Na Freddy Macha
Janet Chapman ni kati ya Waingereza wanaojitolea (bila malipo ), miaka mingi kujaribu kusaidia Afrika, hususan Tanzania. Akiwa mwanachama wa Shirika la Misaada ya Maendeleo Tanzania (TDT) na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) karibuni amejihusisha na suala la kutokomeza Ukeketaji. Katika mahojiano na Kwa Simu Toka London - Mei 11, 2017 anafafanua mradi mpya wa kujenga ramani vijijini Tanzania, yaani "Mapping". Je maana na faida yake nini? Kufaidi zaidi mahojiano bofya CC dirisha la You Tube upate maelezo yaliyoandikwa kitaaluma kuelewa kinachosemwa.