Na Veronica Simba - Arusha
Jumla ya wanawake 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini, jana (Mei 19, 2017) wamehitimu mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.
Wahitimu hao wa awamu ya nne, wamefanya idadi ya waliohitimu tangu kuanzishwa mafunzo husika katika Kituo hicho kufikia 65.
Akizungumza katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, alitoa wito kwa wadau wa madini ya vito nchini, kuwapa ajira na ushauri wa kitaalam wahitimu, ili waweze kujiajiri katika shughuli za uongezaji thamani madini.
"Lengo ni kuhakikisha kuwa ukataji unafanyika kwa viwango vya kimataifa ili kuweza kuuza zetu kwenye masoko ya nje."
Aidha, Dkt. Pallangyo alitoa changamoto kwa wadau wote wa madini ya vito kuendelea kukuza shughuli za uongezaji thamani madini kwa kubadilishana uzoefu na wakataji wa madini ya vito mahiri duniani.
"Kwa wale wafanyabiashara wa madini ya vito, mlioajiri wataalam wa kigen, natoa rai muendelee kuwahimiza watoe mafunzo kwa watanzania wanaofanya nao kazi, ili kuhawilisha utaalam huu adimu," alisisitiza.
Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito, zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, akisoma historia ya Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mwanafunzi bora, Happiness Ernest, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi.Mgeni Rasmi katika sherehe za mahafali ya Nne ya Mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito nchini, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua – walioketi) na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA