Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117375

Rais Dkt. Magufuli akabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais Museveni wa Uganda

$
0
0

Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati katika ukumbi wa mikutano wa Kikwete  Ikulu Jijini Dar es Salaam, ukiwa umehudhuriwa na  ujumbe kutoka nchi zote sita wanachama.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya. 
Aidha, mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa  Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kuna kila sababu ya kulinda na kudumisha mtangamano uliopo kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama. 
Mkutano huo pia  umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Mhandisi Steven Mrote kutoka Tanzania.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwenye Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
Meza kuu ya viongozi ikiwa imesimama wakati wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano huo.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribishwa kitini pake Mwenyekiti mpya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli na anayeingia Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakirekebisha mpangilio wa majina.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117375

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>