Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MTABIRI BINGWA WA KWANZA WA HALI YA HEWA TANZANIA NA MKURUGENZI MKUU WA KWANZA WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AFARIKI DUNIA

$
0
0
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mtabiri bingwa wa kwanza wa hali ya hewa na mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw. Urban Blass Lifigahani (Pichani). Hayati Lifiga  alizaliwa tarehe 27 Novemba 1936, kifo chake kilichotokea Jumatatu tarehe 15 Julai 2013 mchana katika hospitali ya Bosph Mbezi kwa Msuguli Dar es Salaam.

Bwana Lifiga alikuwa mtabiri bingwa wa kwanza Tanzania na Mwaafrika wa kwanza kujiunga Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashariki iliyokuwa chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo kwa wakati huu makao yake makuu yalikuwa Nairobi, Kenya. Bwana Lifaga aliteuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa, Tanzania. Alishisiriki na kushauri Serikali katika kuanzisha kwa Idara hiyo.
Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alichaguliwa kuwa Mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Dunia. Nafasi nyingine aliyeishika wakati wa uhai wake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashiriki.
Bwana Lifiga atakubumbuka kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sayansi ya hali ya hewa nchini, Afrika na Duniani.
Ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu cha Makerere na alichukua shahada ya udhamili chuo kikuu cha Nairobi. Hapa nchini alipata mafuzo ya Sekondari katika shule za Kwiro Sekondari, Mahenge na Pugu Sekondari, Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 19 Julai 2013  nyumbani kwake Msakuzi.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe; AMENI


IMETOLEWA NA OFISI YA UHISIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles