Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119823 articles
Browse latest View live

FIKRA ZA KARUME ZINASTAHIKI KUENZIWA MUDA WOTE - OTHMAN MASOUD

$
0
0






MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud, amesema licha ya miaka 49 tangu kifo cha Hayati Mzee Abeid Amani Karume, bado mchango wa kiongozi huyo katika maendeleo ya Zanzibar ni mkubwa na unapaswa kuheshimiwa.

"Ni wazi kwamba jina na Karume halitosahaulika katika ukombozi wa visiwa vya Zanzibar", Mheshimiwa Othman ameyasema hayo katika Kongamano la Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Visiwa vya Zanzibar, Hayati Mzee Karume, ambapo alimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mheshimiwa Othman amesema kongamano hilo limefanyika ili kutoa fursa pia kwa wasomi na wananchi mbalimbali kutambua kikamilifu hekima, falsafa na fikra za kimapinduzi za kiongozi huyu shupavu zilizotokea katika historia ya taifa letu.

"Kwa kweli leo tuna heshima kubwa kuhudhuria kongamano hili lenye lengo la kuzienzi ndoto, fikra na falsafa za kiongozi huyu mweledi katika kuleta ukombozi wa nchi yetu. Karume ameiletea Zanzibar fahari kubwa sambamba na kuwafanya watu kuwa huru hata kujiamulia mambo yao wenyewe kwa uhuru na amani", alisema Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Katika kusisitiza umuhimu wa kongamano hilo, Mheshimiwa Othman alisema ni dhahiri kwamba kongamano hili linawaleta waandishi na wasomi pamoja ili kupambanua kwa makini fikra na mchango wa Hayati Mzee Karume, ambapo mtu mmoja mmoja ataweza kuelewa kwa undani mambo aliyoyafanya kiongozi huyo wa kwanza wa Zanzibar na kuyaweka katika vitendo kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Bwana Steven Wasira, amesema shabaha ya kongamano hilo ni kurithisha historia kutoka kizazi kimoja kwenda chengine.

"Tuna mengi ya kujifunza kwa Karume, kwani alikuwa ni miongoni mwa viongozi wakuu wa bara la Afrika kudai uhuru wa nchi zao pamoja na bara la Afrika kwa ujumla," amesema Bwana Wassira.

Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na viongozi, wafanyakazi na wanafunzi kutoka katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere pamoja na wageni waalikwa limefanyika katika chuo hicho kilichopo Bububu, nje kidogo ya mji wa Unguja.


MAJALIWA: TUTAYAENZI MAONO, JITIHADA NA JUHUDI ZA HAYATI MAGUFULI

$
0
0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba Serikali itaenzi na kuendeleza jitihada, maono na juhudi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli hususan katika ulinzi wa rasilimali za Taifa pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Pia, Waziri Mkuu ametaja mambo mengine yatakayoendelezwa ni pamoja na  nidhamu katika matumizi ya fedha za umma, utekelezaji wa miradi ya kimkakati, kuenzi lugha ya Kiswahili, kuunganisha na kuwajali wananchi wanyonge na kudumisha umoja wa Kitaifa.

 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 13, 2021) wakati akiwasilisha hotuba ya Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/2022, Bungeni jijini Dodoma.

 

Amesema Serikali itatekeleza kwa kasi miradi ya kimkakati ambayo inalenga kukuza uchumi, kuimarisha huduma za jamii na kuongeza fursa za ajira. “Kwa kasi tuliyoanza nayo, Serikali itaendelea kuongeza nguvu zake na hatimaye kukamilisha miradi hiyo.”

 

“Serikali itaendelea kuimarisha huduma za jamii zikiwemo afya, elimu na maji pamoja na utekelezaji wa miradi inayoendelea na uanzishwaji wa miradi mipya. Pia itaimarisha makusanyo ya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na mashine za POS na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma na kuendeleza rasilimali fedha katika miradi ya kimkakati na kielelezo.”

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo kutekeleza miradi na programu mbalimbali zinazolenga kuimarisha huduma za kiuchumi na kijamii na kuchukua hatua za kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko kwa kuzingatia maelekezo  yanayotolewa na wataalam.

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa, kidini na kikabila waendelee kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, ufanisi, uaminifu na kupiga vita rushwa ili waweze kulinda mafanikio waliyoyapata. “Jitihada hizo ndizo zimetuwezesha kuingia katika nchi za uchumi wa kati.”


Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh.116,784,244,000.00 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake kwa matumizi ya mwaka 2021/2022. Amesema kati ya fedha hizo, sh. 93,303,370,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 23,480,874,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

 

“Mheshimiwa Spika, vilevile naliomba Bunge lako tukufu liidhinishe jumla ya shilingi 128,873,377,000.00 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, shilingi 121,875,906,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na shilingi 6,997,471,000.00 ni kwa ajili ya maendeleo.”


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA

JUMANNE, APRILI 13, 2021.

Rais Samia amemudu nafasi hiyo-Sabiniani

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
WATANZANIA na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameendelea kumuenzi Hayati Dkt. John Magufuli na kusema kuwa hawatasahau mchango wake kwenye Nchi, huku wakimpongeza Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumudu vizuri nafasi hiyo na kuahidi kuendelea kusimamia miradi ya kimkakati.

Kauli hiyo ilitolewa Jijini Dar es Salaam jana na Kada wa CCM Charles Sabiniani wakati akitoa zawadi za kanga kwa vikundi mbalimbali vya Wanawake ikiwa ni jitihada za kumpongeza Rais Mama Samia Hassan Suluhu.
Sabiniani ambaye pia ni Mjasiliamali maalufu alisema kuwa anaguswa zaidi na uongozi wa mama na ndio maana ameamua kutoa zaidi hiyo.

Mmoja wa waliyepata Kanga hizo ni Anneth Kagenda, alisema kuwa anampongeza Rais Mama kwa kuongoza Nchi.

Alisema kuwa anamuombea kila la kheri kwa Mungu mama pamoja na Makamu wake Mhe. Mpango katika kuongoza Taifa.

Hata hivyo alitoa pongezi kwa Kada huyo kwa kumpatia zawadi ya kanga.


Kada za CCM Charles Sabinian pichani akiwa ametoa kanga kwa ajili ya kumpongeza Rais Mama Samia Hassan Suluhu.

Mkurugenzi TAMWA ataka jamii isiwashangae wanawake kuwa viongozi

$
0
0

Wanahabari tofauti kutoka Tanzania wakibadika karatasi ambazo zinalenga kuonesha ni vitu gani wanapaswa kufanya wanaume na vitu gani ambavyo vinapaswa kufanya wanawake na ni vipi wanaweza kufanya wote kwa pamoja.
Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Daily news kwa upande wa Zanzibar Issa Yussuf akichangia miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
Mwakilishi wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.UNESCO Nacy Kaizilege akitoa neon kwa niaba ya shirika hilo.
Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari 30 Tanzania yenye lengo la kuwawezesha wanahabari hao kuandika habari za kijinsia pamoja na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauto wakijianda kubadika karasai ambazo zinalenga kuonesha ni mambo gani anayostahiki kufanya mwaname na mwanamke.

Na Muhammed Khamis, TAMWA
MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Rose Reuben amesema wakati umefika kwa jamii kubadili mtanzamo na kuona kuwa nafasi ya uongozi kwa mwanamke sio bahati bali ni jambo analostahiki kama walivyo wanaume.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa White Sand hote Mbezi Jijini Dar Es Salam katika mafunzo maalumu ya siku tatu ya waandishi wa habari 30 kutoka vyombo tofauti Tanzania yaliolenga kuwajenga uwezo waandishi hao kuhusu maswala ya kijinsia na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.

Alisema wanawake katika jamii bado wanaonekana si watu wenye kustahiki kuwa viongozi na ndio maana uwepo wa Rais Samia madarakati hadi leo hii kuna watu wanaendelea na mshangao.
Kufuatia dhana hiyo Mkurugenzi huyo alisema waandishi wa habari ndio wenye wajibu wa kubadili mitazamo hio kwa jamii ili waweze kuamini kuwa mwanamke ni kama sehemu nyengine ya wanaopaswa kuwa viongozi.

Alisema kwa kuwa wanahabari wana sauti kubwa kuliko watu wengine ama taasisi basi wanapaswa kutumia vyema fursa walionayo kuibadili jamii ya kitanzania kutoka kwenye mawazo yasiopaswa kuwepo hadi sasa.

‘’Tunahitaji kuona mifumo ya usawa kwenye jamii zetu ili wanawake wasiedelee kuonekana kuwa watu dhaifu na wasiofaa kushika nafasi mbali mbali za uongozi.’’Aliongezea.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la umoja wa kimataifa linalojihusisha na maswala ya wanawake UNWOME Hodan Addov alisema wataendelea kushirikia na TAMWA katika pande zote mbili kwa lengo kwa lengo la kuleta usawa katika jamii.

Alieleza kuwa anaamini uwepo wa usana ni dhana inayostahiki kuwepo kwa lengo la kujenga Tanzania imara kwa watu waote bila upande mmoja wa jinsia kuonekana kuwa na nguvu zaidi na mwengine ni dhaifu.

Nae mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.UNESCO Nacy Kaizilege alisema wanahabari wanawajibu kupasa sauti zaidi za wanawake kupitia taarifa zao za kila siku huku wakijua kuwa wanawake ni watu wanaohitaji kupaziwa sauti zao zaidi.

Sambamba na hilo aliwataka pia wanahabari hao kutoacha kupaza sauti zao kuhusu maswala ya udhalilishaji katika Nyanja mbali mbali zikiwemo za kisiasa ambapo hadi sasa kumekuwepo na taarifa mbali mbali za udhalilishaji kwa wanawake kupitia siasa.

IDDI NADO AJITIA KITANZINI MIAKA MIWILI TENA

$
0
0

 

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

KUFUATIA  kuonesha kiwango bora ndani ya Azam Fc Kiungo mshambuliaji wa wa timu hiyo Idd  Seleman 'Nado', ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwa matajiri wa Chamazi.

Nado amesaini mkataba huo leo mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.

Popat amesema, Nado amekuwa na kiwango bora tokea msimu uliopita alipojiunga nao akitokea timu ya Jiji la Mbeya Mbeya City alipoonesha kiwango kikubwa hadi kuvutiwa naye.

Amesema, katika msimu wa 2020/21 Nado  amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.

Kwa sasa Azam Fc ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi akiwa na alama 47 nyuma ya vinara Yanga wenye alama 51 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 46.

CWT YAWEKA MSIMAMO WA KUPINGA UANZISHWAJI WA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU [TANZANIA TEACHERS PROFESSIONAL BOARD.]

$
0
0



CHAMA cha walimu Tanzania [CWT] kimesema kitaendelea kupinga na kukataa  juu ya zoezi la uanzishwaji wa Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania kwani  bodi hiyo imelenga kumkandamiza Mwalimu badala ya kumsaidia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma  leo Aprili 13, 2021 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania Mwalimu Leah Ulaya amesema majukumu yaliyooneshwa kwenye bodi hiyo  yanafanana na yale   yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa walimu  [TSC] iliyopo sasa.

“Mnamo  mwaka 2019 , Chama cha walimu Tanzania kilialikwa kutoa maoni kuhusu uanzishwaji  wa Bodi hiyo kimsingi sisi CWT,tuliikataa  kwa nguvu zote  baada ya kusoma sheria hiyo  tukajiridhisha pasi  na shaka  kwamba chombo hiki  kililenga kumgandamiza mwalimu  badala ya kumsaidia ,aidha majukumu yaliyo kwenye bodi hiyo yanafanana  na yale yanayofanywa na Tume ya utumishi wa walimu.'' Amesema Ulaya

Rais huyo wa CWT ameendelea kufafanua kuwa;

”Mnamo Tarehe 12 April,2021 CWT tulialikwa na katibu wa bunge  kukutana na kamati ndogo ya Bunge ya sheria juu  ya kanuni za uendeshaji  wa bodi hiyo ambayo msingi wake  ni sheria mama ambayo sisi CWT  tulikataa tangu mwanzo,katika kikao hicho  cha tarehe 12,April,2021 Chama cha Walimu Tanzania  kiliendelea na msimamo wake  wa usitishwaji wa chombo hiki  na kuimarisha utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu[TSC.]

Aidha, Rais huyo wa CWT ametaja   sababu kadhaa za msimamo  kupinga uwepo wa bodi hiyo kuwa ni pamoja na gharama za bodi ambapo uendeshwaji  utategemea pesa ya mwalimu mfukoni   na ada ni elfu hamsini kwa mwaka  pamoja na kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu.

 “Bodi hii tunaipinga kwa nguvu zote kwa sababu ,uendeshaji wa bodi hii utategemea pesa ya walimu mfukoni kwa ajili ya usajili,leseni na ada kwa mwaka ambayo si chini ya Tsh.50,000/=,gharama za kusikiliza mashauri,gharama za semina  ya kila mwaka ambayo ni lazima  kuhuisha leseni hiyo ,kushindwa kufanya hivyo mwalimu  atanyang’anywa leseni  na hivyo kupoteza sifa ya kufundisha na sababu nyinyine ya kuikataa bodi hii ni kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu na majukumu yakifanana.” Amesema.

Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani ameiomba serikali kuendelea  kuwamini na kuwatia moyo walimu.

“Walimu tunafanya kazi kwa bidii na ukiangalia ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kinachotakiwa ni serikali kuendelea kuamini walimu pamoja na kuwatia moyo.'' Amesema.

Katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania[CWT] Deus Seif amesema endapo bodi hiyo itapitishwa makato ya mwalimu kila mwezi itakuwa ni Tsh. 4200 huku Naibu katibu Mkuu CWT,Maganga Japhet Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania haina faida yoyote bali itadidimiza uchumi wa walimu.

ZAKHIA SULEIMAN AWANIA TUZO ZA 'JASIRI AWARDS 2021'

#VIDEO: Benki ya CRDB, TIOB wazindua Kadi mpya kwa wanachama wa TIOB

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Wadogo na Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Kadi ya Uanachama wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB) uliofanyika leo Aprili 13, 2021 kwenye ofisi za Taasisi hiyo, zilizopo eneo la Kinondoni Morocco, Dar es salaam. Kadi hiyo pia inaweza kutumika kama Kadi ya Malipo ya kibenki ambayo inaweza kutumia kufanya malipo mbalimbali, kutoa fedha kwenye ATMs au kwa Wakala yeyote wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB),Patrick Mususa  na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif.



Baadhi ya Wanachama wa 
Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB) na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.



DANIDA YATOA RUZUKU INAYOLENGA KUSAIDIA WAMAMA NA WATOTO

$
0
0
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kulia) wakisaini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kulia) wakibadilishana nyaraka za makubaliano baada ya tukio la kutiliana saini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari na Desemba 2021, unaotekelezwa na LSF.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kulia) wakifurahia pamoja baada ya tukio la kutiliana Saini kwa mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akisaini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya LSF kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari na Desemba 2021.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Norgaard Dissing-Spandet akitia saini mkataba wa ruzuku ya nyongeza kiasi cha shilingi za kitanzania 5.6 bilioni (USD 2.4 million) zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya Januari na Desemba 2021 unaotekelezwa na LSF.

SHIRIKA Lisilola Kiserikali linalotoa msaada wa kisheria (LSF) limesaini mkataba wa kupokea ruzuku.

Kiasi cha Shilingi bilioni 5.6 (USD 2.4) Kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa upatikanaji wa haki nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya januari hadi mwishoni mwa disemba mwaka huu.

Ruzuku hiyo iliyopokelewa inalenga kuboresha Mazingira ya Uwekezaji wa kisheria nchini kwa kuzijengea uwezo Taasisi zinazotoa huduma ya msaada wa kisheria pamoja na huduma za wasaidizi wa kisheria kwa makundi mbalimbali katika jamii hususani wanawake na watoto.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini,Balozi wa Denmark nchini Mette Norgaard amesema kuwa Shirika la Maendeleo Kutoka Denmark (DANIDA) imeamua kuwaongezea ruzuku Shirika linalotoa msaada wa kisheria nchini (LSF) kama sehemu ya uwajibikaji katika kuhakikisha suala la upatikanaji haki nchini linazingatiwa.

"Shirika linalotoa msaada wa kisheria(LSF) limekua mdau wetu mkubwa takribani miaka 10 na tumeamua kuongeza ruzuku hiyo ili kusaidia zaidi utekelezaji wa mradi wa (LSF) unaotekelezwa kwa ajili ya kusaidia wakina Mama na watoto ambao ndio wahanga wakubwa wa maswala ya haki zao." Amesema Mette.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika linalotoa Msaada wa kisheria nchini (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema kuwa ruzuku iliyotolewa na wadau wake itasaidia kikamilifu katika kuendelea kutekeleza Mradi wa upatikanaji wa haki nchini unaotekelezwa nchi nzima kwa upande ea Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Ng'wanakilala ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (LSF) imekuwa imishirikiana na wadau wake mbalimbali ikiwemo Shirika la Maendeleo Kutoka Denmark (DANIDA) ambapo imeweza kusaidia kuboresha sekta ya msaada wa kisheria nchini kupitia uwezeshaji wa kisheria zaidi ya 4000 nchi nzima

Pia aliongeza kuwa Wanaamini ruzuku hii itawasaidia katika kuboresha Mifumo ya utoaji haki iliyo rasmi na isiyo rasmi ili kuwezesha upatikanaji haki kwa wakati.

WAZIRI MCHENGERWA AWAPA NENO MA-RC NA MA-DC WANAOTUMIA MAMLAKA YAO KUWEKA WATU NDANI

$
0
0





Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha kutumia vibaya mamlaka zao kuwaweka ndani kinyume na sheria watu wanaotenda makosa huku akiwataka kuzingatia Utawala wa haki na sheria.

Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Wizara yake ikiwa ni siku kadhaa tangu ateuliwe na Rais Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo akichukua nafasi ya Kepteni George Mkuchika ambaye ameteuliwa kuwa Waziri asiye na wizara.

Akizungumza katika kikao hiko, Mchengerwa amesema Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya wamekua wakitumia vibaya mamlaka yao waliyopewa kikatiba ya kuwaweka ndani masaa 24 hadi 48 watu waliofanya makosa huku akisisitiza viongozi hao kutambua kuwa Serikali ya Rais Samia inazingatia haki na utawala bora.

Waziri Mchengerwa pia ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuondoa kesi zote zilizopo mahakamani ambazo wanaona kwamba serikali haina uelekeo wa kushinda.

" Kumekua na mfulululizo wa kesi nyingi ambazo TAKUKURU inazipeleka mahakamani lakini haina ushahidi wa kutosha, niwaombe kuziondoa kesi zote ambazo hatuna uhakika wa kushinda, ni kupoteza fedha na muda kuendesha kesi ambazo mwisho wake wenyewe tunaona hatutoshinda.

Maelekezo mengine ni kwamba TAKUKURU iharakishe uchunguzi ambao Rais Samia aliagiza ufanyike kwenye Mamlaka ya Bandari nchini TPA, lakini pia iongeze juhudi za haraka kufikisha kesi za rushwa mahakamani kwa sababu hakuna kesi nyingi zilizopelekwa mahakamani badala yake kumekuepo na majadiliano nje ya mahakama," Amesema Mchengerwa.

Ametoa pia onyo kwa maafisa utumishi wote nchini kuhakikisha wanasimamia na kutatua changamoto za watumishi nchi na yeyote ambaye atashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo hatosita kumuagiza Katibu Mkuu Utumishi kumuondoa kwenye nafasi hiyo.

" Haiwezekani watumishi wapate changamoto kwenye nafasi zao halafu kuna Maafisa Utumishi, niwatake maafisa utumishi wote kushughulika na changamoto za watumishi nchini na atakayeshindwa tutamuondoa kwenye nafasi hiyo," Amesema Mchengerwa.

NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZINGATIA NIDHAMU NA MAADILI " SIYO MTUMISHI WA UMMA UNAONGOZA KWA KUMPIGA MKEO"

$
0
0





Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewataka watumishi wake nchini kuwa mfano wa kuigwa mbele ya jamii kwa kuwa wenye maadili huku wakizingatia nidhamu kwenye maeneo yao ya kazi na kwenye jamii inayowazunguka.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wizara hiyo kilichoendeshwa na Waziri wa wizara hiyo, Mohammed Mchengerwa jijini Dodoma.

Ndejembi amesema ni jambo la ajabu kuona mtumishi wa serikali anakua wa kwanza kufanya vitendo ambavyo siyo vya kimaadili kazini au kwenye maeneo ya nje ya kazi jambo ambalo linaitia doa serikali na hivyo kusisitiza utii na nidhamu kwa watumishi hao.

Ndejembi amesema kumekuepo na tabia ya watumishi kutokua na lugha za staha kwa wananchi wanaofika kupata huduma kwenye ofisi za serikali ambapo amekemea tabia hiyo akisisitiza kwamba watachukulia hatua wote wanaoenda kinyume na maadili ya kazi.

" Zipo taarifa za watumishi wanaotoa lugha mbaya kwa wananchi wanaofika kupata huduma, wengine lugha za ubabe na wakichelewesha huduma kwa mteja, niseme tu hatutomvumilia mtumishi wa namna hii kwa sababu atakua anaigombanisha serikali na wananchi.

Siyo kwenye maeneo ya kazi tu hata kwenye makazi yetu tunapaswa kuwa mfano mzuri wa watu wenye maadili, siyo mtumishi wa serikali ndio unaongoza kwa kupiga mkeo kila siku, mtumishi wa serikali unaongoza kwa ulevi na lugha chafu au unaongoza kwa madeni, tuziepuke sifa hizo mbali ili kulinda sura ya Serikali yetu," Amesema Ndejembi.

SERIKALI YAZINDUA RASMI MKAKATI WA UNYWAJI MAZIWA KWENYE OFISI ZA UMMA, YAANZA NA WIZARA 10

$
0
0







Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imezindua mkakati mahususi wa unywaji maziwa katika Ofisi za Umma nchini lengo likiwa ni kuongeza Soko la maziwa ya ndani lakini pia kukuza kipato cha wafugaji.

Mkakati huo umezinduliwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ambaye ametoa wito kwa watumishi wa Umma nchini na wananchi kwa ujumla kuunga juhudi mkakati huo ili pia kuimarisha ubora wa afya zao.

Waziri Mashimba amesema kwa kuanza mkakati huo utahusisha wizara 10 ambazo ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Biashara, Tamisemi, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.

Mashimba amesema mkakati huo wameshirikiana na Kampuni za uzalishaji maziwa ambazo zimejitokea majokofu ya kuhifadhia maziwa hayo ili yasiharibike.

" Leo tunazindua awamu ya kwanza ya unywaji maziwa kwenye ofisi za serikali na kwa kuanza tumeanza na wizara hizi 10 lakini tunaamini tutakakua na awamu zingine za uzinduzi zikihusisha wizara zingine, taasisi na mashirika ya umma.

Unywaji wa maziwa maofisini utachangia kwa kiwango kikubwa Soko la maziwa yanayotengenezwa nchini na kuepuka unywaji wa maziwa ya nje, hivyo tutakuza pato la wafugaji pia na kuchochea kiwango cha ajira kwenye Viwanda vinavyotengeneza maziwa nchini," Amesema Waziri Mashimba.

Amesema itakua ni jambo la ajabu kuona ofisi ya serikali inaagiza maziwa yanayotengenezwa nje ya nchi kwani kufanya hivyo ni kuchochea pato la nje na kukuza uchumi wa mataifa mengine.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Kazi wa nchini, Dk George Msalya amesema anaimani kama ofisi zote za serikali ambapo watumishi wa umma wanafika takribani Laki Tano zitaunga mkono unywaji huo wa mazingira itakua ni fursa nzuri na pana ya kukuza soko la maziwa ya ndani.

#VIDEO: MAKAMANDA WATATU WA IDARA MAALUM ZANZIBAR WASIMAMISHWA KAZI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.


TBS Yateketeza Bidhaa Zenye Thamani ya Milioni 19

$
0
0
Na Mwandishi Wetu- Mbeya
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa hafifu za vyakula na vipodozi zenye thamani ya shilingi milioni 19 katika maeneo mbalimbali ya biashara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Kwa Mujibu wa Meneja wa Shirika hilo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Abel Mwakasonda, bidhaa hizo hafifu zilikamatwa wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni uliofanyika katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2021 katika mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya.

“Bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji aina ya soda,bia, vyakula kama biskuti,mafuta ya kula, siagi na sabuni za kuogea ambazo muda wake wa matumizi umekwisha”, inaeleza taarifa hiyo.

Vilevile vipodozi vilivyokamatwa ni vile visivyoruhusiwa kuingizwa hapa nchini kutokana na kuwa na viambata sumu kama vile madini tembo (lead), zebaki (Mercury) na Hydroquinone.

Matumizi ya vipodozi hivyo vyenye viambata sumu yana madhara kiafya ambayo husababisha magonjwa ya saratani kwa binadamu, na kwamba, vyakula vilivyokwisha muda wa matumizi husababisha magonjwa ya homa za matumbo.

Aidha, Taarifa hiyo inaeleza kuwa matumizi ya bidhaa hafifu huleta madhara ya kiuchumi kwa muuzaji na mnunuzi wa bidhaa husika baada ya kuthibitishwa kuwa bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya binadamu na kutakiwa kuondolewa sokoni na kuharibiwa.

Ukaguzi wa bidhaa sokoni unafanywa kwa kuzingatia sheria ya Viwango Na 2 ya mwaka 2009 na Sheria ya Fedha Na 8 ya mwaka 2019 ambayo ilihamisha majukumu ya usajili wa majengo ya vyakula na vipodozi yaliyokuwa yakifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwenda kwa TBS.

Shirika linatoa rai kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaingiza sokoni bidhaa ambazo TBS imethibitisha ubora wake na kuziondoa sokoni bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi badala ya kuendelea kuziuza.Tingatinga likitetekeleza bidhaa hafifu zilizokamatwa katika mikoa ya Nyanda za Juu kusini kufuatia ukaguzi uliofanywa na Shirika la Viwango Tanzani (TBS ) katika mikoa hiyo kati ya Januari na Machi, 2021.Bidhaa hafifu zikishushwa katika eneo la utekekezaji katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kukamatwa kufuatia ukaguzi uliofanywa na Shirika la Viwango Tanzani (TBS ) katika mikoa hiyo kati ya Januari na Machi, 2021.

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI DODOMA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye Ndege ya Shirika la Ndege ATCL mara baada ya kuwasili jijini Dodoma leo tarehe 13 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili jijini Dodoma leo tarehe 13 Aprili, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Marubani pamoja na Wahudumu wa Ndege ya Shirika la Ndege ATCL mara baada ya kuwasili jijini Dodoma leo tarehe 13 Aprili, 2021. (Picha na Ikulu.)

 


Kampuni ya EKARI Moja Tanzania yagawa Miche elfu 45 ARUMERU

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv
WANANCHI wa vijiji 13 wilayani Arumeru, Mkoani Arusha wameanza kunufaika na mpango wa ugawaji bure wa miche ya kuotesha katika makazi yao itakayowasaidia kuboresha mazingira na kuwaongezea kipato.

Akiongea mapema leo katika zoezi la ugawaji miche 6000 kwa wananchi wa Kijiji Cha Sakila Juu wilayani humo, msimamizi wa miradi ya miti wa kampuni ya Kilimo ya eka Moja Tanzania inayogawa miche hiyo, Esaria Meena alisema kampuni hiyo imejipanga kugawa miche 45,000 kwa vijiji hivyo Katika kipindi cha wiki moja.

Alisema kuwa tangu wazindue mpango huo mwaka 2018 wameshagawa Miche ikiwwmo ya matunda zaidi ya 500,000 na wanampango wa kugawa Miche milioni 5 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

"Tangu tumeanzisha mpango huu Wananchi wengi wamenufaika kwa kuboresha mazingira,miti ya Matunda, Miche ya mbao ambayo imewasaidia kuongeza kipato na ajira. "Alisema Meena

Alivitaja vijiji vinavyonufaika na mpango huo kuwa ni Njeku, Kikatiti, Maji Moto,Kwa ugoro, Manyire, Maroroni, Migadini, Ngongongare, Muungano, Oldonyongire na Nasholi A na B.

Awali afisa misitu wa halmashauri ya Arusha ,Joseph Masawe ameipongeza kampuni ya Eka Moja Tanzania kwa kuunga mkono sera ya serikali ya upandaji miti ya mwaka 1998 na waraka namba moja ya waziri mkuu inayoitaka kila halmashauri kupanda miti milioni1.5 kila mwaka.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sakila Juu, Richard Mbise amesema kuwa wananchi wamekuwa na hamasa kubwa ya upandaji wa miti na kuwataka wadau wengine wa mazingira kujitokeza kugawa miti hiyo kwani Katika eneo la ukanda wa Meru linahitaji kupandwa miti ya asili kwa ajili ya mvua na miti ya mikaratusi kwa ajili ya uvunaji wa mbao.

"Mwitikio ni mkubwa sana kwa wananchi wa Sakila Juu hivyo Kuna uhitaji zaidi wa Miche ipatayo 200,000 hivyo tukipata miche hiyo itatosheleza kaya zipatazo 1400. "Alisema

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Sakila Juu, Emmanuel Mbise na Ekael Palangyo ambao wamenufaika na mpango huo kwa kupata Miche 30 kila mmoja ya aina mbalimbali wamesema kuwa miti hiyo itawanufaisha kwa kuleta mvua na kuvuna mbao na kulitaka kampuni hilo kuendelea kuwapatia miche ya miti ili kuwaongezea kipato.
Mwakilishi wa kampuni ya EKARI Moja Tanzania, Esaria Meena kulia, akimkabidhi miche 30 mwenyekiti wa Kijiji Cha Sakila juu Richard Mbise (kushoto), katika zoezi la ugawaji wa Miche, lililofanyika juzi Wilayani Arumeru katikati ni Afisa misitu wa halmashauri ya Arusha DC,Joseph Masawe(picha na Woinde Shizza, ARUSHA).

Je, tunahitaji uzoefu wa Kazi ili kuweza kuajiriwa?

$
0
0

 MEKUWA ikiwapa wakati mgumu sana hasa wale wanaokuwa wamemaliza masomo yao kwa muda mfupi na kuingia katika harakati za kutafuta ajira. Ofisi nyingi sana hasa Mashirika Binafsi (yasiyo ya Kiserikali) na Makampuni binafsi yamekuwa yakiongeza suala la Uzoefu wa kazi kama kigezo cha kupata ajira. Hivyo kampuni ya simu ya Infinix ikaona ni vyema kuwakutanisha vijana kutoka sehemu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo kuweza kujadili suala hili kupitia mdahalo unaosema “Je, tunahitaji uzoefu wa kazi ili kuweza kuajiriwa?” ambapo ilifanyika katika Ukumbi wa Sahara Ventures uliopo Morocco siku ya Jumamosi Tarehe 10/04/2021. 

Mdahalo huu uliwataka vijana kujigawa katika vikundi viwili  wenye kukubaliana na mada ambao walifahamika kama Kundi Black na kundi White wenye kupinga kwamba ili kuajiriwa uzoefu si kitu cha lazima. Mdahalo huu uliongozwa na watu Maarufu kama vile MC. Anthony Luvanda, Bi. Shamila Mshangama na Mr. Erick Benard (Mr. Ben)


Mchuano ulikuwa ni makali mno kuanzia kwenye vikundi hivyo viwili hadi kwa wageni waalikwa ambao ndio walikuwa kama majudge na waongozaji wa mdahalo mzima.

Bi. Shamila alianza kwa kuipinga mada “kupata kazi sio lazima uwe umeajiriwa maana unaweza kujiajiri kwa kuwa na taasisi ambapo unaweza kuonwa kutokana na juhudi ulizofanya, hivyo utakuwa umepata uzoefu kupitia hapo lakini hujaajiriwa”. 



Lakini pia MC Luvanda aliikataa hoja kwa kusema “unaweza kuwa huna uzoefu wowote na bado ukafanya vizuri saana na mwenye uzoefu asifanye vizuri pia”. 


Vijana wote katika makundi yao nao walionekana kuwa wamejiandaa vya kutosha kila upande ulkiwa na hoja zenye kujitosheleza iliyopelekea kutopata mshindi mmoja kwani kila mmoja aliibuka  kidedea na kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile Simu, Tshirt, Wireless Keyboards za kompyuta pamoja na Note 8 package iliyokuwa na vitu mbali mbali kama (Mwamvuli, Notebook, Power bank, chupa ya chai/maji, zilizoandaliwa na Mdhamini Mkuu ambayo ni kampuni yenye kujihusisha na uzalishaji wa simu janja Infinix Mobile.


Infinix Pamoja ya kuwa ni kampuni iliyojikita kwenye soko la simu lakini pia ni kampuni yenye kumjali Zaidi mwanafunzi wa leo kwa kumuandaa kwajili ya kesho yake. Kupitia XTOK Infinix imeweza kuwafikia wanafunzi wengi sana kwa wakati mmoja ambapo kila mwanafunzi hujifunza kitu kipya katika Tafrija hii ya XTOK. 



Infinix mobile Tz kuwaahidi vijana na wote walio hudhuria kwenye mdahalo huu kuwa watakuwa nao Pamoja kwenye shughuli zote za vijana na pia kuwasihi wasikose mdahalo ujao kwa kuwapa nafasi pia wao kuchagua mada ambayo itakuwa ya Xtok inayofata, mada inaendelea kwenye kurasa zao za kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter na pia kwenye kiunga chao cha Xclub.


Tembelea link hii kuona mdahalo huu ulivyoenda https://www.instagram.com/p/CNmyuLYHfO_/?igshid=o67ietlqew7k 

RC SANARE AMALIZA MGOGORO ARDHI ULIODUMU KWA MIAKA TISA.

$
0
0
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero,kuhakikisha shule ya Msingi shikizi ya Sokoine inapata Walimu wa kuajiliwa na Serikali, kwani kwa sasa Shule hiyo haina Walimu ambao wanasifa na vigezo vya kufundisha Wanafunzi.

Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo mbele ya Wananchi katika mkutano wa Hadhara wenye lengo la kutatua mgogoro Ardhi kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Wilaya ya Mvomero, uliodumu ndani ya miaka tisa,wakigombania mpaka wa Kijiji cha Mkono wa mara,ambapo kila upande ukidai Kijiji hicho kipo katika Wilaya yake.

Akizungumza mala baada ya kutatua mgogoro huo Mkuu wa Mkoa Ole Sanare,akaitaka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kukamilisha ujenzi wa madarasa kwenye shule ya Msingi Shikizi ya Sokoine ambayo ainachumba kimoja cha madarasa,huku ikiwa na wanafunzi zaidi ya mia tatu walio katika mikondo tofauti.

Aidha akizungumzia mgogoro huo Mkuu wa amkoa wa Morogoro amesema mgogoro huo umedumu kwa kipindi kirefu lakini ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya ardhi tayari wamemaliza mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Ole Sanare amewataka viongozi wa Vijiji kuacha tabia ya kuuza maeeneo pasipo kufuata sheria na taratibu jambo ambalo linasababisha migogoro ya Ardhi ya katika maeneo mengi Mkoani Morogoro.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa kaenda mbali zaidi na kuwataja baadi ya viongozi wakiwemo wa chama cha Mapinduzi CCM wanaotuhumiwa kuuza maeneo pasipo kufuata sharia katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomoro akiwemo Mzee Kinyau na Mzee Koka,huku akiagiza kufanywa uhakiki kwa wale wote wanaomiliki maeneo katika Halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Morogoro Frank Minnzikuntwe amesema baada ya kupokea maagizo ya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa aliunda tume iliyohusisha pande zote mbili za Wilaya ya Mvomero na Morogoro na kumaliza kabisa mgogoro huo.

Nao baadhi ya wananchi wasema kutatuliwa kwa mgogoro huo utachochea maendeleo kwani walikosa namna ya kutatua kero zao kwai walikua hawajua wapo upande gani. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO KAMPUNI YA TANZANIA DAIMA.

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) amekutana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Tanzania Daima Gerva Lyenda (Kushoto) Leo April 13, 2021 Dodoma. Mkurugenzi huyo alifika ofisi za Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na Michezo na kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mhe. Bashungwa kuwasilisha ombi lao na kwa majadiliano zaidi kuiomba serikali kama itawezakuwapa leseni ya kuanza kazi ya kuchapisha tena gazeti la Tanzania Daima ambalo lilizuiliwa leseni yao tangu June 24, 2020.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari alifuta leseni ya gazeti hilo ikiwa ni baada ya kulionya gazeti mara kadhaa huku gazeti lenyewe lililazimika kuomba radhi. Kufuatiwa kufungiwa huko Mkurugenzi Lyenda alimueleza Waziri Bashungwa kuwa “gazeti limeajiri watu 90 na wanahangaika kwakukosa leseni tumejifunza na hatutorudia makosa” na akaongeza kwakushukuru “Asante kwa kutusikiliza hii ni fursa kubwa kwetu, maana miezi zaidi ya nane ni mingi sana na hatujafanya kazi yoyote.

Waziri Bashungwa amewapa wito wakuheshimu tasnia ya habari kwakuwa wote tunajenga nchi moja na kuongeza kwa kusema “watanzania wa sasa wameamka wanajua lipi ni baya na lipi ni zuri sasa kama unatoa habari zakupotosha tu utakuwa unawakosea haki yao ya kuhabarishwa”. Pia Waziri ametoa wito kwa wadau wa tasnia ya habari kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassani kuona haki ya uhuru wa habari inaendana na wajibu na uzingatiaji sheria, kanuni na misingi ya taaluma ya habari.





 

RC SINGIDA AITAKA BRELA KUTOA SEMINA KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA DINI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa Wa Singida Dk Rehema Nchimbi akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mjini hapa.
Maafisa kutoka Brela wakimkaribisha Mkuu wa mkoa kwa ajili ya kufungua mafunzo hayo. Wa pili kutoka kushoto ni Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi Utawala  kutoka Brela, Saada Kilabula na kulia ni Afisa Tehama kutoka Brela Hillary Mwendo.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkutano ukiendelea.
 

Na Boniphace Jilili na Dotto Mwaibale, Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameutaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) kutoa semina ya biashara kwa viongozi wa Serikali na dini ili kuwa na uelewa kutokana na wao kukutana na watu wengi jambo litakalosaidia wananchi kuwa na uelewa wanapofanya biashara zao.

Dkt. Nchimbi alitoa kauli hiyo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yanayotolewa na wakala huo kwa wafanyabiashara mkoani hapa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RC Mission.

Alisema wananchi wanachokihitaji sio kuifahamu Brela bali kupata matokeo chanya kwenye biashara zao kupitia Brela,hivyo anategemea kuona mabadiliko makubwa baada ya mafunzo hayo.

"Niwaombe njooni mtoe Semina kwa watendaji wa Serikali na Viongozi wa dini hawa wanawatu wengi wakielewa hawa mtakuwa mmefundisha wengi,tuko tayari kutenga muda hata masaa mawili ili mtupe hii elimu."

Aidha Dkt. Nchimbi aliutaka wakala huo kuendesha kwa haraka zoezi la usajili wa biashara na leseni kutokana na sasa kutumia teknolojia inayokwenda kwa haraka ili kuondoa usumbufu wa kufuatilia mara kwa mara mfanyabiashara, huku akiwataka wafanyabiashara kufuata taratibu, maadili na nidhamu katika biashara.

"Nawapongeza Brela kwa ubunifu huu wa kutoa mafunzo ya kuwaelimisha wafanyabiashara ili kuelewa namna ya ufanyaji biashara yatatoa fursa kwa maendeleo ya nchi.Utumishi ni kuwafuata wananchi hongereni sana." alisema Dk Nchimbi na kuongeza.

"Haya mafunzo yatatujengea uelewa,kuelewa sisi wote ni wamoja,tuko kwenye mnyororo mmoja,akiharibu mmoja ameharibu mfumo wote wa kibiashara.Biashara inahitaji nidhamu,umakini maadili na bidii." alisema Dkt. Nchimbi.

Kwa upande wake Msaidizi wa ofisi Mwandamizi Utawala kutoka Brela Saada Kilabula alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa wananchi ambapo yameanza hapa Singida na baadaye Dodoma na kuhitimishwa mkoani Morogoro kwa awamu hii ambapo pia zoezi hilo kwa baadaye linatarajiwa kufanyika hadi ngazi za Wilaya na lengo hasa wananchi wawe na uelewa wa kibiashara.

Brela iliona kuna haja ya kutoa mafunzo hayo kwa wananchi kutokana na baadhi ya watu wasiowaaminifu kuwatoza fedha nyingi wananchi wanapohitaji kusajili biashara zao hivyo kupitia mafunzo hayo yataondoa huo usumbufu na kutambulisha mfumo wa namna ya kujasili biashara kupitia simu za mkononi.

"Hatujawahi kutoa mafunzo haya lakini tuliona kuna haja ya kuja huku chini kwa wananchi tuwape elimu kutokana na wengi kutozwa fedha nyingi wanaposajili biashara zao na baadhi ya watu wasiowaaminifu." alisema Kilabula.



Viewing all 119823 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>