Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119887 articles
Browse latest View live

MONETARY POLICY STATEMENT

$
0
0

 



Monetary Policy Committee Statement

The Monetary Policy Committee (MPC) held its 213th Ordinary Meeting on 6th April 2021 to assess the recent performance of the economy and outcome of monetary policy. The MPC was satisfied with the performance of the economy, amidst circumstances of gloomy global growth caused by COVID-19. Against this backdrop, the MPC decided to maintain monetary policy easing stance to facilitate fast economic growth and lending to the private sector. The decision is in line with the objective of achieving inflation of 3-5 percent in 2020/21.

 

 The MPC was concerned about the slow pace of recovery of the global economy over recent months due to COVID-19 pandemic, and observed that the outlook has improved owing to fiscal stimulus and accommodative monetary policy executed in several countries. The improved growth prospects provide favourable environment for exports and investment in the country.

 On domestic economy, the MPC observed that the performance was fairly satisfactory compared to regional peers, despite global effects of the pandemic on economies. The economy grew at 4.7 percent in the first three quarters of 2020, driven by construction, agriculture, transport, and mining and quarrying. Given the relatively good performance of some sectors in the fourth quarter, growth projection of 5.5 percent in 2020 could be realized. In 2021, the economy is projected to grow at 5.7 percent or higher, due to sustained public investment, normalization of global trade and investment, and rolling out of measures to improve the business environment and bank lending to the private sector.

 The MPC also took note of rebasing of consumer price index (CPI) in January 2021, to reflect current consumption pattern of goods and services by households, due to changes in taste, preference and technology. The new CPI covers 383 consumer goods and services compared to 278 in the old CPI. The proportion of core increased to 73.9 percent from 54.3 percent, while that of food declined to 28.2 percent from 38.5 percent, indicating growth in average income of households. Inflation remained low, within the target range of 3-5 percent, and is projected to remain low, despite renewed increase in oil prices in the world market. 

The external sector remained sustainable, benefiting from higher gold prices and subdued oil prices in the world market, despite realizing reduced tourism receipts. Foreign exchange reserves were adequate, sufficient to cover about 6.2 months of imports. Government fiscal operations were broadly on track, with satisfactory revenue performance, notwithstanding the global challenging environment on some sources. The country debt remains sustainable, with low risk of distress. 

 The MPC took note of the progress made by the Bank of Tanzania in addressing constraints to credit to the private sector and high lending rates, and underscored the need to expedite implementation of the measures adopted to facilitate growth of the economy. In addition, the MPC noted the extension of LIBOR cessation to 2023, and urged the Bank of Tanzania to continue engaging stakeholders during the transition period, with a view to reaching consensus on available alternative reference rates.

 

 Governor

  Bank of Tanzania


WAZIRI MKUU BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, Bungeni jijini Dodoma, Aprili  9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 

KUTOKA MTAANI KWETU NDANI YA CHANIKA

$
0
0
Vijana wa Bobadoba  wakiwa katika kituo cha Mabasi cha Chanika  jiji la Ilala Mkoa wa Dar es Salaam wakisubiri wateja kama wanvyoonekana pichani)(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Wakazi wa Chanika wilaya Ilala jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kazini kama wanavyoonekana katika picha.

JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA LAKAMATA WATUHUMIWA ZAIDI YA 100 KWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha  ACP-Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi 2021, lilifanya operesheni maalum ya kupambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa Arusha ambapo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 157waliokutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Bhangi na Mirungi.

Akionge na waandishi wa habari Kamanda w polisi mkoa wa Arusha ACP-Justine Masejo alisema kuwa kufuatia Operesheni hiyo walifanikiwa kukamata watuhumiwa 12 wote wa Kiume wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine kiasi cha gramu 536 na jumla ya kesi 11 zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema kwa upande wa madawa ya kulevya aina ya bhangi, kesi 81 zilifunguliwa ambapo jumla ya kilogramu 114 na gramu 624 zilipatikana pamoja na watuhumiwa 87 kukamatwa kati yao wanaume 76 na wanawake 11 huku akibainisha kuwa kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali za kiupelelezi.

"Aidha katika operesheni hiyo tulifanikiwa kupata kilogramu 271 za Mirungi
ambapo jumla ya kesi 49 na watuhumiwa 58 walikamatwa kati yao wa
kiume 53 na wa kike ni 05 kesi hizo pia zipo katika hatua mbalimbali za
upelelezi."Alisema

Alibainisha kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na operesheni kali dhidi ya wananchi wanaojihusisha na madawa ya kulevya pamoja na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kusema kuwa hawata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria pindi tutakapo wakamata ambapo pia aliwaomba wananchi kushirikiana na nao ilikutokomeza kabisa matumizi na Biashara ya madawa ya kulevya

Alitoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo ya madawa ya kulevya ambapo aliwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu ili mkoa uendele kuwa shwari asanteni.

KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA AITAKA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI KUZINGATIA UWAZI NA MIIKO YA KAZI YAO

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza wakati akifungua Kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali unaofanyika jijini Dodoma.

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata akitoa utangulizi wa ufunguzi wa Kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali unaofanyika jijini Dodoma.

 Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu Wizara ya Katiba na sheria, Prof. Sifuni Mchome amewataka watumishi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali kuzingatia ushirikishwaji katika ngazi zote sambamba na kufanya kazi kwa uwazi, huku wakifuata miiko ya kazi yao.

Prof. Mchome ameyabainisha hayo jijini Dodoma wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili mkuu wa Serikali ambapo amesema kutokana na unyeti wa ofisi hiyo inahitajika kila mtumishi kufanya kazi wa weredi huku wakilenga kutafuta matokeo.

“ Mfuate maadili ya kazi yenu maadili yanakusaidia katika kutekeleza majukumu yako kikamilifu, sekta yenu ni muhimu sheria ikisimama na hata nchi itatulia” amesema Prof. Mchome.

Amesema mabaraza ya wafanyakazi ni muhimu sana katika maeneo ya kazi kwa sababu huko ndiko ushirikishwaji utafanyika ni muhimu kila taasisi iwe na mabaraza hayo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria.

“Serikali itahakikisha taasisi zake zote zinatekeleza takwa hili la sheria la kuwa na mabaraza ya wafanyakazi huku ndiko kutafanyika ushirikishwaji katika mambo mbalimbali kwa watumishi katika ngazi zote” amesema.

Amesema katika majukumu yao wafanye kazi wakilenga kupata matokeo chanya katika kutafuta ushindi katika kesi mbalimbali ambazo wanazisimamia katika ofisi zao zilizopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amewataka kujenga utaratibu wa kufanya tathmini za mara kwa mara katika kazi wanazozifanya ili kuona namna ya kuboresha kazi zao kwani bila tathmini hawawezi kupata kile walichokusudia katika sekta ya sheria hapa nchini.

Ameongeza kuwa “mkasikilize kero za wananchi tunakofanya ziara huko mikoani malalamiko ni mengi, naamini huko mnaofisi zenu mkashughulikie hayo malalamiko ni mengi sanaesema.

Aidha amewataka wataalamu hao kwendana na kasi ya sasa na sio kufanyakazi kwa mazoea kwani kwa sasa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo nao wabadilishe namna ya ufanyaji kazi ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati ili kama nchi kupata mafanikio zaidi.

Awali Wakili Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo, Gabriel Malata amesema kikao hicho ni cha pili kwa mwaka wa fedha 2020 -2021, ambao wanakutana kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu ofisi hiyo.

Pia amebainisha kuwa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa Feb, 12, 2018 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt John Magufuli na kupewa jukumu la kuendesha, kuratibu, na kusimamia mashauri mbalimbali yanayohusu Serikali na taasisi zake.

Amesema katika kipindi cha mwezi julai 2020, hadi Februari 2021 ofisi hiyo imeshughulikia jumla ya mashauri 3715, kati ya hayo mashauri ya madai ni 3625 na 90 ni ya usuluhishi, jumla ya mashauri 451 kati ya 3715 yaliendeshwa na kumalizika.

Kati ya mashauri hayo 422 ni ya madai ambayo yanajumuisha mashauri 418 ya madai ya ndani ya nchi yakiwamo 13 ya uchaguzi na mashauri manne (4)ya madai ya nje ya nchi, na kukamilika kwa mashauri hayo kumepelekea kuokoa zaidi ya shilingi  bilioni 643.7, ambazo zingelipwa na serikali kama ingeshindwa.

Aidha amesema ofisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya kukosa muundo wa uendeshaji wa ofisi hiyo ambapo kwa sasa wanatumia muundo wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

ECLA AFRICA CONSULT KUTOA MAFUNZO YA KUANDAA MAHESABU KWA MFUMO WA IPSAS

$
0
0

Na Mwandishi Wetu.

TAASISI ya ECLA Africa Consult  yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam, inayojihusisha na masuala ya ukaguzi, ushauri wa kifedha na kodi  inatarajia kuendesha kwa vitendo mafunzo ya siku tano kwa wahasibu na wakaguzi  kutoka NGO's, taasisi za Kidini na  mashirika ya serikali.

Aidha mafunzo  yatahusisha mbinu ya kuandaa taarifa za fedha (financial statements)  kwa kutumia mfumo wa IPSAS (IPSAS framework).

Mafunzo hayo yameandaliwa kufuatia maamuzi ya Bodi ya wahasibu na wakaguzi, ya 22 June 2020 kubadili mfumo wa kuandaa taarifa za kifedha kutoka IFRS (International Financial Reporting Standards) kwenda IPSAS (International Public Sector Accounting standards)  kwa NGOs, Taasisi za dini na Mashirika.

Akizungumza juu ya mafunzo hayo Meneja Ubia  wa ECLA Africa Consult,  Lauden Cheyo, alisema kuwa, mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika  kuanzia 12 Aprili hadi 16 Aprili, mwaka huu katika hoteli ya Regency Park , iliyopo Mikocheni Jijijini Dar es Salaam.

"ECLA Africa Consult, tayari tumefungua milango kuanzia  Aprili Mosi mwaka huu kwa washiriki kujiunga na mafunzo haya kwa vitendo  kwa kulipia kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni moja (Mil.1000000)" alisema Cheyo  na kuongeza kuwa

"Nafasi bado zipo kwa mshiriki kuweza kulipia kupitia benki ya CRDB akaunti namba 0150554143800, jina la akaunti Ecla Africa Consult."

Aidha Cheyo  alieleza kuwa, washiriki watapata wasaa wa kupata mafunzo hayo ya kibobezi na mwisho wa mafunzo hayo  washiriki wote  watatunukiwa vyeti maalum.

Aidha, washiriki pia wanaweza kuwasiliana na waandaji hao moja kwa moja kupitia mawasiliano yao +255762148095 ama +255713040994.

Pamoja na mambo mengine  Cheyo alijinasibu kuwa Kampuni ya ECLA Africa Consult inaamini mafunzo hayo yataleta tija kwa washiriki kwa kuwawezesha kuandaa taarifa za fedha zinazokidhi viwango vya mfumo wa IPSAS.

Meneja Ubia wa ECLA Africa Consult, Lauden Cheyo

TISA MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MUME NA MKE

$
0
0
Na Amiri Kilagalila,Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe linawashikilia watu tisa wa mtaa wa Itulike kata ya Ramadhani mjini Njombe kwa tuhuma za kutekeleza mauji ya Mume na Mke huku sababu kubwa ikitajwa kuwa mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.

Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah,amesema familia iliyouawa kwa nyakati tofauti kwa kupishana siku moja ni Nikodemas Ng’ande (60) mwanaume pamoja na Renatha Mtega (60) mwanamke wote wakazi wa Itulike.

“Tukio hili ni la kusikitisha wameuawa mke na mume,wameuawa kwa kupishana siku moja katika kijiji cha Itulike kata ya ramadhani.tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka huu aliuawa mama Renatha Henry Mtega na maiti yake ikaenda kutupwa kwenye msitu wa TANWAT msitu huu ni wakupandwa miti aina ya paini”alisema Kamanda Hamis

Amemtaja marehemu mwingine kuwa ni Nikodemas Ng’ande “Tarehe ishirini akauawa mme wake    akabebwa kutoka Itulike akapelekwa Maheve na mwili ulihifadhiwa hapo ukiwa umefungwa kwenye turbai.”Alisema Kamanda Issa.

Kamanda Issah amesema taarifa za mauaji hayo zilipatikana mara baada ya mtoto wa marehemu Bwana Emmanuel Danford alipofika nyumbani kwao na kukuta nyumba tupu bila mtu yeyote hatua iliyomlazimu kuanza kutoa taarifa kwenye uongozi wa eneo husika.

Aidha amesema jeshi hilo limewakamata watu tisa kwa tuhuma za kukaa na kutengeneza mpango wa mauaji ya familia hiyo.

“Polisi ilianza kufanya uchunguzi na kukamata watu 9 ambao walikaa katika mahabusu ya polisi na baadaye katika ilibainika kuwa ndio walio kaa na kupanga kuua hawa watu wa familia moja na matokeo yake tarehe ya jana waliweza kwenda kuonyesha mwili wa marehemu mzee Nicodemas akiwa amekufa kikatili.” Alisema Kamanda Issah

Vile vile amesema watuhumiwa waliweza kuonyesha vifaa vilivyotumika katika kutekeleza mauaji hayo ikiwe Nyundo na Sululu huku sehemu za miili ya marehemu ikiwemo kichwani zikiwa zimeharibiwa kikatili.

Ametoa rai kwa jamii ya mkoa wa Njombe kuacha imani za kishirikina zinazopelekea mauaji ya kutisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watuhumiwa walioko katika magereza ya mkoa huo yametokana na kesi za mauaji huku wengi wao wakiwa ndugu waliotekeleza kutokana na migogoro ya aina mbali mbali.

EL CLASSICO KUCHEZWA WIKIENDI HII!

$
0
0

Meridianbet Inakuletea Odds Kubwa Na Za Kijanja Kabisa Kukamilisha Wiki yako.


Timu kubwa kibao kukutana katika viwanja mbalimbali wikiendi hii. 

Chagua Meridianbet na uweze kuwa mshindi wa kibingwa. Mchongo mzima upo hivi;


Kwenye Ligue 1 Ijumaa hii, Lille watakuwa wageni wa Metz. Hii ni nafasi nyingine kwa Lille kukaribia ubingwa.Meridianbet imekuandalia Odds ya 1.85 kwa Lille.


La Liga kutakuwa na EL Classico, Pale Estadio De Stefano Real Madrid watawaalika Barcelona, katika kutafuta usukani wa ligi hiyo. Meridianbet imekuwekea odds ya 2.40 kwa Barcelona


EPL kuendelea Jumamosi hii. Kwenye Uwanja wa Anfield, Liverpool watakuwa wenyeji wa Aston Villa. Ukichagua Meridianbet, utakuta Odds ya 1.60 kwa Liverpool.


Jumamosi hii pia, katika Bundesliga, kutakuwa na mechi kati ya Bayern Munich na Union Berlin. Ukichagua na Meridianbet, utakuta Odds ya 1.42 kwa Bayern Munich. 


Siku ya jumapili, katika ligi kuu Uingereza, Tottenham watawaalika Manchester United. Weka Utabiri wako, kwani Meridianbet tumekuwekea Odds ya 2.50 kwa Manchester United


Kule Italia katika Serie A, Lazio watakuwa wageni wa Verona. Na ukichagua Meridianbet, utakuta Odds ya 2.15 kwa Lazio.  


Katika La Liga Siku ya Jumatatu, baada ya kuwafunga Atletico Madrid, Sevilla watakuwa ugenini kuwakabili Celta Vigo. Meridianbet kumekuwekea Odds ya 2.25 kwa Sevilla


Meridianbet, Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!


WAZIRI GWAJIMA AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA KUKUBALI MABADILIKO ILI KUBORESHA WELEDI KAZINI

$
0
0


Na WAMJW-Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka watumishi wa Wizara hiyo pamoja na Sekta ya Afya kwa ujumla kukubali mabadiliko ya uongozi na kuangalia namna ya uendeshaji ili kuzidisha uweledi katika maeneo yao ya kazi.

Waziri Gwajima amesema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwapokea viongozi wapya walioteuliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuapishwa mapema wiki hii.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale ambao leo wameripoti rasmi ofisi za  Wizara  jijini Dodoma.

"Tuimalishe mifumo ya kufanya kazi pamoja kama tulivyoimarisha mifumo ya kufanya na mataifa mengine, tuna makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kutekeleza dira ya afya duniani. Tunashindwaje kuwa na makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kutekeleza sera yetu?". amehoji Waziri Gwajima.

Waziri Gwajima ameongeza kuwa kuna watu huwa wanaanzisha ajenda ambazo kimsingi Wizara inakua haina haja nazo huku akitoa onyo kwa watumishi wa Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoandaa vikao ambavyo ajenda zake zinakua siyo za kueleweka.

Aidha, Waziri Gwajima ameagiza wakurugenzi wa idara zilizopo Wizarani kutengeneza vikao vya mashirikiano ili kuwezesha mnyororo wa kutoa huduma za afya kufanyika kwa uweledi na kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema ushirikiano baina ya viongozi mbalimbali wa Wizara pamoja na taasisi zake ni chachu kubwa ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kuongeza kuwa viongozi hao wote ni washauri wa Mhe. Waziri wakiwa na lengo la kuboresha huduma za afya nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi amesema ana imani kubwa kuwa wataalamu waliopo katika Sekta ya Afya wanaweza kufanya kazi nzuri katika kusimamia afya za Watanzania na kuweza kutimiza matarajio ya Rais. Lakini pia Prof. Makubi amewashukuru watumishi wa afya kwa kazi kubwa na hakusita kuomba ushirikiano kutoka kwao ili kuweza kuitekeleza sera ya afya ambayo iliandaliwa na Wizara.

Vilevile Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale akitoa Shukrani zake mbele ya Waziri Gwajima amebainisha maeneo yake kadhaa ya utendaji ili kuboresha sekta ya afya.

Ametaja  maeneo hayo ni Uongozi, Uwajibikaji na Utawala bora. Eneo la pili ni kuhusu masuala ya fedha, eneo la tatu ni kuhusu bidhaa za afya, Nne ni Rasilimali watu, Tano ni Masuala ya TEHAMA, Sita ni Huduma kwa Mteja, Saba ni kuhusu masuala ya utafiti na la Nane ni Kuhusu ushirikiano na Sekta Binafsi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na kutoa maelekezo kadhaa kwa watumishi wa Wizara hiyo wakati wa hafla ya kuwapokea viongozi wapya jijini Dodoma.
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akitoa neno la shukrani kwa watumishi wa Wizara ya Afya (Hawapo pichani) wakati akipokelewa katika Wizara hiyo Jijini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe akiongea mbele ya Watumishi wa Wizara ya Afya katika ukumbi mdogo wa Wizara uliopo Area D jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Abel Makubi akipokea kadi ya kumtakia heri katika majukumu yake mapya kutoka kwa Waziri Dkt. Gwajima na Naibu Waziri Dkt. Mollel katika hafla ya mapokezi jijini Dodoma.
 

UTARATIBU MBOVU KUIGHARIMU BENKI IWAPO FEDHA ZA MTEJA ZITAIBWA

$
0
0

 

Na. Peter Haule na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Serikali imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hutoa adhabu kwa Benki yeyote itakayobainika kusababisha fedha za mteja kuibwa kutokana na utaratibu uliowekwa na Benki husika kuwa na kasoro.

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi, Hamad Yussuf Masauni (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Jang’ombe, Bw. Ali Hassan King, aliyehoji wizi unapotokea kwenye akaunti ya benki ya mteja uliofanywa na mtumishi wa benki nani mwenye wajibu wa kumlipa mteja.

“Endapo itabainika kuwa wizi umefanywa na mtumishi wa Benki, hatua stahiki huchukuliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na mteja kulipwa kiasi alichoibiwa”, alisema Mhandisi Masauni.

Alieleza kuwa mhalifu huchukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili Sheria ichukue mkondo wake.

Mhandisi Masauni alibainisha kuwa, wizi unapotokea kwenye akaunti ya benki ya mteja, uchunguzi wa kina hufanywa na vyombo husika katika masuala ya upelelezi ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kadri hali na mazingira ya tukio yatakavyokuwa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Mhandisi, Hamad Yussuf Masauni (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Jangómbe, Mhe. Ali Hassan Omar King, kuhusu wajibu wa kumlipa mteja aliyeibiwa fedha kwenye akaunti ya benki, bungeni jijini Dodoma.



 

WAKAZI 70 WA KATA YA UHAMAKA WAPATA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UKATILI.

$
0
0

Afisa Mradi  wa Shirika  lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL)Mkoa wa Singida, Philbert Swai, akielekeza jambo katika  mafunzo ya kuwawezesha vijana kupambana na ukatili wa kijinsia yaliyofanyika juzi Kata ya Uhamaka.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Edna Mtui akitoa mada.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza ukatili na ukeketaji kutoka Shirika hilo,   Annamaria Mashaka akitoa mada katika mafunzo hayo.
Vijana wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Elizabeth Haji akitoa mada.
Mafunzo yakiendelea.
Mkunga wa Jadi, Monica Irumba, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Rajab Chagama akitoa mada.
Mwakilishi wa kundi la vijana, Zainabu Kijanga, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, John Nzungu akitoa mada.
Washiriki wa Kundi la Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Viongozi wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


VIONGOZI wa dini wamewataka wazazi kutowaruhusu na kuwaelekeza watoto wao mambo ya kufanya na yale yasio wapasa kuyafanya kuliko kuogopa wakidhani kufanya hivyo ni kuwajengea tabia mbaya.

Hayo yalisemwa jana na viongozi hao katika Kata ya Uhamaka Manispaa ya Singida walipokuwa wakipatiwa mafunzo ya kuwawezesha kupambana na ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Shirika lisilokuwa la Serikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la mkoani hapa.

Katika Mafunzo hayo yaliyoshirikisha makundi mbalimbali yenye zaidi ya watu 70 ya vijana, wakunga wa jadi, mangariba wastaafu,watu maarufu pamoja na viongozi wa dini ndani ya kata hiyo, Viongozi hao walieleza bayana kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa kuwa wakiwaachia uhuru sana watoto wao na kupelekea kujifunza mambo yasiyofaa ambayo yanakuja kuzaa vitendo vya ukatili.

"Wapo wazazi hasa wa kike wanatumia hizi simu kubwa angali hawajui vitu vingi vilivyopo kwenye hiyo simu,kuitumia hiyo simu sio shida lakini unakuta mtoto ndio anajua vitu vingi kwenye Simu ya Mzazi mpaka Video za Ngono na mzazi yupo anaangalia baada ya siku utasikia amebaka ama amepata ujauzito kabla ya wakati."

Aidha waliomba viongozi kwenye nyumba zao za ibada kukemea kwa nguvu zote na kutoruhusu ndoa za utotoni huku wakiwafundisha waumini wao bila kuogopa mambo yasiyofaa kwenye jamii bila kuyaficha ficha ili kuokoa na kujenga jamii itakayo kuwa na maadili mema.

 Monica Irumba ambaye ni Mkunga wa Jadi alisema kukosekana kwa elimu kwa wazazi ni chanzo mojawapo ya kuendelea kuwepo ukatili wa kijinsia kwani wazazi wengi wanaishi kwa mazoea ndio maana wengine ukiwauliza kwanini anamkeketa mtoto atakwambia nimekuta bibi yangu anafanya hivi.

"Niwaombe wazazi wenzangu tuishi kwa upendo, upendo ukikosekana ndio inapelekea kuwepo Vitendo vya ukatili,tuache mazoea,tuachane na mila zisizofaa." alieleza Monica kwa uchungu.

ESTL imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya kuiwezesha jamii kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao kupitia mradi wao wa kutokomeza ukatili na ukeketaji mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Finland hapa nchini ukitekelezwa na Shirika hilo chini ya Mratibu Annamaria Mashaka.

Mume wa Malkia Elizabeth II, Prince Philip Afariki Dunia akiwa na umri wa miaka 99

$
0
0

 

 Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.

Tangazo kutoka Kasri ya Buckingham linaeleza: "Ni kwa masikitiko makubwa, Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpenzi, Mwanamfalme Philip, Duke (Mtawala) wa Edinburgh."

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anasema ni "kwa huzuni kubwa" kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham.

Mwanamfalme Philip alimuoa Bintimfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na amekuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MALKIA ELIZABETH II,KUFUATIA KIFO CHA PRINCE PHILIP

UINGEREZA YAMLILIA MWANAMFALME PHILIP

$
0
0





 

Mwanamfalme Philip akiwa na mkewe Malkia Elizabeth II wakati wa uhai uhai wake.


MWANAMFALME Philip ambaye pia ni mume wa Malkia Elizabeth II amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kasri ya Buckingham kwa niaba ya Malkia imeelezwa  kuwa, "Kwa masikitiko Malkia anatangaza  kifo cha mumewe kipenzi,  Mwanamfalme Philip mtawala wa Edinburgh aliyefariki dunia kwa amani leo asubuhi Katika kasri ya Windsor Castle."

Mwanamfalme Philip alimuoa binti mfalme Elizabeth mwaka 1947 kabla ya kuwa Malkia miaka mitano baadaye na kuwa Malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza.

Mwanamfalme Philip alipata heshima kutoka kwa watu wengi kutokana na kujitolea na kumuunga mkono mkewe Malkia Elizabeth II katika kazi zake, na malkia alipenda  kumwelezea mumewe kwa maneno mawili ya  'Strength and Stay.'

Viongozi mbalimbali wametuma salamu za rambirambi kwa familia huku Waziri mkuu wa Taifa hilo Boris Johson akimwelezea Mwanamfalme Philip kuwa ni jasiri aliyeongoza familia ya kifalme na ufalme kwa upendo wa hali ya juu.

ZIMA MOTO KUBORESHA HUDUMA ZA UOKOAJI

$
0
0

Na Farida Saidy, MOROGORO.

KATIKA kuboresha na kuimarisha huduma za uokoaji kwa lengo la kuondoa malalamiko ya Wananchi wakati wa majanga mbalimbali Nchini, Jeshi la zimamoto na Uokoaji limeanza kutekeleza makubaliano kati ya Jeshi hilo na chama cha Skauti juu ya kushirikiana katika majukumu kwa kuanza kutoa mafunzo ya awali ya zima moto na uokoaji kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji John Masunga kwenye kikao kazi cha Baraza dogo la Wafanyakazi wa Jeshi hilo kwa ajili ya kupokea taarifa ya Bajeti ya Mwaka 2020 na mwelekeo wa fedha wa 2021.

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji amesema,Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linamaliza malalamiko ya Wananchi wakati kunapotokea majanga mbalimbali katika maeneo kwa kuboresha huduma za uokoaji.

“Nataka niwambie sisi kama Jeshi la zima moto tunatalajia ifikapo mwaka 2023 tutakuwa tumefika wilaya zote za Tanzania Bara ili kuhimarisha huduma za uokoaji kwa Wananchi”.Alisema Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji John Masunga.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Skauti Wilaya ya Morogoro Bwana Frank Kaundula ameeleza namna watakavyo shirikiana na Jeshi la zimamoto na uokoaji inapo tokea majanga mabalimbali katika mane ohayo.

“Kama wilaya tumeshaanza kutengeneza makundi maalumu ya vijana wa Skauti kutoka katika shule za Sekondari na Msingi watakaopatiwa mafunzo maalumu ya uokoaji kutoka kwa Askali ya zimamoto na uokoaji.”Alisema Naibu Kamishna wa Skauti Wilaya ya Morogoro Bwana Frank Kaundula
Hata hivyo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bwana Emmanuel Kayui amewataka Askari wa Jeshi la zimamoto na uokoaji kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia sharia.

WIZARA MPYA TUCHAPE KAZI KWA KASI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0

 Na Prisca Ulomi, WMTH
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka watumishi wa Wizara yake pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan
 
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati akifungua mkutano namba 2/2020/2021 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Dodoma
 
Amewaeleza wafanyakazi wa Wizara hiyo kuwa wameyasikia maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara yetu ikiwemo usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), mikakati ya kufikisha mawasiliano kwenye maeneo ya pembezoni mwa nchi yetu na kuangalia upya suala la mabando na kuweka uratibu mzuri wa utekelezaji wake pamoja na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ambapo tayari Wizara ilianza kuyatekeleza na kufanyia kazi hivyo ana imani kuwa wataalamu wa Wizara wana majibu yote na ndio umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano
 
Vile vile, amesisitiza kwa wafanyakazi hao kuwa Wizara hii sio ya kwake wala ya menejimenti ya Wizara hiyo bali ni Wizara ya wafanyakazi wote, hivyo wafanyakazi wote wana wajibu wa kutumikia watanzania kuendana na majukumu ya kila mfanyakazi kwa kuongeza kasi zaidi ya kutekeleza majukumu ya Wizara ikizingatiwa kuwa Wizara imeongezewa bajeti kutoka shilingi bilioni kumi na sita kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 na kufikia shilingi bilioni 216 kwa mwaka wa fedha wa 2021/22.
 
Pia, amewataka wafanyakazi kuhakikishia wanaongeza kasi ya kuitambulisha Wizara mpya kwa wananchi ili waelewe majukumu ya Wizara kwa kuzingatia kuwa Wizara hii ndiyo yenye dhamana ya masuala ya TEHAMA nchi nzima na inasimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya TEHAMA na Wizara hii ni mtambuka, ni kiungo mchezeshaji kwa kuwa inagusa nyanja ya kijamii, kiuchumi, ulinzi na usalama
 
Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Andrea Mathew amewaeleza wafanyakazi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita ni sawa na makocha wa mpira, hivyo kila mmoja awajibike kutekeleza majukumu yake na kuonesha anatosha katika nafasi yake na kuendeleza ushirikiano baina ya wafanyakazi na viongozi ili Wizara iweze kutekeleza majukumu yake kuendana na matakwa ya Serikali ya sasa
 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa lengo la Mkutano huo ni kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 na kuwasilisha mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/22; mada mbali mbali zinazohusu afya na ustawi wa wafanyakazi mahali pa kazi na kuhimiza viongozi kuzingatia maslahi ya wafanyakazi na kuleta umoja, mshikamano na upendo kazini.
 
Mwenyekiti wa TUGHE wa tawi la Mawasiliano, Laurencia Masigo, akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara hiyo, amewashukuru viongozi wa Wizara kwa kuchochea amani mahali pa kazi na kuwaomba viongozi kufuatilia mwongozo wa gharama za usafiri wa mabasi kutoka kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Usafiri Nchi Kavu (LATRA) ili watumishi waweze kulipwa nauli stahiki wakati wa likizo zao na kufuatilia malipo ya malimbikizo ya mishahara kwa watumishi kwa mamlaka husika ili watumishi 19 waliobaki kati ya watumishi 30 waweze kulipwa.
 


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile(wa pili kulia) akifungua baraza la wafanyakazi la Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma. Kulia ni Naibu wake Mhandisi Kundo Mathew, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi. 

Viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiimba wimbo wa mshikamano daima wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonazi, akifuatiwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Zainab Chaula, akifuatiwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile na Mwisho ni Naibu wake, Mhandisi Kundo Mathew
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara ya Mawasiliano Teknolojia ya Habari Laurencia Masigo
akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma. Kulia ni ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula (kulia) akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma.katikati ni Naibu wake Dkt. Jim Yonazi na Kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara ya Mawasiliano Laurencia Masigo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wake Dkt. Faustine Ndugulile akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kushoto ni Naibu wake Dkt. Jim Yonazi
Viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakipokea zawadi za pongezi kutoka kwa menejimenti ya Wizara hiyo kwa kuaminiwa na Mhe. Rais kuendelea kuongoza Wizara hiyo



Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akisalimiana na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Laurensia Masigo (kushoto) katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa  Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma wa Pili kulia ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile akifuatiwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Zainab Chaula akifuatiwa na Naibu wake Dkt. Jim Yonazi

Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo (hayupo pichani) wakati akifungua baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma.

MAMLAKA YA MASOKO YA MITAJI NA DHAMANA (CMSA) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI SHINDANO LA MASOKO YA MITAJI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU

$
0
0

 

 SHINDANO maalumu la 'The Capital Markets, Universities and Higher Learning Institutions Challenge' kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu za Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar lililoendeshwa kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana limefika tamati na jumla ya washindi  80 sawa na asilimia 0.4 ya washiriki 21338 wamepatikana na kupatiwa zawadi zao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama alisema kuwa Mamlaka hiyo iliendesha shindano kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu kwa malengo ya kujenga uelewa na weledi wa masoko ya mitaji na uwekezaji nchini.

"Shindano hili lilifunguliwa Agosti 4,2020 na kufungwa Novemba 30, 2020 na liligawanyika katika makundi mawili ambalo kundi la kwanza lilikuwa ni la kujibu maswali 100 yaliyolenga kujenge uwezo kwa washiriki kuhusiana na masuala ya masoko ya mitaji na uwekezaji, na kundi la pili lilikuwa ni la kuandika Insha ya kueleza fursa na faida zinazopatikana katika uwekezaji wa masoko ya mitaji kwa mifano." Amesema.

Mkama amesema, katika mashindano hayo washindi ni wale waliopata alama za juu kuzidi washiriki wengine na hafla hiyo ni muendelezo ya kujenga uelewa zaidi kuhusiana na masuala ya masoko ya mitaji na uwekezaji, sekta ambayo inazidi kuendelea zaidi kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

"Ushiriki wa wanafunzi umezidi kuongezeka zaidi kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo tunatumia simu za mkononi, Internet na barua pepe katika kuwafikia washiriki na tunaona wanafunzi hapa wametoka katika vyuo mbalimbali ikiwemo Mzumbe- Morogoro, Dar es Salaam, UDOM,St.Joseph, St.Augustine na Zanzibar." Amesema.

Amesema shindano hilo ni la kwanza kufanyika barani Afrika kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano na limekuwa kivutio kwa wasimamizi wengi wa masoko ya mitaji barani humo na wengi wametoa hitaji la kutaka kujifunza na kuliendesha katika nchi zao.

Katika shindano hilo mshindi wa kwanza kwa kila shindano amezawadiwa fedha za kitanzania shilingi milioni moja na laki nane, mshindi wa pili milioni moja na laki nne, mshindi wa tatu shilingi laki nane, washindi wa tano hadi 20 shilingi laki mbili na washindi walioingia katika fainali wamepatiwa vyeti vya utambuzi pamoja na T-Shirt.

 ''Washindi watatu waliopata alama za juu katika makundi yote watagharamiwa ziara ya kwenda kujifunza na kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo inagharamiwa na Mamlaka ya Masoko ya mitaji na Dhamana, Mamlaka hii uwekezaji wa Trilioni 29 fedha za kitanzania ambapo trilioni 15 ni uwekezaji katika hisa, Trilioni 11 ni hati fungani (serikali na kampuni,) na Bilioni 500 ni uwekezaji wa mifuko ya pamoja hii inathibitisha umuhimu wa Mamlaka hii katika sekta ya fedha na uchumi.'' Amesema.

Shindano hilo lililoanza na washiriki 2000 limefikia kiwango cha kuwafikia washiriki 20,000 zaidi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar huku matunda ya mashindano hayo yakionekana kwa baadhi ya washiriki kuwekeza katika masoko ya mitaji na mifuko ya pamoja.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama akizungumza wakati akihitimisha  Shindano maalumu la 'The Capital Markets, Universities and Higher Learning Institutions Challenge' kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu za Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar lililoendeshwa kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ,ambapo jumla ya washindi  80 sawa na asilimia 0.4 ya washiriki 21338 wamepatikana na kupatiwa zawadi zao.
Washindi wa  Shindano maalumu la 'The Capital Markets, Universities and Higher Learning Institutions Challenge' wakiwa katika picha ya pamoja na Waandaji wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama (pichani kati),Mashindano hayo yalikuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu za Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar lililoendeshwa kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano.

Baadhi ya Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Shindano maalumu la 'The Capital Markets, Universities and Higher Learning Institutions Challenge' kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu za Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar lililoendeshwa kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana likifikia tamati,ambapo jumla ya washindi  80 sawa na asilimia 0.4 ya washiriki 21338 wamepatikana na kupatiwa zawadi zao.
Majaji waktafuta washindi wa shindano hilo
Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa kutafuta Washindi

MFUKO WA PAMOJA WA SACCOS WAZINDULIWA

$
0
0
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amekitaka Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) kuwa wabunifu katika kubuni bidhaa zenye manufaaa kwa Vyama Wanachama ili kuonesha na kutoa fursa ya wanachama wa SACCOS kupata mikopo nafuu itakayosaidia kuondoa umasikini na kukuza Uchumi wa Taifa.

Mrajis ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Mfuko wa Pamoja wa SACCOS kukopeshana Central Financing Facility (CFF) uliofanyika Aprili 09, 2021 Mkoani Dar es salaam.

Akizindua Mfuko huo Mrajis ameitaka SCCULT kubuni bidhaa mbalimbali za mikopo itakayoendana na mahitaji ya wanachama wa SACCOS pamoja na kutumia mifumo ya TEHAMA katika uendeshaji na utunzaji mzuri wa taarifa za Wanachama.

“Ni lazima bidhaa zitazofaa wanaushirika ili waone faida na thamani ya kukopa ndani ya Mfuko unaoundwa na SACCOS zetu kwa lengo la kuhakikisha Chombo chetu cha SCCULT kinaimarika na kuwezesha SACCOS kusaidia Wanachama wengi zaidi,” alisema Dkt. Ndiege

Aidha, Mrajis Alisisitiza kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali ina wajibu wa kulinda maslahi ya wanaushirika. Hivyo, haitosita kuchukua hatua endapo yeyote atakiuka Sheria, Kanuni na taratibu za Ushirika zilizowekwa kwakuwa Ushirika ni Sekta mtambuka inayogusa Uchumi na maisha ya watu.

Akielezea malengo ya Mfuko huo Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) Ltd Dkt. Gervas Machimu alibainisha kuwa Mfuko wa CFF ni muungano wa nguvu za kifedha za SACCOS wanachama ambao unatoa fursa kwa SACCOS hizo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa fedha pindi SACCOS inapokuwa na changamoto za Kifedha kwaajili ya kutoa huduma kwa wanachama wake hususani mikopo.

Katika uzinduzi huo Dkt. Machimu ameeleza SCCULT tayari imepata kiasi cha Fedha cha Shillingi Millioni 270 kutoka kwa Wadau wa Ushirika ambayo itatumika kukopesha (SACCOS) ili kuhakikisha vyama hivyo vinakuwa na ukwasi wa kutosha kuweza kukopesha wanachama wake. Akiongeza kwa kutoa rai kwa SACCOS na Wadau wengine kujitokeza kuendelea kuchangia Mfuko huo kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa SACCOS.

Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa SACCOS zitakazokopeshwa fedha hizo ni zile ambazo ni wanachama wa SCCULT na ambazo zitakazo kuwa ni sehemu ya Mfuko huo kwa kuweka Akiba na kujisajili na Mfuko wa CFF. Akiongeza kuwa ili kuhakikisha Mfuko huo unakuwa na usimamizi imara tayari kuna masharti yaliyoainishwa kwa mujibu wa Sera za Mfuko zilizoandaliwa.

“Vyama vitakavyokopa katika Mfuko huo ni vile ambavyo vimepata Leseni ya Usimamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Vyama vilivyokakuguliwa, vilivyo na Ukomo wa Madeni yanayopitishwa na Mrajis wa Ushirika,” alisema Dkt. Machimu

Dkt. Machimu alifafanua zaidi kuwa Mikopo itakayoanza kutolewa ni ile ya itakayofuata taratibu za kupungua salio la usawa (reducing balance) kwa kiasi cha 10%, akieleza kuwa SACCOS zitakazopata mkopo zitatoa mikopo hiyo kwa riba isiyozidi 17%.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akizindua Mfuko wa Pamoja wa SACCOS kukopeshana kwa kukata utepe wa vijitabu vya Sera mbalimbali za Mfuko huo, Jijini Dar es salaam.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiongea na Wanaushirika wakati wa Uzinduzi wa Mfuko wa Pamoja wa SACCOS kukopesha (Central Financing Facility) Mkoani Dar es salaam

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) Ltd Dkt. Gervas Machimu akieleza namna Mfuko wa Pamoja wa SACCOS utakavyosaidia kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo.

MGANGA MKUU WA SERIKALI ATAKIWA KUSIMAMIA MIFUMO YA UWAJIBIKAJI SEKTA YA AFYA NCHINI KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO

$
0
0

 Na WAMJW- Dom

Mganga Mkuu wa Serikali ametakiwa kusimamia mifumo ya uwajibikaji katika sekta ya afya nchini ili kupunguza vifo vya wajawazito pamoja na kupanua huduma za kibingwa ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuvutia nchi za jirani kupata huduma za afya hapa nchini

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Afya), Prof. Abel Makubi, leo tarehe 9 Aprili,2021 wakati  akimkabidhi ofisi Mganga Mkuu wa Serikali  Dkt. Aifelo  Sichalwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali  iliyopo katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Prof. Makubi ambaye alihudhumu nafasi ya Mganga Mkuu wa Serikali  hapo awali amempongezà Dkt. Sichalwe kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Aidha, Prof. Makubi amemtaka CMO huyo kusimamia  kusimamia suala la dawa, vifaa na vifaa tiba, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza,  huduma za tiba asili,  ujenzi wa miundombinu pamoja na kusimamia mwenendo wa kuanza kwa Bima ya Afya kwa wote.





 



RAIA WA POLAND NA MKE WAKE 'WATUPWA' JELA MIAKA 30 KWA KULIMA BANGI

Viewing all 119887 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>