Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120391 articles
Browse latest View live

MAJALIWA: ASANTENI WATANZANIA KWA UZALENDO NA MSHIKAMANO

$
0
0

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania wote kwa kuonesha mshikamano na uzalendo wa hali ya juu wakati wa kutangazwa na kipindi chote cha maombolezo ya msiba hadi mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 7, 2021) alipozungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Visiwani Zanzibar katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume.

Machi 17, 2021 aliyekuwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan majira ya saa 5.15 usiku aliwatangania wananchi kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli kilichotokea saa 12.00 jioni katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Baada ya kutangaza taarifa za kifo hicho pia alitangaza siku 21 za maombolezo pamoja na taratibu za kuuaga mwili na mazishi, ambapo Machi 20 na 21, 2021 viongozi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani walipata fursa ya kuaga katika uwanja wa Uhuru.

Machi 22 yalifanyika mazishi ya Kitaifa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma ambayo yaliongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Marais tisa, Machi 23 zoezi la kuaga lilifanyika kwa wananchi wa Zanzibar.

Machi 24 wananchi wa mkoa wa Mwanza walipata fursa ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli, Machi 25 wananchi wa mkoa wa Geita walimuaga katika Uwanja wa Magufuli wilayani Chato na Machi 26, 2021 alizikwa nyumbani kwake Chato, Geita

Waziri Mkuu amesema anawashukuru Watanzania wote kwa namna walivyoshiriki katika zoezi hilo, hivyo amewaomba waendeleze utulivu na mshikamano mkubwa waliounesha katika kipindi chote cha majonzi. ”Wakati wote tangu msiba ulipotangazwa Watanzania walikuwa watulivu hadi leo tunapomaliza siku 21 za maombolezo, tunawashukuru sana.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa miongozo yake aliyoitoa ambayo iliiwezesha kamati ya mazishi ya kitaifa kuratibu vizuri zoezi hilo na kufanikisha mazishi ya Hayati Dkt. Magufuli. ”Kauli yake iliwasaidia Watanzania kuendelea kuwa watulivu huku wakimuombea Hayati Dkt. Magufuli.”

Pia, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano mkubwa alioutoa kupitia kwa Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya mazishi ya kitaifa ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine.

”...Nawashukuru wajumbe wa kamati ya mazishi ya kitaifa, mikoa na wilaya. Pia navishukuru vyombo vya habari kwa ushiriki wao ambao umewawezesha Watanzania wote kupata taarifa za tukio zima kuanzia siku ya kutangazwa kwa kifo hadi mazishi. Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata taarifa za matukio mbalimbali.”

”Pia navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha zoezi zima linafanyika kwa amani na utulivu katika maeneo yote nchini. Nawashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi chama ambacho Hayati Dkt. Magufuli alikuwa Mwenyeti wake wa Taifa, kwani nao walishiriki kikamilifu.”

Waziri Mkuu amesema baada ya kumaliza siku 21 za maombolezo ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Watanzania wanatakiwa waendelee kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili Taifa lizidi kupata maendeleo. ”Tuendelee kuwa watulivu, tushikamane na tushirikiane katika kufanya kazi.”

Akizungumzia kuhusu watumishi, amesema kila mwenye dhamana ndani ya Serikali anajukumu la kuhakikisha kuwa anawapokea, anawasikiliza na kuwahudumia ipasavyo wananchi wote wanaohitaji kuhudumiwa ili malengo yaliyowekwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025  yafikiwe.


RAIS MWINYI AONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KATIKA DUA MAALUM YA KUMUOMBEA MAREHEMU MZEE ABEID AMANI KARUME LEO.

$
0
0

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisoma na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) na Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali.

AKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dkt. Amani Karume, Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf Alhajj Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu wakiitikia dua katika hafla ya kisomo cha Hitma na Dua iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume n a (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa.

VIONGOZI wa Dini na Waumini wa Kiislam wakisoma hitma na dua kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, kisomo hicho kimefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza kisoma cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi.

MJANE wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume,MAMA Fatma Karume akishiriki katika kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea marehemu iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na (kulia) Mke wac Rais Mstaaf wa Zanzibar Mama Shadya Karume na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Mgeni Hassan Juma.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitika ubani wakati  wa hafla ya kisoma cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume na (kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kisomo hicho kimefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma ikisomwa na Bi.Maryam Mliwa (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zuhura Kassim na (kulia kwa Rais) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan. Wakiitikia dua.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehe Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo maalum na dua iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Musta Kitwana wakiitikia dua ikisomwa na Naib u Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Othman Hassan Ngwali katika kaburi la Marehemu Abeid Amani Karume.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Mama Fatma Karume na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakiwa katika viwanja vya kaburi la Marehemu Abeid Amani Karume wakati wa kumuombea dua.

(Picha na Ikulu)

SURA 3 ZA RAIS SAMIA

$
0
0

Na Emmanuel J. Shilatu

Tangua aapishwe kuwa Rais wa awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha sura kuu 3 zinazotoa mwelekeo wa kiutendaji kwake.

A: UHODARI NA TUMAINI

Rais Samia amepokea kijiti cha Urais kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa 5 wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli na wa kipindi chote ameliongoza vyema Taifa kwa uhodari wa ufariji kwa Watanzania wote. Rais Samia amewafariji wafiwa upande wa familia, amewafariji Watanzania na kujawa faraja, tumaini na nguvu mpya.

Rais Samia ameonyesha uhodari katika ulezi ambapo amesimama kama Mama ndani ya uongozi kwa kuwapa onyo, angalizo ambalo ni sawa na kuwapa fursa nyingine ya kujisahihisha ili safari ijayo vijana wakizingua basi Mama atawazingua vyema.

Rais Samia ameonyesha namna alivyo komaa kiuongozi kwa kusimamia vyema utawala wa sheria kwa kuwasimamisha wenye tuhuma kwanza kupisha uchunguzi na sio kuwatimua moja kwa moja pasipo kutoa nafasi ya kumsikiliza ili kubaini ukweli wa tuhuma. Huyo ndio Mama yetu Rais Samia.

Rais Samia ameanza kwa kutoa agizo vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe. Nyota njema ya uendelezwaji wa uhuru wa habari nchini uliokuwapo miaka na miaka.

B: UZALENDO

Rais Samia ameonyesha uzalendo wa kuzilinda rasilimali zetu nchini kama ambavyo mtangulizi wake Hayati Dkt Magufuli amefanya.

Mathalani, Rais Samia amekemea utoroshwaji na uchimbaji kiholela wa madini ya Tanzanite kwenye machimbo ya mererani. Ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha madini tuliyobarikiwa yanatunufaisha Watanzania.

C: UCHAPA KAZI

Katika kuonyesha zege halilali, Rais Samia ndani ya muda mfupi amefanya teuzi na tenguzi mbalimbali za viongozi na kuwaapisha.

Pia ametoa mwelekeo wa Serikali yake; kazi ya utekelezaji ilani ya uchaguzi inaendelea;  ameendeleza urithi wa miradi ya kimkakati ya kimaendeleo aliyoiacha Hayati Dkt Magufuli.

Itoshe kusema kazi inaendelea kupitia sura 3 za uchapa kazi, uzalendo na uhodari wa Rais Samia.

Ndugu zangu, Tuendelee kunywa mtori, nyama tumezikaribia.

Shilatu, E.J

Rais wa awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan

WAMPONGEZA RAIS SAMIA KURUHUSU UCHIMBAJI MADINI KUENDELEA

$
0
0

 

Na Woinde Shizza ,Michuzi Tv

Mchimbaji mdogo  wa Madini ya Ruby yaliyopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido Mkoani Arusha Sendeu Laizer amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kubaini mwenendo usioridhisha wa ukusanyaji kodi pamoja na kuruhusu wachimbaji Madini kuendelea kuchimba Madini

Aliyasema hayo leo wakati akizungumza na Vyombo vya Habari, ambapo  alisema kuwa baada ya kuwaapisha Mawaziri Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia alimtaka Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kutanua wigo wa ukusanyaji kodi akionya kile alichokiita kuwaua walipa kodi kwa kufunga biashara zao, kuchukua fedha na vifaa vyao vya kazi pamoja na kufunga akaunti zao.

Alisema kuwa kauli hiyo imerejesha amani kwa wafanyabiashara na itaongeza uwekezaji chini Katika sekta mbalimbali ikiwemo ya madini

“Tunampongeza sana Rais na tunamuunga mkono ambacho kilikuwa kinafanyika ni kibaya sana, watu kuvamia katika biashara, kufunga akaunti na kuchukua fedha,  kwa nchi nyingine ni kesi kubwa tunamuombea mungu aendelee kumlinda," alisema.

Alisema kauli hii itasaidia sasa wafanyabiashara kuendeleza biashara zao na kulipa kodi ya Serikali lakini bila kuua biashara zao

 Sendeu Laizer ambaye kampuni yake hivi karibuni  ilipewa  tuzo na serikali ya upambanaji kwa jitiada kubwa alizofanya bila kukata tamaa ,ambapo alizingatia sheria zote za nchi pamoja na sheria zote za uchimbaji wa  madini  ,uhuzaji wa madini na uhusiano

Alisema tuzo hiyo  alikabidhiwa na Rais wa sasa wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia 
Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Samia Suluhu  kwa niaba ya hayati Rais magufuli kipindi alipokuwa makamu wa rais. 

 cha kutambua mchango wake sekta ya biashara ya madini ya vito, amesema  Rais ameonyesha huruma kwa wafanyabiashara na watahakikisha wanahamasishana kulipa kodi. 

Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuhamasisha  uchimbaji wa madini , kwani utawezesha wawekezaji wengi wa ndani na nje kujitokeza kuja kuchimba Madini hayo.

Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza wakafanya mambo yakaenda sawa.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bilionea Sendeu Laizer tuzo wakati alipokuwa  Makamu wa Rais.
 

VIJANA IKUNGI WAONESHA UZALENDO, WACHANGIA MADAWATI SHULE YA MSINGI MWISI

$
0
0

Viongozi pamoja na wananchi wa Kijiji cha Mwisi wilayani Ikungi mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya makabidhiano ya madawati Shule ya Msingi Mwisi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa Kijiji cha Mwisi kwenye shughuli za kukabidhi madawati.

Afisa Maendeleo Wilaya ya Ikungi Haika Masawe akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.

Afisa Mtendaji Kata ya Ndung'unyi, Yahaya Njiku ambaye pia ni mdau wa maendeleo akizungumza kwenye halfa hiyo ya kukabidhi madawati Shule ya Msingi Mwisi.

Wananchi wa Kijiji cha Mwisi wakiwasikiliza kwa makini viongozi kwenye halfa hiyo.
Madawati yakikabidhiwa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Lighwa Borgius Ntandu.
Saimon Philipo mmoja wa vijana waliochangia madawati hayo akielezea namna walivyoguswa na kuamua kutoa msaada wao.
Viongozi wakiwa meza kuu.



Na Dotto Mwaibale, Singida.


VIJANA wazalendo kutoka Kijiji cha Mwisi Kata ya Lighwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wametoa Madawati kwenye Shule ya Msingi Mwisi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha watoto wote wanakaa kwenye madawati wakati wa masomo yao.

Vijana hao ambapo kwa sasa wako maeneo mbalimbali,wameona vema kuunga mkono juhudi za Serikali na wameamua kuanzia nyumbani kwenye Shule walikosomea ambapo wamechangia madawati 37.

Akikabidhi Madawati hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi amewapongeza Vijana hao ambapo amesema amefarijika kuona wazalendo wanaokumbuka kurudisha fadhila nyumbani.

"Hongereni sana ni watu wachache sana wanaokumbuka kurudisha fadhila,hivyo endeleeni kuchangia mnapoona kuna changamoto katika kijiji chenu.Na mimi nachangia madawati 20." alisema Kijazi na kuongeza.

"Vijana kwenye risala yenu mumesema kuna uhitaji wa kukarabati chumba cha Darasa katika Shule hii ambalo litatumika kama Ukumbi, nachangia mifuko 30 ya Saruji pamoja na kumlipa fundi,hivyo mtakapoanza mipango niambieni." alisema.

Kijazi aliwataka Vijana kubuni Miradi mbalimbali ili kufungua fursa za ajira zitakazopelekea maendeleo ya Elimu na mambo mengine ambapo aliwaahidi kuwa Halmashauri kupitia asilimia 10% zinazotengwa itatoa mikopo hiyo kwa Vijana watakao anzisha miradi ya maendeleo.

Aidha mmoja wa vijana hao waliounda umoja wa wanadarasa waliohitimu Shule ya Msingi Mwisi Mwaka 2007,Saimon Philipo alisema waliona zawadi pekee ya kulipa nyumbani ni kutengeneza madawati ili wadogo zao wasome kwenye mazingira mazuri.

"Sisi tuliamua kuanzisha umoja wetu ili tuweze kuchangia shughuli za maendeleo,Sio tu hapa tutafanya hata maeneo mengine lakini tuaona tuanzie kwanza nyumbani." alisema Saimon.

Naye Diwani wa Kata hiyo Borgius Ntandu aliwataka Vijana wa Kata hiyo kuwa chachu ya maendeleo kwa kuiga mfano wa Vijana wengine wazalendo wanaunga mkono juhudi za Serikali.

Hata hivyo Diwani huyo aliwapongeza wananchi wa kijiji cha Mwisi kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi wake.

Kwa upande wake Mdau wa maendeleo wilayani humo Yahaya Njiku ambaye pia ni Afisa Mtendaji Kata ya Ndung'unyi alisema uzalendo wa vijana utapimwa kwa utendaji kazi wao na sii vingine,hivyo akawaomba vijana wengine kuwa wazalendo kwa kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

"Huyu Saimon mmoja waliochangia madawati haya nimesoma naye kidato cha tano na sita na amekuwa rafiki yangu sana,nimeona nimuunge mkono katika hili na hata mengine.Nachangia sh.elfu Hamsini." alisema Njiku.

CAFE AMIMZA KAHAWA BORA TANZANIA

NGOMA MPYA YA PROF. JAY - UTANIAMBAI NINI?

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Jijini Dar es Salaam wakati akitokea Zanzibar

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akitokea Zanzibar. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wahudumu wa Shirika la Ndege ATCL mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akitokea Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akitokea Zanzibar leo tarehe 08 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akitokea Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kuondoka Zanzibar na kurejea jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Aprili 2021.PICHA NA IKULU.

KMC WAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA YANGA JUMAMOSI

$
0
0
Kikosi cha timu ya KMC FC kimeendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga ukataopigwa siku ya Jumamosi ya Aprili 10 katika uwanja wa Mkapa kuanzia majira saa moja kamili jioni (19:00).

Katika mchezo huo KMC FC inakutana na Yanga kwa mara ya pili  huku ikiwa ugenini  kwenye msimu huu wa Ligi Kuu 2020/2021.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema wamejipanga kuhakikisha kwamba kikosi chao kinaleta furaha kwa mashabiki kwa kuondoka na alama tatu hivyo wajitokeze uwanjani kutoa sapoti kwa wachezaji.

Amesema, Kino Boys inakwenda kupambania alama tatu muhimu kwenye mchezo huo ambapo katika mchezo wa duru ya kwanza walipoteza kwa goli 2-1 mechi iliyochezwa CCM Kirumba Mwanza 
KMC FC  inatafuta ushindi huo ili kujiimarisha katika msimamo wa ligi Kuu na kwamba licha ya kuwa na upinzani mkubwa wakupambania alama tatu lakini hakuna kitakachoshindikana.

“Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi hautakuwa mwepesi kutokana na aina ya timu ambayo tunakutana nayo, ni nzuri, wanafanya vizuri, lakini pia wanaongoza ligi, hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini pamoja na yote bado KMC FC tunasema kwamba tunakwenda kupambanania alama tatu na tunaimani kubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wetu," amesema.

Katika msimuu huu KMC FC ilikutana na yanga Oktoba mwaka jana katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kupoteza mchezo huo ambapo walifunga magoli mawili kwa moja, Goli la KMC lilifungwa na Hassan Kabunda kipindi cha kwanza katika dakika ya 23.Kocha Mkuu wa Timu ya KMC FC , John Simkoko akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Timu hiyo katika mazoezi ambayo KinoBoys wanaendelea nayo hivi sasa.Goli Kipa wa Timu ya KMC FC Sudi Dondola akiwa kwenye mazoezi ya kujifua kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo Jumamosi.
wachezaji wa Timu ya KMC FC wakiwa kwenye mazoezi.

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AFANIKISHA UPATIKANAJI WA SH MILIONI 85 ZA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KATA YA MANCHALI NA CHILONWA

$
0
0

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na viongozi wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata za Manchali na Chilonwa zilizopo jimboni kwake Chamwino, jijini Dodoma.

Charles James, Michuzi TV

ELIMU kwanza! Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amesema kipaumbele chake kwa sasa ndani ya Jimbo lake ni elimu na kwamba amepanga kutokomeza zero kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne.

Naibu Waziri Ndejembi ametoa kauli hiyo leo alipokua akizungumza na viongozi wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata za Manchali na Chilonwa zilizopo jimboni kwake Chamwino ambapo amefanikisha upatikanaji wa Sh Milioni 35 na mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya sekta ya elimu kwenye Kata hizo mbili.

Akiwa katika kata ya Manchali, Ndejembi amesema tayari kiasi cha Sh Milioni 35 zimeshaingia kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Maabara huku Milioni tano zingine zikiwa zikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Hosteli kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Katika kata ya Chilonwa, Naibu Waziri Ndejembi amefanikisha upatikanaji wa Sh Milioni 50 za kujenga Zahanati huku pia akichangia mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mapinduzi.

Amesema katika kukuza kiwango cha elimu jimboni hapo amepanga kuanzisha makambi ya elimu kwa shule zote zilizopo jimboni kwake ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuwaandaa wanafunzi hao kikamilifu kwa ajili ya mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne.

" Mimi nitaanzisha makambi ya elimu Julai lengo langu ni kutokomeza zero kwa watoto wetu kwa sababu haziwasaidii, ili tuondoe zero ni kuweka walimu wetu na wanafunzi karibu ili waweze kufundishana, suala la chakula nitagharamia mimi Mbunge wao, ni lazima tuwe na kizazi cha vijana wasomi ambao watakua msaada mkubwa kwa familia zao na Taifa letu kwa ujumla.

Kuwaweka wanafunzi sehemu moja na walimu wao kwa miezi mitatu wananolewa nina uhakika tutaondoa zero kabisa, Dunia ya sasa hivi na Tanzania yetu tunahitaji watu wasomi kwa ajili ya kuwawezesha kuingia kwenye ushindani wa ajira na Biashara kwa ujumla, niwahakikishie nitalibeba hilo Mbunge wenu," Amesema Ndejembi.

Amesema katika kukamilisha mpango huo anaangalia namna nzuri ya kuyaweka makambi hayo kama ni kitarafa au kikanda ambapo wanafunzi wote watakaa sehemu moja huku akiahidi kuwapa walimu motisha.

" Hii ni kwa ajili ya maslahi ya watoto wetu na Jimbo letu, tutatoa motisha kwa walimu maana tutawaomba waongeze muda wa ufundishaji, niwaombe wazazi tuungane pamoja ili kuzalisha akina Mama Samia wengine ambao watatoka katika Jimbo la Chamwino, tuzalisha wakina Ndejembi wengine ambao kesho ndio watakua msaada kwetu," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Ndejembi amesema katika mwaka wake huu wa kwanza akiwa Mbunge wa Chamwino ni kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa kiwango kikubwa huku pia akikamilisha miundombinu ya elimu kwa maana ya Madarasa, Hosteli na Maabara ili kurahisisha ufundishaji kwani pia miundombinu bora ya elimu huongeza kiwango cha ufaulu.

Ndejembi pia amewaomba wananchi wa kata hizo mbili na Jimbo la Chamwino kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii wakiendelea kumpa ushirikiano Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwani ni kiongozi mzuri ambaye uzoefu wake alionao na busara ya uongozi iliyopo ndani yake kwa pamoja itailetea mafanikio makubwa ya kimaendeleo Tanzania.

Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena leo

$
0
0
 
Baada ya Mapumziko ya takriban wiki tatu Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika Viwanja viwili tofauti.

Katika mchezo wa kwanza utakaopigwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya itazikutanisha timu ya Mbeya City akikmaribisha Kagera Sugar mechi itakayopigwa kuanzia saa 8 mchana. 

Mchezo wa Pili utawakutanisha wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa kombe la Shirikisho Namungo akiwa nyumbani kumkaribisha Ihefu kwenye dimba la Majaliwa Mkoani Lindi.

Ratiba hiyo inaonesha pia, kesho Aprili 09, inaonesha Timu ya Biashara United itamkaribisha Polisi Tanzania katika Uwanja wa Karume Mkoani Mara huku JKT Tanzania akiwa nyumbani dhidi ya Mwadui FC.

Katika mchezo mwingine Azam Fc wataikaribisha Mtibwa Mechi itakayochezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ligi Kuu itaendelea tena Jumamosu kwa michezo mitatu kupigwa katika Viwanja vitatu tofauti, Vinara wa Ligi Kuu Yanga wakiwakaribisha KMC katika Dimba la Benjamin Mkapa huku Tanzania Prisons akimkaribisha Dodoma Jijini Uwanja wa Nelson Mandela.

Mchezo wa mwingine ni Gwambina wakiwa nyumbani dhidi ya Coastal Union huku mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Simba ukisogezwa mbele kutoka na wawakilishi hao kuwa katika majukumu ya Klabu Bingwa Afrika.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO 2021/22 – 2025/26

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Jangómbe, Mhe. Ali Hassan Omar King kuhusu wajibu wa kumlipa mteja anayeibiwa fedha kwenya akaunti ya benki muda mchache kabla ya uwasilishaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, kulia ni baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, bungeni jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo baada ya kuwasilisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, baada ya kuwasilisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mlalo, Rashid Shanagazi (kulia) na Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 8, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillaly, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 8, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIMAMOTO DODOMA YAZINDUA KAMBI YA MAFUNZO KWA VIJANA SKAUTI

$
0
0

 

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Champumba, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, ambako uzinduzi wa Mafunzo ya Vitendo kwa vijana wa Skauti ya kuwajengea uwezo wa kuokoa, kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali katika jamii ikiwemo, moto, mafuriko pamoja na ajali za barabarani umefanyika mapema leo.

Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma, Salama Katunda, akifafanua jambo mbele ya mgeni rasmi Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mafunzo ya Vitendo kwa vijana wa Skauti ya kuwajengea uwezo wa kuokoa, kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali katika jamii ikiwemo, moto, mafuriko pamoja na ajali za barabarani uliyofanyika leo katika Kijiji cha Champumba, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga, akiimba nyimbo za hamasa pamoja na vijana wa skauti, wakati wa uzinduzi wa Mafunzo ya Vitendo kwa vijana wa Skauti ya kuwajengea uwezo wa kuokoa, kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali katika jamii ikiwemo, moto, mafuriko pamoja na ajali za barabarani uliyofanyika leo katika Kijiji cha Champumba, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga, akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma, Salama Katunda, (Wa pili kushoto), Mratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa, Sajini Yona Benjamin (kushoto), na Viongozi wa Kijiji cha Champumba, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, ambako uzinduzi wa Mafunzo ya Vitendo kwa vijana wa Skauti ya kuwajengea uwezo wa kuokoa, kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali katika jamii ikiwemo, moto, mafuriko pamoja na ajali za barabarani umefanyika mapema leo. (Picha Zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

********************************

DODOMA, 08 Aprili 2021

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Dodoma limeanza kutoa Mafunzo ya Vitendo kwa vijana 130 wa Skauti Mkoa wa Dodoma lengo ni kuwajengea uwezo wa kuokoa, kuzuia na kukabiliana na majanga mbalimbali katika jamii ikiwemo, moto, mafuriko pamoja na ajali za barabarani.

Akifungua mafunzo hayo leo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishaeli Mfinanga amesema ni muda muafaka wa kutoa elimu kwa vitendo kwa vijana wa skauti ili kuwawezesha kukabiliana na majanga wawapo shuleni na hata katika jamii inayowazunguka.

Akizungumzia mafunzo hayo Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma, Salama Katunda, amemshukuru Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo John Masunga kwa kuwapatia Wakufunzi wanaowezesha mafunzo hayo na kuahidi kusimamia na kuhakikisha mafunzo hayo kwa Vijana wa Chama cha Skauti yanaenda kuwa chachu kwa kuhakikisha majanga mbalimbali yanadhibitiwa ili kulinda maisha ya watu pamoja na mali zao.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa siku 7 na Askari Wakufunzi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa, Uongozi wa Chama cha Skauti ngazi ya Wilaya na Mkoa pamoja na taasisi nyingine za Kiserikali, ambapo yanafanyika katika Kijiji cha Champumba, Kata ya Chiboli, Tarafa ya Makang’ara, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Aidha Mafunzo hayo ni mwendelezo wa makubaliano ya Februari 26 mwaka huu ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji liliingia makubaliano ya Ushirikiano wa Programu ya Mafunzo kati ya Jeshi hilo na Chama cha Skauti Tanzania, kwa kutoa elimu kwa vijana wa Skauti nchini ili kuwajengea uwezo katika kukabiliana na majanga mbalimbali.

Kwa upande wake Mratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sajini Yona Benjamin, amesema mafunzo hayo yametolewa muda muafaka ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodoma.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Vijana wa Skauti wameeleza juu ya umuhimu wa mafunzo hayo katika kukabiliana na majanga wawapo shuleni na hata katika jamii zao na kulishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

WAZIRI NDUMBARO ATEMBELEA KITALU CHA UWINDAJI CHA LAKE NATRON EAST

$
0
0

 

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea Kitalu cha Uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron East kilichopo Wilayani Longido mkoani Arusha kilichokuwa kikimilikiwa na Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Green Miles Safari Ltd kwa lengo la kukagua Kambi ya mwekezaji huyo, kusikiliza kero na maoni ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka kitalu hicho.

Ziara hiyo ya kikazi inafuatia Kampuni ya Green Mile iliyokuwa ikimiliki kitalu hicho na baadaye kufutiwa leseni mwaka 2019 kuwasilisha ombi la kufanyika kwa mapitio ya uamuzi uliotolewa.

Akiwa katika eneo la kitalu hicho ,Dkt. Ndumbaro amesema lengo la amejionea hali halisi katika eneo hilo na kuwaahidi wananchi kuwa maamuzi kuhusu suala hilo yatafanyika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu za kusikiliza pande zote zenye maslahi na kitalu hicho.

“Nawaahidi wananchi, Serikali imewasikiliza wadau wote wanaohusika na suala hili wakiwemo viongozi wenu katika ngazi zote na wale wa wilaya, tambueni kuwa Serikali inawapenda na inawajali wananchi wake na ndio maana leo nimekuja hapa na Katibu Mkuu Dkt. Allan Kijazi na viongozi wengine ”, amesisitiza Dkt. Ndumbaro

Amewaeleza wananchi hao kuwa katika kufanya maamuzi kuhusu mgogoro uliopo Serikali lazima ifuate Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo kwa kuwa Tanzania inaongozwa kwa Misingi ya kufuata Sheria, hivyo amewataka wananchi hao wawe watulivu kabla ya kufanyika kwa maamuzi.


CAG AANIKA MASHIRIKA YA UMMA YALIYOSHINDWA KUWASILISHA TAARIFA ZAO ZA MAHESABU, ATAJA HALMASHAURI ZILIZOPATA HATI MBAYA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG)Charles Kichere amesema mashirika 11 ya umma hayajakuliwa kutokana na kushindwa kuwasilisha taarifa za mahesabu yao kwa kuhofia huenda yakikaguliwa yatapata hati mbaya.

Akizungumza leo Aprili 8,2021 ,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG) kichere amesema ameshindwa kutoa maoni kwa mashirika ya umma 11 kwani hakufanikiwa kukagua hesabu zake ili kutoa naoni.

" Kuna mashirika ya umma 11 hatukumaliza kuyagau kwani walishindwa kuwasilisha taarifa za mahesabu yao na wale ambao waliwasilisha walileta nje ya muda wa ukaguzi na hata tulipokagua tulibaini kuna makosa wakafanye marekebisho lakini hawakuleta tena,"amesema.

Ameyataja mashirika hayo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kampuni ya Mbolea Tanzania, Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya, Mfuko wa UTT, Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Shirika la Posta Tanzania, Shirika la Reli Tanzania, Kampuni ya Simu Tanzania, Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) Soko la Bidhaa Tanzania na Taasisi ya Mifupa  Muhimbili.

Hivyo ametoa mwito kwa Menejimenti,Bodi ya Wakurugenzi na Maofisa Masuhuli wa mashirika hayo kuhakikisha wanatimiza matakwa ya kikatiba na kisheria kuwasilisha hesabu kila mwaka kwa ajili ya kutolewa maoni ya ukaguzi.

Pia wanatakiwa kufanya mawasilisho ya hesabu ili kukaguliwa na kufikiaa kiwango cha kimataifa." Aidha wawasilishe taarifa ndani ya wakati ili tuweze kutoa maoni badala ya kuogopa kwa kutowasilisha taarifa zao kuhofia kupata hati wasizozipenda.Ni muhimu kufanyiwa ukaguzi wa mahesabu."

Wakati huo huo amesema ametoa hati mbaya kwa Halmashauri ya Shinyanga,Halmashauri ya Singida, Halmashauri ya Itigi, Halmashauri ya Igunga,Halmashauri ya Sikonge, Wilaya ya Urambo, Wilaya ya Momba, Manispaa ya Tabora, Tume ya Unesco pamoja na Hospitali ya Rufaa Morogoro .Pia amesema ametoa hati zenye mashaka kwa taasisi kwa taasisi 81.

"Katika Serikali Kuu wanajitahidi maana vitabu vyao wa mahesabu wanachukua katika mfumo ambao unaeleka lakini kwa Serikali za Mitaa vitabu vyao vya hesabu vina shida sana kwani hesabu zao ziko nje ya mfumo.

"Nitoe mwito kwa Serikali kutoa mafunzo kwa wanaohusika na kuandaa vitabu vya hesabu katika halmashauri na Wilaya ili waweze kuandaa vitabu kwa kiwango cha kimataifa kutokana na mfumo ambao tunautumia katika ukaguzi.Wanaandaa figa ili kubalansisha tu hesabu ,ukiwaambia waandike tena wanaharibu kabisa,"amesema Kichere.

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG)Charles Kichere 

RC HAPI AWATAKA MAKANDARASI KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

$
0
0

 JOSEPH MPANGALA  -IRINGA

 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameitaka kampuni SINO HYDRO ya Inayotekeleza ujenzi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa Kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo kwa Viwango na wakati kutokana Pesa zote kukamilishwa kupewa.

Hapi ameyasema hayo alipotembelea Mradi wa ujenzi Huo Unaogharimu Shilingi Billion 41 na unatarajiwa Kukamilika June 23 mwaka 2022.

 “Wakandarasi wababaishaji natakanitume salam kwao hawatakuwa na nafasi kwenye Mkoa wetu wa Iringa na hawatakuwa na nafasi kwenye serikali hii habari za kuomba kuongezewa muda kuchelewesha miradi,kufanya miradi chini ya kiwango hayo hayatakuwa na nafasi tutakuwa wakali zaidi tulivyokuwa jana”Ally Hapi wakati akikagua Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa

Awali Ujenzi huo Ulisimama kutokana na Kuchelewa kwa Malipo ya Fidia za Mali za  wakazi wa kata ya Nduli ambapo Ujenzi Huo Unafanyika.







 

waziri jafo aupa miezi sita uongozi wa machinjio ya kisasa kizota jijini Dodoma kurekebisha changamoto zao

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa katika eneo la Kizota jiji Dodoma alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma. Kushoto ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula na mmiliki wa kiwanda hicho Wang Zuo Min.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa kutoka kwa Meneja wa machinjio hayo katika eneo la Kizota jiji Dodoma Chacha Mwita alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma.





Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma.  (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

=========  =======  ======  ======

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameupa uongozi wa machinjio ya kisasa ya Kizota jijini Dodoma miezi sita kurekebisha changamoto ya utiririshaji wa majitaka ovyo.

Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 8, 2021 alipofanya ziara ya kikazi katika machinjo hiyo kwa ajili ya kukagua udhibiti wa majitaka na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Alisema kuwa kila kiwanda lazima kiwe na mpango wa namna ya kuyatibu majitaka na kudhibiti utiririshaji wake kuepusha yasiende kwenye makazi yao watu na kusababisha madhara ya kiafya.

“Nafahamu machinjio hii ni miongoni mwa machinjo kubwa na ina soko kubwa katika nchi za Mashariki ya Kati wananunua nyama nami nimekuja hapa kujiridhisha kuhusu suala zima la utiririshaji wa majitaka,” alisema.

Alimuelekeza Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula kufuatilia kazi ya kuhakikisha machinjio hiyo inatengeneza mfumo wa kutibu majitaka haraka. 

MBUNGE KISWAGA ACHANGIA MILIONI 46 UJENZI WAMIUNDOMBINU YA SHULE NA MADARASA JIMBONI KWAKE

$
0
0

NA DENIS MLOWE, IRINGA

MBUNGE wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa , Jackson Kiswaga amechangia, 
shillingi millioni 46 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mfuko wa jimbo lengo la ujenzi wa miundo mbinu ya shule na ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata zote za Jimbo hilo.

Akizungumza kwenye ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari Lipuli , Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini Bashir Muhoja alisema kuwa mbunge huyo ametoa fedha hizo za mfuko wa jimbo ambazo zimepelekea kuunda bodi ambayo hadi sasa imekuwa ikiendelea na uboreshaji wa miundombinu mashuleni.

Alisema kuwa mfuko wa jimbo na ni kitu ambacho kimeanzishwa na bunge na fedha hizi zinavyokuja zinakuwa na kamati yake
ndani ya halmashauri na imepokea fedha za majimbo yote mawili Jimbo la Ismani na Kalenga na baada ya kupitia vipaumbele na mahitaji ya husika.

Muhoja alisema kuwa Mbunge Kiswaga alitazama mahitaji yanayotakiwa kurekebishwa mapema kwanza ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Tanangozi na shule nyingine ndipo walipoelekeza fedha hizo zitumike.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga alisema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo kwenye jamii na kutokana na fedha walizozipata ikapelekea kuunda kamati ambayo ilikuwa msaada kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na madarasa mashuleni.

Alisema kuwa wanaishukuru serikali ya mama Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo anaendelea na kufanya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuendelea kufikia lengo lililokusudiwa

 “Katika fedha ambazo huwa tunapatiwa mbunge huwa anaunda kamati na tukaangalia vipaumbele kulingana na mahitaji tuliyonayo kwa hiyo vipaumbele vyetu tulivyonavyo hasa kupunguza changamoto tuliyonayo kwa upande wa madawati lakini pia kuna ujenzi mwingine ambao unaendelea katika shule zetu pamoja na zahanati 

.Kiswaga alisema kuwa wananchi wawe na imani naye kwani bado yupo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Naye diwani wa kata ya Kalenga, Shakira Kiwanga alisema kuwa anashukuru kwa utekelezaji unaoendelea pamojana kuahidi ujenzi kuanza mara moja kwani vitendea kazi tayari vimeshatengwa 

Alisema kuwa viongozi watoe ushirikiano kwa kuwahamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo pamoja na kutambua kazi inayofanywa na mh.mbunge kwani kwa kipindi cha nyuma katika shule ya sekondari Isakalilo wanafunzi walikuwa wanaingia kwa awamu ambapo changamoto hiyo imetatuliwa kutokana na fedha kiasi Cha sh milioni .12 kusaidia kuboresha eneo hilo hasa kwenye madarasa.

Mbunge Jackson Kiswaga amafanya utekelezaji huo kwa kutoa madawati 325 ambapo kwa shule ya lipuli ametoa madawati 20 pamoja na saruji itakayosaidia katika uboreshaji wa madarasa.
 Mbunge wa Jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga akimkabidhi mkuu wa Shule ya sekondari Lipuli,Peter Mbata saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa,Bashir Muhoja kulia akizungumza na mbunge wa Jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga

Jackson Kiswaga akizungumza
 


 

SHERIA ZA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA TAMASHA LA URITHI HAIKUFUATWA -RIPOTI YA CAG"

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana imebaini mapungufu makubwa katika uanzishwaji na uendeshaji wa Tamasha la Urithi Sh Bilioni 2.09.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo jijini Dodoma mbele y wandishi wa habari baada ya kuiwasilisha Bungeni, CAG Charles Kichere amesema amesema katika ukaguzi wake wa Tamasha la Urithi lililokua na lengo la kukuza utalii na Urithi wa kitaifa aliambiwa kamati iliyoundwa iliidhinisha bajeti ya Sh Bilioni 1.60 kwa ajili ya utekelezaji wa hafla hiyo lakini bajeti hiyo haikuwasilishwa kwa ajili ya ukaguzi.

CAG Kichere amesema ukaguzi wake umebaini hakukua na mpango wa utekelezaji wa tamasha hilo hivyo kutokana na kukosekana kwa mpango huo alibaini Wizara ya Maliasili na Utalii iliomba wakala zake nne kuchangia jumla ya Sh Bilioni Moja ambazo hazikua kwenye bajeti ili kuweza kufanikisha tamasha hilo.

Amesema ili kuongezea bajeti hiyo Wizara ya Maliasili na Utalii ilichangia Sh Milioni 299, Mfuko wa Tozo wa Maendeleo ulichangia Sh Milioni 270 ambapo jumla ya Sh Bilioni 1.57 zilipatikana ili kufanikisha utekelezaji wa tamasha hilo ambapo fedha zote hazikua kwenye bajeti ya Wizara na Taasisi husika.

" Wakati wa utekelezaji nilibaini Kituo cha Televisheni cha Clouds na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) walilipwa jumla ya Sh Milioni 629 na Sh Milioni 204 mtawalia kwa ajili ya kurusha matangazo ya tamasha la urithi hata hivyo hakukua na risiti za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha kupokelewa kwa malipo hayo.

Pia kodi ya zuio ya Sh Milioni 31 na Sh Milioni 10 kutoka Clouds na TBC haikukatwa katika malipo yaliyofanyika," Amesema CAG Kichere.

Amesema amebaini kuwa jumla ya Sh Milioni 487 zilipelekwa kwenye Tamasha la Urithi lakini hakukua na nyaraka zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi ili kuthibitisha matumizi hayo.

" Nilibaini matumizi ya Sh Milioni 585.5 yaliyolipwa na Mhasibu wa Mfuko wa Tozo ya Maendeleo ya Utalii bila ya kuwa na nyaraka toshelezi, hivyo nilishindwa kuthibitisha uhalali na usahihi wa malipo hayo.

Aidha nilibaini Wizara ya Maliasili na Utalii ililipa Sh Milioni 140 kwa kampuni ya Wasafi kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Iringa na Dodoma lakini hakukua na mkataba wowote uliosainiwa kati ya kampuni hiyo na wizara hivyo kushindwa kuhakiki wigo wa kazi pamoja na huduma zilizotolewa na kampuni hiyo," Amesema Kichere.

Amesema kulikua na maagizo ya Waziri  wa Maliasili na Utalii (Hamis Kigwangala) yakielekeza malipo kwa kampuni ya wasafi, katika mahojiano na waziri huyo alikiri kuwa kampuni ya wasafi iliomba zabuni ya kutangaza tamasha hilo kwenye mikoa iliyotajwa na kutoa maagizo ya kufanya malipo hayo.

CAG Kichere amesema kuwa kiasi cha Sh Milioni 140 kikicholipwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kampuni ya Wasafi kufuatia maelekezo ya Waziri wake hakiendani na sheria za manunuzi ya fedha za umma.


 

Viewing all 120391 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>