Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120377 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI SILINDE ATAKA MAAFISA ELIMU KATA KUSIMAMIA KWA WELEDI MIRADI YOTE YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KWA UKAMILIFU

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewaagiza maafisa elimu kata kuhakikisha wanasimamia fedha na miradi yote ya  elimu katika  shule za msingi na sekondari ili ikamilike kwa wakati na kuleta manufaa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde wakati akifungua kikao cha maafisa elimu kata nchini(UMEKTA).

“Kuhusu usimamizi wa fedha na miradi ya elimu, kila Afisa Elimu kata asimamie miradi na fedha zote za serikali ndani ya kata yake kwa shule zote za msingi na sekondari.

Baadhi yenu mnazembea kwenye usimamizi na kuisababishia Serikali hasara na kutokuonekana kwa thamani ya fedha kwenye baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Kata zetu,” Amesema Silinde.

Silinde amesema  imebainika kuwa baadhi ya walimu wamekuwa na mikopo mingi kupita kiasi hali inayopelekea kukosa utulivu kazini na kusababisha utendaji kazi usioridhishi hivyo kila Afisa Elimu kata ametakiwa kuhakikisha, walimu wanaelimishwa juu ya madhara ya mikopo hiyo.

Amesisitiza maafisa elimu kata wanatakiwa kusimamia  kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi katika Shule za Msingi na Sekondari kwa kuwa imebainika kuwa baadhi ya Maafisa Elimu kata hawasimamii shule za Sekondari.

“Kila Afisa Elimu Kata afanye tathmini ya maendeleo ya taaluma kwenye kata yake ili kubaini changamoto zinazokwamisha utoaji wa elimu bora ndani ya kata husika na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikisha jamii na viongozi wa kata husika,” Amesema Naibu Waziri Silinde.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Mweli amesema  Serikali imewawezesha maafisa elimu kata kwa  kuwapa nyenzo ya usafiri pamoja na posho ya kuwasaidia kutekeleza majukumu yao.

Amesema hata hivyo, baadhi wamekuwa hawatimizi majukumu yeo ipasavyo ikiwemo kutokufika kwenye shule kwa muda mrefu.

“Tutakuwa na usimamizi wa karibu kuona kuwa, mnatekeleza majukumu yenu, na pale ambapo itabainika kuwa na udhaifu au uzembe, hatua kali za kisheria na kiutumishi zitachukuliwa dhidi ya wahusika,” Amesema Mweli.

Mweli ameongeza kuwa ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwenye Shule za Msingi na Sekondari, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali, Washirika wa Maendeleo na jamii imejenga vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na hivyo kuongezeka kutoka 115,665 mwaka 2015 hadi kufikia 136,292 mwaka 2020.

“Wakati huo huo, idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi 17,804 mwaka 2020 na shule za Sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi 5,330 mwaka 2020,” Amesema Mweli.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde 


PROF NDALICHAKO AWAONYA WANAOFANYA UDANGANYIFU KWENYE UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI MITIHANI DARASA LA SABA

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako amezionya Halmashauri zote nchini ambazo zimekua na tabia ya kufanya udanganyifu kwenye uandikishwaji wa wanafunzi ambao wanamaliza Darasa la Saba.

Prof Ndalichako ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokua akizindua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo ambapo amewataka watumishi wote wa Wizara kuzingatia weledi na kuacha kutumia lugha za ubabe wanapowahudumia wateja wao.

Akizungumzia suala la udanganyifu wa wanafunzi wanaoandikishwa kwa ajili ya mitihai ya kumaliza Darasa la Saba, Prof Ndalichako amesema amepata taarifa ya halmashauri ambazo zimeondoa majina ya wanafunzi wanaotakiwa kufanya mitihani hiyo kwa kuepuka kwamba watafeli na kuziletea sifa mbaya halmashauri hizo.

Ametoa onyo kwa maafisa elimu wa halmashauri hizo na walimu wakuu kwenye shule ambazo zimeondoa majina ya wanafunzi hao kuacha mara moja na wale watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

" Nimepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuhusu hii tabia kwenye Halmashauri nchini ambapo kwa makusudi kabisa maafisa elimu na walimu wakuu wanaondoa majina ya wanafunzi wenye uwezo mdogo kwa kuepuka kwamba watafeli na halmashauri zao kuonekana zinafanya vibaya, wanachokifanya wanawarudisha hao wanafunzi darasa la sita.

Nitoe onyo kwa maafisa elimu wote kuacha mara moja tabia hiyo na wale wote waliofanya udanganyifu huo majina yao ntayapeleka Tamisemi ili wachukuliwe hatua maana Tamisemi ndio wanahusika nao," Amesema Prof Ndalichako.

Amesema serikali imeamua kuwekeza kwenye elimu kwa kutoa elimu bila malipo hivyo kitendo cha kuwaondoa wanafunzi hao ni kuchongesha serikali na wananchi kwani hao wanafunzi wanaorudishwa nyuma bila mpango wa serikali wanakua hawapo kwenye hesabu ya elimu bila malipo.

" Unajua serikali tunatenga fedha nyingi kwenye Sera hii ya elimu bila malipo, hawa maafisa elimu na walimu wakuu wanavyowarudisha nyuma hawa wanafunzi wakati serikali ishatenga bajeti yao inaajua wanamaliza matokeo yake mwaka unaofuata idadi ya wanafunzi inaongezeka nje ya kiasi kilichopangwa," Amesema Prof Ndalichako.

Waziri Ndalichako amewatoa hofu pia watumishi wote wenye sifa za kupandishwa madaraja kuwa watapandishwa kwani tayari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo ameshapeleka taarifa zao Ofisi ya Rais Utumishi.

" Niwaombe mfanye kazi kwa bidii ili kuipa sifa zaidi wizara yetu, Rais Mama Samia ameendelea kutuamini ndio maana mnaona timu yote Mimi, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wote tumerudishwa hajatubadilisha, hiyo maana yake anatuamini sana, twendeni tukafanye kazi kwa weledi kwa kufuata taratibu na sheria zetu na watakaofanya vizuri basi tunawapandisha madaraja maana inakua ni haki yao, mtu akifanya vizuri lazima apewe haki yake.

Nisisitize tena nidhamu makazini hasa kuwa waungwana na wastaarabu kwa wananchi wetu, haiwezekani mtu amefunga safari amefuata huduma toka asubuhi hadi jioni yupo tu na bado unamwambia arudi kesho, huu siyo uungwana ni kuwagombanisha wananchi na serikali yao, tabia hii sitaki kuiona nachotaka ni utii, ufanisi na utendaji kazi uliotukuka," Amesema Prof Ndalichako.

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako

MRADI WA BILION 5. 6 WA MAJI MKURANGA WAKAMILIKA, KUONDOA KERO YA MAJI YA MUDA MREFU

$
0
0


 Zainab Nyamka, Michuzi Tv

WANANCHI wa Wilaya ya Mkuranga waanza kunufaika na mradi wa Mkubwa wa Maji uliotumia takribani Bilion 5.6 hadi kukamilika.

Mradi wa Maji Mkuranga umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuondoa adha ya maji ya muda mrefu kwa  wakazi wa eneo hilo.

Mamlaka imewezea kutumia fedha za ndani kukamilisha mradi huo ambapo zoezi lililobaki ni kuanza maunganisho mapya kwa wateja walioomba kupatiwa huduma ya maji safi.

Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo, Mhandisi wa DAWASA Mkuranga Richard Katwiga amesema tayari maji yameshaingia kuanzia Aprili 02, mwaka huu katika tanki lenye ujazo wa lita 1.5 na leo mafundi watafungulia ili kuweza kuyaruhusu maji kusafisha mtandao wa mabomba waliyoyalaza kabla ya kuanza kupeleka huduma kwa wateja.

Amesema, wamelaza mtandao wa mabomba takribani km 65 katika kata ya Mkuranga na Kiparang'anda ambazo zitaanza kufaidika na mradi huo kwenys awamu ya kwanza kabla ya kwenda maeneo mengine ya karibu.

"Maji tayari yameshaingia katika tanki letu hatua iliyobaki ni kuyaruhusu kutoka ili yakasafishe mtandao wa mabomba ambao tumeulaza kwa km 65 kwenye kata za Mkuranga na Kiparang'anda," amesema.

Katwiga amesema, wapo wananchi walioathirika wakati wa ujenzi wa mradi wa Mkuranga lakini kufikia Oktoba 2019 walianza kupata huduma ya maji kupitia mtandao mpya wa mabomba waliyoyalaza kwa kutumia tanki la zamani lililojenga mwaka 2002

Aidha, amesema kuanzia Aprili 9 mwaka huu wanatarajia kufanya maunganisho ya tanki kubwa la maji kwenye mtandoa mpya ili wananchi waendelee kupata huduma kama kawaida na kuanza kufanya maunganisho mapya kwa wateja waliofanya maombi.

"Kuna jumla ya wateja 50 wameshaomba kuunganishiwa huduma ya maji, tutaanza kuwatembelea ili kuwaunganishia huduma ya maji na zaidi lengo la Dawasa ni kuwafikia wananchi wengi zaidi ndani ya mji wa Mkuranga," amesema Katwiga

"Lengo letu ni kukusanya milion 60 kwa mwezi na hilo litawezekana kama tutafanya maunganisho kwa wateja wengi na ili kutoa huduma zaidi Dawasa tutaanza kutembelea maeneo wateja walipo ili kuweza kuwasogezea huduma zaidi kwa ukaribi,"

Hata hivyo, Katwiga ameeleza kuwa chanzo cha maji kina uwezo mkubwa wa ambapo kwa saa Lita za ujazo 284,500 zinazalishwa sawa na Lita milion 6.8 kwa siku.

Mradi huo uliweza kuhusisha ujenzi wa Tanki la maji Lita 1.5 kituo cha kusukumia maji kutoka kwenye chanzo na ulazaji wa mabomba kwa urefu wa Km 65 na wanufaika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo ni wananchi katika Vijiji vya Mkwalia Kitumbo, Kididimo, Sunguvuni na Kiguza wa kata ya Mkuranga huku Kata ya Kiparang'anda ni Kiparang'anda A, Kiparang'anda B na Magoza.

Mhandisi wa Miradi Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mkuranga Richard Katwiga akitoa maelezo kwa moja ya mafundi wakati wa kuyaruhusu maji yaanze kwenda katika mtandao ili kuyasafisha na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa Mkuranga kupitia mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Bilion 5.6 uliohusisha na ujenzi wa tanki la lita Milion 1.5
Mhandisi wa Miradi Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mkuranga Richard Katwiga akionesha na kutoa maelezo ya  chanzo cha maji kinachotumika katika mradi wa maji wa Mkuranga. Chanzo hicho kina uwezo wa kuzalisha lita za maji milion 6.8  kwa siku sawa na lita 284,500 kwa saa

Kituo cha kusukumia maji kikiwa katika hatua za mwisho za ukarabati. Pampu moja ikiwa tayari imeshafungwa.

 Tanki la Ujazo wa Lita Milion 1.5 likiwa limekamilika na kuanza kupokea maji kutoka chanzo kilichopo Kijiji cha Mkwalia Kitumbo

MAPOKEZI YA NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO LEO.

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa pamoja na Wakuu wa Wizara wamemkaribisha rasmi Naibu waziri Mheshimiwa Pauline Gekul kuanza kazi rasmi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumhamisha kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Mheshimiwa Pauline Gekul alisaini kitabu cha wageni katika ofisi yake pia kutembelea ofisi ya Waziri na baadae alikutana na viongozi wa wizara na kufanya nao mazungumzo ya ndani.











 

CAG ABAINI UPOTEVU WA MAPATO KWA MAMLAKA YA BANDARI YA DOLA ZA MAREKANI 979, 126 ZILIZOSABABISHWA NA KUTOA MSAMAHA WA KODI USIOSTAHILI

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amefanya ukaguzi maalum katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kubaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa ikiwemo upotevu wa mapato kwa kutoa msamaha usiostahili wa Dola za Marekani 979,126.5 kwa Kampuni ya Saruji ya Mbeya.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya CAG aliyoisoma leo kwa wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo ambaini pia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu wa malipo ya Sh Bilioni 3.76.

Akizungumzia ukaguzi huo wa TPA, CAG Charles Kichere amesema April 30, 2018 menejimenti ya TPA ilipeleka kwenye Bodi ya Usimamizi maombi ya msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 kuiombe kampuni ya saruji Mbeya kwa ajili ya wateja wake waliopo Burundi na DR Congo wanaosafirisha saruji kupitia Bandari ya Kasanga.

Amesema Kampuni hiyo ilieleza kuwa wateja wao walipata changamoto ya kukosa meli za kuja Bandari ya Kasanga kuchukua shehena za saruji zao walizokua wameagiza na hivyo kupelekea shehena hiyo kuharibika.

Amesema April 17, 2019 kupitia azimio la Bodi ilitoa msamaha wa asilimia 100 kama ilivyoombwa hivyo kampuni hiyo ya Saruji Mbeya ilipaswa kulipa Dola za Marekani 50,000 kama gharama za utunzaji wa shehena hizo na Dola za Marekani 7,726 kwa ada tu ya kuondolea shehena.

CAG Kichere amesema ukaguzi wake uliangalia ukweli wa msamaha uliotolewa na uligundua shehena ya tani 1,445 (mifuko 28,904) ambayo iliharibika katika Bandari ya Kasanga ilikua na malimbikizo ya gharama ya Dola za Marekani 543,224 iliyostahili kutolewa msamaha.

" Maombi ya msamaha yaliyopelekwa katika Bodi April 14, 2019 yalikua ya Dola za Marekani Milioni 1.52 yakijumuisha madeni ya saruji iliyoharibika ya Dola za  Marekani 543,244 na gharama za utunzaji Dola za Marekani 979,126 kwa shehena zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Kasanga katika kipindi cha Januari 2013 na Oktoba 2017 na hakukua na hasara iliyopatikana na hivyo  kutostahili msamaha.

Kuchukulia shehena nzima ya tani 1445.2 kama imeharibika na kutoa msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 badala ya gharama sahihi ya Dola 543,244 kuliisababishia hasara TPA ya upotevu wa mapato wa Dola za Marekani 979, 126.59.


 

MAJALIWA AZUNGUMZA NA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU, BAADHI YA MAKAMISHINA NA WAKUU WA TAASISI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.

Manaibu Mawaziri, David Silinde, Ofisi ya Rais– TAMISEMI (kushoto) na Hussein Bashe wa Wizara ya Kilimo, wakinukuu maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu (kushoto) akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinoloji, Profesa Joyce Ndalichako katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makakatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu, Makamishina na Wakuu Taasisi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima akimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu akimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 8, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

KISWAHILI RASMI UMOJA WA NCHI WAZALISHAJI WA ALMASI AFRIKA, TANZANIA YAKABIDHIWA UENYEKITI

$
0
0

 

    Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza na Wanahabari  wakati  akifunga Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Nchi za Afrika Zinazozalisha Madini ya Almasi (ADPA) uliofanyika  kwa Njia ya Video tarehe 8 Aprili, 2021 Jijini Dodoma

   Waziri wa Madini Doto Biteko na baadhi ya Wataalam wa Madini waliohudhuria Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Nchi za Afrika Zinazozalisha Madini ya Almasi (ADPA) kwa Njia ya Video uliofanyika  tarehe 8 Aprili, 2021 Jijini Dodoma

    Picha ya pamoja ya Waziri wa Madini Doto Biteko (Katikati), Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (Kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia) wakati wakifuatilia Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Nchi za Afrika Zinazozalisha Madini ya Almasi (ADPA) uliofanyika  kwa Njia ya Video tarehe 8 Aprili, 2021 Jijini Dodoma

Asteria Muhozya na Steven Nyamiti, Dodoma

Kiswahili kimekubalika kuwa moja ya Lugha ya Mawasiliano zitakazotumika katika Umoja wa nchi Zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika na hivyo kuongeza idadi ya lugha zilizokuwa zikitumika awali  katika umoja  huo za  Kiingereza, Kireno na Kifaransa.

 Hayo yamesemwa  Aprili 8, na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifunga Mkutano wa 7  wa Mawaziri wa nchi zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika  ( African Diamond Producers Association- ADPA) uliofanyika kwa njia ya Video Conference na kutanguliwa na Mkutano wa  Wataalam wa jumuiya hiyo ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Aidha, Tanzania imekabidhiwa  Uenyekiti wa Jumuiya hiyo nafasi ambayo itadumu nayo kwa kipindi cha miaka 2 ikipokea kutoka kwa nchi ya Jamhuri ya  Namibia ambayo ilikuwa Mwenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja. Pia, nchi ya Zimbabwe imekubalika kuwa Makamu Mwenyekiti na inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano  wa 8.

Akieleza kuhusu yaliyojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano huo, Waziri Biteko amesema kuwa mkutano huo umekubaliana kuwa Kamati Tendaji ya umoja huo kupitia upya mifumo ya kiutendaji  ya umoja huo ndani ya kipindi cha miezi sita  na kutoa mrejesho.

Aidha, Waziri Biteko ametumia fursa ya Uenyekiti wa jumuiya hiyo  kuzisisitiza nchi wanachama kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa maeneo mbalimbali nchini, akilenga kuzifanya nchi wanachama kuyatumia masoko hayo kufanya biashara ya madini  ili manufaa ya madini hayo yaendelee kubaki Afrika na kwa wanachi wenyewe.

Awali, Waziri Biteko amewaeleza mawaziri walioshiriki mkutano huo kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Madini kufuatia Marekebisho yaliyofanywa kwenye Sheria ya Madini ambayo pamoja na mambo mengine, yalipelekea kuanzishwa kwa masoko ya madini katika mikoa mbalimbali nchini ambapo hadi sasa, Tanzania ina jumla ya Masoko ya Madini 39 na Vituo vya Ununuzi wa Madini 41.

Naye, Waziri wa Madini na Nishati wa Jamhuri ya Namibia, Tom Alweendo wa nchi ambayo imemaliza uenyekiti wake, ameutaka umoja huo kupata viongozi shupavu wa kamati tendaji watakaosaidia kuweka msukumo katika utekelezaji wa malengo ya jumuiya hiyo.

 Ameongeza kuwa, kama wanachama ni lazima  wachochee na kuweka mikakati ya kupigania maslahi ya Afrika kwa madini ya Almasi ikiwemo kuzitaka  nchi hizo  kuhakikisha zinalipa  michango yao kwa mujibu wa sheria.

Pia, Ametumia fursa hiyo kuelezea yale ambayo yalifanywa na nchi hiyo wakati ikishikilia kiti cha Uenyekiti na kueleza kuwa, pamoja na kipindi chake kukabiliwa na changamoto za janga la ugonjwa wa Corona, ilifanikiwa kuunda kamati ya uendeshaji ya jumuiya hiyo.

Mkutano wa 7 wa Mawaziri wa Nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika, umehudhuriwa na nchi zote 19 wanachama wa umoja huo zikiwemo  Nchi za Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Namibia, Tanzania, Zimbabwe, Cameroon, Afrika ya Kati, Ghana, Togo, Guinea na Sierra Leone. Nchi waangalizi zilizoshiriki ni Algeria, Jamhuri ya Congo, Cote D’ivore, Gabon, Liberia, Mali na Mauritania pia zimeshiriki.

TAKUKURU MANYARA YAMDAKA KARANI WA MAHAKAMA KWA RUSHWA YA SHILINGI ELFU 30

$
0
0

 Na Mwandishi wetu, Babati


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, inamshikilia karani wa Mahakama ya mwanzo Magugu Wilayani Babati, Alfred Jackson Ntatirwa kwa kudaiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu 30 ili ampatie mwananchi nakala ya hukumu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Babati, Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amesema tukio hilo limetokea Aprili 6 mwaka huu mji mdogo wa Magugu.

Makungu ameeleza kuwa Ntatirwa anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume na kufungua cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Amesema karani huyo Ntatirwa anatuhumiwa kuomba rushwa ya shilingi elfu 30 na kukamatwa na maofisa wa TAKUKURU akiwa amepokea kiasi hicho cha fedha ili atoe nakala ya hukumu ya kesi.

Amesema Ntatirwa aliomba fedha hiyo ili amsaidie mtu mmoja aliyeomba nakala ya hukumu ya kesi iliyokuwepo mahakama ya mwanzo Magugu ambaye hakuridhika na hukumu hiyo na alitaka kukata rufaa mahakama ya Wilaya.

Ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili akajibu mashtaka hayo yanayomkabili.

"Wananchi wote wanapaswa kufahamu kuwa hawalazimiki kulipia tozo yoyote inayohusiana na nakala za hukumu na maamuzi ya mahakama Kuu, mahakama ya Hakimu mkazi na mahakama ya mwanzo," amesema Makungu.

Amesema Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma alikwashatoa maelekezo kwa mahakama zote nchini kuwa hawatalazimika kulipa tozo yoyote kuhusiana  na nakala za hukumu na maamuzi mbalimbali kwa maana ya Judgement, Rulings, Order, Decrees and Drawn orders.

"Kwa hiyo mwananchi yeyote akidaiwa fedha katika orodha hiyo fahamu kuwa ni rushwa na unapaswa kutoa taarifa TAKUKURU kwa kutumia namba za dharura 111 ili hatua stahiki zichukuliwe," amesema Makungu.
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Babati.
 

WAGANGA WA TIBA ASILI MAGU WAKUMBUSHWA MAADILI,WAASWA WASIWAFILISI WATEJA WAO

$
0
0
 

Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na waganga wa tiba asili zaidi ya 300 kutoka katika vijiji 82 wilayani humo baada ya kujadili kero na changamoto zinazowakabili.

Ramadhan Mela Mayandagila, mmoja wa waganga wa tiba asili wilayani Magu alichangoa jambo kwenye mkutao wao uliofanyika mjini Magu ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Kalli.

Picha na Baltazar Mashaka

……………………………………………………………………………….

NA BALTAZAR MASHAKA, Magu 

MKUU wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, amewataka Waganga Tiba asili wilayani humo, wasiwafilisi na kuwasababishia umasikini wateja wao sababu ya tamaa ya fedha bali wawahudumie kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo. 

Pia amewataka waganga hao kuchangia shughuli za maendeleo wilaya hiyo na taifa ili kuunga mkono juhudi za serikali na kuwaasa wasomeshe watoto ili kupata watalaamu mbalimbali wakiwemo wa tiba mbadala.

Kalli,alitoa rai hiyo hivi karibuni alipokutana na wataalamu wa tiba asili kutoka kwenye vijiji 82 vya tarafa za Ndagalu,Sanjo,Kahangara na  Itumbili, mjini Magu.

Alisema waganga wa tiba asili wanaisaidia jamii kwa tiba hizo lakini baadhi wasio waaminifu wanawalaghai na kuwafilisi wateja wao na kuwasababishia umasikini kwa tamaa ya kujipatia fedha.

“Mnafanya kazi nzuri ya kuhudumia jamii yenye changamoto ya maradhi na sikuwahi kuamini mtu anavunjika mfupa wa mkono anaponea kwa mganga wa jadi lakini zingatieni maadili ya tiba mnayoitoa na  kuwafichia siri wateja wenu,”alisema Kalli.

Aliongeza kuwa wanapowatibu wakapona wasiwatoze gharama kubwa za kuwafanya wafirisike kiuchumi na kuwafanya kuwa masikini bali wakipona warudi kuzalisha mali na kukua kiuchumi.

“Mkitoa huduma nzuri ya tiba kwa kuzingatia maadili ya utaalamu mlionao mtaongeza wateja nao watawapenda hasa wenye gharama nafuu, hivyo msiwasababishe kuwa masikini,” alisema  Mkuu huyo wa wilaya.

Aliwapongeza wataalamu hao wa tiba asili kwa namna walivyozuia na kukomesha mauaji yaliyopamba moto Kanda ya Ziwa ya watu wenye ualibino na ya wazee yaliyosababishwa na imani za kishirikina na kuwafanya waishi kwa amani na kusistiza maadili ili wilaya ya Magu iwe ya mfano kwa tiba asili. 

Mratibu wa Tiba Asili Wilaya ya Magu, Casteur Kahema Mawe,alisema mtandao wa waganga wa tiba asili wilayani humo ulitengenezwa tangu 2007 ukilenga kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ualibinism. 

Pia alisema wameanzisha na kutoa tiba ya mifupa kwa dawa asili nje ya hospitali ya wilaya na wameanza kupata mafunzo ya tiba ya mifupa kwa dawa asili kwa kushirikiana na madaktari wataalamu kutoka Canada ambapo wanatarajia kupata wahadhiri 6 kutoka nchini humo wenye ujuzi zaidi.

Aidha waganga hao walitumia fursa hiyo kuiomba serikali chumba cha kutolea huduma za tiba asili ndani ya eneo la hospitali ya wilaya kwa sababu wanao uwezo wa kutibu kwa dawa asili na kusaidia jamii.

Mkuu wa Wilaya alisema kinachosubiriwa ni waraka baada ya sheria ili waganga wa tiba asili waruhusiwe kutoa huduma ya tiba hizo ndani ya hospitali tofauti na ilivyo sasa.

WANAKIJIJI NYASHIGWE MAGU WACHONGA MADAWATI 54 NA KUIKADHIBI SHULE

$
0
0
 
Wananchi wa Kijiji cha Nyashige, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, kabla ya kukabidhi madawati yaliyochongwa na wnanchi hao kwa ajili ya shule ya msingi ya kijiji hicho.



Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na wanacnhi wa Kijiji cha Nyashigwe, Kata ya Chabura wilayani humo jana.



Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli (kulia), akiwakabidhi moja ya madawati yaliyotengezwa na wananchi wa Kijiji cha Nyashigwe, wanafunzi wa shule ya kijiji hicho, Patrick Costantine (kushoto), Kado Safari (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wao, Ishengoma Kabuche (wa pili kulia).Picha zote na Baltazar Mashaka

…………………………………………………………………………….

NA BALTAZAR MASHAKA, Magu

WANANCHI wa Kijiji cha Nyashingwe,Kata ya Chabula wilayani Magu, wakabidhi madawati 54 yenye thamani ya sh. milioni 2.7 kwa shule ya msingi ya kijiji hicho ili kutatua changamoto ya watoto kukaa chini.

Pia wamejenga maboma mawili ya madarasa na ofisi ya walimu kwa nguvu zao katika jitihada za kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani mradi ambao umegharimu sh.milioni 6.3.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Devota Aloys alisema jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli, wakati akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi kijijini humo.

Alisema kaya sita kila kitongoji za vitongoji vinne zimetengeneza dawati moja ambapo kitongoji cha Nyashigwe kimetengeneza madawati 9 kati ya 11,Kibambu 19 (bado 2), Nyamilomate 20 wanadaiwa moja 1 na Zuli 6 kati ya 8 hivyo madawati 54 kati ya 62 yamepatikana kulingana na mgawanyo wa kila kitongoji.

Aloys alisema madawati hayo yamepunguza uhitaji katika Shule hiyo ya Msingi Nyashigwe yenye wanafunzi 750 kutoka 146 hadi 84,ambapo ina madasara 7 kati ya 17 ili kukidhi mahitaji hivyo madarasa yaliyojengwa na wananchi yakiezekwa yatasaidia.

Pia alisema shule hiyo ina uhaba wa matundu 29 ya vyoo yaliyopo ni 6 kati ya 35 na kuiomba serikali iwasaidie kujenga vya kisasa ili kunusuru afya za wanafunzi na baada ya wananchi kujenga zahanati kwa nguvu zao na kukamilisha boma kwa sh. milioni 8 linahitaji kuezekwa.

Kwa upande wake Kalli alisema serikali lazima iunge mkono juhudi za wananchi na itaendelea kuboresha elimu baada ya kufuta ada kuanzia darasa la awali hadi sekondari kidato cha nne ili watoto wasome hasa wa kike na kwa heshima ya wananchi kwa kazi waliyoifanya atapeleka madawati 10 kwenye shule hiyo.

“Elimu ni bure na madawati haya yatawanufaisha watoto,hivyo wazazi muache tamaa ya maliwa, waacheni watoto wa kike wasome,ni tunu katika taifa letu na hapa watatoka makamu wa rais, naibu spika,mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu wanawake,kwanza ni waaminifu hawapindishi maneno kama wanaume,”alisema Kalli na kuwataka watoto wawaenzi wazazi na wananchi kwa kufaulu mitihani yao vizuri.

Pia aliahidi ifikapo Aprili 30,atapaua na kuezeka vyumba vya madarasa vilivyojengwa na wananchi hao na kumwagiza Meneja wa Tanesco Magu kwenda kwenye shule hiyo kupima nguzo zinazohitajika ili waunganishwe kwenye Mradi wa Umeme Vijijini (REA).

Aidha baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo,waliwashukuru wazazi na wananchi kwa kujitoa kwao na kuwajengea madarasa pamoja na kuwatengenezea madawati.

“Tunawashukuru wazazi kwa jitihada zao,wengi mavazi yalichafuka kwa tulikuwa tunakaa chini, pia tunamshukuru Hayati Rais John Magufuli kwa kutoa elimu bure na tutaendelea kumkumbuka kwa hilo,”alisema Bulala Simba.

Patrick Costantine yeye alisema madawati hayo yatakuwa kichochea cha kusoma kwa bidii ili wafaulu masomo na kutimiza ndoto zao huku Kado Safari akisema kuondolewa kwa changamoto ya kukaa chini wataongeza bidii ya kujifunza zaidi. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ishengoma Kabuche, alisema uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa uliathiri utoaji wa taaluma na kushusha ufaulu, hivyo jitihada na mchango wa wananchi wa kuchonga madawati 54,ujenzi madarasa mawili na ofisi ya walimu kutaondoa msongamano wa wanafunzi darasan

MAAFISA ELIMU KATA WAASWA KUSIMAMIA UBORESHWAJI ELIMU

$
0
0

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde, akifungua Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, akizungumza wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayesimamia Elimu ya Awali na Msingi ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Suzan Nussu, akizungumza wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama akichangia mada katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi, Maadili na Nidhamu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwalimu Robert Likwolela akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Kyerwa, Oscar Tumwesige, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Bagamoyo, Hamisi  Mwanankuta, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Muheza, Danstan Mahiza, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde (katikati) akiungana na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, kuimba Wimbo wa Taifa, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano huo Aprili 8, 2021 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama (kulia-mbele) na Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu Mectildis Kapinga (wa tatu kutoka kushoto – mbele), wakiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, wakifuatilia mkutano huo katika siku ya kwanza, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

******************************

Na Veronica Simba – TSC

Maafisa Elimu Kata kote nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kutoa msaada wa kitaaluma ili kuwawezesha walimu katika maeneo yao kufundisha kwa ufanisi na hivyo kuboresha kiwango cha elimu.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde, alipokuwa akifungua Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8 mwaka huu, jijini Dodoma.

Aidha, Naibu Waziri Silinde, amewataka Maafisa Elimu Kata kusimamia kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari huku akieleza kuwa imebainika baadhi ya Maafisa hao hawasimamii shule za sekondari.

“Mnajikita zaidi katika shule za msingi na kujisahau kusimamia shule za sekondari. Kote ni wajibu wenu na hakuna mtu anayepaswa kuwazuia. Akijitokeza wa kuwazuia tupeni taarifa tutamchukulia hatua,” alisisitiza.

Akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume ya Utumishi wa Walimu katika Mkutano huo, Mkurugenzi Msaidizi, Maadili na Nidhamu, Mwalimu Robert Likwolela aliwataka Maafisa Elimu hao kushughulikia makosa yanayofanywa na walimu, ambayo hayapewi umuhimu kwa kudhaniwa ni madogo.

Akifafanua, Mwl. Lwikolela alitoa mfano wa kosa la utoro kwa walimu kuwa pamoja na kuathiri utoaji elimu lakini limekuwa halitiliwi maanani kwa kuchukuliwa kama halina uzito.

“Wako baadhi ya Walimu hata hawaandai Mpango wa Somo (Lesson Plan) na wanafundisha vipindi vichache tofauti na walivyopangiwa lakini wanaachwa tu. Ni wajibu wenu kuwafuatilia hao na kushirikiana na Wakuu wa Shule katika kuwarudisha kwenye mstari.”

Hata hivyo, akitoa ufafanuzi zaidi katika masuala ya nidhamu kwa walimu, Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu, Mectildis Kapinga, alisema endapo Mwalimu atabainika kutenda kosa, anayepaswa kutoa adhabu kwake kwa mujibu wa sheria ni Mamlaka yake ya Nidhamu ambayo ni Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), na siyo vinginevyo.

Hivyo aliwatahadharisha Maafisa Elimu Kata kutojichukulia sheria mkononi badala yake, ikitokea wamebaini Mwalimu anakiuka maadili ya kazi yake, washirikiane na Mkuu wa Shule kumkanya ili abadili mwenendo wake na asipojirekebisha wamripoti kwa Mamlaka yake ya Nidhamu ili imchukulie hatua.

Kwa upande wake, akitilia mkazo suala la uwajibishaji walimu wanaokiuka maadili ya kazi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka TSC, Moses Chitama, alishauri kabla ya muhusika kuripotiwa kwa Tume, zifanyike jitihada katika ngazi ya shule na kata, kukaa na kuzungumza naye ili kumkanya, hususan kwa makosa madogomadogo ambayo yanarekebishika.

Mkutano huo wa Maafisa Elimu Kata unatarajiwa kuhitimishwa rasmi Aprili 9, 2021 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu.

MILIONI 311.9 KUTUMIKA KUCHONGA BARABARA HIFADHI ZA TAIFA IBANDA KYERWA NA RUMANYIKA KARAGWE.

$
0
0

 Serikali imetenga shilingi  milioni 311.9 zitakazotumika  kuchonga Barabara yenye urefu wa kilometa 20 katika hifadhi ya Taifa  Rumanyika karagwe na kilometa 51 katika  Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kyerwa Mhe. Innocent Sebba  Bilakwate (CCM)  ambaye alihoji kuhusu mpango wa  Serikali  wa kuweka miundombinu mizuri ya Barabara katika hifadhi hizo Ili kuvutia watalii.

Akijibu Swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro  ,Mhe. Masanja ameeleza kuwa hifadhi za Taifa za Ibanda Kyerwa na Rumanyika karagwe  zilianzishwa kupitia tangazo la Serikali Na 509 na 510 la tarehe 5/7/2019 .

Amesema hifadhi hizo zilitokana na kupandishwa hadhi kwa yaliyokuwa mapori ya akiba ya Ibanda na Rumanyika .

"Ili  kuwezesha hifadhi hifadhi hizo kufikika kwa urahisi Serikali kupitia  TANROADS na TARURA iliyokuwa ikitengeneza Barabara mbalimbali zinazorahisha kufika kwa watalii katika hifadhi hizo , Barabara hizo ni pamoja Mgamkorongo iliyopo wilaya ya korogwe hadi murongo wilayani Kyerwa yenye urefu wa kilometa 112 ambayo inafanyiwa   matengenezo na TANROADS kila mwaka na imewekwa  katika mpango wa Kujengwa kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha 2020/2021" Amesisitiza Mhe.Mary Masanja.

Aidha, amesema jitihada hizo za kuboresha miundombinu ya Barabara katika hifadhi ya Taifa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe na maeneo mengine yote ya hifadhi zitasaidia kuweka Mazingira mazuri  yatakayowezesha hifadhi hizo kutembelewa na watalii wengi wa maeneo ya karibu pamoja na wageni kutoka nchi jirani.

Kuhusu ulinzi wa maeneo hayo  ameeleza  kuwa wizara imekuwa ikiyaanisha maeneo yote na kuweka mipaka.

" Katika hifadhi ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika tulifanya tathmini baada ya  wataalamu wetu kuainisha mipaka, utekelezaji wake tunaendelea nao kwa kuandaa Mazingira ya kuwapeleka wataalamu kwa ajili ya gharama za uthamini na kuanisha maeneo ambayo yanachangamoto za uhifadhi " Amesisitiza.

 


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akiwasili katika viwanja vya Bunge kuhudhuria mkutano wa 3 wa Kikao cha 5 cha Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema leo April 08, 2021 Jijini Dodoma.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO APRIL 9,2021

WANAWAKE SIHA VINARA UREJESHAJI WA MIKOPO

$
0
0

 

Na Mwandishi wetu, Siha

 

Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro imekabidhi jumla ya kiasi cha shilingi milioni 72 kwa ajili ya mkopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Wilayani humo ikiwa ni fedha zinazotokana asilimia 10 mapato ya Halmashauri hiyo.

 

Akikabidhi fedha hizo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amewapongeza wanavikundi kwa kurejesha mikopo yao kwa wakati ili fedha hizo ziweze kuwanufaisha walengwa wengi zaidi.

 

Aidha, amewataka walengwa hao kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii ili kujiinua kiuchumi na hatimaye kufanikisha Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

 

Amesema Serikali itaendelea kuwashika mkono ili kuhakikisha wanaimarika zaidi katika vikundi vyao pamoja na mtu mmoja mmoja.

 

Dkt. Mollel pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwa kubuni vyanzo zaidi vya mapato na kuweza kuhakikisha inatenga zaidi ya Sh.Mil.48 kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

 

" Tunapoelekea sasa tutaangalia zaidi sheria hii ili wanufaika hawa waweze kupewa mmoja badala ya vikundi, tumetembea maeneo mengi lakini Wilaya ya Siha mnafanya vizuri" alisema Dkt.Mollel.

 

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswela alisema mikopo hiyo imechangia kupungua kwa vitendo vya unyanyanyasaji wa kijinsia katika Wilaya hiyo kutokana na wanawake wengi kujikwamua kiuchumi.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndaki Stephano alisema hakuna vikundi ambavyo ni sugu kulipa na kuongeza kuwa, mikopo hiyo inawasaidia hasa wanawake na kuwa Halmashauri inaendelea kuwatembelea vikundi hivyo na kuwapatia elimu ya mikopo.

 

Ndaki aliongeza kuwa Halmashauri ina mpango wa kutenga fedha zaidi ili vikundi hivyo viweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyosaidia kutoa ajira nma kukuza uchumi.

 

Awali akitoa taarifa ya mikopo hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Marco Masue alisema kiasi cha Sh.Mil. 48.5 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na Sh.Mil 23.7 ni marejesho ya mikopo hivyo imesaidia katika kuwafikia wanufaika wengi zaidi kupata mikopo .

 

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika Penina Maduhu na  Michael Nko wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata mikopo hiyo na kueleza kuwa inawasaidia kuinua uchumi wa familia zao na kuongeza wigo wa shughuli wanazozifanya.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akimpongeza mmoja wa akina mama wa Wilaya ya Siha kwa kupata mkopo wa Sh.Mil. 3 kutokana na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Baadhi ya wanufaika wa mkopo wa Sh. Mil. 72 zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel (hayupo pichani) kabla ya kukabidhiwa mkopo huo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wanufaika wa mkopo wa Sh. Mil. 72 uliotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha kutokana na mapato ya ndani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswela.

 

 

MISA NA SHUKRANI

$
0
0

  


MKE, WATOTO NA FAMILIA YA MAREHEMU WILLIE LADISLAUS MBUNGA, WANATOA SHUKRANI ZAO ZA DHATI KWA MAJIRANI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIJITOA KWA HALI NA MALI KUSHIRIKIANA NAO KWENYE MSIBA NA MAZISHI YA MPENDWA WAO MAREHEMU WILLIE LADISLAUS MBUGA ALIYEFARIKI TAREHE 3 FEBRUARI, 2021 AKIWA  NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI YA MLOGANZILA NA KUZIKWA TAREHE 6 FEBRUARI, 2021 NYUMBANI KWAKE TEMBOMGWAZA, TABATA KISUKULU.

 PIA WANAWASHUKURU MAPADRE WALIOHUDUMU KWENYE MSIBA NA MAZISHI, KWAYA YA DON BOSCO WALIOKESHA KUIMBA, VIKUNDI NA VYAMA MBALIMBALI WALIOTOA RAMBIRAMBI ZAO ZA UPENDO.

 MUNGU BABA AWABARIKI WOTE NA KUWAPATIA THAWABU KWA UPENDO WAO ULIOPITILIZA.

 IBADA YA SHUKRANI (MISA) ITAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 10 APRILI 2021, KUANZIA SAA SABA MCHANA NYUMBANI KWA MAREHEMU TEMBOMGWAZA, TABATA KISUKULU.

           “MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI”

                                                        AMEEEEEN


MRAJISI WA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI ZANZIBAR ZAWATAKA WAKULIMA KUCHANGAMKIA FURSA MRADI WA VIUNGO,MBOGA MBOGA NA MATUNDA

$
0
0

 MRAJISI wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla, amewataka wakulima kisiwani Pemba kuchangamkia fursa za uwepo wa mradi wa  Viungo, Mboga na Matunda Zanzibar ili uwasaidie kujikwamua kiuchumi kupitia uzalishaji wa mazao hayo.

Mrajisi ametoa wito huo wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya shamba darasa yaliyotengwa kwaajili ya kuwafundishia wakulima wanufaika wa mradi huko katika Shehia za Ole na Mjini Ole Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema Serikali inamatumaini makubwa na utekelezaji wa mradi huo kwa wakulima Zanzibar kwani unalenga kuwakomboa wakulima wa mazao hayo kwa kukuza uchumi pamoja na upatikanaji wa chakula majumbani.

“Serikali inaridhishwa sana na mradi huu kwani ni mradi ambao umekuja kuisaidia serikali kuwainua wakulima wetu kupitia shughuli hizi za kilimo ambacho mradi unafanyia kazi. Nikuombeni endeleeni kuchangamkia fursa hii kwa kutumia taaluma mnayoipata kila siku kutoka kwa wataalam huku mkitambua kwamba serikali inaungana nayi katika kila hatua,” alisema.

Aliwataka wakulima kutokatishwa tamaa na changamoto zinazowakabili katika hatua ya awali na badala yake kufanyakazi kwa karibu na wataalam wa kilimo ili kuzitaftia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza.

“Naomba tusivunjike moyo, tuendelee tuwe na ari ya kufanya kazi. Nafahamu mwanzo ni mgumu lakini tunatakiwa tushirikiane na tupokee yale tunayoelekezwa na wataalam wetu wa kilimo. Najua kwenye jamii wapo baadhi ya watu watakao wabeza kwa juhudi zenu, lakini fanyeni malengo yenu yaliyokusudiwa na mradi huu hatimaye mtakuja kuona faida yake,” alisema.

Katika hatua nyingine Ahmed alisema ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) utaisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi kufanikisha kutekeleza ahadi yake ya upatikanaji wa ajira laki tatu Zanzibar.

Alisema, “Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, imezungumzia suala la ajira laki tatu. Nimearifiwa kwamba mradi huu ukikamilika karibu ajira 21,000 zinaweza kupatikana, sasa ajira hizi zikipatikana maana yake lengo la Serikali kuongeza fursa za ajira limetekelezeka.”

Meneja wa mradi huo, Amina Ussi Khamis alisema ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya uandaaji wa shamba darasa na kubaini changamoto zinazowakabili wakulima katika uandaaji wa maashamba hayo wakati ambapo wakulima wanaendelea na zoezi la uandaaji wa mashamba yao kwaajili ya upandaji wa mazao.

Alisema, “leo tumekuja hapa kwa lengo la kuangalia maendeleo yetu ya maandalizi ya shamba darasa ili tuweze kujua kila hatua ambayo tumeifikia katika utekelezaji wa mradi wetu wa Viungo.”

Mapema akitoa maelezo wakati wa ziara hiyo, afisa kilimo anayeshughulika na mboga kanda ya Pemba,  Sada Juma Segeja, alisema taaluma inayotolewa na wataalam wa kilimo kupitia Shamba darasa zilizoandaliwa katika Shehia ambazo mradi unatekelezwa itasaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao na kufanikisha kwa haraka ufikiaji wa malengo ya mradi.

Wakulima kupitia mradi huo wameshukuru uwepo wa mradi kutokana na taaluma wanayoipata kupitia shamba darasa imewawezesha kila mkulima kuanza maandalizi ya shamba lake kwaajili ya uzalishaji.

Ziara hiyo ya Mrajisi wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar ni  mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Viungo, Mboga na Matunda unatekelezwa Zanzibar na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, Zanzibar, (TAMWA ZNZ), People’s Development Forums, (PDF) na Community Forests Pemba (CFP) kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).


Meneja wa mradi huo, Amina Ussi Khamis (kushoto), mrajisi wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla(katikati) na meneja uendeshaji wa mradi wa VIUNGO kanda ya Pemba Sharif Maalim Hamad (kulia) wakiwa shambani wakati wa ziara.
 

Meneja wa mradi wa VIUNGO, Amina Ussi Khamis akizungumza wakati wa ziara.
MRAJISI wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla akitoa maelekezo kwa wakulima.

Maelekezo: afisa kilimo anayeshughulika na mboga kanda ya Pemba,  Sada Juma Segeja, (kushoto) akitoa maelezo kwa mrajisi wa asasi zisizo za kiserikali wakati wa ziara.

Half of Pakistan's income owned by 20 pc of population

$
0
0

 

Representative Image
Representative Image

Karachi [Pakistan], April 6 (ANI): The speakers at a session on human development and inequality on Saturday called for the redressal of systemic flaws that have led to a rise in income inequality in Pakistan.

The panellists at the session titled, Human Development and Inequality, of the first international conference on economics and sustainable development hosted online by the Institute of Business Administration (IBA), expressed the view that the issues of inequality must be understood in terms of wealth and ownership in the economy, and discourse on fighting inequality must be along the lines of foreign influences, gender disparity and social mobility, reported The Express Tribune.

The session, held in collaboration with the United Nations Development Programme (UNDP), began with opening remarks by UNDP Pakistan's resident representative Knut Ostby, who emphasised the need to understand economic situations through the lens of power, policy and people.

To address inequality in Pakistan, he stressed on thinking of sustainable growth in lines with income and social mobility. Approximately 20 per cent of the population holds half of the total income generated in Pakistan, he said.

The panel also featured Special Assistant to the Prime Minister (SAPM) on Social Protection and Poverty Alleviation Dr Sania Nishtar, senior researcher at the Collective for Social Science Research Ayesha Khan, SAPM on Revenue Dr Waqar Masood Khan, IBA executive director Dr Akbar Zaidi.

Adding to Osby's initial remarks, Dr Zaidi emphasised on the factor of land ownership and the influence landowners have on the country's politics - and by extension, in policy-making, reported The Express Tribune.

Dr Masood posed the question of fiscal policies and factors that contributed to inequality in the country. He argued that financial exclusion, which refers to a lack of financial services such as credit transfers and loan facilities, was a major contributor to inequality. (ANI)

Amid rising tensions, China, US send warships in disputed waters

$
0
0

 

Representative image
Representative image

Beijing [China], April 6 (ANI): China and the United States have sailed aircraft carriers into the disputed waters in the East and South China Seas, as Beijing continues to assert its maritime claims in the region and Washington has ramped up military exercises to counter it.

This comes as Beijing has moored over 200 vessels in the Whitsun Reef in the South China Sea claimed by both China and the Philippines.

The Philippine foreign ministry on Monday said China's claims that the boats were sheltering from bad weather were "blatant falsehoods" and "clearly [a] false narrative of China's expansive and illegitimate claims in the West Philippine Sea".

On Sunday, a US aircraft carrier strike group led by the USS Theodore Roosevelt entered the South China Sea from the Strait of Malacca, according to the Beijing-based South China Sea Strategic Situation Probing Initiative, citing satellite data.

It said the USS Mustin guided-missile destroyer was also operating in the East China Sea and edged close to China's Yangtze River on Saturday.

Meanwhile, Chinese aircraft carrier the Liaoning passed through the Miyako Strait off southwestern Japan on Saturday, days after China's defence ministry urged Japan to "stop all provocative moves" over the contested Diaoyu Islands in the East China Sea, which Tokyo calls the Senkakus.

The PLA Navy announced on social media on Monday night that the Liaoning was en route to conduct "scheduled exercises" near Taiwan, to "test the effectiveness of troop training, and to improve the capacity to safeguard the country's sovereignty, safety and development interests". Similar naval exercises would continue to be organised as planned, it said.

After China's carrier group was spotted passing the waterway between Okinawa and Miyako islands towards the Pacific on Saturday, Japan has also sent destroyer JS Suzutsuki, a P-1 maritime patrol aircraft and a P-3C anti-submarine warfare patrol aircraft to gather information and monitor the movements of the Chinese vessels.

Regional tensions have also been rising over Taiwan, where Beijing has in recent months ramped up "grey zone" warfare tactics against the democratic island it claims as its own.

China claims sovereignty over almost the entire South China Sea and has overlapping territorial claims with Brunei, Malaysia, the Philippines, Vietnam and Taiwan.

China has been increasing its maritime activities in both the South China Sea and the East China Sea over the past few months, partly in response to Beijing's concerns over the increasing US military presence in the region because of escalating Sino-US tensions.

Beijing's rising assertiveness against counter claimants in the East and South Sea has resulted in unprecedented agreement across the Indo-Pacific.

The Philippines' defence chief Delfin Lorenzana on Sunday said the continued presence of Chinese maritime militias around the Whitsun Reef reveals their intent to further occupy features in the West Philippine Sea.

This comes as Lorenzana has called for the Chinese boats to leave Whitsun Reef (Julian Felipe Reef), located within its exclusive economic zone in the South China Sea.

The Whitsun Reef belongs to the Spratly archipelago, the territory of which is claimed by Brunei, China, Malaysia, the Philippines, Taiwan, and Vietnam.

China considers the Spratly archipelago to be its territory, despite the Hague-based Permanent Court of Arbitration ruling, which said there was no legal basis for China's maritime claims. The arbitration proceeding was initiated by the Philippines in January 2013, Sputnik reported. (ANI)

KATIBU MKUU NZUNDA AHIMIZA KASI NA MATOKEO OFISI YA WAZIRI MKUU

$
0
0

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Bunge) mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi  ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya (kulia) kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, anaeshughulikia (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda (kushoto).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Mtumba Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akipokea ua kutoka kwa Afisa Utumishi wa ofisi hiyo Bi. Faith Lazaro wakati wa mapokezi rasmi alipowasili na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili8, 2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Jamal Katundu kwa watumishi wa Ofisi hiyo eneo la Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  mara baada ya kupokelewa katika ofisi hizo Mtumba Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akiweka saini katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo upande wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo  Aprili 8, 2021 eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi  ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Kaspar Mmuya kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Uwekezaji).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akipokea ua kutoka kwa Afisa Tawala wa ofisi hiyo Bi. Leah Kibasa wakati wa mapokezi alipowasili rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili8, 2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya asalimiana na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi hiyo, aliyeongozana naye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa ofisi hiyo Bw. Greyson Mwaigombe.

 

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU KATIKA MAKAO MAKUU YA WIZARA – DODOMA

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab leo amewasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kupolewa na Watumishi na Menejimenti ya Wizara.

Balozi Fatma Rajab baada ya mapokezi hayo alipata wasaha wa kuongea na Wakuu wa Idara na Vitengo ambapo licha yakuwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi na juhudi amewaahidi ushirikiano katika kuteleza majumu yao ya kila siku. 

Balozi Fatma aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tarehe 6 Aprili, 2021.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akipokelewa Wizarani Mtumba, jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Anisa Mbega alipowasili Wizarani. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Stephen P. Mbundi wakati anapokelewa Wizarani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi na Menejimenti ya Wizara mara baada ya mapokezi ya kukaribishwa Wizarani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akiongea na Watumishi na Menejimenti ya Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Wizarani
Viewing all 120377 articles
Browse latest View live