Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imesema mpango wa utekelezaji uanzishaji wa Anwani za Makazi na Misimbo ya posta itasaidia kurahisisha mawaslimo na kuchochea maendeleo nchini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Profesa Patrick Makungu aliwambia wanandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua semina ya siku moja ya wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara, juu ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta..
“Jambo hili ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa katika kurahishsisha mawasiliano na maendeleo,” na aliongeza kusema kwa jiji la Dar es Salaam ni mhimu zaidi sababu huchangia asilimia 70 ya mapato ya kodi.
Alisema awamu ya kwanza ya mpango huo kwa jiji la Dar es Salaam ilizinduliwa rasmi na Septemba 14, 2012 na Rais Jakaya Kikwete ambapo utekelezaji wake unahusisha serikali taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutekeleza mpango huu ambapo tayari baadhi ya wizara na taasisi zimezana kutumia misimbo hiyo ya posta na wananchi wahamasike kuupokea .
Alisema kamati tendaji kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano ,sayansi na tekonolojia na mamalaka ya mawasiliano Tanzania, Shirika la Posta, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam na wadau mbalimbali wameandaa mipango ya utekelezaji katika jiji nzima.
Mkurugenzi Maswala ya Posta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Bi.Rehema Makubwi alisema program hiyo itasaidia huduma za posta kuimarika ambapo mwananchi atapata barua na vifurushi kwa urahisi zaidi.
”Pia inasaidia katika kutambua wananchi walipo, na wakati wa dharura ya majanga kama magonjwa na moto kupata huduma kwa urahisi ,” na hii ndiyo mfumo nzuri zaidi katika kukabili maswala haya.
Aliongeza kusema pia itawawezesha wafanyabiashara kupata mikopo benki kwa urahisi kutokana anwani ya makazi na misimbo ya posta huruhisisha mawasiliano ya kuwapata.
Naye, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Uchukuzi, Bw.Issa Nchasi alisema mpango huo katika wizara yake umefika wakati mwafaka kwani ita rahisisha na ni mwongozo wa kitaifa wa uwekezaji wa majina ya mitaa na namba za nyumba.
“ Hii itaongeza ufanisi katika Mamlaka ya usimamimizi wa Bandari na Maziwa (TPA) mizigo au bidha kumfikia mmiliki moja kwamoja,” bila ya kubahatisha alipo kutokana na kuwepo kwa anwani za uhakiaka.
Mpango huo ulitekelezwa kwa majaribio katika kata nane za Manispaa ya Arusha na Manispaa ya Dodoma kata saba na sasa unateklezwa jijini Dar es Salaam kwa kuanzia na majengo ya Serikali yote ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wake.