Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117404

MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO NDG JOHN L. KAYOMBO AFANYA KIKAO CHA MARIDHIANO NA KANISA LA KKKT KABLA YA KUVUNJWA UKUTA ULIOJENGWA KWENYE ENEO LA SHULE YA MSINGI UBUNGO PLAZA

$
0
0

Na Mathias Canal, Dar essalaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo tarehe 23, Mei 2017 amefanya mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za usharika wa KKKT Ubungo kilikuwa na Agenda ya kujadili nanma bora ya uvunjaji wa Ukuta wa eneo la kanisa hilo ambao umeingia katika eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza Jambo linalopelekea Kushindwa kuanza ujenzi wa madarasa nane mapya kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao kwa sasa wanasoma katika madarasa ambayo majengo yake si rafiki kwa ajili ya usomaji.

Alisisitiza kuwa ujenzi huo utakuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alilolitoa Mei 19, 2017 wakati wa mkutano wake na walimu wa shule hiyo sambamba na wananchi wa Mtaa huo ukiwajumuisha Afisa mtendaji wa Kata na wajumbe wa mitaa.

MD Kayombo alisema kuwa baadhi ya shule katika Manispaa ya Ubungo hazifanyi vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa kutokana na uduni wa miundombinu ikiwemo madarasa Jambo ambalo pia limepelekea Manispaa ya Ubungo kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuwa rafiki kwa wanafunzi kujifunzia. 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017 
Darasa lililokabidhiwa na Uongozi wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ubungo kwa Uongozi wa Manispaa ya ubungo mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 117404

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>