Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir, akisoma taarifa ya shule kwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 29 ya kidato cha Sita, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka (kulia), wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu Rashid Kassim.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akizungumza na wahitimu hao, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha Kiongozi Bora, mhitimu Khadija Mashaka, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti Mwanafunzi Bora katika somo la Geography, mhitimu Mussa Baruti, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.