Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TSCP), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ambao ulizinduliwa rasmi 2010, umedhihirisha jinsi ulivyoshamiri kwa kiwango kikubwa. Mabadiliko makubwa yameshaanza kuonekana katika Miji 7 ambamo Mradi huu unaendelea na shughuli zake. Mikoa hii ni; Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Tanga na Kigoma Haya yalibainishwa hivi karibuni wakati wa Kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tscp kilichofanyika Dodoma Hoteli – Dodoma. Kikao hicho kilikusanya wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri kwa kusudi la kutathimini kama Mradi huo unaendelea vyema kufanya ipaswavyo au la. Pia kubaini kama matakwa ya mipango ya Mradi yanafanikiwa na kutoa ushauri ambao utasaidia kufanikisha mafanikio ya kutimiza makusudi ya Mradi kama inavyotarajiwa.
wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri wakiwa katika mazungumzo juu ya mradi huo.
UJENZI WA STANDI YA MABASI MAKUBWA DODOMAUKIENDELEA, UJENZI HUU UNAOFANYWA NA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI WA TSCP, ULIO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI.