Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.
Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga, imewataka Wafanyabiasha wilayani humo, kuhakikisha kuwa wananunua na kutumia mashine za TRA za kielektroniki (EFD) katika kutoa risiti wakati wanapouza bidhaa zao kwani kutotoa stakabadhi ni kosa la jinai.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, wakati alipokuwa akifanya uzinduzi wa matuminzi sahihi ya mashine hizo za kielektroniki (EFD) wilayani humo na kusema kuwa itakapobainika kwa mfanyabiashara anauza bidhaa bila ya kutoa stakabadhi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Bw. Rweyemamu amesema kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.
Bw. Rweyemamu amesema kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.
Amesema kuwa mbali ya kuwa kwa kutumia mashine hiyo Serikali haitakosa mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madukani, lakini pia itakuwa ni faida kwa watumiaji kwa vile inahifadhi kumbukumbu za mauzo yao.
Awali Meneja wa TRA wilayani Handeni Bw. Charles Kamuhanda, alimwambia Mkuu huyo wa wilaya kuwa, wafanyabiashara wwengi hawataki kutoa risti wanapouza bidhaa katika maduka yao kwa lengo la kukwepa ushuru.
Hivyo amewataka kujenga tabia ya kutoa risiti kwa kila mmteja atakayenunua bidhaa katika duka husika na kwa kutokufanya hivyo ni sawa na kukwepa ushuru wa Serikali.
Bw. Kamuhanda alisema kuwa mnunuzi yeyote anatakiwa kudai na kupewa risiti kama sehemu ya uwajibikaji kwa taifa na kwamba ni haki kwa kila mteja kudai na kupewa risiti kwani hata wafanyabiashara wanapokwenda kufungasha wanatakiwa kudai na kupewa risiti pia.
Aidha Bw. Kamuhanda ameitaja faida nyingine za mashine hizo kuwa mbali ya kutunza kumbukumbu za mauzo kwa muda wa miaka mitano, lakini pia mfanyabiashara anaweza kudhibiti wizi endapo anamuachia muuzaji mwingine ambaye sie mwaminifu.