Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117375

Nafasi za masomo Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya ngazi za Cheti na Diploma katika kampasi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya katika kozi zifuatazo:

Uhasibu (Accountancy),  Utawala katika Biashara (Business Administration), Masoko (Marketing), Manunuzi na Ugavi (Procurement & Supplies Management), TEHAMA (ICT) na Vipimo na Mizani (Legal & Industrial Metrology).Katika mwaka wa masomo 2017/18 Chuo kitatumia mitaala mipya inayoendana na hali halisi ya mahitaji ya soko la ajira.
SIFA ZA KUJIUNGA
CHETI - Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau "D" nne.
DIPLOMA - Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita na kupata angalau, principal pass
moja na subsidiary pass moja, Au mwenye elimu ya ngazi ya cheti kutoka katika Chuo kinachotambulika na NACTE
NAMNA YA KUFANYA MAOMBI
- Online kupitia www.cbe.ac.tz
- Au fika katika Kampasi yoyote ya CBE na Vyeti halisi, pamoja na  Ada ya maombi 25,000/=

 Pia Chuo kinatoa Bachelor degree, Postgraduate diploma na Masters degree. Maombi ya kujiunga yanaendelea.
MASTER'S DEGREE NI HIZI ZIFUATAZO
1) ICT Project Management - DAR Campus
2) ICT for Development - DAR Campus
3) Supply Chain Management - DAR, DODOMA
4) International Business Management - DAR na DODOMA
VILEVILE, kampasi za Dar na Dodoma, kuna kozi nzuri ya Ualimu wa Masomo wa Biashara, yaani Bachelor of Business Studies with Education (BBSE), Changamkia


ADA ZETU NI NAFUU NA ZITALIPWA KWA AWAMU
Kumbuka, Chuo ni cha Serikali na kinao uzoefu wa miaka 52 katika Elimu ya Biashara

Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Masoko,
Chuo cha Elimu ya Biashara
0715 722 467

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117375

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>