Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania Mhe. Mussa Zungu Azzan akifungua kikao cha Kamati tandaji pamoja na Sekretarieti jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 44 wa CPA Kanda ya Afrika utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto kwake ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa CPA Bwana Demetrius Mgalami. Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mkamu wa Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa CPA Kanda ya Afrika.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti
Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Kilindi Mhe. Beatrice Matumbo Shelukindo akichangia wakati wa mjadala.
Wajumbe wa CPA Tawi la Tanzania (Na Prosper Minja - Bunge)