Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji ameendelea kutembeklea vituo mbalimbali vya Bajaji na Bodaboda jijijni katika juhudi za Jeshi la Polisi kupunguza kama si kuondoa kabisa ajali za barabarani. ACP Awadhi leo ametembelea kituo cha Africa sana eneo la Sinza na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa vyombo hivyo vy abiria, akiwataka kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani pamoja kuhakikisha wanatengeneza pikipiki zao ili ziwe katika ubora wa kubeba abiria. Madereva hao wamefurahia hatua ya kamanda huyo kupita kila pembe ya jiji kutoa elimu, wakisema hatua hiyo ni ya kutia moyo kwani inaimarisha uhusiano mwema kati yao na wana usalama barabarani.
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akielezea umuhimu wa kuwa na Bajaji na Bodaboda zisizo na hitilafu ili kuhakikisha usalama wa abiria
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akisisitiza umuhimu wa kuvaa helmet kwa dereva pamoja na abiria
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akikagua uimara wa Bodaboda