↧
PRESIDENT MAGUFULI MEETS PROFESSOR PLO LUMUMBA AT THE STATE HOUSE IN DAR ES SALAAM
↧
Invest with Yetu Microfinance Bank Plc
Yetu Microfinance Bank Plc formerly known as YOSEFO is a Microfinance Bank in Tanzania with operations in 6 regions, namely Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara and Tanga and the Island of Zanzibar.
Before becoming a Microfinance Bank in 2017, it Yetu Microfinance Bank Plc has been a pioneer in Microfinance industry for the past 20 years with the flagship name of “YOSEFO” group lending being their major business.
↧
↧
BREAKING NEWZZZ: YANGA WAMRUDISHA JERRY MURO, WAFUNGUKA SARE 4, NUGAZ KUPIGANA
↧
ZOLA kuzawadia vifaa vya umeme wanafunzi wataofanya vizuri katika mitihani yao wilayani Kisarawe
Kampuni ya kuzalisha vifaa vya umeme wa jua ya ZOLA Electric Tanzania, ambayo zamani ilijulikana kama Mpower, imeeleza dhamira yake ya kusaidia jamii na kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha sekta ya elimu ambapo imetangaza kuwazawadia vifaa vya nishati ya umeme wa jua wanafunzi wa kidato cha nne watakaofanya vizuri kwenye mtihani wa Taifa katika wilaya ya Kisarawe mwaka huu kupitia kampeni yake inayoendelea inayojulikana kama ‘Bukua na Ushinde’.
Akitangaza ofa hiyo ,Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ZOLA Tanzania, Yusuph Nassoro,amesema ‘Bukua na Ushinde’Imelenga kuchochea motisha kwa wanafunzi waliopo mashuleni kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani yao vizuri hususani katika maeneo yenye changamoto ya nishati ya umeme kutoka gridi ya taifa.
“Kampuni yetu tunaamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na jamii ikielimika, inaweza kupiga hatua ya maendeleo kwa haraka,ndio maana tumekuja na mpango huu wa kutoa motisha kwa wanafunzi mashuleni, hususani maeneo yenye changamoto ya nishati ya umeme ikiwa ni moja ya sera yetu ya kusaidia jamii sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini”,alisema Nassoro.
Alisema wanafunzi watakaofanikiwa kuingia katika 10 bora katika mithani ya taifa ya majaribio watapatiwa zawadi ya vifaa vya kusomea na wanafunzi watatu watakaofanikiwa kuingia katika 3 bora watafungiwa mitambo ya umeme wa sola kwenye familia zao sambamba na kupatiwa vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo kutoka kampuni ya ZOLA.
Nasoro,alisema mpango huo wa kusaidia wanafunzi utafanyika katika wilaya mbalimbali nchini ambako kampuni hiyo inaendesha shughuli zake, katika siku za karibuni ilitangaza ofa hiyo kwa wanafunzi wa sekondari katika wilaya ya Longido, mkoani Arusha.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ameipongeza kampuni ya Zola, kwa kubuni mpango huu wenye lengo la kuinua sekta ya elimu kupitia kutoa motisha kwa wanafunzi “Nawapongeza Zola kwa kuja na ubunifu huu ambao utachangia kuinua sekta ya elimu katika maeneo ya vijijini vilevile kwa kuikumbuka wilaya ya Kisarawe”alisema.
Aliwataka wanafunzi kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili ziwasaidie kupata mafanikio na kukamilisha ndoto zao na watambue kuwa kusoma kwa bidii na kupata maarifa ni moja ya njia itakayowapeleka katika kupata mafanikio katika Maisha yao sambamba na kutoa mchango wa kuendeleza Taifa.
Alimalizia kutoa wito kwa makampuni mengine ya biashara kusaidia huduma za kijamii zenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko sambamba na kubuni biashara zinazochochea kuongeza fursa za ajira na kujiajiri kama ilivyo kampuni ya Zola.
Kampuni ya ZOLA Electric, ambayo zamani ilijulikana kama Mpower ilianza kutoa huduma zake nchini mwaka 2012 ikiwa inatoa huduma za neshati ya umeme wa jua na kuuza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ,Jokate Mwegelo akiongea wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ZOLA Tanzania, Yusuph Nassoro,akiongea na baadhi ya wanafunzi wa skkondari wilayani Kisarawe
.Baadhi ya wanafunzi wa skkondari za Kisarawe wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampene hiyo
↧
MANGULA ALIA NA AMANI YA TANZANIA

MbungewaJimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka aliyenyanyua mikono akitoa ufafanuzi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula (mwenyemiwani) wakati alipotembelea kwenye mradi mkubwa washamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo kulia kwa Mangula ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa (pichana John Mapepele)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula akikagua Mkorosho kwenye mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku saba katika Mkoa wa Singida(Pichana John Mapepele

Makamu Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula akikata keki maalum ya miaka 43 ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha tathmini na majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani Singida kwenye ukumbi wa maktaba wilayani Manyoni leo kulia ni Mwenyekitiwa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma kilimba kushoto ni Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Manyoni Jumanne Mahanda anayefuata Katibu wa CCM Mkoa wa Singida AlexndrinaKatabi(Pichana John Mapepele)

Umati wa wanachama wa CCM uliohudhuria mkutano wa Makamu Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula(Picha na John Mapepele)
Apongeza Mkoa wa Singida
Na John Mapepele
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula amewataka watanzania kutochezea amani na kuyumbishwa na wanasiasia na badala yake waione amani walio nayo kama mtaji mkubwa wa kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Mangula ameyasema haya leo katika ukumbi wa maktaba Manyoni wakati alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba kwenye Mkoa wa Singida ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani ambayo imebahatika kuwa amani katika kipindi chote kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema hivyo ni wajibu wa kila mwananchi mzalendo kuilinda kwa kuwa watu wengi hawapendi kuona Tanzania ina amani na kupiga maendeleo ya haraka kama inavyofanya sasa.
“Ndugu zangu hata tukichukulia mfano mdogo tu, katika kipindi cha miaka 75 ambayo tulitawaliwa na Wajerumani na Waingereza kwenye Wilaya yote ya Manyoni hatukuwa hata na Shule mmoja ya Sekondari lakini leo tuna zaidi ya shule 30 katika kipindi kifupi, je hayo siyo maendeleo makubwa ?” alihoji Mangula
Alisisitiza kuwa mapinduzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli yanatokana na msingi imara uliojengwa ambao ni amani na kwamba wachafuzi wa kubwa wa amani dunani kote ni wanasiasa ambao wamekuwa wakisukumwa na tamaa ya madaraka ambapo yakitokea wanaoumia ni watoto, wazee na akina mama.
Akitolea mfano wa machafuko ya kisiasa ya Rwanda ya mwaka 1994 alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo, alishuhudia wimbi kubwa la watoto na akina mama wakiteseka na kufa njiani wakati wakijaribu kukimbia nchi yao kunuisuru maisha yao.
“Nilishuhudia mama akina mama wakitanda kanga na kumsaidia mama mwenzao kujifungua mtoto pembeni mwa barabara na baada ya kujifungua tu wakaendelea na safari, kwa kweli huwa sipendi kukumbuka hali ile maana ni hatari na ukatili usioelezeka” aliongeza Mangula
Akiwa katika mkutano huo amesisitiza suala la uadilifu na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za chama cha Mapinduzi ambapo amesema vitendo vyoyote vya rushwa na wagombea kuanza kujipitisha kabla ya kipindi rasmi cha kuchukua fomu za kugombea na kuanza mchakato wa uchaguzi hakikubaliki na kusisitiza kuwa chama kitachukua hatua kwa wote watakao bainika kufanya hivyo.
Aidha Kamati za Siasa katika maeneo husika zitakazoshindwa kuwachukulia hatua wanachama watakaofanya makosa zitaadhibiwa.
Akiwa katika ziara hiyo ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mkoa wa Singida ambapo mradi wa mwisho alioutembelea ni mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati kwenye Wilaya ya Manyoni na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.
Amesema alama ya Chama Cha Mapinduzi ni jembe na nyundo ambapo amesema jembe ni alama ya mkulima na nyundo ni mfanyakazi hivyo CCM inaamini kuwa wakulima na wafanyakazi wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi yao na kuwa mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania yameletwa na kilimo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka akimwelezea Mangula kwenye shamba la Korosho la Masagati ameshukuru Serikali ya Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kushirikisha wananchi katika kuwabadili mawazo na mtazamo wa kutafuta maendeleo ya kweli kwa kulima shamba la pamoja la korosho ambapo amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Mhe. Mtuka amesema kutokana na utafiti uliofanyika na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya Kilimo Kanda ya Kati uliofanyika kuanzia mwaka 2002, matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa hali ya hewa na udongo vinafaa kwa kilimo cha korosho hivyo wakaanza kuwahamashisha wananchi kulima zao hilo
“ Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri tuliamua kuanzisha zao la korosho kimkakati ili kuchochea kwa kasi kubwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla’” aliongeza Mhe. Mtuka.
Aidha,alipongeza Serikali ya Mkoa kwa kubuni wazo la kuanzishwa kituo kwa kikubwa cha hija duniani cha Bikira Maria katika eneo la Sukamahela, sehemu ambayo ni katikati ya nchi ya Tanzania kwa ajili ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuhiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fussi amesema kuwa kazi zinazoendelea katika eneo hilo kwa sasa ni kuhamasisha wakulima wajiunge na kilimo cha korosho, kuendelea kutoa huduma za ugani kwa wakulima ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa kushirikiana na TARI na Bodi ya Korosho, kuendelea kazi ya kusafisha na kugawa mashamba kwa wakulima na kuzalisha miche bora korosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa amemhakikishia Mangula kuwa serikali itaendelea kusimamia kikamilifu na kuwa hamasisha wananchi kutoka sehemu mbali mbali nchini kuja kuwekeza katika kilimo cha korosho kwenye eneo hilo kwa kuwa mradi huo na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya ya Manyoni na Taifa kwa ujumla.
Ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na udhibiti wa visumbufu kama magonjwa na wadudu,udhibiti wa ubora wa korosho kutokana na usimamizi wa karibu, upatikanaji wa uhakika wa soko katika eneo la mradi,kurahisisha upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuhudumia eneo kubwa kwa wakati mmoja na chanzo kikuu cha malighafi za viwanda vya kusindika korosho.
Manufaa mengine ya mradi ni kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri kupitia ushuru na kodi za biashara mbalimbali zitokanazo na ongezeko la uchumi katika sekta mtambuka zinazoendana na zao hilo, hali ya maisha kuboreka ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makazi bora na kuongezeka uhakika wa chakula katika kaya.
↧
↧
NAIBU WAZIRI ARIDHISHWA NA KASI YA USAMBAZAJI UMEME KWENYE TAASISI ZA UMMA
Naibu Waziri wa Nishati, akipata taarifa wa hali ya umeme ya Wilaya ya Liwale kutoka kwa Meneja Tanesco wa Wilaya ya Liwale Festo Nhembo wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme.

Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,akiongea na wananchi wa kata ya Liwale mjini kabla ya kuwasha umeme kwenye shule ya msingi ya kata hiyo, kulia Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwambwa.![]()

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifurahi pamoja na kina mama wa kijiji cha Makata, mara baada ya kuwashwa kwa umeme kwenye zahanati ya kijiji hicho kilichopo kata ya Makata,Wilaya wa Liwale Mkoa wa Lindi.![]()

Wananchi wa kijiji cha Makata wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kijijini humo.
*****************************
Hafsa Omar-LINDI
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema amefurahishwa na kuridhishwa na kasi ya uunganishwaji umeme kwenye Taasisi za Umma zilizopo Wilayani Liwale kama Serikali ilivyoagiza.
Ameyasema hayo,Februari 24,2020,kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Liwale mjini na wa kijiji cha Makata, Kata ya Makata, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi kabla ya kuwasha umeme kwenye Zahanati ya kijiji hicho na kwenye ya Shule ya Msingi Naluleo.
Aidha, alisema ziara yake hiyo,Mkoani humo lengo lake kukagua kazi za usambazaji umeme zinavyoendelea katika Mkoa huo na pia kujionea mwenyewe kasi ya usambazwaji wa umeme katika Taasisi za umma kama Serikali ilivyoagiza zipelekewe umeme na amefurahishwa kuona shule na zahanati nyingi za Wilaya hiyo zimeunganishwa na huduma hiyo.
“Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliagiza umeme huu tunavyoupeleka vijijini basi tunganishe kwenye taasisi za umma hususani Shule,Zahanati, vituo vya afya,miradi ya maji, ofisi za Serikali kwahiyo nimefurahi leo tunazindua kwenye shule ya Msingi ambao Watoto wenu wanasoma hapa”Alisema.
Alisema, lengo la kupeleka umeme kwenye Taasisi hizo, kuhakikisha kuwa huduma hizo zinazotolewa zinakuwa za kiwango na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi.
Alieleza kuwa, unganishwaji umeme katika kwenye Shule ya kijiji hicho utaongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo,kwakuwa kutakuwa na kambi ya kujisome yenye uhakika wa usalama kwasababu mwanga utapatikana muda wote katika shule hiyo na wanafunzi kuweza kujisomea.
Vilevile, alisema kupatikana kwa umeme kwenye Zahanati kwenye kata ya Makata itasaidia kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwenye zahanati hiyo ambapo huduma hizo zinatolewa zitapatikana kwa muda wote na hakutakuwa na kisingizo cha kutotoa huduma kwasababu ya giza.
Pia, aliwataka wananchi wa vijiji hivyo wasitumie umeme kwa matumizi ya nyumbani, bali watumie umeme huo katika kujiletea maendeleo kwa kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.
“ Tumieni umeme kujiletea maendeleo,kazi ya umeme ni pamoja na usalama majumbani,uboreshaji wa huduma za afya,umeme unasaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja, na kwa jamii kwa familia na Wilaya pia nataka Liwale iende mbali kiuchumi na nawalika wawekezaji wakubwa na wadogo waje kuwekeza kwasababu kuna umeme wa uhakika” Alisema.
Nae mbunge wa jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru Serikali kwa kufanya kazi kubwa ya usambazaji umeme nchini na kupeleke huduma hiyo kwenye wilaya humo na kuahidi kuwa wananchi wa jimbo hilo watautumia umeme kwa matumizi sahihi ambayo yatasaidia kujiletea maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kwa wilaya pia.
↧
THRDC yapongeza uamuzi wa JPM kuwateua Makamishna THBUB

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma leo Februari 24, 2020. Ambapo pamoja na mambo mengine alipongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuwateua Makamishna hao wa tume.

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimuaga Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa (kulia) mara baada ya kumaliza kikao chao kifupi kilichofanyika katika ofisi za THBUB leo,
Februari 24, 2020.
**************************
Na Mbaraka Kambona,
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) nchini umepongeza hatua ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kuwateua Makamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora (THBUB).
Pongezi hizo zimetolewa na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa alipokutana na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ofisini kwake jijini
Dodoma leo Februari 24, 2020.
Akiongea na Mwenyekiti huyo wa THBUB alisema kuwa uteuzi huo umefurahiwa na wadau wengi wa haki za binadamu kwani utaiwezesha tume kufanya kazi zake kama inavyopaswa. Alisema kuwa THBUB ni chombo cha kitaifa ambacho kimeundwa kikatiba na kupewa mamlaka ya kuhamasisha na kulinda haki za binadamu nchini na wananchi wengi wanakitegemea chombo hicho kwa ajili ya kuwasidia kutetea haki zao.
Aliongeza kwa kusema kuwa THBUB kukaa muda mrefu bila Makamishna kulikwamisha mambo mengi kwa kuwa wao ndio wenye kufanya maamuzi mbalimbali katika taasisi hiyo. Olengurumwa alisema pia kukosekana kwa Makamishna hao kulipelekea kudorora kwa ushirikiano baina ya wadau wa haki za binadamu na taasisi hiyo, lakini sasa anaamini kwa kuwepo wao katika uongozi huduma za tume kwa wananchi zitatolewa kama inavyotegemewa.
Aidha, Olengurumwa alimuhakikishia Mwenyekiti wa THBUB ushirikiano wa karibu na kumueleza kuwa watakaa kuona maeneo gani wanaweza kushirikiana, lakini kwa kuanzia alimuahidi Jaji Mwaimu kuwa THRDC itatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa
tume kuhusu namna bora ya kufanya utetezi wa haki za binadamu kwa wananchi.
Akiongea mapema wakati akimkaribisha Mratibu huyo, Jaji Mwaimu alimueleza kwa ufupi kuhusu majukumu ya THBUB na mipango ya taasisi hiyo kwa mwaka huu. Aidha mwenyekiti huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo THRDC akisema kuwa tume peke yake bila kushirikiana na wadau wengine haitaweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa Makamishna hao mwishoni mwa mwaka jana baada ya THBUB kukaa bila Makamishna kwa takriban miaka mitatu.
↧
Zuriel Oduwole Launches "Project Pilot" in Johannesburg - SOUTH AFRICA
Three days after meeting with the Governor of Lagos State in Nigeria to explore a child friendly creative and multimedia education curriculum for schools, Zuriel launched a major pilot in South Africa for a Femicare drive, to support girls education in that country. An idea several months in the making, it focused on girls in schools in needy parts of Johannesburg, including the township of Alexandra starting the day with 2000 students, and also students in the township of Soweto.
She created a partnership with the makers of the Lil-Lets brand range of Femicare line, to ensure girls in low income areas across the Gauteng province, starting with the Johannesburg region do not miss school, because of their cycles.
↧
TAKUKURU ICHUNGUZENI KAMPUNI INAYOCHUKUA MAPATO YA FAINI ZA MAROLI- RC MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kushoto) akizungumza na watendaji wote wa Barabara katika ukumbi wa Anatoglo Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam,ampoa Makonda aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchungunguza Kampuni inayochukua mapato ya faini za Maroli na kulipa fedha zote ilizokusanya tangu mwaka juzi.
Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto (kushoto) akizungumza na watendaji wote wa Barabara katika ukumbi wa Anatoglo Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija (wapili kushoto) katika mkutano wa watendaji wote wa Barabara katika ukumbi wa Anatoglo Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wakuu wa Wilaya na viongozi mbalimbali wa kiwa katika mkutano wa watendaji wote wa Barabara katika ukumbi wa Anatoglo Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkutano ukiendelea.
↧
↧
Mafunzo ya IPSAS kuondoa hoja za Wakaguzi – CPA Kolola
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka yaViwanja vya Ndege Tanzania (TAA), CPA Josephine Kolola leo akizungumza na Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka hiyo, wanaoshiriki mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2). Mafunzo hayo yamefunguliwa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Renatus Msanjira.![]()

Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakimsikiliza kwa makini aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Renatus Msangira akifungua mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2).![]()

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Renatus Msangira akifungua mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2), kwa kushirikisha Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani.![]()

Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (kushoto) akizungumza na Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Bakari Mrisho (wa pili kushoto),aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Renatus Msangira (kulia), na Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu na Mafunzo, Abdi Mkwizu.![]()

Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo wakiwa kwenye mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yanayofanyikakwa siku tano kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2).
******************************
Na Bahati Mollel, TAA.
MAFUNZO ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yameelezwa kuwa yataondoa hoja za Wakaguzi wa ndani na nje.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), CPA Josephine Kolola amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoanza leo kwenye Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB2) kwa kushirikisha Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka hiyo, ambapo yanashirikisha washiriki 56 kutoka Viwanja vya ndege vya serikali vilivyopo Tanzania Bara.
“Pia ni matarajio yangu baada ya mafunzo haya kutawezesha kupungua kwa kiasi kikubwa na hata kutokuwepo kabisa kwa hoja za wakaguzi wa ndani na nje kutokana na uelewa utakapopatikana kwa washiriki,” amesema CPA Kolola.
CPA Kolola amesema mafunzo hayo pia yatashirikisha suala zima la maadili ya Uhasibu (Code of Conduct & Ethics for Professional accountants); uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya kifedha kadiri inavyotolewa na serikali (MoFP), hivyo kutoa taarifa za fedha zenye kuonesha uhalisia na mwelekeo wa Mamlaka wenye tija kwa watumiaji wa taarifa hizo.
“Mafunzo haya yatawakumbusha wahasibu wote wa Mamlaka dhamana waliyonayo katika masuala yote ya kifedha hivyo kuwa makini katika kazi zao za kila siku kwa kuhakikisha umakini wa kuingiza data za mapato, matumizi, madeni nk, hivyo kuepusha makosa kwenye vitabu vya hesabu,” amesema CPA Kolola.
Awali akifungua mafunzo hayo aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Renatus Msangira akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Mshauri Julius Ndyamukama, aliwataka wahasibu na wakaguzi hao wa ndani kuhakikisha wanatunza siri za hesabu ya taasisi hiyo, kwa kuwa ni kosa la kisheria kuzitoa kwa watu wasiohusika.
“Hesabu za taasisi au ofisi yeyote ya Umma hazipaswi kusambazwa hovyo kwa watu wasiostahili hizo ni moja ya siri na zinapaswa kutunzwa vyema, na hutolewa kwa kibali maalum endapo itahitajika, lakini sio zaidi ya hapo” alisisitiza Msangira.
Pia amewataka washiriki hao wapatao 56 kutoka viwanja mbalimbali vya ndege Tanzania Bara watumie fursa hiyo kwa kuboresha utendaji wao wa kazi kwa kushirikiana vyema na Vitengo na Idara zilizopo, ili kufanikisha lengo la Mamlaka la kuwa na hesabu bora.
Hatahivyo, aliwasisitizia kufanya kazi kwa upendo, uadilifu na amani kwa kutojiwekea msongo wa mawazo kwani wanaweza kuharibu kazi kutokana na akili kutokuwa sawa.
“Nina imani kubwa kwamba mafunzo haya yatawaongezea kitu kikubwa sana katika kada zenu, hivyo mjaribu kuzingatia kazi na kada zenu na msiingilie kazi zisizowahusu,” amesema.
Halikadhalika aliwasisitizia kujiendeleza zaidi kitaaluma ili wapate CPA, ambayo itawaruhusu kukafanya kazi kwa viwango vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.
Mafunzo hayo ya siku tano yanaendeshwa na Wataalam kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA).
↧
UNESCO YATAMBUA KISWAHILI KAMA LUGHA ITAKAYOSAIDIA KUKUZA UTANGAMANO BARANI AFRIKA
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu katika UNESCO, Mhe. Samwel Shelukindo akizungumza kwenye Mjadala kuhusu "Fursa na Changamoto za Kukitambua Kiswahili kama Lugha rasmi ya Bara la Afrika kwa ajili ya kukuza Utangamano. Mjadala huo uliandaliwa na Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yaliyofanyika jijini Paris, Ufaransa hivi karibuni.
Sehemu ya Wataalam wa Lugha ya Kiswahili akiwemo Prof. Aldin Mutembei (wa pili kushoto) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishiriki kwenye mjadala kuhusu Lugha ya Kiswahili wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yaliyofanyika Paris, Ufaransa hivi karibuni
Sehemu ya washiriki wa Mjadala huo wakifuatilia kama wanavyoonekana katika picha
Mhe. Balozi Shelukindo (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya Wajumbe kutoka UNESCO wakiangalia machapisho mbalimbali ya Lugha ya Kiswahili yaliyoandaliwa na Ubalozi baada ya kushiriki mjadala kuhusu Lugha ya Kiswahili ulioandaliwa na Ubalozi kwa kushirikiana na UNESCO.
UNESCO YATAMBUA KISWAHILI KAMA LUGHA ITAKAYOSAIDIA KUKUZA UTANGAMANO BARANI AFRIKA
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeitambua Lugha ya Kiswahili kama lugha itakayosaidia kukuza utangamano Barani Afrika wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yenye kaulimbiu “Lugha Bila Mipaka” iliyofanyika jijini Paris, Ufaransa hivi karibuni.
Katika kuadhimisha siku hiyo, Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na UNESCO uliandaa mjadala kuhusu "Fursa na Changamoto za Kukitambua Kiswahili kama Lugha rasmi ya Bara la Afrika kwa ajili ya kukuza Utangamano".
Akizungumza wakati wa Mjadala huo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu katika UNESCO, Mhe. Samwel Shelukindo pamoja na mambo mengine, alieleza hatua iliyochukuliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha zitakazotumika katika Jumuiya hiyo.
Aidha, Mhe. Balozi Shelukindo alizipongeza nchi za Afrika Kusini na Namibia kwa kuwa nchi za kwanza Kusini mwa Afrika zilizoamua kuanzisha ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika shule mbalimbali. Mjadala huo uliwashirikisha Wataalam mbalimbali akiwemo Prof. Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Kufanyika kwa mjadala huo katika UNESCO ni moja ya juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa za kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha zitakazotumika katika UNESCO. ![]()
↧
RELP TV: HANDAKI NAMBA 1 NA 2 LAELEKEA UKINGONI KUKAMILIKA, UCHORONGAJI WAHAMIA HANDAKI NAMBA 3 NA 4.
↧
TECNO Yawakumbuka Watoto Yatima
Tukiwa katika mwanzo wa muhula wa kwanza wa masomo, kampuni ya simu za mkononi ya TECNO, imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Chanika Children Shelter kilichopo Chanika Jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kurudi mashuleni.
Msaada huo ukiwemo wa ada kiasi cha Shilingi Milioni tatu, vifaa vya masomo, Chakula na mahitaji mengine ya kila siku umetolewa mwishoni mwa wiki.
Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Afisa Uhusiano wa kampuni ya TECNO Eric Mkomoye alisema msaada huo ni sehemu ya kuonesha ukarimu kwa watoto hao kwani jukumu la kusaidia watoto hao ni la kila mtu.
“Sisi TECNO ni sehemu ya jamii ya Kitanzania na hivyo jukumu la kuwalea watoto hawa katika kuwapatia mahitaji yao ya kila siku na kuhakikisha wanaendelea na masomo vizuri ili kutimiza ndoto zao ni letu sote” Alisema Mkomoye.
Kampeni ya msaada huo inayojulikana kama “Kuwa Shujaa Wangu, Kwa pamoja Tuwasaidie”, iliungwa mkono na mwanamama maarufu Esha Buheti pamoja na kampuni ya kutengeneza na kusambaza taulo za kike ya Soft Plus.
Kwa upande wake Bi Esha Buhet aliwashukuru TECNO kwa kuonesha moyo wa ukarimu na kuomba makampuni mengine yaige mfano kwa TECNO.
“Ni jambo lililonipa msukumo mkubwa sana! Nilivyoona TECNO wametoa stori yenye simanzi ya mtoto mmoja hivi kutoka hapa, na nilisikia sio mara ya kwanza kuja wameshawahi kuja mara kadhaa, ndio maana na mimi nikaona niwaunge mkono kwa hiki kidogo nilichowaleletea, naomba na makampuni mengine yaige mfano kwa TECNO na Soft Plus” Alisema Bi Esha.
Naye Mkurugenzi wa kituo hicho aliishukuru kampuni ya TECNO pamoja na wote walioungana kupeleka misaada mbalilmbali kwa watoto hao yatima.
“Tunashukuru sana uongozi mzima wa TECNO pamoja na wafanyakazi wote, tunawashukuru wote mlioambatana na TECNO kuja kutupatia misaada hii. Asanteni sana” Alisema mkurugenzi wa kituo hicho.
Kituo hicho chenye zaidi ya watoto Mia moja wakike na kiume kimewahi kupelekewa msaada wa Shilingi Milioni Tano na TECNO Mwanzoni mwa mwaka 2019, pamoja na mahitaji mengine mbalimbali ya kila siku ikiwemo Chakula.
Baadhi ya Watoto walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TECNO waliofika kukabidhi msaada.
Bi. Esha akikabidhi baadhi ya misaada kwa watoto wa kituo cha Chanika Children Shelter
Afisa Mahusiano wa kampuni ya TECNO Eric Mkomoye akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
William Motta Meneja Masoko wa TECNO akipeana mkono na Mkurugenzi wa kituo cha Chanika Children Shelter wakati wa kukabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Tatu.
↧
↧
TANZANIA YAWEKA WAZI MIKAKATI KUFANIKISHA UZALISHAJI NA USAMBAZAJI WA NISHATI UKANDA WA SADC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said akizungumza katika Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) alipowasili kufungua Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi JR.
Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mapolao Rosemary Makoena akizungumza katika Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) alipowasili kufungua Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mapolao Rosemary Makoena mara baada ya kufungua Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo,katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo,katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said akimsikiliza Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mapolao Rosemary Makoena kabla ya kuufungua mkutano huo wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
Wawakilishi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulifunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulifunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
========= == ====== =========
SERIKALI ya Tanzania imeweka wazi mipango na mikakati yake ya ufanikishaji wa malengo ya makubaliano ya kukuza uzalishaji, kujenga miundombinu na usambazaji wa nishati katika Nchi 15 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yaliyofikiwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa na Mawaziri wa sekta ya Nishati katika Jumuiya hiyo Mwezi Agosti mwaka 2019.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wataalamu wa nishati kutoka Nchi za SADC unaoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumanne (Februari 25, 2020), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said alisema mkutano huo unalenga kuanisha vyanzo na miradi mbalimbali ya kimkakati itakayowezesha utoshelevu wa nishati katika nchi za SADC.
Mhandisi Zena alisema kupitia Mkutano wataalamu wa sekta ya nishati wa Tanzania wataweza kubainisha fursa zilizopo katika kuhakikisha utoshelevu wa sekta ya nishati nchini ikiwemo Ujenzi wa Mradi Bwawa la kuzalisha Umeme kwa Kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajia kuzalisha unaotarajia kuzalisha Megawati 2115.
‘’Tumeshuhudia majanga mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya baia nchi, sasa wataalamu wetu wa masuala ya nishati, mafuta na gesi watakutana na kujadili kwa pamoja ili kupata njia bora zaidi za kuweza kuzalisha nishati ya umeme itakayoweza kuwasaidia wananchi wetu’’ alisema Mhandisi Zena.
Alisema mipango na mikakati ya kuimarisha sekta ya nishati katika ukanda wa SADC ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Viongozi wa Kitaifa na Mawaziri wa sekta ya nishati katika Jumuiya ya SADC na Tanzania imepanga kuutumia vyema mkutano huo ili kuhakikisha kuwa sekta ya nishati inakuwa ya kibiashara na hivyo kuweza kutengeneza fursa kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa Mhandisi Zena alisema mkutano huo wa wataalamu unatarajia kuhitimishwa mwishoni mwa wiki hii, ambapo mwezi Mei mwaka huu kunatarajia kufanyika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa sekta ya nishati katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC, ili kuona namna bora zaidi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta tija na maendeleo endelevu kwa wananchi wa ukanda wa SADC.
Aliongeza kuwa mbali na miradi hiyo ya kimkakati, wataalamu hao hao pia watajadili fursa za nishati jadidifu na namna zinavyoweza kuongeza uwezo wa upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuwawezesha wananchi wa ukanda wa SADC kuweza kuwa na nishati ya uhakika na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake Kamishna wa Nishati na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Adam Zuberi alisema mkutano huo umeshirisha jumla ya nchi wanachama 12 wa Jumuiya hiyo, ambao wanaandaa maazimio mbalimbali yanayotarajiwa kujadiliwa katika Baraza la Mawaziri wa sekta ya Nishati wa Jumuiya hiyo mwezi Mei mwaka huu.
Aliongeza kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao pia watapata fursa ya kushiriki semina zitakazohusisha uwasilishaji wa mada na makongamano mbalimbali ya wadau wa sekta ya nishati ndani ya ukanda wa SADC.
↧
Spika Ndugai ampeleka Jafo Site Inapojengwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bunge



***************************
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amempeleka Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo eneo inapojengwa shule maalumu ya wasichana itakayojulikana kama Shule ya Sekondari ya Wasichana Bunge inayojengwa katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma
Akiwa katika eneo hilo la ujenzi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amesema ni vyema Waziri anayehusika na uendeshaji na usimamizi wa shule akajua mapema sehemu inapojengwa na mendeleo ya ujenzi wake ili kama kuna maboresho aweze kuyatoa mapema na kufanyiwa kazi.
“Hapa tunajengwa kwa kutumia ‘Force Account’ mfumo ule ule ulioasisiwa na TAMISEMI na ramani za majengo ni zile zile za TAMISEMI ila kuna baadhi ya maeneo tumeboresha kidogo lakini hatujaenda nje ya maelekezo ya Wizara hii kuhusu ujenzi wa miundombinu ya shule” Alisema Spika Mhe. Ndugai.
Akizungumzia wazo wa kujenga shule hiyo Spika Ndugai alisema Waheshimiwa Wabunge Walifanya changisho kupitia matukio ya kijamii na wadau mbalimbali wakachangia jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.2 fedha hiyo ilipatikana kutoka katika sehemu ya posho za Wabunge na michango ya wadau hao.
“Lengo la awali ilikua kujenga vyoo vya mfano vya wasichana katika kila Jimbo Nchini lakini baadae tukaona tuunganishe nguvu tujenge kitu kimoja kikubwa kitakachoacha alama ya Bunge la 11 mara litakapomaliza muda wake”.
Hakika katika hili Bunge la 11 limefanya kazi ya zaida, zaidi ya ile ambayo tumeizoea na ipo Kisheria ambayo ni kutunga Sheria wakati huu tumeamua tufanya kazi ya Jamii itakayoboresha Elimu ya mtoto wa Kike wa Tanzania na tukaelekeza nguvu katika ujenzi wa shule hii ya mfano ya Wasichana alisema Spika Ndugai.
“Shule hii inayojengwa itakua na miundombinu yote inayohitajika kwa ajili ya Shule ya Sekondari kuanzia madarasa ya kutosha, maabara, mabweni, bwalo la kisasa, vyoo, ofisi za walimu, jengo la utawala pamoja na library yenye miundombinu ya TEHAMA” aliongeza Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai ameweka wazi kuwa ujenzi wa shule hiyo utakamilika Mwezi Juni, 2020 na kwa umoja wa Bunge la 11 wataikabidhi kwa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Jafo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
Akizungumza akiwa katika eneo la ujenzi wa shule hiyo Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amemshukuru Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai pamoja na Wabunge wote wa Bunge la 11 kwa michango yao na wazo lenye tija la kujenga shule maalumu ya Wasichana ya Bunge.
“Nimefarijika sana kuaona wazo hili limeanza kutekelezwa na ndoto ya Bunge la 11 sasa inaanza kutimia na kwa sababu Spika amekuja kunionyesha kuanzia leo na mimi nitakuwa napita mara kwa mara kuangalia maendeleo ya ujenzi huu ili kwa pamoja tuweze kuikamilisha ndoto hii ya Bunge letu” Alisema Jafo.
Nitahakikisha kuwa Shule hii mara inapokamilika na kukabidhiwa TAMISEMI tunapanga walimu wenye ubora na wanafunzi wenye ufaulu mzuri ili kwa pamoja waweze kuleta matokeo mazuri ya shule hii, tunakata shule hii iwe ya mfano na maalumu kwa heshima ya Bunge la 11 alisema Jafo.
“Tunataka tuienzi shule hii kwa heshima ya Bunge la 11 tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanafunzi watakaosoma hapa wanafaulu kwa viwango vya juu ili shule hii iweze kuingia katika shule kumi bora za Tanzania katika matokeo ya kidato cha sita alisisitiza Jafo.
↧
TANZANIA YASHIRIKI KWA MARA KWANZA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA KILIMO YA PARIS 2020, UFARANSA

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris yanayofanyika mjini humo kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.

Wageni mbalimbali wakipata maelezo kuhusu fursa za bidhaa za kilimo zinazopatikana Tanzania walipotembelea Banda la la Tanzania wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo yanayofanyika jijini Paris kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.
************************
Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris 2020 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.
Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Mhe. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, yanatarajiwakutembelewa na zaidi ya watu 600,000.
Wakati wa maonesho hayo, Tanzania itapata fursa ya kuonyesha bidhaa zake yakiwemo mazao ya kimkakati. Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaongozwa na Bw. Victor Rugemalila kutoka TANTRADE.
Ubalozi wa Tanzania ambao unaratibu maonesho hayo kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, unaishukuru Kampuni ya Tanzania Re-assurance (TAN-RE) ya Dar es Salaam, Tanzania, kwa kufadhili kwa kiasi kikubwa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho. Aidha, Ubalozi unatambua mchango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya Kahawa ya Inter State.
↧
Waziri Mwakyembe Apokea Ujumbe wa Wadau wa Michezo toka Nchini Misri

Kiongozi wa ujumbe toka nchini Misri akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) wakati ujumbe huoulipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo jijini Dar es Salaam mapema hii leo na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo ikiwemo la ujenzi wa eneo changamani la michezo.

Balozi wa Misri nchini, Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) wakati walipomtembelea Waziri na ujumbe toka nchini Misri na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo ikiwemo la ujenzi wa eneo changamani la michezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe toka nchini Misri na wadau wa michezo nchini wakati walipomtembelea leo 25 Februari 2020 katika ofisi ndogo za jijini Dar es Salaam na kujadiliana
masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo ikiwemo la ujenzi wa eneo changamani la michezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akielekeza jambo kwa ujumbe toka nchini Misri wakati walipomtembelea leo 25 Februari 2020 katika ofisi ndogo za jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo ikiwemo la ujenzi wa eneo changamani la michezo.

Balozi wa Misri nchini, Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto)akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Waziri na ujumbe toka nchini Misri na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo ikiwemo la ujenzi wa eneo changamani la michezo. Picha na WHUSM – Dar es Salaam
25 Februari, 2020
↧
↧
MWAKALINGA AAHIDI MAZURI OSBP KASUMULU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Mbunifu Majengo, Daniel Mandari (Wa pili kushoto), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambae anasimamia ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), cha Kasumulu mkoani Mbeya, kuhusu ujenzi wa kituo hicho.![]()

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (Wa Tatu kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), chaKasumulu mkoani Mbeya. Kituo hiki kipo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Malawi.![]()

Mbunifu Majengo, Daniel Mandari (Wa Tatu kushoto), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambae anasimamia ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), cha Kasumulu mkoani Mbeya, akimuonesha KatibuMkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, ramani ya ujenzi huo.![]()

Mbunifu Majengo, Daniel Mandari, kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambae anasimamia ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), cha Kasumulu mkoani Mbeya, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuuwa Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (Wa Pili Kushoto), alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.![]()
![]()


Muonekano wa mradi wa ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), cha Kasumulu mkoani Mbeya pindi utakapokamilika. Ujenzi huo utajumuisha jengo la abiria, malori, ghala, mifugo, jengo la kupima uzito namaegesho.
PICHA NA WUUM
********************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, amesema kuwa ataongea na uongozi wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hivi karibuni ili kukubalianakwa pamoja kuhamisha miundombinu ya mkongo wa Taifa na umeme katika eneo la ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP), eneo la Kasumulu mkoani Mbeya.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kipo mpakani mwa Tanzania na Malawi, Katibu Mkuu huyo amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata ridhaa kutoka kwa viongozi hao ili kuruhusu ujenzi huo kuendelea katika maeneo ambayomradi huo utapita mara baada ya kuhamisha miundombinu yao.
Mwakalinga, amesema kuwa mradi huo ni wa Taifa, hivyo ni muhimu kwa pande zote kukaa na kukubaliana masuala hayo bila kuathiri ufanisi wa miundombinu wa kila mmoja wao.
“Nitazungumza na viongozi wa Mashirika haya ili kuona namna ya kusaidiana kuhamisha miundombinu yao na kuruhusu ujenzi uendelee kwenye maeneo haya yenye changamoto za muingiliano wa kimiundombinu mara baada ya kukubaliana”, amesema Mwakalinga.
Amefafanua kuwa kuhusu suala la fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo ni kwamba Serikali inaendelea kulipa fidia hizo ambapo mpaka sasa wamebaki watu 10 ambao bado hawajalipwa na hii ni kutokana na kusubirimchakato wa mwisho ili nao kuweza kulipwa.
Kwa upande wake, Mbunifu Majengo, kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Daniel Mandari, amesema kuwa mradi huo unakabiliwa na chngamoto ya uwepo wa baadhi ya miundombinu kama ya Mkongo wa Taifa na umeme katika eneo la mradi ambayo bado haijaondolewa, nahivyo kupelekea mradi huo kusimama kwa baadhi ya maeneo.
Mandari, amefafanua kuwa mradi huo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia na kujengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CGC kutoka nchini China, unagharimu Bilioni 26.4 na kwa sasa umefika asilimia 16.
Katika hatua nyingine Mwakalinga amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kikusya – Matema Beach (Km 39.1) mkoani humo ambapo amekipongeza Kitengo cha usimamizi wa miradi cha TECU kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuisimamia vizuri kipande chakilometa 4 cha barabara hiyo ambacho Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza kikamilike haraka.
Ukaguzi wa miradi hiyo ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo katika mikoa mbalimbali nchini ili kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasailiano (Sekta yaUjenzi).
↧
NG'OMBE MWENYE VICHWA VIWILI, MIDOMO MIWILI NA MACHO MATATU AZUA TAHARUKI
Na Woinde Shizza, Arusha
TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wananchi wa Kijiji cha Ngiresi kilichopo kwenye Kata ya Sokoni 2 katika Halmashauri ya Arusha baada kuzaliwa ng'ombe mwenye vichwa viwili ,midomo miwili na macho matatu .
Kuzaliwa kwa ng'ombe huyo katika eneo hilo kumeibua maswali mengi yasiyo na majibu kwa wananchi hao huku wengi wao wakionekana kushangaa.
Akizungumzia tukio hilo, Mmiliki wa ng'ombe huyo Eliakimu Mungasi ameiambia Michuzi Globu ya jamii kwamba wakati anapewa taarifa ya kuzaliwa kwa ng'ombe huyo alipata mshutuko mkubwa kwani haijawahi kutokea katika maisha yake na kwamba ng'ombe huyo amezaliwa Februari 3 mwaka huu na hasi sasa ametimiza siku 23.
Amesema huu ni uzao wa tano wa ng'ombe aliyezaa ndama huyo ambaye amewashangaza wengi Wa tano ngombe huyo imzaa ndama huyo na kwamba huko nyuma ng'ombe wote walizaliwa walikuwa salama na hawana tatizo lolote.
"Watu wanaongea mengi, wengine wanasema ni mambo ya ushirikina kwa maana ya uchawi, wengine wanasema ni laana lakini mimi sijali, nachojua ni mpango wa Mungu na tutaendelea kumtunza,"amesema Mungasi
Kwa upande wake Elizabeth Mungasi ambaye ni mke wa mfugaji huyo amesema yeye ndio alikuwepo wakati ndama huyo alipokuwa akizaliwa na alishutushwa baada ya kuona mnyama wa aina yake na anatofauti kubwa na ng'ombe wengine.
" Kwani ukizaa mtoto kilema unaweza kumuua, hivyo mimi kama mama nitamlea na nitakaa nae hadi pale ndama huyu atakapo kufa.Tulishamuita daktari akaja akamuona akatuambia hana jinsi ya kutisaidia ,kwa hiyo tukae nae hadi atakapokufa, ndama huyu hawezi kula kitu tunachofanya ni kumkamulia maziwa na kumnyeshwa"alisema Elizabeth
Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashaur ya Arusha Arusha Charles Ngiroriti amesema hali hiyo ni kawaida kutokea kwa wanyama.Katika utungaji wa kiumbe inaweza ikatokea cell zikagawanyika ,kama vile zilitaka kutengeneza viumbe viwili.
Ameongeza lakini zikishindwa kigawanyika na kufika mwisho ndio anatokea kiumbe wa aina hiyo na kwamba hali hiyo haiuhusiani na imani za kishirikina, hivyo watu waache kuzusha maneno.
↧
WATU WANNE MIKONONI MWA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MABILIONI YA FEDHA YA BENKI YA NBC, POLISI TISA NAO MBARONI
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanne waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S Security kwa tuhuma za wizi wa Sh.1.280,000,000, Dola za Marekani 402,000 na Euro 27,700 huku pia likiwashikilia askari wa polisi tisa kwa tuhuma za kuchukua sehemu ya fedha hizo kutoka kwa mmoja ya watuhumiwa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam , Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewataja watu wanaoshikiliwa kwa wizi huo ni Chistopher Rugemalila(34)ambaye ni dereva wa G4S mkazi wa Chanika, Mohamedi Ramadhani (40) mlinzi G4S anayeishi Mtoni Kijichi, Ibrahim Maunga Mlinzi G4S na mkazi wa kiluvya pamoja na Salim Shamte(45) Mkazi wa Mbagala kizuiani.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa Februari 7 mwaka huu watuhumiwa watatu ambao ni Christopher Rugemalila, Mohamed Athuman na Ibrahim Maunga wakiwa na gari namba T 728 BAN, Nissan Hard Body mali ya kampuni ya G4S,linalotumika kusindikiza fedha walikabidhiwa fedha kutoka tawi la benki ya NBC Kariakoo na NBC samora ili wazipeleke makao makuu ya benki ya NBC yaliyopo Posta ya Zamani katika Mtaa wa Sokoine Drive lakini hawakufanya hivyo, matokeo yake walipanga njama na kuelekea maeneo ya Temeke Maduka mawili karibu na kituo cha mafuta cha CAMEL.
"Baada ya hapo wakachukua fedha zote na kupakia kwenye gari ndogo T134 DHY Toyota IST ikiendeshwa na Salim Shamte. Watuhumiwa hao baada ya kufanikisha uhalifu huo walitelekeza gari la Kampuni ya G4S, silaha mbili mali ya G4S, moja aina ya pump action, na bastola moja, mashine ya kuhesabia fedha na muhuri wa Benki ya CBA kisha kuondoka kusikojulikana.
"Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hizo liliunda kikosi kazi na kuanza ufuatiliaji mara moja, ambapo Februari 17, 2020 mchana huko Mongo la ndege mtuhumiwa wa kwanza aitwaye Christopher Rugemalila alikamatwa na alipopekuliwa alikutwa na Sh. 110,000,000, Dola za Marekani USD 19,000 zikiwa ndani ya gari lake T 691 BMW DSU,"amesema Kamanda Mambosasa.
Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa amekiri kununua magari matano yenye namba za usajili T691DSU BMW yenye thamani ya Sh.15,000,000, gari namba T909DSU Toyota Runx yenye thamani Tsh 13,000,000, gari namba T627DSU Toyota IST yenye thamani ya Tsh 11,000,000, gari namba T653DSU Toyota IST yenye thamani ya Sh.11,000,000 na gari namba T857DSU Toyota IST yenye thamani ya Sh. 11,000,000.
Amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kuendelea kuhojiwa alikiri tayari ameshanunua nyumba mbili na kiwanja kimoja vyenye thamani ya Sh.107,000,000, samani za ndani vyenye thamani ya Sh. 5,000,000, na kufanya jumla ya mali na fedha taslimu Sh.297,110,000, dola za Marekani 21,000.
Mambosasa amesema kuwa Febrauri 21 mwaka huu Jeshi la Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Mohamed Ramadhan na Salim Shamte huko maeneo ya Mbagala na walipopekuliwa walikutwa na Sh. 332,000,000, Dola za Marekani 50,000, EURO 5010 na gari moja aina ya IST namba T134 DHY ambayo ndio iliyotumika kubebea fedha baada ya kuiba na kutelekeza gari la kampuni ya G4S.
Amesema watuhumiwa wote wawili baada ya mahojiano wamekiri kununua viwanja viwanja viwili maeneo ya Kisemvule na Kivule vyenye thamani ya Sh. 25,000,000. Jumla kuu ya mali na fedha taslimu ni walizokutwa nazo watuhumiwa hao wawili ni Sh.357,000,000, dola za Marekani 50,000 na EURO 50,10 3.
" Aidha upelelezi uliendelea na Februari 24, 2020 mtuhumiwa Ibrahim Maunga alikamatwa na baada ya kupekuliwa alikutwa na Sh. 195,213,450,dola za Marekani 70,600, nyumba aliyonunua Kibaha yenye thamani ya Sh.milioni 30 pamoja na samani za ndani zenye thamani ya Sh.milioni 10 na kufanya jumla Jumla kuu ya mali na fedha ni Sh. 253,000,000.Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa wote watatu pamoja na mtuhumiwa aliyewasaidia kukamilisha wizi huo,"amesema Mambosasa na kuongeza pia wanawashikilia askari Polisi tisa kwa kukiuka maadili ya kazi wakati wa ufutiliaji na upekuzi wa tukio hilo.
↧