Mambo vipi Ankal,
naomba hii video uiweke kwenye blog yako kwani imenisikitisha sana kuona polisi anavyochukua hatua mikononi mwake na kutumia kazi yake kunyanyasa raia. Video hii nimetumiwa na ndugu yangu ambaye aliirikodi kwa simu yake na kunirushia mimi huku nilipo na mimi nikaamua kuitia katika YouTube , lakini nikaona kwa kuwa blog yako inatembelewa na watu wengi duniani nikaona itakuwa vizuri kwani watu wataona ni jinsi gani traffic wanavyotumia nguvu na kuwaonea raia. Shukrani
Mdau Zenji