Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (kushoto) akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Semina hiyo ilihusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi kabla ya kuanza kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika semina hiyo. Mada zilizowasilishwa katika semina hiyo ni Kwanini Watanzania tuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori, Athari za Muingiliano wa Mifugo na Wanyamapori, Maendeleo ya Utalii na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na Umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu Nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jeneral Gaudence Milanzi akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa askiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Watanzania kuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori katika semina hiyo. Kushoto waliokaa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya viongozi na wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.