MFANYAKAZI bora wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, John Kopwe, toka Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala, akipokea cheti kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambazo kitaifa zilifanyika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mfuko PPF umetoa kiasi cha shilingi milioni tano kwa Kopwe ikiwa ni motisha kwa kila mfanyakazi bora wa mwaka wa Mfuko wa PPF.
BAADHI ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambazo kitaifa zilifanyika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro.