Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117112

RUBADA yawapa changamoto madiwani Makambako kuchapa kazi zaidi

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja akisisitiza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watendaji na madiwani wa halmashauri ya mji wa Makambako juu ya Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) jana mkoani Njombe.

Na Mwandishi wetu, Makambako

Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) imewataka madiwani na watendaji wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Makambako kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake watumie fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na rasilimali watu ili kuchoche kasi ya ukuaji wa maendeleo katika halmashauri hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, Bw. Aloyce Masanja Alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watendaji na madiwani wa halmashauri hiyo juu ya Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) jana mkoani Njombe.

“Ndugu zangu naomba tufanye kazi, haya mambo ya kulaumiana hayawezi kutufikisha popote, ni vema kila mtu akatimiza wajibu wake mahala pake pa kazi, ili kufikisha taifa hili kule linakotakiwa kwenda,” alisema.

Aidha alimewaomba madiwani na watendaji kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo katika kuanisha maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo ili yaweze kutafutiwa wawekezaji watakaowekeza katika sekta hiyo pana hapa nchini na kuleta maendeleo katika mji huo.

“Mamlaka siku zote inahakikisha wananchi wanafaidika sambamba na uwekezaji unaofanyika katika maeneo yao…nawaomba wana Makambako mlitambue hilo,” alisisitiza Masanja.

Aliwataka watendaji hao kuwatumikia wananchi wao kwa nguvu zao zote ikizingatiwa kuwa mji huo bado ni mdogo na unahitaji kuendelezwa kwa kiasi kikubwa ili kuubadilishisha tofauiti na ilivyo sasa.

“Makambako bado inakuwa hivyo ni jukumu lenu kuanza kutumia fursa ambazo mnazo hasa rasilimali watu, nimeona vijana wa hapa wana nguvu na wanajituma katika kufanya kazi za shamba, watumieni hawa mtaona faida yao,” alieleza Mkurugenzi huyo.

Aliwakumbusha watendaji hao kuwa katika mkakati wa serikali wa matokeo makubwa sasa, (Big Results Now) hakuna kulala na kwamba kasi katika kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ndio jambo la msingi.

“Kila mtu atakuwa akipimwa kutokana na utendaji wake, kama hutaweza kutekeleza yale uliwekewa kuyafanya basi utajikuta unawekwa pembeni…tufanye kazi kujenga nchi na si vinginevyo,” aliongeza.

Akizungumza kwa niaba ya madiwani na watendaji wa halmashauri ya mji Makambako, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo diwani Chesco Mfikwa alisema halmashauri hiyo imejipanga vema katika kuibua miradi mingi ya maendeleo.

“Sisi wana Makambako tupo tayari kushirikiana na RUBADA katika mpango wa SAGCOT ili kujenga uchumi wa mji wetu na watu wetu ili tuweze kujitegemea,” alisema Mfikwa.

Aliongeza kuwa semina waliyopata kutoka kwa mamlaka hiyo imewafungua macho kwa kiasi kikubwa hivyo mkakati wao ni kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuendeleza kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji katika eneo hilo.

“Semina imetujenga kwa kiasi kikubwa mimi nikiwa mwenyekiti nitakuwa mstari wa mbele kuwahimiza vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili kukuza kilimo katika halmashauri yetu na kuleta mabadiliko ya kweli,” aliongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117112

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>