Na Dotto Mwaibale
MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.
Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB).
"Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.
Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.
Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.
Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.
Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA