Waziri wa Kazi na Ajira,Mhe. Gaudentia Mugosi Kabaka, akihutubia Kikao cha 102 cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kinachoendelea kufanyika, Geneva Uswisi. Kikao hiki kinakutanisha Wawakilishi wa Serikali, Vyama vya Waajiri na Wafanyakazi toka nchi wanachama 189 wa Shirika hilo. Kikao kilianza tarehe 5/6/2013 na kinatarajia kuisha tarehe 20/6/2013.
↧