Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115478

Taasisi ya Aisha Sururu yamsaidia mlemavu

$
0
0
TAASISI ya Aisha Sururu, imetoa msaada wa baiskeli maalum kwa mtoto mlemavu, Saada Hamis Hamad (14), ambaye ni mshindi wa kwanza, kundi maalum, katika mashindano ya kuhifadhi Quran Tukufu, kitaifa.

Saada ambaye mikono na miguu yake imelemaa, alikabidhiwa baiskeli hiyo juzi jioni, na mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aisha Sururu, ambapo alisema ina mahitaji muhimu kwa mtu mwenye ulemavu, ikiwemo sehemu ya kujisaidia.

Akizungumza mara baada ya kupokea baiskeli hiyo, aliishukuru taasisi kwa kumsaidia kwa mambo mengi, ikiwemo kuibua kipaji chake cha kuhifadhi Quran na kumsafirisha kwa mara ya kwanza.

Alisema tangu apate akili, amekuwa akijisaidia kwa tabu bila staha na kwamba kupitia baiskeli hiyo, itamsaidia mambo mengi ikiwemo kuzunguka maeneo mbalimbali, ambapo hapo awali alishindwa kwani ili kutoka sehemu moja kwenda nyingine ilikuwa lazima abebwe.

"Kabla ya hapo nilikuwa nipo tu nyumbani, sikuwahi kupelekwa shule wala kutoka nje ya mji wangu, lakini nashukuru nimejifunza mengi na nimepata msaada huu,"aliongeza Saada.

Mtoto huyo, ambaye ni mkazi wa Mamoja, Pemba, alisema kuwa, ana ndugu zake wanne, ambao wawili kati yao ni walemavu kama yeye isipokuwa kaka yake wa kwanza ambaye alizaliwa akiwa mzima wa viungo.

Aisha, ambaye pia ni diwani wa viti maalum Ilala, aliwataka wahisani wengine kujitokeza na kununua baiskeli mbili kwa ajili ya ndugu zake Saada hasa mdogo wake ambaye anasoma chekechekea.

"Mdogo wake amekuwa akibebwa kwa ajili ya kupelekwa shule na kuridishwa nyumbani, hivyo baiskeli hiyo itapunguza adha na kumsaidia kuhudhuria masomo bila wasiwasi,"aliongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115478

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>