Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group iliyokuwa ikijenga majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Bw. Zhang Chengwei akitia saini hati ya makabidhiano kabla ya kukabidhi majengo hayo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria (hayupo pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akitia saini hati ya makabidhiano ya majengo ya Law School of Tanzania wakati wa shughuli ya makabidhiano ya majengo hayo iliyofanyika jana Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Emmanuel Mayeji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria (wa kwanza kulia), Mh. Jaji Gerald Ndika Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (wa pili kulia), na wa kwanza kushoto ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji kutoka Co-architecture.
Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei akimkabidhi hati ya makabidhiano ya majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi jana Julai 16, 2013 jijini Dar Es Salaam, baada ya ujenzi wa majengo hayo kukamilika. Anayepiga makofi katikati ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa Co-Architecture.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akipokea funguo za majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kutoka kwa Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei iliyokuwa ikijenga majengo hayo. Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam.