Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri Prof. Riziki Shemdoe.
Taarifa hiyo imevitaja vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi wa afya ya jamii kuwa, ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa Jiwe la msingi, uzinduzi wa Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.
Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe, akizindua Zahanati ya ya kijiji cha Vikula halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Mwenyakiti wa Halmashauri Mh. Festo Mgina, akizindua Zahanati ya Kijiji cha Nundwe Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Mwenyekiti wa halmashauri akiwahamasisha wakazi wa Kijiji cha Ihalimba kuchangia Mfuko wa CHF kabla ya kuweka jiwe la Msingi kwenye jengo la zahanati ya Kijiji hicho. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA