Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119390 articles
Browse latest View live

Njombe:Wazidi kulia na ugumu wa biashara

$
0
0
Na Amiri Kilagalila, Njombe

Hali ya biashara kwa wakazi wa mji wa Njombe imetajwa kuwa kwenye mkwamo kutokana na Ongezeko la kodi hasa katika ukadiriaji wa kodi hatua inayowalazimu baadhi ya wafanyabiashara kufunga milango yao.

Katika mkutano wa kwanza mwaka 2020 wa jumuiya ya wafanyabiashara mjini Njombe,baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Agnetha Sanga na Nathaniel mgani wanakiri kuwa hali ya biashara kwa sasa imekuwa ngumu na mauzo kupungua kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali hiyo serikali inaombwa kuangalia namna ya kuwapunguzia mlundikano wa kodi kwani hakuwezi kuwa na makusanyo makubwa ya mapato ilihali biashara hakuna.

"Kwanza tozo kwa kweli imekuwa ni kubwa kuliko vipato,kwa hiyo utakuta ni wafanyabiashara wachache sana leo watakwambia nimeuza na wengine wameamua kufunga milango kwasababu biashara hamna,leo sio sawa na miaka iliyopita angalau tulikuwa tunasema tunafanya kazi"aliseama mmoja wa wafanyabiashara

Eliud Mgeni[Pangamawe] ni mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe anasema bado wafanyabaishara wanayo nafasi ya kujitoa walipo kwa kuongeza usimamiaji wa biashara zao badala ya kukata tamaa.

"Kwa mwaka huu tunaomba TRA kuwa na sababu ya kuhakikisha wafanyabiashara wote wanalipa kodi kwa hiali zinazolipika bila ya kuwa na maumivu,mapato ya kodi ya serikali tunalipa faida inayotokana na biashara kwa hiyo kama hujapata faida unaenda kulipa nini"alisema Pangamawe

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe Musibu Shaaban anasema makadirio ya kodi yanafanyika kulingana na mauzo na hivyo ili kuondoa malalamiko hayo ndiyo maana wanaendelea kusisitiza kutumia mashine za EFD.

"sisi kama TRA huwa tunakadiria kulingana na mauzo ya mtu,kwa hiyo swala lakusema biashara imekuwa ngumu hilo siwezi kuzungumzia lakini cha msingi kama mtu biashara yake imeshuka kidogo lazima mauzo yaonekana na ndio maana tunasisitiza sana watu watumie mashine za EFD kwasababu zinaonyesha kila kitu"alisema Musib Shaaban

Jumuiya ya wafanyabiashara mji wa Njombe imetoka na maadhimio mbalimbali ikiwemo kwenda kujiweka sawa kiuongozi na kusajili wanachama wote ambao watakuwa na nguvu ya pamoja katika kusogeza mbele uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.
 Baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe wakiwa katika kikao na wafanyabiashara wa halmashauri ya mji wa Njombe.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa makini kusikiliza ajenda za mkutano

NZELENTIN NAHIMANA AWA MWENYEKITI WA KIKAO CHA BUNGE EALA BAADA YA SPIKA KUTOTOKEA KWENYE

$
0
0
Mwenyekiti wa kikao cha bunge la EALA Nzeintin Nahimana akiingia kuongoza kikao cha Tatu cha bunge la Nne jioni hii jijini Arusha 
Mwenyekiti wa kikao cha tatu Nzelentin Nahimana akiwa kwenye chumba baada ya kupitishwa kuwa Mwenyekiti wa kikao cha bunge la nne kuongoza kikao cha Tatu cha bunge hilo leo jioni jijini Arusha.

Ahmed Mahmoud Arusha
Bunge la Afrika mashariki limempitisha Mbunge wa bunge hilo Leontin Nzeimanah kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Tatu mkutano wa nne kuendesha baada ya Spika kutotokea kwenye kikao hicho.

Bunge hilo liliingia kwenye mjadala wa muda na hatimaye kufikia muafaka wa kumchagua Mwenyekiti wa Kikao ili kuendelea na shughuli za bunge hilo baada ya Spika kutotokea kwa sababu za kibinadamu jambo ambalo sheria inaweka wazi kupatikana kwa Mwenyekiti wa kuendesha kikao hicho.

Mh.Nzelentin Nahimana mbunge kutoka nchini Burundi alipigiwa kura 27 dhidi ya Mbunge Fatuma Ndangiza aliepata kura 18 ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 45 Kwa wajumbe wote 54 wa bunge hilo.

Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kutoa hoja ya kumchagua Mwenyekiti huyo Mbunge wa bunge hilo Abdulkadir Aden alitoa hoja kwa baraza hilo kuona umuhimu wa kuwa na Naibu Spika ili siku ambayo Spika hayupo shughuli ziweze kuendelea.

"Naomba baraza la mawaziri kuona umuhimu wa kulipeleka suala hili kwa mkutano wa Marais kuona linafanyiwa kazi na kuondoa changamoto hii ambayo imekuwa ikitokea kila wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa bunge hilo Mhandisi Habib Mnyaa alisema haoni sababu ya kuwepo kwa Spika na Naibu Spika wakati sheria ipo ya kuchagua Mwenyekiti wa kuendesha kikao pindi Spika akiwa hayupo kwa sababu za kibinadamu.

Alisema kuwa bunge hilo bado ni dogo  halina bajeti yenye kukidhi matakwa hayo na gharama ni kubwa za kumlipa Naibu Spika haoni sababu kuwa ni kiti hicho kwa Sasa Ila sekretariet ikiona inauwezo wa kifedha hakuna shida.

"Jua kuwa sheria zipo za kuendesha bunge hili jumuiya hii bado ni ndogo mimi sioni sababu ya kuwa na Naibu Spika kwa Sasa ikiwa ni kupunguza gharama na bado sheria zipo hivyo busara ipo mikononi mwa wakuu wa nchi kubadilisha sheria"

SUGU AKIMBIWA NA MADIWANI 11, DK BASHIRU AWAPOKEA KWA KISHINDO DODOMA

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAMEKIMBIA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lundo la madiwani 11 wa Jiji la Mbeya wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao 11 wakiongozwa na Meya wa Jiji hilo, David Mwashilindi na Katibu wa Wilaya wa Chadema wametangaza kuhamia CCM leo jijini Dodoma na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk Bashiru Ally.

Akizungumza baada ya kuwapokea kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dk Bashiru amesema wingi huo wa madiwani umevunja rekodi na kwamba sasa wapinzani wamekwisha Mbeya.

Madiwani hao ambao kata wanazoongoza  ziko kwenye mabano ni Fabian
Sanga (Ghana), Fanuel Kyanula (Sinde) ambaye pia ni Naibu Meya,
Davidi Mwashilindi (Nzouwa) ambaye ni Meya, Anyandwile Mwaluhubh
(Isanga), Kigenda Kasebwa (Ilomba Viti Maalum) na Dickson Mwakilasa
(Ilomba).

Wengine ni Costantine Mwakyoma (kalobe) Furaha Mwandalim (Ilemi) Henry Mwangambaku (Forest) ambaye pia ni katibu wa Wilaya, Anderson Ngao (Mwasanga) na Ibrahim Mwampwani (Isyesye).

Jiji la Mbeya linaongozwa na Mbunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambalo limekua likitajwa kama mojawapo ya ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani lakini kuhama kwa madiwani hao 11 kumetoa mwanya kwa CCM kuanza kuwa na matumaini makubwa kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

" Hii si mara ya kwanza kupokea madiwani na meya kwa wakati mmoja tulishapokea meya wa Ilala, meya wa Jiji la Arusha na huu ni
muendelezo tu.

Niwahakikishie ujio wa madiwani hawa ni uthibitisho tosha wa namna gani Rais Dk John Magufuli na serikali yetu ya CCM inafanya kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi kiasi cha viongozi wa upinzani kuamua kwa mapenzi yao kuunga mkono," Dk Bashiru.

Aidha Dk Bashiru amekanusha taarifa zinazosambwa mitandaoni zikionesha gari la Katibu Mkuu wa CCM likilindwa na Jeshi la Polisi ambapo amesema ni uongo na zile picha zinazosambazwa ni za kutengeneza.

Akizungumza baada ya kupokelewa na Dk Bashiru, Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi amesema yeye sio Chadema tena na amerudi kwenye chama chake kilichomlea na ambacho kimekua kikishughulika na kero za wananachi.

" Ndugu zangu sijataka kuwa mnafiki, kwa miaka minne ya Rais Magufuli nimeshuhudia kazi kubwa ambayo kwa hakika imekua sababu tosha ya mimi kurejea CCM, Rais aliahidi na anatekeza.

Chini ya Magufuli kila sekta imeguswa, afya, miundombinu, elimu na zaidi mafisadi hawapo awamu hii, kuendelea kubaki upinzani ni kukosa uzalendo, Chadema kule hakuna ajenda zaidi ya ugomvi na kupinga mambo makubwa yanayofanywa," Amesema Mwashilindi.
 Meya wa Jiji la Dodoma anayetokana na Chadema ambaye amehamia CCM, David Mwashilindi akizungumza baada ya kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk Bashiru Ally jijini Dodoma leo.
 Wandishi kutoka vyombo mbali mbalimbali na madiwani wa Chadema waliohamia CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM , Dk Bashiru Ally jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk Bashiru Ally akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma baada ya kuwapokea madiwani 11 wa Jiji la Mbeya wanaotokana na Chadema.

TANZANIA NA FINLAND ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA KUONGEZA IDADI YA WATALII NCHINI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI za Tanzania na Finland zimekubaliana kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii nchini pamoja na sekta zingine za kimaendeleo lengo likiwa ni kuinua uchumi wa Nchi.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara, Ville Skinnari.

Akizungumza baada ya mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Finland nchini, Riita Swan, Katibu Mkuu Prof Mkenda amesema serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje ya Nchi kuja kuwekeza na kufanya biashara.

Amesema katika mazungumzo hayo yalijikita katika kuzungumzia manufaa ya misitu na namna ambavyo wataweza kumaliza changamoto ya uchomaji misitu na kuhamasisha upandaji miti.

" Tunawashukuru wenzetu wa Finland ambao kwa hakika tumekua tukishirikiana kwa muda mrefu, tumejadili kwa pamoja umuhimu wa kuendeleza nishati mbadala ili kuepuka matumizi ya mkaa ambayo husabahisha uchomaji wa misitu.

Lakini wao pia wametuahidi kutusaidia katika uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu kwani wao wamekua ni wabobezi kwenye eneo hilo," Amesema Prof Mkenda.

Amesema pia wamewaalika wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza kwenye viwanda hivyo ikiwa ni sera ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

" Tumemualika Mhe Waziri kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu ili awe Balozi mzuri wa kututangaza na kuhakikisha tunanufaika na wingi wa watalii wanaotoka Finland.

Pia tumewaalika kuja kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini kwetu hasa katika eneo la Hoteli na tumewahakikishia kwamba mazingira ni salama na tutawapa ushirikiano wote," Amesema Prof Mkenda.

Kwa upande wake Waziri huyo wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara, Mhe Ville Skinnari amesema wamekuja Tanzania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wizara mbalimbali ili kuendeleza ushirikiano wa Nchi hizi mbili pamoja na kufungua Milango ya uwekezaji.

Amesema sekta ya utalii imekua ikifanya vizuri na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna ambavyo serikali yake imetengeneza sera nzuri zinazovutia watalii na wawekezaji kwa ujumla.

" Tumewaeleza wenzetu kwamba suala la utunzaji wa mazingira hasa kulinda misitu yetu ni muhimu sana, tumewaahidi tutashirikiana katika kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu ili kuongeza pia fursa ya ajira na kukuza uchumi wa Nchi," Amesema Skinnari.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kikao chake na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Ville Skinnari (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kikao chake na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii (kulia) leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Ville Skinnari akimkabidhi zawadi ya Tai Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda baada ya kumalizika kwa kikao chao leo jijini Dodoma.
 Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii (kulia) wakiwa kwenye kikao cha pamoja na viongozi kutoka serikali ya Finland. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

JESHI LA POLISI DODOMA LATANGAZA KUMSHIKILIA MUSIBA

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mwanaharakati huru Cyprian Musiba kwa kutuhuma za kusambaza habari  za kutaka kuuliwa  bila kuripoti   kwenye vyombo  vya dola jambo ambalo ni kinyume na Sheria.

Akizungumza na Wandishi wa Habari leo Feb.24.2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha kulalamika kutishiwa kuuwawa na baadhi ya wanasiasa .

" Tunamshikilia kwa mahojiano ili aweze kutueleza kwa undani juu ya malalamiko hayo anayoyatoa, na hii ni kwa sababu yeye mwenyewe licha ya kulalamika kutaka kuuliwa hajatoa ripoti zozote kwa Jeshi letu," Amesema Muroto.

Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai  kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo linamshikilia Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo kuhusiana na kumshikilia mwanaharakati huru, Cyprian Musiba.
 

NBC YAZINDUA KLABU YA BIASHARA TANGA, YATOA MAFUNZO YA KIBIASHARA

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Maheji ameipongeza Benki ya NBC kwa kuamua kufungua klabu na kutoa elimu ya mlipakodi, utunzaji wa kumbukumbu na jinsi ya kuweka mahesabu sawa. 

Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa Klabu ya NBC B Club iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii. “Niipongeze Benki ya NBC kwa uzinduzi wa klabu hii na kutoa mafunzo haya kwani moja ya eneo  ambalo wafanyabiashara wengi wanakosa ni hili la utunzaji wa taarifa za biashara zao yaania 
kumbukumbu, hivyo niimani yangu kuwa litapunguza sana migogoro kati ya wafanyabisha na Serikali hasa TRA wakati wa ukadiriaji wa kodi zao’ amesema Maheji. 

Benki hiyo imezindua klabu ya biashara Katika mkoa wa Tanga yenye Lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati pamoja ili kupeana  fursa, mbinu na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusi biashara zao. 

Katika uzinduzi huo, NBC wameendesha mafunzo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati kwa lengo pia la kuwaongezea uwezo, uelewa na ubunifu katika ufanyaji wa 
biashara zao. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Klabu hiyo ya Biashara mkoani Tanga, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NBC, Elvis Ndunguru amesema kuwa benki hiyo imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali hususani wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini. 

Amesema kuzinduliwa kwa klabu hiyo ya Biashara kunafanya klabu za biashara katika benki hiyo nchini kuwa malengo yake ni kuwaunganisha na kuwakutanisha wafanyabishara pamoja ili kutafuta fursa za ufanyaji wa biashara na kubadilishana uzoefu. 

Ndunguru amesema klabu hizo za biashara zimekuwa sehemu ya wafanyabiashara kupata masoko na kuongeza kuwa katika kuhakikisha benki inachangia ukuaji wa sekta ya biashara nchini, imeamua kuanzisha vilabu hivyo vya wafanyabiashara (NBC B Clubs) ili kukuza na 
kuimarisha biashara nchini. 

"NBC B Club ni mahali muafaka pa kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara na tangu kuanzishwa kwa klabu hizi za biashara, wanachama wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia vitabu vya mahesabu, elimu ya  masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA," 
amesema na kuongeza. 

"Klabu hizo zimekuwa zikipanua masoko kwa wafanyabiashara, kwa mfano kwa miaka minne mfululizo sasa tumekuwa tukipeleka wafanyabiashara China na mwaka huu tunatarajia kuwapeleka Ujerumani kwa sababu kuna maonesho ya viwanda lakini pia tunafikiria kupeleka watu Ulaya na Marekani kwa ajili ya kukutana na wenye viwanda na wanaotengeneza mashine mbalimbali jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wetu," 
alisema 

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka TRA makao makuu, Julius Mjenga  amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa makini katika kutunza kumbukumbu za biashara ili kuepusha migororo na TRA hasa waka; wa ukadiliaji wa kodi. 

"Napenda kuwaambia wafanyabiashara kwamba ili waweze kukadiliwa kodi zao vizuri ni  muhimu watunze kumbukumbu zao, hata hivyo changamoto kubwa inayoonekana ka; ya  TRA Na wafanyabiashara ni kulalamikia makadirio ya kodi sasa ili hii iondoke watunze  kumbukumbu zao," amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Tanga, Liberat Macha  amesema wamekuwa walitoa mikopo kwa wajasiriamali wanaoanza na kuendelea na biashara hivyo watu wasisite kuja kuchukua kwani vigezo ni kuwa na mradi halali unaoendeshwa kwa mujibu wa utaratibu unaotambulika kisheria. 

Kwa upande wake mfanyabiashara ambaye ni mteja wa NBC aliyenufaika na klabu za biashara, Haji Mambo amesema kupitia klabu hizo wameweza kuunganishwa na watu mbalimbali duniani ambapo yeye alifanikiwa kwenda China na kuonana na wafanyabiashara wengine waliombadilisha mawazo na mitazamo katika biashara zake. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanga, Daudi Mahej (Wa pili kulia), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru kuashiria uzinduzi rasmi wa Club ya biashara katika Mkoa wa Tanga (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa wadogo na wakati wa NBC Evance Luhimbo pamoja na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Tanga Asia Chambega. Uzinduzi huo umefanyika Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Halmashauli ya jiji la Tanga Daudi Mahej akifafanua jambo kwa maofisa wa Benki ya NBC, baada ya kuzindua rasmi mafunzo ya wafanya Biashara wadogo na wakati yalioandaliwa na Benki ya NBC (kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Benki ya Kiislam Nbc Mohamedi Nuh (Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wakati Evance Luhimbo, pamoja na Meneja wa NBC tawi la Tanga Asia Chambega
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru akishikana mikono na Afisa Mkuu Msimamizi wa kodi TRA makao makuu, Julius Mjenga baada ya kumaliza mafunzo ya yabiashara yalioandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanya Biashara wa Mkoa wa tanga mwengine pichani ni Meneja Uhusiano Benki ya NBC William Kallaghe
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru akizungumza wakati wa Mafunzo ya Biashara kwa wafanya Biashara wadogo na wakati wa Mkoa wa Tanga wakati wa Uzinduzi wa Club ya Biashara mkoani tanga hafla ya uzinduzi huo umefanyika jijini Tanga.

MWANDISHI ERICK KABENDERA AUHUKUMIWA KILIPA SHILINGI MILIONI 273, MAHAKAMA YA MUACHIA HURU

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii

MWANDISHI maarufu wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera amehukumiwa kulipa faini na Fidia ya jumla ya sh. Milioni 273 baada ya kukiri makosa ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi.
Aidha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Kabendera kulipa faini ya sh.250,000 ama kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kukiri kosa la kukwepa kodi huku pia akifutiwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Hata hivyo mshtakiwa Kabendera ameishalipa Sh. Milioni 100 na kiasi kilichobakia cha sh. Milioni 173 atatakiwa kulipa kwa awamu katika kipindi cha miezi sita kuanzia leo Februari 24,2020.
Hatua hiyo imekuja baada ya mshtakiwa Kabendera  kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya kuomba msamaha na kukiri makosa ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili.
Hukumu hiyo imesomwa leo Februari 24,mwaka 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ambapo akisoma adhabu hiyo katika kosa la kwanza la ukwepaji kodi mshtakiwa ametakiwa kulipa faini ya Sh. 250,000 au kifungo cha miezi mitatu jela pia atatakiwa kulipa fidia ya Sh. Milioni 173.
Hakimu Mtega alisema katika kosa la pili la utakatishaji fedha mshitakiwa Kabendera atatakiwa kulipa faini ya sh. Milioni 100 na kusisitiza kuwa adhabu hizo zitakwenda peke yake.
Kutokana na adhabu hiyo Kabendera amelipa faini ya sh. 250,000 na anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.Milioni 273 ambapo tayari ameshalipa kiasi cha sh. Milioni 100 na kiasi cha Milioni 173 kukilipa  ndani ya miezi 6 kuanzia leo.

KABENDERA YUKO HURU 
Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mtuhumiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na hawana kumbukumbu  ya makosa ya nyuma hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano yaliyofanyika.
Kwa upande wake, Wakili wa Mshitakiwa huyo, Jebra Kambole alidai kuwa kukiri makosa yake kumeipunguzia muda mahakama kuendesha mashitaka, ana familia na ndugu wanaomtegemea pia ni zaidi ya miezi sita sasa amekaa maabusu.
Alidai pia mshitakiwa huyo hali yake ya kiafya sio nzuri na wanaomba katika kosa la kwanza aweze kupewa faini ya sh. 250,000 kwa mujibu wa sheria ya kodi  na kwa kosa la pili aweze kupewa faini pia kwa mujibu wa sheria.
Mapema, akisoma makubaliano ya mshitakiwa huyo na DPP, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai kuwa wameingia makubaliano na mshtakiwa huyo baada ya kukiri kosa la utakatishaji fedha na ukwepaji kodi hivyo DPP ameamua kumeondolea kosa la kuongoza genge la uhalifu.
Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Mtega alimuapisha mshtakiwa na kumuuliza  kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.
Miongoni mwa maelezo ya awali yaliyosomwa ni kuwa kati ya Januari Mosi, 2010 na Julai 29,2019 mshitakiwa alijihusisha na genge la uhalifu kwa kuingia mikataba isiyo halali na watu wengine ambao wapo nje ya Tanzania ikiwemo watu maarufu ambao hawapo mahakamani ambapo anadaiwa kukubali kufanya makosa ikiwemo kughushi, kukwepa kodi na utakatishaji fedha ambayo yanachangia kudidimiza uchumi.
Nchimbi alidai Machi 23, 2010 na kampuni yake iliyosajiliwa kama Voxy Media Center (T) Ltd na Wakala wa Usajili (Brela) na kwamba Januari 11, 2016 mshitakiwa pamoja na mkewe Loy Kabendera ambaye anajulikana pia Loyce Nganga walisajili kampuni ya Sitrep Company Limited na katika usajili huo waligushi fomu mbalimbali na kuonesha ofisi ya kampuni hiyo inapatikana kwenye nyuma namba 13 kitalu namba 23 Mbweni Mpiji Kinondoni ambayo ni nyumba yao ya kuishi.
Alidai mshitakiwa huyo pia katika mkakati wake wa kiuhalifu alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa Serikali kwa lengo la kuidanganya serikali na kujipatia fedha kwa njia ya uhalifu.
Imedaiwa April 2, mwaka 2016  mshitakiwa huyo pamoja na mkewe walifungua akaunti mbili za fedha katika benki ya CRDB moja ikiwa ya fedha za kigeni, pia mshitakiwa alifungua akaunti yake binafsi na Januari Mosi, 2015 alipokea USD 230,358.83 kutoka kwa washitakiwa wenzake kupitia akaunti yake binafsi ambazo zilitoka kwa watu mbalimbali ikiwemo kampuni ya K2 Intelligence Ltd, Palladium (Tanzania) Ltd, Sitrep Co. Ltd, Eurasia Group Ltd, International Crisis Rou na taasisi zingine za kigeni.
Nchimbi alidai, Januari Mosi, 2015 na Agosti 29, 2019 mshitakiwa na mkewe Loy wakiwa wakurugenzi wa Kampuni ya Sitrep walipokea USD 432,000,541 na Paundi 119, 000,130 na katika kipindi chote hicho hawakuwai kulipa kodi kwaTRA.
Hata hivyo Nchimbi alidai kuwa mshitakiwa huyo aliwaambia maofisa wa Polisi kuwa ajapokea fedha zozote kinyume na taratibu kutoka katika vyanzo visivyohalali.
Aidha uchunguzi wa awali ulionesha mshitakiwa huyo alijihusisha na shughuli za kihalifu na kufuatia uchunguzi huo alifunguliwa mashitaka mbele ya mahakama hii ambayo aliyakiri  kuyafanya.
Katika mashtaka mapya, imedaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2015 na Agosti 29,2019  kipindi hicho, Kabendera alikwepa kodi kiasi cha Sh.173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe TRA.

Pia katika shitaka la pili, Kabendera anadaiwa alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la ukwepaji kodi.

HUKUMU YA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIONGOZI CHADEMA KUTOLEWA MACHI 10, 2020

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii
MAHAKAMA Ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 10, mwaka huu kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi dhudi ya viongozi nane wa Chadema akiwemo  Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk.Vicent Mashinji ambaye hivi karibuni  amehamia CCM.
 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema sheria inaelekeza pande zote kufanya majumuisho ili kuisaidia mahakama kutoa uamuzi kwa kuangalia masuala ya kisheria yaliyoibuliwa wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo na wametoa maelekezo kwa pande hizo kuwasilisha hoja zao katika siku tano za kazi baada ya mahakama kukamilisha uchapaji wa nyaraka zilizopo kwenye kesi hiyo na kuwapatia.

Amesema, anatambua kesi hiyo inamvuto kwa jamii, hivyo ni lazima iishe ili kila mmoja aweze kuendelea na shughuli zake na kuongeza  "Majumuisho ya mwisho mnatakiwa muyawasilishe siku tano za kazi," amesema Hakimu Simba. Ameongeza kesi hiyo inakurasa zaidi ya 1,000 ambazo anatakiwa kuzipitia na kutoa hukumu hivyo hukumu ya kesi hiyo itatolewa Machi 10, mwaka huu saa 4:30 asubuhi.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu,  Katibu Mkuu Chadema na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Jumla ya mashahidi nane wa upande wa mashtaka walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo mahakama iliwaona washitakiwa wote kuwa na kesi ya kujibu na walijitetea kwa kuleta mashahidi kumi na tatu.
Mwaka 2018, viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa  na mashitaka 13 ikiwemo ya kufanya mkusanyiko usiohalali uliosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline.


Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.


CCM CHATO YASEMA WAZIRI KALEMANI AMEITENDEA HAKI ILANI

$
0
0
Veronica Simba – Chato

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato kimekiri kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt Medard Kalemani.

Ameyasema hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Chato, Ramadhani Ndaki na kuongeza kuwa kwa utendaji kazi wake mahiri, Dkt Kalemani ameitendea haki Ilani ya Chama hicho ambacho ndicho kinaongoza nchi.

Kiongozi huyo wa Chama alikuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Waziri Kalemani kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Bukamila, Kata ya Kigongo, Februari 22, 2020.

“Utendaji kazi mzuri wa Dkt Kalemani umetupa matumaini sisi viongozi kuwa Ilani ya Chama inatekelezwa ipasavyo na kwakweli wakati ukifika, tutamtendea haki,” amesema Ndaki.

Akifafanua zaidi kuhusu utendaji kazi wa Dkt Kalemani, Ndaki alieleza kuwa, akiwa ni Waziri mwenye dhamana ya nishati, pamoja na mambo mengine, amefanya bidii kubwa kuhakikisha wananchi hasa walioko vijijini nchi nzima wanafikiwa na umeme.

Kwa upande wa Chato, Ndaki alieleza kuwa Dkt Kalemani amefanya makubwa katika sekta ya nishati ambapo mpaka sasa Kata zote 23 za Jimbo hilo zimekwishafikiwa na umeme.

Awali, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho cha Bukamila, Dkt Kalemani alibainisha kuwa hadi sasa jumla ya vijiji takribani 9,000 vimekwishaunganishiwa umeme nchini kati ya 12,268 vilivyopo, sawa na asilimia 74.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu, jumla ya vijiji 10,446 vitakuwa vimeunganishwa na umeme na kwamba ifikapo Juni 2021, vijiji vyote vya Tanzania Bara vitakuwa vimefikiwa na nishati hiyo.

Alimpongeza na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini na akaahidi kuwa yeye na viongozi wenzake waandamizi wa Wizara, wataendelea kusimamia vyema matumizi yake kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
 Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Chato, Ramadhani Ndaki, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, Chato. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Februari 22, 2020 alikuwa ni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani).
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akifurahia mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto), akiwatambulisha viongozi waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mbele ya wananchi wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Kazi ya kuunganisha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato ikiendelea. Taswira hii ilinaswa Februari 22, 2020 wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akiwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
 Baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.

WAKULIMA MAZAO YA VIUNGO WATOA OMBI KWA SERIKALI , SAT WAELEZA WANAVYOSAIDIA KUTAFUTA SOKO LA UHAKIKA

$
0
0

Baadhi ya wakulima wa kilimo hai mkoani Morogoro wakiwa katika moja ya mkutano wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kilimo hicho ambapo wametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Serikali kuanzisha bodi ambayo itahusika kusimamia mazao ya kilimo hai yakiwemo mazao ya viungo ambayo yamekuwa yakilimwa na baadhi ya wakulima ambao wako chini ya mradi wa unaosimamiwa na Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT).
Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu kilimo cha viungo ambacho kinalimwa na baadhi ya wakulima katika wilaya ya Morogoro Vijijini na Mvomero mkoani Morogoro
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAT (hayupo pichani) wakati akielezea jitihada ambazo zinafanywa na shirika lake katika kutafuta masoko ya mazao ya viungo ndani na nje ya Tanzania.
Janeth Maro ambaye ni Mkurugezi Mtendaji wa SAT akisisitiza jambo kuhusu kilimo cha viungo



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

WAKULIMA wa mazao ya viungo mbalimbali vinavyotokana na kilimo hai mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuunda bodi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia bidhaa zao kama ilivyokuwa kwenye zao la pamba ili kuhakikisha wananufaika na kilimo hicho.

Wametoa ombi hilo baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti cha Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania kilichopo mkoani Morogoro ambapo wakulima hao wanatoka katika Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Lubondo.

Wakulima hao wamesema pamoja na kupatiwa mafunzo ya kilimo hai na wao kujikita katika kilimo cha viungo mchanganyiko lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni soko la uhakika.

Mmoja wa wakulima na mfugaji kutoka katika kijiji hicho cha Lubondo Pendo Ndeme amesema wanatoa shukrani kwa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) kwa kuendeleza kilimo hai mkoani hapo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ya kutoa elimu ya kilimo hicho na namna ya kukiendleza.

Amesema SAT Imekuwa na mchango mkubwa hasa katika kutoa elimu ya kilimo hai, hivyo wao kama wananchi ambao wanatoka katika kata ya Lubondo ,kijiji cha Lubondo wameweza kuhamasika na kujikita katika kilimo cha viungo mbalimbali na kwa kiasi kikubwa wanafanya vizuri lakini changamoto kubwa wanayoipata ni soko la uhakika.

Ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Serikali kuangalia upya katika eneo hilo kwani kama watawawezesha kwa kuwapatia bodi ya yao kuwasimamia kama ilivyo kwenye zao la pamba wanaamini watanufaika zaidi na kilimo hicho cha viungo ambacho kwa sasa wanaona faida yake.

"Hivi sasa tunazalisha kwa wingi mazao ya viungo lakini tatizo kubwa ni soko pamoja kwamba shirika la SAT linajitahidi kutafuta masoko kwa ajili wakulima bado tunaona iko haja kwa Serikali kuongeza nguvu katika eneo hili, SAT wametuhamasisha kulima na wakulima tumeitikia kwa mwitikio mkubwa sana,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro amesema wanatambua faida za kilimo cha mazao ya viungo na kupitia miradi mbalimbali ambayo wamekuwa wakifanya kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho kimetoa hamasa kwa wakulima wa mkoa huo na hasa wa Wilaya ya Mvomero na Morogoro Vijijini.

‘’SAT pamoja na mambo mengine yanayohusu kilimo hai tumekuwa na jukumu la kuhakikisha tunatafuta soko kwa ajili ya kuhakikisha mazao ya wakulima ambayo yanazalishwa yanapata soko la uhakika na ndio maana baadhi ya mazao tumeyayatafutia soko nchi za nje ikiwemo nchi ya Uswis,"amesema.

SHIRIKA LA KILIMO ENDELEVU TANZANIA LAKAMILISHA MTALAA MPYA WA KILIMO,VYUO 29 KUANZA KUUTUMIA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii 

SHIRIKA la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) likamilisha mtaala mpya wa kilimo ambao unatarajiwa kuanza kutumia kwenye vyuo vya mafunzo ya kilimo 29 nchini ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha mtaala huo unaendana na mahitaji ya sasa. 

Akizungumza na waandishi wa habari za kilimohai wakati wa mafunzo maalumu ya kilimo hicho, Meneja wa Mradi wa SAT Mgeta Daud amesema mtaala huo wameufanikisha kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Divisheni ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti kwa hisani ya Shirika la Maendeleo la Leichtenstein. 

Amefafanua awamu ya kwanza ya mtaala huo ulianza kufundishwa katika vyuo saba vya Mati Kartini, Chuo cha Taifa cha Sukari(NSI), Mati-Ilonga, Mati horti-Tengeru, KATC-Moshi, TRACDI na Chuo cha St.John's. 

"Mradi huu unaendelea kupanua wigo wake na kufikia vyote vyote 29 vya mafunzo ya kilimo nchini katika kanda zote saba za kilimo.Mradi huu ambao unafahamika kama CISTI unatekelezwa katika ngazi tatu kuu.Ngazi ya kwanza mradi unajenga uwezo wa wakufunzi wa vyuo vilivyopo katika mradi. 

"Katika ngazi ya pili mradi unaimarisha uwezo wa vyuo ya mafunzo ya kilimo kimiundombinu ili kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa mtaala mpya wa kilimo na tatu mradi unashirikiana na divisheni ya mafunzo, huduma za ugani na utafiti ya wizara ya kilimo ambayo ndiyo ina dhamana ya kusimamia vyuo vyote vya kilimo kuhakikisha mtaala unatekelezwa vyema na matokeo chanya yanatokea,"amesema Daud. 

Akifafanua zaidi kuhusu mtaala huo,amesema matokeo ya upembuzi yakinifu wa hali halisi ya soko la ajira , hali halisi ya vyuo vya mafunzo ya kilimo na uwezo wa wakufunzi katika kufundisha mtaala, ulisababisha kuanza mchakato wa kuhuisha mtaala uliokuwepo ili uendane na mahitaji ya sasa ya maarifa na utalaamu unaohitajika katika soko la ajira. 

Ameongeza Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania lilishiriki kikamilifu katika hatua zote za muhimu za kuhuisha mtaala na hatimaye ushawishi wake ulisababisha kuingizwa kuingizwa kwa moduli mpya tatu za kilimo hai, jinsia katika kilimo na usimamizi wa mazingira katika mtaala mpya. 

"Mchakato wa kuihusha mtaala ulikamilika baada ya taratibu zote kufuatwa na kuthibitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa(NACTE)na kilele cha mchakato huu kilihitimishwa kwa kuzinduliwa kwa mtaala mpya ambao ndio unachukua nafasi ya mtaala wa zamani,"amesema. 

Mbali ya kuzungumzia mtaala huo mpya, ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa SAT pamoja na mambo mengine ya kilimo ikiwemo ya kufanya tafiti, yenyewe imejikita katika kilimohai ambacho kinalenga katika kuleta uendelevu wa rutuba ya udongo, bioanuai, na hifadhi ya mazingira huku afya za walaji wa vyakula vya kilimo hicho zikilindwa na kuboreshwa. 

"Kuna taasisi na kampuni takribani 30 yanajihusisha na kilimo hai na wakulima wapatao 148,610 na eneo la hekta 268,729 nchini Tanzania.Namna bora ya kuongeza wigo wa kilimo hai Tanzania ni kuzalisha wageni wenye umahili katika maarifa na ujuzi wa kilimo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro akionesha zao la bizali ambalo linalimwa katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo hai ambacho kinamilikiwa na Shirika hilo
:Mmoja ya waandishi wa habari kutoka Capital TV ambaye pia ni Mshauri wa masuala mbalimbali katika jamii Austine Makani akifuatilia kwa makini maelezo ya watalaamu wa kilimo hai katika Kituo cha Utafiti cha kilimo kinachomilikiwa na Shirika la kilimo Endelevu (SAT).
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika moja ya bwawa la kufugia samaki baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT).
Mkurugenzi Mtandaji wa SAT Janeth Maro akiwa ameshika jani la Mnyonyo wakati anaeleza faida ya jani hilo katika kukomesha wadudu waharibifu wa mazao.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya kilimo hai yaliyofanyika katika Kituo cha Utafiti wa kilimo kinachomilikiwa na SAT.
Mkurugenzi Mtandaji wa SAT Janeth Maro akiwa ameshika jani la Mnyonyo wakati anaeleza faida ya jani hilo katika kukomesha wadudu waharibifu wa mazao.





Mbogamboga za majani zikiwa zimepandwa katika mfuko maarufu kwa jina la kiroba .Mfumo huo wa upandaji wa mbogamboga unatumia eneo dogo.
Meneja wa Mradi wa Mtaala mpya wa kilimo kutoka Shirika la Kilimo Endelevu( SAT) Mgeta Daud akizungumzia kukamilika kwa mtaala huo ambao unatarajiwa kuanza kutumia kwenye vyuo 29 nchini na kwamba mtaala huo umekamilika kwa ushirikiano kati yao na Wizara ya Kilimo kupitia Divisheni ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti kwa hisani ya Shirika la Maendeleo la Leichtenstein.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) Janeth Maro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo zimetumika hadi kukamilika kwa mtaala huo wa ambao utakwenda kutumika kwenye vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo nchini kwa ngazi ya cheti na Diploma.
Mazao mbalimbali yakiwemo kweye 'Green House' katika eneo la Kituo cha Utafiti cha kilimo Hai ambacho kinamilikiwa Shirika la Kilimo Endelevu( SAT).Kituo hicho kimekuwa kikitumika kutoa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali yakiwemo ya kufanya tafiti mbalimbali za kilimo.

UONGOZI WA YANGA WAMPONGEZA DKT TOBIAS LINGALANGALA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umempongeza Mjumbe wa Kudumu na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Dkt Tobias Lingalangala kwa kutunukiwa shahada ya uzamivu (PHD) kutoka Shirika la LeadImpact ya nchini Marekani.

Lingalangala ametunukiwa shahada ya uzamivu ya Doctorate in humanity baada ya taasisi hiyo kuona juhudi kubwa alizozifanya kwa jamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumpongeza, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla amesema baada ya kupata taarifa kuwa mmoja wa watendaji wa muda mrefu ndani ya Klabu ya amefurahi ametunukiwa shahadu ya uzamivu tena katika masuala ya jamii ambalo ni jambo kubwa sana.

Msolla amesema, uongozi wa Yanga unampongeza sana Dkt Lingalangala kwa hatua kubwa aliyoipiga katika kusaidia jamii na kurudisha mchango wake hadi kufikia hatua ya kutunukiwa shahada hiyo.

"Sisi kama uongozi wa Yanga tunajivunia kuwa na kiongozi kama Dkt Lingalangala kwani amekuwa ni moja ya viongozi wanaojitoa sana nilifikiri ni kwa klabu ya Yanga tu kumbe hadi kwa jamii, amefanya  mambo makubwa sana nasi kama uongozi wa Yanga tunampongeza," Dkt Msolla.

Ameeleza kuwa, Lingalangala ameifanyia makubwa sana Yanga ikiwemo kufanya usajili wa mchezaji mmoja na hasa akiwa kamati ya mashindano ambayo ni nyeti ndani ya klabu yao.

Kwa upande wake Dkt Lingalangala ametoa shukrani kwa uongozi wa Yanga kwa kuendelea kumuamini ndani ya Klabu hiyo kwa kumpatia ujumbe wa kudumu.

Amesema, hakutegemea kupata shahada hiyo kwani hakufahamu kama mchango wake kwa jamii una thamani kubwa sana na ameishukuru Shirika la LeadImpact kwa kumtunuku kitu  chenye thamani kubwa kwenye maisha yake.

Pia, ameishukuru familia yake kwa ujumla kwa kumpasapoti kwa kila jambo analofanya kwa jamii na ana imani kuwa huu ni mwanzo bali ataendelea kujitoa kwa kila atakachokipata.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali, Lingalangala amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kumuamini na amewataka kuwa na subira kwani kwani bado wanaendelea kuijenga timu yao.

Mwishoni mwa wiki hii, Lingangala alikua ni moja ya watunukiwa shahada za uzamivu (Doctorate in Humanity PHD) Kutoka shirika la LeadImpact la nchini Marekani baada ya kujenga mradi mkubwa wa maji kwenye mji wa Njombe pamoja na kutoa elimu ya kilimo na ufugaji wa kisasa kwa wananchi wa mji huo.

MKATABA MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA EU UIMARISHE SEKTA ZA MAENDELEO

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, baada ya kumaliza kwa mkutano kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.


Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, akizungumza kuhusu uboreshaji wa miundombinu ili kuchochea biashara, wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Adolf Ndunguru (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati wa kikao na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo Fanti (hayupo pichani), jijini Dodoma.



Ujumbe kutoka Ubalozi wa Umoja wa Ulaya ukiongozwa na Balozi Mhe. Manfredo Fanti (katikati), wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), alipokuwa akielezea masuala ya msaada wa kibajeti, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo ambayo tayari inatekelezwa katika mkataba mpya wa Ushirikiano na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa mkutano na Balozi wa EU nchini, Mhe. Manfredo Fanti, jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano kulia), na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti, (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Umoja wa Ulaya Jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Mhe. Ville Skinnari (kushoto), wakati wa wakati wa mkutano uliofanyika, jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo na Waziri wa Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Mhe. Ville Skinnari, baada ya kumaliza mazungumzo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dodoma.



Mazungumzo yakiendelea kati ya Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, (katikati) na Ujumbe kutoka Finland uliyoongozwa na Waziri wa Ushirikiano wa Biashara wa Finland Mhe. Ville Skinnari, jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri wa Ushirikiano wa Biashara wa Finland Mhe. Ville Skinnari (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania na Finland baada ya kumaliza mazungumzo Jijini Dodoma. (Picha na Peter Haule Wizara ya Fedha na Mipango). 

……………………………………………..

Na. Peter Haule na Josephine Majula, WFM, Dodoma

Serikali imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo ambayo tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021 hadi 2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na EU unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 ni vema ukaendelea kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza kutekelezwa na Serikali hususani katika Sekta ya Elimu, Afya, miundombinu na mingine ili kufikia malengo endelevu.

“Tuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye rasilimali watu kwa kuwa miradi kama miundombinu haiwezi kufikia malengo yake bila kuwa na uwekezaji katika rasilimali hiyo na ndio maana kama Serikali tumeamua kutoa elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari”, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa katika suala la miundombinu, Serikali inaangalia uwezekano wa kuanza ujenzi wa Reli kutoka Bandari ya Mtwara katika Bahari ya Hindi hadi Bandari ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa, ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuokoa fedha nyingi zinazotumika kukarabati barabara zinazoharibika kwa usafirishaji wa bidhaa kwa njia ya barabara.

Aidha alieleza kuwa miundombinu hiyo ya reli itakuwa na matawi kuelekea Liganga ambako kunapatikana madini ya Chuma na Mchuchuma ambako kuna hazina kubwa ya Makaa ya Mawe.

Alisema Reli hiyo itasaidia pia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kwenda nchi jirani ikiwemo Malawi, hivyo kuchochoa biashara na kuongeza mapato.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, aliipongeza Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo lakini pia akasema kuwa ili kuboresha mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo yanayohitajika ni pamoja na Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa kidigitali na siasa bora, mambo ambayo Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyatekeleza.

Mkataba wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi uliokuwa ukitekelezwa kuanzia mwaka 2014 unamalizika mwaka huu ilihali kwa sasa kunatarajiwa kuwepo kwa majadiliano ya mkataba mwingine wa ushirikiano unatarajia kuanza kutekelezwa mwaka 2021 na kumalizika 2027.

Katika tukio jingine, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango namekutana na mkufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikianao wa Biashara wa Finland, Mhe. Ville Skinnari, ambapo walijadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi.

DKT.JINGU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAENDELEO NA BIASHARA YA KIMATAIFA WA FINLAND

$
0
0


Waziri wa maendeleo na biashara ya nje wa Finland Bw. Ville Skinnari na ujumbe wake alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Wizarani hapo, Jijini Dodoma leo tarehe 24/02/2020 
………………………… 

Waziri wa Maendeleo na Biashara ya kimataifa wa Finland Bw. Ville Skinnari amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Mendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu kuhusu maendeleo na usawa wa jinsia hapa nchini.
Akizungumzia masuala ya Jinsia, Katibu Mkuu Jingu amesema Serikali imechukua hatua madhubiti kuboresha usawa wa kijinsia na haki ya mtoto wa kike. 

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewekeza katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na masuala ya uongozi. Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkakati kukabiliana na mimba katika umri mdogo na kupinga mila zilizopitwa na wakati ikiwemo ukeketaji. 

Aidha, ameongeza kuwa sera ya Taifa ni kushirikisha wananchi katika jitihada za kukabiliana na vikwazo vilivyopo. Dkt. Jingu amesema Serikali katika ngazi mbalimbali za uongozi imeunda kamati maalum za kulinda na kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa. 

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo na Biashara ya Kimataifa kutoka Finland Bw. Ville Skinnari amesema nchi yake inaunga mkono juhudi za Tanzania kupambana na changamoto zilizopo.

LEONTINE NZEYMANE AWA MWENYEKITI WA KIKAO CHA BUNGE LA EALA BAADA YA SPIKA KUTOTOKEA KIKAONI KUTOKANA NA UDHURU

$
0
0

Mwenyekiti wa kikao cha bunge la EALA Nzeintin Nahimana akiingia kuongoza kikao cha Tatu cha bunge la Nne jioni hii jijini Arusha

Mwenyekiti wa kikao cha tatu Nzelentin Nahimana akiwa kwenye chumba baada ya kupitishwa kuwa Mwenyekiti wa kikao cha bunge la nne kuongoza kikao cha Tatu cha bunge hilo leo jioni jijini Arusha.

Ahmed Mahmoud Arusha 

Bunge la Afrika mashariki limempitisha Mbunge wa bunge hilo Leontin Nzeimanah kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Tatu mkutano wa nne kuendesha baada ya Spika kutotokea kwenye kikao hicho. 

Bunge hilo liliingia kwenye mjadala wa muda na hatimaye kufikia muafaka wa kumchagua Mwenyekiti wa Kikao ili kuendelea na shughuli za bunge hilo baada ya Spika kutotokea kwa sababu za kibinadamu jambo ambalo sheria inaweka wazi kupatikana kwa Mwenyekiti wa kuendesha kikao hicho. 

Mh.Nzelentin Nahimana mbunge kutoka nchini Burundi alipigiwa kura 27 dhidi ya Mbunge Fatuma Ndangiza aliepata kura 18 ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 45 Kwa wajumbe wote 54 wa bunge hilo. 

Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kutoa hoja ya kumchagua Mwenyekiti huyo Mbunge wa bunge hilo Abdulkadir Aden alitoa hoja kwa baraza hilo kuona umuhimu wa kuwa na Naibu Spika ili siku ambayo Spika hayupo shughuli ziweze kuendelea. 

“Naomba baraza la mawaziri kuona umuhimu wa kulipeleka suala hili kwa mkutano wa Marais kuona linafanyiwa kazi na kuondoa changamoto hii ambayo imekuwa ikitokea kila wakati. 

Kwa upande wake Mbunge wa bunge hilo Mhandisi Habib Mnyaa alisema haoni sababu ya kuwepo kwa Spika na Naibu Spika wakati sheria ipo ya kuchagua Mwenyekiti wa kuendesha kikao pindi Spika akiwa hayupo kwa sababu za kibinadamu. 

Alisema kuwa bunge hilo bado ni dogo halina bajeti yenye kukidhi matakwa hayo na gharama ni kubwa za kumlipa Naibu Spika haoni sababu kuwa ni kiti hicho kwa Sasa Ila sekretariet ikiona inauwezo wa kifedha hakuna shida.
“Jua kuwa sheria zipo za kuendesha bunge hili jumuiya hii bado ni ndogo mimi sioni sababu ya kuwa na Naibu Spika kwa Sasa ikiwa ni kupunguza gharama na bado sheria zipo hivyo busara ipo mikononi mwa wakuu wa nchi kubadilisha sheria”

Majadiliano Sekta ya Umma na Binafsi Chachu Ukuaji wa Uchumi

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa, Dkt. Godwill Wanga (kushoto) baada ya uzinduzi wa Muongozo wa majadiliano kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika ngazi ya Mikoa na Wilaya uliofanyika leo jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akikabidhiwa kitabu cha Muongozo wa Majadiliano kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika ngazi za Mikoa na Wilaya na Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa, Dkt. Godwill Wanga (kushoto). Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa muongozo huo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi kitabu cha Muongozo wa Majadiliano kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika ngazi za Mikoa na Wilaya.Amepokea kitabu hicho kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchi nzima.
………………………………….

Na Jacquiiline Mrisho – MAELEZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa majadiliano ya mabaraza ya biashara yanayofanyika katika ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya yameendelea kusaidia uchumi wa nchi kuimarika.

Waziri Mhagama ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati akizindua Muongozo wa majadiliano kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika ngazi ya Mikoa na Wilaya uliofanyika jijini humo ambapo amesema kuwa inawezekana mabaraza ya biashara yalikuwa hayafanyiki vizuri kwa sababu watu walikuwa wanashindwa kutumia mazingira waliyonayo kujipanga kuendesha mabaraza haya lakini, muongozo huo utasaidia watu kukutana kwa ajili ya majadiliano yenye tija.

“Ili kuwa na utendaji unaotukuka lazima tuwe na muongozo wa nini kifanyike, wakati gani, kwa utaratibu upi na kwa rasilimali zipi, hatuwezi kuzungumza uchumi wa viwanda wala utekelezaji wa Dira ya Maendeleo bila sekta binafsi hivyo kuna kila haja ya kutengeneza mazingira wezeshi yatakayoifanya sekta ya umma isaidiane na ishirikiane kwa karibu na sekta binafsi ili yaliyopangwa yaweze kutekelezwa”, alisema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amesisitiza wahusika kutoa mrejesho wa majadiliano ya mabaraza ya biashara katika ngazi za mikoa na wilaya kwani kama yatafanyika maamuzi na kujiwekea malengo ambayo hayatekelezeki hakutakuwa na maana ya vikao hivyo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema kuwa muongozo huo ni kitendea kazi katika ngazi zetu za mikoa na wilaya kitakachowezesha uendeshaji wa mabaraza haya ambayo kwa kiasi kikubwa yataleta tija.

“Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Mikoa 26 ni mikoa 16 pekee ambayo ilifanya mabaraza hayo, sasa muongozo umeshatolewa hivyo miongoni mwa taarifa za wakuu wa Mikoa zinazoletwa TAMISEMI lazima taarifa ya Uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara katika mikoa yenu iwepo”, alisema Waziri Jafo.

Vile vile, Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa, Dkt. Godwill Wanga amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kupitia majadiliano kati ya sekta hizo mbili ambapo inasimamia kwa karibu majadiliano hayo kama njia muafaka ya kufikia maridhiano yatakayoboresha uchumi na maendeleo endelevu ya nchi.

“TNBC tunatoa wito kwa wadau wote kutumia majadiliano haya kuainisha matatizo ya miradi ya pamoja kati ya sekta hizi mbili inayolenga kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini”, alisema Dkt. Wanga.

Akiishkuru Serikali ya Awamu ya Tano, Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPFS), Rehema Mbogi amesema kuwa Serikali imeonesha umakini katika masuala yanayohusu majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Umma katika ngazi zote kwani sekta binafsi imekua ikishirikishwa katika mabaraza ya biashara pamoja na kupata nafasi za kujadiliana masuala mbalimbali viongozi wa Serikali.

“Mnamo mwaka juzi nilishiriki katika mkutano nchini Afrika Kusini uliohusu mfumo wa majadiliano katika nchi za Kusini mwa Afrika nilifurahishwa kuona kwamba nimesimamishwa kuelezwa kwamba nchi yetu Tanzania ina mfumo bora wa majadiliano unaoeleweka kuanzia ngazi ya Taifa hivyo hii ni fursa nzuri ambayo tukiitumia vizuri tunaweza kufika mbali katika nchi”, alisema Bi.Rehema.

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR IKULU

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, katika mkutano wa uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Ofisi hiyo kwa kipindi cha mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akiwasilisha  muktasari wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Ofisi yake kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Waziri) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na (kulia kwa Waziri) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.  Mihayo Juma N’hunga
BAADHI ya Wakurugenzi wa Idara za Ofisi  mbalimbali za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, wakifuatilia  mkutano huo wa uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020. Ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani)  uliuofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
BAADHI ya Maofisa wa Idara mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , wakifuatila taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi  kwa Ofisi yao kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, wakati Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo akiwasilisha Taarifa ya Mpango kazi, Ndg. Abdalla Hassan Mitawi,(hayupo pichani) mkutano  uliofanyika  ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Abdalla Hassan Mitawi akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kulia) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
KATIBU wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg.Mohammed Ali Abdalla, akijibu maswali yaliouliza katika mkutano huo wa uwasilishwaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020. Uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) (Picha na Ikulu)

Msafara wa kijinsia unaolenga kutokomeza vitendo vya kikatili kuelekea Siku ya Wanawake Duniani wazinduliwa rasmi mkoani Katavi.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Katavi

Msafara wa kijinsia unaolenga kutokomeza vitendo vya kikatili kuelekea Siku ya Wanawake Duniani umezinduliwa rasmi mkoani Katavi.

Akizungumza wakati akizindua Msafara huo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera amesema kuwa vitendo vya kikatili vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii zetu hivyo vinatakiwa kupatiwa mbinu ya kupambana navyo.

Ameongeza kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona wanawake na watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili hivyo itahakikisha inazishugulikia kesi zote za vitendo vya ukatili.

"Sheria ifuate mkondo hata mimi naweza kutelekezwa na hata mimi nikitelekeza nikamatwe tu" alisema

Mhe. Homera amesisitiza vyombo vya Sheria na Taasisi zisizo za Kiserikali kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanapata mbinu stahiki itakayosaidia kuondokana na vitendo vya ukatili.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bi. Imelda Kamugisha amesema lengo la msafara huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili na namna ya kupambana na vitendo hivyo kuelekea maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.

"Msafara huu umelenga kutoa elimu kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kuendeleza jitihada za Serikali na wadau katika kuhakikisha tunaondokana na vitendo vya kikatili" alisema

Naye Nurdin Bilal Maarufu Shetta amesema wasanii wameungana na Serikali katika kusambaza elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili ili kuwezesha kuondokana na vitendo hivyo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.

"Tuko tayari na tumeamua wasanii kuingia katika haya mapambano muhimu ya kitaifa dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii Caren Mitta kuhusu utaoji wa huduma za Ustawi wa jamii katika Msafara huo uliozinduliwa leo mkoani Katavi.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Katavi na wasanii mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia leo mkoani humo.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akieleza lengo la msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili uliozinduliwa leo Mkoani Katavi.
 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na wananchi wa Wilaya Mpanda wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia leo mkoani humo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta akitumbuzia wanafunzi wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkaoni Katavi.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiagana na Msanii Shetta mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkoani Katavi.

BoT KURASIMISHA MATUMIZI YA KWACHA YA ZAMBIA NA SHILINGI YA TANZANIA KWENYE MPAKA WA TUNDUMA/NAKONDE

PROF. KABUDI AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI AKIWA GENEVA - USWISI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akisaini katika kitabu cha wageni katika ubalozi  wa kudumu wa Tanzania umoja wa Mataifa uliopo Geneva Nchini Uswisi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika kikao cha 43 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika Geneva,Uswisi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand(hayupo Pichani). Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya Ofisi za UNHCR zilizopo Geneva-Uswisi

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani)
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya Ofisi za UNHCR zilizopo Geneva-Uswisi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya Ofisi za UNHCR zilizopo Geneva-Uswisi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Ofisi za UNHCR zilizopo Geneva-Uswisi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland Mhe. Simon Coveney. Mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu Geneva,Uswisi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland Mhe. Simon Coveney akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu Geneva,Uswisi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland Mhe. Simon Coveney mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu Geneva,Uswisi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa mambo ya Nje wa Denmark Bw. Jeppe Kofod.Mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu Geneva,Uswisi. Anayeshuhudia kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania umoja wa Mataifa Geneva,Balozi Maimuna Tarishi.
Viewing all 119390 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>