Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120471 articles
Browse latest View live

BAADA YA SIKU 21 ZA MAOMBOLEZO, WABUNGE CHADEMA WASEMA WANA IMANI NA RAIS SAMIA

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

IKIWA leo ni Siku ya mwisho ya maombolezo ya siku 21 ya kifo cha aliyekua Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli wabunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamewataka wanasiasa vijana kuepuka kuwa na ndimi mbili huku wakimtakia heri Rais Mama Samia.

Wakizungumza nje ya Bunge jijini Dodoma, wabunge hao Hawa Mwaifunga na Nusrat Hanje wamesema wanaamini  Rais Mama Samia ana uwezo wa kuiongoza nchi vizuri na kufanya vizuri kwani tayari alikuepo serikalini.

Akizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa ambao wameanza kutoa kauli za tofauti na zile walizokua wakizitoa kipindi cha Dk Magufuli wakitolea mfano suala la Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamis Kigwangala kuhusu msimamo wake wa kujifukiza.

" Ni mshangao mkubwa kuona hata siku 21 za maombolezo hazijaisha watu waliokua wanamuunga mkono Dk Magufuli kuhusu kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa kujifukiza.

Kwa sisi wanasiasa vijana tunapaswa tuchunge ndimi zetu kwa sababu watanzania waliotuchagua wametuamini sana kugeuka misimamo yetu ni kuwaonesha kwamba hatufai kupewa uongozi," Amesema Mwaifunga.

Amesema ana imani kubwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuiongoza Tanzania na kwamba anaamini atafanya kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania kwani anaifahamu Serikali.

Nae Nusrat Hanje amesema siku 21 za maombolezo zimeisha leo hivyo anaamini watanzania wamezitumia katika kuyaenzi mazuri yaliyofanywa na Dk Magufuli kwamba ana imani kubwa ya Rais Samia kufanya kazi nzuri ya kuiletea Nchi maendeleo.

" Hatuna shaka na Mama Samia katika kuwaendeleza yale yote ambayo aliyaanzisha Magufuli lakini anaweza kufanya makubwa zaidi kwani amekua sehemu ya Serikali kwa miaka sita," Amesema Nusrat Hanje.

Amewataka wanasiasa vijana waliobadilika misimamo yao ya Corona kujifunza kuwa na msimamo mmoja kwani kubadilika huko kunawavunjia heshima na kuwaondolea imani yao kwa Wananchi.


 


MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AREJEA DODOMA KUTOKA DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akitokea Jijini Dar es salaam alikohudhuria Hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu wa Wizara mbalimbali pamoja na Baadhi ya Makamishna wa Taasisi za Serikali, leo April 06,2021  Ikulu Jijini Dar es salaam.



 

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA PAMOJA NA NAIBU WAKE WAMEWASILI OFISI NDOGO YA WIZARA DSM

$
0
0

 

 

***********************************

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Doto M. James na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, Leo tar. 6 Aprili, 2021 wamewasili katika ofisi ndogo za Wizara Waterfront jijini Dar es salaam punde baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Viongozi hawa wamepokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof, Kitila Mkumbo (Mb) ambapo wamepata nafasi ya kutambulishwa kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Katika Kikao hicho, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amewakaribisha katika Wizara ya Viwanda na Biashara huku akihaidi kufanya nao kazi kama timu moja katika kufikia malengo ya kuifanya nchi kuwa ya Viwanda ifikapo 2025.

Kwa upande wao Makatibu hao wamekubaliana kushirikiana na mawaziri ili kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais ya Kukuza sekta ya Viwanda na Biashara nchini hasa katika kukuza pato la Taifa na Ajira kwa watanzania kwa kutunga sera na sheria ambazo ni rafiki kwa wawekezaji kuanzisha Viwanda vinavyochakata malighafi za ndani.

Rais Samia Suluhu Hassan awasili Zanzibar

$
0
0

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 06 Aprili 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 06 Aprili 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuwasili Zanzibar leo tarehe 06 Aprili 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuwasili Zanzibar leo tarehe 06 Aprili 2021.  PICHA NA IKULU


 

MBUNGE KINGU AWATAKA WATANZANIA KUMPA USHIRIKIANO RAIS SAMIA

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema ana imani kubwa kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia watanzania kwani ameonesha uwezo wa uongozi toka alivyoapishwa kuwa Rais na hata alivyokua Makamu wa Rais.

Kingu ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokua akitoa maoni yake ya uongozi wa Mama Samia ambapo amewataka watanzania kumuamini kwani ana uwezo mkubwa wa uongozi.

Amesema toka kuingia kwa Mama Samia tayari yeye kwenye Jimbo lake ameshaletewa kiasi cha Sh Bilioni Tatu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo jambo linaloonesha jinsi gani amepanga kuwatumikia watanzania kwa nguvu na kasi zaidi.

" Sina shaka na uwezo wa Mama amekuepo Serikali kwa muda mrefu na tunapoona mafanikio tuliyonayo kwa miaka mitano hii basi Mama amechangia kwa kiasi kikubwa kwani nae alikua sehemu ya uongozi, niwatoe hofu watanzania kwamba tuna Rais hodari na mwenye uwezo," Amesema Samia Suluhu.

Akizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa kubadilisha msimamo wao wa Corona, Kingu amesema ni kweli ugonjwa huo upo lakini ni ukweli usio na shaka kwamba njia ya kujifukiza imesaidia sana watanzania wengi.

" Hatuwezi kukataa kwamba Corona ipo lakini njia ya kujifukiza ilitusaidia wengi, nitoe rai kwa sisi vijana kuwa na misimamo na kauli zetu ambazo tunakua tunazitoa ili kuendelea kuaminika kwa wananchi, " Amesema Kingu.


 

VIBALI VYA UKUSANYAJI, USAFIRISHAJI NA UHIFADHI WA CHUMA CHAKAVU VITOLEWE KWA MIAKA MITATU- WAZIRI JAFO

$
0
0

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo, akitoa maelekezo kwa msimamizi wa kiwanda cha Metal Steel kilichopo Kiwalani Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Dkt.Muhandisi Samuel Gwamaka (katikati) akizungumza jambo na Msimamizi wa kiwanda cha Master Steel  ltd kilichopo Chang’ombe Jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili kiwandani hapo.

Bw. Ramadhani Kalenge Afisa Uhusiano katika kiwanda cha Master Steel Ltd kilichopo Chang'ombe Jijijini Dar es Salaam akimuonyesha Waziri Mhe. Jafo (katikati) vyuma mbalimbali katika kiwanda hicho. Akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Muhandisi Samuel Gwamaka (wa kwanza  kushoto) na Meneja wa Kanda ya Mashariki Kusini Taimur Kisiwa (wa pili kulia)

 

*************************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Suleiman Jafo ametoa agizo kuwa vibali vyote vya ukusanyaji, usafirishaji na uhifadhi wa vyuma chakavu vitolewe kwa muda wa miaka mitatu na sio kwa mwaka mmoja kama ilivyokua awali ili kuepusha usumbufu kwa Wawekezaji. Ametoa agizo hilo alipokuwa katika ukaguzi kwenye  kiwanda cha Metro  steel Ltd kinachozalisha nondo kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Aidha akiwa katika kiwanda hicho pia Mh. Jafo ametoa onyo kwa wenye viwanda kwa kutokufuata sheria, taratibu na kanuni za mazingira. Pia alitoa rai kwa wenye viwanda kwa kulinda miundombinu ya Nchi na  kutokufanya uharibifu katika kupata vyuma chakavu.

Ameendelea kusema kiwanda hicho cha Metro Steel Ltd  kinalalamikiwa na wananchi kuwa muda wa usiku kinatoa moshi na kupelekea kero kwa wakazi walio karibu na kiwanda.

“Natoa onyo kali kwa kiwanda hiki leo sijaja kupiga faini ningeweza kumwambia Mkurugenzi Mkuu wa NEMC awapige faini ila ninawapa onyo  mjirekebishe katika hili”. Alisema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.  Samuel Gwamaka amesema kiwanda cha Metro steel kina kibali cha usafirishaji lakini kibali hakina tarehe wala kiasi cha chuma chakavu kilichosafirishwa na kushushwa kiwandani. “Utaratibu uliopo lazima kibali kiandikwe tarehe na kiasi cha chuma chakavu kinachosafirishwa na vinginevyo kutoandikwa tarehe kibali kimoja kinaweza kutumika bila kikomo hivyo kuwa na kibali kisichoandikwa tarehe ni makosa”. Dkt. Gwamaka

Katika ziara hiyo pia Waziri Jafo alifanya ziara alitembelea kiwanda cha Steel Masters kukagua uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutoka katika chuma  chakavu. Akiwa katika kiwanda hicho pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa laHifadhi na  Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Samwel Gwamaka, walikagua lori lenye usajili T620 AQW likiwa na bidhaa mbalimbali za chuma likingojea kushusha mzigo ambapo walijiridhisha kuwa lori hilo linakidhi mahitaji yote ya kisheria yanayotakiwa.

Waziri Jafo amefanya ziara katika viwanda viwili katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kukagua masuala ya mazingira katika viwanda hivyo.

WAZIRI NDAKI AMTUMBUA OFISA MSIMAMIZI WA MNADA IGUNGA

$
0
0


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amemsimamisha kazi Ofisa anayesimamia Mnada wa Mifugo wa Upili ulioko Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Bw. Juma Athuman kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mapato.

Mhe. Ndaki amechukua hatua hiyo juzi alipotembelea mnada huo ili kuangalia ufanisi wake ambapo alibaini kutokuwepo nyaraka za kumbukumbu ya mifugo inayoingia na kutoka katika mnada huo kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Alisema kukosekana kwa kumbukumbu hizo kumetoa mwanya wa upotevu wa mapato hivyo kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha, jambo hilo halikubaliki hata kidogo.

“Naagiza Uongozi wa Halmashauri kumwondoa kazini mara moja Ofisa Afya ya Mifugo Mohamed Kifamba na askari polisi wote waliokuwa wakisimamia mnada huo nao waondolewe mara moja, OCD shughulikia hilo” alisema Mhe. Ndaki.

Licha ya kusimamishwa kazi watuhumiwa hao Waziri Ndaki aliagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma hizo za ubadhirifu wa mapato ya serikali kwa kipindi chote cha miaka 4 ili sheria ichukue mkondo wake.

“Kila siku ya mnada fedha nyingi zinakusanywa lakini hazionekani, zinaingia mifukoni mwa watu, hili halikubaliki na serikali haiwezi kufumbia macho vitendo vya namna hiyo kwa kuwa vinaikosesha mapato mengi sana,” aliongeza Waziri.

Aidha, alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel kupeleka wataalamu wilayani humo ili kuchunguza mapato ya mnada huo yaliyopotea katika kipindi chote hicho ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa ikiwemo wahusika kulipa fedha hizo.

Pia waziri huyo alichukua hatua ya kumkaimisha msimamizi wa mnada huo Bw. Haidari Mwinyihija nafasi usimamizi wa mnada, wakati utaratibu wa kumpata Ofisa mwingine atakayesimamia mnada huo ukiendelea kufanyika.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia) akikagua vitabu vya kumbukumbu kikiwemo cha idadi ya mifugo inayoingia na kutoka katika Mnada wa Upili wa Igunga unaosimamiwa na wizara hiyo.


TOGETHER WE CAN: VODAFONE CELEBRATES COLLABORATIVE POWER OF TECHNOLOGY AND HUMAN AMBITION WITH NEW BRAND POSITION

$
0
0

 Vodafone celebrates what the human spirit can achieve when combined with technology in a multi-market update to its brand position, that was launched last week. The company will introduce a new Vodafone tagline - ‘Together We Can’ – to accompany its new position, along with a 12-month programme of television, print and digital advertising demonstrating Vodafone’s profound belief that the partnership between technology and society can build a better future.

“Together We Can’ places the emphasis on ‘we’, and how collaboration between the human spirit and innovation can achieve great things,” says Alex Froment-Curtil, Group Chief Commercial Officer, Vodafone. “The experience of these last 12 months during the COVID-19 crisis has demonstrated more than ever the critical role of connectivity and technology to keeping society, businesses and governments connected. As a purpose-led company, Vodafone fundamentally believes that technology can improve lives, and this new positioning builds further momentum to our purpose to connect for a better future and enable an inclusive, sustainable digital society.”

Vodafone’s new brand position is inspired by consumer research carried out by the company which revealed that the role of technology is profoundly transforming in people’s lives. Findings identified how technology has evolved from something that simply excites people on a personal level, to playing a more meaningful part in the world at large, in particular, in making a difference on issues such as sustainability and societal development. 


For example, over the last year sustainability has increased in importance and in terms of trust requirements for consumers in their brand preferences, with nearly eight in 10 people indicating that it was key for them. Over the coming months, Vodafone’s Together We Can message will be further set in motion by the company’s deployment of gigabit networks enhancing connectivity to people and communities alike, embracing communications technology to reduce carbon emissions, and supporting education, health and wellbeing to create a more inclusive and sustainable society.

The Together We Can campaign commenced on 1nd April 2020, with a new 60-second commercial, The Irrepressible Girl, featuring a young girl posing questions about the world around her, on the role technology can play in curing disease, fighting climate change and addressing digital inclusion. The commercial, along with a series of stories that will appear in print and digital advertising, will shine a spotlight on Vodafone’s critical role to help answer these questions, from the rollout of 5G, Gigabit networks and connectivity to the most remote parts of the world.

The campaign will mark the introduction of a refreshed brand identity with Vodafone’s iconic Speechmark logo and red colour scheme. The programme will run in 30 markets, including Germany, Spain, the UK, Italy, Romania, Greece, Ireland, Hungary, Albania, the Netherlands (via Vodafone-Ziggo), Portugal, Czech Republic, Turkey, Australia, South Africa, Ghana, Democratic Republic of the Congo, Tanzania, Lesotho and Mozambique. Vodafone’s partner markets, including Qatar and New Zealand, will also run the campaign.

#LIVE: RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA HAYATI ABEID AMAN KARUME

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO APRIL 7,2021

TANZIA

SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA KUWAINUA WAKULIMA WA KOROSHO KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA FEDHA

$
0
0


Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuwainua wakulima wa zao la Korosho nchini, Serikali imekutana na Taasisi za Kibenki na kukubaliana nazo kufungua akaunti ya pamoja kwa ajili ya kuwasaidia wakulima hao kuweza kufanya kilimo chao vizuri.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na wawakilishi wa mabenki hayo ambapo lengo ni kuwawezesha pia wakulima kupata pembejeo kwa wakati.

Akizungumza na wandishi wa habari, Naibu Waziri Bashe amesema amefanya kikao na Benki ya Equity ambayo imeonesha wazi nia yake ya kuwainua wakulima huku akiongeza kuwa Benki zingine ambazo zimeonesha nia hiyo na kukubaliana ni pamoja na Benki ya NMB na CRDB.

" Kama mnavyofahamu kwa muda mrefu tumekua tukiangalia njia ambazo zitawawezesha wakulima wetu kupata pembejeo kwa wakati na kwa gharama nafuu, kwa muda mrefu mazao haya ya kimkakati kama Korosho mkulima anaenda Benki anakopa fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo lakini anaenda Benki anakopa kwa riba iliyopo kwa wakati huo.

Sasa sisi kama Wizara tulikubaliana tuje na mkakati wa kumpunguzia gharama mkulima kwenye sekta ya kilimo hivyo tumeona ili kuondoa changamoto hiyo tutumie chama kimoja cha ushirika katika kushughulika nazo," Amesema Bashe.

Amesema baada ya kuangalia mapato yaliyopo wameangalia uhitaji wa wakulima wa Korosho ambapo kama ni Pembejeo hivyo kuamua mahitaji yote ya sekta yachukuliwe pamoja na kutumia chama kimoja cha ushirika kutangaza zabuni na ili mzabuni apeleke dawa ni lazima chama kikakope fedha Benki na kitatakiwa kulipa riba ya asilimia 16 hadi 20.

Amesema au kama siyo chama kukopa basi mkulima mmoja mmoja akakope Benki  hivyo baada ya mkataba huo wazabuni watapeleka mikataba benki LC kutoka taasisi za fedha ambazo gharama yake ni asilimia mbili ya riba.

" Kwahiyo gharama kwenye pamba imekua ni asilimia mbili na mabenki yameshatoa zaidi ya Bilioni 36 lakini pia tunafanya hivyo hivyo kwenye korosho mwaka huu ambapo wakulima watagaiwa dawa bure na pembejeo zote bure za korosho ambapo sasa watarudisha gharama hizo kutokana na mjengeko wa bei  na tayari washakaa na wanunuzi wa korosho na wamekubaliana watachangia kweye mfuko huo.

Ukitazama kwa miaka mitatu iliyopita zao liliendelea kushuka kwa sababu mkulima hakua na uwezo na alikua hakopesheki hivyo tunachokifanya sisi kama Wizara ni kusimamia kufunguliwa kwa Escrow akaunti ambayo itakaa katika benki ambazo tumekubaliana  ,tunashukurubenki tatu nilizozitaja tushakubaliana nazo na mchakato unaofanywa na wizara hivi sasa ni kufungua akaunti hizo ambazo zitasimamia na Chama cha Ushirika na Bodi ya Korosho, " Amesema Bashe.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na wawakilishi wa taasisi za fedha ambao amefanya nao kikao ofisini kwake jijini Dodoma cha kuangalia namna ya kuwainua wakulima wa zao la korosho nchini.

Wawakilishi wa Taasisi za Fedha na watendaji wa wizara ya kilimo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye kikao chao cha kujadili namna ya kuwainua wakulima wa zao la korosho nchini.
 

DC ARUMERU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAENENDELEO UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA,VYOO SHULE ZA MSINGI

$
0
0

 Na Jusline Marco-Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Ndg.Jerry Muro amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo katika shule za msingi wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Muro alisema kuwa kupitia kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya yake kwaajili ya shule za sekondari waliweza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa asilimia zaidi ya 90 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka huu.

"Zoezi hili tumelielekeza maalumu kwenye shule za msingi na kupitia kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa tumepokea watoto wote ambao wanapaswa kupokewa katika shule zetu za sekondari".Alisema Muro

Aidha alieleza kuwa katika zoezi la upokeaji wa wanafunzi hao kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wanafunzi kutoripoti katika shule walizochaguliwa kutokana na wazazi wao kuwa miongoni mwa jamii ya kuhamahama kutafuta malisho ya mifugo yao.

"Tulichunguza kwanini watoto hao hawajaripoti shuleni,tukagundua wazazi wao ni jamii ya wafugaji ambao wanahama na mifugo kutafuta malisho ambapo tulibaini kuwa wamehamia katika upande wa Longido."Alieleza Muro

Aliongeza kuwa zoezi hilo la ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari wilayani humo limemalizia ambapo sasa hivi wapo katika zoezi la ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi wilayani humo.

Vilevile Muro alitolea ufafanuzi wa picha ya choo cha shule ya Olimringaringa ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa mtandao wa jamii forum siyo picha halisi ya choo cha shule hilo ambapo alisema kuwa wanatambua changamoto ya matundu ya choo hayatoshi kulingana na idadi ya wanafunzi ambao hupokelewa kwenye shule za msingi na katika maeneo mengine.

"Hakuna shule kwenye wilaya ya Arumeru yenye choo kama kile,Shule ya Olimringaringa ina choo chenye matundu 18 kwa 16 hivyo katika awamu hii tunachofanya kwenye wilaya ya Arumeru ni ujenzi wa vyoo na madarasa mengine kwenye shule za msingi.Alisema Muro

Vilevile aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 9,kampeni inayoendelea niya ujenzi wa vyumba vya madarasa 50 na matundu ya vyoo 120 ambapo kuanzia mwezi huu wa 4 hadi mwezi wa 12 mwishoni ujenzi huo utakuwa umekamilika ambapo ujenzi huo umeanza katika shule za Olimringaringa,Olosiva,Mringa,Oldonyowasi ambapo aliweza kufanya ziara ya kuhimiza kamati za shule kwa kushirikiana na wazazi kuweza kujenga madarasa na matundu hayo ya vyoo.

Sambamba na hayo DC Muro alieleza kuwa katika Wilaya yake kuna zoezi endelevu ambalo limefanyika takribani wiki mbili la kuthibiti na kukamata mtandao wa wezi wa mifugo ikiwemo ng'ombe na mbuzi.

"Tulifanya zoezi hili hasa kwenye kipindi cha sherehe za Pasaka tukiwa tunalenga kuhakikisha katika kipindi cha sherehe ya sikukuu ya Pasaka kunakuwa hakuna mwananchi anayekumbwa na adha ya wizi wa ng'ombe,mbuzi,kuku au bata."Alisema Muro

"Imezoeleka katika baadhi ya maeneo nyakati hizi za majira ya sikukuu ndiyo nyakati ambazo watu wanaendesha mtandao wa wizi wa mifugo ya watu."Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya

Alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja kumekuwa na wizi wa ng'ombe takribani 31 katika maeneo kadhaa huku maeneo sugu yaliyokithiri kwa wizi huo yakiwa ni maeneo ya Kata ya Kikwe,Akheri pamoja na Mulala ambapo baada ya kupokea taarifa za wizi huo walihakikisha wanaendesha operesheni kwa kushirikiana na wananchi kutafuta taarifa zitakazo wasaidia kuwakamata wezi hao na wahusika.

Aliongeza kuwa operesheni nyingine amabayo inaendelea ni utekelezaji wa mtandao huo wa wizi wa ng'ombe ambapo wamefanikiwa katika Tarafa ya Mukulat,Ngaramtoni,Oldonyowasi,Oldonyosambu na walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9 ambao baadhi walikiri kuiba mbuzi na ng'ombe na kuwakabidhi katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

Kutokanana uchinjaji holela unaofanywa na wezi wa mifugo hiyo ipo sheria ya mazingira inayoelekeza kuwepo kwa  maeneo maalum kwa ajili ya machinjio ambayo kimsingi ndiyo yanayotakiwa kufanyika shughuli za uchinjaji huku sheria ya utunzaji mazingira ikielekeza uchafu unaotokana na shughuli za uchinjaji uwe wa namna gani.

Pamoja na hayo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazo wasaidia kuwaibua wezi hao ili kuweza kudhibiti na kutokomeza mtandao huo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha Ndg.Jery Muro akizungumza na wananchi katika Opareshi ya kukamata na kudhibiti mtandao wa wezi hao wa mifugo.

RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA MAALUM YA KUMUOMBEA HAYATI RAIS ABEID AMANI KARUME LEO ZANZIBAR

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Karume Day.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya Dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika siku ya Kumbukumbu ya Karume (Karume Day) iliyofanyika leo tarehe 07 April 2021 katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.  

Mhe Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi  CCM Kisiwandui  mahali alipozikwa  Hayati Rais   Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea  katika siku ya kumbukumbu yake.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mhe Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi  CCM Kisiwandui  mahali alipozikwa  Hayati  Rais Abeid  Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar  ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea  katika siku ya kumbukumbu yake.

Mhe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki  Dua  maalumu ya kumuombea Hayati rais   Abeid Amani  Karume Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar   katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi  CCM Kisiwandui  mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .

Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na  Mjane wa Hayati Rais Abeid Aman Karume  Mama Fatuma Karume , wakati alipowasili kwenye   Dua  maalumu ya kumuombea Hayati Rais   Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar   katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi  CCM Kisiwandui  mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Mke wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanziba Dkt. Hussein  Ali Mwinyi , Mama Mariam Mwinyi,  na Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said wakishiriki  Dua  maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid  Amani Karume,Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar   katika siku ya kumbukumbu yake, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi  CCM Kisiwandui  mahali alipozikwa,  leo April 7, 2021 .

PICHA NA IKULU

DIWANI WA KATA YA MBAGALA KUU AFIA GESTI AKIDAIWA KUWA NA MWANAMKE

$
0
0

Diwani  Kata ya Mbagala Kuu,  Shabani Othman Abubakari enzi za uhai wake.

Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu,  Shabani Othman Abubakari, akizungumza na walimu wote wa shule za msingi na sekondari za kata hiyo enzi za uhai wake.


Na Dotto Mwaibale 

DIWANI wa Kata ya Mbagala Kuu Shabani Othman Abubakari (CCM) amefariki dunia katika moja ya nyumba ya kulala wageni iliyoyopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam alipokuwa na mwanamke anayedaiwa ni  mchepuko wake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtimika na kuwa mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Tanita yaliyopo eneo la Kibonde Maji.

Mmoja wa wahudumu nyumba hiyo ya kulala wageni  (jina lake linahifadhiwa) alisema diwani huyo alifika akiwa na gari lake wakiwa na msichana huyo usiku wa kuamkia juzi na kuchukua moja ya chumba katika nyumba hiyo.

Alisema asubuhi baada ya kuamka wakati akifanya usafi ndipo alipoukuta ufunguo wa chumba alichokuwa amekichukua diwani huyo na msichana huyo ukiwa umetupwa chini ambapo alishituka na kwenda katika chumba hicho na kukuta kikiwa kimefungwa na kilipofunguliwa walimkuta diwani huyo akiwa amefariki lakini yule msichana waliyekuwa naye hayupo.

Muhudumu huyo alisema baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na baada ya kuwahoji  waliuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada ya kupigiwa simu yake mara kadhaa ikawa inaita bila ya kupokelewa.


MDAU WA MAENDELEO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUANZA VYEMA

$
0
0

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv

Uongozi shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY umempongeza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama,Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuanza vizuri kazi yake na kukubalika na makundi yote katika jamii ya Watanzania.

Pongezi hizo zimetolewa na muwekezaji wa shule hizo ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Mwl.Ezekiel Eliphas Meivule Mollel ambapo alimuahidi Rais Samia kumpa ushirikiano wa asilimia zote katika sekta ya elimu.

Aidha pia alisema kasi aliyoingia nayo Rais Samia ni nzuri na anauhakika kabisa itaweza kuivusha nchi ya Tanzania , na kuwafikisha watanzania mbali zaidi katika swala la Maendeleo ukizingatia nchi yetu ina vitega uchumi vingi.

Aliongeza kuwa wataendelea kumuweka katika maombi yeye na viongozi wenzake wa serikali ili waweze kuyatekeleza yale yote ambayo amekusudia kuwafanyia watanzania ikiwemo kumaliza miradi yote mikubwa iliyoachwa na hayati John Magufuli pamoja na kuwaletea maendeleo ya nchi pamoja na mtu mmoja mmoja.

Alisema wanaona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi pamoja na kusaidia katika kuleta Maendeleo ya nchi .

Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuongeza ajira kwa walimu 6000 ambao wapo mtaani na kusema kuwa hii itadaidia kuboresha elimu yetu iendelee kuwa bora zaidi,pia alipongeza mikakati mipya aliyoitagaza ikiwemo kuhamasisha uchimbaji wa madini

Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza wakafanya mambo yakaenda sawa.

Alibainisha kuwa jamii yenye ufahamu wa kutosha juu ya wajibu wake katika utawala bora, demokrasia na haki za binadamu, ni jamii inayowajibika na inayoshiriki  kikamilifu, na kwa hiari katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa taifa. 





Mwekezaji wa shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA pamoja na BLESSINGS DAY zilizopo mwanza ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Ezekiel Mollel alipokuwa akizungumza na Michuzi TV

SALAAM ZA SHUKRANI KWA WATEJA KWA KUTOA PONGEZI, MAONI NA KERO ZA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

$
0
0

Ndugu Wananchi, Awali ya yote nachukua fursa hii kuwatakia watumiaji wote wa huduma za afya nchini Tanzania Heri ya Siku ya kumbukizi ya Hayati Abeid Amani Karume leo tarehe 7/04/2021. Tumkumbuke kwa ushujaa na uzalendo wake daima.

Aidha, napenda kutoa Shukrani kwa Wananchi wote ambao wamekuwa wakiwasilisha Pongezi, Maoni na Kero zao kupitia mifumo mbalimbali ya mawasiliano ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikiwemo kwa barua, mitandao yetu ya kijamii, simu na ujumbe mfupi kupitia namba 199. Nikiri kuwa taarifa hizo zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika kutambua maeneo yanayofanya vizuri na yale yenye changamoto.

Ndugu Wananchi, Vilevile, nawashukuru maelfu ya Wananchi ambao pale wanapoona hawakupata msaada kwenye ngazi ya Kituo, Halmashauri, Mkoa au Wizara kupitia namba husika zilizotangazwa wamekuwa wakizingatia kunitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu mimi Waziri ya 0734124191 kama nilivyoitangaza Disemba 19, 2020.

Ndugu Wananchi, Napenda kuwakumbusha kuwa, kwa pongezi na kero za huduma za afya kamwe msikose mahali pa kusemea bali muendelee kutumia mifumo ya mawasiliano ya haraka huku mkizingatia maelekezo yaliyotolewa. Mahsusi kwa simu yangu Waziri wa Afya ya 0734124191 mawasiliano haya ni kwa ujumbe mfupi tu.

Nawahakikishia kuendelea kujibu na nikiona inafaa nitapiga simu au kutoa maelekezo kwa wasaidizi wangu wafuatilie na kusimamia jambo hilo na kunipa mrejesho.

Kwenu watumishi wataalamu wa afya, Natoa pongezi kwa wale wote ambao wamekuwa wakijituma kwa bidii kuwahudumia wateja wanaohitaji huduma za afya. Hakika kupitia maoni ya wateja tumeendelea kuwatambua watumishi wengi wenye moyo wa uzalendo na upendo katika kutimiza wajibu wao. Wale wenye changamoto nao tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

Ndugu Wananchi, Natoa Shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu na tuendelee kushirikiana daima.

Dkt. Dorothy Gwajima.
WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
07/04/2021.
Simu. 0734124191 (tuma ujumbe mfupi tu)

Waziri Jafo awaasa vijana kuuenzi Muungano

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amewaasa vijana kuendelea kuuenzi Muungano kwa kudumisha amani nchini.

Jafo ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza mara baada ya kuhudhuria Dua maalumu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Hayati Sheikh Abeid Aman Karume iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kisiwandui.

Amesema kuwa vijana wa sasa wanapaswa kuona fahari ya Muungano na kuyaenzi yale yaliyoachwa na Hayati Karume ambaye ameacha alama Zanzibar hususan katika ujenzi wa miundombinu na kuwajali wananchi.

Aliongeza kuwa kiongozi huyo alikuwa na maono makubwa kwa wananchi wake na kuweza kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine hapa nchini na hata Afrika kwa ujumla.

“Tukumbuke kwamba Hayati Karume na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walifanya kazi kubwa ya kuasisi Muungano na leo hii tunajivunia kuwa Watanzania hivyo kwetu sisi ni faraja hatuna nchi nyingine isipokuwa ni Tanzania,” alisema.

Aidha Waziri Jafo alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa uongozi wake ambao umewafanya wananchi kuwa na Imani kubwa kwake.

Alitoa rai kwa Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kwa yale anayoendelea kuyatekeleza na kuwa ameonesha weledi katika utendaji wake ambao unaakisi aliyofanya Hayati Karume hasa katika ujenzi wa makazi bora kwa wananchi.

Aprili 7 ya kila mwaka ni kumbukumbu ya kifo cha Karume ambaye alifariki mwaka 1972 na Dua maalumu ya kumuombea imefanyika katika Ofisi za CCM Kisiwandui, Zanzibar ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wameshiriki.

MAKAMPUNI 49 TANZANIA YAIDHINISHWA NA MAMLAKA YA FORODHA CHINA KUUZA MAHARAGE YA SOYA

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. HUSSEIN ALI MWINYI AELEKEA NCHINI MSUMBIJI KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA SADC AKIMUWAKILISHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.SAMIA SULUHU HASSAN

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka Zanzibar kuelekea Nchini Msumbiji kumuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC unaofanyika Jijini Maputo Msumbiji (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana Meya wa Jiji la Zanzibar Mhe. Mahmoud Mohammed Mussa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC, kumuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Idrisa Mustafa Kitwana, akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, unaofanyeka Jijini Maputo Msumbuji.(Picha na Ikulu)

Viewing all 120471 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>