KATIKA kuhakikisha watanzania wengi wanapata matangazo yake, Kituo cha Utangazaji cha Efm kimetanua matangazo yake kwa kuongeza masafa ya 91.3 fm Mkoani Mwanza huku Uongozi ukibainisha kuwa, matarajio ni kuhakikisha Matangazo hayo yanafika katika mikoa mingine kumi, ikifuatiwa na Mkoa wa Mbeya.
Mikoa mingine ni pamoja na, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara, Tanga , Kigoma na Dodoma.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa EFM Radio, Denis Ssebo amesema lengo la kuanza na Mkoa wa Mwanza, wameangalia idadi ya watu ambao wanapatikana kupitia Kanda ya Ziwa Victoria lakini pia ukubwa wa jiji baada ya jiji la Dar es salaam.
Lengo la Efm Radio ni kuhakikisha inahabarisha, kuburudisha, kuwawezesha pamoja na kuwapa elimu wasikilizaji wake wote katika kila mkoa itakaposikika. Hivyo mikoa mingine ikae mkao wakula, “tutawafuata mlipo… Denis Ssebo”.
EFM NI KWIKWI