Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119361 articles
Browse latest View live

WALIMU MBWARA WAJICHANGA FEDHA KUWEKA UMEME MADARASANI

$
0
0




NA MWAMVUA MWINYI,RUFIJI 

WALIMU wa shule ya Sekondari ya Kata ya Mbwara ,Jimbo la Rufiji Mkoani Pwani, wameweka umeme katika vyumba vya madarasa shuleni hapo pamoja na nyumba wanazoishi kwa gharama ya sh.milioni tatu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa umeme iliyokuwepo .
Juhudi hiyo ,itasaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo ,kwani wanaweza kujisomea nyakati za usiku . 

Mwalimu Mkuu shuleni ya sekondari Mbwara, Millo Msovela, akieleza juu ya suala hilo wakati mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Zainab Vullu alipokwenda kuzungumza na wanafunzi na walimu shuleni hapo,alisema kwasasa changamoto ya ukosefu wa umeme imebakia katika mabweni ya wasichana. 

“Hatua hii imetokana na mafundi wa Tanesco kufika kijijini hapa na kuweka miundombinu hiyo, wakati shule ikiwa haina pesa, Mabweni ya wasichana, ilishindikana kutokana na kukosa shilingi laki nne za kuunganishia huduma hiyo,”alieleza Millo. 

Aidha alisema, pia shule inadaiwa sh. milioni kumi na Mzabuni aliyetengeneza vitanda 40 kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi 80 wa kike, kati ya 188 waliopo shuleni hapo ukiachilia mbali wavulana 162 wanaosoma kwenye shule hiyo ambapo wanatokea majumbani mwao. 

Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa, alipongeza hatua ya walimu kujichangisha fedha na kuvuta umeme, huku akiahidi kushirikiana na viongozi wenzake ili kurejesha fedha hizo na kuweka umeme katika eneo la mabweni ambalo limesalia. 

“Katika taarifa ya mwalimu imegusia changamoto ya deni la vitanda, nitawasiliana na taasisi ya TEA iliyoratibu mradi husika, kuhusu umeme katika mabweni nimewasiliana na meneja wa Tanesco ameniahidi ndani ya wiki mbili umeme utawaka hapa” alisema Mchengerwa. 

Nae Zaynab Vullu kabla ya kwenda kukabidhi vifaa tiba kwenye zahanati ya Kijiji cha Mbwara, akiwa shuleni hapo alikabidhi magodoro kumi, huku akiahidi mifuko mitano ya saruji ambapo ameunga mkono mifuko 15 iliyoaihidiwa na Mchengerwa kwa lengo la kukarabati sakafu kwenye majengo shuleni humo. 

Vullu hakusita kukemea mimba za shuleni na kuwaasa wanafunzi wa kike kuachana na vishawishi na tamaa za kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni, rift za bodaboda na chips na badala yake wajali masomo kwa manufaa yao ya baadae.

HOSPITALI YA TUNDURU WAANZA KUWATUMIA WAGANGA WA TIBA ASILI KUWAIBUA WAHISIWA WA KIFUA KIKUU

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Tunduru

BAADHI ya wananchi wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wameipongeza Serikali kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya ya Tunduru kuanza kuwatumia waganga wa Tiba asili na tiba mbadala waliosajiliwa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu na kutoa rufaa ya kwenda hospitali kupata matibabu.

Wananchi hao waliokutwa katika kitongoji cha Mdingula kijiji cha Namasalau wakipata tiba katika moja ya kilinge cha mganga maarufu wa tiba asili na tiba mbadala Hausi Mohamed wakipata huduma, wameishauri Serikali iendelea kuwaamini na kuwaunga mkono waganga hao kwani wana mchango mkubwa katika kutokomeza ugonjwa huo na kuokoa maisha ya watu.

Rahim Hussen na Mohamed Abdala walisema, iwapo Serikali itawatumia waganga wa Tiba asili kwenye kampeni na mkakati dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu, mafanikio yake yatakuwa makubwa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali wanaofika kwa waganga hao kwa ajili ya kupata huduma kutokana na shida zao.

Rahim alisema, kwenye vilinge vya waganga wa tiba asili kuna makundi makubwa ya watu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani na hata nchi jirani ya Msumbuji.

Alisema,ushiriki wao katika kuibua wahisiwa wa kifua kikuu wanaofika katika vilinge vyao na kuwapa rufaa ya kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo na matibabu wataokoa maisha ya wananchi wengi wenye maradhi hayo wanaokimbilia kwa waganga wa tiba asili.

Mohamed Abdala alisema, jamii kubwa inaaamini sana tiba mbadala kama suluhisho la matatizo waliyonayo kwani baadhi ya maradhi hayana tiba za kitaalam,lakini wanapofika kwa waganga wanapona kabisa na kuungana na familia zao na kushiriki katika kazi za maendeleo.

“sisi kama wananchi tunashukuru sana katika kijiji chetu kupata mganga wa tiba asili ambaye amekuwa mkombozi mkubwa wa shida zetu,tulikuwa na shida ambazo tulikwenda hospitali lakini hatukupona, na mara baada ya kuja kwa mganga afya zetu zimeimarika,naiomba Serikali iendelea kuwatumia na kushirikiana na waganga kwani ni msaada mkubwa kwetu sisi wananchi”alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema, tayari kuna waganga wa tiba asili zaidi ya arobaini wamepata mafunzo ya namna ya kuwaibua wagonjwa wenye maambukizi ya kifua kikuu na kuwapa rufaa kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

Dkt Kihongole ambaye ni mratibu wa tiba asili na tiba mbadala alisema,kutokana na tatizo kubwa la kifua kikuu katika jamii yetu Serikali imeona umuhimu wa kuwatambua na kuwashirikisha waganga hao katika kampeni yake ya kutokomeza TB ifikapo mwaka 2035.

Alieleza kuwa, lengo la kuwashirikisha waganga hao ni baada ya kubaini asilimia sitini kati ya mia moja ya Watanzania wanaamini na kukimbilia kwa waganga hao kupata matibabu kulingana na shida walizo nazo na asilimia arobaini tu ndiyo wanaofika Hospitali.

Alisema, moja kati ya mkakati wa Serikali katika kutokomeza TB ni kushirikiana na waganga ambao utasaidia kuwahisi wale wenye vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwapa rufaa kwenda Hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi badala ya kuwakumbatia jambo ambalo ni hatari kubwa kwa maisha ya waganga wenyewe na watu wengine.

Aidha Kihongole,amewataka waganga hao kuacha kufanya shughuli zao kwa kujificha bali wafanye katika mazingira rafiki, bora na safi ili kufikiwa kwa urahisi na watu wengi zaidi.

Alieleza wananchi waliokutwa katika Kilinge hicho kuwa, tiba asili ni salama kwani ilianza kutumiwa tangu enzi za Yesu Kristo na kuwataka viongozi kuanzia ngazi ya kijiji kuweka utaratibu mzuri utakao wezesha vijiji vyao kupata fedha kutokana na uchimbaji mizizi na miti dawa inayotumika kwa ajili ya tiba, badala ya kuwaachia waganga na watu kutoka nje ya wilaya hiyo wakinufaika na rasilimali za mitidawa inayopatikana kwa wingi katika wilaya ya Tunduru.

Mmoja wa Waganga wa tiba asili Hausi Mohamed(Babu Manjenje), ambaye ni mingoni mwa waganga waliopata mafunzo ya kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu, ameishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuona umuhimu wa kushirikisha katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu.

Alisema, kuna watu wengi wenye shida mbalimbali wanaofika katika Vilinge vyao kwa ajili ya kupata tiba, hivyo uamuzi wa Serikali kuwatumia waganga katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo utasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengi ambao wako hatarini kupoteza maisha kwa ugonjwa wa TB huku baadhi yao wakihusisha maradhi yao na Imani za kishirikina.

Babu Manjenje alisema, waganga wa tiba asili katika wilaya hiyo wote kwa pamoja wamekubali kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa huo ili kuokoa maisha ya watu Watanzania wenzao ambao bado wanaendelea kutokana na kukosa tiba sahihi ya magonjwa yanayowasumbua.

Ameipongeza Hospitali ya wilaya kwa kutoa mafunzo kwa waganga kwani yatasaidia wao kuwatambua wagonjwa wenye viashilia vya ugonjwa huo wanaofika katika vilinge kupata tiba na kusisitiza kuwa,mafunzo hayo yataepusha waganga wa tiba asili kuuwa watu wanaofika katika vilinge huku wakiwa na matatizo ambayo matibabu yake ni ya kitaalam. 
 

CCM CHATO YASEMA WAZIRI KALEMANI AMEITENDEA HAKI ILANI

$
0
0
Veronica Simba – Chato

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato kimekiri kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt Medard Kalemani.

Ameyasema hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Chato, Ramadhani Ndaki na kuongeza kuwa kwa utendaji kazi wake mahiri, Dkt Kalemani ameitendea haki Ilani ya Chama hicho ambacho ndicho kinaongoza nchi.

Kiongozi huyo wa Chama alikuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Waziri Kalemani kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Bukamila, Kata ya Kigongo, Februari 22, 2020.

“Utendaji kazi mzuri wa Dkt Kalemani umetupa matumaini sisi viongozi kuwa Ilani ya Chama inatekelezwa ipasavyo na kwakweli wakati ukifika, tutamtendea haki,” amesema Ndaki.

Akifafanua zaidi kuhusu utendaji kazi wa Dkt Kalemani, Ndaki alieleza kuwa, akiwa ni Waziri mwenye dhamana ya nishati, pamoja na mambo mengine, amefanya bidii kubwa kuhakikisha wananchi hasa walioko vijijini nchi nzima wanafikiwa na umeme.

Kwa upande wa Chato, Ndaki alieleza kuwa Dkt Kalemani amefanya makubwa katika sekta ya nishati ambapo mpaka sasa Kata zote 23 za Jimbo hilo zimekwishafikiwa na umeme.

Awali, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho cha Bukamila, Dkt Kalemani alibainisha kuwa hadi sasa jumla ya vijiji takribani 9,000 vimekwishaunganishiwa umeme nchini kati ya 12,268 vilivyopo, sawa na asilimia 74.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu, jumla ya vijiji 10,446 vitakuwa vimeunganishwa na umeme na kwamba ifikapo Juni 2021, vijiji vyote vya Tanzania Bara vitakuwa vimefikiwa na nishati hiyo.

Alimpongeza na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini na akaahidi kuwa yeye na viongozi wenzake waandamizi wa Wizara, wataendelea kusimamia vyema matumizi yake kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
 Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Chato, Ramadhani Ndaki, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, Chato. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Februari 22, 2020 alikuwa ni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani).
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akifurahia mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto), akiwatambulisha viongozi waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mbele ya wananchi wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.
 Kazi ya kuunganisha umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato ikiendelea. Taswira hii ilinaswa Februari 22, 2020 wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akiwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
 Baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Bukamila, wilayani Chato, Februari 22, 2020.

TUNDURU WAANZA KUWATUMIA WAGANGA WA TIBA ASILI KUWAIBUA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU

$
0
0

BAADHI ya wananchi wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameipongeza Serikali kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya ya Tunduru kuanza kuwatumia waganga wa Tiba asili na tiba mbadala waliosajiliwa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu na kutoa rufaa ya kwenda  hospitali kupata matibabu.

Wananchi hao waliokutwa katika  kitongoji cha Mdingula kijiji cha Namasalau wakipata tiba katika moja ya kilinge cha mganga maarufu wa tiba asili na tiba mbadala  Hausi Mohamed wakipata huduma, wameishauri Serikali iendelea kuwaamini na kuwaunga mkono waganga hao  kwani wana  mchango mkubwa katika  kutokomeza ugonjwa huo na kuokoa maisha ya watu.

Rahim Hussen na Mohamed Abdala walisema, iwapo Serikali  itawatumia waganga wa Tiba asili  kwenye kampeni na mkakati dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu, mafanikio yake yatakuwa makubwa  kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali wanaofika kwa waganga hao kwa ajili ya kupata huduma kutokana na shida zao.

Rahim alisema,  kwenye vilinge vya waganga wa tiba asili kuna makundi makubwa ya watu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani na hata nchi jirani ya Msumbuji.

Alisema,ushiriki wao katika kuibua wahisiwa  wa kifua kikuu wanaofika katika vilinge vyao na kuwapa rufaa ya kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo na matibabu wataokoa maisha ya wananchi wengi wenye maradhi hayo wanaokimbilia kwa waganga wa tiba asili.

Mohamed Abdala alisema, jamii kubwa inaaamini sana tiba mbadala kama suluhisho la matatizo waliyonayo kwani  baadhi ya maradhi  hayana tiba za kitaalam,lakini wanapofika kwa waganga wanapona kabisa  na kuungana na familia zao  na kushiriki katika kazi za maendeleo.

“sisi kama wananchi tunashukuru sana katika kijiji chetu kupata mganga wa tiba asili ambaye amekuwa mkombozi mkubwa wa shida zetu,tulikuwa na shida ambazo  tulikwenda hospitali  lakini  hatukupona, na mara  baada ya kuja kwa mganga  afya  zetu zimeimarika,naiomba Serikali iendelea kuwatumia na kushirikiana na waganga kwani ni msaada mkubwa kwetu sisi wananchi”alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema, tayari  kuna waganga wa tiba asili zaidi ya arobaini  wamepata mafunzo ya namna  ya kuwaibua  wagonjwa wenye maambukizi ya kifua kikuu na kuwapa rufaa kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

Dkt Kihongole ambaye ni mratibu wa tiba asili na tiba mbadala alisema,kutokana na tatizo kubwa la kifua kikuu katika jamii yetu Serikali imeona umuhimu wa kuwatambua na kuwashirikisha waganga hao katika kampeni yake ya kutokomeza TB ifikapo mwaka 2035.

Alieleza kuwa, lengo la kuwashirikisha waganga hao ni baada ya kubaini asilimia sitini  kati ya mia moja ya Watanzania wanaamini na kukimbilia kwa waganga hao kupata matibabu kulingana na shida walizo nazo na asilimia arobaini tu ndiyo wanaofika Hospitali.

Alisema, moja kati ya mkakati wa Serikali katika kutokomeza TB ni kushirikiana na waganga ambao  utasaidia  kuwahisi wale wenye  vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwapa rufaa kwenda Hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi badala ya kuwakumbatia jambo ambalo ni hatari kubwa kwa maisha ya waganga wenyewe na watu wengine.

Aidha Kihongole,amewataka waganga hao kuacha kufanya shughuli zao kwa kujificha bali wafanye katika mazingira rafiki, bora na safi  ili kufikiwa kwa urahisi na watu wengi zaidi.

Alieleza wananchi waliokutwa katika Kilinge hicho kuwa, tiba asili ni salama kwani ilianza kutumiwa tangu enzi za  Yesu Kristo  na kuwataka viongozi  kuanzia ngazi ya kijiji kuweka utaratibu mzuri utakao wezesha vijiji vyao kupata fedha kutokana na  uchimbaji mizizi na miti dawa inayotumika kwa ajili ya tiba, badala ya kuwaachia waganga na watu kutoka nje ya wilaya hiyo wakinufaika na rasilimali za mitidawa inayopatikana kwa wingi katika wilaya ya Tunduru.

Mmoja wa Waganga wa tiba asili    Hausi Mohamed(Babu Manjenje), ambaye ni  mingoni mwa waganga waliopata mafunzo ya kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu, ameishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuona umuhimu wa kushirikisha  katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu.

Alisema, kuna watu wengi  wenye shida mbalimbali wanaofika katika Vilinge vyao kwa ajili ya kupata tiba, hivyo uamuzi wa Serikali kuwatumia waganga katika  mapambano dhidi ya ugonjwa huo utasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengi ambao wako hatarini kupoteza maisha kwa ugonjwa wa TB huku baadhi yao  wakihusisha maradhi yao na Imani za kishirikina.

Babu Manjenje alisema, waganga wa tiba asili katika wilaya hiyo wote kwa pamoja wamekubali kushiriki kikamilifu katika kampeni ya  kutokomeza ugonjwa huo ili kuokoa  maisha ya watu Watanzania wenzao ambao  bado wanaendelea kutokana na kukosa tiba sahihi ya magonjwa yanayowasumbua.

Ameipongeza Hospitali ya wilaya kwa kutoa mafunzo kwa waganga kwani yatasaidia wao kuwatambua wagonjwa wenye viashilia vya ugonjwa huo wanaofika katika vilinge kupata tiba na kusisitiza kuwa,mafunzo hayo yataepusha waganga wa tiba asili kuuwa watu wanaofika katika vilinge huku wakiwa na matatizo ambayo  matibabu yake ni ya kitaalam.

Mganga wa tiba asili na tiba mbadala Huasi Mohamed aliyevaa shuka nyeupeambaye ameepata mafunzo ya kuwaibua na kuwahisi wagonjwa wa kifua kikuu wanaofika katika kilinge akiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa kifua kikuu,ukoma na tiba asili katika Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole wa pili kushoto na baadhi ya wazazi wake,Mganga huyo amekuwa msaada mkubwa katika kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu wanaofika kwake kwa ajili ya kupata huduma ambapo wale wanaohisiwa wanapewa rufaa ya kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Serikali yaimarisha usikivu wa TBC kwa asilimia zaidi ya 73.

$
0
0
Serikali yaimarisha usikivu wa TBC kwa asilimia zaidi ya 73. Shamimu Nyaki-WHUSM, Dodoma Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni chombo cha Habari cha Umma chenye wajibu wa kuhabarisha kuelimisha pamoja na kueleza mikakati ya Serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Katika kuhakikisha yote hayo yanafanyika Serikali inafanya juhudi kubwa za kuimarisha usikivu wa Shirika hilo katika mikoa yote ya Tanzania ili wananchi wapate taarifa sahihi zilizokusudiwa tena kwa wakati.

Moja ya mikakati ambayo Serikali imeweka katika kuimarisha usikivu wa Shirika hilo ni kubadilisha mitambo ya zamani na kuweka mipya na kuhamisha mitambo kutoka sehemu ambayo mawimbi ya FM hayafiki na kuipeleka maeneo ya vilima vilivyopo juu zaidi ambapo wataalamu wameona kuwa ndio maeneo sahihi yatakayosaidia kupeleka mawimbi ya redio na televisheni kuwafikia wananchi nchi nzima.

Shirika hili chini ya uongozi wake Mkurugenzi Mkuu Dkt. Ayoub Ryoba linaendelea kuweka mipango na mikakati ya kuhakiksha wananchi wanapata habari ambapo matarajio ni kukakikisha usikivu wa redio unzifikia wilaya 117 nchi nzima.

Serikali imefanya mageuzi makubwa katika kuhakikisha usikivu unaimarika ambapo umeongezeka kutoka Wilaya 87 mwaka 2017 sawa na asilima 54 hadi wilaya 102
mwaka 2019 ambapo pia imejenga vituo vitano ambavyo tayari ujenzi wake umekamilika na vimeanza kutumika.

Wilaya za mpakani ndizo zimenufaika na ujenzi huo ikiwemo Rombo, Kibondo, Tarime, Kankonko, Longido eneo la Namanga, Nyasa hadi Mbambabay.

Yapo maeneo ambayo usikivu ni hafifu hali ambayo imeilazimu Serikali kuweka mitambo ya redio katika ameneo yenye changamoto hiyo ambayo katika mikao
mitano ya Lindi, Katavi, Njombe, Simiyu, Songwe ambapo nguvu hiyo pia inaelekezwa katika mikoa ya Unguja na Pemb..

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa TBC inaendelea na mpango wa kupanua usikivu maeneo
yote ya nchi ili wananchi wengi wapate manufaa ya shirika lao ambapo amesema lengo la Serikali ni kuiwezesha TBC Redio kufikia usikivu nchi nzima kama ambavyo TBC Televisheni inaonekana kupitia visimbuzi na satellite vyote zilizosajiliwa nchini.

Ni dhahiri ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyoifanya hivi karibuni katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro,
Arusha, Manyara na Singida ilikuwa ni muendelezo wa ziara za kikazi ambayo ilikuwa na lengo la kuona na kujiridhisha kuhusu usikivu wa TBC katika maeneo
hayo na hatua zilizochukuliwa na shirika hilo katika kutatua changamoto zinazowakabili ili kuhakikisha matangazo ya redio yanawafikia wananchi wote
inavyotakaiwa kwa wakati ikiwa ni haki yao ya msingi ya Kikatiba ya kupata taarifa za Serikali.

Akiwa katika Mkoa wa Tanga Dkt. Mwakyembe alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha usikivu wa matangazo ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kuimarisha mitambo ya kurushia matangazo katika kituo cha Mnyusi kilichopo Hale wilaya ya Korogwe na Kwemashai wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Dkt. Harrison Mwakyembe alisema kuwa usikivu wa TBC Taifa mwaka 2015 ulikuwa ni asilimia 54 ambapo kwa sasa baada ya Serikali kuboresha vituo hivyo usikivu umefikia kiwango cha asilimia 73 na inatarajiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020 utafikia zaidi ya asilimia 90.

Katika Mkoa wa Kilimanjaro Waziri Mwakyembe alitembelea kituo cha TBC Taifa Mabungo kilichopo wilayani Moshi kinachorusha matangazo katika masafa ya FM 87. 9 Mhz na TBC FM katika masafa ya 90.0 Mhz pamoja na kituo cha Tarakea kilichopo katika Wilaya ya Rombo ambacho matangazo ya TBC Taifa yanapataikana kupitiamasafa ya 87.9Mhz na TBC FM inarusha kupitia 90.0 Mhz.

Akiwa mkoani Arusha Dkt.Mwakyembe alitembelea eneo la Themi ambalo ndio mitambo ya TBC imewekwa ambayo inarusha matangazo yake kupitia masafa ya 89.9 Mhz kwa FM na 87.7 Mhz pamoja na kituo cha cha Namanga kilichopo katika Wilaya la Longido.

Hata hivyo usikivu umeendelea kuimarishwa katika mikoa ya Singida pamoja na Manyara ambayo pia Waziri mwenye dhamana ya habari alifanya ziara ya kikazi katika mikoa hiyo kukagua hali ya usikivu na kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayoub Ryioba ambaye alitoa taarifa kuwa mkoa wa Singida ulikua na changamoto ya usikivu baada ya mtambo kuharibika ambapotayari Serikali imechukua hatua ya kutafuta mitambo mingine.

Dkt. Ryoba amesema kuwa mitambo miwili ya Khts 2 sawa na Wats 2000 imeshawasili nchini tayari kwa kufungwa katika eneo la Mikumbi Mkoani hapo ili kuongeza usikivu katika maeneo mengi ya mkoa huo ambao matarajio nikuimarisha usikivu kwa zaidi ya asilimia 70 mwishoni mwa mwaka huu.

“Hizi jitihada kubwa kwa Serikali za kuhakikisha kuwa inatekeleza Ibara ya 18 d ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoeleza kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata taarifa sahihi, hivyo ni jukumu la Serikali kuweka mazingira bora kwa vyombo vya habari kutoa habari bila changamoto zozote na kuzifikisha kwawalengwa kwa usahihi na kwa wakati” alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Aidha, Dkt. Mwakyembe alipata pia fursa ya kutembelea mkoa wa Manyara ambapo tayari Serikali imeanza kuhamisha mitambo ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoka katika jengo la Mkoa wa Manyara kupeleka katika eneo la Gitsmii ambalo lina mwinuko utakaosaidia kuimarisha usikivu katika mkoa huo ambao nao una
kabiliwa na changamoto ya kutosikika vizuri kwa matangazo ya TBC katika maeneo mengi.

Waziri Mkwayembe alisema kuwa Serikali inafahamu changamoto ya usikivu wa TBC Manyara ndio maana wataalam wamekuja na suluhisho la changamoto hiyo yakuhamisha mtambo kupeleka eneo ambalo wameona litarahisisha upatikananji wa wa matangazo vizuri.

Katika ziara yake katika mikoa hiyo, Waziri amejionea changamoto ya miundombinu mibovu ya kufika eneo la mitambo ambapo alitoa maagizo kwa mikoa hiyo kushirikiana na TANROADS, TANESCO pamoja na Idara ya Maji kutatua changamoto hizo za barabara pamoja na umeme ili kuhakikisha wanaweka miundombinu rafiki kwa ajili ya ulinzi wa mali ya umma kwa manufaa ya wananchina taifa kwa ujumla.

Dkt. Mwakyembe alieleza kuwa barabara za kuelekea kituo cha Gitsmii Manyara, Mnyusi Hale pamoja na kwemashai Lushoto zinapaswa kujengwa kwa lami au zengekwakuwa sehemu hizo zina miinuko mikali pamoja kona nyingi, ambapo vituo vya Namanga Wilayani Longido, Mbungo Moshi na Themi Arusha vinahitaji barabara yalami pia.

Hata hivyo Wakuu wa Mikoa hiyo wameahidi kutekeleza maagizo hayo ambayo ni kipaumbele kwa wananchi ili waweze kupata matangazo ya redio yao kwa kuwa inalengo la kuhabarisha, kuelimisha, kuonya pamoja na kuburudisha na wameunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha usikivu katika maeneo yao.

Kwa upande wao Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe na Agnes Hokororo wilaya ya Rombo wamesema kuwa kwa sasa TBC imekuwa chanzo kikuu kwa wananchi wa wilaya zao kupata taarifa za maendeleo ya nchi zao tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo wananchi walikuwa wakipata taarifa kutokanchi za jirani.

Wananchi katika mikoa ambayo Waziri Dkt. Mwakyembe alitembelea wamesema kuboreshwa miundombinu kufika maeneo ambayo TBC imesimika mitambo yake yakurusha matangazo ikiwemo barabara, umeme na maji itasidia pia kuboresha maisha yao kiuchumi na kijamii na itasaidia kuwa kiunganishi kikubwa katika kuletamaendeleo ya kaya zao pamoja na Taifa.

Mashinji akutana na viongozi Chadema,Hukumu yao sasa Machi 10

$
0
0
IKIWA ni siku Chache tangu kukihama Chama cha Chadema na kuhamia CCM leo Februari 24,2020 aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Vincent Mashinji amekutana na viongozi wa chama hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yao ya uchochezi inayowakabili.

Mashinji amefika mahakamani hapo kisha akaanza kusalimiana na viongozi mbalimbali wa CHADEMA ambao wapo katika kesi moja ambapo miongoni mwao ni Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Salum Mwalimu.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Kawe Halima Mdee alikataa kumpatia mkono Mashinji huku akiwa busy na simu yake ya mkono.

Aidha Dkt. Mashinji alionana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama licha ya kuwa hawakupeana mikono na mpaka anaondoka mahakamani hapo hawakuonekana kusalimiana.

Hata hivyo Mahakama imepanga kutoa hukumu dhidi ya vigo hao wa CHADEMA Machi 10, mwaka huu.

RAIS DKT. SHEIN AMEKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi kwa robo mbili ya Julai-Disemba 2019/2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu)
 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Nd,Marium Abdalla Saadala (kushoto) pamoja na watendaji mbali mbali katika Wizara hiyo wakiwa katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa robo mbiili ya Julai-Disemba 2019/2020, kilichofanyika leo ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Ikulu Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Manga Mjengo Mjawiri(kushoto) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Mpango kazi kwa robo mbili ya kipindi cha Julai-Disemba 2019/2020 katika kikao cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar, Mwenyekiti wake akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee (kulia).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilikmo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi  Nd,Marium Abdalla Saadala  (kushoto) alipokuwa  akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mapango kazi kwa robo mbili Julai-Disemba 2019/2020  katika mkutano wa Wizara hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Raios wa Zanzib ar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Naibu Katibu Mkuu anayeshuhulikia (Mifugo na Uvuvi) Dkt.Omar (kulia)
 Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa robo mbili ya  Julai-Disemba 2019/2020 iliyosomwa katika kikao maalum kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambapo  Mwenyekiti wake alikuwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Wakuu wa Idara mbalimbali na Maafisa katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wakiwa  katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa robo mbili ya  Julai-Disemba 2019/2020 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi kwa robo mbili ya Julai-Disemba 2019/2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mtendaji,Wakala wa Serikali wa huduma za Matrekta na Zana za Kilimo, Affan Othman Maalim (katikati) akichangia katika kikao cha Utekelezaji wa Mapango kazi kwa robo mbili Julai-Disemba 2019/2020  katika mkutano wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) mwengine (kushoto) Mkurugenzi Idara ya Utumishina Uendeshaji Nd,Noah Saleh Said.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Nd,Mussa Aboud Jumbe (kushoto) alipokuwa akichangia katika kikao cha Utekelezaji wa Mapango kazi kwa robo mbili Julai-Disemba 2019/2020  katika mkutano wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi  uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), (Picha na  Ikulu)

BALOZI SEIF AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA UTII WAKATI WA KAZI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Watumishi wachanga na wale wanaoendelea na Majukumu  yao kwa sasa katika Taasisi za Umma na zile Binafsi kuzingatia kwa kina suala la Utii kwenye utekelezaji wa Kazi za kuhudumia Jamii mahali popote pale.

Alisema Utii ndio dhana nzito, sahihi na inayobeba ngao kubwa kwa Mtumishi ye yote na matokeo yake hujikuta akipata fursa nyingi zinazomuwezesha kuheshimika sambamba na kupanda daraja katika maeneo yake ya Kazi.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa wasia huo kufuatia Uongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kumfanyia tafrija ndogo ya kushtukiza baada ya kutimiza Miaka 78 ya Siku yake ya kuzaliwa ifikapo Tarehe 23 Febuari ya kila Mwaka.

Alisema yeye akiwa miongoni mwa Watumishi wa umri mrefu wa kazi usiopungua Miaka Sitini katika nafasi mbali mbali za Utumishi wa Umma ameshuhudia mambo mengi katika mafanikio ya huduma za Kijamii yaliyobebwa na dhana ya Utii uliotukuka.

“ Huwezi kupata mafanikio yoyote katika Taasisi iwe za Umma, Binafsi na hata Familia kama hutakuwa na Utii kwa wale waliokuzunguuka muda wote katika matendo yako ya kila Siku”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Balozi Seif  alieleza kwamba katika umri wake hata akiwa nje ya Utumushi wa Umma ataendelea kutoa busara zake kwa wale wote watakaokuwa tayari kuchota busara hizo muhimu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi pamoja na Watendaji wote wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote cha kuiongoza Wizara hiyo ndani ya Muda wa Miaka Tisa na Nusu.

Alisema Ushirikiano huo kwa kiasi kikubwa ndio ulioleta mafanikio makubwa ndani ya Wizara hiyo iliyo inayosimamia Shughuili za Serikali yanayoshuhudiwa na Wananchi walio wengi Mjini na Vijijini.

Akitoa shukrani kwa Niaba ya Uongozi na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Abdullah Hassan Mitawi alisema Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi ni Tanuri lenye mambo mengi yanayoweza kutumiwa na Watendaji wachanga.

Kaimu Katibu Mkuu Mitawi alisema tanuri hilo lililojaa busara, uzoefu pamoja na hekina  za takriban Miaka Sitini litakuwa chachu ya kuchotwa na Viongozi na Watendaji wachanga katika Utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya kuwatumikia Wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alizaliwa Mnamo Tarehe 23 Febuari Mwaka 1942 katika Kijiji cha Mgambo Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja na kupata Elimu za Dini na Dunia kama walivyo Watoto wote wa Ukanda wa Mwambao.

Balozi Seif alipata Mafunzo ya Ualimu Beit El Ras na kuanza Kazi ya Kufundisha katika Skuli ya Kinyasini iliyo jirani na Kijiji chake ambapo jitihada zake zilimuwezesha kuteuliwa kuhamia Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania akiwa Afisa wa Kawaida.

Aliendelea na wadhifa huo uliobadilika kila kukicha kutokana na Utii wake katika kazi iliyompandisha daraja na kuwa Balozi kamili wa kuiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi kirefu na Mataifa mbali mbali Duniani.

Balozi Seif Ali Iddi alistaafu Kazi kwa mujibu wa Utumishi wa Umma na kuamua kuingia katika ulingo wa Kisiasa uliomuewesha kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi {CCM} kwa Upande wa Zanzibar.

Ulingo huo wa Kisiasa ulimfungulia njia na kuchaguliwa na Wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo lililokuwa la Kitope kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi {CCM} katika Vipindi Viwili na kupata nafasi ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania Miaka Mitano ya awali.

Kutokana na Utii aliokuwa nao Balozi Seif  wakati bado akiendelea kuwa Mbunge wa Kitope Awamu ya Pili ulimshawishi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kumteuwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Baadae aliamua kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar nafasi iliyompa fursa ya Kuteuliwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya kipindi cha Miaka na Nusu sasa.

Balozi Seif  Ali Iddi wakati akiyafungua Mafunzo ya Vijana katika Chuo cha Ujasiri Amali cha Wadi ya Mahonda hapo kwenye Tawi la CCM Kitope “B” Mnamo Tarehe 15 Oktoba Mwaka 2018 alitoa kauli ya kutogombea tena nafasi ye yote ameshatangaza Rasmi kujipumzisha na shughuli za Kisiasa.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kumfanyia tafrija ndogo ya kushtukiza Bosi wao Mhe. Balozi Seif Ali Iddi baada ya kutimiza Miaka 78 ya Siku yake ya kuzaliwa kila ifikapo Tarehe 23 Febuari.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaasa Wafanyakazi kazi wake kuwa na Utii katika majukumu yao wakati walipomfanyia Tafrija ya Kushtukizia ya Siku yake ya Kuzaliwa.
  Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakishiriki kwenye tukio hilo la kushtukizia.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi akitoa shukrani kwa niaba ya Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi yake mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Mitawi akimlisha kipande cha Keki Balozi Seif kama ishara ya kumpongeza kwa kutimia Miaka 78. Picha na – OMPR – ZNZ.

KILIMANJARO MARATHON YAWAONYA WADANGANYIFU

$
0
0
Waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2020 wametoa onyo kalikwa washiriki wanaopanga kutumia njia za udanganyifu kushiriki mbio hizo kwa lengo la kujipatia medali na zawadi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji hao ilisema watu wa aina hiyo wamekuwa wakijitokeza kila mwaka huku wakitaka kushiriki kwa kutumia namba bandia. 

Mkurugenzi wa mbio hizo kitaifa, John Bayo alisema safari hii watashirikiana na jeshi la polisi na walinzikutoka kampuni ya Garda World kuwaondoa wadanganyifu hao na kuwashitaki ili sharia ichukue mkondo wake.

“Tunatoa onyo kali kwa wote wenye nia ya kutumia udanganyifu kwani hili ni kosa kubwa na tutawshitaki,” akisema na kutolea mfano wa wale ambao wanatumia namba za km 5 kumimbia mbio za Kilimanjaro Premium Lager KM 42 au za Tigo Km 21.

Alisema wengi hudanganya katika mbio hizi mbili kwa sababu zina medali na zawadi za fedha taslimu.

“Washiriki wote wanatakiwa kutambua kuwa tuna mtambo wa kisasa kabisa unaotunza muda na kumfuatilia kila mshiriki ambao unawezeshwa na mtandao wa Tigo wa 4G kwa hivyo tuna uwezo wa kuwanasa wadanganyifu wote kwa hivyo tunawaonya kwa sababu safari hii hatutawaachia bure tutawachukulia hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, zoezi la utoaji namba za kukimbilia kwa mbio za Km 42 na 21 lilianza kwa kasi ikiwemo pia kujiandikisha kwa mbio za km 5.

Baada ya hapo zoezi hilo litahamia Arusha kesho Jumanne na Jumatano katika hoteli ya Kibo Palace kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usiku na baadaye Moshi Februari 27 kuania saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni, Februari 28 saa nne asubuhi hadi saa mbili mchana na Februari 29 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni  baada ya hapo zoezi zima litasitishwa tayari kwa mashindano.

Wadhamini wa mwaka huu ni  Kilimanjaro Premium Lager-42km, TIGO 21km, Grand Malt-5km, Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Unilever, Absa Bank Tanzania Limited na watoa huduma rasmi ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.

Mbio hizo zitanfanyika Machi 1, katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.
 Wakazi wa Dar es Salaam wakichukua namba za kukimbilia kwa ajili yam bio za KM 42 za Kilimanjaro Premium Lager na Km 21 za Tigo na kujiandikisha kwa mbio za Km 5 za Grand Malt katika viwanja vya Mlimani City mwishoni mwa wiki. Zoezi hilo litahamia Arusha kesho Jumanne na Jumatano.





TANZANIA YASHINDA TUZO YA UTALII NCHINI INDIA

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kulia) akipokea Tuzo ya Utalii baada ya Tanzania kuibuka mshindi kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la Utalii wa Wanyamapori duniani nchini India kwa mwaka 2020 (The Best International Wildlife Destination) iliyotangazwa katika hafla ya kutoa tuzo hizo zilizotolewa na Jarida la Utalii la "Outlook Traveller Magazine" na kufanyika katika Hoteli ya Rossette jijini New Delhi, India tarehe 22 Februari 2020.
Mhe. Balozi Luvanda akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kutoa tuzo za utalii zilizotolewa na Jarida la "Outlook Traveller Magazine" na kufanyika katika Hoteli ya Rossette jijini New Delhi, India tarehe 22 Februari 2020. Tanzania iliibuka mshindi kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii wa wanyamapori duniani nchini India kwa mwaka 2020.
===============================================================

Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii wa wanyamapori duniani nchini India kwa mwaka 2020 (The Best International Wildlife Destination).

Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka H. Luvanda amepokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kihindi la “Outlook Traveller Magazine” katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Roseate jijini New Delhi kwa niaba ya Tanzania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na takriban washiriki 200.  

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “Outlook Traveller” lililoshirikisha wapiga kura 1,200,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka nchini India, washiriki kupitia jarida hilo wameichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii wa wanyamapori duniani.

Aidha, Shelisheli na Indonesia kwa pamoja zilishinda tuzo kama maeneo bora zaidi duniani kwenye utalii wa fukwe.

The Outlook Traveller Award ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini India na hutolewa na Jarida la Utalii la “Outlook Traveller Magazine” ambalo ni jarida namba moja nchini India linalojishughulisha kutangaza utalii, ndani na nje ya India.

Wakati akipokea tuzo hiyo, pamoja na mambo mengine Balozi Luvanda aliushukuru uongozi wa Jarida hilo kwa kuandaa tuzo hizo muhimu ambazo zinasaidia kutanganza utalii wa nchi mbalimbali nchini India na akaeleza kuwa kupitia tuzo hiyo, watu wengi zaidi wataijua Tanzania na vivutio vingi vya utalii vilivyopo nchini na kuwavutia kutembelea Tanzania.

Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini India, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo India.

Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka India imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo iliongezeka kutoka watalii 39,115 mwaka 2016 hadi watalii 69,876 mwaka 2017.  

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Balozi zake ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini India na wadau wengine itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kuhakikisha idadi ya watalii kutoka India na nchi zingine duniani inaongezeka. Hii ni pamoja na kutumia Shirika la Ndege la Tanzania ambalo limeanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai kuanzia mwezi Julai 2019 kwa upande wa India.

Wazalishaji watakiwa kuzingatia viwango

$
0
0
Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali mkoani Singida wametakiwa kutambua kuwa suala la viwango ni la kisheria hivyo ni lazima kuthibitisha ubora wa bidhaa ili kumlinda mlaji na kupata uhakika wa soko la bidhaa wanazozizalisha.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipokuwa akifungua mafunzo ya wazalishaji wa bidhaa za vyakula yakiwemo mafuta ya alizeti na wauzaji wa vipodozi na vyakula yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA mkoani Singida. Dkt. Nchimbi alisema suala la ubora wa bidhaa linapaswa kuzingatiwa katika mnyororo wote wa uzalishaji ili mlaji awe salama na kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kutozingatia viwango.

“Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ndiyo hakikisho la wazalishaji na fursa zinazotengenezwa zitakuwa dhahiri iwapo masuala ya viwango yatazingatiwa, vilevile TBS ni daraja kati ya mzalishaji na soko, hivyo mzalishaji ni lazima kufuata utaratibu,” alisisitiza Dkt. Nchimbi.

Alisema maisha ya binadamu ni chakula hivyo ni muhimu kuzingatia usalama wake, kwani bidhaa hafifu zinagharimu afya ya walaji na kwamba magonjwa mengi yanatokana na jinsi tunavyoandaa chakula na tunavyokula, hivyo wazalishaji wanapaswa kuwa waaminifu katika kuzalisha bidhaa yoyote. Dkt. Nchimbi alisema TBS siyo adui wazalishaji hawapaswi kuichukia na wajenge dhana kuwa TBS ni usama hivyo wazalishaji wa Singida wahakikishe kuwa wanazalisha bidhaa bora wakati wote ili kudhidhirisha kauli kwamba Singida ni njema wakati wote.

Akizungumzia kwa upande wa TBS, Dkt. Nchimbi alisema Shirika linapaswa kuangalia namna ya kuongea na wajasiriamali ili kuhakikisha kuwa yale wanayowafundisha wanaelewa kikamilifu. Mafunzo haya yawe na kipimo ili kujua kama yameeleweka vizuri na kwamba watakaopokea mafunzo ndiyo watakaowapima. Kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Utafiti kutoka TBS Bw. Hamisi Sudi alisema Shirika litaendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali ili kuhakikisha kuwa wanazalisha bidhaa kwa kuzingatia viwango.

Alisema Shirika linatambua kuwa wajasiriamali wana mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi hivyo Shirika lina mchakato endelevu wa kutoa elimu kwa jamii hasa wajasiriamali kwakuwa ni mojawapo ya majukumu yake ya kila siku.

Shirika likiwa mkoani Singida limetoa mafunzo kwa wajasiriamali 221 Katika wilaya za Iramba, Singida na Manyoni, ambayo pia yamewashirikisha watendaji wa Halmashauri wakiwemo maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii na Afya pamoja na Maafisa kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO). Pia Shirika linatarajia kutoa mafunzo katika wilaya za Kondoa, Kongwa na ikiwa ni muendelezo wa mafunzo katika Kanda ya Kati.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo maalum kwa wazalishaji wa mafuta ya alizeti pamoja na wauzaji wa bidhaa za vyakula na vipodozi, mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa VETA mkoani Singida, wengine walioketi kulia ni Afisa Biashara wa mkoa wa Singida Bw.Daniel Munyi, wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Mafunzo na Utafiti kutoka TBS, Bw. Hamisi Sudi, kushoto ni Meneja wa SIDO Singida, Bi Agnes Yeseya na wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa Mkanda ya Kati - TBS Bw. Sileja Lushibika.

VULLU AKABIDHI VIFAA TIBA KIKONGO

$
0
0
MWAMVUA MWINYI, PWANI
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Pwani Zaynab Vullu, amekabidhi vifaa tiba katika zahanati za Kikongo na Disunyara, Kibaha Vijijini lengo ni kuwapunguzia changamoto wagonjwa wanaopatiwa tiba kwenye zahanati hizo.
 Akizungumza kwenye zahanati ya Kikongo kabla ya kukabidhi vifaa hivyo ikiwemo mashuka, vipomo vya presha, sukari, apron za kuvaa kifuani na mipira ya kitanda ya kuzuia shuka zisichafuke, Vulu amesema kuwa kwa uchache wake ameamua kufika hapo kukabidhi vifaa tiba hivyo.

Pamoja na hayo, Vullu amekitembelea kikundi cha Umoja ni Nguvu kilichopo Kikongo, ambacho amekikabidhi cherehani moja na jora la kitambaa kitachotumika kuwashonea sketi na kaptura wanafunzi 70 wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wakisaidiwa na kikundi hicho.
 Alisema,ametoa misaada hiyo kutokana na kuguswa na changamoto hizo ili kupunguza upungufu uliopo.

"Nilishakuja kukabidhi tenki hili la maji, leo nawakabidhi vifaa hivi vichache ambavyo nina imani vitatusaidia katika kuwapatia huduma wananchi wetu," alisema Vulu.

Pia zahanati ya Kilangalanga, ambapo mganga Mkuu wa zahanati hiyo Raya Mohamed alishukuru na kutaja changamoto nyingine ya vipimo vya presha na kisukari vimeharibika.
Akizungumza na wanakikundi wa Umoja ni Nguvu kabla ya kuwakabidhi cherehani na jora la kitambaa, Vullu alisema , amefika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Humoud Jumaa, alipokuwa kwenye hafla ya kumaliza mzunguko wa mwaka, ambapo alitoa ahadi za wabunge watatu wa Viti Maalumu.

NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA AWATAKA WATUMISHI NIDA KUTUNZA SIRI, KUSHIRIKIANA NA KUWAJIBIKA

$
0
0
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (katikati) akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kailima aliwataka watumishi wa NIDA kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa, pamoja na kutunza siri za ofisi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Arnold Kihaule. Kushoto ni Katibu wa Baraza, Lulu Ishengoma.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (wapili kushoto meza kuu), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule (wapili kulia meza kuu), Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Hassa Hassan (kulia), Katibu wa Baraza hilo, Lulu Ishengoma (kushoto), wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule akizungumza katika Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Mgeni rasmi wa Kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (wapili kushoto) aliwataka watumishi wa NIDA kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa, pamoja na kutunza siri za ofisi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hassan Hassan. Na kushoto ni Katibu wa Baraza, Lulu Ishengoma.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati alipokuwa anawasili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (katikati) akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kailima aliwataka watumishi wa NIDA kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa, pamoja na kutunza siri za ofisi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Arnold Kihaule. Na kushoto ni Katibu wa Baraza, Lulu Ishengoma.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Felix Mwagara, MOHA.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amewataka watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji na kutunza siri za ofisi kwa mujibu wa sheria. 

Akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Tawi la NIDA, Kailima alisema mafanikio ya Mamlaka hiyo ni pamoja na kushirikiana katika utendaji wa kazi ili kuleta weledi, na pia kuepuka kutoa siri za ofisi kwa mujibu wa utaratibu wa utumishi wa umma. 

Pia aliwakumbusha watumishi hao kutoka Makao Makuu ya NIDA na Ofisi zake Mikoani, kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa kwa kufanyiwa kazi kile kinachotakiwa kufanyiwa kazi na kisichohitajika kuifanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria. 

“Tukoseane kwa nia ya kuboresha, tusikoseane kwa nia ya kubomoa kwa sababu ya kupata fursa hii ya kuwa na haki na hadhi sawa, na pande zote mbili ziwajibike kuwajibishana,” alisema Kailima.

Aliongeza kuwa, watumishi wanapaswa kupewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka na masuala yanayowahusu kwa utaratibu wa ofisi au unaoidhinishwa na Mkurugenzi Mkuu na si vinginevyo. 

“Muhakikishe mnatoa huduma kwa wananchi sehemu zote nchini kwa weledi, maafisa wafike mapema katika maeneo ya kazi na kutoa vitambulisho vya Taifa mapema, na wananchi waridhike na huduma hiyo mnayoitoa, kwa hatua hiyo mtapunguza malalamiko ya wananchi,” alisema Kailima.  

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Arnold Kihaule alitoa mafanikio ya Mamlaka yake hadi kufikia Desemba mwaka 2019, alisema NIDA imefanikiwa kusajili wananchi 21,511,321, Wageni wakaazi, 19,311 na Wakimbizi 274,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

“Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imezalisha namba za utambulisho 16,211,654 na kutoa vitambulisho 5,787,869, na vimewafikia wananchi ilipofika mwezi Desemba 2019,” alisema Dkt. Kihaule.

Kikao cha Baraza hilo cha siku moja pia kilipitia Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2019/20 kwa Kipindi cha kwanza cha Mwezi Julai hadi Desemba na Makadirio ya Bajeti ya Mamlaka kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUMU WA KANSELA WA UJERUMANI NA PROFESA PLO LUMUMBA IKULU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Afrika wa Kansela wa Ujermani Bw. Guenter Nooke alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Afrika wa Kansela wa Ujermani Bw. Guenter Nooke alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Afrika wa Kansela wa Ujermani Bw. Guenter Nooke baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Afrika wa Kansela wa Ujermani Bw. Guenter Nooke na ujumbe wake alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Ibuge
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi ya kinyago cha Umoja Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Afrika wa Kansela wa Ujermani Bw. Guenter Nooke alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwamini wa Muunganiko wa Bara la Afrika kutoka Kenya Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba ( Maarufu zaidi kama Profesa PLO Lumumba) alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwamini wa Muunganiko wa Afrika kutoka Kenya Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba ( Maarufu zaidi kama Profesa PLO Lumumba) alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi ya kinyago cha Umoja Mwamini wa Muunganiko wa Afrika kutoka Kenya Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba ( Maarufu zaidi kama Profesa PLO Lumumba) alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mwamini wa Muunganiko wa Afrika kutoka Kenya Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba ( Maarufu zaidi kama Profesa PLO Lumumba) baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwamini wa Muunganiko wa Afrika kutoka Kenya Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba ( Maarufu zaidi kama Profesa PLO Lumumba) baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 24. 2020. PICHA NA IKULU

MASHINE NNE ZA UTRA SOUND KUFUNGWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE

$
0
0
 Muonekano wa hospitali ya Rufaa ya Temeke.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akitembelea maeneo ya ospitali ya Rufaa ya Temeke.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisikiliza wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, alipotemelea hospitali hiyo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
HOSPITALI ya Rufaa ya mkoa wa Temeke mbioni kufungwa mashine nne za Utra Sound  kwaajili kuongeza ubora wa huduma za Afya katika hospitali hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar ea Salaam leo.

Waziri Ummy alipofika katika Hospitali ya Temeke aliongea na wagonjwa waliokuwepo hospitali hapo.

Mmoja ya wangonjwa ametoa lalamiko hukusu ukosefu wa mashine za Utra Sound pamoja na mfumo wa malipo ambao haujakaa sawa.

Amepotolea majibu malalamko yao juu ya mashine hizo amesema kuwa mashine hizo zitafungwa katika hospitali hiyo.

Hata hivyo ametoa rai kwa wakazi wa jiji la Dar es Saalam kufuata  mfumo wa Rufaa na kutokukimbilia moja kwa moja katika hospitali ya Temeke.

"Nitoe rai kwa wakazi wa Dar es Salaam tufuate mfumo wa rufaa tusikimbilie moja kwa moja Temeke kuna baadhi ya huduma zinaweza zikapatikana katika vituo vya afya pamoja na hospitali ya wilaya. Sisi kama serikali tunaboresha vituo vya afya na katika vituo vyote vya afya, tutaweka mashine za  Utra Sound na kunabaadhi tumeshaanza kuweka mashine za RMO kwahiyo kwa kiasi kikubwa huduma za afya zote zitakuwa zinapatika katika vituo vya afya na Temeke ukija hapa tunataka kwaajili ya huduma za kibingwa." Amesema Waziri Ummy.

Na alipotembelea wagonjwa waliokuwa katika foleni ya dirisha la bima za afya hapo aliwashauri wananchi kutumia bima za afya ili kuepukana na gharama zisizo za lazima.

Hata hivyo waziri Ummy ameridhishwa na utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Temeke ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo kulikuwa na mapungufu.

"Mimi napenda kumpongeza Dkt. Shimwela tulimleta hapa septemba 2019 Temeke ya 2019 na ya 2020 ni tofauti amejiongeza kwa kupaka rangi majengo pamoja na kuanzisha huduma mbalimbali za kibingwa." Amesema Waziri Ummy.

Hata Waziri Ummy ametembelea wodi la wazazi na kuwapongeza madaktari na watoa huduma kwa kupunguza vifo vya kinamama.

"Kubwa ambalo tumeliona ni kupungua kwa vifo vya kinamama wajawazito 2018 vifo vya kinamama 16, 2019 vifo 8 lakini pia ukiangalia takwimu zao kuanzia Novemba 2019 hadi sasa hakuna mwanamke yeyote mjamzito ambaye amekuja Temeke akapoteza maisha, kwa hiyo hili sasa ninataka kuwapongeza Madaktari, wauguzi na watoa  huduma za Afya pamoja na maafisa Afya." Amesema Waziri Ummy.

Haya hivyo hospitali ya Rufaa ya Temeke kwa sasa inatoa huduma ya Afya ya meno.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dkt. Shimwela ameshukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwani minong'ono ya uzushi iliyokuwa ikiendelea kuhusiana na kubadilishana watoto hicho kitu hakipo kwa sababu ya uboreshaji wa huduma pamoja na vifaa mhimu vya kisasa vilivyoletwa.

"Hakuna mtoto ambaye alibadilishana kwa kuwa vipimo vya DNA na vifaa vya kisasa vinaonyesha."

SPIKA NDUGAI ATOA NENO KWA VIONGOZI WAKUU WA DINI KUHUSU MAPAMBANO DHIDI VIRUSI VYA UKIMWI, UNYANYAPAA

$
0
0
 Na Mwandishi Wetu, Michuzi Globu ya jami
SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameziomba  taasisi za dini pamoja na viongozi wakuu wa dini zote kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI huku akitoa rai ya kuondoa unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Ametoa ombi hilo jijini Arusha wakati akifungua mkutano maalum ulioandaliwa na ofisi yake kupitia NACOPHA chini ya mradi wa Hebu Tuyajenge unaofadhiliwa na USAID kutoka kwa watu wa Marekani. Mutano huo ulihusisha Taasisi na viongozi wakuu wa dini nchini, TACAIDS pamoja na wadau mbalimbali wanaoshughulikia maswala ya VVU,  kwa lengo la kuweka mkakati wa pamoja wa kujadili na kuona njia sahihi  zinazoweza kutumika kukabiliana na maambukizi ya ya Virusi vya UKIMWI.

Akizungumza zaidi wakati wa mkutano huo Spika Ndugai amewaambia viongozi wa dini na wadau wengine kuwa  zipo sababu nyingi   zinazorudisha nyuma mwitikio wa juhudi za kutokomeza maambuki ya VVU ikiwemo ya  unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo nchini.

Hivyo ametoa mwito kwa viongozi wa dini nchini kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na changamoto hizo huku akieleza kuwa wao Bunge nalo chini ya  ushauri wa wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya masuala ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Dawa za Kulevya inayoongozwa na Oscar Mukasa(Mb) na kwa kushirikiana na wadau mbali itahakikisha inafikia malengo ya 95-95-95.

Ndugai amefafanua asilimia 95 ya watu wawe wanatambua hali zao za maambukizi na asilimia 95 wawe wanatumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI na asilimia 95 ya walio katika dawa wawe na kiwango cha chini cha Virusi vya UKIMWI ifikapo mwaka 2030 na kwamba moja ya mambo makubwa kabisa yanayokwaza ni unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI lakini pia hiyo inasababisha wapimaji kupungua sana. 

"Tumeona tushirikiane nanyi viongozi wa dini ili kuondokana na tatizo hili kubwa la unyanyapaa,Katika ushirikiano wetu, Bunge tutatekeleza wajibu wetu wa kutunga sheria dhidi ya unyanyapaa, tutaishauri Serikali hatua madhubuti za kuchukua dhidi ya unyanyapaa na pia tutakuwa tukiomba kutoka Serikalini taarifa za utekelezaji ili zitusaidie wote kujua tulipo na tunapoelekea katika kufanikiwa kutokomeza unyanyapaa na hili linawezekana tukifanya kazi kwa pamoja,"amesema Ndugai

Ameongeza mkutano huo kwa kiasi kikubwa ni wa kujiandaa na mkutano mkubwa utakaofanya Dodoma Machi ambao utashirikisha wabunge wote, viongozi wa dini na kwa upande mwingine uwakilishi wa juu kabisa wa Serikali ili kuwakabidhi yale ambayo utatoa maazimio yao na kisha yafanyiwe kazi.

 Amesema siku hiyo itakuwa ni mjumuiko mkubwa utakaoshirikisha viongozi wengine kutoka nje ya nchi ambao watatoa ushuhuda wa kadhia hii ya unyanyapaa, tutakuwa na Wabunge, Majaji na Viongozi wa Dini.

Amesisitiza kwamba vingozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuvunja ukimya,kuonesha na kuamsha huruma; kuwafariji waliokata tamaa na kufungua fursa ya msamaha na kutoa matumaini mapya.Pia viongozi wa dini wana uwezo wa kubadili mawazo na mitazamo hasi na kujenga jamii yenye mtazamo mpya na kwambaTaasisi za dini zina uzoefu wa kutoa huduma bora, rafiki na zenye kufikika na wengi.

Hivyo amesema  taasisi za dini zina vyombo na mifumo imara ya kupashana habari zinazoaminika kwa urahisi na jamii,na Viongozi wa dini wanasikilizwa, wanaaminika na wanaheshimika sana na kwamba zaidi ya asilimia 90 ya watanzania ni waumini wa dini na wanashiriki kwa hiari bila kushurutishwa na hivyo ni rahisi kufikisha ujumbe ukafanyiwa kazi.

"Kimsingi sisi kama wawakilishi wa wananchi tunaguswa sana changamoto za mwitikio wa jamii katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI, ni miaka 37 sasa tunaendelea na kasi ndogo ya mwitikio. Ziko sababu nyingi ambazo zinarudishanyuma mwitikio wa juhudi za kutokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa amesema viongozi wakuu wa dini ambao wameshiriki mkutano huo wapo tayari kupokea na kuyafanyia kazi yote ambayo yameelezwa mkutanoni huo.
 Rutatwa ameeleza wazi wao kwa nafasi yao kama wadau katika mapambano dhidi ya UKIMWI wamekuwa wakikutana kwa kufanya mikutano mbalimbali yenye lengo la kuona jamii ya Watanzania inakuwa salama na hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo na kwa wale ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI wanaishi bila kunyanyapaliwa na yoyote.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kulia) akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA wakati wa mkutano wa wadau wakiwamo viongozi wakuu wa dini nchini waliokutana kujadili na kuweka mkakati wa kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na kukomesha unyanyapaa. Kati kati ni Spika wa Bunge Job Ndugai.
Spika Job  Ndugai akiwa na baadhi ya viongozi wa dini wakijadiliana jambo wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kukomesha unyanyapaa kwa watu wanaoshi na VVU.
 Spika wa Bunge Job Ndugai( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wakuu wa dini wakati wa mkutano wa kujadili namna bora ya kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI na kukomesha unyanyapaa.

MADALALI NA WAENDESHA MINADA WASIOFUATA SHERIA KUKIONA CHA MOTO

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya udalali kwa mujibu wa Sheria.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo  kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya udalali kwa mujibu wa Sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  kuwasilisha maombi ya leseni zao kupitia mfumo huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akimkabidhi leseni ya udalali iliyotolewa kwa njia ya Kieletroniki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Bi. Scholastika Kevela, mara baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo wa  Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza na wawakilishi wa madalali pamoja na wahakiki mali wa mikoa Tanzania Bara kabla ya kuzindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Mwenyekiti wa Madalali wa Mahakama Tanzania Bara Bi. Mwamvua Kigulu (kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya madalali wa mahakama wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Mwenyekiti wa Madalali Binafsi Tanzania Bara Bw. Phidel Katundu (kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya madalali binafsi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya Madalili na Wahakiki mali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara mara baada ya kuzindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo  kuwasilisha maombi yao ya leseni.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………………………………………………………

Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James mewaonya madadali na waendesha minada Tanzania Bara kuacha mara moja kufanya biashara hiyo bilaa kujisajili kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Bw. James ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizundua Mfumo Mpya wa Kieletroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ya hadhara Tanzania Bara ambapo watoa huduma hiyo kuanza sasa wanatakiwa kujisajili kupitia mfumo huo kwa njia ya mtandao wa Internet ama kupitia simu zao za kiganjani.

‘’Napenda kuwafikishia taarifa hii wananchi wote, hasa Madalali na waendesha minada, kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa wote watakaojuhusisha na shughuli za udalali na uendeshaji wa minada bila kuwa na leseni halali’’ alisema Bw. James.
Aliziagiza Taasisi zote za Serikali kufanya kazi na Madalali na waendesha minada ambao wanatambulika kisheria na kwa kufanya hivyo watakuwa wameisaidia Serikali kujipatia mapato yatakayotokana na ada ya leseni itakayolipwa na wafanyabiashara ya udali na waendesha minada.

“Mfumo huu utapunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zinatumia mlolongo mrefu wa kupata leseni kwa kuwa mfumo huo  umeunganishwa na Mfumo wa Malipo wa GePG ambapo mwombaji ataweza kulipia ada ya leseni kwa kutumia benki, mawakala au simu za kiganjani na hivyo kurahisisha na kuboresha ulipaji, kupunguza gharama za ulipaji na kuongeza uwazi na udhibiti wa Fedha za Umma.

Bw. James aliutangazia Umma kuwa kuanzia  tarehe 24 Februari, 2020 maombi yote ya leseni za Udalali na Uendeshaji wa Minada Tanzania Bara yawasilishwe kupitia Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada ambao unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango (www.mof.go.tz);
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, amesema biashara ya udalali na uendeshaji wa minada hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi na hivyo kutengeneza ajira, kuongeza kipato pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Bw. Chotto aliongeza kuwa leseni za Udalali na uendeshaji wa minada Tanzania Bara zinatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mujibu wa sheria ya waendesha minada ya Mwaka 1928 iliyorejewa Mwaka 2002, na Wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wadau hawa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Wakizungumza kwa niaba ya madalali, Mwenyekiti wa Chama cha Mdalali wa Mahakama Bi. Mwamvua Kigulu na Mwenyekiti wa madalali Binafsi Bw. Phidel Katundu, wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kubuni mfumo huo utakao wapunguzia gharama ya kufuata huduma ya usajili jijini Dodoma.

Wameiomba Serikali kudhibiti madalali wasio na leseni au wale wasiosajiliwa kwa kuwa wanaikosesha Serikali mapato pamoja na kuchafua taswira ya biashara ya udalali nchini.

Wamemwomba Katibu Mkuu Bw. Doto James kupitia upya Sheria ya Udalali ya Mwaka 1928 ambayo wamesema imepitwa na wakati na inakwaza shughuli za udalali nchini ikiwemo urasimu wa ufanyakazi kazi zao kutoka kwa mamlaka za Serikali Kuu hasa makatibu Tawala wa Wilaya ambao wanataka kupata vibali kutoka kwao kabla ya kutekeleza kazi zao za udalali katika maeneo husika.

VIFO VYA WAJAWAZITO KIPINDI CHA KUJIFUNGUA VYAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE

$
0
0


 Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali akina mama wajawazito waliolazwa kwenye wodi ya wazazi ambapo vifo vitokanavyo na uzazi hosputalini hapo vimepungua.
Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua miundombinu ya hospitali ya rufaa ya mkoa Temeke ,Waziri Ummy amempongeza Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo.Dkt. Meshack Shimwela kwa maboresho makubwa ya hospitali hiyo.
Muonekano wa jengo la dharura lililofanyiwa ukarabati hosputalini hapo
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na wananchi waliofika hospitalini hapo kupata matibabu
Waziri.Ummy Mwalimu akikagua moja ya ukarabati wa jengo hosputalini hapo na kusema kuwa wizara yake inaimarisha huduma za afya kwenye hospitali za rufaa za mikoa kwa kukarabati miundombinu pamoja na kuweka vifaa tiba ili huduma zote za kipingwa zipatikane.
****************************
Na. Catherine Sungura – Dar es Salaam 
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa temeke imejipanga kuokoa maisha ya wakina mama, wajawazito hususan katika kipindi cha kujifungua, kutimiza lengo hilo imeboresha miundombinu yake, vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za afya kwenye ngazi za msingi.
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambako alikwenda kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo.
 
“Mwaka 2018 walikuwa na vifo 19 vya wajawazito na 2019 walikuwa na vifo 8 tu, lakini kwa takwimu za kuanzia Novemba 2019 hadi leo hakuna mwanamke mjamzito aliyekuja hospitalini hapa na kupoteza maisha, niwapongeze madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hapa kwa hatua hii,” amesema Waziri Ummy.
 
Aidha, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada za makusudi, kuwekeza kwenye huduma za afya nchini sambamba na ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.
 
“Sasa hivi hapa temeke kuna huduma za kibingwa za meno ambapo zamani haikuwepo,” amesema.
 
Waziri Ummy amesisitiza Wizara ina mpango pia wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinazohitajika zinakuwepo kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa.
 
Hata hivyo amesema kuwa wanawake 15 kati ya wanawake 100 ndio ambao huhitaji kupelekwa kujifungulia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa hususan wale wenye changamoto za ujauzito, kwa mfano mtoto amekaa vibaya au viashiria vya uzazi pingamizi.
 
Kwa upande  wa vipimo waziri huyo amesema kuwa Wizara yake imeongeza vipimo vya utra sound hivi sasa serikali imeboresha vituo vya afya na kwamba vipimo hivyo vinaanza kutolewa kuanzia ngazi za vituo vya afya vya umma na hospitali za wilaya nchini.
 
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kuanzia ngazi ya msingi na hospitali za rufaa za mikoa ni kwa wagonjwa watakaopata rufaa.
 
“Kwa yeyeote atakayefanya makusudi kukorofisha vipimo ili watu waende kupima kwenye vutuo binafsi tutawachukulia hatua kwani ni wahujumu uchumi, tunataka vipimo vyote vifanyike ndani ya hospitali ila pale mashine haipo tutaruhusu, lengo letu ni kujitosheleza kwa vipimo vyote kwenye vituo vya afya vya umma,” amesisitiza Waziri Ummy.
 
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa kutokana na maboresho ya miundombinu, wataalam na vifaa tiba kwa mkoa huu wameweza kupunguza vifo vipatavyo arobaini kwa mwaka ukilinganisha na vifo186 mwaka 2018 hadi vifo 140 mwaka 2019 na matarajio yao ni kupunguza zaidi.
 
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa  hospitali hiyo imeondoa msongamano wa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wananchi wengi wanafuata mfumo wa rufaa.
 
“Hivyo wakina mama wajawazito wanaofika kwenye hospitali hii ni wale wenye changamoto ya uzazi kwa maana hiyo wengi wanajifungulia kwenye ngazi za chini ambapo huduma za afya nazo zimeboreshwa,” amesema.

ASKARI WA AMANI AZIDI KUTANGAZA VIVUTIO VYA TANZANIA, WATALII WAVUTIWA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

 KAZI inayofanywa na Askari Polisi wa Amani nchini Congo kutoka Arusha- Tanzania Ally Babu ya kukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili na vivutio vya Utalii  vilivyopo nchini Tanzania, imeweza kuleta matokeo chanya.

Hilo limekuja baada ya watalii kutokea nchini congo wanaofanya kazi Umoja wa Mataifa kuja nchini kwaajili ya utalii.

Essam Ghoneim raia mwenye asili ya Misri mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Congo amekuwa mtalii wa kwanza kufika nchini Tanzania akiwa na mwenzake kuja kutembelea vivutio vya utalii.

Ikumbukwe kuwa, Watalii hao wameweza kufika nchini baada ya kupata ush meawishi kutoka kwa askari polisi anaeshiriki ulinzi wa Amani nchini Congo Ally Babu.

Watalii hao wamewasili nchini Februari 18 mwaka huu, na kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii na kuahidi kurejea tena.

Watalii hao waliwasili na kuelekea katika mji wa Kilimanjaro na baadae Arusha wakifurahi kufika nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kurudi kwa utalii Zaidi katika maeneo mengine ya nchi wapatapo likizo.

Aidha katika ukuzaji wa Kiswahili baadhi ya askari kutoka nchi mbali mbali duniani wanaojifunza kiswahili kupitia Ally Babu wameanza kuelewa na kuongea kiswahili.

Ally Babu ambaye pia ni mwanasheria  amekuwa akijitolea kutangaza utalii na kufundisha walinzi wa Amani wenzake wa umoja wa mataifa lugha ya Kiswahili katika muda wake wa ziada baada ya majukumu yake ya kazi. 

Haya ni matunda ya uzalendo wa kitanzania kukuza na kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili na vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.
 Essam Ghoneim (kushoto)  raia mwenye asili ya Misri mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa Nchini akiwa na rafiki yake baada ya kufika nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.
Picha ya Mlima Kilimanjaro iliyopigwa na Essam Ghoneim baada ya kutembelea kivutio hicho.

WANANCHI WA MAKONGOLOSI CHUNYA WALILIA BARABARA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa wahandisi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya- Makongolosi (Km 39) kutoka kampuni ya SMEC alipokuwa akikagua daraja la mto Lupa, mkoani Mbeya.
 Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya SMEC, Daniel Goshima, akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (Wanne kulia), nguzo za daraja jipya la mto Lupa (halipo pichani), ambalo linajengwa pembezoni mwa daraja la zamani, mkoani Mbeya. 
 Muonekano wa nguzo za daraja jipya la mto Lupa ambalo linajengwa na Mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation. Ujenzi wa daraja hilo ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya – Makongolosi (Km 39), mkoani Mbeya.
 Wafanyakazi wa Mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation, anayejenga barabara ya Chunya- Makongolosi (Km 39) wakiendelea na kazi za ujazaji wa mawe na kifusi katika daraja la Chipoka, mkoani Mbeya.
Muonekano wa barabara ya Chunya – Makongolosi (Km 39) kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake unaendelea. Mradi huu umefikia asilimia 61 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

Wananchi  wa Makongolosi Wilayani  Chunya, mkoani Mbeya, wameiomba Serikali kuharakisha  ujenzi  wa barabara ya Chunya - Makongolosi (Km 39), kwa kiwango cha lami  ili kutataua changamoto ya usafiri na usafirishaji katika eneo hilo.

Akizungumza wilayani Chunya, mkoani Mbeya, mmoja wa wananchi hao, Joana Makwezo, amesema kuwa kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango hicho kutarahisisha huduma za usafirishaji na kutasaidia kukuza shughuli za kijamii na kiuchumi ikiwemo biashara ya madini ambayo ndio biashara kuu katika eneo hilo.


"Tunaiomba Serikali itusaidie barabara hii ikamilike haraka, sisi wengine ni wagonjwa  na tunachelewa kwenda kupata huduma za matibabu kutokana na changamoto ya barabara, wakati mwingine huduma za usafiri zinakuwa juu kutokana na changamoto ya barabara na umbali, naamini barabara ikikamilika hata vyombo vya usafiri vitaongezeka na gharama za usafiri zitashuka", amesema Joana Makwezo


Naye, Dereva Ally Kondo, amesema kuwa wasafirishaji wengi wanashindwa kuleta magari katika eneo hilo kutokana na kuwepo kwa changamoto katika barabara hiyo, hivyo anaamini kuwa ujenzi kwa kiwango cha lami pindi utakapokamilika, utapelekea magari mengi kuongezeka na wasafiri kufika kwa wakati katika shughuli zao.


Ameiomba Serikali kuziba mashimo yaliyopo kwenye njia mbadala inayotumika sasa   kwani magari mengi huharibika kutokana na kuwepo kwa mashimo kwenye barabara hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, amesema kuwa mradi huo unaendelea vizuri na hivyo kumtaka Mkandarasi kuongeza kazi ya ujenzi ili barabara hiyo ikamilike haraka kwa viwango na kwa muda uliopangwa. 
Mwakalinga, amempongeza Mkandarasi huyo kwa kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga kituo cha Afya ambapo amemuelekeza mkandarasi huyo kutatua changamoto za kitaalamu alizozibaini katika mradi huo kabla ya kukabidhi kwa Serikali.
Ametoa wito kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha wanatoa maelekezo na kuweka vibao vya kiusalama katika maeneo ambayo yanajengwa barabara hususan katika vipindi hivi vya mvua ili kumsaidia dereva kutambua njia sahihi ya kupita. 
Aidha, amemtaka Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kukarabati njia mbadala inayotumiwa na wasafirishaji ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kuwepo kwa mashimo katika baadhi ya maeneo.
Awali wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi kwa Katibu Mkuu huyo,  Mhandisi Mshauri, Daniel Goshima, amemuhakikishia Mwakalinga kumaliza mradi huo kwa wakati na kwamba kwa sasa umefikia asilimia 61 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya- Makongolosi (Km39) ni seehemu ya barabara iliyo katika ushoroba wa kati magharibi, yaani Mbeya- Rungwe- Ipole - Tabora hadi Nzega na inafadhiliwa na Serikali kwa asilimia mia moja. 
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Viewing all 119361 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>