Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117361

Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

$
0
0
Na Nuru Juma-MAELEZO

Serikali inamkakati wa kuhakikisha inajenga Magereza katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa kilimo ambayo pia yana ukubwa wa kutosha ili kazi ya kuwarekebisha wafungwa iwe rahisi kufanyika huku shughuli za uzalishaji zikiwa zinaendelea.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mhe Devotha Minja Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro. 

“Magereza hayo yatajengwa katika maeneo yenye Kilimo na yatakuwa ni kwa ajili ya watu waliokwisha hukumiwa huku yale Magereza ya mijini yawe kwa ajili ya mahabusu tu ili wawe karibu na Mahakama,”alisema Mwigulu. 

Aliongeza kuwa mkakati huo wa Serikali ni wa muda mrefu na wanahitaji kufanya hivyo ili kurahisisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wafungwa na pia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Magereza.

Hili pia linatokana na tamko la Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilowahi kulitoa hivi karibuni kuwa wafungwa wako katika kutumikia adhabu hivyo wanatakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ili kwanza kujipatia chakula na sio kukaa tu bure na kusubiri kila kitu wafanyiwe na serikali.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117361

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>