Makamu wa Rais wa Chama cha Wabunge wa CPA Barani Afrika, Mhe. Spika Anne Makinda akitambulishwa kwa Rais wa Namibia, Mhe. Hifikepunye Pohamba wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa 44 wa Chama hicho (CPA) barani Afrika. Katikati ni mwenyeji wa mkutano huo na Spika wa Bunge la Namibia, Mhe. Asser Kapere. Jumla ya Wabunge 500 toka nchi 19 wanachama wa CPA barani Afrika wanahudhuria mkutano huo.
Spika Makinda akihutubia katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa CPA, Spika Makinda akiwa na baadhi ya wabunge na maafisa wa Tanzania katika mkutano huo pamoja na watanzania, Balozi Bandora ambae ni mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Namibia (kwanza kulia) na Dr. William Shija, Katibu Mkuu wa CPA Duniani (kwanza kushoto).