Na Father Kidevu Blog
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.
Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.
Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.
Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.
"Marehemu Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya Kinondoni kesho lakini kabla ya mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, "alisema Lwendo.Lwendo amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00 mchana ambapo pia ndugu jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Wende.
Mmmoja wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba kimoja na marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo chuoni kwao na kwake kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si chuoni lakini hata kabla hawaja jiunga na chuo hicho.
Boswell amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.
Aidha amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea kuwa Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu vikubwa anavyo vipenda.
"Marehemu alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda kwqenda kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach kuogelea na siku ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi wengine wakiwapo wazungu ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa kimasomo," alisema Boswell.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam ukisubiri maziko.