Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar za kusaidia wananchi wanaokabiliwa na hali duni ya maisha kwa kuahidi kutoa mifuko ya saruji 1000 na mabati 600 kwa ajili ya kusaidia wananchi hao.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo mjini Unguja wakati anazindua kampeni maalum ya MIMI NA WEWE inayolenga kuhamasisha wananchi kuungana pamoja katika kutoa misaada ya hali na mali ili kuboresha huduma za kijamii katika sekta za afya, elimu,mazingira,maji safi na salama, matumizi bora ya ardhi na kusaidia watu wasiojiweza.
Makamu wa Rais katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo amekemea vikali tabia ya ubinafsi kwa baadhi ya viongozi inayosababisha wananchi kutopatiwa taarifa muhimu za maendeleo yao hali inayopelekea uduni katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi katika maeneo mbalimbali kujenga tabia ya kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazopata na jinsi zilivyotumika ili kuwapa moyo wananchi katika kuchangia kwenye shughuli za maendeleo kwa sababu watakuwa na imani kuwa fedha zao walizochanga zinatumika vizuri.
“Maendeleo endelevu ni lazima yazingatie Utu na heshima ya mtu, mshikamano wa dhati na mafungamano ya Kijamii,” Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe uliofanyika kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. ![]()
Bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha wananchi walijitokeza na kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa mjini Magharibi, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)![]()
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi,Wafadhili waliochangia kufanikisha kampeni ya Mimi na Wewe inaleta tija kwa wananchi wa mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha wananchi walijitokeza na kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa mjini Magharibi, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi,Wafadhili waliochangia kufanikisha kampeni ya Mimi na Wewe inaleta tija kwa wananchi wa mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).