkubwa kwa Wananchi wa maeneo hayo kwa Sasa.
Dkt. Samson Rweikiza (Mb) akiongea katika Mkutano wa Hadhara alipofika Kata Katoro Bukoba Vijijini, ili kubaini Changamoto zilizopo Kata hiyo pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua yeye na Chama Cha Mapinduzi Uchaguzi Mkuu uliopita.

Wananchi wa Jimbo la Bukoba Vijijini kutoka Kata Katoro na Viunga vyake wakiendelea kumsikiliza Mbunge wao Dkt Rweikiza alipofika kuwashukuru mapama Aprili 09 Mwaka huu.
 

Waziri Mhagama atoa maagizo 22 kwa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu

$
0
0

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, ametoa maagizo kwa menejimenti ya ofisi hiyo ili kuboresha  utendaji katika ofisi hiyo kutokana na mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanywa  hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa sasa majukumu ya ofisi hiyo ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yatakuwa yanasimamiwa na Katibu Mkuu mmoja na Manaibu Makatibu Wakuu wawili, awali majukumu hayo yalikuwa yanasimamiwa na  Makatibu Wakuu wa tatu kwa kila mmoja akisimamia majukumu yake.

Kabla ya kutoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi na menejimenti ya ofisi hiyo kilichojumuisha wakuu wa idara, vitengo na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo leo tarehe 9 Aprili, 2021 Jijini Dodoma, Waziri Mhagama amebainisha kutoridhishwa na baadhi ya watendaji kutoshiriki kikamilifu kwenye kikao cha Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala kama ilivyotakiwa na mkaguzi huyo.

“Kila tunachofanya ni kwa ajili ya taswira ya Mhe. Waziri Mkuu na  ofisi ya  Waziri Mkuu,  nasikitika miongoni mwetu tukishindwa kutekeleza wajibu wetu tutatia doa ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu mkuu fikiria utaratibu wa kudhibiti uzembe lazima kila mmoja awajibike. Tumepanga katika mambo ya msingi hatutasita kufuatilia utendaji ili kila mmoja atekeleze wajibu wake.”Amesema Mhe. Mhagama.

Akitoa maagizo katika kikao hicho amewataka watumishi kutanguliza taifa kwa kila jambo pia na kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao. Aidha amewataka kutumia ubobezi wa  taaluma walizo nazo ili kuleta matokeo yenye tija kwenye ofisi hiyo. Amewasistiza kuwa wabunifu katika  utendaji wa shughuli zao kwa kuizingatia kasi ya serikali ya  awamu ya sita.

Aidha, Mhe. Mhagama ameagiza kufanyika kwa  vikao vya kila robo muhula ili kujipima na kutathimini namna ya utendaji wa shughuli za idara na taasisi za ofisi hiyo, amesisitiza vikao hivyo vitaweza kuchangia kuleta mabadiliko ya haraka ya kiutendaji katika idara zote na kupata matokeo yaliyo kusudiwa.

Pia, Mhe.Mhagama amezitaka Idara na Taasisi zilizo chini ya  ofisi hiyo kuendeleza dhana ya mshikamano katika utekelezaji wa shughuli za ofisi hiyo. Amefafanua kuwa mafanikio ya moja ya idara ya ofisi hiyo  ni mafanikio ya ofisi nzima hivyo amewataka watumishi wote kushirikiana.

Mhe.Mhagama ameagiza kuhakikisha Mabaraza ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yaendelee kufanyika.Aidha,  amesisitiza kuhakikisha katika idara,wizara  na tasisi za serikali  pamoja na  kwenye sekta binafsi mabaraza hayo yanafanyika ili  waweze kuimarisha mauhusiano kati ya waajiri na wafanyakazi.

Aidha Waziri  ameagiza kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Aprili, mfumo wa kielektroniki wa vibali vya kazi na ukaazi kwa wageni  uwe umezinduliwa na kufanya kazi ili kudhibiti mianya ya rushwa. Mfumo huo utasaidia kupunguza urasimu wa utoaji vibali kwa wawekezaji.

“Tayari tumesha wafukuza baadhi ya maafisa kazi wanye tabia ya kupokea rushwa kwenye vibali, tunataka mfumo huo kusaidia kuondoa tatizo la  rushwa kwenye vibali, tunazo taarifa sisi tukisha pitisha utoaji vibali hivyo vinachukua zaidi ya wiki mbili havijatolewa ili kumfikia muhusika. Nataka mfumo huo uanze kufanya kazi.” Amesisitiza Mhe. Mhagama.

Pia, Mhe. Mhagama meagiza andaliwe kikao na maafisa rasilimali watu kutoka kwenye makampuni makubwa ya uwekezaji nchini,  ili waelezwe utaratibu sahihi wa utoaji vibali. Amefafanua kwamba baadhi ya mawakala wanao wasaidia makampuni hayo katika kupata vibali hivyo wamekuwa wakikiuka taratibu na tayari wamewachukulia hatua. Aidha ameagiza kuhakikisha kuwa mikataba ya ajira inatolewa na wajiri nchini pamoja na kuzingatia  masuala ya mishahara.

Mhe.Waziri ameagiza  kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi,  ufanyike utekelezaji wa  Mpango kazi wa  kushughulikia kero  na malalmiko za wafanyakazi, waajiri na  ya wadau wengine katika sekta ya kazi na ajira.Aidha,  ameagiza kufanyika ukaguzi kwenye makampuni na migodi, miradi ya kimkakati na makampuni, amesema kuwa ukaguzi huo utasaidia uwekezaji kuwa wa tija  kwa watanzania kwa kuwa  na uwiano wa ajira pamoja na mishahara. 

“Natambua tupo kipindi cha mpito cha kubadili mifuko ya hifadhi ya jamii nataka ndani ya wiki moja Katibu Mkuu hakikisha vikao vya kimkakati tulivyo viweka kwa kushirikiana vyama vya waajiri, vyama vya wafanyakazi na sisi serikali vinaanza kufanyika ili zoezi hilo liweze kukamilika kama lilivyo agizwa. ” Amesisitiza Mhe.Mhagama.

Masuala mengine ambayo ameagiza Mhe.Mhagama ni kufuatilia mradi wa kukuza ujuzi, mafunzo ya uwanagenzi, mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu, suala la migogoro kwa wafanyakazi kupitia tume ya usuluishi na uwamuzi, masuala ya mawakala kukagua mahali pa kazi. Pia ameitaka Kitengo cha Huduma za Ajira kushirikiana na Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwa kuibua ajira zenye staha nje ya nchi na kuangalia masuala ya mikataba ya  ajira hizo.

Aidha,   ameelekeza utekelezaji wa maagizo yake kwenye miradi ya Mbigili na Mkulazi iliyopo chini ya NSSF. Ameagiza  aandaliwe kikao kazi  na timu ya NSSF kwajili ya miradi hiyo pia ameelekeza kukutana na maafisa matekelezo wa mikoa wa NSSF. Amesisitiza  na kuagiza ni muhimu shughuli zote zinazotekelzwa kwenye ofisi hiyo zizingatie kuhusisha masuala ya wenye ulemavu pia na ameataka wahakikishi hata sekta nyingine kufanya hivyo.

Kwa upande wake katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajiara na Wenye Ulemavu) Tixon Nzunda, amemhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza Maagizo yote  kwa kuzingatia misingi ya weledi, Uadilifu, bidii ya kazi ili kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kwa wakati.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Ngeriananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda pamoja na Manaibu Makatibu Wakuu ; Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao hicho, kuushoto kwake ni Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya.

Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nchina Menejimenti hiyo alipokutana nao kwa lengo la kuboresha utendaji wa ofisi hiyo.
Kamishna Msaidizi Idara ya Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Mwalwisi akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nchina Menejimenti hiyo alipokutana nao kwa lengo la kuboresha utendaji wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ,maagizo kwa Menejimenti ya ofisi hiyo alipokutana nao kwa lengo la kuboresha utendaji wa shughuli za ofisi hiyo. Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga  na kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda (wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu Profesa Jamal Katundu (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. Kaspar Mmuya (mwenye tai) wakifuatilia kikao hicho.
Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nchina Menejimenti hiyo alipokutana nao kwa lengo la kuboresha utendaji wa ofisi hiyo.

RC NDIKILO ASISITIZA KUTENGWA KWA ASILIMIA 10 YA MAPATO KWA AJILI YA VIJANA,WANAWAKE,WENYE ULEMAVU

$
0
0

 

Na MWAMVUA MWINYI,PWANI

MKUU wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo, amekemea baadhi ya halmashauri kutumia fedha zinazotengwa kwa ajili ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya mikopo ya kundi la walemavu,wanawake na vijana na kuzitaka ziendelee kutenga fedha hizo ili kunufaisha vikundi hivyo.

Alitoa rai hiyo ,katika makabidhiano ya Vifaa na Fedha Taslimu vyenye thamani ya Sh.milioni 245,867,100 kama Mikopo  ya Asilimia10 ya Mapato ya Halmashauri ya Mji Kibaha kwa makundi ya Vijana, Wanawake  na Watu wenye  Walemavu.

Pia mkuu huyo wa mkoa ,amekabidhi Pikipiki 12, Bajaji 1, Toyo 1 Mashine 1 ya kutengeneza sabuni na Fedha taslimu sh.177,746,400 kwa vikundi 68.

Ndikilo alisema utoaji wa mikopo hiyo ni takwa  kisheria  (Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019),na ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Cha Mapinduzi 2020-2025.  

Akieleza  hali ya utoaji mikopo hiyo na marejesho Mkoani hapo alisema mwaka 2019/20 Jumla ya Shilingi  Bilioni 2.666  zilitolewa kwa vikundi 672 sawa na Asilimia 108 ya fedha zilizopangwa kutolewa na marejesho yalikuwa Sh. 645,770,927 sawa na asilimia 54 ya fedha zilizokopeshwa.

 "Marejesho haya ni Duni"  fedha hizi ni za Serikali lazima mrejeshe ili watanzania wengine wanufaike  na matunda ya  Serikali yao"

Ndikilo alisema kwa mwaka 2020/21 fedha za asilimia 10 zitakazotengwa   na Halmashauri zote 9  ni Bilion 2,124,500,000  hadi Februari 2021 fedha zilizokusanywa   ni Bilioni 1,713,172,068 sawa na asilimia 78.54 ya fedha zilizopangwa, fedha ambazo zimefikishwa kwenye vikundi hadi Februari 2021 ni Sh. Bn 1,149,459,447 sawa na asilimia 66.92.

Nawataka kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na vifaa wanavyokabidhiwa, "Hakuna fedha ndogo lazima muwe na mipango  thabiti ili fedha ziongezeke" alisema Ndikilo.

Nae mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Jeniffer Omolo ,alieleza kwa mwaka 2020/2021 vimeundwa vikundi 254 katika kata zote 14 za halmashauri hiyo.

Omolo alifafanua,Utoaji wa mikopo ,wanatenga fedha asilimia 10 kwa kufuata sheria ambapo wametoa milioni 83 mwaka 2017 /2018,na milioni 161 kwa 2018/2019 pia milioni 276 kwa mwaka 2019/2020 na milioni 373 kwa mwaka huu.



 

MBUNGE MWANYIKA AIBANA SERIKALI BUNGENI KUTUMIA VIGEZO UGAWAJI AJIRA ZA WALIMU VIJIJINI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika akiuliza swali kwa Serikali kwamba inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Dodoma.Spika, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu katika Shule za Msingi na Sekondari, Serikali imeahidi kuendelea kuajiri walimu ili kuziba pengo hilo. Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi David Silinde wakati akijibu swali la mbunge wa Njombe mjini Deodatus Mwanyika (CCM). 

Naibu Waziri amesema kuanzia Disemba 2015 hadi Septemba 2020, Serikali imeshaajiri walimu 10,666 wa Shule za Msingi na Walimu 7,515 wa Shule za Sekondari na ambapo wamepangwa kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa. Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini. 

Katika swali la nyongeza Mwanyika ameuliza iwapo Serikali itakuwa na mkakati thabiti wa kuajiri walimu wengi kutokana na utoaji wa elimu bure ulioongeza idadi ya wanafunzi na kuangalia maeneo yenye uhitaji mkubwa. Silinde alisema, katika kipindi cha Desemba 2015 hadi Septemba 2020, Halmashauri ya Mji Njombe imeajiri walimu 21 wa Shule za Msingi na 111 wa Shule za Sekondari. 

"Vilevile Ofisi ya Rais-Tamisemi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri Walimu wapya 6,000 wa Shule za Msingi na Sekondari ifikapo Juni 2021 ili kujaza nafasi zilizoachwa na Walimu waliofariki ama kustaafu kazi," alisema Silinde. 

Alisema Tamisemi imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozi katika maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye Shule zenye uhaba wa walimu ambazo nyingi zipo maeneo ya vijijini. 

Kwa mujibu wa Silinde, Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga walimu kwenye Shule za Msingi na Sekondari hasa zenye mahitaji makubwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video Mbunge Mwanyika akiibana Serikali kuhusu suala hilo na Naibu Waziri wa Tamisemi, Silnde akijibu....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

WAZIRI WA KILIMO PROF. MKENDA AMUOMBA BALOZI WA UHOLANZI WAWEKEZAJI ZAIDI KWENYE KILIMO

$
0
0

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akifanya mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Uholanzi nchini Jeroen Verheul ofisini kwake Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiangalia kitabu cha mbegu bora za aina mbalimbali za viazi mviringo vilivyoboreshwa ambacho kimeandaliwa na kuchapishwa na Ubalozi wa Uholanzi nchini ambacho alipewa na Balozi Jeroen Verheul ofisini kwake Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi ya kitabu chenye taarifa mbali kuhusu taifa la Uholanzi kutoka kwa Mgeni wake Balozi Jeroen Verheul ofisini kwake Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wataalam kutoka Ubalozi wa Uholanzi wakiongozwa Abdallah Msambachi (Kulia) ambaye ni Mshauri wa masuala la kilimo wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Kilimo na Balozi wa Uholanzi.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja na Mgeni wake Balozi wa Uholanzi nchini Jeroen Verheul nje ya ofisi yake Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

*************************************

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda leo (Jana) tarehe 9 Aprili 2021 amekutana na Balozi wa Uholanzi nchi Jeroen Verheul na kumwambia Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji katika Sekta ya Kilimo na kumuomba kushawishi uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo hususan kwenye uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta, usindikaji wa mafuta ya kula, uzalishji wa mazao ya mboga, matunda, viungo,maua pamoja na upatikanaji masoko ya mazao hayo.

“Nafikisha ombi kwako la kutusaidia kushawishi Wawekezaji zaidi nchini kwenye eneo la uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta, usindikaji wa mafuta ya kula na usindikaji wa mazao ya aina mbalimbali kwenye Sekta ya Kilimo pamoja na masoko ya mzao hayo.” Amesisitiza Waziri Mkenda.

Waziri Mkenda amesema Wizara ya Kilimo imejipanga ili kuhakikisha Sekta ya Kilimo inachangia ukuaji wa uchumi kwa kuongeza mara dufu fedha katika eneo la utafiti wa mazao ya mbegu za mafuta kama alizeti na pamba, uzalishaji wa mazo ya kimkakati pamoja na huduma za ugani na kuahidi kuwa mambo hayo yamewekwa kwenye utekelezaji wa bajeti inayokuja ya mwaka 2021/2022.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa fedha na msisitizo umewekwa kwenye kuzalisha mazao ya mbegu za mafuta ili kupunguza utegemezi kwenye eneo hilo ambalo nchi imekuwa ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 400 kuagiza mafuta ya kula kutoka nje.

Waziri Mkenda amesema kwa kuanzia Vituo vya Utafiti vitajikita katika kutafiti mbegu bora za mazao ya mbegu za mafuta ili kuja na mbegu bora lakini pia Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kupitia mashamba yake; ASA itazalisha mbegu bora kwa wingi ambazo zitauzwa kwa Wakulima kwa bei nafuu.

Eneo lingine ni pamoja na kuimarisha huduma za ugani kote nchini na kwa kuanzia Wizara imepanga  kuwawezesha Maafisa Ugani wa mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu kupata vitendea kazi kama kama pikipiki na kuwezeshwa pembejeo bora za kuanzisha mashamba darasa kwa kila Afisa Ugani.

“Pamoja na juhudi zote hizo lengo letu ni kuhakikisha tunatatua tatizo la masoko kwa Wakulima wetu lakini pia kuongeza uwekezaji kwa ujumla na ndiyo maana tunaona juhudi hizi tuwashirikishe na Sekta Binafsi ambayo itasaidia katika mageuzi katika kuendesha kilimo cha kisasa”. Amekaririwa Profesa Mkenda.

Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Jeroen Verheul ameahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Kilimo hususan kwenye uzalishaji wa mbegu bora za zao la viazi mviringo kupitia Mradi wa SHAWISHA unaotarajiwa kuanza baada ya kusimama kwa muda.

“Tutaendela kusaidia kwenye biashara ya mazao ya kilimo na uwekezaji kwa ujumla kwa sasa na kwa baadae hususan kwenye eneo la uzalishaji wa mbegu bora za viazi mviringo”. Amesisitiza Balozi Jeroen Verheul.

Lengo la Serikali ni kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 5 ifikapo mwaka 2025- Dkt. Allan Kijazi

$
0
0

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na Maafisa Utalii waliohudhuria Mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) yaliyofanyika katika ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na Maafisa Utalii waliohudhuria Mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) yaliyofanyika katika ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma leo.

Baadhi ya Maafisa Utalii  wakimsikiliza Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (hayupo pichani) alipokuwa akifunga Mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) yaliyofanyika katika ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma leo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga (katikati) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) baada ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kushoto) kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma leo.

************************************

 Na Happiness Shayo – Dodoma

Serikali iko katika mikakati ya kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka kutoka milioni 1.5 kabla ya Covid 19 hadi kufikia watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025 na pia kuongeza mapato yatokanayo na utalii kutoka dola milioni 2.6 hadi kufikia dola milioni 6 mwaka 2015.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi alipokuwa akifunga mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) yaliyofanyika katika ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma leo.

Dkt. Kijazi ameiagiza Idara ya Utalii  kuwa kinara katika kuongoza shughuli za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuhakikisha lengo la Serikali la kuongeza idadi ya watalii na kuongeza mapato yatokanayo na utalii linafikiwa.

“ Mafunzo haya ni moja ya mkakati wa Wizara hii ya kuhakikisha tunafikia lengo la Serikali la kuongeza idadi ya watalii na kuongeza mapato yatokanayo na utalii  nchini” Dkt. Kijazi amefafanua.

Aidha, Dkt. Kijazi ameongeza kuwa moja ya changamoto iliyopo ni kutokuwapo kwa takwimu sahihi za idadi ya maeneo yanayotoa huduma za malazi nchini hivyo kupelekea makusanyo ya mapato yatokanayo ya wageni kuwa kidogo kuliko hali halisi.

“Nimepewa taarifa kwamba kumbukumbu za maeneo yenye huduma za malazi zinafikia 1800, lakini kiuhalisia huduma za malazi zinatolewa katika maeneo mengi nchini” Dkt. Kijazi amesisitiza.

Ameongeza kuwa idadi ndogo ya huduma za malazi zilizopo zinazotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya mapato ni ishara ya Serikali kupoteza mapato katika maeneo mengi ambayo bado hayajaorodheshwa.

Amefafanua kuwa mafunzo ya Usajili wa Huduma za Malazi katika Mfumo wa Accommodation Services in Tanzania –(AserT) ni muhimu kwa sababu yatasaidia katika zoezi la utambuzi na uhakiki wa huduma za malazi kufanyika kwa ufanisi mkubwa ili Serikali iweze kupata matokeo yanayotarajia na pia yatasaidia kuwapo kwa kumbukumbu sahihi za watalii wanaopokelewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Dtk. Kijazi amewataka Maafisa watakaoshiriki katika zoezi la utambuzi na uhakiki wa huduma za malazi kuwa na nidhamu, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kufanikisha zoezi hilo.

“Hatutegemei mtumie rasilimali za Wizara halafu mje na takwimu ambazo si sahihi. Tusije tukaona kwamba hii ndio fursa ya kwenda kutembea yaani unaenda maeneo mawili halafu unaishia mtaani” Dkt. Kijazi  amesema.

Pia ametoa onyo la kuwachukulia hatua za kinidhamu  Maafisa watakaobainika kufanya kazi kwa mazoea.

“ Tukigundua kwamba haufanyi kazi yako kwa umakini tutakuchukulia hatua kwa sababu hii ni fursa pekee ya kutuwezesha sisi kupata takwimu sahihi kuhusu maeneo yenye huduma za malazi” Dkt. Kijazi amesema.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, ameahidi kutekeleza maagizo yote ya Katibu Mkuu, Dkt. Kijazi na kwamba kila mshiriki wa zoezi utambuzi na uhakiki wa huduma za malazi atapimwa kwa matokeo kwa sababu ni kazi muhimu sana kwa Wizara na kwa nchi.

Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo ambaye ni Afisa Utalii Mwandamizi, Franklin Mwenyembegu, amesema kuwa mafunzo hayo yamegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza iligusia mfumo wa Kieletroniki wa Tathmini ya Upangaji wa Huduma za Malazi na Chakula katika ubora wa Madaraja (Accommodation Services in Tanzania – AserT) utakaotumika na wamiliki wa huduma za malazi kufanya tathmini binafsi (Self-Assessment) ya huduma wanazozitoa kwa mujibu wa vigezo na hivyo kupanga madaraja ya ubora wa nyota wao wenyewe kabla ya kuthibitishwa na wathamini wa Serikali.

Amesema sehemu ya pili ya mafunzo hayo ilihusisha namna bora ya uchukuaji wa taarifa za huduma za malazi nchi nzima zitakazosaidia katika ukusanyaji wa tozo ya maendeleo ya utalii.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Maafisa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Utalii kutoka Ofisi za Utalii za Kanda ya Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mwanza

Rais Samia apokea ujumbe maalum wa Rais Kenyatta leo Ikulu,mkoani Dar es Salaam.

$
0
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Barua yenye Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta iliyowasilishwa kwake na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais Kenyatta leo tarehe 10 Aprili 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassanakisalimiana na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassanakisalimiana na Balozi wa Kenya hapa nchini Mheshimiwa Dan Kazungu ambaye aliambatana na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuwasilisha Ujumbe huo pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

 

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanahabari mara baada ya kupokea Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta wakwanza kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga wakwanza (kulia) pamoja Balozi wa Kenya hapa nchini Balozi Dan Kazungu mwenye tai nyekundu, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.


 

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZRI JAFO NA MHE, CHANDE

$
0
0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdori Mpango, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Selemani Jafo kushoto na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa  Hamad Hassan Chande kulia, kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais katika makazi yake Jijini Dodoma leo April  2021. katika mazungumzo yao Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mpango  amesisitiza juu ya utekelezaji wa haraka masuala ya Changamoto zilizobaki za Muungano na Mazingira ikiwemo suala la Mabadiliko ya Tabia Nchi.


KANISA LA WASABATO WAADVENTISTA WASHIRIKI IBADA YA PAMOJA NA WATU KUTOKA DINI MBALI MBALI

$
0
0

 


 
Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni, Baraka Butoke, akiongea na waandishi wa Habari akielezea dhumuni la ibada hiyo ya pamoja iliyofanyika katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam.
 
Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni, Baraka Butoke akiongoza ibada kwa maombi, katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam.
 
Waimba kwaya wakiimba nyimbo za kumsifu na kumtukuza Mungu, katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam.
 
Waumini wakiwa wanasikiliza neno kutoka kwa Mcungaji Baraka Butoke, katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam
 
Wageni waalikwa kutoka Maeneo mbali mbali wakiwa wamekaa kujumuika katika ibada ya pamoja, katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam.
Wageni waalikwa kutoka Maeneo mbali mbali wakiwa wamekaa kujumuika katika ibada ya pamoja, katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Leo Jumamosi 10/04/2021, Dar Es Salaam. 
 
********************
Na Mwandishi wetu.
Akizungumza na waandishi wa habari  Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni, Baraka Butoke amesema, Leo ni sabato malaamu ambayo kanisa limeamua kujumuika na jamii inayotuzunguka katika kumuabudu Mungu na kula chakula kwa pamoja

Mchungaji Baraka Butoke amesema, Ni sabato ambayo tumealika marafiki zetu majirani zetu na watu ambao wanaoshi katika mazingira magumu hasa ambao sio waimani yetu, ili waje waone tunavyo abudu pia washiliki kula pamoja nasi na Kumsifu Mungu.

Aidha amesema, dhumuni hasa ni kuabudu pamoja na kula chakula pamoja, pia tumefanya mialiko maalumu kwa viongozi wa dini hasa kwenye makanisa na misikiti iliyopo katika eneo hili linalo tuzunguka, na wote kwa pamoja wamejumuika nasi katika iba hii ya leo.
 
"Pia tumealika watoto wanao wanao lelewa katika vituo vya kuleleaa watoto yatima na ambao wapo katika mazingira magumu ili waje washiriki na watoto wetu ili nao wahisi upendo kutoka kanisa hili." Aamesema. 
 
"Hii sio mara ya kwanza sisi kushirikiana na watu mbali mbali katika ibada ya pamoja mfano, kama sabato tatu zilizopita kulikua na kundi maalumu ambalo tulienda kuwatembelea huko walipo na kuwapelekea maitaji mbali mbali, na hii ni programu endelevu tutaendelea kushirikiana nao na kisaidiana nao tunawajenga kimwili lakini pia tunawajenga kiroho." Amesema.

MKURUGENZI MKUU WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) ASIMAMISHWA KAZI

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb), amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi ili kupisha uchunguzi wa madai ya   ubadhirifu wa fedha pamoja na masuala ya kiutawala yanayohusu Rasilimali Watu katika ofisi yake.

Kufuatia hatua hiyo Mhe. Waziri amemteua Betrita James Lyimo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

Aidha, Dkt. Damas Ndumbaro ameielekeza Bodi ya Wakurugenzi ya TTB kuwasimamisha kazi watumishi wengine wanaohusika na tuhuma hizo kwa kuwa suala hilo lipo chini ya  Mamlaka yao ili waweza kupisha uchunguzi dhidi ya madai yanayowakabili.

Hata hivyo, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema maamuzi hayo hayahusiani na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Uteuzi huo unaanza rasmi leo tarehe 10 Aprili, 2021.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi

MKAZI WA TABORA ASHINDA TSH 521,471,360/- SPORTPESA, AMELIPA KODI MILIONI 100

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Mkazi wa Tabora - Sikonge, ambaye ni Maajiriwa wa Duka la Dawa na Maabara, Abdulaziz M. Ibrahim (24) amejishindia kitita cha Shilingi 521,471,360/- alichoshinda katika Jackpot ya Mechi 13 akiwa Mshindi wa awamu ya Sita wa Jackpot hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Abbas Tarimba amesema mshindi huyo wa Jackpot ya Mechi 13 atakabidhiwa kitita cha Shilingi 417,177,488/- na atalipa Kodi ya Shilingi 104,293,872/-

Tarimba amesema ili Wachezaji wa Jackpot hiyo washinde ilikuwa lazima watabiri matokeo yote 13 ya michezo hiyo kwa usahihi kwa matokeo yanayotokea uwanjani.

Kwa upande wake, Mshindi wa Jackpot hiyo, Abdulaziz M. Ibrahim amesema ushindi huo alioupata kupitia Jackpot hiyo ana malengo ya kujenga Msikiti, amesema hana maelngo ya kupata jiko kwa sasa hivyo atatumia pesa hiyo kwa masuala mengine.

 Wachezaji wa Young Africans, Farid Mussa, Bakari Mwamnyeto, Carlos Carlinhos na Mchezaji wa Simba SC, Miraji Athuman wakimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa awamu ya Sita wa Jackpot ya Sportpesa, Abdulaziz M. Ibrahim (24) alijishindia kitita cha  
Shilingi 521,471,360/-

2 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Abbas Tarimba akimkabidhi Mshindi mfano wa Hundi yenye kiasi hicho cha fedha.




MAJALIWA: SERIKALI ITAENDELEA KUTOA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI

$
0
0

 

 

 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akikagua kazi ya ujenzi wa Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Nyerere wilayani Rufiji, Aprili 10, 2021. 

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akiwapungia wajenzi wakati  alipokagua kazi ya ujenzi wa Mradi wa  Bwawa la kuzalisha umeme la Nyerere wilayani Rufiji, Aprili 10, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akikagua kazi ya ujenzi wa Mradi wa  Bwawa la kuzalisha umeme la Nyerere wilayani Rufiji, Aprili 10, 2021. Kulia  ni Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato  na kushoto ni  Mhandisi Mkazi wa Mradi, John Mageni.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………………………..

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha za kugharamia mradi wa umeme wa maji ya Mto Rufiji (RHPP) ili ukamilike kwa wakati.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 10, 2021) baada ya kukagua mwenendo wa mradi huo unatarajiwa kukamilika June 2022. Amesema kuwa Serikali itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.

Waziri Mkuu amesema amefarijika kuona kazi nzuri yenye viwango na ubora wa hali ya juu inayofanywa na Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy  Electric zote kutoka nchini Misri chini ya usimamizi wa TANESCO, TANROADS na Wizara ya Nishati.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha Watanzania kupata umeme mwingi na wa gharama nafuu ambao utasambazwa nchini kote na ziada kuuzwa nje ya nchi ili kulipatia Taifa fedha za kigeni.

Waziri Mkuu amesema bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 ambazo zikijumlishwa na megawati 1,500 zinazozalishwa na vyanzo mbalimbali nchini hivi sasa zitaifanya Tanzania kuwa na umeme utakaotosheleza mahitaji yake na ziada kuuzwa kwa majirani.

”Lengo la kuanzisha mradi huu ni moja ya juhudi za Serikali za kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa sababu uzalishaji wake ni wa gharama nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine. Uniti moja ya umeme unaozalishwa kwa kutumia maji inagharimu shilingi 36 hadi shilingi 50 huku umeme unaotumia vyanzo vya mafuta uniti moja inazalishwa kwa gharama ya shilingi 440 hadi shilingi 600.”

Amesema faida nyingine ya ujenzi wa mradi huo ni pamoja na kuzalisha ajira kwa Watanzania mbalimbali wanaoshiriki katika kuujenga na kutoa huduma mbalimbali kama wauzaji wa vifaa vya ujenzi, mafuta, vyakula na huduma nyingine zinazohitajika kwenye mradi huo.

Waziri Mkuu amesema tayari TANESCO imeshatangaza zabuni ya ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka kwenye chanzo cha mradi huo hadi Chalinze mkoani Pwani na ukifika Chalinze njia moja itakwenda Dar es Salaam na nyingine Dodoma ili kuwezesha umeme huo kusambazwa nchi nzima.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Nishati ifuatilie changamoto zote zinazoweza kukwamisha ujenzi wa mradi huo ili kuzipatia ufumbuzi na ihakikishe unakamilika kwa wakati. Pia amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kutoa ushirikiano kwa wajenzi kwa kuwahakikishia usalama wao, mali zao na vifaa vinavyotumika katika ujenzi huo.

Mapema, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameishukuru Serikali kwa kuwa wakati wote tangu kuanza kwa mradi huo hadi sasa imeendelea kutoa fedha za kugharamia mradi huo kwa wakati na tayari imeshatoa zaidi ya shilingi trilioni mbili. Hadi kukamilika mradi huo utagharimu shilingi trilioni 6.5.

WAZIRI CHAMURIHO ATAKA TAASISI ZA UJENZI, UCHUKUZI KUWAJIBIKA

$
0
0

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho, akizungumza na Wakurugenzi wa Wizara, Wakuu wa Vitengo,  pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake (hawapo pichani), katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Mwita Waitara.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Mwita Waitara, akisisitiza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Wakurugenzi wa Wizara, Wakuu wa Vitengo pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho. 

Wakurugenzi wa Wizara, Wakuu wa Vitengo pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho (hayupo pichani),  katika kikao kazi kilichowakutanisha viongozi hao jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire (Wakwanza kushoto), akitoa maoni yake kuhusu uboreshaji wa Utendaji wa Wizara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho, katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandsi Patrick Mfugale akishauri jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Wakurugenzi wa Wizara, Wakuu wa Vitengo pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi jijini Dodoma. PICHA NA WUU

************************************

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake kuhakikisha wanaandaa taarifa kila mwezi zinazoelezea utekelezaji wa majukumu yao ili kusaidia Wizara kufahamu kwa undani utendaji wa Taasisi hizo ikiwemo mafanikio na changamoto zake.

Hayo aliyasema Waziri huyo, jijini Dodoma, katika kikao kazi cha kumtambulisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mhe. Mwita Waitara, kwa mara ya kwanza kwa viongozi wa Taasisi hizo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa Wizara itakuwa inaandaa vikao kama hivyo  mara nne kwa mwaka ili kujadiliana kwa pamoja na kupata tathmini na  mwelekeo wa Wizara katika ufanisi wake wa utendaji kazi.

“Nimeamua leo kuitisha kikao hiki ili kumtambulisha Naibu Waziri kwa wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yangu, pia kukumbushana kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyo katika Taasisi zao”, amesema Waziri Chamuriho.

Aidha, Chamuriho amezisisitiza Taasisi hizo kushirikiana na kuwajibika ipasavyo katika miradi wanayoitekeleza kwani mingi huigusa jamii ambapo ameongeza kuwa, kufanya hivyo kutapelekea maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.Mwita Waitara, amewataka viongozi hao wa Taasisi kumpa ushirikiano wa kutosha na kwamba ofisi yake itakuwa wazi kwa ajili ya kupokea ushauri na maoni mbalimbali  lengo likiwa ni kusaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara hiyo ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

“Naomba Wakuu wa Taasisi wanipe tu ushirikiano wa kutosha na niwabainishie kuwa Ofisi yangu itakuwa wazi wakati wote kwa ajili ya kupokea ushauri lengo likiwa ni kuleta tija na maendeleo kwa wananchi”, amefafanua Naibu Waziri Waitara.

Naye, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Arch.Edwin Nunduma,  amesema kuwa agizo hilo la Waziri la kuleta taarifa za utekelezaji Wizarani litawafanya kuwajibika zaidi kutokana na kuwa Wizara itafuatilia kwa karibu utendaji wao.

“Utaratibu huu ni mzuri, kwani hata changamoto zikitokea itakuwa ni rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema na kwa haraka kuliko kusubiri kuleta taarifa ya robo mwaka  kwa kila kota kama ilivyo awali”, amesema Nunduma.

Kikao hiki cha siku moja ambacho kimemkutanisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.Mwita Waitara, Menejimenti ya Wizara hiyo pamoja na viongozi wakuu wa Taasisi 23 zilizo chini ya Wizara hiyo , kilikuwa na lengo la kutambuana na kukumbushana kuhusu uwajibikaji katika Taasisi zao.

DC ARUMERU ATOA SIKU 30 ZA MAZUNGUMZO YA FAMILIA KUFUATIA KUWEPO KWA MGOGORO WA ARDHI

$
0
0

Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro ametoa siku 30 za mazungumzo ya familia ya Losujake Sung'are ikiwa ni pamoja na kuifunga njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na mmoja wa wanafamilia hao.

Hatua hiyo imefuatia kutokana na kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina ya wanafamilia hao ambapo Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza kufungwa kwa njia hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa ipo njia nyingine ya umma ambayo itamuwezesha kupita na mahakama itakapotoa hukumu.

"Eneo hili halitapita tena mtu mpaka hapo mahakama itakapoamua,wewe mama hutapita yena hapa na wewe kijana hutakanyaga kwenye hii nyumba mpaka mahakama itakapotoa maamuzi."Alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya

Aidha Muro alieleza kuwa ametoa uamuzi huo baada ya kuzunguka eneo na kujiridhisha pasipo shaka kuwa ipo njia nyingine ya umma ambayo anaweza kupita ambapo amesema mamlaka hiyo anayo kwani sheria ya usalama wa yaifabinampa nguvu kuzuia ili watu wasiendeleze mgogoro kwa kipindi hicho alichokitoa.

Awali Mkuu huyo akisikiliza malalamiko ya pande zote mbili aliwataka wanafamilia hao kutouza maeneo yao ya urithi baada ya mgogoro huo kuisha kwani kila mmoja anastahili kupata haki sawa na mwingine kutoka katika urithi wa wazazi wao na kusema kuwa mgogoro unatokea pale mtu mmoja anapotaka kupata sehemu mara mbili ambapo amemtaka kila mmoja kuridhika na alichonacho.

Kwa upande wa wanafamilia hao aliejitambulisha kwa jina la Withness Osujake mama mdogo wa Olais Osujake amesema kuwa hajaridhishwa na uamuzi alioutoa Mkuu huyo wa Wilaya wa kumzuia kupita akidai kuwa hana mahali pengine pa kupita ili hali Olais Osujake alitenga njia mbadala ya mama huyo kupita.

Alieleza kuwa kitu kilichokuwa na mgogoro siyo barabara bali ni nyumba hivyo ataendelea kupita katika barabara hiyo ambapo ameiomba serikali imsaidie ili aweze kupata haki yake.

Naye Olais Osujake Laizer ambaye eneo lake ndilo yenye mgogoro ameunga mkono maamuzi aliyoyatoa Mkuu wa Wilaya hiyo ya kumzuia kwa muda wa siku 30 mama huyo kupita katika njia iluyopo kwenye eneo lake na yeye kutoingia katika nyumba hiyo yenye mgogoro mpaka pale watakapo weka mambo yao sawa na mahakama kutoa maamuzi kwani mama huyo amekuwa akitoa kauli za matusi wakati anapopita katika eneo hilo ameiomba serikali kumsaidia ili aweze kupata haki yake.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha,Bi.Eliasifiwe Kileo amesema kuwa suala lolote linapofikishwa mahakamani kinachotakiwa kutekelezwa ni maamuzi ya mahakama hivyo amewataka wanafamilia hao kufuata amri iliyitolewa na mahakama ya kurudia kusikiliza utekelezaji wa amri ya baraza la kata katika baraza la ardhi la nyumba la wilaya.

Pamoja na hayo Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha,Bi.Hadija Ntimizi amesema kuwa migogoro mingi ya ardhi inatokana na maeneo kutorasimishwa hivyo kutokana na mgogoro huo amesema kuwa eneo hilo halina njia katikati.

"Moja ya kanuni katika urasimishaji kila kipande cha ardhi kifikike ili kuweza kutoa urahisi wa huduma pindi majanga yanapotoa ikiwa ni pamoja na kutokomeza vichochoro."Alieleza Bi.Hadija

Katika hatua nyingine Muro amesitisha ujenzi wa nyumba na utaratibu wa kuomba maeneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba katika maeneo katika eneo lililowazi kwa muda wa siku 7 hadi atakapokaa na kuzungumza na uongozi wa halmashauri,wakala wa mbegu ASA pamoja na wakaazi walio katika maeneo hayo.

Muro ameleza kuwa lengo ni kutafuta ukweli kama wakala wa mbegu ASA wametoa eneo hilo kwa Halmashauri na baada ya upimaji wa eneo hilo halmashauri waliweza kutoa kipaumbele kwa wananchi wanaokaa katika eneo hilo au lah!ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu kama Halmashauri imepima na kuuza viwanja.

"Katika hatua ya awali tumesitisha chchote hapa mpaka serikali ya wilaya itakapomaliza kulichunguza jambo hili na kuja kutoa taarifa rasmi kwenu wananchi ya nani anamiliki nini na nani ni nani katika eneo husika."Alieleza Muro.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Ndg.Jerry Muro katikati akitoa ushauri kwa familia ya mzee Osujake ili kuweza kupata utatuzi katika  mgogoro wa ardhi kwenye familia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akiwataka wakazi wa Ngaramtoni walio katika eneo lililokuwa likimilikiwa na wakala wa mbegu ASA kuwa na subiri wakati serikali ya wilaya ikifanya mazungumzo na ASA pamoja na Halmashauri ya Arusha kuweza kubaini eneo hilo kama limepimwa na ninani miliki halali wa eneo hilo ili kuweza kutoa fursa kwa wakazi hao kununua eneo hilo na kujenga makazi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa na wanafamilia wenye mgogoro wa nyumba,mali ya marehemu mama yao.
 

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI UGANDA

Bolt yapokea uwekezaji wa Euro 20 milioni kutoka IFC

$
0
0

 

 


BOLT yapokea uwekezaji wa Euro 20 millioni kutoka IFC kuongeza upatikanaji wa huduma za usafiri katika nchi zinazoendelea

 Kampuni inayoongoza ya usafiri kwa njia ya mtandao, Bolt imepokea uwekezaji wa €20 millioni (Euro) kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) utakaosaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za usafiri katika masoko yanayokua, ikiwemo Tanzania.

 Uwekezaji huo ambao unajumuisha huduma za ushauri kutoka IFC – mshirika wa Benki Ya Dunia, itasaidia Bolt kupanua huduma za usafiri zinazochangia ukuaji wa biashara ndogo ndogo, kukuza fursa za ajira na kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri katika masoko ya Afrika na Ulaya Mashariki.

  “Tuna matarajio makubwa ya kushirikiana na IFC kuchangia ujasiriamali, kuwezesha wanawake na kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za usafiri barani Afrika na Ulaya Mashariki. Uwekezaji huu ukijumuishwa na ule tuliopata mwaka jana kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya inatufanya tuwe na washirika wengi wakubwa wanaoamini umuhimu wa Bolt katika masoko mapya,” Markus Villig, Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Bolt alisema.

 Stephanie von Friedeburg, ambaye ni Makamu Mkuu wa Rais wa IFC anayesimamia masuala ya utendaji alisema “Teknologia inaweza na inafaa kufungua fursa mpya za maendeleo endelevu na kuwawezesha wanawake. Uwekezaji wetu katika kampuni ya Bolt unalenga kuwezesha teknologia kuleta mageuzi chanya katika sekta ya usafiri kwa njia ambazo ni rafiki kwa mazingira, kutoa fursa zaidi za ajira kwa wanawake na kuleta usafiri salama na wa gharama nafuu katika masoko yanayochipuka.”

 Bolt kwa sasa inapatikana katika nchi 7 barani Afrika huku ikitoa fursa za kipato wa madereva 400,000 katika miji 70 barani.

 “Tunaongeza kipato miongoni mwa jamii kwa kuwapa madereva wanaotumia mfumo wetu fursa za kujipatia malipo. Huduma zetu zinaleta mageuzi ya usafiri wa haraka na nafuu kwa mamilioni ya watu wanaoishi mjini,” Mkurugenzi wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka alisema.

 Nchini Tanzania, Bolt inatoa huduma za usafiri wa magari, pikipiki (bodaboda) na pikipiki za miguu mitatu almaarufu bajajii katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza.

Viewing all 119842 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>