Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

THE DESK& CHAIR FOUNDATION YASAIDIA WALEMAVU MKOANI MWANZA

$
0
0
TAASISI isiyo ya kiserikali ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) tawi la Tanzania imekabidhi misaada ya baiskeli za miguu mitatu (wheel chair)  na visaidizi kwa watu mbalimbali wenye ulemavu pamoja na vifaa vya mazishi.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7.6 vilikabidhiwa jana kwa walengwa na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani Wilaya ya Nyamagana.
 Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee akimkaribisha mgeni rasmi kukabidhi msaada huo alisema walipokea maombi mengi kutoka kwa wahitaji lakini kutokana na maombi wamefanikiwa kuwapa wachache na kuahidi waliokosa watapa awamu nyingine.
“Niwashukuru wafadhili wanaotuwezesha kuwasaidia watu wasio na uwezo pamoja na vyombo vya habari. Misaada hii ni endelevu , niwaombe ndugu zangu mliokosa kwa sababu ya wingi wa maombi muwe wavumilivu endapo ufadhili utapatikana tutawasaidia kulingana na mahitaji ya kila mmoja,” alisema Meghjee.
Aliitaja misaada hiyo kuwa ni Wheel Chair nne, baiskeli 10 za magurudumu matatu, magongo seti moja,visaidizi viwili vya kuwawezesha  watoto kutembea (baby walker), vifaa vya mazishi (chepeo 4, sululu 2 na majembe 4), sahani na vikombe 204.
Akizungumza kabla ya kuikabidhi misaada hiyo Kotecha aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa inayoifanya ya kusaidia jamii pamoja na serikali kwenye sekta za elimu, afya na maji.
Alisema kuwepo kwa taasisi hiyo Watanzania wengi hasa wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na mingine, wataendelea kunufaika na laiti tungepata taasisi nyingi kama The Desk & Chair Foundation nchi ingepata maendeleo ya haraka.
“Naamini uadilifu wenu katika kutekeleza kazi zenu zinazotokana na fedha za wafadhili zimewafanya muendelee kuaminika kwao.Mgekuwa wapigaji msingefanikiwa,” alisema Kotecha.
Naibu Meya huyo na Diwani wa CCM Kata ya Nyamagana alisema taasisi hiyo imefanya mengi kwenye sekta za elimu,maji na afya  kwa kutengeneza madawati, kuchimba visima vya maji , kulipa gharama za matibabu na ada za masomo kwa wanafunzi mbalimbali.
Alisema taasisi hiyo imekuwa ikijenga miradi ya vyoo na kuchimba visima vya maji vyenye ubora kwa gharama nafuu,vinavyokidhi thamani ya fedha na kuiomba serikali kuisaidia na kuiunga mkono kutokana na kufanya kazi kubwa ya kusaidia jamii.  
“Nakosa maneno ya kusema juu ya Desk & Chair, wanayoyafanya hawayafanyi kwa kujionyesha,lengo ni kuwasaidia watanzania maana  hawaangalii dini, rangi wala kabila.Si kama wengine wanofanya kwa kujinufaisha wao.Nawashukuru sana,”alisema Naibu Meya huyo wa Jiji.
Naye Skeih Hashim Ramadhan wa Bilal Muslim Mission Of Tanzania Tawi la Mwanza alieleza kuwa ni jambo jema kutoa kitu chochote ili kusaidia watu  wenye mahitaji lakini pia ni sadaka na thawabu
 Mtoto Teddy Shirikale mkazi wa Kisesa Magu, mwenye ulemavu uliotokana na kipigo kutoka kwa mama yake aliyefahamika kwa jina moja la Enjoy na kusababisha mguu wa kushoto uoze na kupata kilema cha kudumu.Mama huyo baada ya kutenda unyakiwa akiwa amekaa kwenye Wheel Chair aliyokabidhiwa na The Desk & Chair Foundation. Anayemsukuma ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki Bhiku Kotecha ambaye alikuwa mgeni rasmi  muda mfupi baada ya kumkabidhi. Anayemrekebisha mkanda ni Mkurugenzi wa taasisi ya Nitetee Flora Lauwo.
 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee wa pili kutoka kulia waliosimama akiwa katika picha ya pamoja na walemavu waliopokea msaada wa baiskeli, wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi Bhiku Kotecha.
 Mmoja wa walemavu walipoata baiskeli Bw. Mwanza Lima akizungumza na 

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee, Mwanza Lima alipata ulemavu baada ya kupigwa kichwani na mkewe.

 Mgeni Rasmi Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha akimkabidhi Bw. Mwanza Lima baiskeli ya magurudumu matatu baada ya kupata ulemavu wa kudumu uliosababishwa na kipigo kutoka kwa mkewe ambaye baada ya tukio hilo alitoroka. 
Bi. Batika Kilaka mkazi wa Bunda akiwa amekaa kwenye Wheel chair aliyokabidhiwa na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Bhiku Kotecha (nyuma yake ) iliyotolewa  na The Desk & Chair Foundation. 
Habari na picha na Baltazar Mashaka


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>