Bi. Vicky Joan Msina wa Benki Kuu Dar es Salaam, kwa niaba ya ndugu zake wote na familia za Msina, Lyimo, Kiiza na Mbuya wa Dar es Salaam, Kilema, Moshi, na Tabora; wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kipindi chote cha kumuuguza na kushiriki shughuli ya msiba wa Mama yao mpendwa Mwalimu Petronella Peter Lyimo, aliyefariki Ijumaa tarehe 28 Aprili, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 04 Mei, 2017Mbweni, Dar es Salaam.

Pia Shukran ziwafikie Majirani wote wa Mbweni wakiongozwa na Bwana na Bibi Mutegeki, Bi Sandra na wengine wote, pamoja na Wana Jumuiya ya mtakatifu Joseph Mfanyakazi – Mbweni kwa kutufariji kwa hali na mali. Vile vile shukran ziende kwa Baba Paroko, Paroko msaidizi na Katekista na wanakwaya wa Parokia ya Mtakatifu Rafael - Mbweni kwa huduma ya kiroho waliyotoa kwa marehemu wakati wa uhai wake na pia kwa kufanikisha Ibada ya Maziko kwa kushirikiana na kaka wa Marehemu Fr. Henry Zawadi wa Kristo Mfalme Moshi.
Kwa namna ya kipekee tunawashukuru sana Uongozi na Wafanyakazi wa Benki Kuu Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango, NMB- Makao Makuu na Tawi la Bank House, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Shule ya Msingi za Pwani- Tegeta na Kiumbageni-Mbweni pamoja na Shule maalum ya wasiosikia- Njombe.
Ni ngumu kumtaja kila mmoja kwa namna mlivyoshiriki kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Tunasema kwenu nyote Asanteni sana na Mungu awabariki daima.
PUMZIKA KWA AMANI MAMA YETU MPENDWA Mwl. PETRONELLA LYIMO.
“BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”.